Monday, November 5, 2012

RHINO RANGERS WAWATANDIKA BAO 2-0 MWADUI NA KUCHUKUA ALMAS ZAO HII LEO

ligi daraja la kwanza imeendelea hii leo katika uwanja wa ALLY HASSAN MWINYI kwa mchezo mmoja wa raundi ya tano kati ya RHINO RANGERS NS MWADUI FC na rhino rangers wametoka kifua mbele kwa mabao 2-0 mabao yaliyofungwa na ALLY NUMBA dk 18 na VICTOR HAGAYA dk ya 86 dhidi ya wachimba almasi mwadui ya shinyanga . na wachezaji wawili wa mwadui mapunda ulanga na aman abdalah walitolewa kwa kadi nyekundu kwa mchezo mbaya na mwamuzi SAID SAID kutoka singida na   siku ya jumamosi kwa michezo minne katika miji ya kigoma ,tabora,dodoma,na mara,,kanembwa JKT vs atakuwa na pamba katika dimba la lake tanganyika kigoma...polisi dodoma vs rhino rangers katika dimba la jamhuri dodoma,,,polisi tabora vs mwadui katika dimba la ally hassan mwinyi,,na mchezo wa mwisho utakuwa kati ya polisi mara vs moran fc katika dimba lakarume mara kule.



Raundi ya tano ya ligi daraja la kwanza FDLjana iliendelea    katika miji mitatu ,tabora,dodoma na mwanza katika KUNDI C .katika uwanja wa ally hassan mwinyi kulikuwa  na mechi kati ya polisi tabora na vibonde wa rhino rangers timu ya kanembwa FC ambayo mchezo uliopita ilitandikwa kwa mara ya kwanza toka ligi ianze na wanajeshi wa tabora kwa bao 3-1.  Na timu ya kanembwa wameibamiza kwa hasira timu ya maafande wa polisi kwa mabao 4-1 mabao ya kanembwa JKT yamefungwa na ally bilali mwese aliyekuwa mwiba kwa mabeki wa polisi tabora kafunga mabao 3 dakika ya 46,60,na 89 na bao la nne limefungwa na bulian akilimali dakika ya 49.


Na bao la kufutia machozi la polisi tabora limefungwa na ibrahimu musa dakika ya 86 na hadi dakika 90 za mchezo zinamalizika refarii salehe mmang'ora anapuliza kipenga cha mwisho timu ya JKT kanembwa ilitoka kifua mbele ya mabao 4-1 na kuendelea kuongoza kundi c ikifikisha jumla ya pointi 12 kwa michezo 5.


Kule dodoma kulikuwa na mchezoo kati ya maafande wa polisi dodoma na polisi mara  na wametoka sare ya bila kufungana 0-0 na mchezo wa mwisho ulikuwa kati ya pamba na morani FC katika dimba la CCM KIRUMBA mwanza na matokeo bado hatujayapata.Na kesho novemba 8 kutakuwa na mchezo mmoja kati ya rhino rangers na mwadui katika dimba la ally hassan mwinyi na ni mchezo wa mwisho wa raundi ya tano katika kundi C.



MATOKEO TOKA LIGI IANZE oktoba 24
===Kanembwa vspolisi dodoma 3-0
===pamba vs polisi mara 3-2
===rhino rangers vs polisi tabora 2-1
mwadui vs moran 3-0

oktoba 27
====polisi tabora vs polisi dodoma 0-1
====mwadui vs polisi mara 3-0
====kanembwa JKT vs moran 2-0
====pamba vs rhino rangers 1-1

oktoba 31
====polisi mara vs rhino rangers 0-0
====moran vs polisi tabora 1-1
====polisi dodoma vs pamba2-0
====kanembwa vs mwadui 3-2

novemba 4
===polisi mara vs polisi tabora 1-1
===moran vs polisi dodoma1-1
===rhino rangers vs kanembwa JKT 3-1
===mwadui vs pamba...2-0......

AZAM YAFUKUZA KIPA NA MABEKI KWA TUHUMA ZA KUHUJUMU DHIDI YA SIMBA, YANGA

Said Morad, kweli kahujumu timu?

AZAM FC imewasimamisha wachezaji wake watatu wa safu ya ulinzi, kipa Deo Munishi ‘Dida’ na mabeki Said Mourad na Erasto Nyoni kwa tuhuma za kuihujumu timu hiyo katika mechi zake za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya vigogo Simba na Yanga hivi karibuni.
Azam ilifungwa na Simba mabao 3-1 Oktoba 27, mwaka huu kabla ya kufungwa mabao 2-0 na Yanga Novemba 4, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mechi za Ligi Kuu.
Baada ya kufungwa na Simba, Azam FC ilimfukuza kocha wake Mserbia, Boris Bunjak na kumrejesha Muingereza, Stewart Hall.
Habari kutoka ndani ya Azam zimesema kwamba baada ya kupata taarifa hizo, uongozi ulizifanyia kazi taratibu na kujiridhisha kabisa wachezaji hao watatu walikula njama za kuihujumu timu katika mechi hizo.
Kwa sababu hiyo, uongozi kwanza umewasimamisha wachezaji hao na hatua zaidi zitafuatia baadaye.
Hata hivyo, Dida hakucheza mechi hata moja kati ya hizo, kwani Oktoba 27, kikosi cha Azam kilikuwa; Mwadini Ali, Ibrahim Shikanda, Samir Hajji Nuhu, Said Mourad, Aggrey Morris, Abdulhalim Humud, Jabir Aziz aliyempisha Abdi Kassim, Himid Mao aliyempisha Kipre Balou, John Bocco ‘Adebayor’ aliyempisha Khamis Mcha ‘Vialli’, Kipre Herman Tcheche na Salum Abubakar.
Siku hiyo, Azam walitangulia kufunga dakika ya nne, kupitia kwa Adebayor ambaye alimtoka beki Mkenya Paschal Ochieng na kumchambua Juma Kaseja, kabla ya Felix Mumba Sunzu Jr., kuisawazishia Simba dakika mbili baadaye, akiunganisha kwa kichwa krosi maridadi ya Mrisho Khalfan Ngassa kutoka wingi ya kulia.
Okwi aliifungia Simba bao la pili dakika ya 40, baada ya kutokea kizaazaa langoni mwa Azam kufuatia mpira uliopigwa langoni mwa timu hiyo na Mwinyi Kazimoto na dakika tano tu tangu kuanza kipindi cha pili, Mganda huyo tena akawainua vitini mashabiki wa Simba, akifumua shuti la umbali wa mita 19, baada ya kuwatoka mabeki wa Azam.
Katika mechi na Yanga, kikosi cha Azam kilikuwa; Mwadini Ally, Erasto Nyoni aliyempisha Samir Hajji Nuhu, Ibrahim Shikanda, Aggrey Morris na Said Mourad, Jabir Aziz aliyempisha Ibrahim Mwaipopo, Kipre Balou, Khamis Mcha ‘Vialli’ aliyempisha Abdi Kassim ‘Babbi’, Salum Abubakar, John Bocco na Kipre Tcheche.
Siku hiyo, mabao ya Yanga yalitiwa kimiani na mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Didier Kvumbangu aliyeunganisha krosi ya Simon Msuva kutoka wingi ya kulia dakika ya tisa na Mganda, Hamisi Kiiza ‘Diego’ dakika ya 68, akiunganisha krosi ya Athumani Iddi ‘Chuji’ kutoka wingi ya kulia.
Habari zaidi zinasema kwamba, uchunguzi unaendelea kufanywa juu ya wachezaji wengine wanaotuhumiwa kuwa katika mkumbo huo wa kuihujumu timu na ikithibitika ni ukweli, watachukuliwa hatua pia bila kujali majina yao.
Azam tayari iko Tanga tangu saa 8:00 mchana wa leo kwa ajili yao ya mchezo wao wa mwisho wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara keshokutwa dhidi ya Mgambo JKT, Uwanja wa Mkwakwani. 

TASWA WAWASHITAKI LIGI KUU MOAT

Mhando kulia akiwa na Mwenyekiti wake, Pinto

CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kimeamua kulipeleka kwa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), suala la kuzuiwa kwa vituo vya Televisheni na Redio nchini kutangaza moja kwa moja michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara pamoja na wapiga picha za Televisheni kuchukua picha kwa ajili ya kutumia kwenye habari.
Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando amesema  leo kwamba, hatua hiyo ina lengo la kuomba mwongozo kwa chama hicho ambacho ndio kinachomiliki vyombo vya habari kuhusiana na suala hili ambalo limekuwa likilalamikiwa kwa kiasi kikubwa na wanachama wake.
Tayari TASWA imefanya mazungumzo ya awali na MOAT, ambayo imeridhia iandikiwe barua rasmi ili jambo hilo lijadiliwe kwenye vikao vyake na baada ya hapo TASWA itapewa mwongozo ambao itautoa kwa waandishi wa habari za michezo.
“Kwa kuwa Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto pia ni mjumbe wa MOAT, basi suala hilo tunaamini litafanyiwa kazi haraka iwezekanavyo, hivyo tunawaomba waandishi wa habari za michezo waendelee kuwa watulivu na wavumilivu kipindi hiki na wafanye majukumu yao kama kawaida,”alisema Mhando.
“Siku zote chama chetu kimekuwa na uhusiano mzuri na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na wadau wengine wote na TASWA haitaki ifike mahali iwe na mgogoro na chama chochote cha michezo, lakini pia haitakuwa tayari kuona wanachama wake wakishindwa kutekeleza majukumu yao,”aliongeza.
Wiki iliyopita kulifanyika kikao cha Kamati ya Ligi na baadhi ya klabu zinazoshiriki ligi hiyo na kuzuia Televisheni na Redio kutangaza moja kwa moja michezo ya Ligi Kuu pamoja na wapiga picha za Televisheni kuchukua picha kwa ajili ya kutumia kwenye habari.
Katika kikao hicho ambacho Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto  alihudhuria kulitoka maelezo mbalimbali ambayo baadhi ya Wana Habari hawakubaliani nayo na wamekuwa wakitaka TASWA ichukue hatua uamuzi mgumu.
Mhando amesema sekreterieti ya TASWA imeona si vizuri kukurupuka kuchukua uamuzi wowote ule kwa sasa kwani yenyewe haina chombo cha habari, lakini wanaofanya kazi kwenye vyombo vya habari ndiyo wanachama wake, hivyo amesema itawasilisha MOAT maazimio ya kikao cha Kamati ya Ligi kuhusiana na jambo hili, tuna hakika tutalimaliza.
Kuhusu Mkutano Mkuu wa TASWA, Mhando amesema Jumatano ya Novemba 16, mwaka huu Kamati ya Utendaji ya TASWA itakutana Dar es Salaam kupitia ajenda za Mkutano huo na Novemba 18 Mwenyekiti wa TASWA, Juma Abbas Pinto atakutana na Waandishi Habari kutangaza mdhamini wa mkutano huo pamoja na tarehe rasmi na mahali utakapofanyika.
“Kutokana na kuandaliwa kwa ajenda mpya ya kuboresha chama na maslahi ya wanachama wake, TASWA inaendelea kutafuta wadhamini zaidi ili kuufanya mkutano huo uwe wa siku mbili,”alisema Mhando.

BALOZI WA HENNESSY KUTUA JUMATATU KUTOKA PARIS

Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya ujio wa Balozi wa kampuni ya Hennessy, bwana Cyrille Auriol, maandalizi ya mapokezi yake yamepamba moto. Balozi Auriol atatua Dar es Salaam jumatatu akitokea Paris kwa ziara ya siku tatu kabla ya kuelekea Nairobi kwa muendelezo wa ziara yake nchi za Afrika Mashariki.
Akiwa Dar es Salaam Balozi Auriol atahudhuria matukio mbalimbali
maalum ya chakula cha jioni na uonjaji wa kinywaji hicho ambazo
zimeandaliwa ili kuwazawadia watumiaji wa kinywaji hicho nchini ambao sasa wanafurahia kampeni ya kinywaji hicho iitwayo ‘ Flaunt Your Taste’.

MSHINDI EBSS KUPATIKANA KESHO DIAMOND JUBILEE

Mkurugenzi wa kampuni ya Benchmark Productions Limited, Ritha Poulsen akizungumza na Waandishi wa Habari mchana wa leo ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam kuhusu shindano Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS) litakalofanyika kesho kwenye ukumbi huo huo wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam. Wengine kulia kwake na kushoto ni miongoni mwa washiriki wa shindano hilo walioingia fainali.


Mkurugenzi wa kampuni ya Benchmark Productions Limited, Ritha Poulsen akizungumza na Waandishi wa Habari mchana wa leo ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam kuhusu shindano Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS) litakalofanyika kesho kwenye ukumbi huo huo wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam. Wengine kulia kwake na kushoto ni miongoni mwa washiriki wa shindano hilo walioingia fainali.

Washiriki wa EBSS Salma Yussuf Abushir, Nsami Nkwabi, NshomaNghangasamala, Walter Chilambo na Wababa Mtuka wakiwa na Ritha Poulsen. Je, nani ataondoka na kitita cha Sh. Milioni 50 kesho?    

BAADA ya miezi mitatu ya mchuano mkali hatimaye mshindi wa shindano la kuimba la Epiq Bongo Star Search atapatikana leo katika fainali kali inayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
Mshindi atajinyakulia shilingi milioni hamsini pamoja na mkataba wa kurekodi kutoka kwa wadhamini pekee wa shindano hilo kampuni ya simu za mikononi ya Zantel.
Washiriki walioingia kwenye fainali hizo ni EBSS06: Nsami Nkwabi, EBSS07: Nshoma Ng’hangasamala, EBSS09: Salma Abushiri, EBSS11: Wababa Mtuka (Dar) na EBSS12: Walter Chilambo (Dar).
Wasanii watakaoburudisha ni Rich Mavoko, Omi Dimpoz, Ben Paul, Lina, Amini, Mzee Yusuf, Haji Ramadhan, Mwasiti, Ditto, Laila Rashid, Linex na Barnaba.   
Akizungumzia fainali hizo, jaji mkuu wa shindano hilo, Madam Ritha Paulsen, aliwashukuru watanzania kwa ushirikiano waliowapa toka shindano limeanza mpaka leo wanahitimisha kwa fainali.
 ‘Kama mlivyoona shindano hili toka lilipoanza mwaka huu limekuwa la kimataifa zaidi, hivyo tarajieni fainali za kipekee na zitakazoweka rekodi kwenye tasnia ya burudani na ni matarajio yetu kwamba mshindi wa usiku huu atafanya vizuri kwenye muziki’ alisema Madam Ritha.
Kwa upande wake Afsa Biashara mkuu wa Zantel, bwana Sajid Khan alisisitiza utayari wa kampuni yake katika kuwaendeleza vijana wa kitanzania kufikia ndoto zao lakini aliomba pia wadau wengine wa sanaa kuwapa washirikiano washiriki wote.
‘Zantel, pamoja na kumpa mshindi zawadi ya milioni hamsini lakini pia tutampa mkataba wa kurekodi, na washiriki wengine watapewa nafasi ya kurekodi wimbo mmoja mmoja lakini juhudi hizi zitafanikiwa ikiwa tutapata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wadau’ alisema Khan.
Shindano hilo limekuwa likirushwa hewani na kituo cha runinga cha ITV, lilianza mwezi wa sita kwa kufanya usaili mikoani, ambalo mwaka huu lilienda mikoa nane-Mbeya, Dodoma, Mwanza, Tanga, Dar es Salaam, Zanzibar, Lindi pamoja na Arusha.
Kwa mara ya kwanza pia shindano hilo liliweza kufanya usaili kwa njia ya simu ili kuwapa nafasi vijana zaidi ambao hawakufikiwa na majaji.
Epiq Bongo Star Search ni kipindi cha televisheni ambacho huibua vipaji vya muziki kwa vijana wa kitanzania na kinatengenezwa na Benchmark Productions, na toka kimeanzishwa mwaka 2006 kimekuwa ni kipindi kinachotazamwa zaidi Afrika mashariki kwa kufikisha watu milioni 3 wanaotazama kwa kila kipindi.
Mwaka huu kinadhaminiwa na kampuni ya simu za mikononi ya Zantel, na mshindi atapata zawadi ya shilingi milioni 50 pamoja na mkataba wa kurekodi.

FILAMU YA SHUJAA KUMPONGEZA RAIS KIKWETE KUZINDULIWA DESEMBA

Mtayarishaji wa filamu mpya iitwayo Shujaa, Adam Kasale akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dar es Salaam asubuhi ya leo kuhusu ‘picha hilo’ ambalo limetayarishwa katika kiwango cha juu cha ubora. 

Mwigizaji wa filamu hiyo, Henry Babuu kushoto na Barbra Kalugira kulia, Meneja Masoko na Mratibu wa filamu hiyo

Isakwisa Kanyenyela kushoto na Adam Semkwiji ‘Snare’ na Innocent Nyika, waliohusika katika idara za kitaalamu kwenye kutayarisha filamu hiyo.


KAMPUNI ya Afronode Films, imeandaa filamu maalum iliyopachikwa jina la Shujaa ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kitwete kwa kuhamasisha wananchi kupima ukimwi kwa hiyari.
Akizungumza mjini Dar es salaam leo, Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Barbra Kalugira, alisema kuwa kila kitu kimekamlika ambapo uzinduzi wake utafanyika Desemba mosi ambayo ni siku ukimwi duniani.
Kalugira alisema kuwa katika filamu hiyo itazungumzia watu kwenda kupima kwa hiyari kama alivyofanya Rais wa Tanzania ambaye ndiye kiongozi pekee katika ukanda wa Afrika kuhamasisha kupima ukimwi.
"Ni kitendo cha kumpongeza sana Rais wetu kwa kwenda kupima kwa hiyari na kuhamasisha wananchi wote wajitokeze kupima hivyo tunazindua filamu hiyo ambayo inazungumzia janga la ukimwi na madhara ya kutopima"alisema Kalugira.
Pia Kalugira alisema kuwa katika filamu hiyo itamzungumzia kijana mmoja ambaye alikataa kwenda kupima alipokutana na msichama ambaye ni muadhirika wa ukimwi.
Alisema mpaka kukamilika kwa filamu hiyo jumla ya sh.milioni 35 zimetumika katika kukamilisha.
Kalugira alisema kuwa mpaka wiki ijayo watakuwa wamejua ni wapi watafanya uzinduzi huo.
"Filamu yetu inaitwa Shujaa ambayo tutazindua Desemba Mosi (2012), lakini bado hatujajua ni wapi tutafanyia uzinduzi huo ambao unaujumbe mkubwa kwa jamii kuhusiana na janga zima la Ukimwi"alisema Kalugira.

POULSEN AAMBIWA AMECHEMKA KUTOMUITA BARTHEZ STARS

Barthez

KOCHA wa makipa wa Yanga, Mfaume Athumani Samatta ameshangazwa na kitendo cha kocha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mdenmark Kim Poulsen kuwaita kwenye kikosi cha Bara makipa Juma Kaseja wa Simba na Deo Munishi ‘Dida’ ambao wote hawako vizuri kwa sasa, huku akimuacha Ally Mustafa ‘Barthez’ ambaye yuko vizuri.
Akizungumza  jana, Samatta alisema Dida alidaka mechi mbili tu mwanzoni mwa msimu huu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, lakini baada ya hapo amekuwa akisugua benchi na Mwadini Ally ndiye amekuwa akidaka mechi zote za Azam.
Kuhusu Kaseja, Mfaume alisema kipa huyo kwa sasa hayuko vizuri na amekuwa akiruhusu mabao rahisi sana, tofauti na Barthez ambaye yuko vema mno.
“Barthez huku anapokezana na Yaw Berko kudaka, lakini amedaka mechi zetu tatu mfululizo zilizopita na hajaruhusu bao hata moja, amedaka na Polisi tumeshinda 3-0, amedaka na JKT Oljoro tumeshinda 1-0 na amedaka na Azam tumeshinda 2-0 na anafanya kazi ambayo wananchi wanaiona na wanakubali,”.
“Kwa kweli mimi maoni yangu katika nafasi ya kipa, kocha kachemka sana, tena sana. Ameita hao watu kwa sababu ya mazoea tu, hajazingatia viwango vyao vya sasa, kwangu mimi ilipofikia Barthez ndiye Tanzania One na hakuna ubishi,”alisema Mfaume.       
Mfaume Athumani
Jana Paulsen amemuorodhesha Kaseja katika kikosi cha wachezaji 22 watakaounda kikosi cha Bara, Kilimanjaro Stars kitakachomenyana na Kenya, Harambee Stars katika mchezo wa kirafiki ulio katika kalenda ya FIFA (Shirikisho la Soka la Kimataifa) Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza wiki ijayo.
Mbali na Kaseja wa Simba, Kim aliyepandishwa kutoka timu ya vijana mwaka huu akirithi mikoba ya Mdenmark mwenzake, Jan Borge Poulsen amemuita pia kipa Deogratius Mushi wa Azam FC.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Mwanza jana, Paulsen aliwataja wachezaji wengine ni mabeki Kevin Yondan wa Yanga, Aggrey Morris, Erasto Nyoni wa Azam FC, Issa Rashid, Nassoro Masoud ‘Cholo’, Shomari Kapombe na Amir Maftah wa Simba, wakati viungo ni Salum Abubakar ‘Sure Boy’ wa Azam FC, Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto, Ramadhan Singano ‘Messi’ na Mrisho Ngassa wa Simba, Athuman Iddi ‘Chuji’, Frank Domayo wa Yanga na Shaaban Nditi wa Mtibwa Sugar.
Washambuliaji walioitwa na Paulsen ni John Bocco ‘Adebayor’ wa Azam FC, Simon Msuva wa Yanga, Christopher Edward wa Simba, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wa Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Hata hivyo, Poulsen hakuchukua wachezaji wengi wa Zanzibar kwa sababu nao watakwenda kujiunga na timu ya Zanzibar, inayojiandaa na michuano ya Kombe la CECAFA Tusker Challenge mwishoni mwa mwezi huu mjini Kampala, Uganda. Alisema hicho ndio kikosi anachotarajia kukutumia katika Challenge. Kambi ya timu hiyo itakuwa mjini Mwanza, kwa kuwa ni jirani na Uganda.
KIKOSI KILI STARS;
Makipa; Juma Kaseja (Simba SC) na Deogratius Mushi ‘Dida’
Mabeki; Kevin Yondan (Yanga), Aggrey Morris, Erasto Nyoni (Azam FC), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Nassoro Masoud ‘Cholo’, Shomari Kapombe na Amir Maftah (Simba).
Viungo; Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (Azam FC), Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto, Ramadhan Singano ‘Messi’ na Mrisho Ngassa (Simba), Athuman Iddi ‘Chuji’, Frank Domayo (Yanga) na Shaaban Nditi (Mtibwa Sugar).
Washambuliaji; John Bocco ‘Adebayor’ (Azam FC), Simon Msuva (Yanga), Christopher Edward (Simba), Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wa (TPM, DRC).

 

HODGSON ATEUA Timu England kwa Kirafiki na Sweden!!


>>WAMO Wilshere, Sterling, Shelvey & Osman!!
>>GERRARD kufikisha MECHI 100, ni mmoja Wachezaji 6 tu!!!
GERRARD_ENGLANDAkitangaza Kikosi cha cha Timu ya Taifa ya England ambacho Jumatano ijayo kitacheza na Sweden, Kocha wa England Roy Hodgson amemchukua tena Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere kwenye Kikosi hicho kwa mara ya kwanza baada ya kuwa nje nacho kwa zaidi ya Mwaka mmoja kufuatia kufuatia kuumia kwake.
Pia yumo Beki wa Arsenal Carl Jenkinson ambae aliwahi kuzichezea Timu za Taifa za Vijana za Finland na sasa anasubiri Kibali cha FIFA aruhusiwe kuichezea England.
Wengine walioitwa kwa mara ya kwanza ni Kiungo wa Evertno, Leon Osman, Miaka 31, na pia wamo Chipukizi Wachezaji wa Liverpool Raheem Sterling, 17, na Jonjo Shelvey, 20.
Steven Gerrard, Nahodha wa Liverpool na England, yupo kundini na akicheza hiyo Mechi ya Jumatano na Sweden basi atafikisha Mechi 100 na kujumuika na Wachezaji 6 wengine waliowahi kuichezea England mara 100.
+++++++++++++++++++
MARA 100 ENGLAND:
-Peter Shilton - 125
-David Beckham - 115
-Bobby Moore - 108
-Bobby Charlton - 106
-Billy Wright - 105
+++++++++++++++++++
Uteuzi wa Hodgson una mabadiliko ya Wachezaji 10 na kile kilichocheza Mechi za Mchujo za Kombe la Dunia dhidi ya Ukraine na Poland Mwezi uliopita.
Walioachwa ni Ashley Cole, ambae ameichezea England mara 99, kwa vile ni majeruhi pamoja na Joleon Lescott, Adam Johnson, James Milner, Andy Carroll, Kieran Gibbs, Michael Carrick, Frank Lampard, Alex Oxlade-Chamberlain na Jermain Defoe.
Winga wa Manchester United Ashley Young nae amerudishwa Kikosini baada ya kuzikosa Mechi za Mwezi uliopita alipokuwa kaumia goti lililomweka nje kwa Wiki mbili.
Kikosi hicho cha Ebgland kitapiga Kambi Jijini Manchester kuanzia Jumapili na kisha kusafiri kwenda huko Sweden.
KIKOSI KAMILI:
MAKIPA: Fraser Forster (Celtic), Joe Hart (Manchester City), John Ruddy (Norwich City).
MABEKI: Leighton Baines (Everton), Ryan Bertrand (Chelsea), Gary Cahill (Chelsea), Steven Caulker (Tottenham), Phil Jagielka (Everton), Glen Johnson (Liverpool), Ryan Shawcross (Stoke City), Kyle Walker (Tottenham).
VIUNGO: Tom Cleverley (Manchester United), Steven Gerrard (Liverpool), Aaron Lennon (Tottenham), Leon Osman (Everton), Jonjo Shelvey (Liverpool), Raheem Sterling (Liverpool), Theo Walcott (Arsenal), Jack Wilshere (Arsenal), Ashley Young (Manchester United).
MAFOWADI: Wayne Rooney (Manchester United), Daniel Sturridge (Chelsea), Daniel Welbeck (Manchester United).

Celtic wailaza CHALI BARCA, Man United wasonga, Chelsea wasogea, Bayern waua!


>>MAN UNITED wafuzu, NI TIMU PEKEE YENYE USHINDI MECHI 4!!
UEFA_CHAMPIONZ_LIGI_LOGO-BOMBAZManchester United, ilitoka nyuma kwa Bao 1-0, ikastahamili umeme kukatika, na kuibuka washindi wa Bao 3-1 walipocheza huko Ureno na Braga na kuwachapa Bao 3-1 na kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 kwa kishindo wakiwa Timu pekee kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI iliyoshinda Mechi zake zote 4.
Huko Celtic Park, Glasgow, Celtic leo walitoa kishindo kikubwa kwa kuichapa Barcelona Bao 2-1.
Nako Stamford Bridge, Chelsea iliichapa Shakhtar Donetsk Bao 3-2 na kuweka hai matumaini yao kusonga mbele.
+++++++++++++++++++++++++++++++
MATOKEO:
Jumatano Novemba 7
Juventus 4 FC Nordsjælland 0
Chelsea FC 3 FC Shakhtar Donetsk 2
Valencia CF 4 FC BATE Borisov 2
FC Bayern München 6 LOSC Lille 1
SL Benfica 2 FC Spartak Moskva 0
Celtic 2 Barcelona 1
CFR 1907 Cluj 1 Galatasaray 3
SC Braga 1 Manchester United 3
+++++++++++++++++++++++++++++++
KUNDI H
BRAGA 1 MAN UNITED 3
===============
MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 4]
Manchester United Pointi 12
CFR Cluj 4
Galatasaray 4
Braga 3
===============
MAGOLI:
Braga: Alan, 49, Penati
Man United: Robin van Persie, 80, Rooney, 84, [Penati], Chicharito, 90 
VIKOSI:
Braga: Beto; Leandro Salino, Nuno André Coelho, Douglão, Elderson; Alan, Custodio, Hugo Viana, Rúben Amorim; Rúben Micael; Eder
Akiba: Quim, Mossoró, Hélder Barbosa, Baiano, Ismaily, Djamal, Zé Luis.
Man United: De Gea; Valencia, Smalling, Evans, Evra; Anderson; Nani, Giggs; Rooney; Hernández, Welbeck
Akiba: Lindegaard, Rafael, Ferdinand, Carrick, Young, Van Persie, Cleverley.
Refa: Felix Brych (Germany).

KUNDI G
CELTIC 2 BARCELONA 1
===============
MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 4]
Barcelona Pointi 9
Celtic 7
Spartak Moscow 4
Benfica 3
===============
MAGOLI:
Celtic: Victor Wanyama, 21, Watt, 83
Barcelona: Messi, 90
VIKOSI:
Celtic: Forster; Matthews, Ambrose, Wilson, Mulgrew, Lustig,
Commons, Ledley, Wanyama, Miku, Samaras.
Barcelona: Victor Valdes, Danil Alves, Mascherano, Bartra, Jordi Alba, Xavi, Iniesta, Song, Alexis Sanchez, Messi, Pedro
Refa: N Kuipers (Holland)
KUNDI E
CHELSEA 3 SHAKHTAR DONETSK 2
===============
MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 4]
Shakhtar Donetsk 7
Chelsea Pointi 7
Juventus 6
Nordsjaelland 1
===============
MAGOLI:
Chelsea: Torres, 6, Oscar, 40, Moses, 90 
Shakhtar: Willian, 9 & 47
VIKOSI:
Chelsea: Petr Cech, Branislav Ivanovic, David Luiz, Gary Cahill, Ryan Bertrand; Ramires, John Obi Mikel; Juan Mata, Oscar, Eden Hazard; Fernando Torres
Akiba: Turnbull, Romeu, Moses, Marin, Sturridge, Terry, Azpilicueta.
Shakhtar Donetsk: Andriy Pyatov; Darijo Srna, Olexandr Kucher, Yaroslav Rakytskiy, Razvan Rat; Fernandinho, Tomas Hubschman; Henrik Mkhitaryan, Willian, Alex Teixeira, Luiz Adriano
Akiba: Kanibolotskiy, Stepanenko, Eduardo, Shevchuk, Douglas Costa, Chygrynskiy, Ilsinho.

Refa: Carlos Velasco Carballo (Spain)
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumanne Novemba 20
FC Nordsjælland v FC Shakhtar Donetsk
Juventus v Chelsea FC
FC BATE Borisov v LOSC Lille
Valencia CF v FC Bayern München
FC Spartak Moskva v FC Barcelona
SL Benfica v Celtic FC
Galatasaray A.S. v Manchester United FC
CFR 1907 Cluj v SC Braga
Jumatano Novemba 21
FC Porto v GNK Dinamo
FC Dynamo Kyiv v Paris SaintvGermain FC
Arsenal FC v Montpellier Hérault SC
FC Schalke 04 v Olympiacos FC
FC Zenit St. Petersburg v Málaga CF
RSC Anderlecht v AC Milan
AFC Ajax v Borussia Dortmund
Manchester City FC v Real Madrid CF
Jumanne Desemba 4
GNK Dinamo v FC Dynamo Kyiv
Paris SaintvGermain FC v FC Porto
Montpellier Hérault SC v FC Schalke 04
Olympiacos FC v Arsenal FC
Málaga CF v RSC Anderlecht
AC Milan v FC Zenit St. Petersburg
Borussia Dortmund v Manchester City FC
Real Madrid CF v AFC Ajax
Jumatano Desemba 5
FC Shakhtar Donetsk v Juventus
Chelsea FC v FC Nordsjælland
LOSC Lille v Valencia CF
FC Bayern München v FC BATE Borisov
FC Barcelona v SL Benfica
Celtic FC v FC Spartak Moskva
Manchester United FC v CFR 1907 Cluj
SC Braga v Galatasaray A.S.