Tuesday, October 9, 2012

TENGA AZITAKA KAMATI ZA UCHAGUZI KUSIMAMIA KANUNI

Tenga katikati akizungumza na Waandishi leo. Kulia ni Sunday Kayuni na kushoto Angetile Osiah

RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amezitaka Kamati za Uchaguzi kufanya kazi kwa kuzingatia Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF ili kuwa na uchaguzi huru na wa haki.
 
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo, makao makuu ya TFF, Ilala, Dar es Salaam, Tenga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), amesema uongozi wa mpira wa miguu unahitaji uamuzi mgumu, hivyo Kamati za Uchaguzi ambazo zimeundwa kwa mujibu wa Katiba zinatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni na si kuangalia sura za watu.
 
Amepongeza kamati zilizosimamia uchaguzi kwa kufuata kanuni, na ingawa kila mtu ana haki ya kuongoza, jambo lolote lazima liwe na kanuni, kwani hata kwenye mikutano ya hadhara kuna kanuni.
 
“Huwezi kufika kwenye mkutano wa hadhara na wewe unaanzisha mkutano wako. Lazima kanuni ziheshimiwe ili kufanya uchaguzi uwe huru na wa haki. Nini kimetokea kwenye maeneo ambayo kuna matatizo? Kila mwanachama wetu (mkoa/chama shiriki) ana Kamati ya Uchaguzi ambayo imeundwa kwa mujibu wa kanuni.
 
“Zile kamati hazitekelezi majukumu yake, unampitisha mtu unajua hana sifa unasema acha akafie mbele (Kamati ya Uchaguzi ya TFF). Kanuni zinasema jaza fomu mwenyewe, weka nakala za vyeti na si kwamba huyu tunamjua. Kanuni zinatakiwa zifuatwe, ukienda kinyume unaondolewa,” amesema.
 
Amesisitiza kamati zifanye kazi kwa kufuata kanuni ili kusaidia mpira wa miguu kwani zimeundwa kihalali, kwa hiyo zisiogope kuengua hata walioziteua kama hawana sifa.
 
Pia Rais Tenga amezitaka Kamati za Utendaji na Sekretarieti kutoziingilia Kamati za Uchaguzi katika mchakato wa uchaguzi, badala yake zinatakiwa kuziwezesha tu (facilitation).
 
Amesema baadhi ya wagombea nao ni tatizo kwani wanaingia kwenye uchaguzi bila kuzielewa Katiba za vyama vyao na Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF, hivyo ni vizuri wakazielewa kwanza.
 
Rais Tenga amesema ni vizuri wanachama wote wakafanya uchaguzi kabla ya uchaguzi wa TFF utakaofanyika Desemba mwaka huu ili wapate fursa ya kupiga kura kwenye uchaguzi huo wa shirikisho.
 
Amewataka pia wadau kujitokeza kwa wingi kuwania uongozi kwenye chaguzi za vyama wanachama wa TFF, kwani mwitikio umeonekana kuwa mdogo kulinganisha na umaarufu wa mchezo wenyewe.
 
Amepongeza vyama vya mikoa ambavyo tayari vimefanya uchaguzi wao. Baadhi ya vyama hivyo ni Arusha, Dodoma, Iringa, Kagera, Kigoma, Kilimanjaro, Manyara, Mara, Morogoro, Mtwara na Singida.

AIRTEL YAHIMIZA WATANZANIA KUCHANGIA MRADI WA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

Afisa uhusiano na matukio  wa Airtel  Dangio Kaniki akiwapatia chai watoto shule ya Uhuru Mchanganyiko wakati Airtel ilipotembelea shule hiyo  itakayofaidika na mpango maalumu wa  Airtel kwa kushirikiana na BAMVITA wenye lengo la kuchangia vitabu kwa watoto wenye mahitaji maalum .  Airtel imeanza kutembelea shule zilizopo Dar es Salaam pamoja na mikoani na kubainisha matatizo wanayokumbana nayo ili kuona namna ya kuwasaidia watoto hao wenye mahitaji maalum.

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel imewahimiza watanzania kuendelea kuchangia katika mradi wa kuchangia vifaa kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalum unaoendeshwa na Kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na  Baraza la maendeleo ya vitabu Tanzania (Bamvita)
 
Afisa uhusiano na matukio wa Airtel Dangio Kaniki amesema kampuni hiyo ikiwa na Balozi wake, AY imeanza kutembelea shule zilizopo Dar es Salaam pamoja na mikoani na kubainisha matatizo wanayokumbana nayo ili kuona namna ya kuwasaidia watoto hao wenye mahitaji maalum. Airtel inaamini kwamba watoto hao wenye mahitaji maalum wakiwezeshwa kielimu wataweza kutimiza ndoto zao na kuchangia katika maendeleo ya kiuchumi nchini.
 
Akiongea wakati walipotembelea shuleni hapo Meneja huduma kwa jamii Hawa Bayumi alisema ” Ni matumaini yetu kuwa watanzania na wale wasio watanzania kwa ujumla wataendelea kutuunga mkono ili kuweza kutimiza lengo hili la awali na kisha kuongeza shule za mikoani mara baada ya kukamilisha mahitaji haya katika shule hizi za Dar es Salaam.
 
 Kampeni hii itaendeshwa kwa muda wa miezi mitatu , na watanzania wanaweza kuchangia kwa kutuma neno “Vitabu”  kwenda namba 15626  na utakuwa umechangia shilingi 200 katika mradi huu au kupitia Airtel Money unapiga *150*60# ingiza jina la biashara VITABU na kuchangia kiwango chochote kile. Tunachukua fulsa hii  kuwaomba  watanzania wote kuchangia ili kuwafikia watoto wengi zaidi nchin”
 
Nae Mwalimu Mkuu wa shule ya Uhuru Mchanganyiko Anna Mang'enya amesema “shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo uhaba wa vifaa vya kufundishia. bila vifaa hivyo maalum itakuwa vigumu kwa wanafunzi kutimiza ndoto zao zakuendelea kielimu”.
 
Aidha Ameishukuru Airtel na BAMVITA kwa kuweza kuanzisha mradi huu na kuweza kuwahamasisha watanzania kuchangia ili waweze kupata vitendea kazi  na kuongeza kuwa shule hiyo bado inakabiliwa na changamoto nyingi katika elimu hivyo kuiomba kampuni hiyo kuendelea kuisaidia katika mambo mengine.
 
Zena Yahaya Mwanafunzi Uhuru Mchanganyiko alikuwa na haya ya kuongeza “tunawashukuru Airtel kwa kuja kututembelea leo, tunawaomba watanzania wote waendelee kutusaidia kwa kushirikiana na Airtel  katika mradi huu wa Vitabu ili kuweza kutusaidia katika kununua vifaa vya kutusaidia hapa shuleni na kuhakikisha tunapata elimu bora.”
 
Airtel inatambua umuhimu wa Elimu na tunaamini Tanzania itajengwa na sisi wenyewe hivyo basi lengo la  mradi huu ni kutoa nafasi kwa jamii yetu kuweza kuchangia elimu  ya msingi kwa watoto wenye mahitaji maalum kwa kuwanunulia vitabu na nyenzo za walimu kufundishia. Kwa kuanzia tumeanza kutembelea shule mbili za jijinini Dar es Salaam zitafaidika na mpango huu ambazo ni Sinza Maalum, Uhuru Mchanganyiko ikifuatiwa na Buguruni Viziwi.
Afisa uhusiano na matukio  wa Airtel  Dangio Kaniki akinywa chai pamoja na watoto wa shule ya Uhuru Mchanganyiko wakati Airtel ilipotembelea shule hiyo  itakayofaidika na mpango maalumu wa  Airtel kwa kushirikiana na BAMVITA wenye lengo la kuchangia vitabu kwa watoto wenye mahitaji maalum .  Airtel imeanza kutembelea shule zilizopo Dar es Salaam pamoja na mikoani na kubainisha matatizo wanayokumbana nayo ili kuona namna ya kuwasaidia watoto hao wenye mahitaji maalum.

FAKI ATISHA KWA MABAO LIGI KUU ZANZIBAR

Na Ally Mohamed, Zanzibar
MSHAMBULIAJI wa Chipukizi, Faki Mwalim ndiye anayeongoza kwa mabao kwa kupachika wavuni mabao matano mpaka sasa, katika Ligi Kuu ya Grand Malt inayoendelea.
Timu zote mpaka sasa zimeshuka uwanjani mara tano, huku Bandari ikiwa inaongoza ligi hiyo kwa kujikusanyia pointi 13, huku Falcon ikiburuza mkia ikiwa na pointi moja tu.
Wakati Faki akiongoza kwa mabao hayo, anafuatiwa kwa karibu na Ali Manzo Mnyovela wa Mtende mwenye mabao manne, huku waliofunga matatu wakiwa ni Mohd Abdurahim wa Mtende na Amour Suleiman anayekipiga Malindi.
Wengine na timu wanazotoka kwenye mabano ni Mussa Omar (Malindi), Mfaume Shaaban (Jamhuri) na Jaku Joma Jaku (Mafunzo), huku aliyepachika mawili akiwa Haitham Khamis (Bandari).
Pamoja na Bandari kuongoza ligi hiyo kwa kujikusanyia pointi hizo, inafuatiwa kwa karibu zaidi na Mtende yenye pointi 10.
Duma ndio yenye kadi nyingi za njano, ikiwa mpaka sasa wachezaji wake wameonyeshwa kadi hizo mara 12, ikiwa pia na kadi moja nyekundu. Mafunzo na Zimamoto kila moja ina kadi mbili nyekundu.
Ligi Kuu ya Grand Malt inatarajiwa kuendelea tena leo kwa mchezo mmoja, wakati Mafunzo itakapoikaribisha Chuoni katika Uwanja wa Amaan, wakati kesho Mtende itakuwa na kibarua kizito kwa KMKM katika uwanja huo.
Jumamosi Malindi itaivaa Chikupikizi ndani ya Uwanja wa Amaan, huku kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba kukiwa na pambano kati ya Duma na Mundu na siku inayofuata Mafunzo ikiivaa Jamhuri ndani ya Amaan.
Ligi Kuu ya Zanzibar ambayo kwa sasa inajulikana kama Grand Malt Premier League inadhaminiwa na kinywaji cha Grand Malt kisicho na kilevi.

KAMATI YA MGONGOLWA KUKUTANA KUJADILI TENA SAKATA LA MBUYU TWITE NA YANGA NA SIMBA

Alex Mgongolwa

MWENYEKITI wa Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wakili Alex Mgongolwa amesema kwamba Kamati yake itakutana tena hivi karibuni, kujadili hatua za kuichukulia klabu ya Yanga kwa kukaidi agizo la kuilipa Simba SC fedha alizochukua mchezaji wao, Mbuyu Twite dola za Kimarekani 32,000.
 
Akizungumza naTANO JUMA KWA NJIA YA SIMU mida hii’, Mgongolwa alisema kwamba tayari amekwishamuagiza Katibu wa TFF, Angetile Osiah aitishe kikao cha Kamati hiyo, kujadili zaidi sakata hilo.
 
“Tutakutana kujadili na kuamua hatua za kuchukua, unajua maamuzi ya awali ya Kamati, yalikuwa Yanga walipe hizo fedha hadi kufika Oktoba 3, lakini kwa kuwa wameshindwa kufanya hivyo, inabidi Kamati ikutane tena kujadili hatua za kuchukua.
 
Ndiyo maana hata wale waliotaka Yanga wakatwe fedha hizo katika mapato yao ya milangoni, ilishindikana kwa kuwa hayo hayakuwa maamuzi ya Kamati yetu,”alisema Mgongolwa.
 
Septemba 10, mwaka huu Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji, iliitaka Yanga kulipa dola 32,000 za Simba alizochukua Twite ndani ya 21, ambazo ziliisha Oktoba 3, mwaka huu.
 
Hatua hiyo, ilifuatia baada ya Twite kusaini Simba na baadaye kuikana klabu hiyo na kusaini Yanga aliyojiunga nayo.
Wajumbe sita kati ya saba waliopo walihudhuria kikao hicho chini ya Mwenyekiti Alex Mgongolwa. Wajumbe hao ni Hussein Mwamba, Imani 
 
Madega, Ismail Aden Rage, Llyod Nchunga na Omari Gumbo.
Ikumbukwe kesi ya msingi ilikuwa ni malalamiko ya Simba kufanyiwa mchezo usio wa kiungwana na watani wao hao wa jadi, Yanga kwa kuingilia usajili wao kwa Twite na kumsaini beki huyo wakati tayari amekwishaingia mkataba na Simba.

TENGA ASEMA YANGA NA VODACOM WATAJUA WENYEWE

Rais wa ^TFF, Leodegar Chilla Tenga (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari. Kulia kwake ni Sunday Burton Kayuni, Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF na kushoto Katibu, Angetile Osiah Malabeja.

RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Chillah Tenga amesema kwamba kwa sasa shirikisho lake linawaachia wadhamini wa Ligi Kuu, Vodacom watumie busara kumalizana na klabu ya Yanga, juu ya mgogoro wao kuhusu nembo ya ligi hiyo.
 
Akijibu swali la TANO JUMA KWA NJIA YA SIMU katika Mkutano wake maalum na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya TFF, kuzungumzia masuala ya uchaguzi wa vyama mbalimbali vya soka nchini, Tenga alisema kwamba kwa kuwa msimu uliopita Vodacom walimalizana na Yanga bila kulishirikisha shirikisho lake, na mwaka huu wanawaachia pia.
 
“Kitendo kilichofanywa na Vodacom mwaka jana, kumalizana na Yanga bila kutushirikisha kuhusu utata wa nembo, sisi tulijua kitaleta matatizo baadaye, na kweli sasa yametokea, na ndiyo maana unaweza kuona, sekretarieti yetu inalipeleka taratibu hili suala,”alisema Tenga.
 
Tenga alisema Vodacom ingewaacha TFF msimu uliopita wakaihukumu Yanga kwa mujibu wa kanuni, hata msimu huu ingekuwa rahisi kwao kuingilia, lakini kwa kuwa msimu uliopita waliingilia na wakaibadilishia klabu hiyo nembo, basi na msimu huu pia wanawaachia wamalizane wenyewe.
 
Mwaka jana Yanga waligoma kuvaa jezi zenye nembo ya wadhamini wa Ligi Kuu, Vodacom kwa sababu zina nembo nyekundu hadi kampuni hiyo ikawabadilishia na kuwapa jezi maalum zenye nembo nyeusi.
 
Mwaka huu pia, Yanga wamekataa kubandikiwa nembo za Vodacom kwenye jezi zao kwa sababu ya rangi hiyo nyekundu na jana wamecheza mechi ya sita bila kuvaa nembo ya mdhamini, wakisistiza wabadilishiwe.
 
Wakati huo huo, kanuni za Ligi Kuu zinasema timu itakayogoma kuvaa nembo ya mdhamini itashushwa Daraja, ingawa tishio hilo la kanuni sasa linapozwa na kauli ya Tenga leo. 

YANGA WAKANUSHA KULALA 'MZUNGU WA NNE' BUKOBA

Mwalusako akizungumza na Waandishi wa Habari Jangwani leo

KATIBU wa Yanga, Lawrence Mwalusako amesema kwamba timu yao ilifungwa kimchezo na labda kwa mbinu nyingine kwenye mechi ya jana dhidi ya Kagera Sugar, lakini si kwa sababu ya malazi mabaya wala lishe mbovu.
 
Mwalusako aliyezungumza na Waandishi wa Habari ‘hivi punde’ makao makuu ya klabu hiyo, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, alikuwa anakanusha habari zilizoandikwa na gazeti moja leo, kwamba wachezaji wake walilala wawili wawili kitanda kimoja mjini Bukoba.
 
“Hizi habari si kweli, wachezaji wetu walilala vizuri tu, tunasikitishwa na habari za kizushi kama hizi, tunapenda kukanusha kwa nguvu zote,”alisema.
 
Mwalusako alisema kufungwa kwao Kagera kumetokana na matokeo ya kawaida ya mchezo na sasa kuelekea mechi ya Alhamisi dhidi ya Toto African mjini Mwanza wataongeza nguvu.
 
“Kuna viongozi wataenda Mwanza kuongeza nguvu, ili kuhakikisha tunashinda mechi hiyo, wanakwenda kwa ajili ya kuwahamasisha wachezaji,”alisema Mwalusako.  
 
Bao pekee la Themi Felix katika dakika ya 67, jana liliwapa Kagera Sugar ushindi wa 1-0 dhidi ya Yanga SC, kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
 
Felix aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mnigeria, Enyinna Darlington kwa kumtungua bao hilo, kipa Mghana wa Yanga, Yaw Berko, ameendeleza rekodi yake kuvifunga vigogo, Simba na Yanga katika Uwanja huo.
 
Hiyo inakuwa mechi ya pili Yanga kufungwa ndani ya mechi sita walizocheza hadi sasa na mbili wametoka sare- maana yake inabaki na pointi zake nane na kuzidi kujipunguzia matumaini ya ubingwa msimu huu, ikiwa sasa inazidiwa pointi nane na vinara wa ligi hiyo Simba SC.
 
Aidha, hii ni mechi ya pili Yanga inacheza chini ya kocha wake mpya, Mholanzi Ernie Blandts aliyerithi mikoba ya Mbelgiji, Tom Saintfiet na katika mechi hizo mbili ameambulia pointi moja kutokana na sare dhidi ya Simba Jumatano.  
 
Kwa ujumla Yanga haijashinda hata mechi moja ya ugenini kati ya tatu ilizocheza hadi sasa, ilitoka 0-0 na Prisons, ikafungwa 3-0 na Mtibwa na jana imechapwa 1-0 na Kagera Sugar, wakati Alhamisi itacheza na Toto African mjini Mwanza.
 
Katika mechi hiyo ya jana, Yanga ilipata pigo dakika ya 23 baada ya mshambuliaji wake mahiri na tegemeo, Said Bahanuzi ‘Spider Man’ kuchanika nyama za paja dakika ya 23, baada ya kugongana na beki Benjamin Effe wa Kagera Sugar na kushindwa kuendelea na mchezo, nafasi yake ikichukuliwa na Jerry Tegete.
 
Tangu ajiunge na Yanga akitokea Mtibwa Sugar msimu huu, leo Bahanuzi amecheza mechi ya 13 kwa dakika hizo 23 na ameifungia timu hiyo jumla ya mabao 12, matatu kati ya hayo kwa penalti.  

 Mchezaji wa yanga Oscar Joshua akiwa ndani ya chumba chake.
 Wachezaji wa timu ya Yanga, Omega Seme kulia na Frank Domayo kushoto wakiwa wamejipumzisha ndani ya vyumba vyao. Je, huu ni mzungu wa nne?

HANS POPPE AWAPA MAKAVU YANGA, AWAAMBIA WAACHE KUDEKA WACHEZE SOKA DUNIA IJIONEE

Hans Pope; Yanga acheni kudeka, chezeni soka

MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amewataka Yanga waache desturi ya kutafuta mchawi nje ya timu yao mambo yanapowaendea mrama na badala yake ya sasa waanze kuangalia matatizo yao ili kuyatatua.
 
Kauli hiyo ya Kapteni wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), inakuja kufuatia madai ya Yanga kwamba Simba wanatia ‘mkono’ kwenye mechi zao ndio maana zinakuwa ngumu.
 
“Tatizo la Yanga ni moja, wanapofanya vibaya, wanaanza kutafuta mchawi nje ya timu yao, ona sasa wanasema Simba wanatia mkono mechi zao, kivipi? Kwa uchawi au kwa nini?”alihoji Hans Poppe.
 
Hans Poppe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Friends Of Simba (F.O.S.) alisema kwamba kama Simba wanakwenda kwa timu ambazo zinacheza Yanga na kuwapa motisha wacheze kwa nguvu, haoni ubaya katika hilo, zaidi linasaidia maendeleo ya soka ya nchi hii.
 
“Lazima wakabiliane na upinzani, ili wakishinda waonekane wana timu imara, wasitake kushinda kwa urahisi rahisi, kwa hivyo ushauri wa bure tunaowapa Yanga, wao wacheze mpira, waache kutafuta mchawi, kwa sababu kama wana uwezo watashinda tu, hata timu ipewe motisha, watashinda kwa uwezo wao, ila kama hawana uwezo, ndio hivi saasa wanaanza kutafuta mchawi,”alisema.   
 
Yanga inadai Simba SC ‘wanatia mkono’ kwenye mechi zao na ndio maana zinakuwa ngumu, ila kuanzia sasa na wao wanaanza ‘fitina’.
 
Madai hayo yanakuja, baada ya jana kuchapwa bao 1-0 na Kagera Sugar katika mchezo wake wa sita wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, uliopigwa Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
 
“Simba ilituma watu Bukoba watie mkono mechi yetu, sisi tuliwashitukia hao watu baadaye sana, lakini tunashangaa kwa nini wanafanya hivi, wakati sisi tulizungumza nao tukakubaliana haya mambo tuyaache, tucheze mpira, sasa wao wanatuzunguka wanaendeleza mchezo mchafu,”alisema kiongozi Mjumbe mmoja wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, ambaye hakutaka kutajwa jina.
 
Mjumbe huyo alisema kwamba wao walijua baada ya makubaliano na Simba kutofanyiana fitina, waliamini mambo hayo hayatakuwapo, lakini baada ya kugundua wenzao wamewageuka sasa na wao wanaanza ‘mchezo huo’.
 
“Na sisi sasa tunaanza kuzicheza mechi zao, wakumbuke tu wao ndio walichokoza nyuki, sasa subirini kuanzia mechi yao na Coastal, wakishinda wao wanaume, na pamoja na kuzicheza mechi zao, tunajizatiti katika mechi zetu. Uzuri watu wote wanaowatumia tumekwishawajua, ni wale wale waliokuja Morogoro, na wale wale waliokuja Bukoba. Tumekwishawajua,”alisema Mjumbe huyo.   
 
Bao pekee la Themi Felix katika dakika ya 67, jana liliwapa Kagera Sugar ushindi wa 1-0 dhidi ya Yanga SC, kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
 
Felix aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mnigeria, Enyinna Darlington kwa kumtungua bao hilo, kipa Mghana wa Yanga, Yaw Berko, ameendeleza rekodi yake kuvifunga vigogo, Simba na Yanga katika Uwanja huo.
 
Hiyo inakuwa mechi ya pili Yanga kufungwa ndani ya mechi sita walizocheza hadi sasa na mbili wametoka sare- maana yake inabaki na pointi zake nane na kuzidi kujipunguzia matumaini ya ubingwa msimu huu, ikiwa sasa inazidiwa pointi nane na vinara wa ligi hiyo Simba SC.
 
Aidha, hii ni mechi ya pili Yanga inacheza chini ya kocha wake mpya, Mholanzi Ernie Blandts aliyerithi mikoba ya Mbelgiji, Tom Saintfiet na katika mechi hizo mbili ameambulia pointi moja kutokana na sare dhidi ya Simba Jumatano.  
 
Kwa ujumla Yanga haijashinda hata mechi moja ya ugenini kati ya tatu ilizocheza hadi sasa, ilitoka 0-0 na Prisons, ikafungwa 3-0 na Mtibwa na jana imechapwa 1-0 na Kagera Sugar, wakati Alhamisi itacheza na Toto African mjini Mwanza.
 
Katika mechi hiyo ya jana, Yanga ilipata pigo dakika ya 23 baada ya mshambuliaji wake mahiri na tegemeo, Said Bahanuzi ‘Spider Man’ kuchanika nyama za paja dakika ya 23, baada ya kugongana na beki Benjamin Effe wa Kagera Sugar na kushindwa kuendelea na mchezo, nafasi yake ikichukuliwa na Jerry Tegete.
 
Tangu ajiunge na Yanga akitokea Mtibwa Sugar msimu huu, leo Bahanuzi amecheza mechi ya 13 kwa dakika hizo 23 na ameifungia timu hiyo jumla ya mabao 12, matatu kati ya hayo kwa penalti. 
 
Katika mechi zilizochezwa juzi za ligi hiyo, Simba SC ilizidi kujiimarisha kileleni kufuatia ushindi wa mabao 4-1 ilioupata kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam dhidi ya JKT Oljoro ya Arusha, ambayo ilimaliza pungufu ya wachezaji wawili baada ya kipa wake Shaibu Issa na mshambuliaji Meshack Nyambele kutolewa kwa kadi nyekundu kipindi cha pili.
 
Katika mechi hiyo iliyochezeshwa na refa Amon Paul wa Mara, aliyesaidiwa na Anold Bugabo wa Singida na Charles Simon wa Dodoma, hadi mapumziko Simba walikuwa tayari mbele kwa mabao 2-1, mabao yake yote yakitiwa kimiani na kiungo Amri Ramadhan Kiemba katika dakika za 16 na 44, wakati la Oljoro lilifungwa na Paul Nonga dakika ya 29.
 
Kiemba alifunga bao la kwanza akiunganisha krosi pasi ya Christopher Edward, wakati bao la pili lilitokana na krosi ya Nassor Masoud ‘Chollo’, yote kutokana na mashambulizi ya upande wa kulia.
 
Ilikuwa rahisi kwa Kiemba kufunga mabao yote akiwa kwenye eneo la hatari, kutokana na mabeki wa Oljoro kumuwekea ulinzi zaidi Felix Sunzu.
Nonga naye alifunga bao lake baada ya kupewa pasi ndefu na kumpiga chenga kipa na Nahodha wa Simba, Juma Kaseja upande wa kulia mwa Uwanja na kuutumbukiza mpira nyavuni kiulaini.
 
Bao hilo lilitokana na beki Paul Ngalema kupokonywa mpira wakati amepanda kusaidia mashambulizi na Oljoro wakafanya shambulizi la haraka.
Kipindi cha pili Simba walirudi vizuri zaidi uwanjani na kuuteka zaidi mchezo- jambo ambalo liliwafanya Oljoro wawapunguze kasi kwa kuwachezea rafu. Hilo liliwagharimu kupoteza wachezaji wao wawili kabla ya filimbi ya mwisho na kufungwa mabao mawili zaidi.
 
Dakika ya 83 Mganda Emanuel Okwi aliifungia Simba bao la tatu na katika dakika ya tatu ya muda wa nyongeza baada ya kutimu dakika 90 za mchezo, Okwi akiwa anaelekea kufunga tena, alikwatuliwa na kipa wa Oljoro Shaibu Issa na refa akaamuru penalti sambamba na kumtoa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja mlinda mlango huyo.
 
Awali ya hapo, Oljoro ilimpoteza mchezaji mwingine, Nyambele dakika ya 78, ambaye alionyeshwa njano ya pili kwa rafu aliyomchezea Jonas Mkude. Nahodha Kaseja alitaka kwenda kupiga, lakini akazuiwa na Felix Mumba Sunzu akaenda kufunga bao la nne kwa mkwaju wa penalti.
 
Kwa ushindi huo, Simba imefikisha pointi 16 baada ya kucheza mechi sita, hivyo kuendelea kuongoza Ligi Kuu, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 13, ingawa imecheza mechi tano.
 
Katika mechi nyingine za jana, Mgambo imepata ushindi wake wa kwanza baada ya kuichapa Polisi Morogoro 1-0, wakati Toto African imeichapa JKT Ruvu 2-1 na Prisons imelazimishwa sare ya bila kufungana na Mtibwa Sugar. 

MILOVAN ASEMA AKUFFO TATIZO KIWANGO NDIO MAANA BENCHI

Daniel Akuffo mbele ya Mrisho Ngassa

KOCHA Mkuu wa Simba SC, Profesa Milovan Cirkovick amesema kwamba mshambuliaji mpya kutoka Ghana, Daniel Akuffo anatakiwa aongeze juhudi na kupandisha kiwango chake, ili apate nafasi kwenye kikosi cha kwanza, lakini kwa sasa ataendelea kuanzia benchi kwa kuwa anazidiwa uwezo na wachezaji wanaoanza.
Akizungumza baada ya mechi dhidi ya JKT Oljoro juzi, Mserbia huyo alisema kwamba Akuffo anaanzia benchi kwa sasa kwa sababu kuna wachezaji walio vizuri mno zaidi yake na ndio wanapewa nafasi. “Ajitahidi, atakapokuwa vizuri atapata nafasi ya kuanza, ila kwa sasa anazidiwa na wanaoanza,”alisema Milovan.
Daniel Akuffo aliyesajiliwa msimu huu kutoka ASEC Mimosa ya Ivory Coast, aliingia kwa kishindo      Simba akifunga katika mechi nne mfululizo, lakini baada ya hapo kasi yake imezimika na amefikisha jumla ya mechi 10, akiwa amefunga mabao matano tu, katika ligi bao moja tu. Katika mabao hayo matano aliyofunga jumla hadi sasa mshambuliaji huyo mrefu, mawili ni ya penalti.
Simba SC juzi ilizidi kujiimarisha kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa mabao 4-1 ilioupata kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam dhidi ya JKT Oljoro ya Arusha, ambayo ilimaliza pungufu ya wachezaji wawili baada ya kipa wake Shaibu Issa na mshambuliaji Meshack Nyambele kutolewa kwa kadi nyekundu kipindi cha pili.
Katika mechi hiyo iliyochezeshwa na refa Amon Paul wa Mara, aliyesaidiwa na Anold Bugabo wa Singida na Charles Simon wa Dodoma, hadi mapumziko Simba walikuwa tayari mbele kwa mabao 2-1, mabao yake yote yakitiwa kimiani na kiungo Amri Ramadhan Kiemba katika dakika za 16 na 44, wakati la Oljoro lilifungwa na Paul Nonga dakika ya 29.
Kiemba alifunga bao la kwanza akiunganisha krosi pasi ya Christopher Edward, wakati bao la pili lilitokana na krosi ya Nassor Masoud ‘Chollo’, yote kutokana na mashambulizi ya upande wa kulia.
Ilikuwa rahisi kwa Kiemba kufunga mabao yote akiwa kwenye eneo la hatari, kutokana na mabeki wa Oljoro kumuwekea ulinzi zaidi Felix Sunzu.
Nonga naye alifunga bao lake baada ya kupewa pasi ndefu na kumpiga chenga kipa na Nahodha wa Simba, Juma Kaseja upande wa kulia mwa Uwanja na kuutumbukiza mpira nyavuni kiulaini.
Bao hilo lilitokana na beki Paul Ngalema kupokonywa mpira wakati amepanda kusaidia mashambulizi na Oljoro wakafanya shambulizi la haraka.
Kipindi cha pili Simba walirudi vizuri zaidi uwanjani na kuuteka zaidi mchezo- jambo ambalo liliwafanya Oljoro wawapunguze kasi kwa kuwachezea rafu. Hilo liliwagharimu kupoteza wachezaji wao wawili kabla ya filimbi ya mwisho na kufungwa mabao mawili zaidi.
Dakika ya 83 Mganda Emanuel Okwi aliifungia Simba bao la tatu na katika dakika ya tatu ya muda wa nyongeza baada ya kutimu dakika 90 za mchezo, Okwi akiwa anaelekea kufunga tena, alikwatuliwa na kipa wa Oljoro Shaibu Issa na refa akaamuru penalti sambamba na kumtoa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja mlinda mlango huyo.
Awali ya hapo, Oljoro ilimpoteza mchezaji mwingine, Nyambele dakika ya 78, ambaye alionyeshwa njano ya pili kwa rafu aliyomchezea Jonas Mkude. Nahodha Kaseja alitaka kwenda kupiga, lakini akazuiwa na Felix Mumba Sunzu akaenda kufunga bao la nne kwa mkwaju wa penalti.
Kwa ushindi huo, Simba imefikisha pointi 16 baada ya kucheza mechi sita, hivyo kuendelea kuongoza Ligi Kuu, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 13, ingawa imecheza mechi tano.

YANGA WAWASHIKA 'UCHAWI' SIMBA SC KIPIGO CHA KAGERA

Yanga SC katika moja ya mechi zao, ambazo wanadai eti Simba wanatia mkono

YANGA SC imesema kwamba wamegundua Simba SC ‘wanatia mkono’ kwenye mechi zao na ndio maana zinakuwa ngumu, ila kuanzia sasa na wao wanaanza ‘fitina’.
Madai hayo yanakuja, baada ya jana kuchapwa bao 1-0 na Kagera Sugar katika mchezo wake wa sita wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, uliopigwa Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
“Simba ilituma watu Bukoba watie mkono mechi yetu, sisi tuliwashitukia hao watu baadaye sana, lakini tunashangaa kwa nini wanafanya hivi, wakati sisi tulizungumza nao tukakubaliana haya mambo tuyaache, tucheze mpira, sasa wao wanatuzunguka wanaendeleza mchezo mchafu,”alisema kiongozi Mjumbe mmoja wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, ambaye hakutaka kutajwa jina.
Mjumbe huyo alisema kwamba wao walijua baada ya makubaliano na Simba kutofanyiana fitina, waliamini mambo hayo hayatakuwapo, lakini baada ya kugundua wenzao wamewageuka sasa na wao wanaanza ‘mchezo huo’.
“Na sisi sasa tunaanza kuzicheza mechi zao, wakumbuke tu wao ndio walichokoza nyuki, sasa subirini kuanzia mechi yao na Coastal, wakishinda wao wanaume, na pamoja na kuzicheza mechi zao, tunajizatiti katika mechi zetu. Uzuri watu wote wanaowatumia tumekwishawajua, ni wale wale waliokuja Morogoro, na wale wale waliokuja Bukoba. Tumekwishawajua,”alisema Mjumbe huyo.   
Bao pekee la Themi Felix katika dakika ya 67, jana liliwapa Kagera Sugar ushindi wa 1-0 dhidi ya Yanga SC, kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Felix aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mnigeria, Enyinna Darlington kwa kumtungua bao hilo, kipa Mghana wa Yanga, Yaw Berko, ameendeleza rekodi yake kuvifunga vigogo, Simba na Yanga katika Uwanja huo.
Hiyo inakuwa mechi ya pili Yanga kufungwa ndani ya mechi sita walizocheza hadi sasa na mbili wametoka sare- maana yake inabaki na pointi zake nane na kuzidi kujipunguzia matumaini ya ubingwa msimu huu, ikiwa sasa inazidiwa pointi nane na vinara wa ligi hiyo Simba SC.
Aidha, hii ni mechi ya pili Yanga inacheza chini ya kocha wake mpya, Mholanzi Ernie Blandts aliyerithi mikoba ya Mbelgiji, Tom Saintfiet na katika mechi hizo mbili ameambulia pointi moja kutokana na sare dhidi ya Simba Jumatano.  
Kwa ujumla Yanga haijashinda hata mechi moja ya ugenini kati ya tatu ilizocheza hadi sasa, ilitoka 0-0 na Prisons, ikafungwa 3-0 na Mtibwa na jana imechapwa 1-0 na Kagera Sugar, wakati Alhamisi itacheza na Toto African mjini Mwanza.
Katika mechi hiyo ya jana, Yanga ilipata pigo dakika ya 23 baada ya mshambuliaji wake mahiri na tegemeo, Said Bahanuzi ‘Spider Man’ kuchanika nyama za paja dakika ya 23, baada ya kugongana na beki Benjamin Effe wa Kagera Sugar na kushindwa kuendelea na mchezo, nafasi yake ikichukuliwa na Jerry Tegete.
Tangu ajiunge na Yanga akitokea Mtibwa Sugar msimu huu, leo Bahanuzi amecheza mechi ya 13 kwa dakika hizo 23 na ameifungia timu hiyo jumla ya mabao 12, matatu kati ya hayo kwa penalti. 
Katika mechi zilizochezwa juzi za ligi hiyo, Simba SC ilizidi kujiimarisha kileleni kufuatia ushindi wa mabao 4-1 ilioupata kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam dhidi ya JKT Oljoro ya Arusha, ambayo ilimaliza pungufu ya wachezaji wawili baada ya kipa wake Shaibu Issa na mshambuliaji Meshack Nyambele kutolewa kwa kadi nyekundu kipindi cha pili.
Katika mechi hiyo iliyochezeshwa na refa Amon Paul wa Mara, aliyesaidiwa na Anold Bugabo wa Singida na Charles Simon wa Dodoma, hadi mapumziko Simba walikuwa tayari mbele kwa mabao 2-1, mabao yake yote yakitiwa kimiani na kiungo Amri Ramadhan Kiemba katika dakika za 16 na 44, wakati la Oljoro lilifungwa na Paul Nonga dakika ya 29.
Kiemba alifunga bao la kwanza akiunganisha krosi pasi ya Christopher Edward, wakati bao la pili lilitokana na krosi ya Nassor Masoud ‘Chollo’, yote kutokana na mashambulizi ya upande wa kulia.
Ilikuwa rahisi kwa Kiemba kufunga mabao yote akiwa kwenye eneo la hatari, kutokana na mabeki wa Oljoro kumuwekea ulinzi zaidi Felix Sunzu.
Nonga naye alifunga bao lake baada ya kupewa pasi ndefu na kumpiga chenga kipa na Nahodha wa Simba, Juma Kaseja upande wa kulia mwa Uwanja na kuutumbukiza mpira nyavuni kiulaini.
Bao hilo lilitokana na beki Paul Ngalema kupokonywa mpira wakati amepanda kusaidia mashambulizi na Oljoro wakafanya shambulizi la haraka.
Kipindi cha pili Simba walirudi vizuri zaidi uwanjani na kuuteka zaidi mchezo- jambo ambalo liliwafanya Oljoro wawapunguze kasi kwa kuwachezea rafu. Hilo liliwagharimu kupoteza wachezaji wao wawili kabla ya filimbi ya mwisho na kufungwa mabao mawili zaidi.
Dakika ya 83 Mganda Emanuel Okwi aliifungia Simba bao la tatu na katika dakika ya tatu ya muda wa nyongeza baada ya kutimu dakika 90 za mchezo, Okwi akiwa anaelekea kufunga tena, alikwatuliwa na kipa wa Oljoro Shaibu Issa na refa akaamuru penalti sambamba na kumtoa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja mlinda mlango huyo.
Awali ya hapo, Oljoro ilimpoteza mchezaji mwingine, Nyambele dakika ya 78, ambaye alionyeshwa njano ya pili kwa rafu aliyomchezea Jonas Mkude. Nahodha Kaseja alitaka kwenda kupiga, lakini akazuiwa na Felix Mumba Sunzu akaenda kufunga bao la nne kwa mkwaju wa penalti.
Kwa ushindi huo, Simba imefikisha pointi 16 baada ya kucheza mechi sita, hivyo kuendelea kuongoza Ligi Kuu, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 13, ingawa imecheza mechi tano.
Katika mechi nyingine za jana, Mgambo imepata ushindi wake wa kwanza baada ya kuichapa Polisi Morogoro 1-0, wakati Toto African imeichapa JKT Ruvu 2-1 na Prisons imelazimishwa sare ya bila kufungana na Mtibwa Sugar.

ZANZIBAR YAJITOA MICHUANO YA CAF 2012

Na Ally Mohamed, Zanzibar
WAWAKILISHI wa Zanzibar katika michuano ya Afrika mwakani, Super Falcon waliofuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika na Jamhuri waliofuzu kucheza Kombe la Shirikisho wamejitoa kwenye michuano hiyo.
Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Rais wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), Aman Ibrahim Makungu, zimesema kwamba timu hizo zimeamua kujitoa katika michuano hiyo kwa sababu hazina fedha, ambapo kila timu ilihitaji kiasi cha dola za Kimarekani 30,000, zaidi ya Sh. Milioni 45 kwa ajili ya maandalizi ya ushiriki wa michuano hiyo.
Kufuatia hatua hiyo ZFA, iko katika mazungumzo na baadhi ya klabu za Ligi Kuu ili kuona kama kuna uwezekano wa kupata timu zitakazochukua nafasi hizo.
Mwaka huu Zanzibar iliwakilishwa na timu ya Mafunzo katika ligi ya Mabingwa Afrika, huku Jamhuri wakipata nafasi ya kushirki katika kombe la Shirikisho.
Hata hivyo timu zote zilishindwa kufanya vizuri baada ya kuondolewa katika hatua ya mwanzo katika michuano hiyo.

YANGA YAPIGWA 1-0 KAITABA

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh  Kanali mstaafu Fabian Massawe akisalimiana na  waamuzi .PICHA ZOTE NA BUKOBASPORTS.COM
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh  Kanali mstaafu Fabian Massawe akisalimiana na wachezaji wa timu ya Kagera sugar

Timu zote mbili zikimsikiliza mkuu wa Mkoa wa Kagera
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh Kanali mstaafu Fabian Massawe akisalimiana na wachezaji wa timu zote mbili Yanga na Kagera Sugar.Timu zikisalimiana kabla ya mtanange jioni hii
Kikosi kamili cha Yanga kilichopewa  kichapo na wakata miwa wa Kagera Sukari jioni ya leo.

Waamuzi wa mpira wa kagera sugar na Yanga (OMARY JUMA - MWANZA, DOMINIQ NYAMSANA - DODOMA-HASSAN ZANI - ARUSHA - CHARLES MBILINYI- MWANZA NA JONESIA LUKYAA-BUKOBA)
Kikosi cha timu ya Kagera Sukari kilicho ifunga  timu ya Yanga 1-0  kwenye uwanja wa kaitaba mjini hapa

 Kocha wa Kagera Abdallah King Kibadeni (kulia) na wasaidizi wake 
Kocha wa Kagera Abdallah King Kibadeni akiendelea kufuatilia mtanange kwa makini 

Bench la Wachezaji wa Kagera Sukari.

Said Bahanuz aliumia na nafasi yake ikachukuliwa Jerson TegeteSaid Bahanuzi akiendelea kujipoza na maumivu ya nyama za pajani baada ya kupata matatizo

Meza kuu
Mkuu wa mkoa wa kagera (katikati) akiwa na Malik Suddy Tibabimale(katibu chama cha mpira BKM) wakifatilia kwa makini mpambano kati ya Kagera Sugar na Yanga.
Kagera Sugar wakifanya mabadiliko 
Hadi Half time hakuna timu iliyokuwa imemchungulia mwenzake.
Wapenzi wa soka Jukwaa la Golani maarufu kama Jukwaa la Balimi.Bench la timu ya Yanga

Wapenzi wa soka Jukwaa la Golani maarufu kama Jukwaa la Balimi. wakiangaliwa kwa makini Askari wa Ulinzi uwanjani hapo
Mdau wa Bukobasports.com akichukua matukio tayari kuyarusha live kwenye libeneke la bukobasports.com
Mashabiki jukwaa kuu 
Mashabiki jukwaa kuu namuona Mr. Mbelwa mpenzi wa soka akiwa ameshika maji jukwaani na huku akiendelea kucheki mtanange
Wadau mbalimbali wakifatilia soka na mimi nilikuwa moja wapo baada ya kuonekana hapa 

Mashabiki 

Mashabiki