Sunday, January 20, 2013

LA LIGA: BARCA WAONJA KICHAPO CHA KWANZA MSIMU HUU!!


>>WAONGOZA 2-0 NDANI YA DAKIKA 25, WAPIGWA 3-2 DAKIKA 90!!
LIONEL_MESSI-HUZUNIREAL SOCIEDAD walitoka nyuma kwa Bao 2-0 ndani ya Dakika 25 na kuwatwanga Vinara wa La Liga Barcelona Bao 3-2 na kuwashushia kipigo chao cha kwanza Msimu huu kwenye Ligi hiyo.
Bao za Lionel Messi na Pedro ziliwapa Barca uongozi wa Bao 2-0 lakini Gonzalo Castro akaifungia Real Sociedad Bao moja kabla Haftaimu.
+++++++++++++++++
MAGOLI:
Real Sociedad 3
-Castro Dakika ya 41 & 63
-Imanol Agirretxe 91
Barcelona 2
-Lionel Messi Dakika ya 7
-Pedro Rodriguez 25
KADI:
-Gerard Pique [Barcelona] 33 & 56

Beki wa Barca Gerard Pique alitolewa nje katika Dakika ya 56 baada ya kulambwa Kadi za Njano mbili na Castro akaisawazishia Real Sociedad kabla Imanol Agirretxe kupiga Bao la 3 na la ushindi katika Dakika ya 91.
RATIBA:
Jumapili Januari 20
Osasuna v Deportivo la Coruna
Valladolid v Zaragoza
Atletico Madrid v Levante
Valencia v Real Madrid
Jumatatu Januari 21
Real Betis v Athletic Bilbao

No comments:

Post a Comment