Monday, December 31, 2012
UHAMISHO WA JANUARI ULAYA NDIO HUO SASA UMEWADIA. NANI ANAKWENDA WAPI NA NANI MWENYE KISU KIKALI. SNEIJDER, BEMBA BA, THEO WALCOTT, DAVID VILLA, MOROUANE FELLAINI, BALOTELLI, ZAHA, BENAT NA GOMIS WOTE SAFARINI.
Inavyo
onekana mara baada ya dirisha dogo la usajili la mwezi Januari 2013 kufunguliwa
mwezi January, hakutakuwa na uhaba wa upatikanaji wa vipaji.
Mwezi January
sasa umefika ambapo dirisha dogo la usajili litakuwa likifunguliwa tena barani
ulaya. Kumekuwepo na majina mengi
makubwa ambayo yamekuwa yakihusishwa na kutaka kuhama kutoka upande mmoja
kuelekea upande mwingine, ambapo vilabu vikubwa katika bara hilo la Ulaya navyo
vikihaha kusaka vipaji vipya.
Kwa msaada
wa mtandao wa Goal.com hebu tuangalie majina hayo yanayotajwa kuwa huenda
wakahama kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine mwezi huu wa January.
Wesley Sneijder, Inter
Kiungo
mchezeshaji huyo raia wa Uholanzi amekuwa hana nafasi tena katika kikosi cha
kwanza San Siro. Sneijder ametamka waziwazi kuwa itakuwa vema kwake kama
ataondoka katika klabu yake katika dirisha hili la usajili, kiasi kuviweka
vilabu vikubwa barani humo kukaa mkao wa kumsubiri.
Taarifa za
awali zinasema kuwa Sneijde ameshakubaliana katika mambo fulani ya msingi na klabu
ya Tottenham na kwamba mpango huo umefikia hatua nzuri ambapo pia kuna vilabu
kadhaa vya ligi kuu ya England vikimtamani kama vile Manchester City, Liverpool
na Manchester United.
Pia Anzhi
Makhachkala ya Russia pia iko katika mpango huo.
Demba Ba, Newcastle
Mshambuliaji
huyu ni raia wa Senegal ambaye amekuwa mfungaji mkubwa wa Newcastle, akiifungia
magoli 29 katika jumla ya michezo 54 aliyocheza klabu hiyo.
Ba, amevutia
vilabu vingi vikubwa ambapo Chelsea na Arsenal ni vilabu ambavyo kuna tetesi
zinasema wanamtaka Ba mwenye umri wa miaka 27,
Kuondoka
kwake kunaweza kumfanya meneja Alan Pardew kuwasajili Mathieu Debuchy na Loic
Remy.
Theo Walcott, Arsenal
Kwa hali ya
mambo ilivyo ni kwamba mkataba wa Theo Walcott katika klabu yake ya Arsenal uko
katika hali ya sintofahamu ambapo kwa kwasasa umekuwa unaangaliwa na vilabu
vingi vikubwa barani Ulaya wakisubiri majaaliwa yake.
Wakati
mkataba huo ukitarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu, vilabu mbalimbali sasa
vimekodoa macho wakirubiri hatma yake mwezi January.
Mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa England mwishoni mwa juma alipiga bao tatu “hat trick”
katika mchezo dhidi ya Newcastle ambayo kwa kweli imeongeza thamani yake katika
mpango wake ujao usajili wa nyongeza kama washika mitutu watashawishika
kumsajili tena Walcott na kwa vyovyote vile itakuwa ni busara kumsajili tena
kuliko kumuacha akiondoka kama mchezaji huru majira ya kiangazi.
Kuna tetesi
kuwa Chelsea na Manchester United wanamtaka nyota wa England, wakati ambapo Juventus
na Paris Saint-Germain wakiwa mbioni kumnasa.
David Villa, Barcelona.
Kama ilivyo
kwa Sneijder, Villa pia ni jina kubwa ambaye amekosa nafasi ya kikosi cha
kwanza katika klabu yake ya Barcelona lakini akionekana kuwa kivutio katika
klabu kubwa za ligi kuu ya England “Premier League”
Mshambuliaji
huyo mwenye umri wa miaka 31 amekuwa katika kikosi kilicho anza cha Barcelona
katika michezo 6 tu kati ya michezo 17 ambayo Barcelona imecheza ya ligi kuu ya
Hispania ‘La Liga’ msimu huu ambapo sasa ameondoshwa rasmi katika orodha ya
wachezaji wa kikosi cha kwanza moja kwa moja.
Meneja wa Chelsea
Rafa Benitez inasemekana anataka kuwaunganisha wachezaji watatu wa timu ya
taifa ya Hispania,Villa,Fernando Torres na Juan Mata katika kikosi chake,
lakini Liverpool na Arsenal huenda wakaingia vitani kutaka saini yake. Pia
huenda El Guaje akasalia Camp Nou kupigania nafasi msimu huu na kusubiri
uhamisho wa majira ya kiangazi.
Marouane Fellaini, Everton
Nyota huyu
raia wa Belgian alikuwa ni miongoni mwa wachezaji waliofanya vizuri msimu huu
katika ligi kuu ya soka nchini England ‘Premier League’ anasifika kwa kipaji,
akili na hata umbile la kisoka ikiwa ni pamoja na uwezo wa kumaliza mipira ya
mwisho akitoa msaada mkubwa katika sehemu ya kiungo ya Everton maarufu “Toffee”.
Fellaini alisaini
mkataba wa miaka mitano mwaka uliopita lakini inasemekana anataka kuondoka Goodison
Park, ambapo vilabu mbalimbali vikiwa vinataka huduma yake.
Real Madrid ni
moja kati ya klabu kubwa inayo muawania mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25,
ambaye anasubiri kuona kama Everton itafuzu klabu bingwa Ulaya msimu huu na
kuamua hatma yake.
Mario Balotelli, Manchester City
Baada ya
kuwepo taarifa kwa muda mrefu kuwa huenda akaondoka katika klabu yake ya Manchester
City, Super Mario Balotelli huenda akatimiza azma hiyo hivi karibuni baada ya dirisha kufunguliwa.
Akiwa
amefunga goli moja msimu huu, mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22
uwanjani ameonekana kutokuwa na thamani hususani kutokana na kuzongwa na matatizo
mengi ya nje ya uwanja.
Itategemea na
taarifa ipi utakayo amini juu ya habari za Balotteli lakini ukweli ni kwamba
meneja Roberto Mancini huenda akamuondosha kikosini ama akampa nafasi ya mwisho
kutegemeana na vile anaona inafa.
Kutokana pia
na City kuwa na azina kubwa ya washambuliaji, City huenda ikalazimika kukubali
taarifa za tetezi kwamba Milan ilikuwa ikimtaka kwa ada ya uhamisho ya pauni
milioni could be forced to accept a rumored 20.
Wilfried Zaha, Crystal Palace
Kiungo huyo
mwenye umri wa miaka 20 amekuwa akivutia na kusisimua sana katika timu
inayoshiriki ligi ndogo ya pili kwa ukubwa nchini England(Championship) ya
Crystal Palace.
Ana mambo mengi yan kuvutia ikiwemo nguvu na
kipaji kiasi kupelekea kuitwa katika kikosi cha hivi karibuni cha timu ya taifa
England.
Zaha ameonyesha
wazi kutaka kuihama klabu yake mwezi januari ambapo tayari kuna klabu kama Liverpool,
Arsenal, Manchester United, Tottenham, Chelsea na hata Real Madrid zikiwa
zinamnyemelea na inaonekana wazi Palace haina ubavu wa kumzuia kiungo
waliomsajili kwa pauni milioni 15.
Benat Etxeberria, Real Betis
Kiungo huyu
ana umri wa miaka 25 raia wa hispania amekuwa anacheza soka la kupendeza katika
klabu ya Betis na kumekuwepo na taarifa za uwezekano mkubwa wa kuihama klabu yake
mwezi huu wa januari dirisha litakapo funguliw.
Kiungo huyo
wa zamani wa Bilbao hivi karibuni aliitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya
Hispania na kuna taarifa kuwa amekuwa akitakiwa na Barcelona.
Spartak
Moscow na Wolfsburg pia zimetajwa kumuhitaji kama ilivyo kwa vilabu vya England
ambavyo ni Tottenham, Liverpool Arsenal.
Bafetimbi Gomis, Lyon.
Nyota wa
kimataifa wa Ufaransa amekuwa katika kiwango kizuri katika msimu huu akiifungia
magoli 11 katika ligi kikosi cha Les Gones. Kwasasa klabu yake ya Lyon ya
nchini Ufaransa imefulia kiunchumi na inalazimika kumuuza mlinda mlango wake
nyota Hugo Lloris kwenda Tottenham majira ya kiangazi.
Gomis mwenye
umri wa miaka 27 huenda akajiunga na Chelsea na Liverpool ambao wote wako
mawindoni kumsaka mshambuliaji huyo aliyethaminishwa kwa pauni milioni 15.
UHAMISHO: CHELSEA KUNASA KADHAA LAKINI BA…??
>>STURRIDGE KUTUA LIVERPOOL??
>>NEWCASTLE YAMPATA BEKI WA KIMATAIFA WA FRANCE!!
![BENITEZ-CHELSEA](http://www.sokainbongo.com/images/stories/BENITEZ-CHELSEA.jpg)
![DEMBA_BA](http://www.sokainbongo.com/images/stories/DEMBA_BA.jpg)
Chelsea walikuwa na nia ya kumnunua
Demba Ba ili awe anatoa sapoti kwa Straika wao Fernando Torres baada ya
kukosa kumchukua Radamel Falcao wa Atletico Madrid katika Dirisha la
Uhamisho la Januari baada ya Klabu hiyo ya Spain kung’ang’ania kuwa
hawezi kuhama sasa labda mwishoni mwa Msimu.
Kuhusu Demba Ba, kikwazo kikubwa ni kuwa
Meneja wa Newcastle, Alan Pardew, hapendezewi kumuuza Straika ambae
amefunga Bao 13 kwenye Ligi na pia Mkataba wa Mchezaji huyo una
kipengele kuwa Uhamisho wowote ule lazima uambatane na Malipo ya Pauni
Milioni 7.5.
Na habari toka ndani ya Klabu ya Chelsea
zimedokeza kuwa Liverpool watailipa Chelsea Pauni Milioni 12 ili
kumnunua Daniel Sturridge ambae imeripotiwa alishapimwa afya yake huko
Liverpool na Uhamisho rasmi unasubiri Januari 1 wakati Dirisha la
Uhamisho litakapofunguliwa.
Nae Meneja wa muda wa Chelsea Rafa
Benitez amekataa kuzungumza lolote kuhusu Ba pale aliposema:
“Hatuzungumzii shughuli zetu hadharani. Yeye ni Mchezaji wa Klabu
nyingine na huwa siongelei Wachezaji wengine!”
NEWCASTLE KUMSAINI MATHIEU DEBUCHY TOKA LILLE
Newcastle imefikia makubaliano kumsaini Beki wa Kimataifa wa France, Mathieu Debuchy, kutoka Klabu ya Ufaransa, Lille.
Beki huyo wa kulia mwenye Miaka 27
alichezea Mechi zote 4 za France kwenye EURO 2012 na inasadikiwa Ada
yake ya Uhamisho ni Pauni Milioni 5.
Debuchy anakuwa Mchezaji wa pili
kusainiwa na Newcastle kutoka Lille hivi karibuni baada ya Klabu hiyo
pia kumchukua Kiungo Yohan Cabaye Juni 2011.
PATRICK LIEWING MFARANSA MPYA WA SIMBA ATUA SIMBA MCHANA WA LEO TU
![]() |
Katibu wa Simba, Evodius Mtawala (kushoto) akiongozana na kocha mpya wa klabu hiyo, Patrcik Liewig baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam mchana huu. |
![]() |
Mtawala na Liewig |
![]() |
Liewig, Mwenyekiti mpya wa Kamati ya Ufundi, Dani Manembe na Mtawala |
![]() |
Anazungumza na Waandishi |
![]() |
Anapanda kibasi |
![]() |
Ndani ya kibasi |
![]() |
Wanachama waliokuja kumlaki |
SEKIETE APORWA MAMILIONI YA SIMBA JUZI KATIKA MGAWO WA MECHI YA SIMBA NA TUSKER
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhtZcGucmYhKLFVfq1NmVkrpwIqi0FGtdVe-Qg4JUottS9yRPl1p4Vva69u9K_ACfEtDzKjyMi45Xw0upsjnqzGgIAzfgWVX28elypoMOH_k9ERZNtQ2zqr8j9G0eDlG7g39bKdw01TLsZG/s400/DSCF5591.jpg)
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela amesema kuwa Sh. milioni 7.59 na dola za Marekani 2,000 ambazo Simba walizipata baada ya makato ya mapato ya mechi yao dhidi ya Tusker FC ya Kenya iliyomalizika kwa wenyeji Simba kuchapwa 3-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
“Simba ilipata mgawo wa Sh. milioni 10.6 na dola za Marekani 2,000 (Sh. milioni tatu) kutokana na mapato ya kiingilio cha mechi yao dhidi ya Tusker. Baada ya makato, walibakiwa na Sh. milioni 7.59 ambazo Sekiete alikabidhiwa,” alisema Kamanda Kenyela.
Amesema kuwa baada ya kukabidhiwa fedha hizo, Sekiete na mwenzake Stanley Phillipo (23) ambaye alidaiwa kuwa ni mwanafunzi, walipanda kwenye gari aina ya Toyota Premio yenye namba za usajili T869 BKS lililokuwa likiendeshwa na Said Pamba na kwamba walipofika eneo hilo, dereva aliwashusha na kwamba wakaanza kutafuta teksi.
Aliendelea kueleza kuwa muda mfupi baada ya kushushwa, Sekiete na Philipo waliamua kuvuka upande wa pili wa barabara iendayo Kijitonyama ili wachukue teksi lakini ghafla walitekwa na watu sita walioshuka kutoka kwenye pikipiki tatu.
“Mmoja wa watu walioshuka kwenye pikipiki alikuwa na bastola na alifyatua risasi hewani wakati wenzake wakipora begi lenye fedha kutoka kwa mhasibu,” alisema Kenyela.
Aliendelea kufafanua kuwa wakati watu hao wakimnyang’anya begi Sekiete walikuwa wakitamka maneno ya kejeli kwa uongozi wa Simba.
Aliyanukuu maneno hayo kwa kusema; “Mnafungwa halafu mnazingua, na kwa kuwa viongozi wenu wanakula pesa za klabu, nasi hizi tunaziiba.”
Kamanda Kenyela alisema kuwa baada ya watu hao kupora fedha hizo, walitokomea kusikojulikana na hadi sasa, Jeshi la Polisi linawashikilia watu watatu akiwamo Sekiete kuhusiana na tukio hilo.
Watu wengine wanaoshikiliwa na jeshi hilo katika Kituo cha Polisi Magomeni ni Pamba na Philipo ambao walikuwa pamoja na Sekiete kwenye gari.
“Sisi (Jeshi la Polisi) tulishaonya watu kusafirisha kiasi kikubwa cha fedha bila ulinzi, tunawashikilia watu hawa watatu kwa sababu huenda walipanga kuiba fedha hizo,” aliongeza.
“Mazingira ya kuporwa kwa fedha hizo yanatia shaka huenda kuna kitu kilikuwa kimepangwa ili fedha hizo ziibwe. Iweje mtu akahifadhi nyumbani kwake kiasi kikubwa cha fedha kama hicho?” alihoji Kamanda Kenyela.
“Kwa sasa mtu yeyote atakayeripoti kuporwa fedha kiasi kikubwa kama hiki na alikuwa akisafirisha pasipo na ulinzi, tutaanza naye.
“Tunawashikilia watatu kwa uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo. Tunaomba ushirikiano kuto
ka watu wenye taarifa juu ya waliohusika na tukio hili.”
Mwenyekiti wa Simba, Aden Rage aliliambia gazeti hili jana kuwa amesikitishwa na taarifa za kuporwa kwa fedha za klabu yao.
“Mhasibu wetu anaishi Sinza. Alizichukua zile fedha za klabu akazihifadhi nyumbani kwake ili leo (jana) azipeleke benki,” alisema Rage.
AFCON 2013: IVORY COAST YATAJA 23, DROGBA, YAYA, GERVINHO NDANI!
![AFCON_2013_LOGO](http://sokainbongo.com/images/stories/AFCON_2013_LOGO.jpg)
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
AFCON 2013
MAKUNDI:
KUNDI A: South Africa, Cape Verde, Morocco, Angola
KUNDI B: Ghana, DR Congo, Niger, Mali
KUNDI C: Zambia, Ethiopia, Nigeria, Burkina Faso
KUNDI D: Ivory Coast, Togo, Tunisia, Algeria
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KIKOSI KAMILI:
MAKIPA: Copa Barry (Lokeren/Belgium), Daniel Yeboah (Hana Klabu), Badara Sangaré (Sewe San Pedro)
MABEKI: Abib Kolo Touré
(Manchester City/England), Souleyman Bamba (Trabzonspor/Turkey),
Emmanuel Eboué (Galatasaray/Turkey), Siaka Tiéné (PSG/France), Arthur
Boka (Stuttgart/Germany), Ismaël Traoré (Brest/France), Igor Lolo (FC
Kuban/Russia)
VIUNGO: Didier Zokora
(Trabzonspor/Turkey), Cheik Tioté (Newcastle/England), Yaya Gnégnéri
Touré (Manchester City/England), Max Gradel (Saint-Etienne/France),
Romaric N'Dri (Saragosse/Spain), Abdul Razak (Manchester City/England),
Didier Ya Konan (Hanovre/Germany)
WASHAMBULIAJI: Salomon
Kalou (Lille/France), Gervinho (Arsenal/England), Didier Drogba
(Shanghaï Shenhua/China), Wilfried Bony (Vitesse Arnhem/Netherlands),
Lacina Traoré (Anzhi Makhachkala/Russia), Arouna Koné (Wigan/England)
MESSI W ALIVERPOOL SUAREZ AIPIGIA BAO MBILI TIMU YAKE IKIIUA QPR 3 BILA
Bao
3 ndani ya Dakika 28 za kwanza leo zimewapa Liverpool, waliocheza bila
Meneja wao Brendan Rodgers ambae ni mgonjwa, ushindi wa 3-0 na kuzidi
kuwadidimiza mkiani mwa Ligi Kuu England QPR huku Liverpool wakipanda
nafasi moja na kumaliza Mwaka 2012 wakiwa nafasi ya 9.
Ushindi wa Liverpool ulipatikana kwa Bao za Luis Suarez, Bao 2, na Daniel Agger.
VIKOSI:
QPR: Julio Cesar, Onuoha, Nelsen, Hill, Traore, Mackie, Diakite, Mbia, Wright-Phillips, Taarabt, Cisse
Akiba: Green, Derry, Ferdinand, Granero, Da Silva, Hoilett, Faurlin.
Liverpool: Reina, Johnson, Skrtel, Agger, Jose Enrique, Allen, Henderson, Downing, Gerrard, Sterling, Suarez
Akiba: Gulacsi, Assaidi, Coates, Lucas, Carragher, Fernandez Saez, Shelvey.
Refa: Anthony Taylor
BPL: MECHI ZA KUANZA 2013 ni JUMANNE JANUARI 1!
![BPL_LOGO](http://sokainbongo.com/images/stories/BPL_LOGO.png)
BPL, Barclays Premier League, itafungua
Mwaka mpya 2013 kwa Mechi 7 Jumanne Januari Mosi na Mechi 3 Jumatano
Januari 2 huku Mabingwa watetezi Manchester City, ambao wako nafasi ya
pili, kucheza nyumbani na Stoke City na Vinara wa Ligi, Manchester
United, kuwa ugenini kuivaa Wigan.
Mechi za Ligi Kuu England kwa Mwezi
Januari zitakuwa zikipisha Mechi za FA CUP kwa Wikiendi ya kuanzia
Januari 5 ambapo Raundi ya 3 ya FA CUP itachezwa, Raundi ambayo Timu za
Ligi Kuu England ndipo zinaanza Mashindano hayo na pia Wikiendi ya
Januari 26 ambapo Raundi ya 4 ya FA CUP itachezwa.
+++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumanne 1 Januari 2013
SAA 9 Dak 45 Mchana]
West Brom v Fulham
[SAA 12 Jioni]
Man City v Stoke City
Swansea v Aston Villa
Tottenham v Reading
West Ham v Norwich
Wigan v Man United
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Southampton v Arsenal
Jumatano 2 Januari 2013
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Chelsea v QPR
Liverpool v Sunderland
[SAA 5 Usiku]
Newcastle v Everton
+++++++++++++++++++++++
Kimsimamo, Manchester United wako mbele
kileleni kwa Pointi 7 wakifuatiwa na Man City na Timu ya 3 ni Chelsea,
wenye Mechi moja mkononi, wakiwa Pointi 4 nyuma ya Man City.
Nafasi ya 4 inakamatwa na Tottenham
lakini Arsenal wana nafasi ya kuikamata nafasi hiyo kwa vile wana Mechi
moja mkononi baada ya Mechi yao na West Ham iliyokuwa ichezwe Desemba 26
kuahirishwa na sasa itachezwa Januari 23.
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO:
=Tofauti ya Magoli inatajwa kwa Timu zilizofungana Pointi
1 Man United Mechi 20 Pointi 49
2 Man City Mechi 20 Pointi 42
3 Chelsea Mechi 19 Pointi 38
4 Tottenham Mechi 20 Pointi 36
5 Arsenal Mechi 19 Pointi 33 [Tofauti ya Magoli 18]
6 Everton Mechi 20 Pointi 33 [Tofauti ya Magoli 8]
7 WBA Mechi 20 Pointi 33 [Tofauti ya Magoli 3]
8 Stoke Mechi 20 Pointi 29
9 Liverpool Mechi 20 Pointi 28 [Tofauti ya Magoli 5]
10 Swansea Mechi 20 Pointi 28 [Tofauti ya Magoli 5]
11 Norwich Mechi 20 Pointi 25 [Tofauti ya Magoli -9]
12 West Ham Mechi 19 Pointi 23
13 Sunderland Mechi 20 Pointi 22
14 Fulham Mechi 20 Pointi 21
15 Newcastle Mechi 20 Pointi 20
16 Wigan Mechi 20 Pointi 18 [Tofauti ya Magoli -13]
17 Aston Villa Mechi 20 Pointi 18 [Tofauti ya Magoli -24]
18 Southampton Mechi 19 Pointi 17
19 Reading Mechi 20 Pointi 13
20 QPR Mechi 20 Pointi 10
+++++++++++++++++++++++
WAFUNGAJI BORA:
Robin van Persie MAGOLI 14
Demba Ba 13
Miguel Michu 13
Luis Suarez 13
Jermain Defoe 10
Gareth Bale 9
Edin Dzeko 8
Marouane Fellaini 8
Steven Fletcher 8
Rickie Lambert 8
Theo Walcott 8
Sergio Aguero 7
Santi Cazorla 7
Juan Mata 7
Wayne Rooney 7
Carlos Tevez 7
Fernando Torres 7
+++++++++++++++++++++++
RATIBA MECHI ZIJAZO-LIGI KUU ENGLAND:
**WIKIENDI YA JANUARI 5 MECHI ZA RAUNDI YA 3 FA CUP
Jumamosi 12 Januari 2013
[SAA 12 Jioni]
Aston Villa V Southampton
Everton V Swansea
Fulham V Wigan
Norwich V Newcastle
Reading V West Brom
Stoke V Chelsea
Sunderland V West Ham
Jumapili 13 Januari 2013
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Man United V Liverpool
[SAA 1 Usiku]
Arsenal V Man City
Jumatatu 14 Januari 2013
[SAA 5 Usiku]
QPR V Tottenham
Jumamosi 19 Januari 2013
[SAA 12 Jioni]
Liverpool V Norwich
Man City V Fulham
Newcastle V Reading
Swansea V Stoke
West Ham V QPR
Wigan V Sunderland
[SAA 2 na Nusu Usiku]
West Brom V Aston Villa
Jumapili 20 Januari 2013
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Chelsea V Arsenal
[SAA 1 Usiku]
Tottenham V Man Utd
Jumatatu 21 Januari 2013
[SAA 5 Usiku]
Southampton V Everton
Jumatano 23 Januari 2013
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Arsenal V West Ham
**WIKIENDI YA JANUARI 26 MECHI ZA RAUNDI YA 4 FA CUP
Jumanne 29 Januari 2013
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Aston Villa V Newcastle
Norwich V Tottenham
QPR V Man City
Stoke V Wigan
Sunderland V Swansea
[SAA 5 Usiku]
Reading V Chelsea
Jumatano 30 Januari 2013
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Arsenal V Liverpool
Everton V West Brom
Fulham V West Ham
[SAA 5 Usiku]
Man United V Southampton
GAZETI LA ;daily mail
Streka wa Newcastle United Demba Ba, 27, yupo karibu kujiunga na chelsea kwa euro £7.5m-january kw akusaini miaka mitatu kuichezea timu ya chelsea katika dimba la t Stamford Bridge.
![Demba Ba](http://news.bbcimg.co.uk/media/images/65015000/jpg/_65015777_demba_ba_getty.jpg)
Demba Ba has scored BA ameshafunga bao 13 msimu huu kwa newcastle
Midfielder wa Liverpool Joe Cole, 31, anatarajia kujiunga na timu ya QPR january na wapo katika mazungumzo ya kumuuza QPR kwa bossi Harry Redknapp
Kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Italy Marcello Lippi wameshakubaliana na AC Milan kumsainisha mshambuliaji wa Shanghai Shenhua na mshambuliaji wa -Chelsea Didier Drogba, 34.
QPR january watampa manager wao Harry Redknapp £20m kwa ajili ya kumsainisha
midfielder wa Rennes ya Ufaransa Yann M'Vila, 22, na Mshambuliaji wa Marseille Loic Remy, 25, na midfielder wa West
Ham united Mohamed Diame, 25.
SEHEMU NYINGINE
Midfielder wa Real Madrid ya Hispania na midfielder wa zamani wa Liverpool Xabi Alonso, 31, anataka kurudi Premier League.
Klabu ya Arsenal imempa mshambuliaji wao Theo Walcott, 23,weeks 2 ili asaini mkataba mpya wa kalabu hiyo.
MCHEZAJI BORA CHALLENGE ATUA AZAM LEO
![]() |
Umony |
MCHEZAJI
bora wa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge, Brian
Umony anatarajiwa kuwasili leo mjini Dar es Salaam kujiunga na klabu yake mpya,
Azam FC.
Umony anawasili
siku mbili tu, baada ya wachezaji wengine wapya wa Azam, kutoka Kenya, beki
Joackins Atudo na kiungo Humphrey Mieno kuwasili Dar es Salaam kujiunga na
klabu yao hiyo mpya.
Nyota hao
wote watatu, watakuwemo kwenye kikosi kitakachokwenda visiwani Zanzibar kesho kwenye
michuano ya Kombe la Mapinduzi.
Brian
amerejea nyumbani Uganda mwaka huu na kujiunga na KCC baada ya kumaliza mkataba
wake katika klabu ya Becamex Binh Duong F.C. ya Vietnam.
Mwaka 2009, ilikuwa
aje kuichezea Simba SC ya Dar es Salaam, lakini Wekundu hao wa Msimbazi wakazidiwa
kete na SuperSport United ya Afrika Kusini.
Umony
aliichezea Supersport United hadi 2010 alipohamia University of Pretoria ya
Afrika Kusini pia hadi mwaka 2011 alipohamia Portland Timbers ya Marekani kwa
mkopo na mwaka huu akatua Becamex Binh Duong F.C. kabla ya kurejea Uganda na
sasa anakuja kuanza maisha mapya Azam FC 2012.
Kwa upande
wa Atudo na Mieno, wao walianza kuichezea Azam katikati ya mwezi huu na
walikuwepo kwenye kikosi cha timu hiyo kilichotwaa Kombe la Hisani la Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), linaloandaliwa na FECOFA, Shirikisho la Soka la
DRC wiki iliyopita, baada ya kuwachapa wenyeji, Dragons FC kwa penalti 4-2
kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90.
Azam iliingia
fainali, baada ya kufanikiwa kuitoa kwa mikwaju ya penalti 5-4 Shark FC ya DRC
Ijumaa, kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90 kwenye Uwanja wa Martyrs.
Kikosi kizima
cha Azam kilichoshiriki mashindano hayo ni Kipre Tchetche, Seif Abdallah, Kipre
Balou, Zahor Pazi, Jackson Wandwi, Malika Ndeule, Uhuru Suleiman, Omar Mtaki,
Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo, Gaudence Mwaikimba, Abdi Kassim, Luckson
Kakolaki, Samih Hajji Nuhu, Mwadini Ally, Himid Mao, David Mwantika, Waziri
Salum, Humphrey Mieno na Joackins Atudo.
Katika
mashindano hayo, Gaudence Mwaikimba aliibuka mfungaji bora kwa mabao yake
matatu, ukiachilia mbali mawili ya penalti. Mchezaji mwingine wa kigeni wa
Azam, Brian Umony wa Uganda, atajiunga na timu hiyo baada ya sikukuu pia.
Azam
wamepangwa Kundi B, katika Kombe la Mapinduzi pamoja na Mtibwa Sugar ya Morogoro,
Coastal Union ya Tanga na Miembeni ya Unguja.
Kundi A lina
timu za Simba SC, Tusker FC ya Kenya, Bandari ya Unguja na Jamhuri ya Pemba.
Michuano ya Kombe
la Mapinduzi, ambayo ni maalum kwa ajili ya kuherehekea Mapinduzi matukufu ya
Zanzaibar, inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 2, hadi kilele cha miaka 49
ya Mapinduzi ya Zanzibar, Januari 12, mwakani, huku ikishirikisha timu kutoka
ndani na nje ya Tanzania.
KOCHA WA SIMBA AWASILI LEO SAA SABA NA NUSU UWANJA WA NDEGE WA JK
![]() |
Liewig |
WAKATI kocha
mpya wa Simba, Mfaransa Patrick Liewig anatarajiwa kuwasili leo saa 7.25 mchana,
kikosi cha Wekundu hao wa Msimbazi kinatarajiwa kuondoka leo kwenda visiwani
Zanzibar kushiriki Kombe la Mapinduzi.
Makamu
Mwenyekiti wa Simba, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ amesema kwamba, Liewig
ambaye ni kocha wa zamani wa Akademi ya Paris Saint Germain (PSG) ya Ufaransa,
ASEC Mimosas ya Ivory Coast na Club Africain ya Tunisia, atakapofika atasaini
mkataba na kuanza kazi mara moja.
Kaburu alisema
kocha huyo mwenye Stashahada ya Juu ya ukocha na Shahada ya tatu ya ualimu wa
soka ya vijana aliyotunukiwa na Mkurugenzi wa Ufundi wa Ufaransa, Gerard Houiller,
atakwenda na timu Zanzibar.
Liewig pia
amehudhuria kozi za ufundishaji mazoezi ya viungo Juni mwaka 1999 katika Chuo
Kikuu cha Dijon.
Kwa upande
wa uzoefu, Liewig alifanya kazi PSG kuanzia mwaka 1989 hadi 1999 kama Kocha
Mkuu wa akademi na kuna wakati alikuwa akishirikishwa pia katika programu za
timu A, ingawa majukumu yake zaidi yalikuwa ni kwa Under 20, Under 18 aliowawezesha
kutwaa Kombe la French Junior Gambardella na Under 16.
Kuanzia
mwaka 1989 hadi 1990: alikuwa Meneja
Mkuu wa Tomislav IVIC, 1990 hadi 1991 alikuwa Msaidizi wa Henri Michel, 1991 hadi
1994 alikuwa Msaidizi wa Artur Jorge, 1994 hadi 1996 alikuwa Msaidizi wa Luis Fernandez,
1996 hadi 1998: alikuwa Msaidizi wa Ricardo Gomez, 1998 hadi 1999 alikuwa
Msaidizi wa Alain Giresse.
Liewig pia
alifundisha Al Wahda FC ya Abu Dhabi kuanzia 1999 hadi 2001, ambayo aliipa
ubingwa wa Ligi Kuu ya nchi hiyo na Kombe la Ligi.
Januari
mwaka 2003 alikuwa Msimamizi wa Chama cha Soka UAE katika fainali za Afrika za
U20 nchini Burkina Faso.
Kuanzia
mwaka 2004 hadi 2009 alikuwa Kocha wa ASEC Mimosas ya Ivory Coast aliyoipa
mataji matatu ya Ligi Kuu ya nchini humo mfululizo, 2004, 2005 na 2006, Super
Cup ya nchini humo 2005, 2007, 2008 na 2009 na akaiwezesha kufuzu hatua ya
makundi ya Ligi ya Mabingwa mara tatu, mara moja akiifikisha Nusu Fainali.
Amekuwa
Kocha bora wa Ivory Coast miaka mitatu mfululizo, 2004, 2005 na 2006 na tangu Septemba
mwaka jana hadi Juni mwaka huu, alikuwa kocha wa Club Africain ya Tunisia.
YANGA WAANZA MAZOEZI LEO ULAYA
![]() |
Hoteli waliyofikia Yanga inavyoonekana, wanakula raha aje? |
Mabingwa
mara tano wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, wapo
nchini humo kwa uenyeji wa kampuni ya Utalii ya Team Travel ya nchini humo na
watakuwa huko kwa wiki mbili kuanzia jana.
Vinara hao
wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, wamefikia katika hoteli ya Fame Residence
Lara & Spa kilomita chahce kutoka katika Uwanja wa ndege wa Antalya, ambako
hoteli ya Fame Residence ipo mwambaoni mwa bahari ya Mediteranian.
Yanga iliondoka
Dar es Salaam Alfajiri ya jana, saa 10:30 na kikosi kizima pamoja na benchi la
ufundi kamili.
Waliopo
Uturuki ni makipa; Ally Mustafa 'Barthez', Said Mohamed na Yussuf Abdul, mabeki
Juma Abdul, Shadrack Nsajigwa, Godfrey Taita, Stefano Mwasyika, Oscar Joshua, Mbuyu
Twite, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Ladisalus Mbogo na Kelvin Yondani.
![](http://api.ning.com:80/files/*JdnwHQL9f778Ln2H7TpTLRlmtT-MZxN98RJbIbqzhPdBwQO7Ipp4AW3zNn0vC3L*9UK7n8DujVWhcfUrc4rlrRKDS1YdpSe/SIMBAVSYANGAOKTOBA320127.jpg?width=650)
Upande wa
benchi la ufundi ni Kocha Mkuu Mholanzi, Ernie Brandts, Kocha Msaidizi Freddy
Felix Minziro na Kocha wa makipa, Razak Ssiwa, na Maofisa wengine ni Daktari wa
timu, Sufiani Juma, Meneja Hafidh Saleh, Ofisa Habari, Baraka Kizuguto Mjumbe
wa Kamati ya Utendaji, Mohammed Nyenge.
Mwandishi wa
Gazeti la Mwanaspoti, Michael Momburi aliondoka jana usiku, yeye akigharamiwa
na kampuni yake.
Ziara ya
mwisho katika nchi ya maana kwa Yanga, ilikuwa mwaka 2008 nchini Afrika Kusini,
ambako iliweka kambi ya zaidi ya wiki mbili wakati huo ikiwa chini ya Profesa
Dusan Savo Kondic, raia wa Serbia.
Zaidi ya
hapo, mwaka huu Yanga ilikwenda Kigali, Rwanda kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya
Bara, kwa mwaliko wa rais wa nchi hiyo, Paul Kagame. Yanga pia imewahi kufanya ziara Brazil mwaka
1974 na Romania 1979.
Yanga SC ni
klabu kongwe Tanzania ambayo kati ya zinazoshiriki Ligi Kuu kwa sasa, yenyewe
ndio yenye umri mkubwa zaidi.
Ingawa
historia inasema Yanga ilizaliwa mwaka 1935 na Simba mwaka 1936, lakini ukizama
ndani utagundua kwamba, huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa utani na upinzani wa jadi,
baina ya miamba hiyo ya soka nchini.
Kulikuwa
kuna timu inaitwa New Youngs, ambayo mwaka 1938 ilisambaratika na baadhi ya
wachezaji wake wakaenda kuunda timu iliyokuwa ikiitwa Sunderland, ambayo hivi
sasa inajulikana kama Simba.
Kabla ya
kutokea vurugu zilizoisambaratisha New Youngs, vijana wa Dar es Salaam walikuwa
wana desturi ya kukutana viwanja vya Jangwani kufanya mazoezi na baada ya muda
wakaamua kuunda timu yao, waliyoipachika jina Jangwani.
Ndani ya
kipindi kifupi tu, timu hiyo iliteka hisia za wengi, waliojitokeza
kujiandikisha uanachama wa klabu hiyo. Miongoni mwa waliovutika na uanachama wa
klabu hiyo ni Tarbu Mangara (sasa marehemu) na ilipofika mwaka 1926, walifanya
mkutano wa kwanza katika eneo ambalo hivi kuna shule ya sekondari ya Tambaza.
Miongoni mwa
yaliyojadiliwa kwenye mkutano huo ni kuiboresha timu hiyo, ambayo wachezaji
wake wengi walikuwa wafanyakazi wa Bandarini na mashabiki wake wengi walikuwa
wabeba mizigo wa bandarini.
Baada ya
mkutano huo, timu hiyo ilibadilishwa jina na kuwa Navigation, iliyotokea kuwa
moto wa kuotea mbali katika timu za Waafrika enzi hizo, kabla ya uhuru wa
Tanganyika. Timu kama Kisutu, Kitumbini, Gerezani na Mtendeni zilikuwa hazifui
dafu kwa wana Jangwani hao.
Ikiwa
inatamba kwa jina la Navigation, wanachama wa timu hiyo walikuwa wakitembea
kifua mbele na kuwatambia wapinzani, kwamba wao ndiyo zaidi. Kwa sababu katika
kipindi hicho, Italia ilikuwa inatamba kwenye ulimwengu wa soka, wanachama wa
timu hiyo nao waliamua kuibadilisha jina timu yao na kuiita Taliana.
Taliana
ilipata mafanikio ya haraka na haikushangaza ilipopanda hadi Ligi Daraja la
Pili Kanda ya Dar es Salaam, mwanzoni mwa miaka ya 1930. jina la Taliana
waliamua kuachana nalo mapema, kabla ya kuingia kwenye ligi hiyo, hivyo
wakaanza kujiita New Youngs.
Lakini kila
ilipokuwa ikibadilisha jina, ilikuwa ikifanya vitu pia, kwani wakiwa na jina la
New Youngs, waliweza kutwaa Kombe la Kassum, lililoshirikisha timu mbalimbali
za Dar es Salaam.
Hatimaye
ukawadia mwaka mbaya kwa New Youngs, 1938 wakati baadhi ya wachezaji
walipojitoa na kwenda kuanzisha Sunderland. Kwa sababu hiyo, waliobaki wakaamua
kubadili jina na kuwa Young Africans, jina ambalo mashabiki wake wengi
walishindwa kulitamka vizuri hivyo kujikuta wakisema Yanga. Safari njema Yanga
SC.
Subscribe to:
Posts (Atom)