Friday, September 28, 2012

kanga moko fashion ni jumamosi hii katika ukumbi wa teofilo kisanji kuanzia majira ya saa mbili wote sana mnakaribishwa kwa shilingi elfu kumi 10000 kwa V.I.P na kawaida ni shilingi  elfu tano  5000

Friday, September 28, 2012

SUPER SPORT YAITANGAZA TANZANIA KIMATAIFA KATIKA MEDANI YA MICHEZO KWA KUZINDUA WIKI YA SOKA TANZANIA


Meneja Mkuu wa Multichoice Tanzania Bw. Peter Fauel akifafanua ujio wa Super Sport nchini Tanzania na kuipongeza TFF kwa kuonyesha ushirikiano na kuwa Chaneli hiyo itaonyesha mechi tano za Ligi ya Tanzania kuanzia leo Ijumaa Septemba 28 hadi Jumatano Oktoba 3 mwaka 2012.

Mkuu wa Super Sport barani Afrika Bw. Andre Venter akielezea furaha yake kuja Tanzania na kupata fursa ya kulitangaza soka la Tanzania kimataifa kupitia chaneli ya Super Sport amesema chaneli hiyo imechafanya kazi katika nchi za Kenya na Uganda na Sasa ni wakati wa Tanzania kuonyesha kiwango chake cha soka Kimataifa.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini (TFF) Bw. Leordiga Tenga akitoa nasaha zake wakati wa uzinduzi wa wiki ya Soka Tanzania ambapo amevitaka vilabu vitakavyopata bahati ya kuonekana katika chaneli hiyo kuonyesha kiwango cha soka la Tanzania na kuzingatia nidhamu haswa mechi ya Watani wa Jadi Yanga na Simba ambao wanatambulika barani Afrika kama timu zenye upinzani mkali.
Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania Bi. Furaha Samalu akifurahi jambo na watangazaji wa kipindi cha Africa Soccer Show wakati wa halfa hiyo.

Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania Barbara Kambogi akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo kuwa Super Sport wakishirikiana na TFF wapo hapa nchini na kwa mara ya kwanza wanaonyesha mechi za Ligi ikiwemo timu ambazo hata siku moja hazijawahi kuonekana kwenye Chaneli ya Super Sport na kuwataka wachezaji wa timu hizo kuonyesha uwezo wao kwa sababu ni fursa ya pekee kuonekana katika nyanja ya Kimataifa. Aidha amewataka Watanzania ambao hawajaunganishwa na DStv wafanye hima kununua ving'amuzi ili waweze kushuhudia mechi hizo pamoja na chaneli nyinginezo zinazopatikana katika DStv.

Meneja Mkuu wa Multichoice Tanzania Bw. Peter Fauel akisalimiana na baadhi ya wageni waalikwa katika hafla fupi ya uzinduzi wa wiki Soka Tanzania iliyofanyika jijini Dar kwenye Hoteli ya Southern Sun.

Dada Levina kutoka Multichoice Tanzania anayetazama kamera akifurahi jambo na wadau.

Meneja fedha wa Multichoice Tanzania Bw. Senguti (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Multichoice Tanzania Bw. Peter Fauel.

Baadhi ya Wadau wa michezo wakipata viburidisho wakati wa uzinduzi wa wiki ya soka Tanzania.

Mkurugenzi Mkuu wa Multichoice Tanzania Bw. Peter Fauel (katikati) katika tete- a -tete na Rais wa TFF Bw. Leordiga Tenga na Mkuu wa Super Sport Afrika Bw. Andre Venter.

Mtangazaji wa Jahazi ya CLOUDS FM Arnold Kayanda (wa pili kulia) na wadau wa tasnia ya michezo wakishow love mbele ya Camera yetu.

Barbara Kambogi akibadilishana mawazo na waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo.

Crew nzima ya Super Sport iliyotua nchini kwa ajili ya wiki ya Soka Tanzania.

Kipindi cha Africa Soccer Show kwa mara ya kwanza kilifanyika LIVE nchini Tanzania. Pichani ni Watangazaji wakifanya mahojiano na Katibu Mkuu wa TFF Bw. Angetile Oseah (katikati).
NA mwandishi tano juma-email tanojuma@gmail.com

Aguero ndani, Tevez bado NJE Argentina!

Ijumaa, 28 Septemba 2012 16:08
Chapisha Toleo la kuchapisha
>> PABLO ZABALETA YUMO! 

>> ARGENTINA kucheza na URUGUAY nyumbani Oktoba 12

BRAZIL_2014_BESTWachezaji wa Manchester City Sergio Agüero na Pablo Zabaleta wameitwa kuichezea Timu ya Taifa ya Argentina itakapocheza Mechi Mwezi ujao ya kuwania kucheza Fainali ya Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Brazil lakini mwenzao wa Klabu moja Carlos Tevez bado hana nafasi kwa Timu hiyo.
Aguero hakucheza Mechi za Argentina za Raundi iliyopita za Kombe la Dunia dhidi ya Paraguay na Peru zilizochezwa mapema Mwezi huu kwa vile alikuwa ameumia goti lakini kutoitwa kwa Tevez sasa kumekuwa kitu cha kawaida toka kwa Kocha wa Timu ya Taifa Alejandro Sabella na badala yake Kocha huyo amemchukua Straika wa Palmeiras Hernan Barcos.
Wachezaji wengine mashuhuri walioachwa ni Beki wa Newcastle Fabricio Coloccini, Kiungo wa Anderlecht Lucas Biglia na Fowadi Internazionale Rodrigo Palacio.
Katika Mechi za Kanda ya Marekani ya Kusini kuwania kucheza Fainali ya Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Brazil, Argentina itacheza nyumbani na Uruguay Oktoba 12 na ugenini na Chile Oktoba 16.
KIKOSI KILICHOITWA:
Mariano Andujar (Catania), Sergio Romero (Sampdoria); Hugo Campagnaro (Napoli), Federico Fernandez (Napoli), Pablo Zabaleta (Manchester City), Ezequiel Garay (Benfica), Marcos Rojo (Sporting Lisbon); Javier Mascherano (Barcelona), Angel Di Maria (Real Madrid), Fernando Gago (Valencia), Enzo Perez (Benfica), Jose Sosa (Metalist Kharkiv), Pablo Guinazu (Internacional); Lionel Messi (Barcelona), Gonzalo Higuain (Real Madrid), Sergio Agüero (Manchester City), Ezequiel Lavezzi (Paris St Germain), Hernán Barcos (Palmeiras).
========================
MSIMAMO KANDA ya NCHI za MAREKANI ya KUSINI:
1 Argentina Mechi 7 Pointi 14
5 Colombia Mechi 7 Pointi 13
3 Ecuador Mechi 7 Pointi 13
4 Uruguay Mechi 7 Pointi 12
2 Chile Mechi 7 Pointi 12
6 Venezuela Mechi 8 Pointi 11
7 Peru Mechi 7 Pointi 7
8 Bolivia Mechi 7 Pointi 4
9 Paraguay Mechi 7 Pointi 4
FAHAMU: Timu 4 za juu zinatinga Fainali Brazil moja kwa moja na ile ya 5 itaenda Mechi ya Mchujo.
 

Eto’o Kundini Cameroun!

Ijumaa, 28 Septemba 2012 15:50
Chapisha Toleo la kuchapisha
Baada ya kufungiwa na Shirikisho la Soka Cameroun Mwezi Novemba Mwaka jana kwa kuongoza mgomo wa Wachezaji kudai malipo yao na baada ya kumaliza kifungo, Nahodha wa zamani wa Cameroun, Samuel Eto’o, aligoma kurudi kuichezea Nchi yake lakini hivi sasa Staa huyo amebadili uamuzi na kukubali kurejea kuichezea tena Cameroun.
Mwezi uliopita Eto’o aliitwa kuichezea Cameroun Mechi ya kwanza ya Raundi ya Mwisho ya Mtoano kuwania nafasi 15 za kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2013, dhidi ya Cape Verde lakini aligoma na Cameroun ikapigwa 2-0 huko Visiwani Cape Verde.
Timu hizi zinatarajiwa kurudiana hapo Oktoba 14.
Kurudi kwa Eto’o  kunafuatia mazungumzo pamoja na Waziri Mkuu Yang, Waziri wa Michezo Adoum Garoua, Meneja wa Timu Song Bahang na Kocha Jean Paul Akon.
Eto’o alitoa tamko kwenye Tovuti yake: “Baada ya kuombwa na uongozi wa juu wa Nchi yetu nimekubali kuichezea Nchi yangu.”
Eto'o ameifungia Cameroun Mabao 53 katika Mechi 109.
SHIRIKI

Kaka Kundini Brazil

Alhamisi, 27 Septemba 2012 23:50
Chapisha Toleo la kuchapisha
NEYMAR_v_MESSIKaka ameitwa kuichezea Brazil kwa ajili ya Mechi za Kimataifa za Kirafiki dhidi ya Iraq na Japan Mwezi ujao baada ya kutochukuliwa tangu Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2010 zilizochezwa huko Afrika Kusini.
Tangu atue Real Madrid, Kaka, Miaka 30, amekuwa na wakati mgumu lakini hivi karibuni nyota yake imeanza kung’ara tena na Jumatano aliifungia Real hetitriki walipocheza Mechi ya Kirafiki na Klabu ya Colombia Millonarios.
Kocha wa Brazil, Mano Menezes, ameamua kumchukua Kaka ili kumpima uwezo wake katika Mechi hizo mbili ambazo zote zitachezwa Ulaya.
Mechi ya Brazil na Iraq itachezwa huko Malmo, Sweden hapo Oktoba 11 na ile ya Japan itachezwa Wroclaw, Poland hapo Oktoba 16.
Kikosi hicho cha Brazil kina Wachezaji wanne ambao wanachezea Klabu za Ligi Kuu England ambao ni watatu kutoka Chelsea, David Luiz, Oscar na Ramires, na Kiungo wa Tottenham Sandro.
Kikosi kamili:
Makipa: Diego Alves (Valencia ), Jefferson (Botafogo), Victor (Atletico-MG)
Mabeki: Daniel Alves (Barcelona ), Marcelo (Real Madrid), Adriano (Barcelona), Alex Sandro (Porto), Thiago Silva (PSG), David Luiz (Chelsea), Dede (Vasco), Leandro Castan (Roma)
Viungo: Sandro (Tottenham), Paulinho (Corinthians), Fernando (Gremio), Giuliano (Dnipro), Lucas Moura (Sao Paulo), Oscar (Chelsea), Ramires (Chelsea), Thiago Neves (Fluminense), Kaka (Real Madrid)
Mastraika: Neymar (Santos), Leandro Damiao (Internacional), Hulk (Zenit)
 

JOEY BARTON aikejeli FA kumfungia Terry Mechi 4 tu!

Alhamisi, 27 Septemba 2012 21:22
Chapisha Toleo la kuchapisha
>>YEYE Kifungo chake 12 kwa VURUGU, ahoji UBAGUZI 4 tu??
>>AHOJI: “Mechi 4? Mwaka mzima uchunguzi, Siku 4 Kesi, ni Mechi 4 tu?”
JOEY_BARTON_n_KOMPANYMchezaji makeke Joey Barton amesema FA inatia aibu sana kwa kumfungia John Terry Mechi 4 kwa Ubaguzi wakati Luis Suarez alipigwa Mechi 8 kwa kosa kama hilo na yeye kwa ugomvi Uwanjani wakati wa Mechi na Manchester City Msimu uliopita alitwangwa Mechi 12.
Joey Barton, ambae alikuwa Nahodha wa QPR, Timu ambayo Beki wake Anton Ferdinand ndie aliekashifiwa kibaguzi na John Terry Oktoba Mwaka jana, kwa sasa yupo Ufaransa akicheza kwa mkopo na Timu ya Marseille na amehoji kupitia Mtandao wa Twitter.
Barton ameandika: “Mechi 4? Mwaka mzima uchunguzi, Siku 4 Kesi na ni Mechi 4 tu? Suarez alipewa 8 sio??”
Aliongeza: “Hii inathibitisha mengi. Ni takataka hii. Mechi 12 kwa ugomvi na 4 kwa hilo. FA lazima wanatia aibu.”
Barton pia alihoji uhalali wa yeye kufungiwa Mechi 12 kwa kuburuzana na Wachezaji wa Manchester City wakati Mbaguzi anapewa Mechi 4 tu.
Alimalizia: “Jana Usiku niliota kuhusu Terry, Watu wanapiga kelele na Kikosi cha Mauaji kipo! Lakini hili sio nilotegemea!”
Wakati huo huo, Kambi ya John Terry imetoa tamko kuwa inasubiri kupewa Ripoti yote ya Kesi iliyomfungia na kisha watatoa uamuzi kama watakata Rufaa au la.
John Terry anao muda wa Siku 14 kukubali makosa au kukata Rufaa akipenda.
SHIRIKI
 

BRAZIL 2014: FIFA yapitisha Saa za Mechi Kuanza FAINALI KOMBE la DUNIA!

Alhamisi, 27 Septemba 2012 20:12
Chapisha Toleo la kuchapisha
>>MECHI ya UFUNGUZI 12 Juni 2014 SAA 5 Usiku Bongo Taimu!
>>FAINALI 13 Julai 2014 SAA 4 Usiku Maracana Stadium!
BRAZIL_2014_BESTLEO Kamati Kuu ya FIFA iliyoketi huko kwenye ‘Nyumba ya FIFA’ Mjini Zurich, Uswisi imepitisha rasmi Saa za kuanza kwa Mechi za Fainali za Kombe la Dunia zitakazochezwa huko Brazil Mwaka 2014.
Mechi ya ufunguzi itachezwa Mjini Sao Paulo kuanzia Saa 5 Usiku Bongo Taimu ikiwa ni Saa 11 Jioni huko Brazil.
Tofauti ya Masaa kati ya Brazil na Tanzania ni Masaa 6 na Tanzania iko mbele kwa Masaa hayo.
Lakini, kwa Mechi ambazo zitachezwa huko Miji ya Cuiaba na Manaus tofauti ya Masaa ni 7.
Mechi za Makundi zitakuwa zikichezwa, kwa Saa za Bongo, Saa 1 Usiku, Saa 4 Usiku, Saa 5 Usiku, Saa 6 Usiku, Saa 7 Usiku na Saa 9 Usiku.
Hatua za Mtoano Mechi zitaanza Saa 1 Usiku na Saa 5 Usiku.
Nusu Fainali zitachezwa Saa 5 Usiku na Fainali, hapo Julai 13, 2014, ni Saa 4 Usiku.
Vile vile, FIFA imethibitisha kuwa Droo kamili ya Ratiba ya Fainali za Kombe la Dunia itafanyika Ijumaa Desemba 6, 2013 huko Costa do Sauipe, Bahia, Brazil.
HABARI ZA AWALI:
FIFA, Ronaldo wamwanua Armadillo, Kinyago maalum kwa Kombe la Dunia 2014!!
KUBATIZWA: MIJUBI au FULECO au ZUZECO!!
FIFA na Wenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 Brazil, kupitia Nguli wao, Ronaldo, wameanua ‘Kinyago’ , au, tuite ‘Katuni maalum’, kwa ajili ya Mashindao hayo ambae ni Mnyama aitwae Armadillo ambae yupo hatarini kuangamizwa na ambae ifikapo Mwezi Novemba atapewa Jina lake maalum.
Kinyago hicho kitabatizwa ama Amijubi, Fuleco au Zuzeco Jina ambalo litachaguliwa na Wabrazil kwa kura.
Tayari Fainali hizo za Mwaka 2014 zimeshapata Mpira maalum uliotengenezwa na Kampuni ya Adidas, uliopewa Jina maalum, "Brazuca" ambalo ni neno la mtaani na la utani likimaanisha Wazalendo wa Brazil na hili limewekwa ili kuonyesha msisitizo wa asili ya Raia wa Brazil.
Armadillo ni Mnyama anaepatikana Kaskazini Mashariki ya Brazil na ni mithili ya Kakakuona ambae ana gamba gumu mgongoni na hujiviringisha kjitetea wakati akitaka kushambuliwa.
Wakati akimwanua Armadillo, Ronaldo alisema: “Nina furaha kumkaribisha Mwanachama mpya muhimu wa Timu yetu ya Mwaka 2014.”
Kinyago hicho kina Rangi za Bendera za Brazil na maandishi ‘Brazil 2014.’
FIFA, kupitia Katibu Mkuu wake Jerome Valcke imesema: “Kwa vile Mnyama huyo ni Kiumbe kinachotishiwa kuangamia kukitumia katika Kombe la Dunia ni kutangaza umuhimu wake katika mazingara na uhai wa Viumbe na Mimea.”
Pia FIFA imesema Majina matatu yaliyotolewa ili kupigiwa Kura kumbatiza Armadillo yana maana zake muhimu.
Amijubi huwakilisha urafiki na furaha wakati Fuleco na Zuzeco yanahusishwa na ujumbe wa uhai wa Viumbe na Mimea.
Katika Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2010 huko Afrika Kusini Kinyago alietumiwa alikuwa ni Chui alieitwa ‘Zakumi’, Fainali za 2006 huko Germany walikuwa na Simba aliepewa Jina la Goleo.
Kinyago wa kwanza kabisa kutumika katika Kombe la Dunia ni katika zile Fainali za Mwaka 1966 huko England na alikuwa ni Simba alievalishwa Bendera ya Uingereza na kuitwa ‘Willie.’
Vinyago vingine vilivyowahi kutumika ni Mtoto alieitwa ‘Juanito’ huko Mexico 1970, Chungwa lililoitwa ‘Naranjito’ huko Spain Mwaka 1982, Mbwa alieitwa ‘Striker’ huko USA 1994 na Jogoo mwenye Jina la ‘Footix’ huko Ufaransa Mwaka 1998.

BOBAN BADO HASOMEKI ZANZIBAR

Mtaalamu Boban

Na tano juma
LABDA leo, lakini jana wamemsubiri hadi boti ya mwisho hakushuka. Haruna Moshi Shaaban, mchezaji pekee ambaye hayupo kambini Simba SC, alitarajiwa kuungana na wenzake jana, visiwani Zanzibar kwa maandalizi ya mchezo dhidi ya wapinzani wao wa jadi, Yangas SC, lakini wapi.
Sasa uongozi wa Simba utamsikilizia mchezaji huyo leo kama atatimiza wajibu wake na tofauti na hapo, watachukua.  
Boban hakucheza mechi iliyopita ya Ligi Kuu kati ya Simba na Ruvu Shooting, kwa sababu alikuwa anaumwa na hakwenda kambini wenzake, kwa kuwa alikuwa anajisikilizia afya yake, ila kuanzia jana alitarajiwa kuungana na wenzake kambini.
Kuna uwezekano mkubwa Boban akapanda boti na wenzake na baada ya mechi ya kesho, dhidi ya Prisons.
Japo Boban hayupo kambini Zanzibar, lakini Simba SC inaendelea vizuri na maandalizi yake ya pambano dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga SC, Oktoba 3, mwaka huu, ikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Chuo cha Kiislam, Kwerekwe, visiwani Zanzibar na kambi yao ipo Chukwani.
Morali ya kambi ipo juu na wachezaji wote wako fiti, wakijifua kwa shauku kubwa ili kumvutia kocha Mserbia, Milovan Cirkovick awape nafasi ya kucheza Oktoba 3, kuanzia sa 1:00 usiku.
Simba itarejea Dar es Salaam kesho kucheza mechi na Prisons ya Mbeya Uwanja wa Taifa, kisha kurejea tena visiwani humo kuendelea na maandalizi ya mchezo wa Jumamosi ijayo.
Hata hivyo, katika michezo miwili ijayo, Simba itamkosa mshambuliaji wake Mganda, Emmanuel Okwi ambaye amefungiwa na Kamati ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, chini ya Mwenyekiti wake, Wallace Karia, sambamba na kumtoza faini ya Sh. 500,000 kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa JKT Ruvu, Kessy Mapande.
Okwi alifanya hivyo akilipa kisasi cha kuchezewa rafu Jumatano iliyopita, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Tayari Okwi amekosa mechi moja dhidi ya Ruvu Shooting na wakati, na sasa atakosa mechi mbili zaidi, dhidi ya Prisons na dhidi ya Yanga na baada ya hapo atakuwa huru kuendelea kumtumikia mwajiri wake.
Siyo siri, kuelekea pambano la watani wa jadi, Okwi alikuwa ni homa kwa Yanga, hasa wakikumbuka namna alivyowanyanyasa katika mechi iliyopita, akifunga mabao mawili kwenye ushindi wa 5-0 na kusababisha mawili.

KOCHA MPYA YANGA AWASILI KIMYAKIMYA

Brandts

Na Mahmoud Zubeiry
KOCHA mpya wa Yanga, Ernstus ‘Ernie’ Wilhelmus Johannes Brandts, beki wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi na klabu ya PSV Eindhoven ya Holanzi, atawasili wakati wowote kuanzia leo kusaini mkataba na kuanza kazi katika klabu hiyo.
Hata hivyo, Yanga imeamua kufanya siri ujio wa kocha huyo, kwa sababu haitaki mapokezi ya mbwembwe, kutokana na rekodi yake ya kutodumu na makocha.
Yanga, imetimiza malengo yake ya kuwa kocha mpya, kabla ya kucheza na wapinzani wao wa jadi, Simba SC, Oktoba 3, mwaka huu baada ya kumfukuza Mbelgiji, Tom Saintfiet, kutokana na kufikia makubaliano na Brandts.
Mholanzi huyo aliyefukuzwa APR ya Rwanda baada ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, Agosti mwaka huu amepewa ukocha wa Yanga, baada ya Mbrazil Marcio Maximo kukataa nafasi hiyo kwa mara ya pili.
Mtaalamu huyo, alizaliwa Februari 3, mwaka 1956 mjini Nieuw-Dijk, Gelderland, mbali na PSV Eindhoven, alichezea pia Roda JC Kerkrade, MVV Maastricht na De Graafschap.
Brandts aliichezea mechi 28 timu ya taifa ya Uholanzi na kuifungia mabao matano na pia alicheza Fainali za Kombe la Dunia mwaka 1978.
Katika fainali hizo, Raundi ya pili kwenye mechi na Italia, aliweka rekodi ya kuwa mchezaji pekee aliyezifungia mabao timu zote katika mechi moja kwenye fainali za Kombe la Dunia.
Alianza kujifunga dakika ya 18, kisha akaisawazishia Uholanzi dakika ya 50 katika mechi ambayo, mchezaji mwenzake Arie Haan baadaye aliifungia timu yake bao la ushindi na kutoka kifua mbele kwa mabao 2–1.
Alipostaafu soka akawa kocha na katikati ya msimu wa 2007–2008, Brandts aliambiwa hataongezewa mkataba NAC-Breda, licha ya matokeo mazuri ya kushika nafasi ya tatu katika Ligi Kuu Uholanzi (Eredivisie), ingawa uamuzi huo haukuwafurahisha mashabiki wa timu hiyo na nafasi yake akapewa Robert Maaskant kuanzia msimu wa 2008–2009.
Akateuliwa kuwa Kocha wa Rah Ahan mwaka 2009, kabla ya kufukuzwa Desemba 2009 na kuibukia APR ya Rwanda mwaka 2010, ambako ‘riziki’ yake imeisha miezi miwili iliyopita na sasa amepata maisha mapya Yanga.
Akiwa APR, Brandts alifungwa mechi zote mbili na Yanga iliyokuwa ikifundishwa na Mbelgiji Tom Saintfiet katika Kombe la Kagame, moja ya makundi 2-0 na nyingine ya Nusu Fainali 1-0. Yanga iliibuka bingwa, ikiifunga Azam FC 2-0 kwenye fainali.
Brandts atakutana na wachezaji wake wa zamani wawili Yanga, beki Mbuyu Twite anayeanza msimu wa kwanza katika klabu hiyo na kiungo Haruna Niyonzima anayeingia katika msimu wa pili, ambao alifanya nao kazi APR.

AZAM KURUDI KILELENI LIGI KUU LEO?

Azam FC

Na Prince Akbar
LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, leo inaingia katika mzunguko wake wa nne kwa mechi za Super Weekend, ambazo zitaonyeshwa moja kwa moja na kituo cha Televisheni cha SuperSport cha Afrika Kusini.
Mechi ya kwanza ambayo itachezwa leo itakuwa kati ya Azam FC na JKT Ruvu Stars, itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 1:00 usiku kwa viingilio vya Sh. 3,000 mzunguko, sh. 5,000 kwa VIP C na VIP B wakati VIP A kiingilio kitakuwa sh. 10,000.
Kesho kutakuwa na mechi kati ya Simba na Tanzania Prisons itakayofanyika Uwanja wa Taifa, pia mjini Dar es Salaam kuanzia saa 11:00 jioni, wakati Yanga na African Lyon zitapambana keshokutwa kwenye Uwanja huo huo kuanzia saa 11:00 jioni.
Uwanja wa Chamazi, maarufu kama Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam wenyewe utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar itakayochezwa Oktoba 1, mwaka huu kuanza saa 10:30 jioni.
Mechi ya mwisho ya Super Weekend itachezwa Oktoba 3 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ikwakutanisha watani wa jadi, Yanga na Simba kuanzia saa 1:00 usiku.
Wakati huo huo: Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Katibu Mkuu mstaafu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Erasto Zambi kilichotokea juzi mjini Dar es Salaam kutokana na maradhi.
Zambi ambaye anatarajiwa kuzikwa Jumapili, kabla ya kuwa kiongozi TOC, kwa muda mrefu alikuwa mwalimu wa michezo katik Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambapo wanamichezo wengi hasa waliokuwa wanafunzi katika chuo hicho wamepita kwake.
Msiba huo ambao uko nyumbani kwake Ubungo Kibangu, Dar es Salaam ni pigo kwa familia ya Zambi, TFF na wanamichezo kwa ujumla nchini kutokana na mchango na mawazo aliyotoa kwa shirikisho wakati akiwa kiongozi wa TOC.
TFF imetoa pole kwa familia ya Zambi, jamaa na marafiki na kuwataka kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki cha msiba huo mzito.

MSIMAMO WA LIGI KUU BARA

                               P    W  D   L    GF       GA      GD     P
Simba SC                3    3    -     -     7          1          6       9
Azam FC                 3    2    1    -     3          1          2       7
Coastal                    3    2    1    -     5          3          2       7
JKT Oljoro               3    1    2    1    2          1          1       5
Mtibwa Sugar          3    1    1    1    3          1          2       4
Yanga SC               3    1    1    1    4          4          -        4
Toto African            3    -     3    1    3          2          1       3
Ruvu Shooting        3    1    -     2    4          5          -1     3
African Lyon            3    1    -     2    2          5          -3     3
JKT Ruvu                3    1    -     2    3          7          -4     3
Prisons                   2    -     2    -     1          1          -        2
Polisi Moro              3    -     2    1    -           1          -1     2
Kagera Sugar         3    -     1    2    2          4          -2     1
JKT Mgambo           3    -     -     3    1          3          -2     0
No comments:

KARAMA, CHEKA WAPIMA UZITO TAYARI KWA PAMBANO LAO KESHO

Bondia  Fransic Cheka akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Karama Nyilawila  litakalofanyika Jumamosi katika ukumbi wa PTA, Sabasaba Dar es Salaam.

Bondia Karama Nyilawila akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Fransic Cheka litakalofanyika Jumamosi katika ukumbi wa PTA, Sabasaba Dar es Salaam.
Picha na 
www.superdboxiongcoach.blogspot.com

KUELEKEA PAMBANO LA WATANI; NGASSA ANA UBAVU WA KUIFUNGA YANGA?


Ngassa

Na Mahmoud Zubeiry
OKTOBA 3, mwaka huu, nyasi za Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam zitawaka moto kwa mpambano mkali wa wapinzani wa jadi katika soka ya Tanzania, Simba na Yanga, huo ukiwa mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baina ya miamba hiyo.
Kama kuna wachezaji ambao tayari wamekwishaanza kuupa joto kali mchezo huo, basi miongoni mwao ni Mrisho Khalfan Ngassa, kiungo mshambuliaji aliye katika msimu wa kwanza Simba SC katika mkataba wake wa miaka miwili.
Akiwa ana jezi ya Simba, hiyo itakuwa mechi yake ya kwanza dhidi ya Yanga, timu yake ya zamani, ambayo aliichezea tangu mwaka 2007 hadi 2010 alipotimkia Azam FC, ambayo Agosti imemtoa kwa mkopo kwa Wekundu wa Msimbazi, walioongeza naye mkataba wa mwaka mmoja.
Wengi hata mashabiki wa Simba SC, wanaamini Ngassa ni Yanga na yupo Msimbazi kwa ajili ya kazi na maslahi na kuelekea mechi ya watani Oktoba 3, anakabiliwa na changamoto ya kufanya kile ambacho walifanya wachezaji waliomtangulia wenye historia kama ya kwake.
Bahati mbaya kwake Ngassa, tangu anaingia hadi anatoka Yanga hakuwahi kutikisa nyavu za Simba, zaidi alitoa pasi kwa wafungaji na alikuwa chachu ya ushindi katika mechi kadhaa.
Sasa Mrisho yupo Simba na mashabiki pamoja na kutaka kuona kiwango chake siku hiyo, ambayo klabu hiyo itamkosa Mganda Emmanuel Okwi anayetumikia adhabu, pia watataka kuona je, atawafunga Yanga?
Kufunga, kwanza ni nia ya mchezaji anayokuwa nayo hata kabla hajaingia uwanjani na ndipo akiwa kazini atajituma kutafuta kutimiza nia yake na hata akishindwa, jitihada huonekana, je Mrisho ana nia ya kuifunga Yanga?
Mrisho ana uwezo na ni kati ya wachezaji ambao kwa sasa dhahiri wanawatia homa mabeki wa Yanga kuelekea mchezo huo- unaweza pia kusema ni moja ya chachandu za mpambano huo ujao wa watani.
Kabla ya Ngassa, ni orodha ndefu ya wachezaji waliotoka Simba kwenda Yanga na kutoka Yanga kwenda Simba, tangu enzi za akina Emanuel Mbele 'Dubu', lakini ni wachache waliong'ara kote kote.
Athumani Mambosasa (sasa marehemu), Zamoyoni Mogella, Method Mogella (sasa marehemu), Hamisi Gaga (sasa marehemu), Deo Njohole, Akida Makunda, Alphonce Modest, Monja Liseki, Shaaban Ramadhan, Eustace Bajwala, Joseph Katuba (sasa marehemu) wote hao ni baadhi ya wachezaji waliotoka Simba na kwenda kucheza Yanga.
Maulid Dilunga 'Mexico', Ezekiel Greyson 'Jujuman', Justin Mtekere (wote marehemu), Ally Yussuf 'Tigana', Yussuf Macho, Godwin Aswile, Ismail Suma, Steven Nemes, Nico Bambaga, Bakari Malima, Willy Martin, Edibily Lunyamila, Mtwa Kihwelo, Omar Hussein 'Keegan', Athumani China, Mohamed Hussein 'Mmachinga', Mohamed Banka, Amri Kiemba wote pia ni baadhi ya wachezaji waliotoka Yanga na kucheza Simba.
Athumani China akiwa Yanga, aliifunga Simba bao la mapema, dakika ya tatu, Oktoba 9, mwaka 1991 kwenye Ligi ya Muungano, wakati watoto wa Jangwani wakiibuka na ushindi wa 2-0. Bao la pili la Yanga lilifungwa na Abubakar Salum 'Sure Boy' dakika ya 54.
China tena aliifunga Yanga akiwa Simba, lilikuwa bao la pili katika ushindi wa 4-1 kwa Wekundu wa Msimbazi, Julai 2, mwaka 1994. Ally Yussuf Suleiman 'Tigana', pia alifunga mabao kote kote, Thomas Kipese kadhalika naye aliwafunga Simba na baadaye Yanga.
Akida Makunda aliihama Simba kuingia Yanga akiwa hana kumbukumbu ya kufunga bao kwenye mechi ya watani, lakini mara baada ya kutua kwa wana Jangwani aliingia kwenye orodha ya nyota waliofunga mabao kwenye mechi baina ya wababe hao wa soka ya Tanzania.
Ilikuwa Februari 21, mwaka 1998 katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wakati huo ikidhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager, wakati Makunda alipofunga bao lililoelekea kuwatoa Yanga kifua mbele kwenye mchezo huo, dakika ya 46.
Lakini Athumani Macheppe alizima shangwe za wana Yanga zikiwa zimesalia dakika mbili mchezo huo kumalizika kwa bao lake safi.
Sahau kuhusu Akida, kama yupo mchezaji ambaye aliyewapa raha mashabiki wa timu zote hizo, basi ni Said Nassor Yussuf Mwamba, maarufu kama Kizota enzi zake, aliyefariki dunia Februari 11, mwaka 2007. Kizota ni mchezaji aliyewasisimua kwa namna yake mashabiki wa Yanga na Simba kutokana na mabao yake.
Kizota alifariki dunia baada ya kugongwa na gari eneo la Veterinary, akiwa anatoka kushuhudia mchezo wa marudiano, Kombe la Shirikisho la Soka Afrika, Raundi ya Awali kati ya wenyeji Simba dhidi ya Textil de Pungue ya Msumbiji. Alitoka kwa huzuni uwanjani siku hiyo baada ya kushuhudia timu yake ya zamani, Simba ikitolewa na wageni kwa mikwaju ya penalti 3-1, kufuatia sare ya jumla ya 2-2.
Mchezo wa kwanza Msumbiji, Simba ililazimisha sare ya 1-1 na marudiano nayo pia walibanwa kwa sare aina hiyo hiyo, hivyo kufanya mshindi aamuliwe kwa mikwaju ya penalti. Ntota ya timu ya kiwanda cha nguo Msumbiji ndiyo iliyong'ara jioni hiyo.
Kama kuna miaka ambayo Kizota alifanya vitu vya 'babu kubwa' kwenye soka ya Tanzania, basi ni 1993, kwani mapema tu mwaka huo aliibuka mfungaji bora kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati mjini Kampala, Uganda, akiiwezesha Yanga pia kutwaa ubingwa wa michuano hiyo kwa kuwafunga wenyeji, SC Villa.
Lakini pia, alikuwa mfungaji bora wa Ligi ya Tanzania. Yote tisa, kumi ni pale Kizota alipofunga mabao mawili peke yake, wakati Yanga inaibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Simba kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi ya Tanzania Bara, Uwanja wa Taifa, (sasa Uhuru) mjini Dar es Salaam.
Ilikuwa ni Machi 27, mwaka huo 1993, wakati Kizota alipomchambua kipa hodari nchini enzi hizo, Mwameja Mohamed katika dakika za 47 na 57.
Simba ikielekea kulala 2-0, shukrani kwake Edward Chumila (naye marehemu pia) aliyewafungia Wekundu wa Msimbazi bao la kufutia machozi, dakika ya 75.
Baada ya kipigo kikali cha mabao 4-1, Julai 2, mwaka 1994, Yanga ilivunja kikosi ikiwafukuza karibu nyota wake wote wa kikosi cha kwanza kwa tuhuma za kuhusika kuihujumu timu katika kipigo hicho kilichotokana na mabao ya George Masatu, Athumani China, Madaraka Selemani na Dua Saidi, bao la kufutia machozi la Yanga likifungwa na beki imara, Constantine Kimanda.
Kati ya nyota waliotupiwa virago Yanga ni Kizota, ambaye kutokana na makali yake wakati huo, akiwa tegemeo la timu ya taifa ya Tanzania na miongoni mwa nyota waliotoa mchango mkubwa kwenye kikosi kilichochukua Kombe la Challenge nchini Kenya, Simba wakamwambia: "Usipate tabu Said, njoo upumzike huku".
Kizota alitaka kuwaonyesha Yanga kwamba, walifanya kosa kumwacha na katika mchezo wa marudiano baina ya watani hao wa jadi wa Ligi Kuu ya Bara, Oktoba 4, 1995, Yanga ikiwa inaelekea kabisa kushinda mchezo huo 1-0, Said Mwamba alitibua furaha ya wana Jangwani dakika ya 70 kwa kufunga bao safi la kusawazisha.
Yanga ilitangulia kupata bao kupitia kwa mpachika mabao wake mahiri enzi hizo, Mohamed Hussein 'Mmachinga' dakika ya 40. Bao la Kizota liliwachanganya Yanga na dakika tisa baadaye, wakapachikwa bao la pili. Safari hiyo alikuwa ni Mchunga Bakari 'Mandela' aliyewaambia wana Jangwani; kutangulia si kufika.
Baada ya msimu huo, Yanga walikiri kosa lao na wakaenda kumpigia magoti Kizota arejee nyumbani. Kwa sababu Kizota alikuwa anaishi nyumba ya pili kutoka klabu ya Yanga, akiishi na mkewe Tosha, Mtaa wa Jangwani, hivyo ilikuwa rahisi kumrubuni na kurejea nyumbani.
Na aliporejea Yanga, Kizota aliifunga tena Simba. Ilikuwa Novemba 9, mwaka 1996, katika sare ya ajabu ya watani, ya mabao 4-4 mjini Arusha.
Kizota aliifungia Yanga bao la kusawazisha lililofanya sare ya 3-3 katika dakika 70, baada ya awali Kipese kuifungia Simba, dakika ya saba, Edibily Lunyamila kuisawazishia Yanga kwa penalti dakika ya 28, Ahmed Mwinyimkuu kuifungia Simba la pili dakika ya 43, kabla ya Dua Said kufunga la tatu dakika ya 60 na Mustafa Hoza kuisawazishia Yanga kwa kujifunga dakika ya 64.
Sanifu Lazaro aliifungia Yanga bao lililoelekea kuwa la ushindi dakika ya 75, lakini walishindwa kulinda lango lao na kuruhusu bao la dakika za lala salama, lililofungwa na Duwa Said dakika ya 90, hivyo kuwa sare ya 4-4.  
Je, Mrisho ataweza kufanya vitu Oktoba 3? Bila shaka hilo ni jambo la kusubiri na kuona.

UWANJANI ULAYA

BPL WIKIENDI=BIGI MECHI: Arsenal v Chelsea, Man United v Spurs!

Alhamisi, 27 Septemba 2012 18:51
Chapisha Toleo la kuchapisha
>>FAHAMU Marefa Mechi zote!
BPL: RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumamosi Septemba 29
[Saa 8 Dak 45 Mchana]
Arsenal v Chelsea
[Saa 11 Jioni]
Everton v Southampton
Fulham v Manchester City
Norwich City v Liverpool
Reading v Newcastle United
Stoke City v Swansea City
Sunderland v Wigan Athletic
[Saa 1 na Nusu Usiku]
Manchester United v Tottenham Hotspur
Jumapili Septemba 30
[Saa 12 Jioni]
Aston Villa v West Bromwich Albion
Jumatatu Oktoba 1
[Saa 4 Usiku]
Queens Park Rangers v West Ham United
======================
Jumamosi Septemba 29 zipo Mechi 8 za Ligi Kuu England [Barclays Premier League, BPL] na kati ya hizo zile zenye mvuto mkubwa, BIGI MECHI, ni ile itayofungua Dimba la Wikiendi itakayochezwa Uwanja wa Emirates kati ya Arsenal na Chelsea na ile itayofunga dimba Siku hiyo hiyo huko Old Trafford kati ya Manchester United na Tottenham Hotspur.
ZIFUATAZO NI DONDOO FUPI kuhusu Mechi hizo:
======================
MSIMAMO Timu za Juu:
[Kila Timu imecheza Mechi 5 isipokuwa inapotajwa]
1 Chelsea Mechi 5 Pointi 13
2 Man United  12
3 Everton 10
4 WBA  10
5 Arsenal  9
6 Fulham  9
7 Man City  9
8 Tottenham 8
9 West Ham 8
10 Newcastle 8
11 Swansea 7
12 Sunderland Mechi 4 Pointi  4
13 Stoke City 4
14 Aston Villa 4
15 Wigan 4
16 Southampton 3
17 Norwich 3
18 Liverpool 2
19 QPR 2
20 Reading Mechi 4 Pointi 1
=======================
BPL_LOGOArsenal v Chelsea
Hii ni gemu muhimu kwa Arsenal ambao wako nafasi ya 5 na Pointi 4 nyuma ya vinara Chelsea kwenye Msimamo wa Ligi.
Wiki iliyopita Timu hizi zilifunga magoli dakika za mwishoni kwa Arsenal kusawazisha kwa bao la Laurent Koscielny na kutoka 1-1 walipocheza na Mabingwa Manchester City huko Etihad na Chelsea kufunga bao moja kupitia Ashley Cole walipoitoa 1-0 Stoke City.
Hadi sasa, Arsenal na Chelsea ni katika Timu 4 ambazo hazijafungwa kwenye Ligi tangu Msimu uanze na nyingine ni Man City na Sunderland.
Refa: Martin Atkinson
Everton v Southampton
Everton, ambao walianza kwa kuifunga Manchester United bao 1-0, walipwaya kidogo lakini wameshinda Mechi yao ya mwisho kwa kuichapa Swansea bao 3-0  lakini pia wanakutana Southampton ambayo baada ya kuanza vibaya wamezinduka na kuitwanga Aston Villa bao 4-1.
Refa: L Probert
Fulham v Manchester City
Man City wametoka kwenye sare ya 1-1 na Arsenal na wao kama Mabingwa watajiona kama walipoteza mchezo huo lakini Msimu huu Difensi yao inavuja mno na huko Craven Cottage watakutana na Fulham ambayo wao na Man United ndio Timu zilizofunga bao nyingi Msimu huu kwenye Ligi, kila moja ikiwa na bao 12.
Refa: M Halsey
Norwich City v Liverpool
Hii ni Mechi inayozikutanisha Timu zilizo nafasi ya 17, Norwich, na ile ya 18, Liverpool, na kama Liverpool hawaanzi kujirekebisha sasa basi Msimu huu ni balaa kwao.
Refa: M Jones
Reading v Newcastle
Hizi ni Timu mbili ambazo hazitabiriki lakini Newcastle wakiwa na Demba Ba na Papiss Cisse ni hatari ikiwa hiyo itakuwa Siku yao.
Refa: Andrew Marriner
Stoke City v Swansea City
Swansea walianza kwa moto Msimu huu huku mfungaji wao Michu akiwa hashikiki lakini baada ya magoli kumkaukia Swansea wamepigwa Mechi mbili mfululizo kwa jumla ya bao 5-0.
Hii ni Mechi ngumu kutabirika.
Refa: J Moss
Sunderland v Wigan Athletic
Sunderland wamecheza Mechi 4 za Ligi na kupata sare 4.
Hii ni nafasi nzuri kwa Sunderland kupata ushindi dhidi ya Wigan ambayo imefungwa Mechi mbili mfululizo.
Refa: Howard Webb
Manchester United v Tottenham Hotspur
Tangu wafungwe bao 1-0 na Everton katika Mechi yao ya ufunguzi ya Ligi Msimu huu, Man United wameshinda Mechi zao zote 4 zilizofuata na sasa wako nafasi ya pili Pointi moja nyuma ya vinara Chelsea.
Lakini Tottenham walianza vibaya na hatimae kushinda Mechi yao ya mwisho kwa kuifunga QPR bao 2-1.
Refa: C Foy
Aston Villa v West Bromwich Albion
WBA ndio Timu ya maajabu Msimu huu kwani imeanza vizuri Ligi na ipo juu ya Timu kama vile Man City, Arsenal na Tottenham kwenye Msimamo wa Ligi.
Refa: A Taylor
Queens Park Rangers v West Ham United
QPR wako nafasi ya 19 na wanapambana na Timu ngumu iliyo chini ya Meneja Sam Allardyce na Nahodha Kevin Nolan.
Ni Mechi ngumu.
Refa: M Clattenburg

DERRICK WALULYA, TONY NDOLO, NA ERNEST BOAKYE WAOMBEWA UHAMISHO WA KIMATAIFA

TFF YATOA ITC KWA WACHEZAJI WANNE
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa wachezaji wanne waliokuwa wakichezea timu mbalimbali nchini.
 
Wachezaji hao ni Tony Ndolo aliyejiunga na KCC ya Uganda kutoka Toto Africans, Felix Amech Stanley aliyekwenda Bahla ya Oman kutoka Coastal Union, Ernest Boakye kutoka Yanga aliyejiunga na Tripoli Athletics Club ya Lebanon na Derrick Walulya aliyerejea URA ya Uganda kutoka Simba.
 
15 WACHUKUA FOMU UCHAGUZI TWFA
Wanamichezo 15 wamechukua fomu kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) utakaofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao.
 
Waliochukua fomu za kuwania uenyekiti ni Lina Kessy, Isabellah Kapera na Joan Minja. Nafasi ya Makamu Mwenyekiti imeombwa na Roseleen Kisiwa pekee wakati Katibu Mkuu ni Amina Karuma na Cecilia Makafu. Macky Mhango pia ni mwombaji pekee aliyeomba nafasi ya Katibu Msaidizi.
 
Waombaji watatu wa nafasi ya mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ni Furaha Francis, Juliet Mndeme na Zena Chande. Nafasi ya Mhazini nayo ina mwombaji mmoja tu ambaye ni Rose Msamila.
 
Sophia Charles, Rahim Maguza, Telephonia Temba na Jasmin Badar Soud wao wanaomba nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya chama hicho kwenye uchaguzi huo ambao utaendeshwa na Kamati ya Uchaguzi ya TWFA chini ya Ombeni Zavalla.
 
MKUTANO VODACOM, KLABU ZA LIGI KUU
Klabu za Ligi Kuu na mdhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom zimekutana jana (Septemba 27 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo yalilenga kipengele ya upekee (exclusivity) kilichopo kwenye mkataba wa udhamini ambacho kitaendelea kuwepo. Klabu zilikuwa zimeomba kwa mdhamini kuangalia uwezekano wa kukiondoa.
 
Pande hizo zimekubaliana kuunda kamati ya pamoja kwa ajili ya kuitafutia kila klabu mdhamini binafsi kwa lengo la kuhakikisha zinashiriki kikamilifu katika ligi hiyo.
 
Klabu zote zimeshapata vifaa kutoka kwa Vodacom ukiondoa African Lyon ambayo ilitarajia kuchukua vifaa hivyo leo kutoka kwa mdhamini wa ligi hiyo.
 
MCHAKATO WA UCHAGUZI WA VIONGOZI TAFCA
Mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA) unaanza rasmi Septemba 30 mwaka huu kwa uchukuaji fomu kwa wagombea.
 
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA, Ramadhan Mambosasa, fomu kwa waombaji uongozi zitaanza kutolewa Septemba 30 mwaka huu, na mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu hizo ni Oktoba 4 mwaka huu.
 
Fomu hizo zinapatikana ofisi za TAFCA zilizopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 10 alasiri. Ada ya fomu kwa waombaji wa nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu na Katibu Msaidizi ni sh. 200,000.
 
Nafasi zilizobaki za Mhazini, mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na wajumbe wa Kamati ya Utendaji, ada ya fomu ni sh. 100,000. Uchaguzi wa TAFCA umepangwa kufanyika Novemba 10 mwaka huu.

Friday, September 28, 2012

AZAM KILELENI LIGI KUU BARA


Na Prince Akbar
AZAM FC imepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuifunga JKT Ruvu mabao 3-0, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, katika mechi iliyoanza saa 1:00.
Mabao ya Azam katika mchezo huo, yalifungwa na John Raphael Bocco ‘Adebayor’ dakika ya 44 kwa penalti, Kipre Herman Tcheche dakika ya 65 na Kipre Michael Balou dakika ya 79.
Ushindi huo, moja kwa moja unaipandisha Azam kileleni mwa ligi hiyo, ikifikisha pointi 10 baada ya kucheza mechi nne na kuipiku Simba SC, yenye pointi tisa, lakini iko nyuma kwa mchezo mmopja.
Kesho Simba itacheza na Tanzania Prisons itakayofanyika Uwanja wa Taifa, pia mjini Dar es Salaam kuanzia saa 11:00 jioni, wakati Yanga na African Lyon zitapambana keshokutwa kwenye Uwanja huo huo kuanzia saa 11:00 jioni.
Uwanja wa Chamazi, maarufu kama Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam wenyewe utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar itakayochezwa Oktoba 1, mwaka huu kuanza saa 10:30 jioni.
Mechi ya mwisho ya Super Weekend itachezwa Oktoba 3 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ikwakutanisha watani wa jadi, Yanga na Simba kuanzia saa 1:00 usiku.