Monday, October 22, 2012

TEGETE: NIMEFUFUA MAKALI, SASA...

 

SIMBA YAREJEA DAR, SASA HASIRA ZOTE KWA AZAM

Simba SC

SIMBA SC imerejea Dar es Salaam leo mchana na inatarajiwa kuingia kambini moja kwa moja kuanza maandalizi ya mechi ijayo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, dhidi ya Azam FC, Oktoba 27, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 
 
Simba SC itakuwa na wiki nzima ya kujiandaa na mechi hiyo, ikitoka kulazimishwa sare ya tatu mfululizo jana kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, baada ya kutoka 0-0 na wenyeji Mgambo Shooting katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
 
 
Matokeo hayo, yanaifanya Simba ifikishe pointi 19, baada ya kucheza mechi tisa na kuendelea kuongoza Ligi Kuu, ingawa wameuweka rehani usukani wa ligi hiyo kwa Azam ambayo Jumatano inacheza na Ruvu Shooting Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.
 
 
Awali ya hapo, Simba ilitoka 2-2 na Kagera Sugar Uwanja wa Taifa na 0-0 na Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani.
 
 
Azam yenye pointi 17, ikishinda itafikisha pointi 20 na kupanda kileleni, tena ikiwa nyuma kwa mchezo mmoja, kwani hadi sasa imecheza mechi saba. Yanga iliyocheza mechi nane, ina pointi 14 katika nafasi ya tatu nayo itacheza na Polisi Morogoro keshokutwa.
 
 
Katika mechi ya jana ya Simba na Mgambo, iliyochezeshwa na refa Athumani Lazi wa Morogoro, dakika 45 za kwanza, timu zote zilishambuliana kwa zamu na zilionyesha kiwango kizuri, ushindani mkubwa- kwa ujumla ilikuwa burudani.
 
 
Kipindi cha pili kadhalika pamoja na kocha Mserbia, Profesa Milovan Cirkovick kufanya mabadiliko akiwatoa Mrisho Ngassa na Amri Kiemba na kuwaingiza Edward Christopher na Salim Kinje, bado walishindwa kuifunga Mgambo iliyopanda Ligi Kuu msimu.
 
 
Katika dakika 10 za mwisho, ilishuhudiwa Mgambo wakicheza kwa kujihami zaidi kutokana na presha kali ya mashambulizi ya Simba SC.
 
 
Katika mechi hiyo, kikosi cha Mgambo kilikuwa; Godson Mmasa, Yassin Awadh, Salum Mlima, Bakari Mtama, Salum Kipanga, Ramadhani Malima, Chande Magoja/Nassor Gumbo dk85, Mussa Ngunda, Issa Kandulu, Fully Mganga na Juma Mwinyimvua.
 

Simba SC;Juma Kaseja, Nassor Masoud ‘Chollo’, Amir Maftah, Hassan Hatibu, Paschal Ochieng, Jonas Mkude, Amri Kiemba/Salim Kinje dk88, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Emmanuel Okwi na Mrisho Ngassa/Edward Christopher dk 79.



 

AZAM SASA WASHINDWE WENYEWE, UTAWALA WA LIGI UPO KWENYE HIMAYA YAO BAADA YA SIMBA KUCHEMSHA

Azam FC

AZAM FC inaweza kupanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Jumatano iwapo itaifunga Ruvu Shooting katika mfululizo wa ligi hiyo, kwani itafikisha pointi 20 baada ya kucheza mechi nane na bado itakuwa inazidiwa mchezo mmoja na vinara wa sasa wa ligi hiyo, Simba SC.
 
Haya yatakuwa mabadiliko ya kwanza kileleni mwa ligi hiyo tangu kuanza kwake, Septemba 15 mwaka huu, kwani ni Simba imekuwa ikiongoza muda wote. Matumaini ya Azam kupaa kileleni Jumatano, yanafuatia jana Simba SC kulazimishwa sare ya 0-0 na wenyeji Mgambo JKT kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
 
 
Simba sasa ina pointi 19, baada ya kucheza mechi tisa na Azam ina pointi 17, baada ya kucheza mechi saba, wakati Yanga iliyocheza mechi nane, ina pointi 14 katika nafasi ya tatu.
 
 
Simba ilianza vema Ligi Kuu, ikishinda mechi tano mfululizo, lakini tangu itoe sare ya 1-1 na Yanga Oktoba 3, mwaka huu, ilishinda mechi moja tu kati ya nne zilizofuata, Oktoba 7, mwaka 2012 ilipoifunga 4-1 JKT Oljoro Uwanja wa Taifa.
 
 
Mechi tatu zilizofuata Simba imetoa sare zote, bila kufungana na Mgambo na Coastal Union mjini Tanga na 2-2 na Kagera Sugar, Uwanja wa Taifa. 



Hadi sasa, Azam na Simba ndio timu pekee ambazo hazijafungwa katika Ligi Kuu na hii inaashiria kwamba bado hizo ndizo timu bora katika ligi hiyo, zikiendeleza upinzani wao wa tangu msimu uliopita.
 
 
Msimu uliopita, Simba ilitwaa ubingwa na Azam ikawa ya pili, wakati Yanga iliambulia nafasi ya tatu na hadi sasa katika msimamo wa Ligi Kuu, mpangilio uko hivyo ingawa ni matarajio ya wengi keshokutwa mambo yatabadilika.
 
 
Lakini pia mbele ya Ruvu Shooting iliyoonyesha upinzani mkubwa ikicheza na Simba na Yanga na kufungwa kwa tabu, tena kukiwa na dalili za wapinzani wao kubebwa kidogo na marefa katika mechi zote, hilo linaweza kuwa gumu.
 
 
Kitu kimoja tu, Azam imekuwa na rekodi nzuri kwenye Uwanja wake, Chamazi na kwa sababu keshokutwa kipute kitapigwa hapo, timu hiyo ya Said Salim Bakhresa na familia yake inaweza kupaa kileleni.
 
 
Azam ni bora, na ndiyo maana kila mashindano inayoshiriki tangu mwaka jana imekuwa ikifika mbali.  Ina Medali za Fedha za Ligi Kuu, Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame na Kombe la Urafiki na pia hawa ni mabingwa wa Kombe la Mapinduzi.   
 
 
Wawakilishi hao wa Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho mwakani, wanajivunia kikosi chao kizuri chenye wachezaji bora kama mfungaji bora wa Ligi Kuu, John Bocco ‘Adebayor’, Kipre Tchetche, Salum Abubakar ‘Sure Boy Jr.’ na wengineo.
Lakini pia kocha mtaalamu, hodari na mchapakazi, Mserbia, Boris Bunjak ambaye Jumamosi alikuwapo Uwanja wa Taifa kuitathmini Ruvu Shooting ilipokuwa ikicheza na Yanga na kufungwa kwa mbinde 3-2.
 
 
Hadi sasa Bunjak ameiongoza Azam FC katika mechi 14, kati ya hizo saba za Ligi Kuu, ambazo ameshinda tano na kutoa sare mbili, zote ugenini 2-2 na Toto African mjini Mwanza na 0-0 na Prisons mjini Mbeya.
 
 
Timu moja tu ambayo imemfunga Bunjak hadi sasa, Simba SC katika mechi tatu, moja ya michuano ya BancABC Sup8R, 2-1, Ngao ya Jamii 3-2 na mchezo wa kirafiki 3-2 pia. Kwa ujumla kulingana na mwenendo wa Ligi Kuu hadi sasa, Azam ikiwa imecheza mechi saba, imeonyesha msimu huu ‘haitaki masihara’.
REKODI YA BORIS BUNJAK AZAM
Azam 2-1 Polisi                    (BancABC)
Azam 2-1 Simba B              (BancABC)
Azam 8-0 Trans Camp       (Kirafiki)
Azam 1-0 Prisons                (Kirafiki)
Azam 2-0 Coastal Union   (Kirafiki)
Azam 2-3 Simba SC            (Ngao ya Jamii)
Azam 1-0 Kagera Sugar     (Ligi Kuu)
Azam 2-2 Toto African      (Ligi Kuu)
Azam 3-0 JKT Ruvu             (Ligi Kuu)
Azam 1-0 Mtibwa Sugar    (Ligi Kuu)
Azam 1-0 African Lyon      (Ligi Kuu)
Azam 2-3 Simba SC            (Kirafiki)
Azam 1-0 Polisi                    (Ligi Kuu)
Azam 0-0 Prisons                (Ligi Kuu)                             


 

KLABU BINGWA AFRIKA: Fainali ni Esperance v Al Ahly Mwezi Novemba!

Egypt?s al-Ahly player Wael Gomaa (L) vies for the ball against Nigeria?s Dele Olorundare of the Sunshine club during their semifinal football match in the African Champions League 
>>AL AHLY 1 SUNSHINE STARS 0
Klabu kongwe na kigogo ya Misri, Al Ahly, imeitungua Klabu ya Nigeria Sunshine Stars bao 1-0 katika Mechi ya marudiano ya Nusu Fainali ya CAF CHAMPIONZ LIGI hapo jana Mjini Cairo na kufanikiwa kuingia Fainali ambako itakutana na Mabingwa watetezi Esperance.


Katika Mechi ya kwanza iliyochezwa huko Nigeria Wiki mbili zilizopita, Sunshine Stars na Al Ahly zilitoka sare ya bao 3-3 na hivyo Al Ahly wamepita kwa jumla ya bao 4-3.


Katika Mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Kijeshi wa Cairo bila ya Watazamaji wowote kufuatia Uongozi wa Misri kuendelea kupiga marufuku Watazamaji kufuatia Vifo vilivyotokea Uwanjani mwanzoni mwa Mwaka, Bao la ushindi la Al Ahly lilifungwa na Mohamed ‘Geddo’ Nagui katika Dakika ya 28 baada ya kupokea pasi ya Hossam Ghaly.


Juzi Jumamosi, katika Nusu Fainali nyingine, Esperance iliitoa TP Mazembe ya Congo DR kwa Bao 1-0 baada ya kutoka 0-0 katika Mechi ya kwanza.


Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Al Ahly kutinga Fainali tangu watwae Ubingwa Mwaka 2008 lakini kwa Mabingwa watetezi Esperance hii ni Fainali yao ya tatu mfululizo.


Fainali hiyo itachezwa hapo Ijumaa Novemba 2 Mjini Cairo, Misri na marudiano ni Ijumaa Novemba 16 huko Tunis, Tunisia.


Mshindi wa Fainali hiyo atatawazwa kuwa Klabu Bingwa Afrika na kuzoa kitita cha Dola Milioni 1 na Nusu na pia ataiwakilisha Afrika katika Mashindano ya FIFA ya kusaka Klabu Bingwa Duniani yatakayochezwa huko Japan Mwezi Novemba.

 

 

ULAYA: La Liga na Serie Jumapili!


Radamel Falcao ni moto mwishoni, Atletico bega kwa began na Barca!!
FALCAO-ATLETICOMATOKEO/RATIBA:
Jumapili Oktoba 21
Getafe 0 Levante 1
Espanyol 3 Rayo Vallecano 2
Granada 1 Real Zaragoza 2
Osasuna 0 Real Betis 0
Real Sociedad 0 Atlético Madrid 1
Jumatatu Oktoba 22
Sevilla FC v Mallorca [Estadio Ramon Sanchez Pizjuan]
================================
Radamel Falcao alifunga Bao la miujiza la frikiki dakika ya mwisho na kuipa ushindi Atletico Madrid na kuwafanya wafungane kwa Pointi 22 na FC Barcelona kileleni mwa La Liga.
Hilo lilikuw ni bao la Falcao la 9 kwenye Ligi msimu huu na ushindi ho wa jana umewafanya Atletico Madrid washinde Mechi 7 za Ligi na kuwa Pointi 8 mbele ya Mahasimu wao wa Jiji la Madrid, Real Madrid ambao wapo nafasi ya 4.


RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumapili Oktoba 28
Athletic Bilbao v  Getafe [Estadio San Mamés]
Atlético Madrid v Osasuna [Vicente Calderon]
Celta Vigo v Deportivo La Coruña [Estadio Balaídos]
Espanyol v Málaga [Cornellà - El Prat]
Levante v Granada [Ciudad de Valencia]
Mallorca v Real Madrid [Estadio Son Moix]
Rayo Vallecano v Barcelona [Campo de Fútbol de Vallecas]
Real Betis v Valencia [Estadio Manuel Ruiz de Lopera]
Real Zaragoza v Sevilla FC [Estadio La Romareda]
Valladolid v Real Sociedad [Estadio Nuevo José Zorrilla]


Inter waifukuza Juve!
MATOKEO:
Jumapili Oktoba 21
Cagliari 1 Bologna 0
Atalanta 2 Siena 1
Chievo Verona 1 Fiorentina 1
Inter Milan 2 Catania 0
Palermo 0 Torino 0
Parma 2 Sampdoria 1
Udinese 1 US Pescara 0
Genoa 2 AS Roma 4
================================

Inter Milan wapo mbioni kuwafukuza vinara Ligi ya Italy Serie A Juventus baada ya kuichapa Catania bao 2-0 kwa bao za Antonio Cassano na Mchezaji wa Kimataifa wa Argentina Rodrigo Palacio na kuwafanya wawe nafasi ya 4 wakiwa Pointi 4 nyuma ya Juve.


Huu ni ushindi wa 4 mfululizo kwa Inter Milan na Novemba 3 watasafiri kwenda kuwavaa Juventus.
Katika Mechi nyingine iliyochezwa Jumapili, AS Roma, wakiongozwa na Francesco Totti, walitoka nyuma kwa bao 2 walizofungwa ndani ya Robo saa na kuibuka washindi kwa bao 4 dhidi ya Genoa kwa bao za Totti, Pablo Osvaldo, bao mbili, na Erik Lamela.


Bao la To tti ni bao lake la 217 kwenye Serie A na kumfanya awe Mfungaji Bora wa 3 katika Historia ya Serie A.

Kabla ya Bao hilo, Totti alikuwa amefungana kwenye nafasi ya 3, kwa kuwa na Bao 216, pamoja na Giuseppe Meazza (Inter, AC Milan, Juventus) na Jose Altafini (AC Milan, Napoli, Juventus).
Ushindi huu umewafanya AS Roma wakamate nafasi ya 5 wakiwa Pointi 8 nyuma ya vinara Juventus.


RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumamosi Oktoba 27
Siena v Palermo Artemio Franchi
AC Milan v Genoa [San Siro]

Jumapili Oktoba 28
Catania v Juventus [Stadio Angelo Massimino]
Bologna v Inter Milan [Stadio Renato Della`Ara]
Fiorentina v Lazio [Stadio Artemio Franchi]
Sampdoria v Cagliari [Comunale Luigi Ferraris]
Torino v Parma [Stadio Olimpico Grande Torino]
US Pescara v Atalanta [Adriatico]
AS Roma v Udinese           [Stadio Olimpico]
Napoli v Chievo Verona [Stadio San Paolo]

 

 

UEFA CHAMPIONZ LIGI: NI TENA Jumanne na Jumatano!!


>>KIMBEMBE: Arsenal v Schalke!
>>MAN CITY ugenini AJAX, MAN UTD nyumbani na BRAGA!
UEFA_CHAMPIONZ_LIGI_LOGO-BOMBAZRATIBA MECHI ZIJAZO:
[MECHI ZOTE Saa 3 Dakika 45 Usiku isipokuwa inapotajwa]
Jumanne Oktoba 23
FC Nordsjælland v Juventus
FC Shakhtar Donetsk v Chelsea FC

FC BATE Borisov v Valencia CF
LOSC Lille v FC Bayern München
FC Spartak Moskva v SL Benfica [SAA 1 USIKU]
FC Barcelona v Celtic FC
Galatasaray A.S. v CFR 1907 Cluj
Manchester United FC v SC Braga
Jumatano Oktoba 24
FC Porto v FC Dynamo Kyiv
GNK Dinamo v Paris SaintvGermain FC
Arsenal FC v FC Schalke 04
Montpellier Hérault SC v Olympiacos FC
FC Zenit St. Petersburg v RSC Anderlecht [SAA 1 USIKU]
Málaga CF v AC Milan
AFC Ajax v Manchester City FC
Borussia Dortmund v Real Madrid CF
++++++++++++++++++++++++++


ZIFUATAZO NI DONDOO FUPI ZA MVUTO KUHUSU MECHI HIZO:
Jumanne Oktoba 23
KUNDI E
-FC Nordsjælland v Juventus
-FC Shakhtar Donetsk v Chelsea FC
Hii ni mara ya kwanza kwa Nordsjælland kucheza na Timu kutoka Italy lakini Juventus washawahi kuivaa Timu ya Denmark mara moja.
Kwa Chelsea, ni mara ya kwanza kwao kucheza na Timu kutoka Ukraine lakini kwa Shakhtar hii ni mara ya 4 katika Misimu mitano kucheza na Timu kutoka England na mara ya mwisho, kwenye Msimu wa 2010/11, waliifunga Arsenal 2-1.


KUNDI F
-FC BATE Borisov v Valencia CF
-LOSC Lille v FC Bayern München
BATE hawajahi kuifunga Klabu kutoka Spain.
Mchezaji wa Lille, Salomon Kalou, alikuwemo kwenye Kikosi cha Chelsea kilichoibwaga Bayern Munich kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI Mwezi Mei Mwaka huu na kutwaa Ubingwa.


KUNDI G
-FC Spartak Moskva v SL Benfica
-FC Barcelona v Celtic FC
Wakiwa na Arsenal, Wachezaji wa sasa wa Barcelona, Cesc Fàbregas na Alex Song, waliwahi kuitwanga Celtic jumla ya Mabao 5-1 katika Mechi mbili za Msimu wa 2009/10 wa UEFA CHAMPIONZ LIGI.


KUNDI H
-Galatasaray AŞ v CFR 1907 Cluj
-Manchester United FC v SC Braga
Kocha wa Braga, José Peseiro, aliwahi kuwa Msaidizi wa Carlos Queiroz wakiwa Real Madrid kwenye Msimu wa Mwaka 2003/4 na Carlos Queiroz aliwahi, mara mbili, kuwa Msaidizi wa Sir Alex Ferguson wa Manchester United.
Jumatano Oktoba 24


KUNDI A
-FC Porto v FC Dynamo Kyiv
-GNK Dinamo Zagreb v Paris SaintvGermain FC
Porto na Dynamo washawahi kukutana Msimu wa 2008/09 kwenye hatua ya Makundi na kila mmoja alimfunga mwenziwe ugenini.
Dinamo wameshapoteza Mechi 4 kati ya 6 walizocheza nyumbani dhdi ya Klabu za France.


KUNDI B
-Arsenal FC v FC Schalke 04
-Montpellier Hérault SC v Olympiacos FC
Schalke hawajawahi kuifunga Timu yeyote ya England katika Mechi zao 5 za Ulaya walizocheza England na kuambua sare ya 2-2 na Wolves mwaka 1958/9 kwenye Kombe la Washindi la Ulaya.
Olympiacos walishinda huko France katika Mechi yao ya mwisho walipoichapa Marseille 1-0 Msimu uliopita lakini wameshafungwa Mechi 8 kati ya 12 walizocheza France.


KUNDI C
-FC Zenit St Petersburg v RSC Anderlecht
-Málaga CF v AC Milan
Kocha wa Zenit Luciano Spalletti hajawahi kufungwa na Klabu ya Ubelgiji katika maisha yake ya Ukocha kuanzia huko kwao Italy akiwa na Smpdoria.
Huu ni Msimu wa pili Barani Ulaya kwa Malaga na hawajawahi kufungwa nyumbani kwenye Mashindano ya Ulaya.


KUNDI D
-AFC Ajax v Manchester City FC
-Borussia Dortmund v Real Madrid CF
Kocha wa Ajax Frank de Boer alianza kuchezea Mechi za Kimataifa kwa Nchi yake Holland Septemba 1990 kwenye Mechi waliyofungwa 1-0 na Timu ya Italy ambayo Meneja wa Manchester City,Roberto Mancini, aliingizwa katika Dakika ya 55 kuichezea Italy huku Msaidizi wa sasa wa Frank de Boer, Dennis Bergkamp, akicheza Mechi hiyo akitokea benchi.
Katika Mechi 23 za Real Madrid zilizopita za kucheza ugenini na Klabu za Germany wamefungwa Mechi 16 na kushinda moja tu nayo ni ile dhidi ya Bayer Leverkusen Mwaka 2000/1 waliposhinda 3-2.
+++++++++++++++++++++++++++


MSIMAMO
[Kila Timu imecheza Mechi 2]
KUNDI A
1 Porto Pointi 6
2 PSG 3
3 Dinamo Kiev 3
4 Dinamo Zagreb 0


KUNDI B
1 Arsenal Pointi 6
2 Schalke 4
3 Montpellier 1
4 Olympiacos 0


KUNDI C
1 Malaga Pointi 6
2 AC Milani 4
3 Anderlecht 1
4 Zenit St Petersburg 0
KUNDI D
1 Real Madrid Pointi 6
2 Borussia Dortmund 4
3 Manchester City 1
4 Ajax 0


KUNDI E
Chelsea Pointi 4
Shakhtar Donetsk 4
Juventus 2
Nordsjaelland 0


KUNDI F
BATE Bprisov Pointi 6
Valencia 3
Bayern Munich 3
Lille 0


KUNDI G
Barcelona Pointi 6
Celtic 4
Benfica 1
Spartak Moscow 0


KUNDI H
Manchester United Pointi 6
CFR Cluj 3
Braga 3
Galatasaray 0

 

 

UEFA YAMBANA TERRY.

BEKI wa klabu ya Chelsea ataamriwa na Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA kuvaa kitambaa mkononi chenye maandishi ya kupinga ubaguzi wa rangi michezoni kama atapewa unahodha wa klabu hiyo wakati wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Shakhtar Donetsk kesho usiku. 
 
 
Hatua hiyo imekuja ikiwa ni wiki moja imepita toka nyota huyo alipoadhibiwa na Chama cha Soka nchini Uingereza-FA kwa kumfanyia vitendo vya kibaguzi beki wa Queens Park Rangers Anton Ferdinand. 
 
 
Katika michuano hiyo ya ligi ya mabingwa ambayo itachezwa leo na kesho manahodha wa vilabu vyote vinavyoshiriki michuano hiyo watatakiwa kuvaa vitambaa vyenye maandishi hayo ikiwa ni kuadhimisha wiki ya kupiga vita vitendo hivyo michezoni.
 
 
 Wiki iliyopita Terry alikubali adhabu ya kufungiwa michezo minne na kutozwa faini ya paundi 220,000 adhabu ambayo atakuwa akiitumikia katika michezo ya mashindano ya nyumbani pekee.
 
 
 
 Katika taarifa iliyotolewa na UEFA timu zote zitakazocheza michuano hiyo wiki hii zitasindikizwa na watoto ambao watakuwa wamevalia fulana zenye maandishi ya kupiga vita ubaguzi huku manahodha wakiwa wamevaa maandishi hayo katika vitambaa mikononi mwao.

 

 

NI NGUMU UBAGUZI KUTOKOMEZWA MOJA KWA MOJA.

MENEJA wa klabu ya Queens Park Rangers-QPR, Mark Hughes ameonya kuwa itakuwa ni suala lisilowezekana moja kwa moja kuondoa tatizo la ubaguzi wa rangi michezoni. 
 
 
Zaidi ya wachezaji 30 kutoka vilabu nane vya Ligi Kuu ya nchini Uingereza walioamua kutovaa fulana za Kick It Out mwishoni mwa wiki fulana ambazo ni mahsusi kwa ajili ya kampeni za kupinga ubaguzi michezoni. 
 
 
Mmoja wapo ya wachezaji ambao hawakuvaa fulana hizo ni pamoja na beki wa QPR Anton Ferdinand ambaye alikumbwa na tatizo la kubaguliwa na nahodha wa Chelsea John Terry msimu uliopita. 
 
 
Hughes amesema kuwa ni vigumu kulitokomeza tatizo la ubaguzi moja kwa moja kama jitihada za makusudi kama kuongeza adhabu kwa watu wanaofanya vitendo hivyo hazitachukuliwa ili kulipa kipaumbele suala hilo.
 
 
 Ferdinand aliungana na wachezaji wenzake Djibril Cisse, Shaun Wright-Phillips, Nedum Onouha na Junior Hoilett kutovaa fulana hizo ili kushinikiza hata kali zaidi zichukuliwe kwa watu wenye vitendo vya kibaguzi.

 

KABLA YA KUJA URUSI NILITAKA KUJIUNGA NA PSG - ETO'O.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi, Samuel Eto’o ameweka wazi kuwa aliwahi kufanya mazungumzo na klabu ya Paris Saint-German-PSG katika kipindi cha majira ya kiangazi.
 
 
 Eto’o mwenye umri wa miaka 31 ambaye alihamia klabu hiyo tajiri nchini Urusi msimu uliopita akitokea Inter Milan kwa ada ambayo inaaminika kumfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani. 
 
 
 
Mshambuliaji huyo kimataifa wa Cameroon amekiri kuwa kabla ya kwenda nchini Urusi alikaribia kujiunga PSG lakini hawakufikia muafaka katika mazungumzo yao na kuamua kumfuata Zlatan Ibrahimovic. 
 
 
Pamoja na mazungumzo aliyofanya na PSG Eto’o ambaye amewahi pia kcheza katika klabu ya Barcelona amesisitiza ana furaha kuwepo nchini Urusi katika klabu hiyo wakati pia anajipanga kuisaidia timu yake ya taifa katika michezo yake ya kimataifa baada ya kuerejea tena kwenye timu hiyo.

 

 

VENUS WILLIAMS AKATA KIU YA MATAJI.

MCHEZA tenisi nyota kutoka Marekani, mwanadada Venus Williams amekata kiu ya miaka miwili ya kutoshinda taji lolote baada ya kunyakuwa taji la michuano ya wazi ya Luxembourg likiwa ni taji la 44 toka aanze kucheza tenisi. 


Williams mwenye umri wa miaka 32 ambaye alikuwa anacheza fainali yake ya 71 toka aanze kucheza mchezo huo alifanikiwa kumfunga Monica Niculescu mwenye umri wa miaka 25 kutoka Romania kwa seti 2-0 zenye alama za 6-2 6-3. 


 Williams ni mmoja wapo ya wachezaji ambao bado wanacheza mchezo huo wenye mataji mengi zaidi akitanguliwa na mdogo wake Serena ambaye ana mataji 45 na ana anafasi ya kuongeza taji lingine katika michuano ya WTA inayotarajiwa kufanyika jijini Istanbul baadae wiki hii.


 Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Venus amesema kuwa alifanya jitihada kubwa kuhakikisha anafika fainali katika michuano hiyo na anamshukuru mungu azma yake imefanikiwa na anatgemea kufanya vizuri zaidi kabla hajaamua kustaafu mchezo huo. 


Mara ya mwisho Williams kushinda taji ilikuwa ni katika michuano ya Acapulco Februari mwaka 2010 ambapo baada ya hapo kiwango chake kikaporomoka.