Tuesday, December 25, 2012

KATIKA MATUKIO YA MWAKA HUU YALIYO HEAD LINE SANA NI PAMOJA NA HILI LA KIFO CHA KIUNGO MAHIRI WA SIMBA PATRICK MUTESA MAFISANGO

MWANADADA KUTOKA TABORA SHILOLE FT. CHILLAH -WIMBO DUDU ATOA VIDEO YAKE INGIA UIANGALIE

Francis Cheka VS Chiokta Chimwemwe


Mabondia Francis Cheka wakitambiana kupigana baada ya kupima uzito na kucheki afya leo asubuhi.

Mafahali mawili wanaotegemea kuzichapa tarehe 25, 2012 kugombea mkanda wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzania Francis Cheka na Mmalawi Chiotcha Chimwemwe nusura wazichape kavukavu wakati wa upimaji uzito na mkutano wa waandishi wa habari katika hoteli ya nyota 5 ya Naura Springs, jijini Arusha leo tarehe 25 Desemba 2012.


Hii ni mara ya kwanza kwa ngumi za kulipwa kupewa hadhi kubwa kama hiyo ya kuwekwa kwenye hoteli ya nyota tano (5) hapa Tanzania.


Wawili hao walikuwa katika hoteli hiyo ya kifahari ya Naura Springs inayomilikiwa na bwana Felix Mrema anayemiliki mahoteli lukuki katika jiji la Arusha na Moshi ambazo ni Naura Springs Hotel, Impala Hotel, Ngurudito Hotel, Impala Moshi na Livingstone Hotel za Moshi!


Mpambano huo uliopewa jina la “Vurumaini chini ya Mlima Meru”umekuwa ni gumzo katika jiji la Arusha, Moshi, Tanga, Dodoma, Manyara pamoja na nchi jirani za Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda na unaandaliwa na kampuni ya kizalendo ya Green Hills (T) Limited inayomilikiwa na bondia wa zamani wa taifa katika ngumi za ridhaa na kuloipwa George Andrew na familia yake.


Aidha, watalii wengi walioko katika jiji la Arusha wakati huu wa sikukuu ya Xmas wameonyesha nia zao za kuliangalia pambano hili na wengine wameshakata tiketi tayari kuingia katika ujwanja wa Sheik Amri Abeid kuwashughudia mafahali hao wawili wakitoana jasho.


Chiotcha mwana wa Chimwemwe mwanajeshi wa ngazi ya Luteini Usu katika jeshi la Malawi amepania kulibeba juu taifa lake lililoko pembezoni mwa ziwa Nyasa kwa kumwonyesha Francis Cheka kuwa ngumi zinaendana na ushupavu.


Chimwemwe anadai kuwa hakuja Tanzania kutalii kama walivyo watalii wengine bali alikuja kuwakilisha nchi yake aipendayo ya Malawi na kurudi kwao na mshipi wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati. Alisema kuwa kushinda kwake sio kitu cha kubahatisha ila ni uhakika.


Naye Francis mwana wa Cheka, Mtanzania aliyeipeperusha vyama bendera ya taifa hili katika mapambano mengi bila kuzivunja nyoyo za mashabiki wa ngumi nchini alisema kuwa “Mwache Mmalawi huyo ajifurahishe tu kwani hajui kinachongojea ulingoni”


Cheka aliyejizolea sifa kemkem kati ya mabondia wa kitanzania aliendelea kusema kuwa yeye sio mzungumzaji sana ila ngumi zake ndizo zitakazozungumza siku ya tareeh 26 Desemba, 2012.


“Asifikirie kuwa ngumi ni kupiga makelele tu na ukashinfa” alisema Chelka akimwangalia Chimwemwe wakati alipokuwa anajigamba kwa sifa kemkem!


Mpambano huo wa kukata na shoka unakuja wakati ambako Arusha imekuwa ni jiji na linataka kutumia mapambano mengi ya ngumi ya kimataifa kukuza hadhi ya jiji hilo kama “Geneva ya Afrika” kutokana na mandari yake na mikutano mingi ya kimataifa inayofanyika katika jiji hili.


Francis Cheka anakutana na Chimwemwe baada ya kuutema mkanda wake wa IBF wakati alipokutana na Karama Nyilawila kugombea mkanda mwingine mbali na IBF hivyo kuupoteza ubingwa wa IBF. Cheka amepania kuuchukua tena mshipi huo na kuudhihirishia ulimwengu kuwa yeye kweli ni moto wa kuotea mbali!


Mpambano huo utahudhuriwa na viongozi wengi wakiongozwa na Meya wa jiji la Arusha Mstahiki Gaudence Lyimo pamoja na wageni wengi wanaofanya kazi kwenye mashirika kadhaa ya kimataifa ikiwa ni pamoja na mahakama ya kimataifa ya wahalifu wa kivita wa Rwanda, Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na Kati, ILO, UNICEF, WFP na nyingine nyingi.


Aidha watalii wengi wameacha kwenda mbugani siku ya pambano ili washughudie wenyewe ni nani zaidi kati ya Cheka na Chimwemwe.,


Pamabano hilo linaratibiwa na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) chini ya Rais wake Onesmo Ngowi na kupewa baraka zote na Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF).


Waamuzi wa pambano ni:
Onesmo Ngowi - Kamishna Mkuu, Roman Chuwa ambaye ndiye Kamishna wa TPBC mkoa wa Arusha –(Kamishna Mkuu Msaidizi), Nemes Kavishe (Refarii), Boniface Wambura – (Jaji), Gallous Ligongo –(Jaji), Mark Hatia –(Jaji).

HASANOOO ALIA BATA JELA -XMASS HIII !!!


Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam,  imezuia dhamana dhidi ya kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoani Pwani (Corefa), Hassani Othman maarufu kama Hasanoo (43) ya mashtaka matatu likiwemo la kuhujumu uchumi na kusafirisha pembe za ndovu zenye thamani ya Sh. bilioni 1.1kutoka Dar es Salaam kwenda Hong Kong kutokana na kutenda kosa hilo akiwa nje kwa dhamana ya kesi nyingine ya wizi wa tani 26 za madini ya shaba yenye thamani ya Sh. milioni 400.

Hata hivyo, mahakama hiyo imekubali kutoa masharti ya dhamana kwa washtakiwa wengine sita ambao ni Ally Kimwaga, Dunstan Mwanga, Godfrey Mwanga, John Mlai, Khalid Fazaldin na Lusekelo Mwakajila.
 Uamuzi huo ulitolewa  na Jaji Zainabu Mruke baada ya kusikiliza hoja za mawakili wa pande zote mbili.

Alisema kipengele cha 36, kifungu kidogo cha (4) kidogo (c) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi, kinaeleza wazi kwamba sheria inaifunga mikono mahakama kuhusu maombi ya dhamana kwa mshtakiwa wa kwanza ambaye amekutwa na tuhuma za uhujumu uchumi akiwa nje kwa dhamana ya kesi nyingine inayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

“Kutokana na sababu hiyo, mahakama haiwezi kutoa dhamana kwa mashtakiwa wa kwanza (Hasanoo) kwani amekutwa na tuhuma za uhujumu uchumi wakati akiwa nje kwa dhamana… mahakama inanifunga mimi kama Jaji kwa mujibu wa kipengele cha 36 kidogo cha (4) na kidogo (c) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi, hakuna dhamana kwa mshtakiwa huyo,” alisema Jaji Mruke.

Alisema mshtakiwa wa pili hadi wa saba, mahakama hiyo imeona wana haki ya kisheria kupata dhamana kwa kufuata masharti yatakayowekwa na mahakama.

Jaji Mruke aliyataja masharti hayo kuwa ni kuwasilisha hatia zao za kusafiria kwa Msajili wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam na kwamba, hawaruhusiwi kutoka nje ya mkoa wa Dar es Salaam bila kibali cha msajili huyo hadi kesi yao ya msingi itakapomalizika.

Alisema vilevile kuwa mshtakiwa wa pili hadi wa saba wajidhamini kwa Sh. milioni 50 au kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika yenye thamani hiyo ya fedha.

“Nakala zote za masharti ya dhamana ziwasilishwe katika Mahakama ya Kisutu inakosikilizwa kesi hii ili kuondoa mkanganyiko” alisema Jaji Mruke.

Baada ya uamuzi huo kusomwa, wanaodaiwa kuwa ndugu wa Hasanoo waliangua kilio kutokana vifungu vya sheria kumbana ndugu kutoka nje kwa dhamana. Uamuzi huo pia ulimaanisha kuwa Hassanoo atakuwa mahabusu katika kipindi chote cha sikukuu za mwisho wa mwaka, ikiwamo ya krismasi (X-Mass) inayosherehekewa leo.

Ijumaa iliyopita katika mahakama hiyo, mawakili wa utetezi Richard Rweyongeza, Majura Magafu, Aliko Mwamanenge, Pascal Chuwa na Charles Semgalawa, kwa nyakati tofauti waliwasilisha hoja za kuwaombea dhamana washitakiwa.

Katika kesi ya msingi, washitakiwa wanakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la uhujumu uchumi na kusafirisha meno ya tembo, yenye thamani ya Sh.bilioni 1.1 kwenda Hong Kong nchini China.

Ilidaiwa kuwa katika shtaka la kwanza, washtakiwa walikula njama na kujihusisha katika biashara ya kusafirisha nyara za Serikali bila leseni, kosa ambalo walilitenda kati ya Septemba Mosi na Novemba 20, mwaka huu, Dar es Salaam na Hong Kong kinyume na kifungu cha 384 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002.

MARRY XMASS NJEMA NA HAPPY NEW YEAR 2013 WASOMAJI WA BLOG YA TANOJUMAIN SPORTS


 

Tanojumainsports.blogspot.com inakutakia sikukuu njema ya krismass waka 2012  na Happy new year mwka 2013 msherehekee kwa amani na upendo daima ili muendelee kujenga Taifa la tanzania kwa kuendeleza kudumisha upendo na amani zaidi.

Mwaka wa 2012  matukio mengi yametokea katika nyanja mbalimbali katika kisiasa ,kiuchumi,kitamaduni,kijamii na mambo mengine mbalimbali.
KISIASA=Mambo mengi yametokea katika nyanja ya kisiasa hapa tanzania kubwa zaidi ni challenge iliyoletwa na chama cha maendeleo CHADEMA kwa kuendelea kuonesha umwamba kwa mpinzani chama tawala CHAMA CHA MAPINDUZI CCM.
Katika siasa mambo mengi yametokea nakumbuka chaguzi mbalimbali zimekuwa na changamoto kubwa sana sana hasa katika uchaguzi wa wilayani Igunga Mkoani Tabora kuziba ile nafasi iliyoachwa na mbunge Rostam Aziz na nafasi yake kuchukuliwa na DK .Kafumu lakini miezi kadhaa akaenguliwa tena na mpaka sasa jimbo la wilayani Igunga lipo wazi.

Katika habari za kimataifa kubwa zaidi ni kuuwawa kwa Raisi wa Libya MUAMAR GADDAFFI aliyekuwa anashikilia madaraka kwa udikteta,Raisi wa ivory coast bw. BAGIBO naye kukamata na kutiwe kitanzini,pia uchaguzi wa marekani, uliochukua nafasi kubwa ya kumchagua  Rais Barack Obama ambayealimshinda hasimu wake wa chama cha Republican katika uchaguzi wa rais wa Marekani, na kwa utaratibu huo kupata fursa nyingine ya kuiongoza nchi hiyo kwa miaka mingine minne. Katika uchaguzi huo uliogharimu fedha nyingi zaidi katika historia ya Marekani, Obama amefanikiwa kumbwaga mpinzani wake Mitty Romney kwa asilimia chache, baada ya kupata kura 303 za 'Electoral College'. Hata hivyo mgawanyiko wa viti katika bunge lijalo la Kongresi ya Marekani haujabadilika, ikilinganishwa na hivi sasa
Weekly Address: The President and First Lady Extend a Holiday Greeting and Thank our Troops for their Service
 BARACK OBAMA

 
 MUAMMAR GADAFFI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhZYWcCr727kB2ceYZsz3Ihu8ah1fTos0h9vVeFDycoNc_mfgm7FnBtFdmYmTAYnDNAb2H_SEduNFl4sZgjMCvHzR1Sd3FSoVQYJO9Nl-a22HBCVNshvBqRqRc1mzpcONNwj0wvzA93g7nd/s1600/LAURENT.jpg
 BAGBO PINDI AMEKAMATWA ikumbukwe Kiongozi huyu  aliyekuwa aking'ang'ania madaraka nchini Cote d'Ivoire, Laurent Gbagbo, alikamatwa na wapiganaji waliokuwa wanaomuunga mkono Alassane Ouattara katika operesheni ya wanajeshi wa Ufaransa na Umoja wa Mataifa.


 Akiwa anavuliwa nguo ilikuwaga taabu kweli
KHERI YA YOTE HAYA TUACHANA NAYO YALIYOPITA TUGANGE YAJAYO ILI TUJENGE TAIFA LETU....NA KUMBUKA KATIKA MAFANIKIO CHANGAMOTO HAZIKOSEKANIIIII!!!!!!!!!!!!!!