Wednesday, January 16, 2013

GUARDIOLA KOCHA MPYA BAYERN MUNICH



Pep Guardiola - Ballon d'Or press conference
Getty
Pep Guardiola will take over from Jupp Heynckes as Bayern Munich coach at the end of the season.
BET:                                                                                                   RETURNS:Bayern £10.80Draw £100.00Greuther Furth £260.00WilliamHill

The 41-year-old former Barca boss left Camp Nou in 2012 having won 14 trophies with the Liga side during his four seasons in charge and has signed a deal with the Bundesliga club until 2016.

Guardiola, who has signed a three-year deal with the German side, had been linked with a hot of top-flight clubs across Europe, but Bayern CEO Karl-Heinz Rummenigge said in a statement he was delighted to have captured the Spaniard.

"We are very happy that we managed to land the expert Pep Guardiola for our club. He was contacted by lots of big clubs," Rummenigge said.

"Pep is one of the most succesful coaches in the world and we are convoinced, that he will not only shine for Bayern but for the whole of German football. We look forward to our common work from July 2013 on.“

Heynckes, who has been in charge of the German side since 2011, told De Roten officials that he would not be continuing in his role before Christmas.

And Rummenigge praised the outgoing Bayern boss, adding that securing the Bundesliga title would be a fitting send off for Heynckes.

"As a club and as Jupp Heynckes' friends we have to show understanding for this decision. We have to accept it and we have to respect it," he said.

"During personal talks with Jupp Heynckes we assured each other that we will do anything we can, and now even more, to have a successful second half of the season 2012/13 where we want to get the title to Munich.“

Bayern currently lie top of the Bundesliga, nine points clear of second-placed Bayer Leverkusen.

KUMEKUCHA KATIKA KOMBE LA MATAIFA AFCON 2013: UFUNGUZI Jumamosi-Afrika Afrika v Cape Verde


AFCON_2013_LOGO>>TATHMINI YA KUNDI kwa KUNDI!
Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2013, yanaanza huko Nchini Afrika Kusini Jumamosi Januari 19 kwa Mechi ya ufunguzi ya Kundi A kati ya Wenyeji Afrika Kusini na Cape Verde kwenye Uwanja wa Taifa Mjini Johannesburg.
IFUATAYO NI TATHMINI YA KILA KUNDI:
**FAHAMU: KILA KUNDI LITATOA TIMU 2 KUTINGA ROBO FAINALI.
KUNDI A:
-Afrika Kusini
-Cape Verde
-Morocco
-Angola

Wenyeji Afrika Kusini, wakishiriki Fainali zao za 8, wametwaa Ubingwa wa Afrika mara moja tu pale Mwaka 1996 walipokuwa pia Wenyeji wa Fainali hizo ambako kwenye Fainali yenyewe waliyotwaa Ubingwa waliichapa Tunisia Bao 2-0 Bao zote zikifungwa na Mark Williams ambae aliwahi kuichezea Wolverhampton Wanderers ya England.
Safari hii, Afrika Kusini, maarufu kama Bafana Bafana, watacheza bila ya Staa wa Everton Stephen Pienaar ambae alistaafu kuichezea Nchi yake Miezi mitatu iliyopita.
Katika Kundi hili, mpinzani mkubwa wa Bafana Bafana anaonekana kuwa Morocco ambao walikuwa Washindi wa Pili wa AFCON 2004 na ambao chini ya Kocha Rachid Taoussi wanaonekana kuimarika huku Uwanjani wakiwategemea Maprofeshenali kadhaa wanaocheza Klabu kubwa Ulaya wakiwemo Karim El Ahmadi wa Aston Villa, Beki wa Udinese Mehdi Benatia na Mchezaji wa Fiorentina, Mounir El Hamadaoui.
Cape Verde, Timu changa inayoshiriki Fainali zao za kwanza kwa kuwabwaga Vigogo Cameroun 3-2 kwenye mchujo, wana Wachezaji kadhaa wanaocheza huko Ureno lakini tegemezi kubwa ni Winga Ryan Mendes, Miaka 22, ambae alifunga Bao 3 kwenye Mechi za Mchujo za AFCON 2013 na ambae aling’ara huko Ufaransa na Klabu ya Le Havre na kuzolewa na Klabu kubwa Lille Mwaka 2012.
Timu ya 4 ya Kundi A ni Angola ambao mara mbili wametinga Robo Fainali za AFCON na kuishia hapo na mashine yao ya Magoli ni Straika wa zamani wa Manchester United, Manucho, ambae ana rekodi ya kufunga Bao 21 kwa Mechi 38 za Angola.
Manucho anazo Bao 6 kwa Klabu yake ya sasa ya Spain, Real Valladolid, zikiwamo Bao 2 alizoipiga Real Madrid walipokutana Mwezi uliopita.
KUNDI B:
-Ghana
-DR Congo
-Niger
-Mali

Bila shaka Ghana, moja ya Timu inayopewa nafasi kubwa kutwaa AFCON 2013, ndio wanaopewa nafasi kubwa kuwa Nambari Wani kwenye Kundi hili na wamesheheni Majina makubwa kama kina Asamoah Gyan, John Pantsil na John Mensah lakini pia watawakosa Mastaa wengine, kina Michael Essien, Sulley Muntari na Andre Ayew, ambao wamefyekwa toka Kikosini na Kocha James Kwesi Appiah.
Mali na Congo DR ndizo zinazotegemewa kuchuana ili kupata nafasi moja kuungana na Ghana kwenye Robo Fainali na zote zina Mastaa maarufu huku Mali ikiwa nao Modibo Maiga wa West Ham na Samba Diakite wa QPR lakini watamkosa Nahodha wao wa zamani Mahamadou Diarra anaechezea Fulham kwa kuumia.
Hata hivyo, Mali wanae tena Mchezaji Momo Sissoko, aliewahi kuichezea Liverpool na sasa yuko Juventus, baada ya kutoichezea Mali kwa Miaka miwili.
Congo DR nao wana Mastaa wao lakini atakaebeba jahazi ni Nahodha Tresor Mputu ambae aliwahi kufungiwa Miezi 12 wakati akiechezea Congo kwa kumpiga Refa.
Niger ni Timu ya 4 kwenye Kundi hili na hii ni Fainali yao ya pili kucheza baada ya AFCON 2012 ambayo hawakuvuka hatua ya Makundi na safari hii tena wanakadiriwa kufanya hivyo hivyo.
KUNDI C:
-Zambia
-Ethiopia
-Nigeria
-Burkina Faso

Kimaandishi, Nigeria wanaonekana kuwa juu kwenye Kundi hili lakini ukweli ni kuwa Kundi hili liko wazi na yeyote ana nafasi ya kusonga.
Nigeria wametinga Fainali za AFCON mara 6 lakini wamechukua Ubingwa mara mbili tu na baada ya kuzikosa AFCON 2012 Nchi hiyo ilimteua Mchezaji wao wa zamani, Stephen Keshi kuwa Kocha.
Keshi ameteua Kikosi mchanganyiko cha Vijana wanaocheza Soka nyumbani na Maprofeshenali kama kina John Mikel Obi na Victor Moses wa Chelsea na Beki wa zamani wa Everton, Joseph Yobo.
Zambia ndio Mabingwa watetezi wa Afrika baada ya kutwaa Taji la AFCON 2012 kwa kuichapa Timu kali Ivory Coast kwa Mikwaju ya Penati 8-7 huko Nchini Gabon na pia wametinga Fainali hizi za AFCON 2013 kwa Mikwaju ya Penati walipoitoa Uganda katika Mechi ya mwisho ya Mchujo.
Tegemezi la Zambia ni pamoja na Mchezaji wa Southampton, Emmanuel Mayuka, Miaka 21, ambae ameichezea Klabu hiyo ya England Mechi 8, 6 akitokea Benchi.
Timu nyingine za Kundi hili ni Ethiopia na Burkina Faso lakini Ethiopia washawahi kuwa Mabingwa wa Afrika mara moja walipotwaa Taji Mwaka 1962 na safari hii Penati ya Dakika ya mwisho ya Mchezaji Adane Girma kwenye Mechi ya mwisho ya Mchujo na Benin ndio imewaingiza Fainali za AFCON 2013.
Matokeo mazuri kwa Burkina Faso kwenye Mashindano haya ya Afrika ni kukamata nafasi ya 4 kwenye Fainali za Mwaka 1998.
KUNDI D
-Ivory Coast
-Togo
-Tunisia
-Algeria

Wanasema hili ndio ‘Kundi la Kifo!’
Lakini Timu ngumu Ivory Coast, iliyosheheni Masupastaa wa kila aina, watataka kufanya vyema kupita AFCON 2012 ambako walitolewa kwenye Fainali na Zambia kwa Matuta 8-7 na safari hii kutwaa Ubingwa wa Afrika kwa mara ya Pili katika historia yao.
Macho yote yatakuwa kwa Supa Straika Didier Drogba, ambae licha ya mafanikio yake makubwa kwenye anga la Soka, hajawahi kutwaa Ubingwa wa Afrika.
Togo wanatinga kwenye AFCON 2013 wakiwa na habari njema baada ya Nahodha wao Emmanuel Adebayor kufuta msimamo wa kususa kuichezea Nchi yake baada ya Rais wa Nchi hiyo kufanya mazungumzo nae.
Wengine kwenye Kundi hili gumu ni Algeria na Tunisia ambao kila mmoja ashawahi kuwa Bingwa wa Afrika mara moja na Timu zote zina Wachezaji kadhaa ambao wako Ulaya.
Algeria wanatawategemea Kiungo wa Valencia Sofiane Feghouli, Winga wa zamani wa Fulham na Watford, Hamed Bouazza na Staa wa Nottingham Forest, Guedioura.
Nae Kocha wa Tunisia, Sami Trabelsi, licha ya kuwa na Mastaa kadhaa, inaelekea amejitia kitanzi mwenyewe baada ya kumtema Nyota Kiungo Nyota wa Atletico Madrid Kader Oueslati na hili huenda likamfanya atimuliwe ikiwa hatafanikiwa kwani Tunisia, ndani ya Miaka minne, washabadilisha Makocha mara 7.

RATIBA:
[SAA za BONGO]
Jumamosi Januari 19
South Africa v Cape Verde Islands [Soccer City Saa 1 Usiku]
Angola v Morocco [Soccer City Saa 4 Usiku]
Jumapili Januari 20
Ghana v Congo DR [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 12 Jioni]
Mali v Niger Nelson [Mandela Bay Stadium Saa 3 Usiku]
Jumatatu Januari 21
Zambia v Ethiopia [Mbombela Stadium Saa 12 Jioni]
Nigeria v Burkina Faso [Mbombela Stadium Saa 3 Usiku]
Jumanne Januari 22
Ivory Coast v Togo [Royal Bafokeng Stadium Saa 12 Jioni]
Tunisia v Algeria [Royal Bafokeng Stadium Saa 3 Usiku]
Jumatano Januari 23
South Africa v Angola [Moses Mabhida Stadium Saa 12 Jioni]
Morocco v Cape Verde Islands [Moses Mabhida Stadium Saa 3 Usiku]
Alhamisi Januari 24
Ghana v Mali [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 12 Jioni]
Niger v Congo DR [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 3 Usiku]
Ijumaa Januari 25
Zambia v Nigeria [Mbombela Stadium Saa 12 Jioni]
Burkina Faso v Ethiopia [Mbombela Stadium Saa 3 Usiku]
Jumamosi Januari 26
Ivory Coast v Tunisia [Royal Bafokeng Stadium Saa 12 Jioni]
Algeria v Togo [Royal Bafokeng Stadium Saa 3 Usiku]
Jumapili Januari 27
Morocco v South Africa [Moses Mabhida Stadium Saa 2 Usiku]
Cape Verde Islands v Angola [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 2 Usiku]
Jumatatu Januari 28
Congo DR v Mali [Moses Mabhida Stadium Saa 2 Usiku]
Niger v Ghana [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 2 Usiku]
Jumanne Januari 29
Ethiopia v Nigeria [Royal Bafokeng Stadium Saa 2 Usiku]
Burkina Faso v Zambia [Mbombela Stadium Saa 2 Usiku]
Jumatano Januari 30
Algeria v Ivory Coast [Royal Bafokeng Stadium Saa 2 Usiku]
Togo v Tunisia [Mbombela Stadium Saa 2 Usiku]
ROBO FAINALI
Jumamosi Februari 2
Mshindi Kundi B v Mshindi wa Pili Kundi A [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 12 Jioni]
Mshindi Kundi A v Mshindi wa Pili Kundi B [Moses Mabhida Stadium Saa 3 na Nusu Usiku]
Jumapili Februari 3
Mshindi Kundi D v Mshindi wa Pili Kundi C [Royal Bafokeng Stadium Saa 12 Jioni]
Mshindi Kundi C v Mshindi wa Pili Kundi D [Mbombela Stadium Saa 3 na Nusu Usiku]
NUSU FAINALI
Jumatano Februari 6
Mshindi RF 3 v Mshindi RF 2 [Mbombela Stadium Saa 12 Jioni]
Mshindi RF 1 v Mshindi RF 4 [Moses Mabhida Stadium Saa 3 na Nusu Usiku]
MSHINDI wa TATU
Jumamosi Februari 9
[Nelson Mandela Bay Stadium Saa 3 Usiku]
FAINALI
Jumapili Februari 10
[Soccer City Saa 3 Usiku]

KIKAPU YAPATA KOCHA MSAIDIZI WA TIMU YA TAIFA JOCQUIS SCONIERS

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiZxCdDa0_cJ6PVmfn3CjEkzNRnnK1t5jRPLkVh5LIBe2zxRKwMnojdWmgHorhuzIinkPY4BNV_66uRkAHsFutx30wUBsmTq0Tjekz6tNDApb3U5bpM127mCtmWs29E4v6p4e24p5tC_H8/s1600/IMG00988-20121102-1956.jpg

Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya mpira wa kikapu, Jocquis Sconiers   anatarajiwa kuanza kazi ya kuinoa timu ya taifa ya wanawake na wanaume ya mchezo huo kwenye uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Sconiers ametua nchini huku akiwa na mikakati kadhaa aliyodai kuwa ikitekelezwa vyema, mchezo wa mpira wa kikapu nchini utsonga mbele kwa kiasi kikubwa na pengine  kuzipiku timu za mataifa ya jirani kama Kenya na Uganda.


Hata hivyo, kocha huyo amebakiwa na wiki moja tu kuinoa timu hiyo kabla ya kuanza kwa michuano ya mchezo huo ya Kanda ya Tano ya Afrika itakayofanyika jijini Dar es Salaam.

  Katibu msaidizi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Michael Maluwe, amesema wamefurahishwa na ujio wa kocha huyo na kuwataka wadau kumpa ushirikiano.

"Tunaomba wachezaji na wadau wa kikapu nchini wampe ushirikiano ili afanye kazi yake vizuri na kusaidia timu zetu," aliongeza  Maluwe.


Aliwataja baadhi ya wachezaji waliopo kwenye kikosi hicho kuwa ni Ladislaus Ikungura,Gerald Baru, Abdallah Ramadhani ‘Dulla’, Henry Mwinuka ‘kidume’ na

Sudi Abdulrazak.

Wengine ni Sylivian Yunzu (Maige), Mussa Chacha, Frankline Simkoko,Small Forward, Mohamed Ally ‘Dibo’, Amir Muhidin Saleh na nahodha, Lusajo Samwel.


Kocha Bahati Mgunda alisema katika timu ya wanaume alikuwa na wachezaji 32 lakini sasa wamechujwa na kubaki 18 ambao watatu kati yao watapunguzwa zaidi na kubaki 15.

FA CUP-MARUDIANO RAUNDI YA 3: LEO ARSENAL, MAN UNITED ZASAKA KUSONGA!!

FERGIE_n_WENGER-KICHEKO>>DONDOO ZA MECHI: MAN UNITED v WEST HAM, ARSENAL v SWANSEA
BAADA ya kwenda sare ugenini za 2-2, Vigogo Manchester United na Arsenal, Klabu ambazo ndizo zinashika Rekodi ya kutwaa FA CUP mara nyingi, leo Usiku kila mmoja atakuwa Uwanja wa nyumbani kucheza Mechi za marudio, ManUnited Uwanjani Old Trafford dhidi ya West Ham, na Arsenal, ndani ya Emirates, kuivaa Swansea City.
ZIFUATAZO ni TAARIFA fupi za Mechi hizo:
MAN UNITED v WEST HAM
Uwanja: Old Trafford
Tarehe: Jumatano, Januari 16
SAA: 5 Dak 5 Usiku
Hali za Wachezaji
Wayne Rooney anatarajiwa kuichezea Manchester United Mechi yake ya kwanza tangu Siku ya Krismasi alipojiumiza Goti mazoezini.
Pia Winga Nani anategemewa kuwemo kwenye Kikosi baada ya kupona Musuli za Paja zilizomfanya azikose Mechi 15 zilizopita.
Mchezaji pekee ambae ni Majeruhi kwa Man United ni Ashley Young alieumia Goti Jumapili iliyopita walipocheza na Liverpool.
Majeruhi wa West Ham ni James Collins, Mark Noble, George McCartney, Joey O'Brien na Andy Carroll huku  Modibo Maiga ametimka kwenda kuichezea Mali kwenye AFCON 2013 na pia Wachezaji wao wapya waliosainiwa Mwezi huu Jnuari, Wellington Paulista na Marouane Chamakh , hawaruhusiwi kucheza Raundi hii.
Uso kwa Uso
-Manchester United imeshinda Mechi 8 kati ya 10 walizocheza mwisho na West Ham na Mwezi Novemba, kwenye Mechi ya Ligi Kuu England, waliifunga West Ham 1-0 kwa Bao la Sekunde ya 33 la Robin van Persie.
Rekodi
Manchester United
-Wametinga Fainali za  FA CUP 18 na kushinda 11, huku 5 zikiwa chini ya Sir Alex Ferguson.
West Ham United
-Walitwaa FA CUP Miaka ya 1964, 1975 na 1980 winners na mara ya mwisho kutinga Fainali ni Mwaka 2006 lakini katika Misimu mitano iliyopita walishindwa kusonga zaidi ya Raundi ya 3 mara 3.
ARSENAL v SWANSEA
Uwanja: Emirates Stadium
Tarehe: Jumatano, Januari 16
SAA:  4 Dak 30 Usiku
Hali za Wachezaji
Arsenal watawakosa Laurent Koscielny na Mikel Arteta wakati  Koscielny akiwa Kifungoni na Kiungo Arteta akiwa majeruhi.
Meneja wa Swansea, Michael Laudrup, ana Kikosi chake kamili bila dosari yeyote ispokuwa Mchezaji mpya wa Mkopo, Roland Lamah, ambae usajili wake ulichelewa kwa ajili ya Mechi hii.
Uso kwa Uso
-Arsenal wameshinda Mechi 6, Sare 2 na kufungwa 5 katika Mechi 13 za mwisho walizocheza na Swansea.
Rekodi
Arsenal
-Arsenal wapo kwenye Rekodi ya kuwa Timu ya Pili kwa kutwaa FA CUP mara nyingi, wametwaa mara 10 wakiwa nyuma ya Manchester United waliolibeba mara 11 katika Fainali 17 walizoshiriki ukilinganisha na 18 za Man United.
-Chini ya Arsene Wenger, Arsenal wametwaa FA CUP mara 4 na mara ya mwisho ni Mwaka 2005.

IOC YATARAJIA KUMNYANG'ANYA MEDALI ARMSTRONG.


MWENDESHA baiskeli Lance Armstrong anatarajiwa kuirejesha medali ya Olimpiki mara mahojiano yake ya kukiri kutumia dawa za kuongeza nguvu michezoni yatakaporushwa hewani kesho. Armstrong ambaye amekuwa akikana kutumia dawa hizo kwa miaka mingi ameandikiwa barua na Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa-IOC baada ya kukiri katika kipindi kinachoendeshwa na mtangazaji maarufu wa Marekani, Oprah Winfrey kutumia dawa hizo. Mjumbe wa IOC, Dick Pound ambaye pia amewahi kuwa kiongozi wa Shirikika la Kupambana na Dawa za Kuongeza Nguvu-WADA amesema ni wajibu wa IOC nao kuchukua hatua juu ya suala la Armstrong ndio maana wamemuandikia barua ya kumtaka kurejesha medali yao. Pamoja na kwamba mazungumzo hayo bado hayajarushwa hewani lakini Winfrey mwenyewe amethibitisha kuwa Armstrong mwenye umri wa miaka 41 amekubali kudanganya kwa kutumia dawa hizo. Armstrong alinyang’anywa mataji saba ya michuano ya baiskeli ya Toure de France baada ya kukutwa na hatia ya kutumia dawa hizo na WADA lakini alikuwa hajazungumza lolote toka akumbwe na sakata hilo.

DAKAR RALLY: TERRANOVA ASHINDA HATUA YA KUMI.


DEREVA Orlando Terranova amewapagawisha mashabiki wa Argentina kwa kuwa dereva wa kwanza wa nchi hiyo kuibuka kidedea katika hatua ya 10 ya mashindano ya Dakar Rally yanayofanyika huko Amerika Kusini. Dereva huyo anayeendesha gari aina ya BMW mwenye umri wa miaka 33 ambaye anashindana katika mbio hizo kwa mara ya saba alishika nafasi ya kwanza katika hatua hiyo akiwa mbele ya Nani Roma kwa dakika mbili na sekunde saba na kufuatiwa na bingwa mtetezi Stephane Peterhansel wa Ufaransa aliyeshika nafasi ya tatu. Akihojiwa mara baada ya ushindi huo Terranova amesema ilikuwa ni rahisi kushinda hatua hiyo kwasababu hawakufanya makosa mara kwa mara na gari lao halikuwaletea matatizo. Bingwa mtetezi Peterhansel mwenye umri wa miaka 47 raia wa Ufaransa anatafuta taji la 11 la mashindano hayo huku nafasi ya yeye kushinda ikiongezeka baada ya aliyekuwa mpinzani wake wa karibu Nasser al-Attiyah kutoka Qatar kujitoa Jumatatu baada ya kuharibikiwa na gari lake.

KUELEKEA MASHINDANO YA MATAIFA NI MAKOCHA WATATU PEKEE NDIO WALIORUDI KATIKA AFCON.


MAKOCHA watatu pekee ambao walikuwepo katika michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon mwaka mmoja uliopita ndio wamerejea katika michuano ya mwaka huu inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Jumamosi. Mmojawapo ni Mfaransa Herve Renard ambaye aliiongoza Zambia kupata mafanikio ya kushangaza jijini Libreville Februari mwaka jana na kuendelea kukinoa kikosi cha nchi hiyo pamoja na kazi China na Mashariki ya Kati. Sami Trabelsi anayefundisha Tunisia ni kocha mwingine ambaye anarejea na timu hiyo huku akiomba kupata matokeo mazuri zaidi baada ya kuifikisha nchi hiyo Robo fainali katika fainali zilizofanyika Gabon na Equatorial Guinea mwaka jana. Mwingine ni Mjerumani Gernot Rohr, ingawa hakuongezewa mkataba na wenyeji wenza wa michuano ya mwaka jana Gabon baada ya kufungwa katika mchezo war obo fainali lakini alipewa mikoba ya kuinoa Niger na kufanikiwa kuipeleka nchini Afrika Kusini kwenye michuano hiyo. Katika orodha ya makocha waliopo Afrika Kusini inajumuisha makocha nane kutoka Ulaya, saba wa Afrika na mmoja kutoka Amerika Kusini.

WATATU WACHUKUA FOMU ZA URAIS TFF


 
 Wadau watatu wa mpira wa miguu wamechukua fomu za kuwania urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kufanya idadi ya waliojitosa katika uchaguzi huo utakaofanyika Februari 24 mwaka huu kufikia 30. Hata hivyo, idadi hiyo ni kwa wale wanaochukua fomu hizo katika ofisi za TFF, kwani vilevile zinapatikana kupitia tovuti ya TFF ya www.tff.or.tzambapo mwisho wa kuchukua na kurejesha ni saa 10 kamili alasiri Januari 18 mwaka huu. Waliochukua leo (Januari 16 mwaka huu) kuwania urais ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athuman Jumanne Nyamlani, Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera (KRFA), Jamal Emil Malinzi na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Kigoma, Omari Mussa Nkwarulo. Mwengine aliyechukua leo ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA), Elias Mwanjala anayewania ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kuwakilisha Kanda ya Iringa na Mbeya. Orodha kamili ya wadau waliochukua fomu kwenye ofisi za TFF ni Athuman Jumanne Nyamlani, Jamal Emil Malinzi na Omari Mussa Nkwarulo (urais), Michael Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace Karia (umakamu wa rais). Kwa upande wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji na kanda zao kwenye mabano ni Salum Chama (Kagera na Geita), Mugisha Galibona, Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano (Mara na Mwanza). Epaphra Swai na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo na Elly Mbise (Arusha na Manyara), Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi na Rukwa) na James Mhagama (Njombe na Ruvuma). Athuman Kambi (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na Singida), Farid Nahdi na Twahili Njoki (Morogoro na Pwani), Elias Mwanjala (Iringa na Mbeya), Khalid Mohamed (Kilimanjaro na Tanga) na Muhsin Balhabou, Shaffih Dauda na Zafarani Damoder (Dar es Salaam). Kwa upande wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) waliochukua fomu kwenye ofisi za TFF mpaka sasa ni wawili tu. Yusuf Manji amechukua fomu ya uenyekiti wakati Said Mohamed amechukua fomu ya kuwania umakamu mwenyekiti.

WAHARIRI, WAANDISHI WAPIGWA MSASA KANUNI ZA UCHAGUZI
Wahariri na Waandishi wa Habari zaidi ya 40 wameshiriki kwenye semina kuhusu Kanuni za Uchaguzi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyofanyika leo (Januari 16 mwaka huu). Wawezeshaji katika semina hiyo iliyofanyika ofisi za TFF walikuwa Kamati ya Uchaguzi ya TFF iliyoongozwa na Mwenyekiti wake Deogratias Lyato na Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah.

MARADONA ASEMA HANA MPANGO WA SOKA TENA I QUIT FOOTBALL - MARADONA.


NGULI wa soka nchini Argentina, Diego Maradona amebainisha kuwa hana mpango wa kushughulika mambo  ya soka tena. Maradona ambaye ni kocha wa zamani wa klabu ya Al Wasl ya Dubai amezungumzia kuishiwa kwake hamu na mchezo huo kufuatia kutimuliwa na kutafutwa mbadala wa haraka wa aliyekuwa kocha wa River Plate Matias Almeyda. Akihojiwa Maradaona amesema baada ya kukasirishwa na jinsi walivyomtimua Almeyda na muda mfupi baadae kumteua Ramon Diaz kuziba nafasi yake hahitaji tena kujishughulisha na masuala ya soka. Maradona ambaye nezi zake aliisaidia nchi yake kunyakuwa Kombe la Dunia mwaka 1986 nchini Mexico, amedai kwamba kitendo hicho cha kubadilisha kocha ndani ya siku tatu ndichio kilichomkera na kuamua kuachana na mambo ya soka.

NADAL KUREJEA MICHUANO YA ATP BRAZIL OPEN.


MCHEZAJI tenisi nyota wa Hispania, Rafael Nadal ambaye yuko nje ya uwanja kuanzia katikati ya msimu uliopita kwa sababu ya majeruhi anatarajia kurejea tena mwezi ujao katika michuano ya ATP Brazil Open itakayofanyika jijini Sao Paulo baada ya kupona kabisa. Ofisa habari wa Nadal, Benito Perez-Barbadillo alithibitisha taarifa za nyota huyo anayeshika namba nne katika orodha za ubora duniani kuwa atashiriki michuano hiyo ya Brazil. Nadal ameshinda mataji 11 ya Grand Slams lakini maumivu yalipelekea nyota huyo raia wa Hispania kutocheza toka June mwaka jana. Nyota huyo alikosa michuano ya wazi ya Australia inayoendelea hivi kwa kupata maambukizi ya tumbo wakati akiendelea na matibabu ya mwisho ya mguu wake.

ZAHOR PAZI ATIMKIA AFRIKA KUSINI KUJARIBIWA


Zahor Pazi
KIUNGO mshambuliaji wa mabingwa wa Kombe la Mapinduzi, Azam FC, Zahor Iddi Pazi ameondoka leo Alfajiri Dar es Salaam kwenda Afrika Kusini kufanya majaribio ya kujiunga na klabu ya Blomomfontein Celtic ya nchini humo.
Baba mzazi wa mchezaji huyo, ambaye Desemba ametolewa kwa mkopo katika klabu ya JKT Ruvu Pwani, amesema  kwamba kijana wake huyo amepatiwa nafasi hiyo na klabu yake ya Azam.
“Alipokuwa Kongo (DRC) na Azam kwenye Kombe la Hisani kuna wakala alivutiwa na kipaji chake akaomba apelekwe kufanya majaribio, basi wakati umefika ameondoka leo,”alisema.
Zahor licha ya kuwa mchezaji mzuri amekuwa hana bahati ndani ya kikosi chs Azam tangu asajiliwe msimu uliopita.
Mwanzoni mwa msimu, Zahor aliomba kwenda kucheza kwa mkopo Coastal Union ya Tanga, lakini uongozi wa klabu hiyo ukamkatalia kabla ya kumtoa kwa mkopo Desemba mwaka jana.

MAMBO YAMEKWIVA UCHAGUZI MKUU WA TFF MALINZI,NYAMLANI WAUTAKA URAIS WA TFF KUMRITHI TENGA NAYE BOSSI WA YANGA YUMO NDANI YUSUPH MANJI NI BALAAAAAAAAAA



Manji anazungumza na Waandishi wa Habari baada ya kuchukua fomu
Mmiliki wa klabu ya African Lyon, Rahim Kangenzi ‘Zamunda’ akimchukulia fomu ya kugombea Uenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu kwa niaba ya klabu za Ligi Kuu zilizompendekeza, Mwenyekiti wa Yanga SC, Yusuf Mehbub Manji (kulia) ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ilala, Dar es Salaam mida hii, kuelekea uchaguzi utakaofanyika Februari 24, mwaka huu mjini Dar es Salaam. Anayetoa fomu hiyo kushoto ni Ofisa wa TFF, Jonathan Aloyce Kakwaya.   
Zamunda anamkabidhi fomu yake Manji
Mhasibu wa TFF anamuandikia Manji risiti

Mwenyekiti wa Chama cha Soka Kagera (KRFA), Jamal Emil Malinzi akirejesha fomu ya kugombea urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ofisi za shirikisho hilo, Ilala, Dar es Salaam mida hii, kuelekea uchaguzi utakaofanyika Februari 24, mwaka huu mjini Dar es Salaam. Anayepokea fomu hiyo ambayo Malinzi alichukua kwenye tovuti ya TFF na kujaza kisha kuilipia katika benki ya CRDB kushoto ni Ofisa wa TFF, Jonathan Aloyce Kakwaya.   
Anashuka kwenye gari

Anaanza kuekelea ofisi za TFF
Anajiorodhesha
Risiti yake ya benki
  

Anazungumza na Waandishi wa Habari


Makamu wa kwanza wa rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Athumani Jumanne Nyamlani akichukua fomu ya kugombea urais wa shirikisho hilo, kwenye ofisi za TFF, Ilala, Dar es Salaam mida hii kwa ajili ya uchaguzi utakaofanyika Februari 24, mwaka huu mjini Dar es Salaam. Anayekabidhi fomu kushoto ni Ofisa wa TFF, Jonathan Aloyce Kakwaya.
Akiwa na rafiki zake waliomsindikiza kuchukua fomu
Anahesabu fedha

Makamu wa kwanza wa rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Athumani Jumanne Nyamlani akikabidhi fedha za malipo ya fomu ya kugombea urais wa shirikisho hilo, katika uchaguzi utakaofanyika Februari 24, mwaka huu mjini Dar es Salaam. Anayepokea kushoto ni Ofisa wa TFF, Jonathan Aloyce Kakwaya.

FA CUP: SUNDERLAND YABWAGWA NA BOLTON, QPR YAICHAPA WBA!

FA_CUP-NEW_LOGO>>FULHAM YASONGA KUWA UGENINI NA MAN UNITED AU WEST HAM!!
>>LEO, ARSENAL v MICHU & SWANSWEA, MAN UNITED v WEST HAM!!
>>PATA RATIBA KAMILI RAUNDI YA 4 FA CUP

FA CUP-Raundi ya 3
MECHI ZA MARUDIANO-MATOKEO
Jumanne Januari 15
Birmingham 1 Leeds 2
Bournemouth 0 Wigan 1
Brentford 2 Southend 1
Leyton Orient 1 Hull 2
MK Dons 2 Sheffield Wed 0
Stoke 4 Crystal Palace 1
Sunderland 0 Bolton 2
Blackpool 1 Fulham 2
West Brom 0 QPR 1

JANA Usiku Mechi 9 za Marudiano ya Raundi ya 3 ya FA CUP zilifanyika na katika Mechi pekee ya Klabu za Ligi Kuu England, ile ya WBA v QPR, QPR waliibuka Washindi kwa Bao 1-0 na ile Mechi pekee ya Timu za Championship, Birmingham v Leeds United, Leeds walisonga kwa kushinda Bao 2-1 huku Bolton Wanderers, walio Daraja la chini, kuibwaga Sunderland Bao 2-0.
Wakikutana kwa mara ya 4 Msimu huu huku WBA wakishinda mara 2 kwenye Ligi na sare moja kwenye FA CUP, safari hii QPR, walio mkiani mwa Ligi Kuu, waligeuza kibao kwa kushinda 1-0 kwa Bao la Dakika ya 75 la Jay Boythroyd na kuwaingiza Raundi ya 4 ambapo watacheza na MK Dons.
Nao Bolton Wanderers, wakicheza ugenini Stadium of Light, waliichapa Sunderland Bao 2-0 na kutinga Raundi ya 4 ambapo watacheza nyumbani na Everton.
Bao zote za Bolton zilifungwa na Straika Marvin Sordell katika Dakika ya 64, kwa Penati, na Dakika ya 73.
Nao Fulham, walioifunga Blackpool Bao 2-1 ugenini, watacheza tena ugenini kwenye Raundi ya 4 kwa kukutana na Mshindi kati ya Manchester United na West Ham wanaorudiana leo Usiku Uwanjani Old Trafford.
Mechi nyingine ya Marudiano ya Raundi ya 3 FA CUP itakayochezwa leo ni kati ya Arsenal na Swansea City Uwanjani Emirates kufuatia sare yao ya 2-2 katika Mechi ya kwanza.

MECHI ZA MARUDIANO- FA CUP-Raundi ya 3
Jumatano Januari 16
[SAA 4 Dak 30 Usiku]
Arsenal v Swansea City
[SAA 5 Usiku]
Man Utd v West Ham

RAUNDI YA 4
Ijumaa Januari 25
[SAA 4 Dak 30 Usiku]
Millwall v Aston Villa
Jumamosi Januari 26
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Stoke City v Manchester City
[SAA 12 Jioni]
Norwich City v Luton Town
Macclesfield Town v Wigan Athletic
Derby County v Blackburn Rovers
Hull City v Barnsley
Middlesbrough v Aldershot Town
Brighton & Hove Albion v Swansea City au Arsenal
Reading v Sheffield United
Huddersfield Town v Leicester
QPR v MK Dons
Bolton v Everton
[SAA 2 na Nusu Usiku]
West Ham United au Manchester United v Fulham
Jumapili Januari 27
[SAA 9 Mchana]
Brentford v Chelsea
[SAA 11 Jioni]
Leeds United v Tottenham Hotspur
[SAA 1 Usiku]
Oldham Athletic v Liverpool

MICHAEL RICHARD WAMBURA AJIRIPUA TENA KWA KUCHUKUA FOMU YA UMAKAMU WA RAIS TFF AMPONGEZA TENGA KWA KUTOGOMBEA TENA. NINI MTAZAMO WAKE HUYU HAPA.


Michael Richard Wambura
Aliyewahi kuwa katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini TFF Michael Richard Wambura na baadaye kukutana na vizingiti lukuki kila alipokuwa anajitokeza kuwania uongozi wa mpira katika ngazi mbalimbali, hii leo amejitokeza tena kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya makamu wa Rais wa shirikisho hilo.
Akionekana ni mwenye matumaini makubwa mara hii na maamuzi yake hayo, Wambura amesema kwasasa amekamilisha jukumu la kwanza la kuchukua fomu kama raia mwenye haki ya kufanya hivyo na kwamba mikakati ya kuelekea katika mchakato mzima wa uchaguzi kwa upande wake ndio unaanzia hapo. 
Amesema angependelea zaidi watanzania zaidi wangejitokeza kuchukua fomu ili kuleta changamoto kubwa zaidi katika mchakato mzima wa uchaguzi huo.
Amempongeza Rais wa sasa Leodigar Tenga kwa kuamua kuachia nafasi hiyo na kwamba hiyo inaonyesha ni namna gani Rais Tenga alivyo muumini mzuri wa vipindi na kuruhusu mawazo mapya na mfumo mpya na watu wapya ili kumpokea nafasi yake.
Michael Wambura akiongea na waandishi wa habari.
Amesema unapokuwa madarakani yapo ambayo utayafanikisha na mengine mazuri watu wayaenzi na yale aliyoshindwa wengine watayapokea kuanzia hapo na kuyaendeleza.
Amesema sababu ambazo zimemfanya kuchukua fomu hii leo siyo za wakati ule na kwamba kila jambo linawakati wake na pengine sababu ambazo zilikuwa zikionekana ni tatizo kwa wakati ule huenda zisiwe hivyo kwasasa.

Wambura amedokeza sababu zilizo msukuma kuwania nafasi hiyo ya makamu wa Rais kwakuwa ni nafasi ambayo inachangamoto nyingi na kwamba kuna mengi ambayo hayajafanyiwa kazi kwa kuwa nafasi hiyo haijapata mtu muafaka na kwamba wale wanaomaliza muda wao wanahitaji kusaidiwa.
Ameizungumzia pia sifa ya Rais ajaye kuwa anatakiwa kuwa amechaguliwa kwa mujibu wa katiba na kuupenda mpira wa miguu.
Awe ni mwenye kuelewa kuwa mpira wa miguu unatakiwa kuchezwa nchi nzima kwa kuwa ni mchezo unaopendwa na wengi kote nchini, vilevile awe na muda wa kuushughulikia mchezo wa soka na mwenye kiu ya maendeleo ya soka.
Amesema kuna haja ya kubadilisha mfumo wa soka uliopo ili kuwa na mpira ulio bora, timu ya taifa bora na kutoa nafasi kwa walio wengi kuucheza mpira wa miguu.

Wambura aliwahi kugombea nafasi ya mwenyekiti mkoa wa mara lakini alienguliwa kutokana na kamati ya uchaguzi kusema kuwa hakuwa muadilifu kabla ya kutaka kujaribu tena bahati yake katika chama cha soka mkoa wa Dar es Salaam DRFA ambapo baadaye aliamua kujitoa na kuelekea katika kamati ya rufaa inayoongozwa na Profesa Mgongo Fimbo ambayo ilimsafisha.
Hata hivyo TFF ilipinga maamuzi hayo na kuelekea shirikisho la soka duniani fifa kuomba mwongozo ambapo FIFA ambalo liliagiza TFF kuunda kamati ya rufaa inayojitegemea ambapo kwasasa mabadiliko hayo yamefanyika.

Kwasasa Wambura yuko safi baada ya maamuzi ya kamati ya rufaa ya Prof Mgongo Fimbo.

MANCHESTER UNITED YAPATA UDHAMINI WA MAKAMPUNI MAWILI NCHINI CHINA YAENDELEA KUWA BALAAAAAA.




 Manchester United imetangaza kupata udhamni wa makampuni mawili ya kichina kwa mkataba wa miaka mitatu.

Mashetani hao wekundu wanaokadiriwa kuwa na takribani mashabiki milioni 108 nchini China, wametangza kupata udhamini kutoka katika kampuni moja inayotengeneza vinywaji baridi ya Wahaha na benki moja maarufu ya ujenzi nchini China (CCB).
Wahaha wamekuwa wazalishaji wakubwa wa vinywaji nchini Chini kwa miaka 11 ni vinywaji vyao vitakuwa ndio vinywaji marafiki nambari moja nchini humo.
Wamekuwa wakizalisha aina mbalimbali ya vinywaji ikiwa ni pamoja maziwa ambayo yalizinduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1987 na Zong Qinghou.
Kwa upande wa benki ya CCB ina maana ya kwamba United itapata haki ya kutengeneza kadi zao ambazo zitakuwa na nembo ya klabu katika nchi ya China, na kuwapa faida mashabiki wao 102 ambao wataanza kutumia benki hiyo

ROBO FAINALI-COPA del REY: Real 2 Valencia 0, COPPA ITALIA: Inter 3 Bologna 2

>>COPA del REY: LEO BARCA v MALAGA!
BARCA_v_REALReal Madrid wamejiweka kwenye mazingira mazuri ya kutinga Nusu Fainali ya COPA del REY baada ya jana kuichapa Valencia Bao 2-0 katika Mechi ya kwanza ya Robo Fainali iliyochezwa Uwanjani Santiago Bernabeu.
Karim Benzema ndie alieipatia Real Bao la kwanza katika Kipindi cha Kwanza na Andrés Guardado kujifunga mwenyewe katika Dakika ya 74 na kuipa Real ushindi wao Bao 2-0 ambao watakwenda nao ugenini kurudiana na Valencia Wiki ijayo.
Katika Mechi hiyo, Kipa wa Valencia, Vicente Guaita, alimkatili Nyota Cristiano Ronaldo mara mbili kwa kuokoa magoli ya wazi.
Mshindi kati ya Valencia na Real atacheza na Mshindi kati ya Barcelona na Malaga ambao leo wanacheza Mechi yao ya kwanza ya Robo Fainali.
Mechi nyingine ya Robo Fainali itakayochezwa leo ni kati ya Real Zaragoza na Sevilla na Alhamisi ni Atlético Madrid na Real Betis.

COPA del REY
ROBO FAINALI
MATOKEO/RATIBA
Jumanne Januari 15
Real Madrid CF 2 Valencia 0
Jumatano Januari 16
[SAA 3 na Nusu Usiku]
Real Zaragoza v Sevilla FC
[SAA 5 na Nusu Usiku]
Barcelona v Malaga
Ijumaa Januari 18
[SAA 6 Usiku]
Atletico Madrid v Real Betis
Jumatano Januari 23
MARUDIANO
Sevilla FC v Real Zaragoza
Valencia v Real Madrid CF
Malaga v Barcelona
Real Betis v Atletico Madrid

COPPA ITALIA: Inter 3 Bologna 2
Inter Milan, wakicheza kwao Stadio Giuseppe Meazza Mjini Milano, jana walitinga Nusu Fainali ya COPPA ITALIA lakini nusura wapokwe tonge mdomoni baada ya kuongoza 2-0 na Bologna kusawazisha katika Dakika 9 za mwisho lakini wakaibuka kidedea baada ya Bao la Sekunde ya mwisho ya Dakika 30 za nyongeza kuwapa ushindi wa 3-2.

MAGOLI:
Inter Milan 3
-Fredy GuarĂ­n Dakika ya 34
-Rodrigo Palacio 77
-Andrea Ranocchia 120
Bologna 2
-Alessandro Diamanti Dakika ya 81
-Manolo Gabbiadini 84

Beki Andrea Ranocchia ndie aliefunga Bao la 3 na la ushindi katika Dakika ya 120 na sasa watacheza Nusu Fainali na Mshindi kati ya  AS Roma au Fiorentina wanaokutana Jumatano Usiku.
Nusu Fainali nyingine ni kati ya Mabingwa wa Italy Juventus na Lazio.

COPPA ITALIA
ROBO FAINALI
RATIBA:
Jumatano Januari 16
[SAA 5 Usiku]
Fiorentina v AS Roma
NUSU FAINALI:
Jumanne Januari 22
SS Lazio v Juventus
Jumanne Januari 29
Juventus v SS Lazio