Tuesday, October 30, 2012

  MASHINDANO YA FDL KESHO NI KIMBEMBE KATIKA VIWANJA MBALI MBALI HAPA TANZANIA

 


Michuano ya ligi daraja la kwanza FDL kesho inaendelea kwa michezo kadhaa hapa nchini,kundi c kuna michezo minne ambayo itachezwa katika miji ya MARA,MANYARA,DODOMA,na MWANZA.

Kule mara polisimara vs rhino rangers katika dimba la karume ,Manyara kule kuna mechi kati ya moran vs polisi tabora katika dimba la kiteto , Dodoma pale kuna mechi kati ya polisi dodoma  vs pamba katika dimba la jamhuri na kule Kigoma kuna mechi kati ya Kanembwa vs Mwadui katika dimba la lake tanganyika kigoma.

KUNDI A 

Mbeya city vs mlale [sokoine mbeya]

Small kids vs mkamba[mandela sumbawanga]

majimaji vs burkinafaso[majimaji ruvuma ]

polisi iringa vs kurugenzi[samora iringa]

KUNDI B 

mechi itakuwepo novemba mosi mwaka huu kati ya Green warriors vs ashanti[mabatini] novemba pili polisi dar vs villa squad chamazi dar es salaam

 

NSA JOB KUTIBIWA INDIA GOTI LAKE

Mshambuliaji wa Coastal Union, Nsa Job, akivunjika goti akigongana na kipa wa JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Chamazi Jumapili Oktoba 28. 2012. Coastal ilishinda 3-0.

Madaktari wakimsaidia Nsa Job baada ya mguu kuhama kutoka kwenye maungio yake ya goti

Nsa Job akiugulia wakati akipelekwa kwenye gari la wagonjwa tayari kwa safari ya kelekea hospitalini Muhimbili

Nsa Job akiugulia baada ya kufikishwa hospitalini. PICHA ZOTE: Kwa hisani ya Gazeti la MWANANCHI
MSHAMBULIAJI wa timu ya Coastal Union ya Tanga, Nsa Job, ambaye alivunjika mguu baada ya kugongana na kipa wa JKT Ruvu juzi wakati timu hizo zilipokutana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Chamazi amefungwa plasta ngumu na atakosa mechi zote tatu za mzunguko wa kwanza wa ligi zilizobakia.Kwa mujibu wa taarifa zilizoandikwa kwenye tovuti ya klabu hiyo na mkurugenzi wa timu hiyo, Nassor Bin Slum, baada ya vipimo kuonyesha kuwa goti la mshambuliaji huyo liligeuka, madaktari wa hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Moi) walifanikiwa kulirejesha katika hali ya kawaida na kumfunga plasta ngumu ili kuufanya urejee kwenye hali ya awali.
Taarifa hiyo inaongeza kuwa baada ya kupatiwa tiba hiyo, mchezaji huyo aliruhusiwa kurejea katika kambi ya timu hiyo ambayo inajiandaa na mechi yake dhidi ya Azam itakayofanyika kesho kwenye Uwanja wa Chamazi.
"Alhamdulillah ule wasiwasi tuliokuwa nao mwanzo baada ya Nsa Job kuumia sasa niseme umepungua kwani baada ya kumfikisha hospitali na kupigwa X-ray ilionekana tatizo ni 'dislocation of joint' (viungo kupishana katika maungio) na madaktari wamefanya kazi ya ziada kulirudisha goti lake katika sehemu yake na ameshafungwa POP, na hivi sasa amerudi kulala hotelini na wenzake. Inshaallah apone haraka aje kutimiza malengo aliyojiwekea " alisema Nassor katika taarifa aliyoitoa.

Habari zaidi zinasema mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga na Simba atakwenda India kwa matibabu zaidi.Mechi nyingine atakayoikosa mshambuliaji huyo aliyeisaidia timu yake kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ni dhidi ya Polisi Morogoro na dhidi ya mabingwa wa mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame), Yanga ambayo ni ya kufunga mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo itakayofanyika Novemba 11 jijini Tanga.
Daktari wa Coastal Union, Dk. Francis Mganga alisema hali ya kiungo wao Mkenya Jerry Santo aliyeumia pia katika mechi hiyo ya juzi ni mbaya na hawatarajii acheze katika mechi zilizobaki za mzunguko wa kwanza na kwamba mchezaji Joseph Malubo pia ni majeruhi wa uvimbe wa goti. (Habari kutoka


Mshambuliaji wa Coastal Union ya Tanga, Nsa Job akiwa amefungwa bandeji gumu (POP) baada ya kuvunjika goti wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara dhidi ya JKT Ruvu uliofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Coastal Union ilishinda 3-0. 

KAVUMBANGU 100% YANGA


DIDIER Fortine Kavumbagu yuko fiti kuichezea klabu yake, Yanga SC katika mechi ya kesho ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Mgambo JKT, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mrundi huyo alivimba mguu baada ya mechi dhidi ya JKT Oljoro na kushindwa kufanya mazoezi jana, lakini amefanya mazoezi na kumpa moyo kocha Mholanzi, Ernie Brandts kwamba anaweza kutumika kesho.
Beki Kevin Patrick Yondan na mshambuliaji Said Rashid Bahanuzi nao wapo fiti kabisa na leo pia wamefanya mazoezi na wenzao kwa ukamilifu Uwanja wa sekondari ya Loyola, Mabibo, Dar es Salaam.
Kipa Said Mohamed Kasarama na kiungo Juma Seif Dion ‘Kijiko’ wanasumbuliwa na Malaria na hawatashiriki mechi hiyo ya kesho, wakati mabeki Salum Abdul Telela, Juma Jaffar Abdul na Ibrahim Job Isaac wote bado majeruhi.
Yanga iliyovuna pointi tatu kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Oljoro, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha na kupanda nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kutimiza pointi 20 katika mechi 10, kesho inatarajiwa kuendeleza mawindo yake.
Yanga sasa iko nyuma kabisa ya wapinzani wao wa jadi, Simba SC wanaoongoza Ligi Kuu kwa pointi zao 22, baada ya kucheza mechi 10 pia.
Mabingwa hao wa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, wanaweza kupanda kileleni kesho, iwapo Simba itatoa sare au kufungwa na Polisi mjini Morogoro katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu.
Mgambo JKT pamoja na kwamba imepanda Ligi Kuu msimu huu, lakini imeonyesha ni timu ya ushindani baada ya kutoa sare ya bila kufungana na Simba SC, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Kwa sababu hiyo, Yanga wamechukua tahadhari ya kutosha kuelekea mchezo huo na tangu juzi Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Abdallah Ahmad Bin Kleb amekuwa ‘akienda mbio’ kuhakikisha timu inashinda keshokutwa.  
Kurejea kwa Yondan na Bahanuzi kunaongeza matumaini ya ushindi kwa Yanga katika mchezo huo, ingawa upande mwingine ni mtihani kwa Brandts, kwani katika kipindi ambacho wachezaji hao wako ‘wadini’, walioshika nafasi zao wamekuwa wakifanya vizuri.    
Mbuyu Twitwe aliyehamishwa kutoka beki ya kulia hadi beki ya kati tangu Yondan aumie Oktoba 3, amekuwa akifanya vizuri sawa na Jerry Tegete aliyempokea Bahanuzi Oktoba 8, alipoumia naye amekuwa akifanya vizuri pia.
Kwa kuzingatia Twite alikuwa ‘uchochoro’ alipokuwa akicheza pembeni, watu wanasubiri kuona kama Brandts atamrudisha huko huko baada ya Yondan kurejea, au ataamua mmoja kati yao na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ataanzia benchi.
Upande wa Tegete na Bahanuzi, kuna uwezekano mmoja wao atakuwa anaanzia benchi kwa sasa na mwingine kumpokea mwenzake baadaye. 

SIMBA WAWAFUATA KIBABE MAAFANDE WANYONGE MOROGORO

SIMBA SC tangu inaondoka leo Dar es Salaam kwenda Morogoro tayari kwa mchezo wao dhidi ya Polisi mjini Morogoro katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kesho, wakitoka kushinda mabao 3-1 dhidi ya Azam FC Jumamosi na kujiimarisha kileleni.
Mabingwa hao watetezi juzi na jana walifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Kinesi, Urafiki, Manzese, Dar es Salaam na kwa ujumla timu vizuri kuelekea mchezo huo wa tatu kucheza nje ya Uwanja wa Taifa, msimu huu baada ya awali kucheza mechi mbili Tanga dhidi ya Coastal Union na Mgambo JKT ambazo zote walilazimishwa sare ya bila kufungana.
Simba imeshinda mechi zake zote Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kutoa sare mbili tu, dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Yanga 1-1 na 2-2 dhidi ya Kagera Sugar ya Bukoba.
Wekundu hao wa Msimbazi, wapo kileleni mwa Ligi Kuu kwa pointi zao 22 baada ya kucheza mechi 10, wakifuatiwa na wapinzani wao wa tangu enzi za bibi na babu, Yanga SC wenye pointi 20 katika nafasi ya pili.
Beki Juma Said Nyosso na kiungo Haruna Moshi Shaaban ‘Boban’ wanaendelea kutumikia adhabu zao za kusimamishwa, lakini wachezaji wote wengine wapo fiti kabisa, ukiondoa Obadia Mungusa aliyefukuzwa mapema tu kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu.
Simba itamenyana na Polisi iliyorejea Ligi Kuu msimu huu, ambayo inashika mkia katika ligi hiyo, ikiwa haijashinda hata mechi moja tangu kuanza kwa ligi hiyo zaidi ya kutoa sare mbili.
Lakini hiyo haiifanyia Simba idharau mechi hiyo na kocha Mserbia, Milovan Cirkovick ameanza maandalizi ya mapema kwa ajili ya mechi hiyo.
Hofu kubwa kwa Simba ni hali ya Uwanja wa Jamhuri, Morogoro- ni mbaya na kulingana na uzoefu walioupata wa kucheza kwenye Uwanja mwingine mbovu wa Mkwakwani, Tanga wanajua watakuwa na shughuli pevu keshokutwa.
Hadi sasa Simba ndio timu pekee katika Ligi Kuu, ambayo haijapoteza mechi, ikiwa imeshinda mechi sita na kutoa sare nne, wakati Yanga imefungwa mechi mbili na Azam FC na Coastal Union zinazoifukuzia timu hiyo, zimefungwa mechi moja moja.  

MIGAMBO WAIFUATA YANGA NA VIRUNGU VILIVYOITULIZA SIMBA MKWAKWANI



TIMU ya soka ya Mgambo JKT ya mjini Handeni mkoani Tanga, imeondoka leo mjini Tanga, ilikokuwa imeweka kambi kwenda Dar es salaam ambako kesho itashuka dimbani kwenye Uwanja wa Taifa kucheza na wenyeji Yanga katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Mgambo inayoshika nafasi ya 10 kwenye msimamo wa Ligi Kuu hadi sasa kwa kuwa na pointi 10 ikiwa imecheza michezo tisa, imeondoka na wachezaji wake 22 na viongozi watatu kwa ajili ya pambano hilo ambalo timu hiyo ilisema kuwa inalichukulia kwa umakini mkubwa ili waweze kuibuka na ushindi kutokana na kujiandaa vilivyo.
Kocha Mkuu wa timu hiyo Mohamed Kampira, alisema jana mjini hapa kwamba, Yanga waailichukulie kuwa watawafunga kirahisi katika mchezo huo badala yake wategemee kupata upinzani hasa kutokana na kwamba timu hiyo ya Mgambo imejiandaa kuibuka na ushindi ili waweze kukaa katika nafasi nzuri katika mzunguko huu wa kwanza.
"Tunaondoka kesho asubuhi (leo) kwenda Dar es salaam, kama timu tumejiandaa vizuri na tunatarajia kuwapa wakati mgumu Yanga na kuishinda, wasitarajie mteremko, sisi ni timu na tunaamini kwamba tutaibuka na pointi zote tatu," alisema kwa kujiamini Kampira aliyevaa viatu vya aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Stephen Matata aliyetimuliwa baada ya timu hiyo kuanza vibaya kwa kufungwa michezo mitano mfululizo tangu kuanza kwa ligi hiyo.
Kampira alisema hadi sasa wachezaji wake wamekuwa na ari kubwa ya kuibuka na ushindi na hakuna majeruhi wote wapo katika hali nzuri ya kupambana na timu hiyo inayousaka ubingwa mwaka huu kwa udi na uvumba na kwamba amewata mashabiki wa timu hiyo kuiamini kwa wachezaji watafanya kazi iliyokusudiwa.
Mgambo JKT ambayo baada ya kumtimua kocha ilikuwa imeshikwa na kocha msaidizi Josepj Lazaro ambaye aliipa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Morogoro, akaifunga Mtibwa Sugar bao 2-1 kwenye uwanja wa Manungu, ikaifunga Toto African bao 2-0 na ikatoka sare ya 0-0 na Simba mchezo ambao Kampira ilikuwa ni mchezo wake wa kwanza kukaa kwenye benchi la timu hiyo.
Wakati huo huo, mashabiki wa klabu ya Coastal Union ya Jijini hapa, wameipongeza timu yao kwa ushindi walioupata juzi walipoifunga JKT Ruvu bao 3-0 katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es salaam hatau ambayo walisema inatia faraja na wamewataka wacheji wazidi kuongeza bidii ili lengo la kumaliza ikiwa nafasi za juu litimie.
Mmoja wa mashabiki hao Fred Tayasar alisema wamejisikia furaha ushindi huo lakini pia umewapa majonzi makubwa kwa mchezaji wao Nsa Job kuvunjika mguu katika pambano hilo hatua ambayo alisema wapenzi wa timu hiyo wanaangalia uwezekano wa kumchangia fedha kwa ajili ya kumpa ili aweze kujikimu katika kipindi atakachokuwa nje ya uwanja.


BUNJAK ATUPIWA VIRAGO AZAM, KOCHA USHINDI AREJESHWA KAZINI



KOCHA Mserbia wa Azam FC, Boris Bunjak amefukuzwa rasmi leo na sasa aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Muingereza Stewart Hall anarudishwa kazini.
Habari kutoka ndani ya Azam FC zimesema kwamba, sababu za kufukuzwa kwa Mserbia huyo ni kushuka kwa kiwango cha timu, hali iliyosababisha sasa ianguke hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
Tayari Bunjak amekwishapewa haki zake zote na ataondoka Alhamisi, siku ambayo Stewart atawasili kuanza tena kazi Azam FC.
Bunjak anaondoka Azam baada ya kuiongoza timu katika mechi 16, akifungwa nne tu, zote dhidi ya Simba ikiwemo ya juzi ya Ligi Kuu, waliyofungwa 3-1 na kutoa sare tatu.
Bunjak mwenye leseni ya Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA), alitua Azam, Agosti 7, mwaka huu akitokea FC Damac ya Saudia Arabia aliyoanza kuifundisha mwaka jana na kabla ya hapo alifundisha klabu kibao za kwao, zikiwemo FK Sloga Kraljevo, FK Javor Ivanjica, Crvena Zvezda Gnjilane, FK Radnicki Nis, FC Uralan Elista, FK Mladi Radnik, FK Crvena Zvezda Beograd, Al-Shaab, FK Hajduk Kula na Al-Nasr.
Awali, Bunjak aliyezaliwa Novemba 17, mwaka 1954 ( miaka 57), alicheza soka katika klabu za FK Sloga (Kraljevo), FK Vozdovac (Beograd), FK Radnicki (Kragujevac), FK Olimpia (Ljubljana), FK Sumadija (Arandjelovac), FK Sloga (Kraljevo), FK Borac (Cacak) na FK Sloga (Kraljevo).
Stewart alifukuzwa kwa kosa la kukaidi maagizo ya Bodi ya Ukurugenzi ya klabu hiyo, kumpanga Mrisho Khalfan Ngassa katika mechi ya fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame dhidi ya Yanga.
Mserbia huyo anakuwa kocha wa tano kufukuzwa Azam, ndani ya miaka minne tangu ianze kucheza Ligi Kuu, 2008 baada ya Stewart, Mbrazil Neider dos Santos, Sylvester Marsh na Itamar Amorin, Mbrazil mwingine.
Lakini Stewart angalau aliacha kumbukumbu ya taji na Medali Azam, baada ya kuiwezesha kutwaa Kombe la Mapinduzi Januari, kushika nafasi ya pili katika Ligi Kuu Aprili, kabla ya kushika nafasi ya pili Kombe la Urafiki na Kagame miezi miwili iliyopita, mambo ambayo bila shaka yamemfanya afikiriwe tena.
Stewart ana sifa ya kutokuwa mbinafsi na mwenye kuwaamini watu wa chini yake, kwa mfano namna ambavyo alikuwa akimpromoti Kali Ongala. Alimkuta Kali kama mchezaji, lakini kwa sababu ya umri kumtupa mkono, akashauriana naye awe Kocha Msaidizi na mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga, akakubali.
Chini ya Stewart, Kali alikuwa akiachiwa timu aiongoze ili kumjengea kujiamini zaidi na mwezi uliopita aliachiwa timu kwenye Kombe la Urafiki, akaifikisha fainali, ambako ilifungwa na Simba kwa penalti kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90.  
WASIFU WA BORIS BUNJAK:
JINA KAMILI: Boris Bunjak
KUZALIWA: Novemba 17, 1954 (Miaka 57)
KLABU ALIZOCHEZEA:
1967- 1975: FK Sloga (Kraljevo)
1975- 1978  FK Vozdovac (Beograd)
1978- 1979  FK  Radnicki (Kragujevac)
1979- 1980  FK Olimpia (Ljubljana)
1980- 1981  FK  Sumadija (Arandjelovac)
1981- 1985  FK  Sloga (Kraljevo)
1985- 1986  FK  Borac (Cacak)
1986- 1990  FK  Sloga (Kraljevo)
KLABU ALIZOFUNDISHA:
1990-1993:   FK Sloga (Kraljevo)
1995-1996:   FK Javor (Ivanjica)
1996-1997:   Crvena Zvezda (Gnjilane)
1999:                      FK Radnicki (Nis)
2000:                      FC Uralan Elista (Urusi)
2000-2002:   FK Mladi (Radnik)
2002-2004:   FK Crvena Zvezda (Beograd)
2004:                      Al-Shaab (UAE)
2005:                      FK Hajduk (Kula)
2006-2007:   Al-Nasr (Oman)
2009:                      Al Oruba Sur (Oman)
2011:                      FC Damac (Saudi Arabia)
2011:                      AL NASER (Oman)
  
REKODI YA BORIS BUNJAK AZAM
Azam 2-1 Polisi                   (BancABC)
Azam 1-2 Simba B              (BancABC)
Azam 8-0 Trans Camp        (Kirafiki)
Azam 1-0 Prisons               (Kirafiki)
Azam 2-0 Coastal Union     (Kirafiki)
Azam 2-3 Simba SC           (Ngao ya Jamii)
Azam 1-0 Kagera Sugar     (Ligi Kuu)
Azam 2-2 Toto African        (Ligi Kuu)
Azam 3-0 JKT Ruvu           (Ligi Kuu)
Azam 1-0 Mtibwa Sugar     (Ligi Kuu)
Azam 1-0 African Lyon       (Ligi Kuu)
Azam 2-3 Simba SC           (Kirafiki)
Azam 1-0 Polisi                  (Ligi Kuu)
Azam 0-0       Prisons         (Ligi Kuu)                                      
Azam 1-1 Ruvu Shooting    (Ligi Kuu)
Azam 1-3 Simba                 (Ligi Kuu)


TFF YASAKA MILIONI 225 ZA KUIPELEKA MOROCCO SERENGETI BOYS



RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Chillah Tenga amesema kwamba timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys inahitaji zaidi ya Sh Milioni 225 kwa ajili ya kampeni yake iliyobakia ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika mwakani nchini Morocco.
Akizungumza na Waandishi wa Habari makao makuu ya TFF, Ilala, Dar es Salaam, Tenga alisema kwamba shirikisho lake kwa sasa halina fedha hizo, kwa sababu hiyo haina mdhamini, zaidi ya kutegemea misaada ya wadau.
Tenga alisema tayari Kamati ya Vijana ya TFF imekwishakutana kuweka mikakati ya kuiwezesha Serengti kushiriki vema kampeni hizo, ikiwemo kuunda Kamati ya kuisaidia timu hiyo.
Hata hivyo, Tenga hakuitaja Kamati iliyoundwa kwa sababu bado hawajazungumza na Wajumbe walioteuliwa.
Alisema kocha wa timu hiyo, Mdenmark Jacob Michelsen ameomba mechi za kujipima nguvu kabla ya kucheza na Kongo Brazaville kuwania tiketi ya Morocco na Kamati ya Vijana inahangaikia suala hilo kwa sasa.
Alisema tayari kuna mwaliko kutoka Botswana wa Serengeti kwenda kucheza, lakini kutokana na ukosefu wa fedha wanashindwa hadi sasa kutoa jibu.
Kikosi cha wachezaji 25 cha Serengeti Boys kipo kambini mjini Dar es Salaam tangu Oktoba 21, mwaka huu kujiandaa na mechi hiyo, ya kwanza ikichezwa nyumbani Novemba 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, wakati mechi ya marudiano itachezwa wiki mbili baadaye.
Tanzania imefuzu bila jasho hadi kufika hatua hiyo, baada ya wapinzani wake wa awali, Kenya na Misri kujitoa katika Raundi ya Kwanza na ya Pili.
Kama Tanzania itafuzu kushiriki Fainali hizo za mwakani, itapoza machungu ya mwaka 2005 walipofuzu kucheza Fainali za Vijana wa umri huo kwa kuzitoa Rwanda, Zambia na Zimbabwe, lakini baadaye kwa sababu ya ‘kufoji’ umri wa Nurdin Bakari, ikaondolewa mashindanoni.
Zaidi ya Fainali za Mataifa ya Afrika 1980 na CHAN 2009, katika soka ya wanaume, Tanzania haijashiriki fainali nyingine zozote za Afrika tangu iingie kwenye soka ya kimataifa.

UCHAGUZI DRFA JIRANI KABISA NA UCHAGUZI WA TFF

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA), Juma Simba ‘Gadaffi’ (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari leo, kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) juu ya uchaguzi wa chama hicho. Simba amesema uchaguzi wa DRFA utafanyika Desemba 8, mwaka huu na fomu za kugombea nafasi mbalimbali zitaanza kutolewa kesho. Novemba 4 hadi 8, Kamati yake itapitia fomu za walioomba uongozi, Novemba 9 hadi 13 utakuwa muda wa pingamizi kwa wagombea, ambazo zitajadiliwa Novemba 14 hadi 16, wakati Novemba 17 hadi 19 watatoa fursa ya kukata rufaa, ambazo zitasikilziwa Novemba 20 hadi 24 na baada ya hapo, Novemba 25 yatatangazwa majina ya wagombea waliopitishwa. Tarehe hii mpya ya uchaguzi wa DRFA inaufanya usogeleane na uchaguzi wa TFF, ambao utafanyika pia Desemba.   


TENGA ACHEMSHA VITA YA RUSHWA TFF



RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Chillah Tenga amesema kwamba vita dhidi ya rushwa katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ni ngumu na inahitaji sapoti kubwa ya wadau na wapenzi wa mchezo wenyewe ili kuifanikisha.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, makao makuu ya TFF, Ilala mjini Dar es Salaam, Tenga alisema kwamba pamoja awali kuwepo kwa mazingira ya ushahidi wa rushwa, lakini wanashindwa kwa sababu wao wana mipaka yao.
“Hili la rushwa kwa kweli ni gumu, ni gumu kwa sababu sisi tuna mipaka yetu, lazima tupate ushirikiano na vyombo husika. Lazima tupate ushirikiano wa wapenzi wenyewe wa mpira,”alisema Tenga.
Beki huyo wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, alisema wakati mwingine inakuwa vita hiyo inakuwa ngumu zaidi anaposikia hata Waandishi wa Habari wanahusika.
“Mimi sijathibitisha, lakini watu wananiambia viongozi wenyewe wanashiriki mchezo huu. Tena nasikia hadi nyinyi Waandishi wa Habari wakati mwingine mnatumiwa kupenyeza rushwa, kwa kweli inasikitisha,”alisema Tenga.
Kuhusu vipimo vya dawa za kulevya katika Ligi Kuu, Tenga alisema kwamba mchakato wa zoezi hilo unaendelea na walichokifanya kwa sasa ni kuwataaribu na kuwapa muda wahusika waache taratibu.
Alisema wamewapa nusu msimu watumiaji wa mihadarati katika soka ya Tanzania kujiondoa taratibu na tayari wamekwishawaambia hadi  viongozi wa klabu zote, ili zoezi hilo likianza liende vizuri.
“Hatutaki kuwaadhiri vijana wetu, ndiyo maana tumewaambia mapema, ili wale ambao wanavuta bangi kwa mfano, waanze taratibu kula chwingamu waache bangi, ili wakati utakapofika, hakutokuwa na mzaha,”alisema Tenga.

SIMBA SC HAKUNA KULALA, INAUA MMOJA INAWINDA MWINGINE

Wachezaji wa Simba SC

SIMBA SC tangu jana wameendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo wao ujao dhidi ya Polisi mjini Morogoro katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, wakitoka kushinda mabao 3-1 dhidi ya Azam FC Jumamosi na kujiimarisha kileleni.
Mabingwa hao watetezi jana walifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Kinesi, Urafiki, Manzese, Dar es Salaam na kwa ujumla timu vizuri kuelekea mchezo huo wa tatu kucheza nje ya Uwanja wa Taifa, msimu huu baada ya awali kucheza mechi mbili Tanga dhidi ya Coastal Union na Mgambo JKT ambazo zote walilazimishwa sare ya bila kufungana.
Simba imeshinda mechi zake zote Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kutoa sare mbili tu, dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Yanga 1-1 na 2-2 dhidi ya Kagera Sugar ya Bukoba.
Wekundu hao wa Msimbazi, wapo kileleni mwa Ligi Kuu kwa pointi zao 22 baada ya kucheza mechi 10, wakifuatiwa na wapinzani wao wa tangu enzi za bibi na babu, Yanga SC wenye pointi 20 katika nafasi ya pili.
Beki Juma Said Nyosso na kiungo Haruna Moshi Shaaban ‘Boban’ wanaendelea kutumikia adhabu zao za kusimamishwa, lakini wachezaji wote wengine wapo fiti kabisa, ukiondoa Obadia Mungusa aliyefukuzwa mapema tu kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu.
Simba inatarajiwa kuondoka kesho Dar es Salaam kwenda Morogoro kwa ajili ya mchezo dhidi ya Polisi ambayo inashika mkia katika ligi hiyo, ikiwa haijashinda hata mechi moja tangu kuanza kwa ligi hiyo zaidi ya kutoa sare mbili.
Lakini hiyo haiifanyia Simba idharau mechi hiyo na kocha Mserbia, Milovan Cirkovick ameanza maandalizi ya mapema kwa ajili ya mechi hiyo.
Hofu kubwa kwa Simba ni hali ya Uwanja wa Jamhuri, Morogoro- ni mbaya na kulingana na uzoefu walioupata wa kucheza kwenye Uwanja mwingine mbovu wa Mkwakwani, Tanga wanajua watakuwa na shughuli pevu keshokutwa.
Hadi sasa Simba ndio timu pekee katika Ligi Kuu, ambayo haijapoteza mechi, ikiwa imeshinda mechi sita na kutoa sare nne.

YONDAN, BAHANUZI WARUDI RASMI KAZINI YANGA

Bahanuzi


BEKI Kevin Yondan na mshambuliaji Said Bahanuzi waliokuwa nje ya Uwanja kwa zaidi ya wiki mbili kutokana na kusumbuliwa na majeruhi, leo wanatarajiwa kuanza programu rasmi ya mazoezi na wenzao baada ya kupata ahueni ya kutosha.
Wachezaji hao wamekuwa wakifanya mazoezi mepesi kwa zaidi ya wiki moja baada ya kupata ahueni kidogo na sasa wamepona kabisa na leo kocha Mholanzi, Ernie Brandts anatarajiwa kuwajumuisha kwenye programu yake kamili, Uwanja wa sekondari ya Loyola, Mabibo, Dar es Salaam.
Yanga imerejea kutoka Arusha, ambako Jumamosi ilivuna pointi tatu kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji JKT Oljoro, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid na kupanda nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, wakitimiza pointi 20 baada ya kucheza mechi 10.
Yanga sasa iko nyuma kabisa ya wapinzani wao wa jadi, Simba SC wanaoongoza Ligi Kuu kwa pointi zao 22, baada ya kucheza mechi 10 pia.
Mabingwa hao wa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame sasa wanajiandaa na mchezo wao ujao wa ligi hiyo, dhidi ya Mgambo JKT Jumatano Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mgambo JKT pamoja na kwamba imepanda Ligi Kuu msimu huu, lakini imeonyesha ni timu ya ushindani baada ya kutoa sare ya bila kufungana na Simba SC, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Kwa sababu hiyo, Yanga wamechukua tahadhari ya kutosha kuelekea mchezo huo na tangu jana Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Abdallah Ahmad Bin Kleb amekuwa ‘akienda mbio’ kuhakikisha timu inashinda keshokutwa.   
Kurejea kwa Yondan na Bahanuzi kunaongeza matumaini ya ushindi kwa Yanga katika mchezo huo, ingawa upande mwingine ni mtihani kwa Brandts, kwani katika kipindi ambacho wachezaji hao wako ‘wadini’, walioshika nafasi zao wamekuwa wakifanya vizuri.     
Mbuyu Twitwe aliyehamishwa kutoka beki ya kulia hadi beki ya kati tangu Yondan aumie Oktoba 3, amekuwa akifanya vizuri sawa na Jerry Tegete aliyempokea Bahanuzi Oktoba 8, alipoumia naye amekuwa akifanya vizuri pia.
Kwa kuzingatia Twite alikuwa ‘uchochoro’ alipokuwa akicheza pembeni, watu wanasubiri kuona kama Brandts atamrudisha huko huko baada ya Yondan kurejea, au ataamua mmoja kati yao na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ataanzia benchi.
Upande wa Tegete na Bahanuzi, kuna uwezekano mmoja wao atakuwa anaanzia benchi kwa sasa na mwingine kumpokea mwenzake baadaye. 

COASTAL WAISHUSHA TENA AZAM FC MBIO ZA UBINGWA LIGI KUU

Azam FC
USHINDI wa mabao 3-0 wa Coastal Union dhidi ya JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana, umebadilisha kabisa taswira ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya Wagosi hao wa Kaya kupanda hadi nafasi ya tatu wakiiengua Azam.
Mapinduzi katika Ligi Kuu yalianza Jumamosi, baada ya Yanga kupanda hadi nafasi ya pili kutokana na ushindi wao wa bao 1-0 dhidi ya JKT Oljoro, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha huku Azam FC ikifungwa na Simba SC mabao 3-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kushuka nafasi ya tatu.
Lakini Coastal jana imeishusha Azam kwa nafasi moja zaidi, na sasa mbio za ubingwa wa Ligi Kuu zinaonekana kuwa za farasi watatu, lakini Azam si miongoni mwao, bali Simba, Yanga na Coastal.
Mwishoni mwa wiki ijayo, Yanga itacheza na Azam FC, mechi ambayo itatengeneza taswira ya namna mzunguko wa kwanza utakavyomalizika.
Azam ikishinda inaweza kurudi nyuma ya Simba SC, lakini tofauti na hapo watu watasubiri kuona kati ya watani hao wa jadi, nani atamaliza mzunguko wa kwanza akiwa kileleni.    
Kabla ya kucheza na Azam, Yanga itacheza Mgambo Shooting Jumatano, wakati Azam itacheza na Coastal Union Chamazi.
Ligi Kuu sasa inazidi kunoga baada ya juzi Simba kuzinduka kutoka kwenye wimbi la sare, baada ya kufanikiwa kuichapa Azam FC mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi huo, unaifanya Simba izidi kujitanua kileleni mwa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 22, baada ya kucheza mechi 10, wakati Azam FC inapromoka hadi nafasi ya nne kwa pointi zake 18, baada ya kucheza mechi tisa, ikiipisha Coastal yenye pointi 19 katika nafasi ya tatu na Yanga sasa ni ya pili kwa pointi zake 20.
Mechi nyingine za ligi hiyo juzi, African Lyon ilitoka sare ya 1-1 Kagera Sugar Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam na Ruvu Shooting ikaifunga 2-1 Polisi Morogoro Uwanja wa Mabatini, Mlandizi.
Mechi kati ya Mgambo JKT na Prisons iliyokuwa ichezawe juzi Uwanja wa Mkwakwani, Tanga imeahirshwa kutokana na wachezaji wa Prisons kupata ajali wakiwa njiani kuelekea Tanga.
JKT Ruvu jana ilifungwa 3-0 na Coastal Union Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam na Toto Africans ilitoka sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Waamuzi wa soka ,Italia  na washika vibendera watakuwa na wakati mgumu sana katika ratiba ya wiki ijayo ambapo  watakuwa katika ulinzi mkali kuliko wakati mwingine wowote baada ya kufanya vibaya mwishoni mwa juma  Serie A  Ndio ligi peke barani ulaya ambayo inatumia washika vibendera zaidi ya wawili utaratibu unaopendwa zaidi na Rais wa shirikisho la soka barani ulaya  UEFA  Michel Platini, ambapo walishindwa kufanya maamuzi sahihi katika mechi kati ya   Catania na  Lazio vile vile  AS Roma Juventus  Aidha  viongozi wa  Juventus na wameingia matatani katika utetezi baada ya kuonekana wakimshawishi mwamuzi kutoa maamuzi ambayo sio sahihi  .
Rais wa Catania  Antonio Pulvirenti alikuwa na hasira pale timu yake ilipokataliwa goli sahihi dhidi ya  Juventus, ambao walishinda goli kwa sifuri   1-0  dhidi  Arturo Vidal kabla ya mapunziko
ambapo rais wa   Juventus  Andrea Agnelli,  ambaye ijumaa hii alisema shirikisho la soka la italia  lilitakiwa kuipora  Catania alama tatu muhimu kama mfano wa kuchezesha soka kwa mchezo wa haki ilikotoa funzo kwa timu nyingine 
juma hili kumetokea na tabia ya kuwatiahoma waamuzi kufanya maamuzi yasiyo sahihi katika ligi ya italia ambapo tuhuma hizi zimeperekwa zaidi katika benchi la timu ya soka ya juventus kwa kuwashinikiza waamuzi kufanya maamuzi yasiyo sahihi. 


 Senghor aliendelea kusema kuwa ataitisha mkutano wa dharura kesho kwa wajumbe 23 wa kamati ya utendaji waliobakia ili kuziba pengo la wajumbe wanne waliojiuzulu.