Monday, November 26, 2012

ANDRE INIESTA AONYESHA KUWA YEYE NI KIUNGO BORA KABISA KWA SASA AKIWA ANAISAIDIA TIMU YAKE YA BARCA DHIDI YA LEVANTE KWA KUFUNGA YEYE BAO MOJA KUSAIDIA MABAO 3 ,MAWILI KWA MESSI NA MOJA KWA FABRIGAS...

YANGA KWENDA UTURIKI KUPIGA KAMBI YA WIKI MBILI, BRANDS APANDISHA MAKINDA MATATU YA B YANGA A

KATIKA kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga ya Dar es Salaam inatarajia kwenda kuweka kambi ya wiki mbili nchini Uturuki mapema mwakani.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Abdallah Ahmad Bin Kleb amesema leo katika Mkutano na Waandishi wa Habari, makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam kwamba ziara hiyo inatarajiwa kufanyika kati ya Desemba na  Februari 25, mwakani.
Alisema pendekezo la kambi hiyo lilitolewa na kocha mkuu wa Yanga, Mholanzi Ernie Brandts ambaye ana uzoefu na nchi hiyo ambayo ina vitu vinavyostahili kwa ajili ya timu kuweka kambi.
Alisema ikiwa huko timu hiyo inatarajiwa kucheza mechi mbili za kitrafiki na timu zitkazotajwa baadaye.
Aidha, kocha mkuu wa timu hiyo amewapandisha wachezaji watatu wa kikosi cha vijana chini ya miaka 20 wakiwemo kipa, Yussuf Abdallah, George Banda na Rehan Kibinga.
Katika hatua nyingine, Bin Kleb aliasema wanajivunia uongozi wa sasa chini ya Mwenyekiti, Alhaj Yussuf Manji, kwani timu imekuwa na mafanikio makubwa ikiwemo kutwaa kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kagame, kufanya vema katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ambao ulimalizika kwa timu kuongoza.
Alisema kufanya vizuri katika Ligi Kuu, ni matunda ya timu hiyo kuweka kambi nchini Rwanda baada ya Kombe la Kagame.

BOCCO ADEBAYOR ATUPIA BAO MBILI NA KUANZA KUNYEMELEA KIATU CHA DHAHABU

JOHN Bocco ‘Adebayor’ ameingia kwenye orodha ya wachezaji wanaowania ufungaji bora wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge kufuatia jana kufunga mabao mawili, Tanzania Bara ikiilaza Sudan 2-0 katika mchezo wa Kundi B, Uwanja wa Mandela, Namboole, Kampala, Uganda.
Bocco aliyeifungia Kilimanjaro Stars, inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager mabao yote hayo kipindi cha kwanza, sasa analingana na washambuliaji wa Burundi, Chris Nduwarugira na Suleiman Ndikumana, ambao kila mmoja ana mabao mawili pia.
Wengine ambao hadi sasa kila mmoja amefunga bao moja ni Yussuf Ndikumana wa Burundi, Mohamed Jabril wa Somalia kwa penalti, Geoffrey Kizito wa Uganda na Yonatal Kebede Teklemariam.
Bocco ana nafasi zaidi ya kuongeza mabao katika mechi za kundi hilo, haswa kwenye mchezo dhidi ya Somalia Desemba 1, kwani hiyo ndio timu dhaifu zaidi kwenye Kundi B.
Lakini Bocco kama atacheza kwa kiwango cha jana, anaweza akawa mwiba hata mbele ya Burundi Novemba 28.
Kwa sasa Bocco anayechezea Azam FC ya Dar es Salaam, ndiye mshambuliaji pekee kwenye kikosi cha Bara, baada ya washambuliaji wengine, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaochezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemomkrasia ya Kongo (DRC) kuzuiliwa na klabu yao.
WAFUNGAJI CECAFA TUSKER CHALLENGE 2012
John Bocco                  Tanzania 2
Yussuf Ndikumana       Burundi   2
Suleiman Ndikumana   Burundi   2
Yussuf Ndikumana       Burundi   1
Mohamed Jabril            Somalia   1(penalti).
Geoffrey Kizito              Uganda    1
Yonatal Teklemariam    Ethiopia   1 

NGASSA ATETEMESHA KAMPALA BALAA, WAGANDA TUMBO JOTO

Ngassa alivyokuwa akiteleza kushoto mwa uwanja wa namboole jana, balaa

SALUTI kwa Mrisho Khalfan Ngassa. Waganda, wamekoma naye. Mashabiki wa soka Uganda, wamekoshwa na soka ya Mrisho Khalfan Ngassa wa Tanzania Bara katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge inayoendelea mjini hapa.
Wakizugumza baada ya mechi kati ya Sudan na Tanzania, mashabiki walikuwa wakimsifia mno mchezaji huyo wa Tanzania Bara aliyekuwa amevalia jezi namba nane na kusema hawajui siku Stars ikikutana na Uganda itakuwaje mbele ya mshambuliaji huyo wa Simba SC ya Dar es Salaam.
Hata Waandishi wa Habari wa Uganda, wamemsifia mno Ngassa wakisema huyo ndiye mchezaji aliyeonyesha kiwango kikubwa zaidi cha uchezaji hadi sasa kwenye michuano hii.
Ngassa jana alikuwa mwiba kweli mbele ya Sudan, akitengeneza mabao yote mawili ya ushindi yaliyofungwa na mshambuliaji John Bocco ‘Adebayor’ wa Azam FC.
Jana Ngassa alipangwa wingi ya kushoto ambako alikuwa akiteleza kwa kasi na kutoa krosi nzuri ambazo bahati mbaya au nzuri ni mbili tu zilizotumiwa vyema na Bocco.
Mashabiki wamemsifia pia Ngassa kwamba si mchezaji mchoyo ambaye muda wote anafikiria zaidi kuwatengenezea wenzake nafasi kuliko kutaka kufunga mwenyewe.
Ngassa ni kati ya wachezaji 10 wa Simba wanaocheza michuano ya mwaka huu mjini hapa, wengine wakiwa ni Nassor Masoud 'Cholo' (Zanzibar), Juma Kaseja (Bara), Shomari Kapombe (Bara) Amir Maftah (Bara), Amri Kiemba, (Bara) Mwinyi Kazimoto (Bara), Ramadhani Singano ‘Messi’ (Bara), Christopher Edward (Bara) na Emanuel Okwi (Uganda).
Timu nyingine za Bara zenye wachezaji hapa ni Azam tisa, Mwadini Ali (Zanzibar), Abdulaghan Gulam (Zanzibar ), Samir Haji Nuhu(Zanzibar), Aggrey Morris(Zanzibar), Khamis Mcha 'Vialli'(Zanzibar), Deogratius Munishi ‘Dida’ (Bara), Erasto Nyoni (Bara), Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (Bara) na John Bocco ‘Adebayor’ (Bara).
Yanga ina wachezaji saba, ambao ni Nadir Haroub Ali 'Canavaro'(Zanzibar), Haruna Niyonzima (Rwanda), Hamisi Kiiza (Uganda), Kevin Yondan (Bara), Athuman Iddi ‘Chuji’ (Bara), Frank Domayo (Bara) na Simon Msuva (Bara), wakati Mtibwa Sugar inao watatu Twaha Mohammed (Zanzibar), Issa Rashid (Bara) na Shaaban Nditi (Bara), JKT Oljoro ina mmoja Amir Hamad (Zanzibar) sawa na Coastal Union Suleiman Kassim 'Selembe' wa  Zanzibar pia. 

ZANZIBAR HEROES WAANZA KAZI LEO KAMPALA

Zanzibar Heroes watang'ara leo?

TIMU ya soka ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes leo inaanza kampeni zake za kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge kwa kumenyana na Eritrea katika mchezo wa Kundi C, utakaonza saa 9:00 alasiri Uwanja wa Mandela, Namboole mjini hapa
Mchezo huo, utafuatiwa na mchezo mwingine wa kundi hilo, ambao unatarajiwa kuwa mkali zaidi na wa kusisimua kati ya Rwanda na Malawi kuanzia saa saa 12:00 jioni.
Kikosi cha Zanzibar Heroes kiliagwa Jumatano visiwani Zanzibar katika Hoteli ya Bwawani ambayo inamilikiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Said Ali Mbarouk.
Kikosi kiliondoka Alhamisi Zanzibar kuaa Kampala kikipitia Dares Salaam na kimeondoka na msafara wa watu 30, wakiwemo wachezaji 20, benchi la ufundi na viongozi wa Serikali na Chama cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA).
Hata hivyo, Heroes itamkosa kiungo wake mahiri Abdulhalim Humud, ambaye ni majeruhi.
Kikosi kinachotarajiwa kuanza leo Heroes ni; Mwadin Ali Mwadini, Nassor Masoud ‘Cholo’, Samir Hajji Nuhu, Agrey Moris, Nadir Haroub Ali 'Canavaro, Sabri Ali, Khamis Mcha 'Vialli', Is-haka Othman, Amir Hamad, Twaha Mohammed na Suleiman Kassim ‘Selembe’.
Tayari mechi za awali za Kundi A na B zimekwishachezwa na leo Kundi C ndio linafichua makali yake kwa mara ya kwanza.
Katika mechi za ufunguzi za Kundi A, Ethiopia waliifunga Sudan Kusini 1-0, wakati Uganda waliichapa Kenya 1-0 pia juzi, Uwanja wa Mandela, Namboole.
Mechi za Kundi B jana, Burundi iliitandika Somalia mabao 5-1, kabla ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars kuilaza Sudan 2-0.   

POULSEN BADO AWALILIA SAMATTA NA ULIMWENGU KAMPALA

Kocha Kili Stars, Kim Poulsen

KOCHA wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Mdenmark Kim Poulsen amesema kwamba bado anawahitaji mno washambuliaji Mbwana Ally Samatta na Thomas Emanuel Ulimwengu wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na iwapo hawatajiunga kabisa na kikosi chake, watamuweka katika wakati mgumu.
Akizungumza  jana mjiniuganda mara , baada ya mchezo dhidi ya Sudan wa Kundi B Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge, ambao walishinda 2-0, Kim alisema jitihada za kuwaomba Mazembe wawaruhusu wachezaji hao zinaendelea.
“Sijui itakuwaje wasipokuja, itanibidi tu niwatumie wachezaji hawa hawa waliopo, najua nina mshambuliaji mmoja, lakini nitawatumia hawa hawa waliopo, Simon Msuva anaweza akawa mshambuliaji, nitafanyeje,”.
“Siwezi kuita mchezaji mwingine kutoka nyumbani kwa sasa, kwa sababu mtu lazima umuone uwezo wake, huwezi kumuita tu, kwa hivyo naomba Mungu tu Samatta na Ulimwengu waje,”alisema Kim.
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, jana ilianza vema kampeni zake za kuwania Kombe la Challenge, baada ya kuichapa mabao 2-0 Sudan kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole, Kampala, Uganda. 
Ushindi huo, unaiweka Stars katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Kundi B, nyuma ya Burundi inayoongoza kwa wastani wa mabao.
Hadi mapumziko, Stars walikuwa mbele kwa mabao 2-0, yote yakipachikwa kimiani na mshambuliaji wa Azam FC, John Raphael Bocco ‘Adebayor’ aliyetumia vema krosi za Mrisho Khalfan Ngassa.
Bocco alifunga bao la kwanza Bocco aliiwahi vema krosi ya Ngassa aliyewatoka mabeki wa Sudan wingi ya kushoto na kuitumbukiza kimiani dakika ya 14.
Adebayor wa Chamazi aliwainua tena vitini mashabiki wa Tanzania dakika ya 28, akiunganisha krosi ya Ngassa tena kutoka kule kule kushoto. 
Kwa ujumla Tanzania Bara walicheza vizuri kipindi cha kwanza, wakishambulia zaidi kupitia pembeni, kulia Simon Msuva ambaye hakuwa na madhara sana na kushoto Ngassa ambaye alikuwa mwiba mchungu haswa kwa Wasudan.
Pamoja na Bara kutawala kipindi cha kwanza, lakini Wasudan walifanya mashambulizi kadhaa ya kushitukiza na sifa zimuendee mlinda mlango Juma Kaseja, ambaye alioko amichomo miwili ya hatari mno. 
Kipindi cha pili Stars, inayofundishwa na Mdenmark Kim Poulsen iliendelea kutawala mchezo, lakini safu ya ulinzi ya Sudan iligangamala.
Kikosi cha Stars jana kilikuwa; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Amir Maftah, Shomari Kapombe, Kevin Yondan, Frank Domayo, Salum Abubakar/Amri Kiemba, John Bocco, Mwinyi Kazimoto na Simon Msuva/Shaaban Nditi.
Sudan; Ebd Elrahman Ali, Moawia El Amin, Sami Abdallah, Faris Abdallah, Hamoda Bashir/Farid Mohamed, Mohamed El Mortada, Sadam Abutalib, Mohamed Mussa Idris, Modathir Mohamed, Adam Sayer/Osama El Rashid na Mohamed Osman/Saed Siddig.   
Katika mchezo wa awali, Burundi walishinda mabao 5-1, mabao yake yakifungwa na Chris Nduwarugira dakika ya 35 na 88, Yussuf Ndikumana dakika ya 41 na Suleiman Ndikumana dakika ya 84 na 90, wakati la Somalia lilifungwa na Mohamed Jabril kwa penalti dakika ya 55.
Matokeo hayo yanalifanya Kundi B lizidi kuwa gumu, kwani Burundi inaongoza kwa pointi zake tatu na mabao mengi, Tanzania ya pili kwa pointi tatu na mabao mawili- lakini bado Sudan wanaweza kupata matokeo mazuri katika mechi zijazo.
MSIMAMO KUNDI B: 

                     P   W  D   L    GF GA GD Pts
Burundi         1    1    0    0    5    1    4    3
Tanzania       1    1    0    0    2    0    2    3
Sudan           1    0    0    1    0    2    -2  0
Somalia         1    0    0    1    1    5    -4  0

KOCHA BURUNDI AMTEMA KAVUMBANGU KIKOSI CHA TUSKER CHALLENGE 2012

Kocha wa Burundi, Lotfy Mohamed

KOCHA wa timu ya soka ya taifa ya Burundi, Int’hamba Murugamba, Mmisri Lotfy Mohamed amesema kwamba amemtema kwenye kikosi chake mshambuliaji wa Yanga SC ya Dar es Salaam, Didier Kavumbangu kwa sababu hamuhitaji kwenye mipango yake ya sasa.
Akizungumza hiyo jana mjini uganda , Mohamed alisema kwamba amekuja na kikosi cha wachezaji ambao wanacheza Ligi ya Burundi pekee na hajachukua mchezaji hata mmoja anayecheza nje.
Amesema sababu ya kufanya hivyo ni kuanza kuwaandaa wachezaji wa kucheza michuano ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za CHAN, ambazo huhusisha nyota wanaocheza ligi za nyumbani kwao pekee.
“Siyo Kavumbangu tu, kuna wachezaji wengine wazuri tu wanaocheza hadi Ulaya, lakini sikuwachukua, kwa sababu siwahitaji katika mipango yangu ya sasa, bado ni wachezaji wa timu ya taifa na naheshimu uwezo wao,”alisema Mohamed.
Kavumbangu alisajiliwa Agosti mwaka huu Yanga akitokea Atletico ya Burundi, baada ya kung’ara kwenye Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Komnbe la Kagame.
Bila Kavumbangu na mastaa wengine wa nje, ikiongozwa na mkongwe Suleiman Ndikumana anayechezea Inter Stars ya nyumbani kwao kwa sasa, Burundi iliichapa Somalia mabao 5-1 jana katika mchezo wa Kundi B wa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge.
Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Mandela, Namboole, Kampala, mabao ya Burundi yalifungwa na Chris Nduwarugira dakika ya 35 na 88, Yussuf Ndikumana dakika ya 41 na Suleiman Ndikumana dakika ya 84 na 90, wakati la Somalia lilifungwa na Mohamed Jabril kwa penalti dakika ya 55.

VETTEL AFANIKIWA KUTETEA TAJI LA DUNIA.

DEREVA nyota wa mbio za Langalanga wa timu ya Red Bull, Sebastian Vettel amefanikiwa kushinda taji la dunia la tatu mfululizo kwa tofauti ya alama tatu katika michuano ya Brazil Grand Prix. Katika tukio ambalo mbio hizo ziliathiriwa na mvua, Vettel alipambana na kufanikiwa kumaliza katika nafasi ya sita baada ya kuporomoka mpaka nafasi ya mwisho katika mzunguko wa kwanza kufuatia kupata ajali. Mpinzani wake katika mbio hizo Fernando Alonso wa Ferrari alimaliza katika nafasi ya pili ambapo alikuwa akihitaji Vettel kumaliza chini ya nafasi ya saba ili aweze kunyakuwa taji la dunia. Dereva wa timu ya Force India, Nico Hulkenberg alikatwa alama baada ya gari lake kupoteza mwelekeo na kumgonga Lewis Hamilton wakati akijaribu kumpita dereva huyo wa timu ya McLaren. Vettel anakuwa dereva mdogo zaidi katika historia kushinda mataji matatu ya dunia akizidiwa miaka sita na Ayrton Senna ambaye ndiye dereva watatu kushinda mataji matatu mfululizo.

MBIO ZA UBINGWA BADO HAZIJAISHA - VILANOVA.

MENEJA wa klabu ya Barcelona, Tito Vilanova amesisitiza kuwa mbio za ubingwa wa Ligi Kuu nchini Hispania maarufu kama La Liga bado hazijaisha pamoja na kikosi chake kuongeza pengo la alama 11 na mabingwa watetezi wa ligi hiyo Real Madrid. Barcelona ilifanikiwa kupata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Levante jana usiku na kutumia nafasi baada ya Real Madrid kupoteza mchezo wao wa Jumamosi kwa kufungwa na Real Betis kwa bao 1-0. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Vilanova aliwapongeza wachezaji kwa kuonyesha juhudi na kuihakiikishia ushindi timu lakini akasisitiza kuwa mbio za ubingwa bado kwakuwa wapo Atletico Madrid ambao wanafuatia katika nafasi ya pili kwa tofauti ya alama tatu pekee. Kocha huyo aliendelea kusema kuwa Atletico wameanza msimu vizuri kitu ambacho sio cha kushangaza kwasababu walimaliza msimu uliopita wakiwa katika kiwango cha juu hivyo inabidi kuhakikisha wanelekeza nguvu zao kushinda kila mchezo ili kuendelea kukalia usukani wa La Liga.

"FULECO" MWANASESERE WA KOMBE LA DUNIA 2014.

SHIRIKISHO LA Soka Duniani-FIFA limetoa jina la Fuleco kwa mwanasesere utakaotumika katika michuano ya Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil, neno ambalo waandaji wamesema kuwa linahusu ufahamu wa mazingira. Karibu nusu ya watu zaidi ya milioni 1.7 ambao walipiga kura katika mitandao walichagua jina Fuleco tofauti na mengine yaliyokuwepo katika kinyang’anyiro hicho ya Zuzeco na Amijubi. Utamaduni wa kuwa na mwanasesere katika Kombe la Dunia ulianza mwaka 1966 wakati wa michuano iliyofanyika Uingereza ambayo waliipa jina la World Cup Wille. Toka kipindi hicho wanasesere wamekuwa wakionekana katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 1974 iliyofanyika Ujerumani ambao iliitwa Tip Tap ikimaanisha wavulana wawili wa nchi hiyo, Pique ikimaanisha pilipili katika michuano ya Kombe la Dunia nchini Mexico mwaka 1986 na Zakumi ikimaanisha Chui jina ambalo lilitumika katika michuano ya Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini. Fuleco anatarajiwa kuonekana rasmi jijini Sao Paulo baadae wiki hii katika sherehe za upangaji wa ratiba ya michuano ya Kombe la Shirikisho ambayo itafanyika Juni mwakani.

CAF KOMBE la SHIRIKISHO: AC Leopards MABINGWA!

Klabu ya Congo, AC Leopards, leo wametwaa Ubingwa wa Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho walipoichapa Djoliba ya Mali Bao 2-1 huko Dolisie, Congo katika Mechi ya pili ya Fainali.
Katika Mechi ya kwanza ya Fainali iliyochezwa huko Mjini Bamako, Mali, Timu hizi mbili zilitoka sare ya Bao 2-2.
Hii ni mara ya 4 kwa Klabu hizi kukutana Msimu huu kwani walikuwa pamoja kwenye Kundi B la Mashindano haya ambapo AC Leopards walitoka sare 1-1 Mjini Bamako, Mali na kushinda 3-0 waliporudiana Nchini Congo.
Djoliba ndio waliomaliza Washindi wa Kundi B na AC Leopards kushika nafasi ya Pili.
Katika Nusu Fainali, AC Leopards na Djoliba, zilizitupa nje Klabu za Sudan kwa Djoliba kuibwaga Al Hilal kwa Mikwaju ya Penati na AC Leopards kuishinda Al Merreikh Nchini Congo na kutoka sare waliporudiana Nchini Sudan.
+++++++++++++++++++++
NUSU FAINALI:
Novemba 2: Al Hilal 2 Djoliba 0
Novemba 4: AC Leopards 2 Al Merreikh 1
Novemba 10: Al Merreikh 0 AC Leopards 0 [Jumla Mabao: Leopards 2 Al Merreikh 1]
Novemba 11: Djoliba 2 Al Hilal 0 [Penati: Djoliba 8 Al Hilal 7]
+++++++++++++++++++++
Mshindi wa Kombe la Shirikisho atapambana kugombea CAF Super Cup na Klabu Bingwa ya Afrika Al Ahly ambayo iliibwaga Esperance kwenye Fainali Wiki iliyopita.
 
SNEIDJER SASA NJIA NYEUPEE KUTUA MAN UNITED, ATIBUANA NA INTER MILAN AFUNGIWA VIOO

On the move? Wesley Sneijder has been told he will not play for Inter Milan until he takes a pay cut

KLABU ya Manchester United sasa imekaa mkao wa kula baada ya Wesley Sneijder kuambiwa hawezi kucheza Inter Milan tena hadi akubali kupunguziwa mshahara wake wa pauni 200,000 kwa wiki.
Kiungo huyo Mholanzi, amegoma kupunguziwa mshahara Inter na Mkurugenzi wa klabu hiyo, Marco Branca amesema hatahusishwa kwenye mipango ya klabu hiyo akubali kupunguziwa mshahara.
Sneijder, ambaye aliiongoza Inter chini ya kocha Jose Mourinho kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa na ya nyumbani mwaka 2010, alikuwa anatakiwa na klabu kadhaa ikiwemo Man United, lakini Sir Alex Ferguson aliamua kuachana naye kutokana na mshahara mkubwa alioutaka. 
Lakini sasa kuna uwezekano Mholanzi huyo akatua United January.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, alisaini mkataba mpya wa miaka mitano wenye mshahara huo mnono wa pauni 200,000 kwa wiki mwaka 2010, lakini Inter hivi sasa iko katika mpango wa kupunguza bajeti yake na matokeo yake ni pamoja na kumuuzaa kipa Julio Cesar kwenda QPR msimu huu.
Branca ametoa taarifa kuhusu Sneijder, ambaye ametemwa kwenye kikosi kinachomenyana na Parma leo, katika tovuti ya klabu hiyo.

KOCHA WA RWANDA ERICK NSHIMIYIMANA ANASEMA KILIMANJARO STARS HAIKAMATIKI AITABIRIA UBINGWA.

Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Rwanda(Amavubi) Erick Nshimiyimana amesema ameiangalia kwa makini timu ya taifa ya Tanzania Bara(Kilimanjaro Stars) na kutamka maneno haya "Hii haikamatiki".
 
Nshimiyimana alitoa kauli hiyo nzito baada ya kuishuhudia Kilimanjaro Stars ikiifunga Sudan mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza wa michuano ya chalenji uliopigwa hapo jana kwenye uwanja Namboole jijini Kampala.
Amekaririwa akimuuliza kwa mshangao mwandishi wa habari hii,
"Hivi huyu kocha ana muda gani?(mwandishi wa habari hii alimjibu kuwa hata mwaka hajafikisha tangu alipokabidhiwa timu ndipo alipoendelea kusema.
"Hii timu imebadilika sana kama itaendelea kucheza hivi hakuna ubishi kwamba itafika mbali na huenda ikachukua hata ubingwa,".alisema Nshimiyimana.

Nshimiyimana ambaye pia ni kocha wa timu ya APR  ya Rwanda amesema, Kilimanjaro Stars imekamilika kila idara kuanzia ufundi hadi fiziki ya wachezaji.
 
"Nimewaangalia kwenye fiziki na hata mbinu wako vizuri na hata wanapotengeneza mashambulizi unaona kabisa yamepangiliwa,"
 
Kilimanjaro Stars hapo jana walianza vema kampeni yake ya kuwania taji la Chalenji baada ya mabao mawili ya kipindi cha kwanza yaliyofungwa na John Raphael Bocco kuiwezesha kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sudini mchezo ambao ulikuwa ni wa pili wa kundi la B wa michuano ya kombe la Chalenji mchezo ambo ulifanyika katika uwanja wa Namboole. 

MICHUANO YA WACHEZAJI WA NDANI (CHAN) YAMKOSESHA CHALENJI KAVUMBAGU

Kocha wa timu ya taifa ya Burundi, Lotfy Mohamed amewatema kwenye kikosi chake kinachoshiriki michuano ya chalenji maprofesheno wote akiwemo mshambuliaji Didier Kavumbagu.
Kavumbagu pamoja na nyota wengine wa Burundi wanaocheza soka la kulipwa katika nchi mbalimbali kwa lengo la kutengeneza kikosi cha michuano ya wachezaji wa ndani (CHAN).
 
Lotfy hakuwatumia wachezaji hao katika kikosi cheke kilichoiangamiza Somalia kwa mabao 5-1 ambao ulikuwa mchezo wake wa ufunguzi wa michuano ya Chalenji katika dimba la Namboole jijini Kampala hapo jana.

Akizungumza jijini Kampala ,Lotfy Mohamed amesema uamuzi wake wa kuwatema mapro hao umelenga kutumia michuano ya chalenji kukipika kikosi chake kitakachoshiriki mechi za kusaka nafasi ya kufuzu kushiriki fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani(CHAN).
 
Desemba 16 Burundi itacheza mechi ya CHAN dhidi ya Kenya hivyo kocha huyo ameona awaache wachezaji ambao hatawatumia katika CHAN kwa lengo la kutengeneza kikosi kupitia michuano ya Chalenji.

Amekaririwa akisema

"Siyo yeye Kavumbagu peke yake, kuna Hamis Cedric ambaye ni tegemeo kabisa kwenye timu ya taifa na wengime wengi ambao nimewacha kwa mtazamo huo wa kuhakikisha tunafanya vizuri katika mechi zetu za kusaka nafasi ya kushiriki  fainali za CHAN,".
 
Akizungumzia nafasi ya timu yake katika michuano ya chalenji inayoendelea na hasa baada ya kuanza harakati zake kwa ushindi mnono wa mabao 5-1 dhidi ya Somalia, Lotfy Mohamed amesema atatumia faida ya kuzifahamu kwa kina Tanzania Bara(Kilimanjaro Stars) na Sudan kuweza kuibuka na ushindi na kufuzu kwa hatua ya robo fainali pale atakapokutana nazo.
 
Barca yaichapa Levante 4-0, Messi apiga 2, bado 3 kumfikia Gerd Muller!!

>>SERIE A: JUVE yachapwa 1-0 na AC MILAN!!
>>BUNDESLIGA: Mabingwa Dortmund kuwasogelea vinara Bayern??
>>WIKIENDI ni Dortmund v Bayern Munich!!
MESSI_ASHANGILIA_GOLIAndreas Iniesta alimtengenezea Lionel Messi Bao 2, alimlisha Cesc Fabregas kufunga moja na yeye mwenyewe kupachika Bao moja na kuifanya Barcelona iwachape Levante 4-0 na kuzidi kuyoyoma kileleni mwa La Liga huku Messi sasa akiwa na Bao 82 kwa Mwaka huu 2012 na kubakisha Bao 3 kuifikia rekodi ya Mjerumani Gerd Muller ya Bao 85 kwa Mwaka mmoja wa Kalenda aliyoiweka Miaka 40 iliyopita.
+++++++++++++++++
MAGOLI:
Levante 0
Barcelona 4
-Messi: Dakika ya 47 & 52
-Iniesta: 57,
-Fábregas: 63
+++++++++++++++++
Barca sasa wapo Pointi 3 mbele ya Timu ya Pili Atletico Madrid ambao jana waliicharaza Sevilla Bao 4-0 na wapo Pointi 11 mbele ya Timu ya 3 Real Madrid ambao juzi walifungwa 1-0 na Real Betis.
+++++++++++++++++++++++
LA LIGA
MSIMAMO:
[Timu za Juu]
1 Barcelona Mechi 13 Pointi 37
2 Atletico Madrid Mechi 13 Pointi 34
3 Real Madrid Mechi 13 Pointi 26
4 Malaga Mechi 13 Pointi 22
5 Real Betis Mechi 13 Pointi 22
6 Levante Mechi 13 Pointi 20
+++++++++++++++++++++++
Kwa Msimu huu, Messi ameshafunga Bao 19 kwenye La Liga na kwa Mwaka 2012 ameifungia Barca Bao 70 na Timu ya Taifa ya Argentina Bao 12.
RATIBA/MATOKEO:
Jumapili Novemba 25
Espanyol 0 Getafe 2
Athletic Bilbao 1 Deportivo La Coruna 1
Atletico Madrid 4 Sevilla 0
Levante 0 Barcelona 4
Jumatatu Novemba 26
Real Zaragoza v Celta Vigo
Ijumaa Novemba 30
Osasuna v Rayo Vallecano
Jumamosi Desemba 1
Getafe v Malaga
Valencia v Real Sociedad
Barcelona v Athletic Bilbao
Real Madrid v Atletico Madrid
BUNDESLIGA: Mabingwa Dortmund kuendeleza ushindi??
Jumanne Mabingwa watetezi Borussia Dortmund wataingia Uwanjani wakiwa kwao kupambana na Fortuna Dusseldorf huku wakitegemea kupata ushindi wao wa 5 mfululizo wakiwafukuza vinara wa Bundesliga Bayern Munich ambao wako Pointi 9 mbele yao na ambao Jumatano wako ugenini kucheza na Freiburg.
Mechi hizo za Dortmund na Bayern Munich ni za utanguliza tu kwani Wikiendi inayokuja, Jumamosi Desemba Mosi, na wanakutana uso kwa uso.
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO-Timu za Juu:
[Kila Timu imecheza Mechi 13]
1 Bayern Munich Pointi 34
2 Borussia Dortmund 25
2 Schalke 24
3 Eintracht Frankfurt 24
4 Bayer Leverkusen 24
5 Freiburg 19
6 Werder Bremen 18
7 Hannover 17
+++++++++++++++++++++++
RATIBA
Jumanne Novemba 27
Borussia Dortmund v Fortuna Dusseldorf
Hamburger v Schalke
Hannover v SpVgg Gr. Furth
Eintracht Frankfurt v Mainz
Jumatano Novemba 28
Stuttgart v Augsburg
Werder Bremen v Bayer Leverkusen
Freiburg v Bayern Munich
Nuremberg v Hoffenheim
Ijumaa Novemba 30
Fortuna Dusseldorf v Eintracht Frankfurt
SERIE A: AC MILAN yawatungua Mabingwa JUVE 1-0!
Jumapili, Juventus wameikosa nafasi ya kupaa juu zaidi kileleni mwa Serie A na kuwa Pointi 7 mbele baada ya Penati ya Robinho ya Dakika ya 31 kuwapa ushindi wa Bao 1-0 Timu inayosuasua AC Milan.
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO-Timu za Juu:
1 Juventus Mechi 14 Pointi 32
2 Fiorentina Mechi 14 Pointi 28
3 Inter Milan Mechi 13 Pointi 28
4 Napoli Mechi 13 Pointi 27
5 AS Roma Mechi 14 Pointi 23
6 Catania Mechi 14 Pointi 19
7 AC Milan Mechi 14 Pointi 18
+++++++++++++++++++++++
Hiki ni kipigo cha pili kwa Mabingwa watetezi Juventus Msimu huu baada ya kuumaliza Msimu uliopita bila kufungwa hata Mechi.
Wiki mbili zilizopita walitandikwa 3-1 na Inter Milan.
RATIBA:
SERIE A
Jumatatu Novemba 26
Cagliari v Napoli
Parma v Inter Milan
Jumatano Novemba 27
Lazio v Udinese
Ijumaa Novemba 30
Catania v AC Milan
Jumamosi  Desemba 1
Juventus v Torino
Jumapili Desemba 2
Napoli v Pescara
Bologna v Atalanta
Inter Milan v Palermo
Lazio v Parma
Udinese v Cagliari
 
FIFA KOMBE la MABARA 2013: Droo kufanyika Desemba MOSI !

FIFA_CONFEDERATION_CUP_2013Mji wa Sao Paulo huko Brazil uko kwenye heka heka ya kupokea Wageni kwa ajili ya Droo ya Michuano ya FIFA ya Kombe la Mabara itakayofanyika Desemba Mosi kwa ajili ya Mashindano hayo yatakayochezwa Nchini humo kuanzia Juni 15, 2013 hadi Juni 30, 2013 na kushirikisha Nchi 8 ambazo ni Wenyeji Brazil, Mabingwa wa Dunia Spain, Bingwa wa Asia Japan, Bingwa CONCACAF Mexico, Marekani ya Kusini ni Uruguay, Bingwa wa Kanda ya Nchi za Oceania, Tahiti, Italy itakayowakilisha Ulaya pamoja na Mabingwa Bara la Afrika, ambao watajulikana Tarehe 10 Februari 2013 baada ya Fainali za AFCON 2013 huko Afrika Kusini.
FIFA ilishatangaza Miji ambayo itatumika kwa ajili ya Mashindano hayo ambayo ni Brasilia, Belo Horizonte, Fortaleza, Rio de Janeiro, Recife na Salvador.
Miongoni mwa Wageni waalikwa watakaouhudhuria Droo hiyo ni Makocha wa Nchi zitakazoshiriki ambao ni Cesare Prandelli (Italy), Alberto Zacceroni (Japan), Jose Manuel de la Torre (Mexico), Vicente del Bosque (Spain), Eddy Etaeta (Tahiti) na Oscar Tabarez (Uruguay).
Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Valcke, ndie atakaeendesha Droo hiyo.

BPL: Man United yabaki JUU, Chelsea v City ngoma ngumu!!

>>LIGI kuendelea katika ya Wiki hii!!
BPL_LOGOMabingwa watetezi Manchester City wakicheza huko Stamford Bridge dhidi ya Chelsea iliyokuwa na Meneja mpya Rafael Benitez akianza himaya kwa Mechi yake ya kwanza na kukaribishwa kwa kuzomewa na Mabango ya Mashabiki wasiomtaka walitoka sare 0-0 na kuwabakiza Manchester United kileleni wakiwa Pointi moja mbele ya City, walio nafasi ya 2, na Pointi 5 mbele ya Chelsea walio nafasi ya 4.
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO-Timu za Juu tu:
1 Man United Mechi 13 Pointi 30
2 Man City Mechi 13 Pointi 29
3 WBA Mechi 13 Pointi 26
4 Chelsea Mechi 13 Pointi 25
5 Everton Mechi 13 Pointi 21
6 Arsenal Mechi 13 Pointi 20
7 Tottenham Mechi 13 Pointi 20
8 West Ham Mechi 13 Pointi 19
9 Swansea Mechi 13 Pointi 17
10 Fulham Mechi 13 Pointi 16
+++++++++++++++++++++++
MATOKEO:
Jumapili Novemba 25
Swansea 0 Liverpool 0
Southampton 2 Newcastle 0
Chelsea 0 Man City 0
Tottenham 3 West Ham 1
+++++++++++++++++++++++
CHELSEA 0 MAN CITY 0
Uwanjani Stamford Bridge, katika Mechi ya kwanza ya Meneja mpya wa Chelsea Rafael Benitez, aliepokewa kwa kuzomewa na mabango ya kumpinga, Chelsea walitoka sare ya 0-0 na matokeo haya yamewafanya Manchester United wabakie kileleni.
VIKOSI:
Chelsea: Cech; Azpilicueta, Ivanovic, Luiz, Cole; Ramires, Mikel; Mata, Oscar, Hazard; Torres.
Manchester City: Hart, Zabaleta, Kompany, Nastasic, Kolarov, Barry, Y Toure, Silva, Milner, Dzeko, Aguero
Refa: Chris Foy
TOTTENHAM 3 WEST HAM 1
Bao mbili za Jermaine Defoe na moja la Gareth Bale leo zimewapa ushindi Tottenham wa Bao 3-1 walipocheza Uwanjani White Hart Lane na West Ham.
Bao la West Ham lilifungwa na Andy Carroll.
VIKOSI:
Tottenham Hotspur: Hugo Lloris, Steven Caulker,  Jan Vertonghen, Kyle Walker, Michael Dawson, Sandro, Gareth Bale, Clint Dempsey, Aaron Lennon, Tom Huddlestone, Jermain Defoe
West Ham United: Jussi Jääskeläinen, Joey O'Brien, James Tomkins, Winston Reid, George McCartney, Modibo Maiga, Kevin Nolan, Mohamed Diamé, Gary O'Neil,  Mark Noble, Andy Carroll
Refa: Andre Marriner
LIVERPOOL O SWANSEA CITY 0
Brendan Rodgers, Meneja wa Liverpool, leo alirudi Uwanja wa Liberty kucheza na Timu yake ya zamani Swansea City lakini akaambulia sare ya 0-0.
Jose Enrique wa Liverpool alifunga bao lakini lilikataliwa kwa kuwa Ofsaidi na shuti la Winga wao Raheem Sterling kugonga mwamba.
Nafasi bora ya Swansea ilimwangukia Ashley Williams ambae kichwa chake kiliokolewa na Joe Allen kwenye mstari wa goli.
Matokeo haya yamewainua Swansea na kukamata nafasi ya 8 na Liverpool wapo nafasi ya 11.
Hii ni Mechi ya 8 ya Ligi kwa Liverpool kutoka Uwanjani bila kufungwa na Swansea wamepoteza Mechi moja tu kati ya 7 walizocheza mwisho.
VIKOSI:
Swansea: Tremmel; Rangel, Williams, Chico, Davies; Routledge, Britton, de Guzman, Hernandez; Michu, Shechter.
Akiba: Cornell, Monk, Tiendalli, Agustien, Ki, Dyer, Lita.
Liverpool: Reina; Johnson, Skrtel, Agger, Enrique; Allen, Henderson, Gerrard; Downing, Sterling, Suarez.
Akiba: Jones, Carragher, Coates, Suso, Shelvey, Cole, Sahin.
Refa: Jon Moss
SOUTHAMPTON 2 NEWCASTLE O
Southampton wamejikwamua kutoka lile eneo denja la Timu 3 za mkiani ambazo hushushwa Daraja mwishoni mwa Msimu kwa kuichapa Newcastle Bao 2-0.
Bao za Southampton zilifungwa na Adam Lallana na Ramirez kupiga Bao la pili.
VIKOSI:
Newcastle: Krul, Simpson, Williamson, S. Taylor, Santon, Gutierrez , Tiote, Anita, Ferguson, Cisse, Ba
Akiba: Harper, Tavernier, Perch, Bigirimana, Marveaux, Sammy Ameobi, Ranger.
Southampton: Gazzaniga, Clyne, Fonte, Yoshida, Shaw, Puncheon, Schneiderlin, Cork, Lallana, Ramirez, Lambert
Akiba: K. Davis, Hooiveld, S. Davis, Rodriguez, Ward-Prowse, Mayuka, Guly.
+++++++++++++++++++++++
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumanne Novemba 27
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Sunderland v QPR
[SAA 5 Usiku]
Aston Villa v Reading
Jumatano Novemba 28
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Chelsea v Fulham
Everton v Arsenal
Southampton v Norwich
Stoke v Newcastle
Swansea v West Brom
Tottenham v Liverpool
Man United v West Ham
[SAA 5 Usiku]
Wigan v Man City