Sunday, November 18, 2012

 

SERENGETI BOYS NA KONGO KATIKA PICHA LEO TAIFA

Kipa wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, ya Kongo Brazzaville, Ombandza Mpea Joe akilalama baada ya mpira wa adhabu uliopigwa na Mufathir Yahya Abbas kutinga nyavuni na kuwapa wenyeji ushindi wa 1-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni ya leo.

Bao pekee leo

Kipa wa Kongo akining'inia kwenye milingoti ya lango baada ya kuukosa mpira uliopaa juu ya lango lake

Mchezaji wa Serengeti, Suleiman Hamisi Bofu akipiga mpira kichwa mbele ya beki wa Kongo, Ondongo Boungena

Beki Okombi Francis wa Kongo akiokoa mbele ya Joseph Kimwaga 

Wachezaji wa Kongo wakimdhibiti mchezaji wa Serengeti

Hussein Twaha 'Messi' akiwafunga tela wachezaji wa Kongo

Makocha wa Serengeti Jacob Michelsen na Msaidizi wake Jamhuri Kihwelo wakiwapa maelekezo vijana wao wakati mpira uliposimama kwa muda

Kipa wa Serengeti Boys, Peter Manyika akiruka hewani kupangua mchomo mkali ulioelekezwa langoni mwake 

Kipa wa Kongo, akimdondokea kiungo wa Serengeti, Farid Mussa Shah kudaka mpira, huku beki wake, Ondongo Boungena akiwa tayari kumsaidia 

Farid kulia na Ondongo kushoto

Kikosi cha vijeba wa Kongo Brazzaville

Beki Ismail Adam Gambo wa Serengeti akimdhibiti Ibara Vinny wa Kongo Brazzazille

Hussein Twaha akiwatoka wachezaji wa Kongo

Serengeti wakishangilia bao lao kwa staili ya aina yake

11 wa kwanza wa Serengeti leo

Wachezaji wa Serengeti Boys wakiimba wimbo wa taifa

Benchi la Ufundi la Serengeti Boys wakati wa wimbo wa taifa

Hussein Twaha akipasua katikati ya msitu wa wachezaji wa Kongo

Hussein Twaha akimiliki mpira mbele ya beki wa Kongo

Joseph Kimwaga akimtoka beki wa Kongo Brazzaville


Beki wa Kongo Okombi Francis baada ya kumpitia kwanja Tumaini Baraka Mosha wa Serengeti
Mudathir akiondoka na mpira

Tumaini Baraka Mosha akimtoka Okombi

Kushoto refa anasema twende, huku Tumaini Baraka Mosha akiwania mpira dhidi ya Ondongo

LIGI za ULAYA: Bayern sare, Dortmund washinda, Barca, Real ushindi, Juve sare!

J
>>MESSI aendelea kutoboa NYAVU, RONALDO KAPA!
BARCA_v_REALVinara wa Bundesliga, Bayern Munich, walibanwa mbavu kwa kutoka sare lakini Mabingwa watetezi wameshinda Mechi yao huku huko Spain, Vigogo Real Madrid na Barcelona, zote zimeshinda Mechi zao na huko Italy, Mabingwa na vinara wa Serie A, Juventus, walitoka sare matokeo ambayo yaliikumba Mechi ya Napoli v AC Milan zilizotoka 2-2.
BUNDESLIGA:
MATOKEO:
Jumamosi Novemba 17
Enitracht Frankfurt 4 Augsburg 2
Borussia Dortmund 3 SpVgg Gr. Furth 1
Hannover 1 Freiburg 2
Borussia Monchengladbach 1 Stuttgart 2
Nuremberg 1 Bayern Munich 1
Hamburger 1 Mainz 0
Bayer Leverkusen 2 Schalke 0Zile mbio za vinara Bayern Munich kwenye Bundesliga zilisimama baada ya kutoka sare 1-1 ugenini na Timu iliyo mkiani Nuremberg lakini bado wako mbele kwa Pointi 8.
Mabingwa watetezi, Borussia Dortmund, ambao wako nafasi ya 4, waliichapa Greuther Fuerth na kupunguza pengo lao na Bayern Munich kuwa Pointi 9.
Eintracht Frankfurt walifunga Augsburg Bao 4-2 na kuwafanya washike nafasi ya 3 wakiwa na Pointi 23.
RATIBA:
Jumapili Novemba 18
Werder Bremen v Fortuna Dusseldorf
Hoffenheim v Wolfsburg
SERIE A
MATOKEO:
Jumamosi Novemba 17
Napoli 2 Milan 2
Juventus 0 Lazio 0
Stephan El Shaarawy alipiga Bao mbili zilizowafanya AC Milan watoke nyuma 2-0 ugenini na Napoli na kupata sare ya Bao 2-2.
Matokeo haya yamepunguza kidogo presha kwa Kocha wa AC Milan Massimiliano Allegri na kuifanya Timu hiyo ishikilie nafasi ya 12 ikiwa na Pointi 15
Katika Mechi hiyo, Napoli walifunga Bao katika Dakika ya 4 baada ya shuti la mbali la Gökhan Inler kubadili mwelekeo na kumbabaisha Kipa Christian Abbiati.
Baada ya Nusu Saa, Lorenzo Insigne aliipigia Napoli Bao la pili.
Juventus, ambao Jumanne wataikaribisha Chelsea Mjini Turin kwenye Mechi muhimu ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, walipanga Kikosi kizito kwenye Mechi na Lazio lakini walishindwa kupata mwanya na kuambua sare ya 2-2.
RATIBA:
Jumapili Novemba 18
Inter Milan v Cagliari
Udinese v Parma
Catania v Chievo Verona
Siena v Pescara
Fiorentina v Atalanta
Bologna v Palermo
Sampdoria v Genoa
LA LIGA
MATOKEO:
Jumamosi Novemba 17
Osasuna 0 Malaga 0
Valencia 2 Espanyol 1
Barcelona 3 Real Zaragoza 1
Real Madrid 5 Athletic Bilbao 1
Barcelona wamezidi kuchanja mbuga kileleni mwa La Liga baada ya kuifunga Real Zaragoza, huku Real Madrid wakiiwasha Athletic Bilbao na Valencia kuitungua Espanyol.
Lionel Messi aliifungia Barcelona Bao mbili na kumtengenezea Bao Alex Song aliefunga Bao lake la kwanza tangu ahamie Barcelona na Bao hizo ziliwapa ushindi wa 3-1 dhidi ya Real Zaragoza.
Karim Benzema aliifungia Real Madrid stayed Bao mbili walipowatandika Athletic Bilbao Bao 5-1 Uwanjani Santiago Bernabeu na kuwafanya wabakie Pointi 8 nyuma ya vinara Barcelona.
Bao nyingine za Real zilifungwa na Mesut Ozil, Sami Khedira na Jon Aurtentxe aliejifunga mwenyewe.
Nao Valencia waliichapa Espanyol Bao 2-1 na kuididimiza Timu hiyo mkiani mwa La Liga.
Bao la ushindi la Valencia lilifungwa kwa Penati ya utata na Robert Soldado, Penati ambayo ilisababisha Moreno na Sergio Garcia wa Espanyol watolewe nje kwa Kadi Nyekundu baada ya kuilalamikia.
RATIBA:
Jumapili Novemba 18
Deportivo La Coruna v Levante
Celta Vigo v Real Mallorca
Getafe v Real Valladolid
Granada v Atletico Madrid
Sevilla v Real Betis

Rage kufikishwa mahakamani

Siku moja baada ya Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, kutangaza uamuzi wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo kulifuta tawi la Mpira Pesa pamoja na kuwafuta uanachama Mwenyekiti wa tawi hilo Masoud Awadh na Ally Bane, wanachama hao wamesema watalifikisha suala hilo mahakamani.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana kwa niaba ya Bane na yeye mwenyewe, Awadh alisema hawakubaliani na maamuzi ya uongozi wa Rage kuwafuta uanachama.
"Kwanza kauli ya Rage ya kusema kuwa sisi si wanachama halali si ya kweli kwa sababu mkutano mkuu wa mwisho wa klabu yetu tulihudhuria," alisema Awadh na kueleza zaidi:
"Sasa kwa nini alituruhusu kuhudhuria kwenye ule mkutano wakati anajua sisi si wanachama halali."
Alisema ni kwa msingi huo hakubaliani na maamuzi hayo ya Rage na kusema watahakikisha wanaipata haki yao hata kwa kulipeleka suala hilo mahakamani.
Aidha, alisema, bado wanatafuta sahihi za wanachama kwa ajili ya kuushinikiza uongozi kuitisha mkutano mkuu wa dharura wa klabu kujadili masuala mbalimbali ya Simba.

SERENGETI YAWAPA RAHA WATANZANIA

Mfungaji wa bao la Serengeti, Mudathir Yahya Abbas kushoto akishangilia huku akipongezwa na wenzake Joseph Kimwaga Lubasha na Ismail Adam Gambo. 


TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys leo imeifunga  1-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Tatu na ya mwisho kuwania tiketi ya kucheza Fainali za vijana wa umri huo Afrika zitakazopigwa nchini Morocco mwakani.
Kwa matokeo hayo, Serengeti sasa inahitaji hata sare yoyote katika mchezo wa marudiano wiki mbili zijazo mjini Brazzaville ili kukata tiketi ya Morocco mwakani.
Kwa ujumla Serengeti walipigana katika mchezo wa leo, kwani wapinzani wao walionekana kuwa bora na wenye uzoefu zaidi yao.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Miiro Nsubuga, aliyesaidiwa na Mark Ssongo, Balikowa Ngobi na Ronnie Kalemba wote kutoka Uganda, hadi mapumziko Serengeti walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililopatikana dakika ya 15.
Bao hilo lilifungwa kwa shuti la mpira wa adhabu na beki Mudathir Yahya Abbas kutoka umbali wa mita 22 na mpira kabla ya kutinga nyavuni ulimbabatiza beki mmoja wa Kongo na kumpoteza njia kipa Ombandza Mpea Joe na kujaa nyavuni.
Faulo hiyo ilitokana na kiungo wa Serengeti, Hussein Twaha Ibrahim ‘Messi’kuangushwa na beki Okombi Francis wakati akiwa analekea kwenye eneo la hatari la Wakongo.
Baada ya bao hilo, Wakongo walijaribu kuongeza jitihada kiuchezaji, lakini ukuta imara wa Serengeti ulioongozwa na kipa Peter Manyika uliwazuia kusawazisha hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinatimia.
Baada ya mechi hiyo, kocha wa Serengeti Boys, Mdenmark, Jacob Michelsen aliwapongeza vijana wake, lakini akasema bado wana kazi kubwa mbele yao.
Kocha wa Kongo, Mfaransa Eddie Hudanski alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 88, baada ya awali kuonywa kwa kutoa lugha chafu, lakini akarudia.
Refa Nsubuga alitoa kadi moja tu ya njano kwa Issambey Lonvreve aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Ibara Vinny.
Tanzania; Peter Manyika Peter, Miza Kriston Abdallah, Mohamed Hussein Mohamed, Ismail Adam Gambo, Miraj Adam Suleiman, Mudathir Yahya Abbas, Mohamed Salum Haroub, Joseph Kimwaga Lubasha/Dickson Isaac Ambundo, Hussein Twaha Ibrahim, Suleiman Hamisi Bofu/Tumaini Baraka Mosha na Farid Mussa Shah.
Kongo Brazzaville; Ombandza Mpea Joe, Tmouele Ngampio, Mabiala Gharlevy, Okimbi Francis, Ondongo Boungena, Ibra Vinny/Issambey Lonvreve, Binguila Handy, Obassi Ngatsongo, Mohendiki Brel, Atoni Mavoungou na Biassadila Arei.

 

HAYATOU KUFUNGUA TUSKER CHALLENGE WIKI IJAYO

Hayatou kushoto akiwa na Rais wa FIFA, Sepp Blatter kulia

RAIS wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Issa Hayatou amekubali kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, Cecafa-Tusker Challenge wiki ijayo mjini Kampala, Uganda.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Uganda (FUFA), Rogers Mulindwa amesema leo kutoka Uganda kwamba, Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) tayari limepokea uthibitisho wa Hayatou kufungua michuano hiyo kutoka makao makuu ya CAF, Cairo, Misri.
Bosi huyo wa soka barani, anatarajiwa kuwasili Kampala Novemba 22, kufuatia mwaliko huo wa Rais wa CECAFA, Leodegar Tenga.
Rais wa FUFA, Lawrence Mulindwa amesema Uganda imefurahia heshima hiyo ya ujio wa Hayatou, ambaye atafuatana na viongozi mbalimbali wa CAF, akiwemo Katibu Mkuu, Hicham El Amrani, Mohamed Raouraoua, Constant Omari na Ngangue Appolinaire. Katika ziara yake hito, Hayatou atahudhuria Mkutano wa CECAFA katiuka hoteli ya Serena Ijumaa ya Novemba 23 kabla ya kufungua rasmi michuano ya mwaka huu ya Cecafa-Tusker Cup Uwanja wa Namboole jioni ya siku inayofuata.
Uganda itawakaribisha jirani zao Kenya katika mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo saa 10:00 jioni, Jumamosi ya Novemba 24.

 

JB MPIANA AJA KUWAPANDISHA PUNDA WABONGO KWENYE UZINDUZI WA ALBAMU YA MASHUJAA

Mkurugenzi wa QS Muhonda J Entertainment, Joseph (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Millennium Business Park, Kijitonyama, Dar es Salaam asubuhi ya leo kuhusu onyesho la JB Mpiana na Mashujaa Band. Wengine kulia ni rais wa Mashujaa, Chaz Baba na kushoto ni Mshauri wa bendi, King Dodo  


Kutoka kulia peomota anayemleta JB, GuyGuy Kiangala, Chaz Baba, Muhonda na Dodo 
MWANAMUZIKI nguli wa dansi Afrika, JB Mpiana anatarajiwa kuwasili nchini Novemba 26, mwaka huu kwa ajili ya kupamba uzinduzi wa albamu ya Mashujaa Band Novemba 30, mwaka huu katika viwanja vya Leaders Club, Dar es Salaam na baadaye katika mikoa ya Arusha Novemba 28 na Mwanza Desemba 2.
Akizungumza na Waandishi wa Habari asubuhi ya leo katika ukumbi wa Millennium Business Park, Kijitonyama, Dar es Salaam, rais wa bendi ya Mashujaa, Charles Gabriel Cyprian ‘Chaz Baba’, alisema mkali huyo wa dansi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) anakuja kundi lake zima la Wenge Musica BCBG.
JB Mpiana ambaye kwa sasa anatamba na albamu yake ya mpya iitwayo Biloko, anatarajiwa kupagawisha Watanzania na rap yake mpya iitwayo Amataka Na Punda yaani, Panda Punda, ambayo kwa Kongo inapendwa ile mbaya.
Chaz Baba alisema kwamba maandalizi ya onyesho lao yanaendela vizuri kwa ujumla na wanamuziki wapo tayari kuwapa raha Watanzania siku hiyo.
Chaz Baba alisema bendi yao itaingia kambini wiki ijayo nje kidogo ya Dar es Salaam, ambako hawataki kuweka wazi, ili kuwaepushia usumbufu wanamuziki wakati zoezi hilo gumu la maandalizi ya shoo ya kufa mtu.
Alisema albamu yao, wanayozindua iitwayo Risasi Kidole ina nyimbo sita, ambazo ni Risasi Kidole yenyewe utunzi wake Chaz Baba, Ungenieleza utunzi wake Raja Ladha, Umeninyima utunzi wa Freddy Masimango, Hukumu ya Mnafiki utunzi wake Jado FFU, Kwa Mkweo utunzi wake Baba Isaya na Penzi la Mvutano, ambao umetungwa na Masoud Namba ya Mwisho.
Chaz Baba alisema kama ilivyopangwa, mbali na JB Mpiana, wanamuziki wengine watakaopamba uzinduzi huo ni MB Dogg, H Baba, Ney wa Mitego na wengineo ambao watajulikana baadaye.
“Sisi kwa upande wetu tumejipanga vizuri kuwapa watu burudani ambayo tunajua kwa muda mrefu wameikosa, Mashujaa tunakuja kushujaa, ushujaa wa kuwaburudisha watu na kukata kabisa kiu yao,”alisema Chaz Baba.
Alisema wanataka kufanya shoo ambayo hata JB mwenyewe akiona atakubali kwamba Tanzania kuna bendi yenye ubora sawa na bendi za kwao, Kongo, ambayo ni Mashujaa.
“Hadi sasa wapenzi wa muziki hapa Dar es Salaam ambao wamebahatika kuona shoo zetu wanakiri sisi ndio mabingwa wapya wa muziki wa dansi Tanzania, sasa tunataka tumdhihirishie hilo na JB Mpiana,”alisema Chaz Baba.
Wakati onyesho la Dar es Salaam litafanyila Leaders, Mwanza itakuwa kwenye ukumbi wa Villa Park na Arusha ni Tripple A.

CHAMA CHA MCHEZO WA PETE (NETBALL) MKOA WA DAR ES SALAAM CHATAMBULISHA VIONGOZI WAKE.

Afisa Michezo Mkoa wa Dar es salaam Adolf Halii akiongea na wachezaji wa netiboli jana kwenye viwanja vya harbours view Kurasini
Baadhi ya viongozi wapya wa CHANEDA.

Uhamiaji Queens waliovaa nyeusi wakipambana na wanaume kombaini, Uhamiaji ilichapwa
Wanaume wakionyesha umahiri wa kucheza netiboli.


  Chama cha mpira pete mkoa wa Dar es Salaam (CHANEDA) kimetambulisha uongozi wake mpya kwa kufanya bonanza la mchezo huo  lililofanyika katika viwanja vya harbours view Kurasini jijini Dar es Salaam.
 Viongozi wapya waliotambulishwa ni pamoja Winfrida Emanuel-Mwenyekiti, Pilly Mogella-Makamu Mwenyekiti, Joseph Ng'anza-Katibu, Christina Kimamla-Katibu msaidizi, Anita Hangoli-Mweka hazina na Mauris Michael-Afisa 
Bonanza hilo lilishirikisha timu sita na mbili zikiwa za wanaume lilianza saa nane mchana juzi.

Awali akizungumza na wanamichezo na uongozi huo mpya wa CHANEDA, mgeni rasmi ambaye ni Afisa Michezo wa Mkoa wa Dar es salaam Adolf Halii aliwataka wachezaji kushirikiana na uongozi mpya na yeye atakuwa karibu nao maana hata yeye ni mchezaji wa netiboli.

"Nawapongeza wote mlioshiriki kwenye bonanza hili ila nawaomba mshirikiane na uongozi huu mpya ili tuendeleze michezo Dar es Salaam maana hata mimi nacheza netiboli nafasi ya GS", alisema Halii.
Naye Edson Abubakar anayechezea timu ya wanaume ya Kaza roho ya Kipunguni aliwataka viongozi waanzishe ligi ya netiboli ya wanaume na kusaidia vilabu ili kuvitia moyo.

Timu zilizoshiriki ni Kipunguni Queens ambayo iliifunga Kiwalani 10-3, Karaza roho ambayo iliifunga Majumba sita (wanaume) 16-10, Bandari B iliifunga Kiwalani 18-5 na Wanaume mchanganyiko wakaifunga uhamiaji 11-10

 

KILA LA HERI SERENGETI BOYS, TWENDENI TUKAWAPE SAPOTI VIJANA TAIFA LEO

Wachezaji wa Serengeti Boys wakiomba dua kabla ya mazoezi yao Alhamisi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mungu ibariki Tanzania. Amin.

TIMU ya ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys, leo inashuka dimbani kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kumenyana na vijana wenzao, Kongo Brazzaville katika mchezo wa kwanza wa raundi ya Tatu nay a mwisho ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Vijana chini ya umri wa miaka 17 nchini Morocco mwakani.
Serengeti wanaingia kwenye mchezo huo, wakiwa na matumaini makubwa ya ushindi kutokana na maandalizi mazuri waliyopewa.
Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Mdenmark Jacob Michelsen amesema ana matumaini ya ushindi katika mchezo huo kutokana na maandalizi mazuri, ingawa amesema anaa wasiwasi wapinzani wake wana wachezaji waliozidi umri.
Michelsen alisema kwamba alikwenda kushuhudia mchezo wa kwanza wa raundi iliyopita, baina ya Kongo na Zimbabwe waliotolewa na wapinzani wao hao na kujionea makali ya wapinzani wao.
Pamoja na kukiri kwamba Kongo ni timu bora na ilicheza Fainali zilizopita za Kombe la Dunia nchini Mexico mwaka jana na kutolewa raundi ya pili, Michelsen alisema bado ana wasiwasi timu hiyo ina ‘vijeba’.
“Nilipokwenda kuwaangalia wakicheza na Zimbabwe, nilikuta kikosini mwao kuna wachezaji sita wa kikosi kilichokwenda Mexico kwenye Kombe la Dunia, inanitia shaka kwa sababu hakuna mchezaji anayeweza kucheza michuano mikubwa kama ile akiwa ana umri wa miaka 15.
Mimi ni kocha wa vijana na ninajua, haiwezekani. Ucheze fainali za Kombe la Dunia za U17 una miaka 15, hakuna,”alisema Michelsen, ambaye aliwataja baadhi ya wachezaji anaowatilia shaka wamezidi umri ni Hady Binguila na Charvely Mabiat.
Amesema wamecheza mechi za kujipima nguvu 15 zikiwemo dhidi ya timu za Ligi Kuu na hawajafungwa hata moja, kitu ambacho anaamini ni kipimo cha ubora wa timu yake.
Nahodha wa Serengeti Boys, Miraj Adam amesema leoo watapigana kwa nguvu zao zote, kuhakikisha wanawafunga Kongo Brazzaville ili watimize ndoto zao za kucheza Fainali za Morocco mwakani.
Adam alisema kwamba hata kama Kongo Brazzaville wamekuja na wachezaji waliovuka umri kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo, lakini kesho watafungwa tu.
“Kongo watakufa, watake wasitake, nasema Kongo watakufa,”alisema.
Kwa upande wake, Msaidizi wake, Hussein Twaha ‘Messi’ alikumbushia maneno waliyoambiwa na mwanasoka bora wa zamani Afrika, Abedi Ayew Pele katika ziara yake nchini hivi karibuni na kusema yatakuwa kichocheo kwao kufanya vizuri na kukata tiketi ya Morocco.
“Pele alituambia mpira unachezwa na watoto kutoka familia masikini, hata yeye alitoka familia ya kimasikini, akajitahidi akafanikiwa na kufanya watoto wake waingie katika mpira wakitokea familia ya kitajiri, hivyo na sisi tunatumia kauli hii kama kichocheo cha kufanya vizuri ili tufuate nyayo zake,”alisema Twaha.
Serengeti imefanikiwa kufuzu hadi Raundi ya Tatu bila jasho, baada ya wapinzani wake wa awali katika Raundi ya Kwanza na ya Pili, Kenya na Misri kujitoa. Iwapo timu hii itafuzu, hii itakuwa mara ya pili kwa Serengeti kukata tiketi ya kucheza fainali hizo, baada ya mwaka 2005.
Hata hivyo, pamoja na kuzitoa Rwanda, Zambia na Zimbabwe, Serengeti haikwenda Gambia mwaka huo kutokana na kuondolewa kwenye michuano hiyo na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), baada ya kubainika walitumia kijana aliyezidi umri, Nurdin Bakari.

KLABU BINGWA AFRIKA ni AL AHLY!!!

CAF Champions League

Mohamed Nagui 

>>NI REKODI, BINGWA AFRIKA MARA 7!!
>>WAZOA DOLA MILIONI 1.5
>>KUCHEZA FIFA KLABU BINGWA DUNIANI Japan Mwezi Desemba!!
Mabao kutoka kwa Mohamed Nagui na Walid Soliman yamewapa Al Ahly ya Misri Taji la Klabu Bingwa Afrika walipoibwaga Esperance de Tunis huko Mjini Tunisi, Uwanjani Rades, kwa Bao 2-1 kufuatia sare ya Bao 1-1 katika Mechi ya kwanza iliyochezwa Cairo, Misri Wiki mbili zilizopita.
Hii ni rekodi kwa Al Ahly kutwaa Ufalme wa Afrika kwa mara ya 7 na ushindu huu umewawezesha kuzoa kitita cha Dola Milioni Moja na Nusu na pia kuiwakilisha Afrika katika michuano ya FIFA ya Klabu Bingwa Duniani itakayochezwa huko Japan Mwezi Desemba.
Bao za Al Ahly zilifungwa katika Dakika za 43 na Mohamed Nagui NA Dakika ya 62 na Walid Soliman na kuwafanya waongoze 2-0 lakini Esperance, ambao ndio walikuwa Mabingwa watetezi, walipata Bao lao pekee katika Dakika ya 85.
Al Ahly pia walikosa Penati katika Dakika ya 89 iliyopigwa na Mohammed Abou Trika.
Al Ahly pia watacheza kwenye CAF Super Cup na Mshindi wa Fainali ya CAF ya Kombe la Shirikisho kati ya Djoliba ya Mali na AC Leopards wa Congo DR ambao leo wanakutana huko Bamako, Mali katika Mechi ya kwanza na watarudiana Novemba 25 huko Nchini Congo DR.
 

BPL: Man United yapigwa, Man City yabaki juu!!

BPL_LOGOKichwa cha Dakika ya 60 cha Anthony Pilkington kufuatia krosi ya Javier Garrido kiliwapa ushindi Norwich City wa Bao 1-0 wakiwa kwao Carrow Road na kuwafanya Manchester United waporomoke hadi nafasi ya Pili huku nafasi ya kwanza ikikamatwa na Mabingwa watetezi Man City ambao jana waliinyuka Aston Villa Bao 5-0.
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO Timu za juu:
1 Man City Mechi 12 Pointi 28
2 Man United Mechi 12 Pointi 27
3 Chelsea Mechi 12 Pointi 24
4 WBA Mechi 12 Pointi 23
5 Everton Mechi 12 Pointi 20
6 Arsenal Mechi 12 Pointi 19
7 West Ham Mechi 11 Pointi 18
8 Tottenham Mechi 12 17
+++++++++++++++++++++++
Katika Mechi hii Man United walionekana kupwaya sana kwenye Kiungo, hasa Ryan Giggs, alionekana dhahiri ni mzungukaji tu na si mchangiaji.
VIKOSI:
Norwich: Ruddy, Whittaker, Bassong, Turner, Garrido, Snodgrass, Johnson, Tettey, Pilkington, Hoolahan, Holt
Akiba: Bunn, Howson, Jackson, Morison, Elliott Bennett, Tierney, Ryan Bennett.
Man Utd: Lindegaard, Da Silva, Ferdinand, Smalling, Evra, Valencia, Carrick, Giggs, Young, van Persie, Hernandez
Akiba: Johnstone, Jones, Anderson, Welbeck, Scholes, Cleverley, Fletcher.
Refa: Anthony Taylor
+++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumapili, Novemba 18, 2012
[SAA 1 Usiku]
Fulham v Sunderland
Jumatatu, Novemba 19, 2012
[SAA 5 Usiku]
WestHam v Stoke City

BPL: Man City wakaa kileleni…..kwa muda?? Chelsea yachapwa!!!

>>LIVERPOOL furaha ANFIELD, NEWCASTLE HOI ST JAMES PARK!!
BPL_LOGOKatika Mechi za Ligi Kuu England, BPL, Mabingwa watetezi, Manchester City, wakicheza kwao Etihad, na kama Wahenga wasemavyo “Mchezaji kwao hutunzwa”, leo ‘wamezawadiwa’ Penati mbili ‘tata’ na kuikung’uta Aston Villa Bao 5-0, ushindi ambao umewafanya wakae kileleni, japo kwa muda ikiwa Man United watashinda Mechi yao ya baadae leo, lakini habari kubwa za leo ni ushindi wa ‘Timu ya Ajabu’ Msimu huu WBA ambayo imewachapa Chelsea Bao 2-1 na kukwea hadi nafasi ya 4 wakiwa Pointi 1 tu nyuma ya Chelsea.
+++++++++++++++++++++++
RATIBA/MATOKEO:
Jumamosi, Novemba 17, 2012
Arsenal 5 Tottenham Hotspur 2
Liverpool 3 Wigan Athletic  0
Manchester City 5 Aston Villa 0
Newcastle United 1 Swansea City 2
Queens Park Rangers 1 Southampton 3
Reading 2 Everton 1
West Bromwich Albion 2 Chelsea 1
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Norwich City v Manchester United
+++++++++++++++++++++++
Huko Anfield, Wenyeji Liverpool, leo wamecheza na Wigan, Timu ambayo hawajaifunga katika Mechi 5 lakini leo wamelamba trufu kwa kuitwanga Bao 3-0.
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO Timu za juu:
1 Man City Mechi 12 Pointi 28
2 Man United Mechi 11 Pointi 27
3 Chelsea Mechi 12 Pointi 24
4 WBA Mechi 12 Pointi 23
5 Everton Mechi 12 Pointi 20
6 Arsenal Mechi 12 Pointi 19
7 West Ham Mechi 11 Pointi 18
8 Tottenham Mechi 12 17
+++++++++++++++++++++++
ZIFUATAZO NO TAARIFA FUPI KUHUSU MECHI ZA LEO:
READING 2 EVERTON 1
Bao mbili za Adam Le Fondre, moja ikiwa Penati, leo zimewapa Reading ushindi wa Bao 2-1 walipocheza na Everton.
Bao la Everton lilifungwa na Naismith.
VIKOSI:
Reading: Federici, Gunter, Morrison, Gorkss, Shorey, Robson-Kanu, Leigertwood, Tabb, McAnuff, Roberts, Le Fondre
Akiba: Stuart Taylor, Mariappa, Pogrebnyak, Hunt, McCleary, Harte, Cummings.
Everton: Howard, Coleman, Heitinga, Jagielka, Baines, Naismith, Osman, Fellaini, Hitzlsperger, Pienaar, Jelavic
Akiba: Mucha, Oviedo, Distin, Vellios, Junior, Kennedy, Duffy.
Refa: Martin Atkinson
WEST BROM 2 CHELSEA 1
Chelsea leo wamepiga Mechi yao ya 4 kwenye Ligi bila ushindi baada ya kuchapwa Bao 2-1 na WBA Uwanjani Hawthorns.
Shane Long ndie alietangulia kuifungia WBA katika Dakika ya 10 lakini Chelsea wakasawazisha kwa Bao la Dakika ya 39 la Eden Hazard.
Mnigeria Peter Odemwingie ndie aliipa ushindi WBA kwa Bao lake la Dakika ya 50.
Ushindi huu umewafanya WBA wapande hadi nafasi ya 4.
VIKOSI:
West Brom: Myhill, Jones, Olsson, Tamas, Ridgewell, Morrison, Yacob, Mulumbu, Gera, Long, Odemwingie
Akiba: Luke Daniels, Reid, Popov, Rosenberg, Brunt, Dorrans, Fortune.
Chelsea: Cech, Azpilicueta, Cahill, Luiz, Bertrand, Romeu, Mikel, Hazard, Sturridge, Torres, Moses
Akiba: Turnbull, Ivanovic, Cole, Ramires, Mata, Oscar, Marin.
Refa: Michael Oliver
LIVERPOOL 3 WIGAN 0
Bao 3 za Kipindi cha Pili, mbili toka kwa Luis Suarez na moja kwa Jose Enrique, leo zimewapa Liverpool ushindi wao wa kwanza dhidi ya Wigan katika Mechi 5 walizokutana na kuifanya Liverpool ipande hadi nafasi ya 11.
VIKOSI:
Liverpool: Reina, Wisdom, Agger, Skrtel, Jose Enrique, Johnson, Gerrard, Allen, Sterling, Suarez, Suso
Akiba: Jones, Sahin, Cole, Henderson, Coates, Carragher, Shelvey.
Wigan: Al Habsi, Ramis, Caldwell, Figueroa, Boyce, Watson, McCarthy, Beausejour, Maloney, Di Santo, Kone
Akiba: Pollitt, Jones, Gomez, McManaman, Boselli, Stam, Miyaichi.
Refa: Kevin Friend
MANCHESTER CITY 5 ASTON VILLA 0
Wakicheza nyumbani, Uwanja wa Etihad, Mabingwa watetezi Man City leo wameitwanga Aston Villa Bao 5-0, zikiwemo Penati ‘tata’ mbili.
Ushindi huu umewafanya Man City wakae kileleni, pengine kwa muda tu, kwani baadae leo Man United wapo Carrow Road kucheza na Norwich City na wakishinda watarudi tena kileleni.
Bao za Man City zilifungwa na Silva, Dakika ya 43, Aguero,54 kwa Penati na 67, Tevez, Dakika ya 65 kwa Penati na 74.
VIKOSI:
Man City: Hart, Maicon, Kompany, Nastasic, Clichy, Toure, Barry, Silva, Tevez, Nasri, Aguero
Akiba: Pantilimon, Zabaleta, Lescott, Dzeko, Sinclair, Kolarov, Javi Garcia.
Aston Villa: Guzan, Stevens, Vlaar, Clark, Lowton, Bannan, Westwood, Agbonlahor, Ireland, Weimann, Benteke
Akiba: Given, El Ahmadi, Albrighton, Holman, Delph, Bowery, Baker.
Refa: Jon Moss
QPR 1 SOUTHAMPTON 3
Bao za Puncheon, Lambert na moja la kujifunga wenyewe kupitia Anton Ferdinand leo zimewadidimiza QPR mkiani na kuwafanya Southampton wawe juu ya tu kwa Pointi 4 mbele yao.
Bao pekee la QPR lilifungwa na Hoillet.
VIKOSI:
QPR: Julio Cesar, Bosingwa, Ferdinand, Nelsen, Traore, Diakite, Faurlin, Granero, Taarabt, Hoilett, Cisse
Akiba: Green, Derry, Wright-Phillips, Mackie, Dyer, Da Silva, Ehmer.
Southampton: Gazzaniga, Clyne, Fonte, Yoshida, Shaw, Schneiderlin, Cork, Puncheon, Ramirez, Lallana, Lambert
Akiba: Kelvin Davis, Hooiveld, Steven Davis, Rodriguez, Fox, Ward-Prowse, Mayuka.
Refa: Mike Dean
NEWCASTLE 1 SWANSEA 2
Bao zote za Mechi hii zilifungwa Kipindi cha Pili na Bao za Swansea zilipachikwa na Michu, Dakika ya 58 na De Guzman, Dakika ya 87 huku Bao la Newcastle likifungwa katika Dakika ya 90 na Demba Ba.
VIKOSI:
Newcastle: Krul, Simpson, Steven Taylor, Williamson, Santon, Ben Arfa, Anita, Tiote, Ferguson, Sammy Ameobi, Ba
Akiba: Elliot, Amalfitano, Bigirimana, Marveaux, Shola Ameobi, Tavernier, Abeid.
Swansea: Tremmel, Rangel, Williams, Monk, Davies, Britton, de Guzman, Dyer, Michu, Hernandez, Shechter
Akiba: Cornell, Chico, Graham, Routledge, Moore, Tiendalli, Agustien.
Refa: Phil Dowd
+++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumapili, Novemba 18, 2012
[SAA 1 Usiku]
Fulham v Sunderland
Jumatatu, Novemba 19, 2012
[SAA 5 Usiku]
WestHam v Stoke City
 

Anthony Pilkington. AIKANDAMIZA MAN UU

Norwich city  Imepata ushindi wa pili dhidi ya Manchester United katika mechi  15 zilizokutana katika ligi ya premier ya uingereza kwa goli safi la   Anthony Pilkington. 

 Mchezaji huyo wa zamani wa -Huddersfield alifunga goli hilo dakika  30 kabla ya mchezo kumalizika  akipalaza kichwa klosi iliyopigwa na  Javier Garrido's kutoka kushoto  

 United, ambao walikuwa wakicheza huku wakiwa katika Hari  ya kutaka kurejea katika uongozi dhidi ya ndugu zao City  walipambana na vijana hao haatari wa Norwich city 

Goal - Anthony Pilkington - Norwich 1 - 0 Man Utd