Saturday, August 24, 2013

ANGALIA PICHA ZA SIMBA WAKIFANYA MAZOEZI TAYARI KUWAKABILI RHINO RANGERS HII LEO


VIJANA WAKO MAZOEZINI HATUMWI MTOTO LEO
KOCHA MKUU ABDALAH KING,KIBADENI MPUTA YUPO MBELE AKIWAPA MAZOEZI WACHEZAJI WAKE ALIYEINAMA

NI NOMAAAAA SANAA

MPUTA  NA BENCHI LAKE LA UFUNDI WAKIFUATILIA MAZOEZI NA TIMU YAKE YA SIMBA

VIJANA WAKIOMBA DUA BAADA YA MAZOEZI TAYARI KUWAKABILI RHINO RANGERS HII LEO KATIKA DIMBA LA LALLY HASSAN MWINYI


NDO USAFIRI WA WEKUNDU WA MSIMBAZI SIMBA THE MNYAMA UKIWA KATIKA DIMBA LA MWINYI

MOYES YUPO KARIBU KUWANASA BAINES NA FELLAINI,NI MAMBO YA MKWANJA HAYO


KOCHA David Moyes anakaribia kushinda vita yake ya kuwania saini za wachezaji wa Everton, Leighton Baines na Marouane Fellaini baada ya kuibuka kwa taarifa kwamba, klabu yake ya zamani iko tayari kuwauza nyota wake hao.
Everton imekuwa ikilalama dhidi ya Moyes na Manchester United tangu ikatae ofa ya mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England ya Pauni Milioni 28 kwa ajili ya nyota hao wawili wa Goodison Park.
Wamekubaliana na ofa hiyo na kocha wa Everton, Roberto Martinez ameisifu United imekuwa na tabia nzuri.
Coming for you: David Moyes is desperate to land his former players Leighton Baines and Marouane Fellaini
Nakuja kwako: David Moyes anakaribia kuwanasa wachezaji wake wa zamani Leighton Baines na Marouane Fellaini
Looking good: Baines was in training with Everton ahead of the weekend's game against West Brom
Anaonekana vizuri: Baines akiwa mazoezini na Everton
Staying or going? Fellaini (right) and Baines are both likely to play a part against West Brom
Anabaki au anaondoka? Fellaini (kulia) na Baines mazoezini na Everton kujiandaa na mchezo dhidi ya West Brom

WE KAMA NI MSHABIKI WA LIGI KUU BARA CHUKUA HIYO,RATIBA NZIMA LIGI KUU TANZANIA BARA MZUNGUKO WA KWANZA


JUMAMOSI
-:- August 24, 2013 Yanga SC vs Ashanti Utd
-:- August 24, 2013 Mtibwa S – Azam FC
-:- August 24, 2013 JKT Oljoro – Coastal U
-:- August 24, 2013 Mgambo – JKTRuvu
-:- August 24, 2013 Rhino – Simba SC
-:- August 24, 2013 Mbeya City – Kagera S
-:- August 24, 2013 R.Shooting – Prisons

JUMATANO
-:- August 28, 2013 Mtibwa S – Kagera S
-:- August 28, 2013 Rhino – Azam FC
-:- August 28, 2013 JKTRuvu – Prisons
-:- August 28, 2013 Mbeya City – R.Shooting
-:- August 28, 2013 Mgambo – Ashanti Utd
-:- August 28, 2013 JKT Oljoro – Simba SC
-:- August 28, 2013 Yanga SC – Coastal U

JUMAMOSI
-:- September 14, 2013 Simba SC – Mtibwa S
-:- September 14, 2013 Coastal U – Prisons
-:- September 14, 2013 R.Shooting – Mgambo
-:- September 14, 2013 JKT Oljoro – Rhino
-:- September 14, 2013 Mbeya City – Yanga SC
-:- September 14, 2013 Kagera S – Azam FC
-:- September 14, 2013 Ashanti Utd – JKTRuvu

JUMATANO
-:- September 18, 2013 Prisons – Yanga SC
-:- September 18, 2013 Simba SC – Mgambo
-:- September 18, 2013 Kagera S – JKT Oljoro
-:- September 18, 2013 Azam FC – Ashanti Utd
-:- September 18, 2013 Coastal U – Rhino
-:- September 18, 2013 Mtibwa S – Mbeya City
-:- September 18, 2013 R.Shooting – JKTRuvu

JUMAMOSI
-:- September 21, 2013 Mgambo – Rhino
-:- September 21, 2013 Prisons – Mtibwa S
-:- September 21, 2013 Simba SC – Mbeya City
-:- September 21, 2013 Kagera S – Ashanti Utd

JUMAPILI
-:- September 22, 2013 JKTRuvu – JKT Oljoro
-:- September 22, 2013 Azam FC – Yanga SC
-:- September 22, 2013 Coastal U – R.Shooting

JUMATANO
-:- September 25, 2013 Rhino – Ashanti Utd

JUMAMOSI
-:- September 28, 2013 Yanga SC – R.Shooting
-:- September 28, 2013 Rhino – Kagera S
-:- September 28, 2013 Mbeya City – Coastal U
-:- September 28, 2013 Mgambo – JKT Oljoro

JUMAPILI
-:- September 29, 2013 Ashanti Utd – Mtibwa S
-:- September 29, 2013 JKTRuvu – Simba SC
-:- September 29, 2013 Prisons – Azam FC

JUMAMOSI
-:- October 5, 2013 R.Shooting – Simba SC
-:- October 5, 2013 JKTRuvu – Kagera S
-:- October 5, 2013 Coastal U – Azam FC
-:- October 5, 2013 JKT Oljoro – Mbeya City

JUMAPILI
-:- October 6, 2013 Mgambo – Prisons
-:- October 6, 2013 Yanga SC – Mtibwa S

JUMATANO
-:- October 9, 2013 Rhino – Mbeya City
-:- October 9, 2013 JKT Oljoro – R.Shooting
-:- October 9, 2013 Azam FC – Mgambo
-:- October 9, 2013 Mtibwa S – JKTRuvu

JUMAMOSI
-:- October 12, 2013 Kagera S – Yanga SC
-:- October 12, 2013 Simba SC – Prisons

JUMAPILI
-:- October 13, 2013 Ashanti Utd – Coastal U
-:- October 13, 2013 R.Shooting – Rhino
-:- October 13, 2013 Mgambo – Mbeya City
-:- October 13, 2013 Azam FC – JKTRuvu
-:- October 13, 2013 Mtibwa S – JKT Oljoro

JUMATANO
-:- October 16, 2013 Ashanti Utd – Prisons

JUMAMOSI
-:- October 19, 2013 Kagera S – Coastal U
-:- October 19, 2013 Ashanti Utd – R.Shooting
-:- October 19, 2013 Mbeya City – JKTRuvu
-:- October 19, 2013 Mtibwa S – Mgambo
-:- October 19, 2013 JKT Oljoro – Azam FC

JUMAPILI
-:- October 20, 2013 Simba SC – Yanga SC

JUMATANO
-:- October 23, 2013 Coastal U – Simba SC
-:- October 23, 2013 Prisons – Kagera S
-:- October 23, 2013 Yanga SC – Rhino

JUMAMOSI
-:- October 26, 2013 Prisons – Mbeya City
-:- October 26, 2013 Coastal U – Mtibwa S
-:- October 26, 2013 JKT Oljoro – Ashanti Utd
-:- October 26, 2013 Yanga SC – Mgambo

JUMAPILI
-:- October 27, 2013 R.Shooting – Kagera S
-:- October 27, 2013 Simba SC – Azam FC
-:- October 27, 2013 Rhino – JKTRuvu

JUMATANO
-:- October 30, 2013 Mgambo – Coastal U
-:- October 30, 2013 Prisons – JKT Oljoro
-:- October 30, 2013 Azam FC – R.Shooting
-:- October 30, 2013 Simba SC – Kagera S
-:- October 30, 2013 Mtibwa S – Rhino
-:- October 30, 2013 Mbeya City – Ashanti Utd

JUMATANO
-:- October 31, 2013 JKTRuvu – Yanga SC

JUMAMOSI
-:- November 2, 2013 JKTRuvu – Coastal U
-:- November 2, 2013 Ashanti Utd – Simba SC

JUMAPILI
-:- November 3, 2013 Kagera S – Mgambo
-:- November 3, 2013 Azam FC – Mbeya City
-:- November 3, 2013 Rhino – Prisons
-:- November 3, 2013 R.Shooting – Mtibwa S
-:- November 3, 2013 Yanga SC – JKT Oljoro

JUMAMOSI
-:- January 25, 2014 Ashanti Utd – Yanga SC
-:- January 25, 2014 Azam FC – Mtibwa S
-:- January 25, 2014 Coastal U – JKT Oljoro
-:- January 25, 2014 Kagera S – Mbeya City
-:- January 25, 2014 Prisons – R.Shooting

JUMAPILI
-:- January 26, 2014 JKTRuvu – Mgambo
-:- January 26, 2014 Simba SC – Rhino

JUMATANO
-:- January 29, 2014 Kagera S – Mtibwa S
-:- January 29, 2014 Azam FC – Rhino
-:- January 29, 2014 Prisons – JKTRuvu
-:- January 29, 2014 R.Shooting – Mbeya City
-:- January 29, 2014 Coastal U – Yanga SC

JUMAMOSI
-:- February 1, 2014 Ashanti Utd – Mgambo
-:- February 1, 2014 Simba SC – JKT Oljoro

JUMAPILI
-:- February 2, 2014 Yanga SC – Mbeya City
-:- February 2, 2014 Prisons – Coastal U
-:- February 2, 2014 Mgambo – R.Shooting
-:- February 2, 2014 Azam FC – Kagera S

JUMATANO
-:- February 5, 2014 Mtibwa S – Simba SC
-:- February 5, 2014 Rhino – JKT Oljoro
-:- February 5, 2014 JKTRuvu – Ashanti Utd

MECHI ZOTE KUANZA SAA KUMI ALASIRI (4:00 pm)

VIWANJA SABA LEO PANACHIMBIKA LIGI KUU BARA VPL,YANGA NA WAUZA MITUBA WA ILALA ASHANTI UNITED,SIMBA NA WANAJESHI WA TABORA RHINO RANGERS


HATIMAYE michuano mikubwa kabisa ya soka nchini, ijulikanayo kama Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inarejea tena kwa mara ya 50 tangu ilipoanzishwa mwaka 1965 kwa wigo finyu na hali dunia kabisa, ikishirikisha klabu za Dar es Salaam pekee.

Naam, msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), unatarajiwa kuanza Jumamosi ya leo, timu 14 zikijitupa dimbani kuwania pointi za mwanzoni, katika mbio za kusaka ubingwa wa ligi, unaoshikiliwa na Wana Jangwani, Yanga SC. 

RATIBA NZIMA YA LIGI KUU TANZANIA BARA MSIMU 2013/14

JUMAMOSI
-:- August 24, 2013 Yanga SC vs Ashanti Utd
-:- August 24, 2013 Mtibwa S – Azam FC
-:- August 24, 2013 JKT Oljoro – Coastal U
-:- August 24, 2013 Mgambo – JKTRuvu
-:- August 24, 2013 Rhino – Simba SC
-:- August 24, 2013 Mbeya City – Kagera S
-:- August 24, 2013 R.Shooting – Prisons

MECHI ZOTE KUANZA SAA KUMI ALASIRI (4:00 pm)
 Historia ya ligi hiyo inaanzia mwaka 1929 ilipoanzishwa kifukara, tu kwa sababu ya mapenzi ya watu na soka wakaamua kuungana na kuanzisha michuano ya kutafuta bingwa, ingawa ni timu za Dar es Salaam pekee zilizokuwa zikishiriki wakati huo.

Kufika mwaka 1965, ilianzishwa michuano ya Klabu Bingwa Tanzania, ambayo ilikuwa inaanzia ngazi ya Wilaya, ikichezwa kwa mtindo wa mtoano, ingawa pia katika miaka miwili ya mwanzoni, timu za Dar es Salaama pekee ndizo zilizoshiriki.
Katika mfumo huo, bingwa wa kwanza ilikuwa ni klabu ya Sunderland ambayo hivi sasa inajulikana kama Simba SC ya Dar es Salaam, ambayo ilifanikiwa kutetea ubingwa wake msimu uliofuata, kabla ya kuutema kwa Cosmopolitan ya Dar es Salaam pia mwaka 1967.
Lakini wakati wote huo, bado Tanzania ilikuwa haijawa mwanachama wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), hivyo Sunderland hawakuwahi kucheza michuano ya Afrika. Cosmo ingekuwa ya kwanza kucheza Klabu Bingwa Afrika mwaka 1968 kama isingejitoa, lakini kwa kujitoa kwao, Yanga ilifungua historia ya ushiriki wa klabu za Tanzania kwenye michuano ya Afrika mwaka 1969, baada ya kutwaa ubingwa wa nchi kwa mara ya kwanza mwaka 1968, kabla ya kuutetea mara nne mfululizo, katika miaka ya 1969, 1970, 1971 na 1972. Baada ya hapo, Sunderland ikiwa tayari imebadili jina na kuitwa Simba kurejesha taji lake mwaka 1973.





70

Simba ilishindwa kuutetea ubingwa wake msimu uliofuata mwaka 1974 baada ya kupokonywa na Yanga katika fainali ya kihistoria iliyofanyika Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza kwa kuchapwa mabao 2-1.  
Mwaka 1975 Yanga iliutema ubingwa huo kwa Mseto SC ya Morogoro, iliyoweka historia ya kuwa klabu ya kwanza kutoka nje ya Dar es Salaam kutwaa ubingwa wa nchi.
Lakini Mseto ilishindwa kuteteqa taji hilo, ikapokonywa na Simba msimu uliofuata- na Wekundu wa Msimbazi walifanikiwa kutetea ubingwa huo kwa miaka mitano mfululizo, kuanzia mwaka 1976 hadi 1980.
Siri ya kutawala kwa Simba kwenye ligi hiyo kwa miaka yote hiyo ni kuyumba kwa Yanga baada ya kukumbwa na mgogoro mkubwa 1976, uliosababisha kukimbiwa na wachezaji wote nyota, hivyo kuanza upya kabisa kuunda timu. 
Ni ndani ya kipindi hicho Simba iliweza kulipa kisasi cha kuchapwa mabao 5-0 na Yanga mwaka 1968, wakati nayo ilipowatandika watani wao hao wa jadi 6-0 mwaka 1977.  
Juni 1, mwaka 1968 Yanga iliigaragaza Simba 5-0, mabao yake yakitiwa kimiani na Maulid Dilunga (sasa marehemu) katika dakika za 18 kwa njia ya penalti na 43, wakati mengine yalitiwa kimiani na Salehe Zimbwe dakika ya 54 na 89 kabla ya Kitwana Manara kupachika la kuhitimisha karamu ya mabao dakika ya 86.
Julai 19, mwaka 1977 Simba nayo ililipa kisasi kwa kuibugiza Yanga mabao 6-0, wafungaji wakiwa ni Abdallah 'King' Kibadeni aliyetikisa nyavu mara tatu katika dakika za 10, 42 na 89, wakati mengine yalifungwa na Jumanne Hassan 'Masimenti' dakika za 60 na 73 na Selemani Sanga wa Yanga alijifunga dakika ya 20.
Kufika mwaka 1981, tayari Yanga ilikuwa imara tena na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara ingawa msimu uliofuata iliutema kwa Pan African. 
Kuanzia mwaka 1982, mfumo wa Ligi ya Tanzania ulibadilishwa na kukawa na ligi tatu, kwanza ni Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara, Ligi Daraja la Kwanza visiwani Zanzibar na Ligi Kuu ya Muungano.
Yaani baada ya kupatikana washindi wawili wa juu wa kila ligi, Bara na Visiwani, walikutana kwenye Ligi Kuu ya Muungano, kutafuta bingwa wa Tanzania na washindi wake.
Wakati huo, bingwa wa Ligi ya Muungano alikwenda kucheza Klabu Bingwa Afrika na mshindi wa pili alicheza Kombe la Washindi.
Baadaye timu ziliongezwa na kuwa tatu kila upande katika Ligi ya Muungano.
Mwaka 1983, Yanga ilirejesha taji hilo kwenye himaya yake, ingawa msimu uliofuata ililitema tena kwa Simba.  Kwa ujumla muongo mzima wa 1980, taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya Bara lilikuwa la kukoponyana, kwani Simba nayo mwaka 1985 ilipokonywa taji hilo na Yanga, ambayo nayo ililitema kwa timu mpya katika Ligi Kuu msimu wa 1986, Tukuyu Stars ya Mbeya.
Tukuyu nayo iliwarejeshea Yanga taji lao mwaka 1987, wakati mwaka 1988 Wagosi wa Kaya, Coastal Union ya Tanga ilijiingiza katika orodha ya timu zilizowahi kutwaa taji hilo. Mwaka 1989, Yanga ilifunga orodha ya mabingwa ya mabingwa wa muongo huo kwa kutwaa tena ubingwa wa Bara.
Simba iliibuka mwaka 1990 na kutwaa ubingwa huo, ikitoka kuponea chupuchupu kushuka daraja msimu uliopita. 
Kupokonyana taji kuliendelea hata kwenye muongo wa 1990, kwani Simba iliutema ubingwa huo kwa Yanga mwaka 1991.
Yanga iliutetea ubingwa huo mara mbili mfululizo katika miaka ya 1992 na 1993, kabla ya kupokonywa na Simba mwaka 1994. Simba ilifanikiwa kuutetea mara moja 1995.
Mwaka 1996 ndipo Ligi Kuu ya Tanzania Bara ilipozaliwa rasmi chini ya udhamini wa Bia ya Safari Lager, bia inayozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) na ikijulikana kama Safari Lager Premier League, Yanga ndiyo iliyokuwa bingwa wake wa kwanza. Yanga iliutetea ubingwa huo kwa miaka miwili mfululizo 1997 na 1998. Mwaka 1999, Yanga ikiwa tayari imetwaa ubingwa kwa matokeo ya uwanjani, aliyekuwa Waziri wa iliyokuwa Wizara ya Kazi Maendeleo ya Vijana na Michezo, Profesa Juma Athumani Kapuya, alitengua matokeo hayo kwa kuiongezea Mtibwa Sugar pointi za mezani, hivyo kuipiku Yanga. Hatimaye Mtibwa ilipata ubingwa wa mezani.
Mtibwa ilifanikiwa kutetea ubingwa mwaka 2000, kabla ya kupokonywa na Simba msimu uliofuata, ingawa Yanga iliibuka mwaka 2002 na kuutwaa tena ubingwa huo.
Mwaka 2003 Simba iliyokuwa kali zaidi ilifanikiwa kuutwaa tena ubingwa huo na kuutetea mwaka 2004 kabla ya kupokonywa na Yanga 2005 ambao waliutetea 2006. Mwaka 2007, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilifanya mabadiliko ya kalenda yake, ikitaka Ligi yake iendane na ligi za Ulaya, hivyo ikaamua kuchezesha ligi ndogo ya mpito kumpata bingwa na mwakilishi wa Kombe la Shirikisho, kabla ya Ligi Kuu kuanza rasmi Agosti.
Simba iliibuka bingwa wa ligi hiyo, baada ya kuifunga Yanga kwenye fainali kwa mikwaju ya penalti 5-4, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro kufuatia sare ya 1-1.
Lakini msimu uliofuata ikiwa chini ya Profesa wa Kiserbia, Dusan Savo Kondic, Yanga ilifanikiwa kuurejesha ubingwa wake msimu wa 2008 na kutetea msimu uliofuata ikiwa chini ya kocha huyo, ambaye hata hivyo msimu uliopita alitupiwa virago katia mzunguko wa kwanza tu wa ligi na nafasi yake kuchukuliwa na Mserbia mwenzake, Kostadin Bozidar Papic, ambaye alishindwa kubakisha taji Jangwani, baada ya Simba kuchukua kwa kishindo.
Simba ilishinda mechi zote ikiwemo mbili dhidi ya watani wa jadi, Yanga na kutoa sare mbili tu dhidi ya Kagera Sugar Bukoba na African Lyon Dar es Salaam, hivyo kutwaa ubingwa kwa mbwembwe za aina yake na kufanikiwa kuutetea 2010.
Mwaka 2011 Yanga SC walirejesha taji lao, kabla ya 2012 kulitema kwa Simba SC na hatimaye mwaka huu wamelitwaa tena na sasa wanaanza mbio za kulitetea, leo wakifungua dimba na Ashanti United ‘Watoto wa Jiji’ Uwanja wa Taifa.
Wakati Ligi Kuu ikizipoteza timu za African Lyon ya Dar es Salaam, Toto African ya Mwanza na Polisi ya Morogoro zilizoshuka daraja msimu uliopita, msimu huu zimeibuka timu nyingine ambazo ni Mbeya City ya Mbeya, Rhino Rangers ya Tabora na Ashanti United ya Dar es Salaam.
Ashanti imewahi kucheza Ligi Kuu mara mbili na kuteremka katika muongo uliopita, wakati Rhino na Mbeya City zinapanda kwa mara ya kwanza. Ashanti ni timu ya mtaani tu Ilala sokoni na inategemea michango ya wanachama wake wachache kujiendesha- wakati City inamilikiwa na Jiji la Mbeya na Rhino inamilikiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
Kwa ujumla timu mpya, zinatarajiwa kuleta changamoto mpya kwenye Ligi kama ilivyokuwa timu zilizopanda msimu uliopita Prisons ya Mbeya, Mgambo JKT ya Tanga na Polisi, ambayo pamoja na kushuka, lakini ilionyesha ushindani. 
Tukirejea kwenye timu zilizobakia kwenye Ligi msimu uliopita, hakuna uhakika kama Yanga itapata fursa ya kuziacha mbali timu nyingine, kama ilivyokuwa msimu uliopita.   
Kama utakumbuka, Top Four ya msimu uliopita ilikuwa inaundwa na Yanga, Azam FC, Simba SC na Kagera Sugar, hizi zote ni timu ambazo msimu huu ziko vizuri tena. 
Lakini chini yao, Coastal Union, Mtibwa Sugar, JKT Ruvu, Prisons, Mgambo JKT, JKT Oljoro na Ruvu Shooting, nazo zinaonekana kabisa kujiandaa kwa ajili ya msimu huu wa Ligi.
Pazia la kuashiria kufunguliwa kwa msimu uliopita lilipenuliwa rasmi kwa mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Yanga SC na Azam Jumamosi iliyopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Pamoja na Yanga SC kushinda 1-0, bao pekee la kiungo Salum Abdul Telela dakika ya pili tu ya mchezo huo, lakini ilikuwa mechi ngumu ambayo timu yoyote ingeweza kushinda- na hiyo ni ishara kwamba msimu huu wa Ligi Kuu hautakuwa laini.
Hakutakuwa na lelemama katika msimu huu wa Ligi, karibu kila timu inaonekana kuwa madhubuti, itakuwa ligi yenye ushindani kwa kiwango kikubwa kupita msimu uliopita. 
Kilio kikubwa cha wapenzi wa soka nchini ni kuhusu waamuzi, hawa wamekuwa wakilalamikiwa sana kwa kuharibu ladha ya ligi, kutokana na kuzibeba baaadhi ya timu.
Kuna kashfa ya rushwa kwa waamuzi Ligi Kuu, kuna timu zinatuhumiwa kuhonga marefa ili zisaidiwe kushinda, hili bado TFF haijatoka na jibu sahihi, lakini kweli waamuzi wanavurunda.   Pamoja na yote, matarajio yanabaki pale pale, itakuwa ligi yenye ushindani mkubwa na ubingwa utapatikana kwa jasho haswa. 
Neema zaidi imeletwa na kampuni ya Azam TV iliyonunua haki za matangazo ya Televisheni, ambayo inafanya kila klabu ipatiwe zaidi ya Sh. Milioni 100 kwa msimu. Wazi, fedha hizi zitasaidia sana klabu, pamoja na zile za wadhamini wa Ligi Kuu, Vodacom maana yake timu zitapunguza matatizo ya kifedha kwa kiasi kikubwa. Karibu Ligi Kuu, kilele cha ladha ya soka ya Tanzania. Zingatia, naitwa Mahmoud Ramadhani Zubeiry, au BIN ZUBEIRY, ndiye nimeandika makala haya. Furahia msimu mpya wa Ligi Kuu.

MABINGWA WA JUMLA LIGI KUU:

1965 : Sunderland (Dar es Salaam) 
1966 : Sunderland (Dar es Salaam) 
1967 : Cosmopolitans (Dar es Salaam) 
1968 : Yanga 
1969 : Yanga 
1970 : Yanga 
1971 : Yanga 
1972 : Yanga 
1973 : Simba 
1974 : Yanga 
1975 : Mseto SC (Morogoro) 
1976 : Simba 
1977 : Simba 
1978 : Simba 
1979 : Simba 
1980 : Simba 
1981 : Yanga 
1982 : Pan African 
1983 : Yanga 
1984 : Simba 
1985 : Yanga 
1986 : Tukuyu Stars (Mbeya) 
1987 : Yanga 
1988 : Coastal Union (Dar es Salaam) 
1989 : Yanga 
1990 : Simba  
1991 : Yanga 
1992 : Yanga 
1993 : Yanga 
1994 : Simba 
1995 : Simba 
1996 : Yanga 
1997 : Yanga 
1998 : Yanga 
1999 : Mtibwa Sugar (Morogoro) 
2000 : Mtibwa Sugar (Morogoro)  
2001 : Simba 
2002 : Yanga 
2003 : Simba 
2004 : Simba 
2005 : Yanga 
2006 : Yanga 
2007 : Simba (Ligi Ndogo) 
2008 : Yanga 
2009:  Yanga  
2010:  Simba 
2011:  Yanga
2012:  Simba 
2013:  Yanga 
2014:  ?????