Thursday, December 13, 2012

SHABIKI PEKEE WA TIMU UWANJANI AKONGA MIOYO!

 

>>NI WA UDINESE, Arrigo Brovedani, UWANJA MZIMA PEKE YAKE!!!
>>MASHABIKI WAPINZANI WAMPIGIA MAKOFI!!
SHABIKI_PEKEE_UWANJANIVyombo vya Habari huko Italy vimemtangaza sana Shabiki wa Udinese, Arrigo Brovedani, baada ya kunaswa akiwa peke yake Uwanja mzima kuishangilia Timu yake ilipocheza ugenini Mjini Genoa dhidi ya Sampdoria kwenye Mechi ya Serie A.
Arrigo Brovedani, Miaka 30, na Muuza Mvinyo, alijikuta yuko Uwanjani peke yake Sehemu ya Mashabiki wa Timu ya Ugenini na Walinzi wa Uwanjani hapo wakamkaribisha Kahawa na baada ya Mechi Mashabiki wa Sampdoria walimkaribisha Vinywaji.
Arrigo Brovedani aliwaambia Wanahabari hakutegemea kukuta Mashabiki wengi wa Udinese kwani si Timu kubwa na kawaida huvutia Mashabiki 50 hadi 60 kwa Mechi zao za ugenini lakini alishangazwa Siku hiyo kujikuta yuko peke yake Uwanjani.
Alisema: “Nilipoingia nilidhani nitakuta Wenzangu 6 au 7, nilipoingia Udinese walikuwa wakipasha moto na nikawapigia kelele kuwasalimia. Nilipoingia, nikiwa na Bendera na Skafu, Mashabiki wa Sampdoria walinizomea, nilichukia. Lakini mwishowe walinipigia makofi, wakanikaribisha Vinywaji, Mameneja wa Uwanja walinizawadia Shati. Wote walinitakia Krismas njema!”
Mji wa Genoa uko mwendo wa Masaa manne kwa Gari kutoka Friulli ambako ndiko Udinese walipo na Arrigo Brovedani, aliekuwepo Genoa kikazi, aliamua kwenda kuitazama Timu yake anayoipenda na Siku zote hutembea na Bendera na Skafu ya Timu yake ndani ya Gari lake.
Kwa bahati njema, Udinese waliifunga Sampdoria Bao 2-0 katika Mechi hiyo na Timu hiyo iliutoa ushindi huo kama spesho kwa Shabiki Pekee Arrigo Brovedani na pia kumwalika awepo kwenye Mechi inayofuata ya Nyumbani ya Udinese.
 

KLABU BINGWA DUNIANI: FAINALI ni CHELSEA v CORINTHIANS!!

>>KUSAKA MSHINDI wa 3: Al Ahly v Monterrey!
FIFA_CLUB_WORLD_CUPChelsea wameanza Mashindano yao ya kwanza kabisa ya FIFA kusaka Klabu Bingwa Duniani kwa kuitandika Monterrey ya Mexico Bao 3-1 katika Nusu Fainali iliyochezwa huko Japan hivi leo.
++++++++++++++++++++++
MAGOLI:
Monterrey 1
-De Nigris Dakika ya 90
Chelsea 3
-Mata Dakika ya 17
-Torres 46
-Chavez 48′ (Kajifunga mwenyewe)
++++++++++++++++++++++
Sasa Chelsea watacheza Fainali hapo Jumapili dhidi ya Klabu ya Brazil, Corinthians, ambao walifuzu Nusu Fainali yao hapo jana kwa kuwafunga Mabingwa wa Afrika, Al Ahly, Bao 1-0.
Al Ahly na Monterrye zitacheza hio Jumapili kabla ya Mechi ya Fainali kutafuta Mshindi wa Tatu wa Mashindano haya.
+++++++++++++++++++++
RATIBA:
MSHINDI wa 3
Desemba 16
[Uwanja wa Yokohama]
[Saa 4 na Nusu Asubuhi]
Al Ahly v Monterrey
FAINALI
[Saa 7 na Nusu Mchana]
Corinthians v Chelsea
+++++++++++++++++++++
Chelsea walitangulia kupata Bao zao 3 kupitia Juan Mata, Fernando Torres na la tatu alifunga alijifunga mwenyewe Mchezaji wa Monterrey Darvin Chavez alipotumbukiza wavuni krosi ya Mata.
Katika Dakika za majeruhi, Monterrey walipata kifutia machozi kwa Bao la Aldo de Nigris.
Katika Mechi ya leo, kivutio kikubwa ni kumwona Sentahafu David Luiz akicheza vizuri kama Kiungo, akiziba vizuri pengo la Kiungo Oriol Romeu ambae aliumia Wiki iliyopita na inasemekana atakuwa nje ya Uwanja kwa Miezi 6.
+++++++++++++++++++++
MABINGWA WALIOPITA:
-2000 - Corinthians
-2005 - Sao Paulo
-2006 - Internacional
-2007 - AC Milan
-2008 - Manchester United
-2009 - Barcelona
-2010 - Inter Milan
-2011 – Barcelona
++++++++++++++++++
KLABU BINGWA DUNIANI 2012
TIMU ZITAKAZOSHIRIKI:
Chelsea-BINGWA ULAYA
Corinthians-BINGWA MAREKANI ya KUSINI
Monterrey-BINGWA MAREKANI ya KATI NA KASKAZINI
Auckland City-BINGWA KANDA ya OCEANIA
Usain Hyundai-BINGWA-Barani Asia
Al Ahly-BINGWA-Barani Afrika
Sanfrecce Hiroshima-BINGWA-Japan J-LIGI
RATIBA/MATOKEO:
Raundi ya Mchujo - Desemba 6, Yokohama
Sanfrecce Hiroshima 1 Auckland City 0
ROBO FAINALI - Desembar 9, Toyota
Usain Hyundai 1 Monterrey 3
Sanfrecce Hiroshima 1 Al Ahly 2
MSHINDI wa 5- Desemba 12, Toyota
[Saa 4 na Nusu Asubuhi]
Usain Hyundai 2 Sanfrecce Hiroshima 3
NUSU FAINALI
Desemba 12, Toyota
[Saa 7 na Nusu Mchana]
Al Ahly 0 Corinthians 1
Desemba 13, Yokohama
[Saa 7 na Nusu Mchana]
Monterrey 1 Chelsea 3
MSHINDI wa 3
Desemba 16
[Uwanja wa Yokohama]
[Saa 4 na Nusu Asubuhi]
Al Ahly v Monterrey
FAINALI
[Saa 7 na Nusu Mchana]
Corinthians v Chelsea

REDDS' MISS TANZANIA 2012 ZIARANI KAGERA

Redd's Miss Tanzania 2012 Brigitte Alfred, alitua jana mjini Bukoba na  leo tarehe 13 Desemba 2012 ametembelea  Shule maalum ya Mugeza Mseto, inayofundisha wanafunzi wenye ulemavu, pia ametembelea  Kituo cha Nusura ambacho kinatunza watoto yatima kilichopo eneo la  Kashai.
Mrembo Brigitte Alfred, ambaye pia ni Balozi wa Walemavu wa ngozi, [Albinos] ametoa misaada ya kijamii katika vituo hivyo. Vifaa hivyo ni pamoja na Fimbo maalum za kutembelea walemavu wasioona, Miwani, Kofia na Madawa ya ngozi kwa ajili ya Walemavu wa ngozi. Pamoja na vyakula.


Redds Miss Tanzania 2012 pia atatembelea Wilaya ya Misenyi Kesho na kutoa misaada kama hiyo katika kituo kimoja kilichopo wilayani hapa.

Ziara ya Miss Tanzania 2012 imedhaminiwa na Optima Lodge & Safaris pamoja na Victoria Perch Hotel zote za Mkoani Kagera.
Kabla ya kurejea jijini DSM Redds Miss Tanzania 2012 ataelekea Mwanza kwa shughuli zingine za kijamii





JKT OLJORO USIPIME, YAICHAKAZA KAGERA SUGAR KARUME


Mshambuliaji wa JKT Oljoro Robert Mjata akipiga shuti golini mwa Kagera Sugar wakati wa mchezo wao wa mashindano ya Uhai uliochezwa leo asubuhi uwanja wa Karume, JKT Oljoro walishinda mabao 3-0.
Benchi la JKT Oljoro B

Benchi la Kagera Sugar B
TIMU B ya JKT Oljoro leo imeanza vema mashindano ya Uhai baada ya kuifunga Kagera Sugar mabao 3-0 kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo ulikuwa wa ushindani sana na timu zote kushambuliana lakini wakichunga lango lao ulipelekea kipindi cha kwanza kumalizika bila kufungana.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko lakini mabadiliko yaliinufaisha JKT Oljoro kwani iliweza kuifunga Kagera mabao ya haraka na kuanza kulinda lango lao.

Mabao ya JKT Oljoro yalifungwa na Hamis Swalehe dakika ya 49 na Shamiri Mohamed alifunga mawili dakika ya 52 na 55.

Kwenye mchezo uliochezwa juzi jioni kwenye uwanja wa Karume Polisi Morogoro waliifunga Azam bao 1-0

Mchezo huo ulikuwa wa ushindani sana kila timu ikitafuta bao kwa hali na mali lakini dakika ya 80 Polisi Morogoro walipata bao baada ya kutokea piga na nikupige langoni kwa Azam.

Bao hilo lilifungwa na Benja Ngasa kwa shuti la karibu na go

Real yalala, Barca yaua

WAKATI Lionel Messi akiifungia mara mbili Barcelona na kuipa ushindi wa 2-0 kwenye mechi ya Kombe la Mfalme "Copa del Rey" dhidi ya Cordoba usiku wa kuamkia jana, Celta Vigo iliinyuka Real Madrid 2-1 katika kinyang'anyiro hicho.
Mario Bermejo na Cristian Bustos ndiyo walioiwezesha Celta kuongoza kwa mabao 2-0 kabla ya Cristiano Ronaldo kufunga bao la usiku na kurejesha matumaini kwa Real kuingia katika mzunguko wa pili.

Seydou Keita arudi Barcelona


Image associated to news article on:  Seydou Keita
KIUNGO wa Dalian Aerbin, Seydou Keita, amerudi kujifua Barca akijiandaa na fainali za Mataifa ya Afrika mwakani baada ya Ligi Kuu ya China kufikia ukiongoni.
Keita, ambaye alikuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Josep Guardiola wakati akiinoa miamba hiyo Camp Nou, aliichezea Barca jumla ya mechi 188 kati ya 2008 na 2012, huku akishinda mataji 14 na 'Blaugrana' hao

-Wenger, Bould kuna mpasuko, mastaa Arsenal hawataki kucheza mfumo kama wa Barca


KIMENUKA! Hilo ndilo neno unaloweza kuanza kulitamka wakati ukielezea hofu kubwa ya wachezaji nyota wa Arsenal ambao wamebaini kuwepo mpasuko katika chumba chao cha kubadilishia kati ya Kocha Mkuu, Arsene Wenger na Msaidizi wake, Steve Bould.
Hali hiyo imebainika katika mechi ya Kombe la Ligi maarufu kama 'Capital One Cup' dhidi ya Bradford ambapo timu hiyo ilitolewa kwa penalti 3-2 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120.
Licha ya nyota hao wa Arsenal kujitahidi kucheza soka la kuvutia, wakati wa mapumziko, Wenger aliwakoromea akidai walishindwa kumudu staili hiyo ya uchezaji.
Kocha huyo pia alimpondo Gervinho kwa kukosa nafasi katika kipindi cha kwanza, lakini yote kwa yote niwachezaji hao kubaini mpasuko kati ya Wenger na Bould ambaye alitua 'The Gunners' katika majira ya joto kuziba nafasi ya Pat Rice.
Chanzo kimoja kilisema: “Kunaonekana hakuna mawasiliano makubwa kati ya wawili hao. Ni aibu kwa sababu wachezaji wote wanaonekana kuwa nyuma ya Wenger, ingawa pia mambo ni sawa kwani wote wanamkubali Bould. Mambo yanatia hofu.”
Chanzo hicho kilieleza kuwa, Wenger bado ndiye kiongozi mkuu wa wachezaji. Kikaongeza: “Bould anawanoa mabeki kabla hata ya kuanza kwa msimu, lakini hajawahi kuruhusiwa kufanya maamuzi, Wenger amekuwa akiamua kila kitu.”
Hilo limewafanya wengi waamini usemi wa nyota wa zamani wa Arsenal, Stewart Robson, ambaye alimuita Wenger  "dikteta".
Hata hivyo, wachezaji hao pia wamemtaka Wenger kubadili mfumo wa uchezaji wa soka la kuvutia kama Barcelona na kucheza soka la nguvu na lakushtukiza.
Gazeti la "The Sun", limeeleza kuwa, wachezaji wa kikosi cha kwanza wameonekana kuwa wanyonge kutokana na kulazimishwa kucheza soka la kuvutia ambalo mara nyingi linawanyima fursa ya kupiga mashuti na hata kushindwa kuingia kwenye 18.
Chanzo hicho kilisema: “Arsenal huwa inacheza soka zuri, lakini haliwezi kuwa na mvuto kama la Barcelona.
“Mbali na hilo, pia wachezaji wanataka kazi ya kupanga safu ya ulinzi ibaki mikononi mwa Bould, huku pia wakishangaa kwanini Gervinho anaruhusiwa kucheza kama mshambuliaji wa kati wakati wengine wakilazimishwa kucheza nafasi zisizo zao.”

COASTAL YAENDELEA KUTAMBA KOMBE LA UHAI


TIMU ya Coastal Union ya Tanga imeendelea kufanya vizuri kwenye michuano ya kuwania Kombe la Uhai inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom baada ya jana (Desemba 12 mwaka huu) kuifunga Toto Africans mabao 3-1.
Mabao ya Coastal katika mechi hiyo ya kundi A iliyochezwa Uwanja wa Chamazi yalifungwa na Mohamed Miraji dakika ya 44, Abdul Banda (dk. ya 62) na Ramadhan Shame (dk. ya 83). Toto Africans ndiyo iliyoanza kupata bao dakika ya 30 lililofungwa na Severin Constantine.
Coastal Union ilishinda mechi yake ya kwanza mabao 2-1 dhidi ya Tanzania Prisons katika michuano hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Said Salim Bakhresa kupitia maji Uhai.
Nayo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya African Lyon katika mechi ya kundi B iliyochezwa leo asubuhi (Desemba 12 mwaka huu) Uwanja wa Karume. Miraji Athuman na Ramadhan Mzee ndiyo walioifungia Simba dakika ya 15 na 47 wakati la African Lyon lilifungwa dakika ya 57 na Mbela Kashakala.
Polisi Morogoro iliifunga Azam bao 1-0 kwenye Uwanja wa Karume wakati katika Uwanja wa Azam, JKT Ruvu iliifunga Tanzania Prisons bao 1-0 lililofungwa dakika ya 16 na Jacob Mambia. Yanga na Ruvu Shooting zilitoka suluhu kwenye Uwanja wa Chamazi.
Katika mechi iliyochezwa leo asubuhi (Desemba 13 mwaka huu) Uwanja wa Karume, Oljoro JKT imeizamisha Kagera Sugar mabao 3-0. Mabao hayo yamefungwa na Hamis Saleh dakika ya 49 huku Shamir Mohamed akipachika mawili dakika ya 52 na 55.
Michuano hiyo itaendelea kesho (Desemba 14 mwaka huu) kwa michezo kati ya Mtibwa Sugar vs Toto Africans (asubuhi- Karume), Coastal Union vs JKT Ruvu (mchana- Karume), Oljoro JKT vs Yanga (asubuhi- Chamazi), Ruvu Shooting vs Kagera Sugar (mchana- Chamazi), Mgambo Shooting vs Simba (asubuhi- Chamazi) na African Lyon vs Azam (jioni- Chamazi).

KOCHA WA PSG AJA KUFUNDISHA SIMBA, KUTUA DAR BAADA YA KRISIMASI

Liewig

KOCHA wa zamani wa Akademi ya Paris Saint Germain (PSG) ya Ufaransa, ASEC Mimosas ya Ivory Coast na Club Africain ya Tunisia, Patrick Liewig ndiye atakayerithi mikoba ya Mserbia, Profesa Milovan Cirkovick katika klabu ya Simba.
Katibu wa Simba SC, Evodius Mtawala amesema  leo kwamba, Liewig atatua nchini baada ya Krisimasi kuja kuanza kazi.
“Atakuja nchini baada ya krisimasi, kila kitu safi akifika anasaini mkataba na kuanza kazi,”alisema Mtawala.
Liewig ana Stashahada ya Juu ya ukocha na Shahada ya tatu ya ualimu wa soka ya vijana aliyotunukiwa na Mkurugenzi wa Ufundi wa Ufaransa, Gerard Houiller na amehudhuria pia kozi za ufundishaji mazoezi ya viungo Juni mwaka 1999 katika Chuo Kikuu cha Dijon.
Kwa upande wa uzoefu, Liewig alifanya kazi PSG kuanzia mwaka 1989 hadi 1999 kama Kocha Mkuu wa akademi na kuna wakati alikuwa akishirikishwa pia katika programu za timu A, ingawa majukumu yake zaidi yalikuwa ni kwa Under 20, Under 18 aliowawezesha kutwaa Kombe la French Junior Gambardella na Under 16.
Kuanzia mwaka 1989 hadi 1990:  alikuwa Meneja Mkuu wa Tomislav IVIC, 1990 hadi 1991 alikuwa Msaidizi wa Henri Michel, 1991 hadi 1994 alikuwa Msaidizi wa Artur Jorge, 1994 hadi 1996 alikuwa Msaidizi wa Luis Fernandez, 1996 hadi 1998: alikuwa Msaidizi wa Ricardo Gomez, 1998 hadi 1999 alikuwa Msaidizi wa Alain Giresse.
Liewig pia alifundisha Al Wahda FC ya Abu Dhabi kuanzia 1999 hadi 2001, ambayo aliipa ubingwa wa Ligi Kuu ya nchi hiyo na Kombe la Ligi.
Januari mwaka 2003 alikuwa Msimamizi wa Chama cha Soka UAE katika fainali za Afrika za U20 nchini Burkina Faso.
Kuanzia mwaka 2004 hadi 2009 alikuwa Kocha wa ASEC Mimosas ya Ivory Coast aliyoipa mataji matatu ya Ligi Kuu ya nchini humo mfululizo, 2004, 2005 na 2006, Super Cup ya nchini humo 2005, 2007, 2008 na 2009 na akaiwezesha kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa mara tatu, mara moja akiifikisha Nusu Fainali.
Amekuwa Kocha bora wa Ivory Coast miaka mitatu mfululizo, 2004, 2005 na 2006 na tangu Septemba mwaka jana hadi Juni mwaka huu, alikuwa kocha wa Club Africain ya Tunisia

UGANDA ONE KULIPWA MILIONI 2 KWA MWEZI SIMBA SC, AAHIDI SHANGWE MSIMBAZI

Dhaira kulia akiwa na Hans Poppe baada ya kusaini miaka miwili Simba SC 
KIPA namba moja wa Uganda, Abbel Dhaira mbali na kusaini mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya dola za Kimarekani 40,000, pia atakuwa akipokea mshahara wa Sh. Mlioni 2 kwa mwezi.
Dhaira alisaini mkataba jana katika hoteli ya JB Belmonte, Dar es Salaam mbele ya Katibu wa Simba, Evodius Mtawala na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo, Zacharia Hans Poppe.
Akizungumza  jana, baada ya kumsajili kipa huyo, Hans Poppe alisema kwamba huyu ni kipa wa kwanza mwenye umbo kubwa tangu, kumalizika kwa zama za Mwameja Mohamed katika klabu hiyo.
“Naamini tumepata mtu sahihi na katika wakati mwafaka, hakuna asiyejua umahiri wa Dhaira langoni, sasa tunasubiri kuvuna matunda ya kumsajili,”alisema Hans Poppe, Kapteni wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania(JWTZ), ambaye leo anapanda ndege kwenda Uingereza kwa mapumziko ya Krisimasi na mwaka mpya.
Hans Poppe aliyepigana vita dhidi ya Uganda, alisema kwamba Dhaira ni kipa ambaye amependekezwa na kipa wao wa kwanza hivi sasa, Juma Kaseja hivyo anaamini wawili hao wataishi vizuri na kushirikiana.
Kwa upande wake, Dhaira ambaye anarejea leo kwao Uganda kwenda kuchukua vifaa vyake vya kazi kwa ajili ya kuja kuanza kumtumikia mwajiri wake mpya, alisema kwamba amefurahi kusaini Simba SC na atafanya vizuri ili kuwafurahisha mashabiki wa klabu hiyo.
“Simba ni klabu kubwa Afrika na inacheza Ligi ya Mabingwa Afrika, kuna wachezaji rafiki zangu na ndugu zangu, Mussa Mudde na Emmanuel Okwi, lakini Afrika Mashariki ni moja, wachezaji wote wa Simba ni ndugu zangu, nitajisikia nipo nyumbani kabisa”alisema Dhaira, anayetua Simba akitokea I.B.V FC ya Iceland.
Dhaira aliyeibukia Express ya Uganda mwaka 2006, mwaka 2008 alihamia U.R.A. pia ya Uganda, ambayo aliichezea hadi mwaka 2010 alipohamia Ulaya.
Kwa kumpata Dhaira, Simba SC imepata kipa wa uhakika wa kusaidiana na kipa wake wa kwanza, Juma Kaseja ambaye amekuwa akisoteshwa peke yake bila kupumzika. Na hiyo inafuatia makipa wengine, Wilbert Mweta na Hamadi Waziri kushindwa kuonyesha uwezo wa kumsaidia Kaseja.
Katika mechi za mwishoni za mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Kaseja alionekana kuchoka na kudaka chini ya kiwango chake, jambo ambalo lilisababisha mashabiki wenye ‘akili mbovu’ wamfanyie fujo baada ya kufungwa mabao mawili katika mechi dhidi ya Mtibwa Sugar, Simba ikilala 2-0.
Kwa sababu hiyo, Kaseja alikasirika na kujiengua kwenye kikosi cha timu hiyo akisema hataki tena kuchezea Simba.
Lakini pamoja na matatizo hayo, Kaseja aliitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ambako ameendelea kufanya vizuri na kuonyesha yeye ni Tanzania One wa ukweli.  

UGANDA ONE ALIVYOMWAGA WINO SIMBA SC LEO

Kulia, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe akizungumza na kipa namba moja wa Uganda, Abbel Dhaira kushoto. Mwingine Katibu wa Simba SC, Evodius Mtawala wakati kipa huyo alipokuwa akisaini mkataba wa  miaka miwili kuichezea Simba SC usiku huu katika hoteli ya JB Belmonte, katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Kulia, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe na kushoto ni wakala wa kipa namba moja wa Uganda, Abbel Dhaira kushoto akihesabu dola za Kimarekani alizolipwa kipa huyo kusaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba SC

K
Kipa namba moja wa Uganda, Abbel Dhaira akisaini mkataba mbele ya Katibu wa Simba SC, Evodius Mtawala .

Wakala wa Dhaira akihesabu mpunga

Dhaira anatia dole gumba

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe kushoto akiwa na kipa namba moja wa Uganda, Abbel Dhaira wakati akisaini mkataba wa  miaka miwili kuichezea Simba SC. 
Tazama mlingoti huo, Dhaira kulia akiwa na Hans Poppe

ZANTEL YAPIGA TAFU MKUTANO MKUU WA TASWA UTAKAOFANYIKA BAGAMOYO

Kampuni ya simu za mkononi Zantel leo imekipiga tafu chama cha waandishi wa habari za michezo kwa kuipatia shilingi milioni sita na elfu arobaini.

Akizungumza kwenye hafla hiyo iliyofanyika kwenye mgahawa wa sports lounge Mkurugenzi wa Corporete Solutions, Ahmed Mohamed alisema wanafurahi kurudisha fadhila kwa jamii kwa kugawana nao faida wanayoipata.

Naye Mkiti wa TASWA Juma Pinto aliishukuru Zantel kwa kuwa sehemu ya mkutano huo kwa kuwashika mkuno kwani mahitaji ya mkutano huo ni zaidi ya milioni 20.
Corporate Solutions Director Ahmed S. Mohamed akimkabidhi M/Kiti wa TASWA mfano wa hundi ambayo ni sehemu ya mchango wa Zantel waliochangia kufanikisha mkutano mkuu wa TASWA utakaofanyika Desemba mwaka huu, Bagamoyo mkoani Pwani



DEOGRATIAS MUNISHI AREJESHWA STARS KUZIBA NAFASI YA MWADINI ALLY AMBAYE ATAKUWA NJE YA NCHI


  Timu ya Taifa (Taifa Stars) imeingia kambini jana jioni  jijini Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya mabingwa wa Afrika, Zambia (Chipolopolo) huku Kocha Kim Poulsen akimjumuisha tena katika kikosi hicho kipa Deogratias Munishi ‘Dida’.
Kocha Poulsen amemjumuisha tena Munishi kwenye kikosi hicho kuziba nafasi ya Mwadini Ally ambaye atakuwa nje ya nchi na timu yake ya Azam inayokwenda kushiriki mashindano maalumu nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Wachezaji wote wengine walioitwa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager wamesharipoti kambini hoteli ya Tansoma, na timu imeanza mazoezi leo asubuhi (Desemba 13 mwaka huu) Uwanja wa Karume, na jioni itafanya mazoezi kwenye uwanja huo huo.
Kuanzia kesho jioni (Desemba 14 mwaka huu) itafanya mazoezi Uwanja wa Uwanja wa Taifa wakati mazoezi ya asubuhi yataendelea kuwa Uwanja wa Karume. Wachezaji ambao bado hawajaripoti kambini ni Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaocheza mpira wa kulipwa nchini DRC.
Mechi kati ya Taifa Stars na mabingwa hao wa Afrika itachezwa Desemba 22 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa. Kocha wa Chipolopolo, Herve Renard ameshataja kikosi chake cha wachezaji 24 kwa ajili ya mechi hiyo.

UCHAGUZI TWFA KUFANYIKA MOROGORO DESEMBA 19

Uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu kwa Wanawake Tanzania (TWFA) unatarajia kufanyika Desemba 19 mwaka huu mjini Morogoro.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TWFA, Ombeni Zavala, uchaguzi huo utatanguliwa na Mkutano Mkuu wa TWFA. Wajumbe wapiga kura wote wa mikoa iliyofanya uchaguzi wake na kutoa taarifa za uchaguzi wao ofisi za TWFA wanatakiwa kufika Morogoro siku moja kabla (Desemba 18 mwaka huu).
Wagombea waliopitishwa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ni kama ifuatavyo; wanaowania uenyekiti ni Isabela Kapera, Joan Minja na Lina Kessy. Rose Kissiwa ni mgombea pekee wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti.
Wanaowania ukatibu mkuu ni Amina Karuma na Cecilia Mkafu. Nafasi ya mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inagombewa na Zena Chande pekee baada ya Furaha Francis kujitoa kutokana na sababu za kifamilia.
Sophia Charles na Triphonia Temba wanawania nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya chama hicho.
Wagombea Rahim Maguza, Macky Mhango na Rose Msamila wameondolewa kwa kushindwa kikidhi matakwa ya Katiba ya TWFA Ibara ya 28(2).

WACHEZAJI STARS WAWASILI KAMBINI KWA MAFUNGU


Wachezaji waliowasili kambini mpaka sasa ni walinda mlango Juma Kaseja, Mwadin Alli na Aishi Manua.

Walinzi waliofika ni Shomari Kapombe,  Samir Nuhu, Erasto Nyoni, Issa Rashidi, Aggrey Moris na Amir Maftaha. Nadir Haroub 'Kanavaro'  na Kelvin Yondani na Nassoro Masudi Cholo bado hawajafika ila Cholo ni mgonjwa.

Viungo waliowasili ni Frank Domayo, Salum 'Abubakar sureboy', Athumani Iddi 'Chuji', Amri Kiemba na Hamisi Mcha Hamisi. Shabani Nditi, Mrisho Ngasa na  Mbwana Samatta bado hawajafika

Washambuliaji ni John Bocco, Simon Msuva na Mwinyi Kazimoto. Thomas Ulimwengu naye bado hajafika.

Baada ya mchezo dhidi ya Zambia tarehe 22/ 12/ 2012, timu hiyo itarejea tena kambini Januari 6 mpaka 20 ikiwa na wachejaji 18 kwa ajili ya michezo ya kujipima nguvu na timu tatu ambazo kocha Kim Poulsen ametaka atafutiwe timu zitakazo shiriki michuano ya wachezaji wa ndani ( CHAN )

Stars inakabiliwa na michezo kadhaa ya kuwania kucheza kombe la dunia ambapo mwezi March itakuwa na kibaru cha awali dhidi ya Morocco kabla ya mchezo wa marudiano utakaochezwa mwezi June.

Mwezi huo huo itakuwa na mchezo mwingine dhidi ya Ivory Coast kuwania kucheza kombe la dunia lakini pia kutakuwa na mchezo mwingine dhidi ya Uganda wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika UGANDA

SIMBA YAANZA VEMA KUTETEA KOMBE LA MASHINDANO YA UHAI, COASTAL UNION NAYO USIPIME



TIMU ya Simba B leo imeanza vema kutetea kombe la  mashindano ya uhai kwa kuifunga African Lyon mabao 2-1 kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Karume asubuhi.

Mashindano haya yamedhaminiwa na kampuni ya Bharessa kupitia bidhaa yake ya maji ya uhai alianza juzi na yanachezwa kwenye viwanja vya Karume na Chamazi.

Mchezo huo wa kundi B ulikuwa wa ushindani na kila timu ilikuwa ikifanya mashambulizi kwa zamu.

Simba ndio ilikuwa ya kwanza baada ya kufunga bao la kwanza dakika ya 15 kupitia kwa Miraji Athuman na la pili lilifungwa na Ramadhan Mzee dakika ya 42.

Bao la African Lyon lilifungwa na Ndela Kashakala dakika ya 50.

Baada ya mchezo kumalizika makocha wa timu zote walilalamikia maamuzi ya waamuzi kuwa yalikuwa na walakini pia kocha wa Simba alisema kuwa anashukuru kwani timu yake ilikuwa haijafanya mazoezi.




Mchezo wa jioni Coastal Union waliifunga Azam FC bao  1-0, bao lililofungwa dakika ya 80 na Benja Ngasa baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Azam

Kwenye michezo wa juzi, Mtibwa ambao walicheza jioni kwenye uwanja wa Karume waliifunga JKT Ruvu bao 3-1.

Mabao ya Mtibwa yalifungwa na Hillary Kapera dakika ya 22, Godfrey Mohamed dakika ya 50 na Richard Jacob dakika ya 89 kwa njia ya penalti.

Bao pekee la JKT Ruvu ambao ndio walikuwa wa kwanza kufunga lilitiwa kimiani na Richard Msenye dakika ya 20.

Timu ya Coastal Union ilishida bao 2-1 dhidi ya Tanzania Prison kwenye mchezo uliochezwa juzi asubuhi kwenye uwanja wa Karume.

Mabao ya Coastal Union yalifungwa na Ramadhan Shame dakika ya 24 na Yusuf Chuma dakika ya 33.

KING CLASS MAWE APEREKA SHANGWE KAMBI YA ILALA BAADA YA KUMTWANGA BONDIA WA TANGA



Bondia Said Mundi wa Tanga akipambana na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati walipokutana katika mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Class alishinda kwa point na kupeleka Shangwe katika Kambi ya Ilala Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto akipambana na Said Mundi wa Tanga wakati wa mpambano wao uliofanyika hivi karibuni King Class alishinda kwa point na kupeleka Shangwe katika Kambi ya Ilala Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila Super D wa pili kushoto akiwa na furaha baada ya kumpandisha bondia  Ibrahimu Class 'King Class Mawe' ulingoni na kumtwanga Said Mundi wa Tanga Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Masabiki wa ngumi wakiwa na Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' na Kocha wake Rajabu Mhamila 'Super D
Bondia Said Mundi wa Tanga akipambana na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati walipokutana katika mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Class alishinda kwa point na kupeleka Shangwe katika Kambi ya Ilala Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Mashabiki wakimpa Ongera Bondia Ibrahimu Class

Bondia King Class Mawe akiwa na wapambe wake baada ya kumdunda said Mundi wa Tanga

MBIO ZA SERENGETI MARATHON 2012 ZAFANA MKOANI SIMIYU

Mshindi wa kwanza wa Serengeti marathon 2012 Dickson Marwa kutoka mkoani Mara, akihitimisha ukimbiaji mbio za nyika mita 21 zilizofanyika jana kwenye mbuga za Serengeti mkoani Simiyu.
Mashindano hato ya kwanza yamevuka malengo kutoka washiriki 80 waliojiandikisha awali hadi kufikia washiriki 207 waliojitokeza mapema asubuhi kabla ya mbio hizo kuanza kutimua vumbi.
Big up sana kwa Mshiriki mwenye ulemavu wa mkono mmoja Edward Joseph aliyemaliza mbio hizo kwa upande wa wanaume akiwa nafasi ya 14.
Mshindi wa kwanza wa Serengeti marathon 2012 Dickson Marwa kutoka mkoani Mara akiwa ameshikilia medali yake ya dhahabu na fedha kiasi cha shilingi laki 5 alichonyakuwa kwenye mbio za kwanza za nyika za Serengeti Marathon.
Hawa ndiyo washindi kumi wa kumi bora upande wa wanaume ukimbiaji mbio za nyika mita 21 zilizofanyika jana kwenye mbuga za Serengeti mkoani Simiyu, mbele ni mshindi wa kumi akifuatia wa tisa hadi wa kwanza nyuma, wakiwa kwenye mstari kwaajili ya kutunukishwa zawadi zao.
Wakuu mbalimbali waliohudhuria michuano ya kwanza ya Serengeti Marathon.
Mshindi wa kwanza wanawake katika Serengeti marathon 2012 Failuna Mohamed kutoka mkoani Arumeru akiwa ameshikilia medali yake ya dhahabu na fedha kiasi cha shilingi laki 5 alichonyakuwa kwenye mbio za kwanza za nyika za Serengeti Marathon.
Maafisa wanyamapori kutoka mbuga ya hifadhi ya taifa ya Serengeti wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri wakati wa utoaji wa zawadi kwa watimua vumbi wa mbio hizo, hawa ndio waliosimamia zoezi la kuhakikisha barabara ni salama kwa wakimbiaji  ili wasishambuliwe na wanyama wakali.

Dr. Mtiro akitoa Huduma ya Kwanza kwa moja ya washiriki wa mbio hizo mara baada ya kumalizika kwa mashindano. 
Vitita na Medali mezani kabla ya kumilikishwa kwa washindi....
Serebuka ya wafukuza upepo.
Mkuu wa wilaya ya Busega Paul Mzindakaya (katikati) akipata picha ya pamoja na washindi watatu watatu kutoka kwa kila pande, Kutoka kushoto ni Ndege Stephen (Nyamagana Mwanza) aliyeshika No. 3, Said Makula (Arumeru ) aliyeshika No. 2 na Dickson Marwa (Mara) mshindi nafasi ya kwanza, Upande wa pili baada ya mweshimiwa ni mwanadada Failuna Mohamed (Arumeru) aliyeshika nafasi ya kwanza wanawake, Grace Jackson (Bariadi mkoani Simiyu) No. 2 na Neema Mathius (Magu mkoani Mwanza)

KLABU BINGWA DUNIANI: CHELSEA KUIGA MAN UNITED KUWA BINGWA DUNIANI?


>>BENITEZ: “NI MASHINDANO MAKUBWA!”
>>BENITEZ KUIPA UBINGWA TIMU ‘ILIYOUNDWA’ na DI MATTEO??
>>2010 BENITEZ ALIIPA INTER UBINGWA ‘TIMU ya MOURINHO’!!
+++++++++++++++++++++
RATIBA:
Alhamisi, Desemba 13
[Saa 7 na Nusu Mchana]
International Stadium, Yokohama, Japan
Monterrey v Chelsea
+++++++++++++++++++++
LEO Chelsea wanaanza Mashindano ya FIFA kusaka Klabu Bingwa Duniani kwenye hatua ya Nusu Fainali na wanapambana na Monterrey ya Mexico ambayo imefika hatua hiyo baada ya kuitoa Usain Hyundai ya Korea Kusini Bao 3-1 kwenye Robo Fainali.
+++++++++++++++++++++
MABINGWA WALIOPITA:
-2000 - Corinthians
-2005 - Sao Paulo
-2006 - Internacional
-2007 - AC Milan
-2008 - Manchester United
-2009 - Barcelona
-2010 - Inter Milan
-2011 – Barcelona
++++++++++++++++++
FIFA_CLUB_WORLD_CUPAkiizungumzia Mechi hii, Meneja wa Chelsea, Rafael Benitez, amesema Klabu Bingwa Duniani ni Mashindano makubwa sana kwao.
Benitez, ambae alitua Chelsea kumrithi Roberto Di Matteo aliefukuzwa, na kupokelewa kwa kupingwa mno na Mashabiki, alianza himaya yake hapo Stamford Bridge kwa kutoshinda katika Mechi 3 za mwanzo lakini Wiki iliyopita alipata ushindi katika Mechi mbili mfululizo kwa kuitandika Nordjaelland ya Denmark Bao 6-1 kweye UEFA CHAMPIONZ LIGI ambayo hata hivyo wametupwa nje na kisha kuifunga Sunderland Bao 3-1 kwenye Ligi Kuu England Jumamosi iliyopita.
Hii ni mara ya 3 kwa Benitez kushiriki kwenye Klabu Bingwa Duniani na mara ya kwanza ilikuwa 2005 alipoiongoza Liverpool, Timu aliyoiunda mwenyewe, lakini wakashindwa baada ya kufungwa na Sao Paolo ya Brazil na Mwaka 2010 aliiongoza Inter Milan, iliyoundwa na Jose Mourinho, na kufanikiwa kutwaa Ubingwa wa Dunia.
Safari hii, Benitez anaiongoza Timu iliyoundwa na Roberto Di Matteo na swali toka kwa Wadau ni: Je atafanikiwa kuiiga Manchester United na kuifanya Chelsea iwe Klabu ya Pili England kuwa Bingwa wa Dunia?
++++++++++++++++++
KLABU BINGWA DUNIANI 2012
TIMU ZITAKAZOSHIRIKI:
Chelsea-BINGWA ULAYA
Corinthians-BINGWA MAREKANI ya KUSINI
Monterrey-BINGWA MAREKANI ya KATI NA KASKAZINI
Auckland City-BINGWA KANDA ya OCEANIA
Usain Hyundai-BINGWA-Barani Asia
Al Ahly-BINGWA-Barani Afrika
Sanfrecce Hiroshima-BINGWA-Japan J-LIGI
RATIBA/MATOKEO:
Raundi ya Mchujo - Desemba 6, Yokohama
Sanfrecce Hiroshima 1 Auckland City 0
ROBO FAINALI - Desembar 9, Toyota
Usain Hyundai 1 Monterrey 3
Sanfrecce Hiroshima 1 Al Ahly 2
MSHINDI wa 5- Desemba 12, Toyota
[Saa 4 na Nusu Asubuhi]
Usain Hyundai 2 Sanfrecce Hiroshima 3
NUSU FAINALI
Desemba 12, Toyota
[Saa 7 na Nusu Mchana]
Al Ahly 0 Corinthians 1
Desemba 13, Yokohama
[Saa 7 na Nusu Mchana]
Monterrey v Chelsea
MSHINDI wa 3
Desemba 16
[Uwanja wa Yokohama]
[Saa 4 na Nusu Asubuhi]
Al Ahly v Chelsea/Monterrey
FAINALI
[Saa 7 na Nusu Mchana]
Corinthians v Chelsea/Monterrey

CAPITAL ONE CUP: Nayo Swansea ipo Nusu Fainali, yaitoa Boro!


>>ROBO FAINALI ILIYOBAKI: LEEDS V CHELSEA
>>TAYARI NUSU FAINALI: VILLA, BRADFORD & SWANSEA CITY!!
>>DROO ya NUSU FAINALI KUFANYIKA DESEMBA 19!!
CAPITAL_ONE_CUP-BESTSwansea City jana wametinga Nusu Fainali ya CAPITAL ONE CUP, hii ikiwa ni mara yao kwanza katika Historia yao kufika hatua hii ya Kombe la Ligi, baada ya kuitungua Middlesbrough Bao 1-0 kwa goli ambalo Boro walijifunga wenyewe.
Middlesbrough walitawala sehemu kubwa ya Mechi hii lakini Kona ya Dakika ya 81 iliunganishwa kwa kichwa na Seb Hines na kujifunga mwenyewe na kuwapa Swansea City ushindi wa Bao 1-0.
+++++++++++++++++++++++++
CAPITAL ONE CUP-Robo Fainali:
RATIBA/MATOKEO:
Jumanne Desemba 11
Norwich 1 Aston Villa 4
Bradford 1 Arsenal 1 [Bradford yasonga Penati 3-2]
Jumatano Desemba 12
Swansea 1 Middlesbrough 0
Jumatano Desemba 19
[Saa 4 Dak 45 Usiku]
Leeds United v Chelsea
+++++++++++++++++++++++++
Timu nyingine ambazo tayari zipo Nusu Fainali ni Aston Villa na Bradford ambao watajumuika na Mshindi wa Mechi ya Robo Fainali ya mwisho kati ya Leeds United na Chelsea itakayochezwa Desemba 19.
DROO ya kupanga Mechi za Nusu Fainali itafanyika Desemba 19.
+++++++++++++++++++++++++
DONDOO MUHIMU za CAPITAL ONE CUP:
-KABLA LILIKUWA ni Carling Cup na Bingwa Mtetezi alikuwa ni Liverpool.
-Linaitwa CAPITAL ONE CUP kwa sababu Mdhamini wake ni Kampuni ya masuala ya Fedha, Capital One.
-Linashirikisha Timu za Ligi za juu England 92 kwa mtindo wa Mtoano [Timu 20 toka Ligi Kuu na 24 kila moja kutoka Madaraja ya Npower, Ligi 1 na 2.
-FAINALI itafanyika Uwanja wa Wembley Tarehe 24 Februari 2013
-Bingwa wa michuano hii hucheza EUROPA LIGI Msimu unaofuata kuanzia Raundi ya Tatu ya Mtoano.

No comments:

Post a Comment