Monday, December 10, 2012

MAULID MWIKALO ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA FRAT TABORA MJINI

Cover Photo
  Maulid Mwikalo amechaguliwa kuwa   Mwenyekiti wa Chama cha waamuzi wilaya ya Tabora mjini kwenye uchaguzi uliofanyika jana, mkoani Tabora.Uchaguzi huo ulifanyika katika  shule ya msingi Gongoni na ulihudhuriwa na wajumbe 16.

Nafasi ya Mwenyekiti ilikuwa na wagombea wawili, ambapo Maulid Mwikalo alimbwaga Fredinandy Machunde kwa kura 10 dhidi ya 5 na kura moja iliharibika.

Nafasi ya Makamu mwenyekiti ilichukuliwa na mgombea pekee Bella Husein aliyepata kura 11 za ndio na kura tano za hapana.

Nafasi ya Katibu Mkuu ilikwenda kwa Athuman Hussein ambaye alipata kura 10 huku mpinzani wake Shaban Masanda akiambulia kura sita.

Katibu msaidizi ni Maliyatabu Chobanga aliyepata kura 14 za ndiyo na mbili za hapana na mweka hazina ni Fredy Mwenisongole ambaye alipata kura 11 na mpinzani wake Nestory Rivangara alipata tano

Mwakilishi wa wanawake ni Justina Charles aliyepata kura 12 za ndiyo na nne za hapana na mjumbe wa Mkutano mkuu haikupata mtu  na  mgombea Masud Ngeleja alipata kura saba za ndiyo na kura tisa zilimkataa

Timu Ya Bunge Ya Tanzania Yawaangamiza Wabunge Wa Kenya Kwa Mabao 5-1.

                    
Tanzania Bunge Sports Club Football imefanya maajabu katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi jana kwa kuwabamizwa wenyeji wao timu ya Kenya Bunge Sports Club Football mabao 5 kwa nunge katika michezo ya mabunge ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea jijini Nairobi. Mashindano hayo yaliyofunguliwa rasmi juzi tarehe 7 Disemba na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mh. Margreth Natongo Zziwa akisisitiza “let the best team win” tayari yamezikutanisha timu ya Bunge la Uganda na timu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo timu hizo zimetoka sare ya 1-1.
Wakati wa kuhitimisha karamu ya mabao kwa timu ya Kenya, Watanzania walijikuta uwanjani peke yao wakishangilia huku mashabiki-wenyeji wakiwa wameondoka uwanjani hapo. 
Leo Tanzania itapambana na Rwanda kwenye mpira wa miguu katika uwanja wa City Stadium, na  Wabunge wanawake watakutana na Kenya kwenye mpira wa kikapu Nyayo Stadium. Mashindano haya yanalenga kuimarisha ushirikiano na kuitangaza zaidi Jum uiya ya Afrika Mashariki.
Katika mashindano haya ambayo hufanyika kila mwaka huyakutanisha mabunge ya nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda. Waratibu wa michezo hii ni Jumuiya pamoja na Bunge la Afrika Mashariki. Kwa mwaka huu Burundi haikushiriki.
Chini ya ukufunzi wa Naibu Waziri (TAMISEMI) Mhe. Kasim Majaliwa (Mb) .na uongozi wa Mhe. Idd Azzan (Mb) mabao hayo yalifungwa na Mhe Amos Makala (Mb), Yusuf Soka (2), Mark Tanda na Mhe. Joshua Nassari.

KOMBE LA UHAI LAANZA KUTIMUA VUMBI KESHO

Rais wa TFF, Leodegar Tenga akinywa maji ya Uhai, 
MICHUANO ya kuwania Kombe la Uhai inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom inaanza kutimua vumbi kesho (Desemba 11 mwaka huu) kwenye viwanja viwili tofauti.
Viwanja vitakavyotumika kwenye michuano hiyo ni Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume na Uwanja wa Azam ulioko Chamazi. Viwanja vyote viko Dar es Salaam.
Timu hizo zimegawanywa katika makundi matatu ya michuano hiyo itakayomalizika Desemba 23 mwaka huu. Kundi A lina timu za Coastal Union, JKT Ruvu, Mtibwa Sugar, Tanzania Prisons na Toto Africans.
Kundi B ni African Lyon, Azam, Mgambo Shooting, Polisi Morogoro na Simba, wakati timu za Kagera Sugar, Oljoro JKT, Ruvu Shooting na Yanga zinaunda kundi C.
Mechi za fungua dimba kundi A ni Coastal Union vs Tanzania Prisons (saa 2 asubuhi- Karume), JKT Ruvu vs Mtibwa Sugar (saa 10 jioni- Karume). Kundi B ni African Lyon vs Polisi Morogoro (saa 3 asubuhi- Chamazi) na Azam vs Mgambo Shooting (saa 10 jioni- Chamazi).
Kundi C litaanza mechi zake Desemba 12 mwaka huu ambapo Kagera Sugar itacheza na Oljoro JKT saa 8 mchana- Karume wakati Yanga na Ruvu Shooting zitakuwa kwenye Uwanja wa Chamazi kuanzia saa 10 kamili jioni. (Ratiba nzima imeambatanishwa)

DHAIRA SASA KESHOKUTWA SIMBA SC, UMONY AOTA MBAWA MSIMBAZI

ZH Poppe aifafanua mambo
MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba, wamemtumia tiketi kipa namba moja wa Uganda, Abbel Dhaira leo na atatua Dar es Salaam kesjokutwa kwa ajili ya kusaini mkataba wa kuanza kuitumikia klabu hiyo.
Akizungumza  leo, Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) aliyepigana vita dhidi ya Uganda, alisema kwamba awali, Dhaira ilikuwa atue leo, lakini kutokana na kukosa ndege sasa atatua keshokutwa.
Kuhusu suala la mshambuliaji Brian Umony pia wa Uganda, Hans Poppe alisema; “Kuna ujgumu kidogo, huyo tunaweza kumkosa,”alisema. 
Kwa upande wake, Dhaira amekwishasema kimsingi yeye yuko tayari kujiunga na Simba kwa kuwa ni klabu kubwa Afrika na inacheza Ligi ya Mabingwa Afrika na angependa kuungana na Mganda mwenzake, Emmanuel Okwi huko.
Tayari Simba SC imefikia makubaliano na kipa huyo namba moja wa Uganda, aliyemaliza mkataba wake na klabu ya I.B.V FC ya Iceland na amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili kwa dau ambalo halijafahamika.
Dhaira alisema kwamba amefikia makubaliano na Simba kusaini mkataba wa miaka miwili kuja kuanza maisha mapya Dear es Salaam.
Dhaira ambaye aliibukia Express ya hapa mwaka 2006 kabla ya 2008 kuhamia U.R.A. pia ya hapa, ambayo aliichezea hadi 2010 alipohamia Ulaya atatua Dar es Salaam Jumatatu kumaliza kila kitu Simba.
Ikimpata Dhaira, Simba SC itakuwa imepata kipa wa uhakika wa kusaidiana na kipa wake wa kwanza, Juma Kaseja ambaye amekuwa akisotoshwa peke yake bila kupumzika. Na hiyo inafuatia makipa wengine, Wilbert Mweta na Hamadi Waziri kushindwa kuonyesha uwezo wa kumsaidia Kaseja.
Katika mechi za mwishoni za mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Kaseja alionekana kuchoka na kudaka chini ya kiwango chake, jambo ambalo lilisababisha mashabiki wenye ‘akili mbovu’ wamfanyie fujo baada ya kufungwa mabao mawili katika mechi dhidi ya Mtibwa Sugar, Simba ikilala 2-0.
Kwa sababu hiyo, Kaseja alikasirika na kujiengua kwenye kikosi cha timu hiyo akisema hataki tena kuchezea Simba.
Lakini pamoja na matatizo hayo, Kaseja aliitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ambako ameendelea kufanya vizuri na kuonyesha yeye ni Tanzania One wa ukweli. 

TIMU YA TAIFA YA NETIBOLI YAREJEA KWA KISHINDO BAADA YA KUTWAA UBINGWA WA MICHUANO YA KIMATAIFA

 Mwenyekiti wa CHANETA, Anna Bayi akiwa Mwenyekiti wa wake za viongozi, Germina Lukuvi mara baada ya timu ya Taifa ya Netiboli (Taifa Queens) iliporejea nchini na Kombe la Michiuano ya Kimataifa iliyofanyika nchini Singapore. 
 Baadhi ya wachezaji wa timu ya Taifa ya Netiboli ‘Taifa Queens’ wakiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo wakitokea Singapore walikokuwa wakishiriki michuano ya Kimataifa na kutwaa Kombe la michuano hiyo. 
 Mlezi wa Chaneta kupitia Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Ain Sharif akikabidhi kitita cha sh. 500,000 ikiwa ni kama zawadi kwa timu hiyo baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya Kimataifa yaliyofanyika Singapore na Taifa Queens kutwaa ubingwa wa michuano hiyo.
Wachezaji na viongozi wa timu ya Taifa ya Netiboli (Taifa Quees) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wao baada ya kuwasili leo kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakitokea nchini Singapore.


TIMU ya taifa ya Netiboli ya Tanzania ‘Taifa Queens’ imerejea kwa kishindo leo baada ya kushiriki na kutwaa Kombe la michuano ya Kimataifa iliyokuwa ikifanyikia Singapore barani Asia.

Taifa Queens ilitwaaa ubingwa huo baada ya kuingia fainali ikiwa na pointi 10 ikicheza na timu ya Malasia iliyokuwa na pointi 4 ambapo ilifanikiwa kuifunga magoli 45-38.

Akizungumza baada ya kurejea, Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA), Anna Bayi alisema maandalizi ni kitu kizuri sana, anaamini kocha aliwapa wachezaji mbinu za kutosha hadi kupelekea ubingwa huo.

“Hii imetusaidia sana maana kocha mwenyewe ni kijana hivyo anambinu za kisasa kitu kilichotusaidia wakati tukiwa ugenini, hakuna kitu kizuri kama kupigiwa wimbo wa taifa lako ukiwa ugenini huku wazungu ambao ni wenyeji wa mashindano hayo wakiwa penbeni,” alisema Bayi.

Kwa upande wake Kocha wa Taifa Queens, Mary Waya alisema mashindano yalikuwa ni magumu anawapongeza wachezaji wake kwa ushindi huo ambao umemuweka pazuri yeye pamoja na Watanzania wote kwa ujumla.

“Kila kitu unatakiwa umtangulize mungu, akili, na nguvu ndio zinafuata naimani wachezaji wangu walikuwa makini na kujua nini wamekifuata huko, akili ni kitu cha muhimu ukiwa mchezoni hivyo mimi sina la kusema zaidi ni kumshukuru mungu kwa ushindi tulioupata,” alisema Kocha huyo ambaye ni Mmalawi.  

Kocha huyo alisema amefurahishwa na ushindi huo na kwamba kwasasa anajipanga kuifua timu hiyo kwaajili ya kushiriki michuano ya kombe la Dunia.
Naye Nahodha wa timu hiyo, Lilian Sadolin alisema anamshukuru mungu kwa ubingwa huo pia Watanzania wanatakiwa kuendelea kuwapa sapoti katika mashindano mbalimbali.

“Wakati tunaondoka niliwaahidi Watanzania lazima turudi na ushindi, sisi ubingwa tushaapata kabla hatujaenda kule tulienda kutimiza wajibu, naimani tuliwazidi mbinu unapokuwa uwanjani unatakiwa kuwa na mbinu za ziada hivyo tunamshukuru mungu kwa ushindi tulioupata,” alisema Lilian.
Mwisho.

Cannavaro

NAHODHA wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amerejeshwa kwenye kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars baada ya kung’ara katika Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge mjini Kampala, Uganda.
Katika michuano hiyo, Cannavaro ambaye pia Nahodha wa Zanzibar, aliiongoza timu hiyo kushika nafasi ya tatu katika michuano iliyoanza Novemba 24 na kufikia tamati Desemba 8, mwaka huu. Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mdenmark, Kim Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 24, ndani yake akiwatema chipukizi aliokuwa akiwakomaza kwenye timu hiyo, Ramadhani Singano ‘Messi’ na Edward Christopher, wote wa SImba SC.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Poulsen alisema kikosi hicho kitaingia kambini keshokutwa kwa ajili ya kujiandaa na mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya mabingwa wa Afrika, Zambia, Chipolopolo itakayochezwa Desemba 22, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mbali na Cannavaro na Aishi Mangula, nyota wengine wapya walioitwa katika kikosi hicho ni pamoja na Hamisi Mcha ‘Vialli’ na Samir Hajji Nuhu wote wa Azam FC.
Wengine walioitwa ni makipa; Juma Kaseja (Simba) na Mwadini Ally (Azam FC), mabeki; Amir Maftah (Simba), Shomari Kapombe (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Nasoro Masoud ‘Chollo’ (Simba) na Aggrey Morris wa Azam FC.
Viungo ni Mwinyi Kazimoto (Simba), Mrisho Ngassa (Simba), Frank Domayo (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Athumani Idd ‘Chuji’ (Yanga), Shaaban Nditi (Mtibwa Sugar), wakati washambuliaji ni Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC), John Bocco (Azam), Simon Msuva (Yanga).

UGANDA ONE ATUA LEO DAR KUMALIZANA NA SIMBA SC

Dhaira
MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba, kipa namba moja wa Uganda, Abbel Dhaira anatua leo Dar es Salaam kwa ajili ya kusaini mkataba wa kuanza kuitumikia klabu hiyo.
Akizungumza   jana, Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) aliyepigana vita dhidi ya Uganda, alisema kwamba baada ya kumalizana na kipa huyo, watahamia kwenye suala la mshambuliaji Brian Umony pia wa Uganda. 
Hata hivyo, mapema juzi akizungumza , Dhaira alisema kwamba anataka Simba wamtume mtu Kampala, Uganda na fedha ili asaini akiwa huko.
Dhaira alisema kwamba hawezi kujihesabu kama tayari yeye ni kipa wa Simba hadi hapo watakaposaini mkataba, kwani kwa sasa wamezungumza na kufikia makubaliano, ila ikitokea timu nyingine ya kumaliza naye haraka, hatasita kufanya hivyo.
“Simba wamezungumza na mimi ndio, lakini hatujamalizana, wao wakituma mtu kuja huku tukasaini, hapo ndio nitakuwa nimejifunga, ila kwa sasa kama ipo timu nyingine hata huko Tanzania inanitaka, milango bado iko wazi,”alisema Dhaira.
Dhaira alisema kimsingi yeye yuko tayari kujiunga na Simba kwa kuwa ni klabu kubwa Afrika na inacheza Ligi ya Mabingwa Afrika na angependa kuungana na Mganda mwenzake, Emmanuel Okwi huko.
Tayari Simba SC imefikia makubaliano na kipa huyo namba moja wa Uganda, aliyemaliza mkataba wake na klabu ya I.B.V FC ya Iceland na amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili kwa dau ambalo halijafahamika.
Dhaira alisema kwamba amefikia makubaliano na Simba kusaini mkataba wa miaka miwili kuja kuanza maisha mapya Dear es Salaam.
Dhaira ambaye aliibukia Express ya hapa mwaka 2006 kabla ya 2008 kuhamia U.R.A. pia ya hapa, ambayo aliichezea hadi 2010 alipohamia Ulaya atatua Dar es Salaam Jumatatu kumaliza kila kitu Simba.
Ikimpata Dhaira, Simba SC itakuwa imepata kipa wa uhakika wa kusaidiana na kipa wake wa kwanza, Juma Kaseja ambaye amekuwa akisotoshwa peke yake bila kupumzika. Na hiyo inafuatia makipa wengine, Wilbert Mweta na Hamadi Waziri kushindwa kuonyesha uwezo wa kumsaidia Kaseja.
Katika mechi za mwishoni za mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Kaseja alionekana kuchoka na kudaka chini ya kiwango chake, jambo ambalo lilisababisha mashabiki wenye ‘akili mbovu’ wamfanyie fujo baada ya kufungwa mabao mawili katika mechi dhidi ya Mtibwa Sugar, Simba ikilala 2-0.
Kwa sababu hiyo, Kaseja alikasirika na kujiengua kwenye kikosi cha timu hiyo akisema hataki tena kuchezea Simba.
Lakini pamoja na matatizo hayo, Kaseja aliitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ambako ameendelea kufanya vizuri na kuonyesha yeye ni Tanzania One wa ukweli.  

AZAM: SIMBA WALIKIUKA MKATABA WETU NA NGASSA

Ngassa

KLABU ya Azam FC imesema kwamba, Simba SC ilikiuka mkataba wao wa kuwauzia kwa mkopo mchezaji Mrisho Ngassa kwa kitendo cha kumsainisha mkataba nyota huyo na kumpa gari aina ya Verosa na Sh. Milioni 18.
Taarifa ya Azam  imesema kwamba, wanashangaa Simba kulalamikia Azam kumuuza El Merreikh ya Sudan bila ya kufikia nao makubaliano, wakati wao walianza kukiuka mkataba. 
“Kwanza tunapenda umma uelewe kwamba, sisi tuliwashirikisha Simba mapema tu katika mpango huu, lakini wao wakataka fedha nyingi, ambazo Merreikh hawakuwa tayari kutoa, na sisi kwa kuzingatia maslahi ya mchezaji na taifa, tukaamua kutumia haki yetu, akiwa mchezaji wetu kwa kuamua kumuuza,”imesema taarifa ya Azam.
Azam imeliandika barua Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) juzi ikiwaomba wamruhusu Ngasa kwenda Sudan kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya katika harakati zake za kujiunga na El Merreikh ya nchini humo.
Azam FC imesema kwamba, katika barua waliyowapelekea TFF, nakala wamewapelekea pia na Simba SC, ambako mchezaji huyo alikuwa anacheza kwa mkopo.
“Msukumo uliotufanya tuandike barua hii ni kwa kutambua kuwa hii ni nafasi muhimu kwa Ngassa na taifa, kwani anakwenda kucheza kwenye timu yenye uwezo na miundombinu mikubwa barani Afrika, na inayoshiriki ligi ya mabingwa Afrika karibu kila msimu, kitu ambacho kitamuongezea Ngassa kiwango na kuwa na msaada kwa tafa,”ilisema taarifa ya Azam.
Aidha, Azam wamesema pia wanapenda kuweka wazi thamani ya usajili na mshahara ambao Ngassa. Wamesema Ngassa atakuwa anapewa na El Merreikh mshahara wa dola za Kimarekani 4,000, kiasi cha Sh. Milioni 6 za Tanzania kwa mwezi, ambazo kwa miaka miwili ni takribani Sh. Milioni 144 Milioni.
Wamesema mchezaji huyo amepewa fedha za kusaini dola za KImarekani 50,000, kiasi cha Sh. Milioni 80.
“Kwa hiyo Ngassa ataweka kibindoni zaidi ya Shilingi Milioni 230 kwa miezi 24, hizi ni fedha nyingi kwa mchezaji wa kitanzania na kwa maendeleo ya mchezaji na familia yake na yatawapa msukumo vijana wengi wenye kipaji kama Ngassa kufanya bidii kwenye soka na kuliletea maendeleo taifa,”ilisema taarifa ya Azam.
Azam FC imeomba TFF imruhusu Ngassa kwenda Sudan akitokea Uganda kwenda kukamilisha vipimo vya Afya na usajili na Azam FC ipo tayari kukaa na Simba na kuzungumza juu ya uhamisho huu kwa usimamizi wa TFF.
“Hapa ieleweke kuwa ingawa Azam FC inajua haki zake kisheria, lakini pia imeamua kupunguza msimamo wake kukubali mazungumzo kwa kuangalia zaidi athari ambazo mchezaji anaweza kupata kimaslahi na kimaendeleo ya uchezaji wake na mpira wa Tanzania kwa ujumla kutokana na mgogoro huu,”iliongeza taarifa hiyo.
Lakini Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ amesema klabu yake haiko tayari kufanya mazungumzo na Azam FC juu ya suala hilo.
Kaburu amesema, klabu yake iliingia mkataba na Azam FC kwa kununua haki zote za huduma za Ngassa kwa mwaka mmoja, hadi Mei 21 mwakani, ikilipa Sh. Milioni 25 kama ada ya kumtumia mchezaji huyo kwa mwaka mmoja pamoja na kumlipa mchezaji haki zake zote stahiki za kimkataba ikiwemo mshahara wake.
Kaburu amesema Azam bila ya kuzingatia mkataba iliousaini na Simba SC, na matakwa ya FIFA yanayohusu mkopo, iliamua kutangaza kumuuza Ngassa bila ya kuihusisha Simba wakati ikijua kuwa ilikuwa na Mkataba na Simba SC ambayo ameishaichezea katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Bara.
“Kitendo cha Azam FC kuongea na Klabu ya El Merreikh FC na kuweka makubaliano ya mauzo ya mchezaji na kumtangaza kuwa kimemuuza mchezaji Ngassa bila ya kuihusisha Simba SC, na baadaye kuiandikia klabu ya Simba kuwa kimeamua kumrudisha mchezaji Ngassa Azam, wakati ikijua kuwa ina mkataba na Simba SC ni uvunjifu mkubwa wa taratibu na umeleta athari kubwa kwenye klabu yetu,”alisema Kaburu na kuongeza;
“Tayari Simba SC ilikwishatuma malalamiko TFF na kupeleka pingamizi lake juu ya sulala hili kwa Rais wa TFF, Leodegar Tenga, ambapo imeamuliwa kuwa suala hili liende kwenye Kamati ya Sheria, Katiba na Hadhi ya Wachezaji likapatiwe ufumbuzi,”alisema.
Amesema Simba imekuwa ni klabu yenye kuangalia zaidi maslahi ya wachezaji na haina kipingamizi kwa kuwaruhusu wachezaji wake kutoka pindi wanapopata timu nje ya nchi kama utaratibu unafuatwa.
Kaburu amesema Simba SC ilikuwa tayari kukaa mezani na Azam kwa mazungumzo, lakini kwa kuwa Azam haipo tayari kutambua haki za Simba SC na imekuwa ikilitekeleza suala hili kiholela, hivyo haioni sababu za kuzungumza na Azam FC na kuliacha suala hili liende kwenye Kamati ya Sheria, Katiba na Hadhi ya Wachezaji kama TFF ilivyoagiza.

MBWANA MATUMLA: CHEKA, MIYEYUSHO YAWEZA KUWA WANATUMIA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU

Miyeyusho kulia akimuadhibu Nassib jana


Mbwana
BINGWA wa zamani wa dunia wa WBU, Mbwana Matumla ‘Golden Boy’, amesema ana wasiwasi Francis Miyeyusho na Francis Cheka wanatumia daw za kuongeza nguvu, zinazopigwa marufuku michezoni.
Akizungumza  jana, Golden Boy alisema kwamba umefika wakati Tanzania kuwe na utaratibu wa kuwapima mabondia kabla na baada ya michezo, kwani inawezekana kutokuwa na utaratibu huo kukatoa mwanya kwa mabondia wengine kutumia dawa hizo.
“Mimi nilipigana na Francis, kweli alinipiga, ila nilipata wasiwasi sana juu ya nguzu zake, kwa kweli hazikuwa za kawaida, sisemi kwamba anatumia, inawezekana ni uwezo wake, lakini nasema nina wasiwasi, yeye na Francis Cheka wanatumia hizo dawa,”alisema Mbwana.
Golden Boy alipigwa na Miyeyusho Oktoba 30, mwaka jana ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, kwa pointi, jaji Omari Yazidu akitoa 113-114, Said Chaku 110-117 na Jalus Lugongo 109-118.
Katika pambano hilo, Francis Miyeyusho alienda chini raundi ya pili, wakati Mbwana Matumla alidondoka raundi ya pili na ya nane na hilo ndilo lilikuwa pambano la mwisho la Golden Boy hadi sasa.
Miyeyusho ‘Chichi Mawe’ jana aliendeleza ubabe wake , baada ya kufanikiwa kutetea taji lake la WBF uzito wa Bantam, kwa kumpiga Nassib Ramadhan kwa Techinical Knockout (TKO) raundi ya 10 kwenye ukumbi wa PTA, Saba Saba, Temeke mjini Dar es Salaam usiku huu.
Nassib alionekana kuishiwa pumzi tangu raundi ya nane, lakini alijikongoja kutaka kumaliza raundi 12 za pambano hilo, ila kwa bahati mbaya, safari ikaishia raundi ya 10.
Hata hivyo, Nassib bondia kutoka Mabibo, Dar es Salaam, alilianza vizuri pambano hilo akimsukumia mpinzani wake makonde mazito yaliyoonekana kumyumbisha.
Naasib aliendelea kutawala pambano hadi raundi ya sita, ila baada ya hapo, mwelekeo wa pambano ulianza kubadilika taratibu, Chichi, Mtoto wa Kinondoni akianza kumuadhibu mpinzani wake kwa makonde yake yaliyoshiba uzito.
Nassib alijitahidi mara moja moja kujibu, lakini zaidi alitumia ujanja wa kumkumbatia Chichi ili kumpunguza kasi.
Hata hivyo, Nassib hakushindwa kwa kupigwa ngumi, bali aliishiwa pumzi jambo ambalo linaashiria kijana huyo ni bondia imara na anaweza kuwa mpinzani wa kweli wa Chichi Mawe.
Kwa ujumla lilikuwa pambano zuri ambalo kwa muda mrefu halijapatikana katika ardhi ya Tanzania- mabondia walikuwa wakipigana, hakukuwa na ujanja ujanja. Wote ni mafundi na mamia waliohudhuria pambano hilo, waliburudika kwa mchezo mzuri.
Katika mapambano ya awali, Deo Samuel alitoka sare na Freddy Sayuni, Mohamed Matumla alimpiga kwa Knockout (KO) raundi ya pili Deo Miyeyusho, Fadhil Majiha alimpiga kwa pointi Juma Fundi na Ibrahim Classic alimpiga kwa pointi Said Mbugi.
Mgeni rasmi, Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara alimvalisha mkanda wa ubingwa Miyeyusho baada ya pambano hilo, lililohudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’.  


WAKONGWE WA SANAA WATUNIKIWA NISHANI NA RAIS KIKWETE

Bibi. Kidude akivishwa nishani na Rais wa Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Kikwete

Akwari ambaye alikuwa mwanariadha

RAIS Jakaya Kikwete amewatunukia nishani ya heshima ya Jamhuri ya Muungano wanamuziki watatu, msanii mmoja wa maigizo na mwanariadha mkongwe.

Wasanii na wanamichezo hao wamepewa tuzo hizo leo jioni katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam.

Utoaji wa nishani hizo ni sehemu ya maadhimisho ya sherehe za miaka 51 ya uhuru wa Tanzania Bara, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Wasanii na wanamichezo waliopewa nishani hizo ni kiongozi wa bendi ya muziki wa dansi ya Msondo Ngoma, Muhidin Gurumo, kiongozi wa zamani wa bendi ya Dar es Salaam International, Marijani Rajabu na mwimbaji mkongwe wa taarab, Fatuma Baraka 'Bi Kidude'.
Wengine ni aliyekuwa msanii maarufu wa maigizo na filamu nchini, marehemu Fundi Saidi 'Mzee Kipara' na mwanariadha mkongwe, John Steven Akwari.
Gurumo, Bi Kidude na Akwari walihudhuria hafla hiyo na kuvishwa nishani zao na Rais Kikwete wakati nishani za Marijani na Mzee Kipara zilipokelewa na watoto wao.

Nishani ya sanaa na michezo, hutolewa kwa wasanii na wanamichezo mashuhuri, ambao kazi zao za sanaa au michezo zimeipatia sifa kubwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Bi Kidude hakuweza kwenda eneo la kupokea nishani kutokana na hali ya afya yake kutokuwa nzuri. Ilibidi Rais Kikwete amfuate mahali alipokuwa ameketi na kumtunukia nishani yake.

Bi Kidude, anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka zaidi ya 100 ni mwimbaji taarbab mkongwe aliyedumu kwenye fani hiyo kwa zaidi ya miaka 50. Ni msanii pekee wa taarab mwenye sifa zilizotukuka kutokana na ukongwe wake na umahiri wake katika kuimba taarab.

Gurumo alianza muziki 1960 na kushiriki katika bendi mbalimbali kama vile NUTA, JUWATA, OTTU, Atomic Jacc, Kiko Kids, Jamhuri Jazz, Kilwa Jazz, Rufiji Jazz, Mlimani Park, Msondo Ngoma. Ametunga nyimbo nyingi zinazoelimisha jamii kuhusu kuheshimu na kufanyakazi kwa juhudi na maarifa, kulinda uhuru wa nchi, kudumisha usawa, haki na amani na kuwaasa wazazi kutimiza wajibu wao kwa kulea watoto na vijana kutimiza wajibu wao.

Marehemu Marijani, maarufu kama Jabali la Muziki, alifariki dunia mwaka 1995. Alitoa mchango mkubwa katika tasnia ya muziki, alishiriki kutunga na kurekodi nyimbo zaidi ya 103, ambazo zilirekodiwa RTD, nyimbo zake zilikuwa na mafunzo mengi kwa jamii na zinaendelea kupigwa katika vituo mbalimbali vya redio nchini.

Mzee Kipara mwaka 1962 alijiunga na waigizaji wa Redio Tanzania, pia ameshiriki maigizo na tamthiria nyingi za kwenye televisheni kama vile Hujafa hujaumbifa, Fukuto, Radi, Gharika, Tufani na Tetemo.

Mzee Akwari aliweka historia ya pekee nchini mwaka 1968 pale aliposhiriki mbio za marathoni za Olimpiki na kuumia goti na kutoka malengelenge, lakini aliushangaza ulimwengu alipoendelea na kumaliza mbio hizo. Alipoulizwa, alisema 'mimi sikutumwa kuja kuanza mbio, nimetumwa kumaliza mbio'. Maneno hayo yamekuwa yakitumika kama mifano duniani

 

KATONGO AJA KUWAPA SHUGHULI MABEKI STARS

Katongo


KOCHA Mkuu wa timu ya Zambia, Chipolopolo, ambayo ni mabingwa wa Afrika, Herve Renard ametaja kikosi cha wachezaji 24 kitakachoikabili Taifa Stars kwenye mechi ya kirafiki itakayochezwa Desemba 22 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Chama cha Soka Zambia (FAZ), wachezaji hao ni Chintu Kampamba, Chisamba Lungu, Christopher Katongo, Danny Munyau, Davy Kaumbwa, Derrick Mwansa, Evans Kangwa, Felix Katongo na Francis Kasonde.
Wengine ni Given Singuluma, Hichani Himonde, Isaac Chansa, James Chamanga, Jimmy Chisenga, Jonas Sakuwaha, Joshua Titima, Kalililo Kakonje, Moses Phiri, Mukuka Mulenga, Rainford Kalaba, Rodrick Kabwe, Salulani Phiri, Shadrack Malambo na Stoppila Sunzu.

MESSI AVUNJA REKODI YA MIAKA 40 YA MULLER!!


>>FALCAO APIGA BAO 5 MECHI MOJA!!
MESSI_ASHANGILIA_GOLILA LIGA
RATIBA/MATOKEO:
Jumapili Desemba 9
Levante 4 Mallorca 0
Athletic Bilbao 1 Celta Vigo 0
Atletico Madrid 6 Deportivo La Coruna 0
Real Betis 1 Barcelona 2
Jumatatu Desemba 10
Rayo Vallecano v Real Zaragoza
++++++++++++++++++++++++++++++
LA LIGA jana ilimshuhudia Supastaa Lionel Messi akiifungia Timu yake Barcelona Bao mbili na kuipa ushindi wa Bao 2-1 dhidi ya Real Betis huku yeye akivunja Rekodi ya tangu Mwaka 1972 ya Straika wa Germany Gerd Muller ya kufunga Bao 85 ndani ya Mwaka mmoja wa Kalenda kwa yeye kufikisha Mabao 86 na wakati huo huo Straika hatari wa Atletico Madrid Radamel Falcao akipiga Mabao 5 katika Mechi moja walipoifunga Deportivo La Coruna Mabao 6-0.
+++++++++++++++
WAFUNGAJI BORA:
-Lionel Messi=Bao 23
-Radamel Falcao=16
-Ronaldo=13
-Aduriz=9
+++++++++++++++
Matokeo hayo ya jana yameifanya Barca izidi kupaa kileleni ikiwa na Pointi 43, Atletico Madrid nafasi ya Pili Pointi 37 na Real Madrid ni wa Tatu Pointi 32.
MSIMAMO-Timu za Juu
[Kila Timu imecheza Mechi 15]
1 Barcelona Pointi 43
2 Atletico Madrid 37
3 Real Madrid 32
4 Malaga 25
5 Real Betis 25
6 Levante 24
7 Getafe 23Bottom of Form


MJUE MESSI TOKA UDOGONI MPAKA LEO ANAPOVUNJA REKODI KIBAO


Lionel Andres Messi anazidi kuishangaza dunia kwa uwezo wake mkubwa karika soka. Lionel Messi aliezaliwa miaka 25 huko Rosario , Argentina. Messi ni mtoto wa Mzee Jorge Horacio Messi ambae alikuwa mfanyakazi wa kiwanda cha Chuma na mama yake  Celia Maria Cuccitti. Kwa upande wa Baba yake Messi anaasili ya Italy tokea mji mmoja unaitwa Ancoma, ambako ilikuwa ni asili ya babu yake aitwae Angelo Messi aliehamia Argentina mwaka 1883. Messi ana kaka wawili na dada mmoja.

Katika umri wa miaka mitano Leo Messi alianza kucheza soka katika club ya Grandoli. Hii ilikuwa klabu ya mtaani kwao iliyokuwa inasimamiwa na Baba ake. Mwaka 1995 Messi alihamia katika klabu ya Newell's Old Boys iliyopo katika mji wake wa Rosario. 
Messi akiwa na miaka 11

Akiwa na miaka 11 Messi aligundulika kukosa hormone za ukuaji. Baada ya kugundulika na tatizo hilo, Klabu ya River Plate moja ya klabu kubwa sana nchini Argentina ilitaka kumchukua ila ikashindwa kutokana na gharama za matibabu yake. Dola $900 ilitakiwa kila mwezi kwa ajili ya gharama za matibabu ya mtoto Messi. Carles Rexach mkurugenzi wa michezo wa Barcelona alikifahamu kipaji cha Messi baada ya kumuona akiwa katika majaribio na Klabu ya Llieda.
Raxach alikubali kumpa Messi mkataba na Barcelona, akiwa hana karatasi yoyote mkononi alimwandikia mkataba wa kwanza Messi katika Leso.
Hatimaye Barcelona walikubali gharama za matibabu ya Messi kwa masharti kuwa ahamie Hispania. Bila kipingamizi Messi na Baba yake wote wakahamia Hispania na Lionel akaanza kuitumikia klabu ya Barcelona akiwa katika katika shule ya vipaji ya  klabu hiyo iliyo maarufu sana kama La Masia. 
Messi na Macarena 

Inasemekana Messi amewahi kuwa na uhusiano na mwanadada Macarena ambae naye anatokea katika mji wa Rosario.  Messi alitambulishwa kwa Rosario na baba yake Rosario kipindi aliporudi kuuguza majeraha yake kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia 2006. Messi pia alishawahi kuwa na uhusiano na mwanamitindo wa Argentina mwanadada Luciana Salazaar.
Januari 2009 katika mahojiano ya kipindi "Hat-Trick Barca'" cha Canal 33 Messi alisema anauhusiano na mwanamke mmoja hivi (hakumtaja jina) na anafuraha kuwa nae swali hilo lilikuja baada ya Messi kuonekana katika sehemu mbalimbali na mwanadada Antonella Roccuzzo. Juni mwaka 2012 Messi akicheza mechi dhidi ya Ecuador alifanikiwa kufunga goli, alishangilia Goli hilo kwakuweka mpira ndani ya jezi yake kuashiria kuwa mpenzi wake ni mjamzito. Siku kadhaa baadae ikaripotiwa na vyombo vya habari kuwa mpenzi wake ana ujauzito wa wiki 12 (miezi 3). Mnamo Tarehe 2 Novemba mwaka 2012 mtoto wa kwanza wa Messi alizaliwa na kupewa jina la Thiago.


Messi akishangilia bao dhidi ya Ecuador




Messi ana ndugu wawili ambao waacheza mpira. Maxi anaichezea klabu ya Club Olimpia nchini Paraguay na Emmanuel Biancucchi. Pamoja na kuishi Spain kwa muda mrefu ila Messi hajaacha kupakumbuka Rosario. KIla mara hutembelea mji huu na pia ana mawasiliano na marafiki na ndugu kadhaa wanaoishi katika mji huo. Inasemekana wakati mmoja Argentina ilipokuwa ikifanya mazoezi mjini Buenos Aires. Messi aliendesha mwendo wa masaa matatu baada ya mazoezi kwenda Rosario kula chakula cha jioni na kulala na kesho yake kugeuza mapema kabla ya mazoezi. Messi bado anamiliki nyumba yao ya zamani ambako alikuwa anaishi na familia yake japokuwa hakuna mwanafamilia anayeishi hapo siku hizi.

  

Mwaka 2007, Messi ameanzisha Charity Foundation kwa ajili ya kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu na wenye uhitaji.
Messi alitangazwa kuwa balozi wakujitolea wa UNICEF katika maswala ya kupigania haki za watoto. Barcelona nao wako nyuma wanamsaidia messi katika hili kwakuwa Barcelona na Messi wana uhusiano mzuri.


Messi alianza kuichezea timu ya wakubwa ya Barcelona tarehe 16 Novemba mwaka 2003 akiwa na umri wa miaka 16 na siku 145 katika mchezo wa kirafiki kati ya Barcelona na F.C Porto ya Ureno.
Miezi michache baadae Frank Rijkaard kocha wa barcelona kipindi hicho alimpatia Messi nafasi ya kucheza ligi ya Spain dhidi ya RCD Espanyol akiwa na Umri wa miaka 17 na siku 114 hivo kumfanya Messi kuwa mchezaji wa tatu mwenye umri mdogo kuichezea Barcelona na mdogo kabisa kuichezea Barcelona katika ligi. Rekodi ambayo baadae ilikuja kuvunjwa na Bojan Krikic. Goli la kwanza la Messi katika timu ya wakubwa alilifunga dhidi ya Albacete Balompie mwezi Mei mwaka 2005. September mwaka huohuo Messi alipata urai wa Spain.
Baada ya hapo amekuwa akicheza kwa mafanikio makubwa. Messi katika kipindi hichi chote toka alipoanza kuichezea Barcelona amepata mafanikio mengi. Mafanikio Binafsi kama mchezaji na Mafanikio ya timu pia. 

Messi ameweza kuvunja rekodi nyingi ambazo ziliwekwa na magwiji wa soka wa zamani. Tukianzia katika klabu yake Messi ameweka rekodi ya kuwa mchezaji anaeongoza kwa kufunga mabao mengi katika historia ya klabu hiyo akiwa na magoli 283 na pia ni mchezaji alieifungia Barcelona mabao mengi katika ligi ya Hispania uku akiwa na mabao 192. Messi anashikilia rekodi ya klabu yakufunga Mabao mengi kwenye msimu mmoja akiwa amefunga magoli 73 katika msimu wa 2011-2012. Messi anashikilia rekodi ya Barcelona ya mchezaji aliefunga magoli mengi katika mashindano ya ulaya akiwa na magoli 57 na 56 katika ligi ya mabingwa ulaya. Messi anaongoza listi ya mchezaji aliefunga magoli mengi katika Spanish Super Cup akiwa na magoli 10.
 
Messi ana rekodi ya kuwa mchezaji alieifunga magoli mengi kwa msimu mmoja katika michuano ya mabingwa ulaya akiwa na magoli 14, Messi huyuhuyu ana rekodi ya kufunga magoli mengi katika mchezo mmoja wa ligi ya mabingwa ulaya akiwa amefunga 5 katika mechi dhidi ya Bayern Leverkusen msimu wa 2011-2012. Messi ana rekodi pia yakufunga hat-tricks nyingi ndani ya msimu mmoja akiwa amefunga hat-trick mara 8 msimu wa 2011-2012. Na bila kusahau Messi anashikilia rekodi ya Barcelona ya kufunga magoli mengi katika ile michuano ya klabu bingwa ya dunia akiwa na magoli 4.


Kwa ujumla Messi anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji aliefunga magoli mengi katika msimu mmoja wa ligi ya hispania akiwa amefunga magoli 50 katika msimu mmoja. anashikilia rekodi ya kufunga magoli mengi katika msimu mmoja wa ligi ya mabingwa huko akiwa a magoli 14 na pia anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji aliefunga magoli mengi ndani ya msimu mmoja akiwa na magoli 73 katika mashindano yote. Messi hajaishia hapo, Jana tarehe 09-Dec-2012 Messi amevinja rekodi ya mkongwe Gerd Muller ya mabao 85 katika mwaka mmoja ambayo ilidumu kwa miaka 40. Messi amefunga goli la 85 na 86 jana akiisaidia Barcelona kushinda mchezo wake dhidi Real Betis. Messi ameweka rekodi hiyo mpya uku akiwa na michezo mitatu mpaka mwisho wa mwaka. 


Messi bado ana rekodi zake binafsi. Messi ameshinda tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka kwa miaka 3 mfululizo (209,2010,2011) na mwaka huu yuko katika ile tatu bora. Messi anashikilia tuzo ya mfungaji bora wa bara la Ulaya ya mwaka 2010 na mwaka 2012. Mshambuliaji bora wa ligi ya Hispania mwaka 2009,2010,2011,2012. Mchezaji bora wa ligi ya hispania mwaka 209,2010,2011,2012.  Mfungaji bora ligi ya Mabingwa ulaya mwaka 2009,2010,2011 na 2012. Man of the match fainali ya ligi ya mabingwa mwaka 2011.
SOURCE:http://valetyno.blogspot.ca

BPL: Everton yashinda mwishoni yakamata nafasi ya 4!!

>>LIVERPOOL YATUMBUKIA 10 BORA MARA YA KWANZA MSIMU HUU!!!
+++++++++++++++++++++++++++++++++
MSIMAMO-Timu za juu:
[Kila Timu Mechi 16]
1 Man United Pointi 39
2 Man City 33
3 Chelsea 29
4 Everton 26
5 Tottenham 26
6 WBA 26
7 Arsenal 24
8 Swansea 23
9 Stoke 23
10 Liverpool 22
+++++++++++++++++++++++++++++++++
BPL_LOGOWEST HAM 2  LIVERPOOL 3
Bao mbili ndani ya Dakika 3 katika Kipindi cha Pili, katika Dakika ya 76 kupitia Joe Cole na Dakika ya 79 kwa kujifunga mwenyewe Collins, kumewafanya Liverpool waibuke toka Bao 2-1 nyuma na kushinda 3-2 walipocheza Uwanjani Upton Park na West Ham.
Liverpool walitangulia kufunga kwa Bao la Glen Johnson na Mark Noble akaisawazishia West Ham kwa Penati kisha Nahodha Steven Gerrard akajifunga mwenyewe na kuwapa West Ham uongozi wa Bao 2-1 hadi mapumziko.
Ushindi huu umewafanya Liverpool wakamate nafasi ya 10 ikiwa ni mara ya kwanza Msimu huu wao wakanyage nusu ya juu ya Msimamo wa Ligi.
VIKOSI:
West Ham: Jaaskelainen, Demel, Collins, Reid, O'Brien, Taylor, Diame, Nolan, Noble, Jarvis, Cole
Akiba: Spiegel, McCartney, Tomkins, Maiga, Spence, O'Neil, Moncur.
Liverpool: Reina, Johnson, Skrtel, Agger, Jose Enrique, Allen, Lucas, Gerrard, Sterling, Shelvey, Downing
Akiba: Jones, Cole, Henderson, Coates, Carragher, Fernandez Saez, Morgan.
Refa: Lee Probert
EVERTON 2 SPURS 1
Goli mbili za Steven Pienaar na Nikica Jelavic katika Dakika za majeruhi zimewapa ushindi Everton wa Bao 2-1 dhidi ya Tottenham Uwanjani Goodison Park.
Tottenham walipata Bao lao katika Dakika ya 76 baada ya shuti la Clint Dempsey kumbabatiza Beki na kutinga.
Ushindi huu umewafanya Everton wapande na kukamata nafasi ya 4 kwenye Msimamo wa Ligi.
VIKOSI:
Everton: Howard, Coleman, Jagielka, Distin, Baines, Mirallas, Gibson, Osman, Pienaar, Fellaini, Jelavic
Akiba: Mucha, Heitinga, Oviedo, Naismith, Hitzlsperger, Barkley, Vellios.
Tottenham: Lloris, Walker, Gallas, Caulker, Vertonghen, Lennon, Dempsey, Dembele, Sandro, Adebayor, Defoe
Akiba: Friedel, Huddlestone, Naughton, Sigurdsson, Falque, Livermore, Townsend.
Refa: Lee Mason
+++++++++++++++++++++++++++
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumatatu 10 Desemba 2012
[SAA 5 Usiku]
Fulham v Newcastle
Jumanne 11 Desemba 2012
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Sunderland v Reading
Jumamosi 15 Desemba 2012
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Newcastle v Man City
[SAA 12 Jioni]
Liverpool V Aston Villa
Man United V Sunderland
Norwich v Wigan
QPR v Fulham
Stoke v Everton
Jumapili 16 Desemba 2012
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Tottenham v  Swansea
[SAA 1 Usiku]
West Brom v West Ham
Jumatatu 17 Desemba 2012
[SAA 5 Usiku]
Reading v Arsenal

CAPITAL ONE CUP: Robo Fainali kuchezwa katikati ya Wiki

>>KLABU LIGI KUU pekee ni Norwich v Villa!!
CAPITAL_ONE_CUP-BESTZILE Robo Fainali za CAPITAL ONE CUP, zamani Carling Cup na Ligi Cup, zitanyika katikati ya Wiki hii isipokuwa Mechi ya Leeds United na Chelsea ambayo itafanyika Wiki ijayo kwa vile Chelsea watakuwa huko Japan kushiriki Mashindano ya FIFA ya Klabu Bingwa Duniani.
+++++++++++++++++++++++++
CAPITAL ONE CUP-Robo Fainali:
[Mechi zote kuchezwa Saa 4 Dak 45 Usiku]
Jumanne Desemba 11
Norwich v Aston Villa
Bradford v Arsenal
Jumatano Desemba 12
Swansea v Middlesbrough
Jumatano Desemba 19
Leeds United v Chelsea
+++++++++++++++++++++++++
Mechi pekee ambayo inazikutanisha Klabu za Ligi Kuu England ni ile kati ya Norwich City na Aston Villa.
+++++++++++++++++++++++++
DONDOO MUHIMU za CAPITAL ONE CUP:
-KABLA LILIKUWA ni Carling Cup na Bingwa Mtetezi alikuwa ni Liverpool.
-Linaitwa CAPITAL ONE CUP kwa sababu Mdhamini wake ni Kampuni ya masuala ya Fedha, Capital One.
-Linashirikisha Timu za Ligi za juu England 92 kwa mtindo wa Mtoano [Timu 20 toka Ligi Kuu na 24 kila moja kutoka Madaraja ya Npower, Ligi 1 na 2.
-Bingwa wa michuano hii hucheza EUROPA LIGI Msimu unaofuata kuanzia Raundi ya Tatu ya Mtoano.
+++++++++++++++++++++++++

MAN UNITED 6 JUU, YAVUNJA REKODI YA CITY KUTOFUNGWA NYUMBANI, YAIBAMIZA 3-2!


>>MASHABIKI WAMPASUA RIO BAADA YA KUCHAPWA BAO LA 3!!!
RVP_in_RED2Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England, Manchester City, leo wamekiona chaROONEY_n_ROBERTO12mtema kuni baada ya kuchapwa Uwanjani kwao Etihad Bao 3-2 na Mahasimu wao Manchester United  na ile rekodi yao ya kutofungwa nyumbani kwa Miaka miwili katika Ligi, jumla ya Mechi 38, kutokomezwa leo.
+++++++++++++++++++++++++++++++++
MAGOLI:
Man City 2
-Yaya Toure, Dak ya 60 & Zabaleta, Dak ya 86
Man United 3
-Rooney, Dak ya 16 na 29, & Robin van Persie, Dak ya 93
+++++++++++++++++++++++++++++++++
Bao la Dakika za Majeruhi la frikiki ya Robin van Persie liliwapa ushindi Man United na sasa wamepaa kileleni wakiwa Pointi 6 mbele ya Man City ambao wako nafasi ya Pili na Pointi 10 mbele ya Timu ya 3 Chelsea.
+++++++++++++++++++++++++++++++++
MSIMAMO-Timu za juu:
[Kila Timu Mechi 16]
1 Man United Pointi 39
2 Man City 33
3 Chelsea 29
4 Tottenham 27
5 WBA 26
6 Arsenal 24
+++++++++++++++++++++++++++++++++
Hadi mapumziko Manchester United walikuwa mbele kwa Bao 2-0 kwa Bao za Wayne Rooney lakini Kipindi cha Pili Man City walipata Bao moja kupitia Yaya Toure na Pablo Zabaleta akasawazisha zikiwa zimebaki Dakika 4.
Lakini Man United watalalamika sana kwa kunyimwa Bao alilofunga Ashley Young, ambalo lingewafanya waongoze 3-0, baada ya kuamuliwa ni Ofsaidi wakati haikuwa hivyo.
Mara baada ya Man United kufunga bao lao la ushindi wakati wanasheherekea Shabiki mmoja alimpiga Rio Ferdinand na kitu kilichompasua juu Jichoni.
VIKOSI:
Man City: Hart, Zabaleta, Kompany, Nastasic, Clichy, Silva, Toure, Barry, Nasri, Aguero, Balotelli
Akiba: Pantilimon, Maicon, Lescott, Dzeko, Javi Garcia, Toure, Tevez.
Man United: De Gea, Da Silva, Ferdinand, Evans, Evra, Valencia, Carrick, Cleverley, Young, Rooney, van Persie
Akiba: Johnstone, Jones, Giggs, Smalling, Hernandez, Welbeck, Scholes.
Refa: Martin Atkinson