Saturday, December 15, 2012

MIENO AKABIDHIWA JEZI YA REDONDO AZAM


Katibu wa Azam, Nassor Idrisa (kulia) akimkabidhi jezi ya klabu hiyo, kiungo wao mpya, Humphrey Mieno waliyemsajili kutoka Sofapaka ya Kenya. Mieno ameungana na kikosi cha Azam mjini hapa Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambako timu hiyo imekuja kucheza Kombe la Hisani. Mieno alikuwepo kwenye kikosi cha Kenya, Harambee Stars kilichofika fainali ya Kombe la CECAFA Tusker Challenge wiki iliyopita na kufungwa 2-1 na wenyeji Uganda, The Cranes.  Amepewa jezi namba 30, ambayo iliwahi kuvaliwa na Ramadhan Chombo ‘Redondo’ aliyehamia SImba SC. 


ZAMALEK YAFUKUZA WAGENI WOTE AKIWEMO OMOTOYOSSI




BEKI wa Zamalek ya Misri, Saied Yousef ametimkia Dhufar ya Oman kwa mkopo wa miezi sita,  habari hii nimeipata kutoka superrsport.com.
Saied alijiunga na Zamalek msimu uliopita akitokea Al Masry ya Misri pia na aling'ara akiwa na White Knights.
"Tumekubali kumruhusu Saied aondoke, na itakuwa nzuri kwake na kwa klabu, ataendelea kulipwa na klabu” Alisema Mjumbe wa Bodi ya Zamalek, Ibrahim Yousef alipozungumza na supersport.com.
"Hajer ya KSA inamtaka beki wetu mwingine Hamada Tolba, lakini tumekataa ofa hiyo” alisema.
Yousef alisema Kocha Mkuu wa timu, Jorvan Vieira anataka kuwatema wachezaji wote wa kigeni kabla ya msimu ujao.
Zamalek ina wageni watatu, ambao ni Abdoulaye Cisse, Razak Omotoyossi na Alexis Enam.

AZAM CHUPUCHUPU WARUDISHIWE AIRPORT KINSHASA, STEWART, KALI NA KINA KIPRE 'WASHUSHIWA' NAIROBI

Askari wa Idara ya Uhamiaji DRC, akiwauzia wachezaji wa Azam FC ya Dar es Salaam kuingia mjini Kinshasa baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa N’djili, mjini Kinshasa usiku wa jana

WAWAKILISHI wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho la Soka Afrika, (CAF), Azam FC wamewasili salama mjini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) majira ya saa 5:58 usiku wa jana kwa saa za huku na saa 7:58 kwa saa nyumbani Tanzania, tayari kucheza mashindano ya Kombe la Hisani mjini hapa.
Hata hivyo, Azam wamewasili pungufu ya watu watano katika msafara wao wa watu 27, kufuatia maofisa na wachezaji wa kigeni kuzuiliwa mjini Nairobi, Kenya kwa kutokuwa na viza za kuingia DRC.
Wenyeji wa Azam, waandaaji wa mashindano waliwahakikishia wageni wao hakutakuwa na tatizo la kuingia DRC bila viza, kwa kuwa wamekwishaandaa utaratibu mzima na msafara mzima utapatiwa viza mara utakapowasili Kinshasa.
Hata hivyo, kwa ujumla hali ilikuwa tofauti, Kocha Mkuu Stewart Hall, Msaidizi wake, Kali Ongala, wote raia wa Uingereza, Daktari Paulo Gomez, raia wa Ujerumani na wachezaji Kipre Tcheche na Kipre Balou raia wa Ivory Coast walizuiwa mjini Nairobi.
Mkuu wa msafara, Katibu wa Azam, Nassor Idrisa alitumia busara kwa kuwapatia fedha za malazi na kujikimu watu hao watano ili wabaki Nairobi kushughulikia viza na wataungana na timu leo baadaye.
Aidha, baada ya kufika Uwanja wa Ndege wa Njili mjini hapa, msafara wa Azam pia ulipata misukosuko mingine, kuanzia uwanjani hapo, wakati Maofisa wa Idara ya Uhamiaji walipokataa kuupokea kwa sababu ya viza.
Ilifikia hatua Maofisa hao wakaagiza msafara urejeshwe kwenye ndege ili kurejea Tanzania, kwa kuwa haukuwa na viza, hata hivyo wenyeji wa mabingwa hao wa Kombe la Mapinduzi, wakafanya jitihada na kufanikiwa kumalizana na Maofisa hao wa Idara ya Uhamiaji.
Kufika katika hoteli ya Florida walipopangiwa kufikia, lilikuwa ni tatizo lingine, kwanza chakula kilikuwa kichache na baadhi ya wachezaji walilala bila kula kabisa. Lakini kwa ujumla mazingira ya hoteli hayakuwa yenye kuridhisha.
Hata hivyo, kwa mara nyingine Katibu, Nassor akatumia busara kwa kukubali timu ilale hadi asubuhi na kupatiwa na hoteli nyingine yenye hadhi, jambo ambalo wenyeji wao waliafiki na kuomba radhi kwa usumbufu wote uliojitokeza.
Katika michuano hiyo, Azam inatarajiwa kufungua dimba leo kwa kumenyana na Dragons kwenye Uwanja wa Martyrs, saa 9:30 za huku, yaani saa 11:30 za nyumbani Tanzania.
Azam ambao ni washindi wa pili wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame na Ligi Kuu, wamepangwa katika Kundi B pamoja na Dragons na Shark FC, ambayo watacheza nayo Desemba 17.
Ikifuzu kwenye kundi lake, Azam itaingia Nusu Fainali moja kwa moja, ambazo zitachezwa Desemba 25 na Desemba 26 itakuwa Fainali na mechi ya kusaka  mshindi wa tatu.  Kundi B, lina timu za DC Motema Pembe, Diables Noirs, FC MK na Real De Kinshasa.  Katibu wa Azam FC, Nassor Idrisa amesema wamekuja kushiriki mashindano haya kwa lengo la kuwapa mazoezi na uzoefu wachezaji wake kabla ya kuingia kwenye Kombe la Shirikisho mwakani.
Alisema Azam pia, itatumia mashindano hayo kama fursa ya kuwapima wachezaji wake kabla ya kuanza kwa Kombe la Shirikisho mwakani, ambako wamepangwa kuanza na Al Nasr Juba ya Sudan Kusini.
Kikosi cha Azam kilichowasili jana hapa, ukiondoa waliozuiwa Nairobi ni; Mwadini Ally, Jackson Wandwi, Gaudence Mwaikimba, Himidi Mao, Ibrahim Mwaipopo, Jabir Aziz, Luckson Kakolaki, Samir Hajji Nuhu, Zahoro Pazi, Seif Abdallah, Malika Ndeule, Omar Mtaki, Abdi Kassim, Uhuru Suleiman, Brian Umony na David Mwantika.
Wachezaji wengine ambao hawahusiki katika safari hiyo, ni wale waliopo kwenye kikosi cha timu ya taifa, Khamis Mcha ‘Vialli’, John Bocco ‘Adebayor’ na Salum Abubakar. Wachezaji wapya, Joseph Mieno na Joackins Atudo kutoka wanaweza kujiunga na timu baadaye mjini hapa.
Katika mchezo wa leo, timu itaongozwa na kocha wa makipa, Iddi Abubakar Mwinchumu ambaye ni ‘Azam Damu’, aliyeipandisha timu kutoka Daraja la Tatu hadi Ligi Kuu kwa kulinda lango vema, huku John Bocco ‘Adebayor’ akitupia nyavuni.
Wachezaji wa Azam FC ya Dar es Salaam wakisubiri kugongewa viza ili watoke ndani ya Uwanja wa Ndege wa N'djili, mjini Kinshasa baada ya kuwasili usiku huu kwa ajili ya kucheza mashindano ya Kombe la Hisani, yanayoanza kesho kwenye Uwanja wa Stade des Martyrs mjini hapa.

Wachezaji wailaumu TFF sakata la Ngasa

Wakati baadhi ya wadau wa soka wakisikitishwa na kitendo cha winga Mrisho Ngassa kukacha kujiunga na timu ya El Merreikh ya Sudan, Chama cha Wachezaji Soka, SPUTANZA, kimelitupia lawama Shirikisho la Soka, TFF, kikidai ndiyo chanzo cha yote.

 Katibu Mkuu wa SPUTANZA, Said George, amesema jana kuwa kutokuwepo kwa elimu ya kutosha kuhusu suala la soka la kulipwa miongoni mwa wachezaji,  mawakala na viongozi wa kandanda nchini ndiko kumesababisha sakata la sasa la uhamisho wa Ngassa.

 George, nyota wa zamani wa timu za Coastal Union na Taifa Stars, amesema SPUTANZA waliliandikia barua TFF mwaka 2008 kutaka iitishe kikao cha uelimishaji kuhusu soka la kulipwa kwa wadau, lakini walipuuzwa.

 Amesema kutokana na ugeni kuhusu soka la kulipwa TFF ilipaswa kutoa elimu ya kutosha ili kuepusha "mambo ya aibu kama yanayotokea sasa", lakini hawakuungwa mkono hivyo inapaswa kulaumiwa.

 Ngassa amekataa kwenda kujiunga na El Mirreikh akidai kuwa uongozi wa klabu mama ya  Azam haukumshirikisha katika hatua za mwanzo za mauzo hayo, kama ambavyo ulimpeleka Simba kwa nguvu kwa mkopo.

 George aliongeza -- kama kungekuwa na elimu ya kutosha kwa wachezaji, viongozi na mawakala kusingekuwa na hali ya ubabaishaji kama ambavyo imekuwa ikitokea kwenye uhamisho na usajili wa wachezaji nchini.

Uongozi huo wa SPUTANZA umetoa kauli hiyo huku kukiwa na maoni tofauti kufuatia Ngassa kuchomoa usajili wa dola za Kimarekani 100,000 na kulipwa mshahara wa dola 4000 (sh. milioni 6) kwa mwezi pamoja na fedha ya ushawishi ya dola 50,000

 

 

SAKATA LA ZENJI DOLA 10,000: SASA ‘BIFU’ ZFA & TFF!!

>>ZFA YADAI TFF KUCHUKUA TAIFA STARS WACHEZAJI WALIOSIMAMISHWA NI DHARAU!!
==RIPOTI na ALLY MOHAMMED, COCONUT 88.9 FM, ZENJI
TFF_LOGO12Kikao cha Kamati Tendaji cha ZFA Taifa, kilichokutana jana kwa ajili ya kujadili tukio la utovu wa nidhamu kilichofanywa na Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar cha kuamua kugawana pesa za zawadi ya ushindi ya dola 10,000 walizopewa baada ya kumaliza nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Chalenji iliyomalizika nchini Uganda, kimeamua kuandika barua kwa TFF kueleza kusikitishwa na hatua ya TFF ya kutowaondoa katika Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Wachezaji wa Zanzibar ambao wamesimamishwa kucheza Soka ndani na nje yanchi.
Akizungumza jana mara baada ya kumaliza kwa kikao cha kamati tendaji cha ZFA Taifa, mjumbe wa kamati tendaji ambaye ni mwanasheria wa Zfa, Abdallah Juma, amesema kitendo cha TFF kuendelea kuwaruhusu wachezaji hao kufanya mazoezi na Timu ya Taifa ni dharau kwa ZFA ambao katika barua ya iliyoandikwa tarehe 11.12.2012 ikiwa na kumbukumbu namba Ref.ZFA/1/2012 kwenda kwa katibu mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF, ililitaka Shirikisho hilo kuwaondosha mara moja kwenye timu hiyo, mpaka pale Zfa watakapotoa taarifa nyengine. 
Hata hivyo Akizungumza juzi, ofisa habari wa TFF Boniface Wambura, alisema kuwa barua hiyo haikuwataka kuwaondoa wachezaji hao kwa vile tu wamesimamishwa na sio kufungiwa.
Wachezaji ambao Zfa imetaka waondolewe katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars ni:
1. Mwadini Ali -  Azam Sport Club
2. Agrey Moris -   Azam Sport Club
3. Samir Haji Nuhu -Azam Sport Club
4. Khamis Mcha - Azam Sport Club
5. Nassor Masoud - Simba Sport Club
6. Nadir Haruob - Young Football Team
7. Twaha Mohamed- Mtibwa Sport Club
8. Suleiman Kassim - Coastal Union
9. Amir Hamad - JKT Oljoro
10. Abdulghan Gulam -African Lyon
Hata hivyo kikao hicho kilichokaa jana mchana kimeshindwa kuangaza adhabu watakazozitoa kwa wachezaji hao mpaka watakapopata baraka kutoka Serikalini.
Wakati huo huo orodha ya wachezaji waliorejesha fedha imeongezeka na mpaka jana jumla ya wachezaji 12 wamerejesha fedha hizo.
BARUA YA ZFA:
ZANZIBAR FOOTBALL ASSOCIATION
MEMBER OF CECAFA
ASSOCIATE MEMBER OF CAF.

P.O BOX 1516,
Tel. +255 24 223 5014,
Fax: +255 24 223 5014.
Email: zfafootball@live.com
11th November 2012
DATE 26/08/2012.
KATIBU MKUU
TANZANIA FOOTBALL FEDERATION
TANZANIA.
KUH: KUSIMAMISHWA WACHEZAJI KWA UTOVU WA NIDHAMU.
Tafadhali husika na mada iliopo hapo juu.
Awali ya yote Napenda kukumbusha  kwamba wachezaji niliowaoredhesha hapa chini ni miongoni mwa wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar heroes)  ambao waliiwakilisha Zanzibar katika mashindano ya challenge  yaliyofanyika mwaka huu nchini Uganda  na kutokea mshindi wa tatu na  timu hio  kupitia Katibu Mkuu kukabidhiwa USD 10,000.00
Kwa bahati mbaya sana wachezaji niliowaorodhesha katika barua hii waliamua isivyo halali kuzipora fedha hizo kutoka kwa Katibu Mkuu wa ZFA  na kugawana kinyume na utaratibu, jambo hili si kwamba limeifedhehesha ZFA tu bali Zanzibar na watu wake hasa ukitilia maanani kwamba timu hiyo ni ya Taifa na ilikuwa ikipeperusha bendera ya Serikali ya Zanzibar.
Kitendo hicho cha kupora  fedha hizo isivyo halali kinaibua shaka ya kutendeka  kosa la Jinai dhidi ya Jamuhuri, bali pia ni  kitendo cha utovu wa nidhamu ambacho hakistahiki  kuvumiliwa kufanywa na mchezaji  yoyote ambaye amepewa heshima kubwa ya kuipeperusha Bendera ya Zanzibar  kwa niaba ya Wazanzibari wote kwenye mashindano hayo huku akilipwa kikamilifu posho na mafao mengine yanayomstahikia  kutoka kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na chama cha mpira wa miguu Zanzibar (ZFA).
Kamati Tendaji ya ZFA Taifa imefanya kikao chake cha dharura leo siku ya tarehe 11 November 2012 kulijadili kwa kina suala hili la utovu wa nidhamu wa hali ya juu uliofanywa na wachezaji hao na kwa kauli moja tumefikia maamuzi ya awali ya kuwasimamisha wachezaji hao kushiriki katika mashindano yoyote ya mpira wa miguu ndani na nje ya Zanzibar.
Kwa barua hii unaombwa kutowa mashirikiano katika kulifanikisha suala hili la kuwazuia wachezaji hao, lakini pia unatakiwa uhakikishe kwamba wachezaji wote waliotajwa humu ambao  wameteuliwa kuwemo katika timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Star) wanaondoshwa mara moja kwenye timu hio, mpaka pale tutakapokupa taarifa nyengine. Wachezaji wenyewe ni hawa wafuatoa:-
1. Mwadini Ali -  Azam Sport Club
2. Agrey Moris -   Azam Sport Club
3. Samir Haji Nuhu -Azam Sport Club
4. Khamis Mcha - Azam Sport Club
5. Nassor Masoud - Simba Sport Club
6. Nadir Haruob - Young Football Team
7. Twaha Mohamed- Mtibwa Sport Club
8. Suleiman Kassim - Coastal Union
9. Amir Hamad - JKT Oljoro
10. Abdulghan Gulam -African Lyon
Kwa nakla ya barua hii vilabu husika mnaombwa kusita kuwatumia wachezaji hao mpaka pale tutakapoamua vyenginevyo.
………………………………
KASSIM HAJI SALUM
KATIBU MKUU
ZANZIBAR FOOTBALL ASSOCIATION

NAKLA:-
  1. Mheshimiwa Waziri
Habari Utamaduni  Utalii na Michezo- Zanzibar.
  1. Mwenyekiti Wa Baraza la Taifa la Michezo-Zanzibar.
  2. Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Michezo.
  3. Makamo wa Rais wa ZFA- Pemba.
  4. Katibu Mkuu- Azam Sport Club
  5. Katibu Mkuu -Simba Sport Club
  6. Katibu Mkuu-Young African Football Team
  7. Katibu- JKT Oljoro
  8. Katibu- African Lyon
10. Katibu – Costal Union

 

SIMBA KUMSAJILI MRITHI WA SUNZU KUTOKA CAMEROON, AGIZO LA KOCHA MPYA BABU PATRICK LIEWIG

VICTOR KOSTA NAMPOKA 'NYUMBA' AWASHANGAA MAKOCHA KWA KUMSUGULISHA BENCHI 

KEITA AFURAHIA UJIO WA KOCHA MPYA WA SIMBA PATRICK LIEWIG AKIAMINI SASA ATANG'ARA SIMBA. ANA MUHESHIMU SANA KAPOMBE. ANSEMA WACHEZAJI WA KIBONGO WAVIVU.

Koman Billi Keita.
Mlinzi wa kati wa klabu ya Simba mwenye mapafu mithili ya mbwa Koman Billi Keita amesema ana imani kocha mpya wa klabu hiyo Patrick Liewig ambaye anatarajiwa kuingia mkataba na klabu hiyi mara baada ya sikukuu ya Chrismass, atampa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Simba kwa kuwa ni falsafa ya makocha wa Ufaransa ni mpira wa nguvu na kasi ya kurosha uwanjani.
Keita ambaye hakuwa na nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha kocha aliyefungashiwa virago Milovan Circovich wakati wa uongozi wake wa benchi la ufundi amesema kwake yeye ni faraja kuona Simba inamleta kocha mfaransa ambaye ana imani wataelewana vizuri kwakuwa wanaongea lugha moja ya kifaransa.
Amesema hakuwa kwenye nafasi ya kucheza wakati wa Milovan kwa kuwa alikuwa mgeni mno katika kikosi cha Simba na pia hakuwa anaujua vizuri mpira wa Tanzania jambo ambalo amesema kwa sio tatizo tena.
Keita amesema anajiamini kuwa yeye ni mchezaji mkubwa sana kwani amecheza soka na wachezaji wakubwa katika timu ya taifa ya Mali kama Mamadou Diara, Seidou Keita, Drissa Diakite, Cedric Kante na Bakaye Traore jambo ambalo anasema limemkuza sana kiwango chake na kujenga kujiamini.
Keita amesema anaheshimu sana uwezo wa mlinzi Shomari Kapombe ambaye anaamini mlinzi huyo kiraka mwenye uwezo wa kucheza eneo lolote katika sehemu ya ulinzi kwamba ana uwezo mkubwa sana na anaweza kucheza soka popote duniani kwani.
“Kapombe ni mchezaji mzuri sana, ana fanana na wachezaji wa Afrika magharibi wenye uwezo na kasi naheshimu sana uwezo wake, anaisaidia sana sehemu ya ulinzi ya Simba”

Somari Kapombe.
Mbali ya Kapombe, Keita anawasifia pia wachezaji wengine kama Mwinyi Kazimoto, Jonas Mkude na Amri Kiemba ambao amesema wanacheza kwa kujituma na si wavivu wa mazoezi.

Kabla ya kujiunga na Simba, Koman Billi Keita amewahi kuvichezea vilabu vya Stade Malienne ya Mali, Shooting Stars ya Nigeria, Jeanne D’arc ya Mali na Iran-Cave ya Iran.

Keita anasema ligi kuu ya soka Tanzania bara ligi ambayo ina wachezaji wengi wenye vipaji lakini soka linachezwa kwa uvivu kwa kuwa wachezaji wengi hawana malengo ya kucheza soka nje ya Tanzania.

"Unajua mchezaji wa Tanzania akienda Mali, Nigeria, Camerron, Nigeria, Ivory Coast, Benin na Ghana hawezi kupata timu ya daraja la kwanza kuchezea kwa kuwa kule ligi ni ngumu. mimi mwenyewe niliposema nakuja Tanzania walinicheka wenzangu kwakuwa Tanzania haijulikani"

"halafu kule watu wanafanya sana mazoezi na ndio maana wanaonekana wana nguvu na miili mikubwa iliyojengeka, sasa hapa ligi ikisimama kidogo wachezaji nao wanasimama, hii inanishangaza sana".    

"Wachezaji wa kule wanataka kucheza Ulaya na ndio maana wanasafiri sana kwenda ulaya kujaribu bahati zao, lakini hapa hawafanyi mazoezi na hawataki kwenda nje, ni vigumu kupata maendeleo"

 Keita amemtaka Haruna Moshi ambaye ni swahiba wake mkubwa akacheze soka ulaya, kwakuwa anakipaji sana na anacheza soka kwa kutumia akili.

Amesema haruna anacheza soka la akili licha ya kwamba hatumii nguvu na kwamba kuna nchi ambazo Haruna anaweza kung'ara sana kama vile Ufaransa na Hispania

BIASHARA: MANCHESTER CITY YATANGAZA HASARA KWA MWAKA WA PILI MFULULIZO.

Manchester City imetangaza hasara ya euro million 120 kwa mwaka wa fedha ulio malizikia May 2012, licha ya kwamba hasara hiyo ni pungufu ukilinganisha na euro milioni 243 iliyotajwa miezi 12 ya nyuma.
 Manchester City imetangaz hasara hiyo ambayo ni mwaka wa pili mfululizo ambapo klabu hiyo tajiri ilipoteza euro milioni 120 katika kipindi cha mwaka mwaka wa fedha wa nyuma ya hapo kwa maana ya 2010/2011.

Licha ya kukusanya euro milioni 283 katika kipindi cha mwaka huo wa 2011/2012 ambacho kimsingi ni kikubwa katika historia ya klabu hiyo, kiasi ambacho kimepanda kutoka euro milioni 184 mwaka uliopita, lakini bado ukilingana na matumizi ya msingi ya uendeshaji ya klabu ndani ya kipindi hicho klabu hiyo imejikuta ikipata hasara.

Inaarifiwa kuwa kushindwa kusonga mbele kwa klabu hiyo katika hatua ya mtoano ya michuano mikubwa ya vilabu barani Ulaya, kunaelezewa kuwa ni sababu kubwa ya kuitia hasara klabu hiyo.

Hata hivyo kiasi hicho kina ashiria maendeleo makubwa kulinganisha na msimu uliopita ambapo City ilipoteza jumla ya euro milioni 243.

Wakati huo huo klabu hiyo imechapisha ongezeko la mapato ya getini na mapato ya malipo ya TV, ambayo kimsingi yameongezeka mara mbili kutoka euro milioni 80 mpaka euro milioni 148.

Kiasi hicho cha fedha sasa kinairuhusu klabu hiyo bingwa nchini England kujiamini kiuwezo kukabiliana na sheria ya shirikisho la soka barani Ulaya( UEFA) ambayo inasimamia udhibiti wa matumizi yasiyopelekea hasara ya kiwango kisichozidi  euro milioni 18.4.

KLABU BINGWA DUNIANI: FAINALI-CORINTHIANS v CHELSEA

>>JUMAPILI Desemba 16, Saa 7 na Nusu Mchana
>>UWANJA: NISSAN, YOKOHAMA, JAPAN
FIFA_CLUB_WORLD_CUPNI FAINALI ya Mashindano ya FIFA kusaka Klabu Bingwa Duniani na yanazikutanisha Klabu ya Brazil, Sport Club Corinthians Paulista, ambao ni Mabingwa wa Marekani ya Kusini baada ya kutwaa Copa Libertadores, dhidi ya Klabu ya England, Chelsea, ambao ni Mabingwa wa Ulaya, baada ya kutwaa UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Kwenye Mashindano haya, Timu zote hizi mbili zilianzia hatua ya Nusu Fainali na Corinthians waliwatoa Al Ahly kwa Bao 1-0 na Chelsea kuifunga Monterrey Bao 3-1.
Kabla ya Mechi ya Fainali kuanza, hapo Saa na Nusu Asubuhi, Mabingwa wa Afrika, Al Ahly, watachuana na Monterrey ya Mexico katika Mechi ya kusaka Mshindi wa Tatu wa Mashindano haya.
+++++++++++++++++++++++
VIKOSI VINATARAJIWA:
Sport Club Corinthians Paulista [Mfumo: 4-2-2-2]:
Cassio
Alessandro, Chicao, P Andre, F Santos
Paulinho, Ralf
Danilo, Douglas,
Guerrero, Emerson
Chelsea [Mfumo:4-2-3-1]:
Cech
Azpilicueta, Ivanovic, Cahill, Cole
Mikel, Luiz
Mata, Oscar, Hazard
Torres
+++++++++++++++++++++++
Kila Timu itaingia kwenye Mechi hii bila majeruhi ingawa Chelsea inao majeruhi wa muda mrefu, Daniel Sturridge (Musuli ya Pajani), John Terry (Goti) na Oriol Romeu (Goti), na ambao hawapo huko Japan.
Kama ilivyokuwa kwenye Nusu Fainali, huenda Beki David Luiz akachezeshwa kwenye Kiungo ambako alicheza vizuri dhidi ya Monterrey.
Kocha Corinthians Tite anategemewa kuendeleza Mfumo wake wa 4-2-2-2 ambao ulimpa mafanikio makubwa kwenye Mashindano ya Copa Libertadores ili umpe Taji lao la Pili la Klabu Bingwa Duniani baada ya kutwaa Taji la kwanza katika Mashindano ya kwanza kabisa Mwaka 2000.
+++++++++++++++++++++

MABINGWA WALIOPITA:
-2000 - Corinthians
-2005 - Sao Paulo
-2006 - Internacional
-2007 - AC Milan
-2008 - Manchester United
-2009 - Barcelona
-2010 - Inter Milan
-2011 – Barcelona
++++++++++++++++++
KLABU BINGWA DUNIANI 2012
TIMU ZITAKAZOSHIRIKI:
Chelsea-BINGWA ULAYA
Corinthians-BINGWA MAREKANI ya KUSINI
Monterrey-BINGWA MAREKANI ya KATI NA KASKAZINI
Auckland City-BINGWA KANDA ya OCEANIA
Usain Hyundai-BINGWA-Barani Asia
Al Ahly-BINGWA-Barani Afrika
Sanfrecce Hiroshima-BINGWA-Japan J-LIGI
RATIBA/MATOKEO:
Raundi ya Mchujo - Desemba 6, Yokohama
Sanfrecce Hiroshima 1 Auckland City 0
ROBO FAINALI - Desembar 9, Toyota
Usain Hyundai 1 Monterrey 3
Sanfrecce Hiroshima 1 Al Ahly 2
MSHINDI wa 5- Desemba 12, Toyota
[Saa 4 na Nusu Asubuhi]
Usain Hyundai 2 Sanfrecce Hiroshima 3
NUSU FAINALI
Desemba 12, Toyota
[Saa 7 na Nusu Mchana]
Al Ahly 0 Corinthians 1
Desemba 13, Yokohama
[Saa 7 na Nusu Mchana]
Monterrey 1 Chelsea 3
MSHINDI wa 3
Desemba 16
[Uwanja wa Yokohama]
[Saa 4 na Nusu Asubuhi]
Al Ahly v Monterrey
FAINALI
[Saa 7 na Nusu Mchana]
Corinthians v Chelsea


BPL: Wikiendi Vigogo Dimbani kasoro Chelsea!!

BPL_LOGO>>VINARA MAN UNITED, FERGIE ATAKA UMAKINI na SUNDERLAND!
>>MANCINI AWEWESEKA, ADAI WAO BORA KULIKO MAN UNITED!!
>>WENGER PRESHA, AKUMBUSHA MAFANIKIO YAKE MIAKA 16!!
+++++++++++++++++++++++
RATIBA MECHI ZIJAZO:  
Jumamosi 15 Desemba 2012
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Newcastle v Man City
[SAA 12 Jioni]
Liverpool v Aston Villa
Man United v Sunderland
Norwich v Wigan
QPR v Fulham
Stoke v Everton
Jumapili 16 Desemba 2012
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Tottenham v  Swansea
[SAA 1 Usiku]
West Brom v West Ham
Jumatatu 17 Desemba 2012
[SAA 5 Usiku]
Reading v Arsenal
+++++++++++++++++++++++
LIGI KUU ENGLAND inaingia kwenye Raundi ya 17 bila ya Chelsea kuwepo kilingeni kwa vile wako Japan kuwania Ubingwa wa Klabu Duniani lakini Vigogo wenzao wanaingia dimbani wakiwa na matarajio na malengo kibao huku vinara Manchester United wakijizatiti kuzidi kuyoyoma kileleni kwa Meneja wao, Sir Alex Ferguson, kuitaka Timu yake kuwa makini ikicheza na Sunderland Uwanjani Old Trafford, mwenzake wa Man City, Roberto Mancini, akijaribu kuinua morali ya Timu yake iliyopata kipigo cha kwanza kwenye Ligi msimu huu na cha kwanza nyumbani kwao Etihad katika Miaka miwili, walipocharazwa na Man United 3-2 Jumapili iliyopita.Wenger & ArsenalWENGER-SITABWAGA_MANYANGA


Ingawa Wadau wengi watakuwa wakizikodolea macho Mechi za Man United v Sunderland na Newcastle v Man City kwa vile tu Man United ndio vinara na Man City wapo nafasi ya Pili wakiwa Pointi 6 nyuma, lakini mvuto mkubwa upo kwa Arsenal na Meneja wao Arsene Wenger ambae amesakamwa sana hasa baada ya juzi kutolewa nje ya CAPITAL ONE CUP na Timu ya Daraja la chini, Bradford City, na kuwakumbusha Wadau wao kuwa huu ni Mwaka wao wa 8 wakiwa hawana Taji lolote kubwa.
++++++++++++++++++++++++++++
PATASHIKA ARSENAL LIGI KUU ENGLAND:
DESEMBA 2012:
Desemba 17: Reading v Arsenal
Desemba 22: Wigan v Arsenal
Desemba 26: Arsenal v West Ham
Desemba 29: Arsenal v Newcastle
JANUARI 2013:
Januari 1: Southamton v Arsenal
Januari 6: Swansea v Arsenal
Januari 13: Arsenal v Man City
Januari 20: Chelsea v Arsenal
Januari 30: Arsenal v Liverpool
++++++++++++++++++++++++++++
Jumatatu Usiku, Arsenal watakuwa ugenini kucheza Mechi ya Ligi na Reading na tayari wako Pointi 15 nyuma ya Vinara Man United, lakini bado pia wamo kwenye vinyang’anyiro vya UEFA CHAMPIONZ LIGI, wameshatinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16, na wataanza hatua ya Raundi ya 3 kwenye FA CUP Mwezi Januari dhidi ya Swansea City.
Wenger, ambae katika himaya yake Arsenal ametwaa Ubingwa wa Ligi mara 3 na FA CUP 4 Kombe la mwisho likiwa Mwaka 2005, ameongelea kuhusu kusakamwa: “Naelewa Watu wakiponda matokeo yakiwa si mazuri. Hiyo ndio hulka ya Dunia ya sasa. Unasema Miaka 16 ni mzigo kuleta mafanikio lakini hilo huleta uzoefu na ni kitu kizuri hukupa uwezo kuibadili Timu, Miaka hiyo inaonyesha unaipenda Timu. Nipo hapa muda wote huo kwa sababu naipenda Klabu. Huko nyuma tulipita wakati mgumu na tulijua nini tubadili! ”
Man City na Mancini
MANCINI_ALIAManchester City, ambao wapo nafasi ya Pili Pointi 6 nyuma ya Man United, wana kibarua kikubwa cha kujizoa kufuatia kipigo chao cha kwanza kwenye Ligi Msimu huu na cha kwanza nyumbani kwao Etihad katika Miaka miwili, walipocharazwa na Man United 3-2 Jumapili iliyopita.
++++++++++++++++++++++++++++
MECHI za MAN CITY Ligi Kuu England:
Des 15 Newcastle v City
Des 22 Man City v Reading
Des 26 Sunderland v City
Des 29 Norwich v Man City
Jan 1 Man City v Stoke
++++++++++++++++++++++++++++
Leo, katika Mechi ya kwanza kabisa ya Ligi Wikiendi hii, Man City watakuwa St James Park kuwavaa Newcastle, Timu ambayo imefungwa Mechi 5 kati ya 6 za Ligi walizocheza mwishoni lakini tatizo lao kubwa si ubovu wa Timu ni kukabiliwa na majeruhi kibao.
Akionyesha waziwazi kujaribu kuinua morali ya Timu yake, Meneja wa Man City Roberto Mancini, ametamka: “Tulionyesha tuko bora kupita Man United. Lakini wao wana uzoefu mkubwa kupita sisi na wanaweza kuibuka upya wakipata pigo. Inabidi tujibadili na pengine Februari mambo yatabadilika.”
Man United na FergusonFERGIE_CASUAL
Nae Bosi wa Vinara Manchester United, Sir Alex Ferguson, amekiri kuwa ni lazima wawe waangalifu na kuwa makini wakicheza na Sunderland na alikumbushia Msimu uliopita wakati walipotoka sare 4-4 na Everton katika Mechi ambayo waliongoza 4-2 hadi Dakika za mwisho.
Ferguson alisema: “Suala sasa ni kuendeleza fomu yetu na kuhakikisha hatufanyi upuuzi. Ile Mechi na Everton ni mfano bora. Man United si Timu ya kubwaga uongozi wa Goli mbili ndani ya Dakika 7. Ile ndio ilitupotezea Ubingwa. Kwa sasa hatutakiwa kutazama wapi tulipo bali kushinda Mechi inayotukabili.”
++++++++++++++++++++++++++++
MECHI za MAN UNITED hadi Januari Mosi:
15 Desemba: Man United v Sunderland
23 Desemba: Swansea v Man United 
26 Desemba: Man United v Newcastle 
29 Desemba: Man United v West Brom 
1 January: Wigan v Man United
++++++++++++++++++++++++++++
Hata hivyo, Wadau wa Man United Siku zote hulia na ile tabia ya asilia ya Sir Alex Ferguson ya kubadili Kikosi chake katika kila Mechi hata kama hamna sababu maalum.
Kati ya Mei 2008 na Machi 2011, Ferguson hakuwahi hata mara moja kupanga Kikosi kilekile na kila Mechi alibadili Timu.
Swali kwa Wadau hao ni Je leo Ferguson anastahili kubadili kile Kikosi. Ambacho wengi wanaamini ndicho Nambari Wani, kilichoizamisha Man City Jumapili iliyopita wakati Wiki nzima ijayo hawana Mechi nyingine yeyote?
+++++++++++++++++++++++++++
MSIMAMO:
[Kila Timu Mechi 16]
1 Man United Pointi 39
2 Man City 33
3 Chelsea 29
4 Everton 26
===============
5 Tottenham 26
6 WBA 26
7 Arsenal 24
8 Swansea 23
9 Stoke 23
10 Liverpool 22
11 West Ham 22
12 Norwich 22
13 Fulham 20
14 Newcastle 17
15 Sunderland 16
16 Southampton 15
17 Aston Villa 15
===============
18 Wigan 15
19 Readind 9
20 QPR 7