Wednesday, January 2, 2013

USAJILI MBALI MBALI BARANI ULAYA UNAVYOENDELEA KWA SASA ANGALIA ILI UWEZE KUJUA NANI ANAENDA WAPI NANI ANATOKA NA NANI ANABAKI



Mlinzi wa Atalanta Federico Peluso amefanyiwa vipimo vya afya hii leo katika klabu ya Juventus na anatarajiwa kukamilisha taratibu za usajili wake hii leo

Mpango wa uhamisho wake ni wa gharama ya euro milioni 1.5 ambapo Bianconeri(Juve) wakiwa na maamuzi ya uhamisho wa kudumu baada ya msimu kumalizika.

Endapo klanbu hiyo itachagua kufanya hivyo, inamaanisha kuwa mabingwa hao wa kandanda nchini Italia watalazimika kulipa eoro milioni 3.5 kwa kupata huduma yake na huku mlinzi huyo wa kati akitarajiwa kuongeza ushindani katika sehemu ya ulinzi wa kati na ulinzi wa kushoto

Taarifa ya klabu kupitia mtandao wake imethibitisha kuwa mchezaji huyo atafanyiwa vipimo hivyo kule Turin kunako taasisi ya tiba za michezo

Peluso alijiunga Atalanta mwaka 2009 akitokea AlbinoLeffe na amekwisha itumikia timu ya taifa ya Italia michezo mitatu.


Ronaldo: Nadhani Mourinho atasalia.


Cristiano Ronaldo anaamini kuwa kocha wake Jose Mourinho atasalia katika klabu yake ya Real Madrid.

Mreno huyo ameanza kuona hatma yake katika klabu hiyo kama inamashaka hasa kutoka na gumzo lililoanza kuchomoza hususani kutokana na Madrid kuachwa kwa mbali na mahasimu wao wa soka la Hispania Barcelona kwa tofauti ya alama 16 katika msimamo wa ligi ya Hispania La Liga.

Hata hivyo, Ronaldo haoni kwamba hiyo ndiyo inaweza kuwa sababu ya kumuondosha Mourinho Santiago Bernabeu, na kusisitiza kuwa bado ni mtu sahihi wa kuendelea kuiongoza klabu hiyo.

Akinukuliwa na vyombo vya habari baada ya kuulizwa juu ya uwezekanao wa Mourinho kuondoka Ronaldo alijibu

"Sijui, itategenea na hali ya mambo itakavyokuwa ndani ya klabu, kwa upande wangu ningependa asalie kwakuwa ni kocha sahihi. Ni kocha wa kiwango cha juu katika timu ya kiwango cha juu. Nadhani atasalia lakini kila mtu ana uchaguzi wake wa mambo yake ya baadaye"

Mourinho alianza kuingia matatizoni kuanzia pale alipoamua kumuweka benchi mlinda mlango namba moja Iker Casillas na kupelekea kichapo kutoka kwa Malaga, lakini Ronaldo anasema maamuzi ya kocha ni ya mwisho.

WAKALA: Pato anaelekea kukamilisha uhamisho wake  Corinthians.

Mshambuliaji wa AC Milan Alexandre Pato anakaribia kukamilisha taratibu za uhamisho wake kuelekea Corinthians, hii ni kwa mujibu wa wakala wa mchezaji huyo Gilmar Veloz.

Kipindi cha utumishi wake wa miaka 23 katika viunga vya San Siro ulitiwa doa na majeraha ambapo taarifa zinasema sasa ameamua kurejea katika ardhi ya nyumbani.

Kuna vilabu kadhaa barani ulaya vimekuwa katika mawindo ya kumtaka Pato, lakini mwakilishi wake amesisitiza kuwa Pato atarejea nyumbani Brazil hivi karibuni.

Benitez: Torres yuko tayari kuwekwa benchi falcao anakuja.
Kocha wa muda wa Chelsea Rafael Benitez, amesisitiza kuwa Fernando Torres atamuelewa tu endapoa atalamika kumuweka benchi katika baadhi ya michezo, wakati huu ambapo klabu hiyo inataka kusajili vijana zaidi katika safu yake ya ushambuliaji katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Hispania alikuwa akihangaika katika kipindi kirefu kusaka kurejesha kiwango chake  tangu aliposajiliwa kutoka Liverpool januari 2012 ambapo angalau kiwango hicho kimeongezeka mara baada ya kuwasili kwa Bernitez.
Mwezi wa November, klabu hiyo kutoka kaskazini mwa jiji la London ilikuwa katika mazungumzo na mshambuliaji wa Atletico Madrid Radamel Falcao ambapo Benitez anaamini kuwa mchezaji huyo ataleta ushinda wenye afya zaidi katika safu yake ya ushambuliaji.

No comments:

Post a Comment