Wednesday, October 31, 2012

YANGA SASA TISHA MBAYA, SIMBA CHUPUCHUPU MOROGORO

Msuva kushoto na Domayo kulia, wakimpongeza
Kavumbangu kufunga bao la pili


YANGA SC imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya jioni ya leo kuichapa Mgambo JKT ya Handeni, Tanga mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi huo, unaifanya Yanga sasa iwe na pointi sawa na mabingwa watetezi, Simba SC waliotoa sare ya 1-1 na Polisi mjini Morogoro leo, ingawa inazidiwa bao moja tu katika wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Hadi mapumziko, Yanga walikuwa mbele kwa mabao 2-0, yaliyotiwa kimiani na beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na mshambuliaji Didier Kavumbangu.
Cannavaro alifunga kwa kichwa akiunganisha krosi ya Oscar Joshua dakika ya pili kutoka wingi ya kulia, wakati Kavumbangu alimalizia pasi ya Hamisi Kiiza dakika ya 39.
Pamoja na kutoka uwanjani wamelowa kipindi cha kwanza, lakini Mgambo JKT walicheza soka ya kuvutia na mara mbili walikaribia kufunga kupitia kwa Juma Mwinyimvua.
Yanga walicheza vema dakika 45 za kipindi cha kwanza, tofauti sana na mechi za awali ambazo wamekuwa ‘wakichezewa’ sana na wapinzani.
Ilishuhudiwa katika kipindi hicho, Yanga wakimiliki zaidi mpira na kupeana pasi za uhakika, ingawa mashambulizi yao mengi walipitisha pembeni, hasa upande wa kulia.
Hamisi Kiiza, Msuva na Kavumbangu walicheza kwa uelewano mkubwa pale mbele na kulitia misukosuko haswa lango la Mgambo. 
Kipindi cha pili, Yanga walirudi na moto wao tena na kuendelea kuwachachafya Mgambo.
Hata hivyo, iliwachukua Yanga dakika 34 kupata bao la tatu, mfungaji akiwa ni Jerry Tegete aliyeingia dakika ya 68 kuchukua nafasi ya Kavumbangu.
Tegete alifunga bao hilo akiunganisha krosi maridadi ya beki wa kushoto, Oscar Joshua.
Pamoja na kufungwa, Mgambo waliendelea kusukuma mashambulizi langoni mwa Yanga, ingawa leo mabeki wa timu hiyo, inayofundishwa na Mholanzi, Ernie Brandts walicheza kwa uelewano mkubwa na kudhibiti hatari zote langoni mwao.  
Mgambo inayofundishwa na Mohamed Kampira, ilipata pigo dakika ya 85, baada ya beki wake wa kulia, Salum Mlima kutolewa kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa kumchezea rafu mbaya Mbuyu Twite.
Baada ya mchezo huo, Brandts alisema dakika 10 za mwanzo timu yake ilikuwa inashindwa kumalizia vizuri mashambulizi yake, lakini baadaye ikatulia na hatimaye kupata ushindi huo, ambao ameufurahia kwani unamuweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
Kwa upande wake, Kampira wa Mgambo alisema kufungwa ni sehemu ya mchezo, akawasifu Yanga kwa kutumia nafasi walizopata, huku akijutia nafasi walizopoteza wachezaji wake leo.
Kikosi cha Yanga leo kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Nsajigwa Shadrack/Kevin Yondan dk 46, Oscar Joshua, Mbuyu Twite, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Athumani Iddi ‘Chuji’, Simon Msuva, Frank Domayo/Nurdin Bakari dk 76, Didier Kavumbangu/Jerry Tegete dk68, Hamisi Kiiza na Haruna Niyonzima.
Mgambo JKT; Godson Mmasa, Salum Mlima, Yassin Awadh, Salum Kipanga/Godfrey Komba dk80, Bakari Mtama, Ramadhani Malima, Chande Magoja, Mussa Ngunda, Issa Kandulu/Nassor Gumbo dk 60, Fully Maganga na Juma Mwinyimvua/Omar Matwiko dk76.
Katika mchezo wa utangulizi, timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Yanga, imeifunga Mgambo JKT ya vijana pia 1-0, bao hilo pekee la Clever Charles dakika ya 65.
Katika mechi nyingine, Simba ilitoka sare ya 1-1 Polisi kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, wenyeji wakitangulia kupata bao dakika ya 35 kupitia kwa Mokili Rambo kabla ya Amri Kiemba kusawazisha dakika ya 57.

 



SIRI YA BUNJAK KUFUKUZWA AZAM HII HAPA

Bunjak

WACHEZAJI wa Azam ndio waliomponza kocha Mserbia, Boris Bunjak kufukuzwa kazi jana, baada ya kuuandikia barua uongozi, wakisema hawaridhishwi na ufundishaji wa kcoha huyo na hawamtaki.
Pamoja na kumchongea kwa uongozi Mserbia huyo, habari za ndani kutoka Azam zimesema kwamba, ni wachezaji hao hao waliopendekeza katika barua yao kurejeshwa kwa aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Muingereza Stewart Hall.
Habari zilizopatikana jana kutoka Azam FC, zilisema kwamba, sababu za kufukuzwa kwa Mserbia huyo ni kushuka kwa kiwango cha timu, hali iliyosababisha sasa ianguke hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
Tayari Bunjak amekwishapewa haki zake zote na ataondoka kesho, siku ambayo Stewart anaweza kuwasili kuanza tena kazi Azam FC.
Bunjak anaondoka Azam baada ya kuiongoza timu katika mechi 16, akifungwa nne tu, zote dhidi ya Simba ikiwemo ya juzi ya Ligi Kuu, waliyofungwa 3-1 na kutoa sare tatu.
Bunjak mwenye leseni ya Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA), alitua Azam, Agosti 7, mwaka huu akitokea FC Damac ya Saudia Arabia aliyoanza kuifundisha mwaka jana na kabla ya hapo alifundisha klabu kibao za kwao, zikiwemo FK Sloga Kraljevo, FK Javor Ivanjica, Crvena Zvezda Gnjilane, FK Radnicki Nis, FC Uralan Elista, FK Mladi Radnik, FK Crvena Zvezda Beograd, Al-Shaab, FK Hajduk Kula na Al-Nasr.
Awali, Bunjak aliyezaliwa Novemba 17, mwaka 1954 ( miaka 57), alicheza soka katika klabu za FK Sloga (Kraljevo), FK Vozdovac (Beograd), FK Radnicki (Kragujevac), FK Olimpia (Ljubljana), FK Sumadija (Arandjelovac), FK Sloga (Kraljevo), FK Borac (Cacak) na FK Sloga (Kraljevo).
Stewart alifukuzwa kwa kosa la kukaidi maagizo ya Bodi ya Ukurugenzi ya klabu hiyo, kumpanga Mrisho Khalfan Ngassa katika mechi ya fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame dhidi ya Yanga.
Mserbia huyo anakuwa kocha wa tano kufukuzwa Azam, ndani ya miaka minne tangu ianze kucheza Ligi Kuu, 2008 baada ya Stewart, Mbrazil Neider dos Santos, Sylvester Marsh na Itamar Amorin, Mbrazil mwingine.
Lakini Stewart angalau aliacha kumbukumbu ya taji na Medali Azam, baada ya kuiwezesha kutwaa Kombe la Mapinduzi Januari, kushika nafasi ya pili katika Ligi Kuu Aprili, kabla ya kushika nafasi ya pili Kombe la Urafiki na Kagame mwezi uliopita, mambo ambayo bila shaka yamemfanya afikiriwe tena.
Stewart ana sifa ya kutokuwa mbinafsi na mwenye kuwaamini watu wa chini yake, kwa mfano namna ambavyo alikuwa akimpromoti Kali Ongala. Alimkuta Kali kama mchezaji, lakini kwa sababu ya umri kumtupa mkono, akashauriana naye awe Kocha Msaidizi na mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga, akakubali.
Chini ya Stewart, Kali alikuwa akiachiwa timu aiongoze ili kumjengea kujiamini zaidi na mwezi uliopita aliachiwa timu kwenye Kombe la Urafiki, akaifikisha fainali, ambako ilifungwa na Simba kwa penalti kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90.  
REKODI YA BORIS BUNJAK AZAM
Azam 2-1 Polisi                   (BancABC)
Azam 1-2 Simba B              (BancABC)
Azam 8-0 Trans Camp        (Kirafiki)
Azam 1-0 Prisons               (Kirafiki)
Azam 2-0 Coastal Union     (Kirafiki)
Azam 2-3 Simba SC           (Ngao ya Jamii)
Azam 1-0 Kagera Sugar     (Ligi Kuu)
Azam 2-2 Toto African        (Ligi Kuu)
Azam 3-0 JKT Ruvu           (Ligi Kuu)
Azam 1-0 Mtibwa Sugar     (Ligi Kuu)
Azam 1-0 African Lyon       (Ligi Kuu)
Azam 2-3 Simba SC           (Kirafiki)
Azam 1-0 Polisi                  (Ligi Kuu)
Azam 0-0       Prisons         (Ligi Kuu)                                      
Azam 1-1 Ruvu Shooting   (Ligi Kuu)
Azam 1-3 Simba                (Ligi Kuu)

 

YANGA B WAITILIA UBANI YANGA A, WAYACHAPA KIDUDE MAKINDA YA MGAMBO


Timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Yanga, imeifunga Mgambo JKT ya vijana pia, bao 1-0 katika mchezo wa utangulizi, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kabla ya kuanza kwa mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baina ya kaka zao, Yanga A dhidi ya Mgambo JKT ya Handeni, Tanga. Bao hilo pekee lilitiwa kimiani na Clever Charles dakika ya 65.
Zuberi Amiri wa Yanga B, akichuana na Charles Domayo wa JKT Mgambo

Joseph Banda wa Yanga B (25) akipasua ukuta wa Mgambo

Meshack Ramadhani wa Yanga kushoto akigombea mpira na beki wa Mgambo

Banda akifumua shuti mbele ya mabeki wa Mgambo, mmoja akijaribu kuzuia

Notikel Masasi wa Yanga B akiwa chini ya ulinzi wa mabeki wa Mgambo

Kocha Ernie Brandts akifuatilia vipaji Yanga B ikicheza na Mgambo

Notikel Masasi wa Yanga B, akichuana na mchezaji wa Mgambo

Clever Charles, mfungaji wa bao la Yanga B leo, akiwa benchi baada ya kupumzishwa. Kulia kwake ni Said Manduta.

LIGI KUU YA VODACOM SASA KWENYE MTANDAO

MILIONEA SEIF MAGARI AKUBALI KUGOMBEA UENYEKITI DRFA

Seif Ahmad 'Magari'
KIGOGO wa Yanga, Seif Ahmad ‘Magari’ amekubali kugombea Uenyekiti wa Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA), baada ya kuombwa na wazee na wadau wa soka mkoani Dar es Salaam.
Wadau wa soka Dar es Salaam tangu wiki iliyopita wamekuwa wakimbembeleza Seif kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo, wakiahidi kumuunga mkono mfanyabiashara huyo wa magari na fedha za kigeni kwa asilimia 100 ashinde nafasi hiyo.
Seif amesema leo kwamba amekubali wito huo wa wana Dar es Salaam na atachukua fomu ya kuwania nafasi hiyo.
Lini? “Itakapokuwa tayari nitakuambia, ila jambo la msingi tu nimekubali,”alisema Seif. Seif amekuwa kwenye Kamati za Yanga tangu wakati wa uongozi wa Francis Mponjoli Kifukwe miaka saba iliyopita na pia amewahi kuwa mmiliki mshiriki wa klabu ya Moro United iliyokuwa Ligi Kuu.
Seif ameendelea kuwa ndani ya Kamati za Yanga katika zama za viongozi waliomfuatia Kifukwe katika klabu hiyo, Imani Madega, Lloyd Nchunga na sasa Yussuf Manji.
Iwapo Seif atachukua fomu, kuna uwezekano mpinzani wake mkuu akawa, Mwenyekiti wa zamani wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Evans Aveva ambaye naye pia ana uzoefu wa kutosha katika uongozi wa soka.
Aveva, aliyekuwa Meneja wa Hoteli ya Embassy na sasa mfanyabiashara mwenye maduka kibao ya simu, amekuwa kwenye Kamati mbalimbali za uongozi Simba tangu enzi za Yussuf Hazali, Mwenyekiti wa klabu hiyo na ameendelea pia hata katika zama za viongozi waliofuatia akina Juma Salum (sasa marehemu) na Hassan Daalal.
Aveva pia amewahi kuwa mmoja wa viongozi wa iliyokuwa Tanzania Stars, timu iliyokuwa ikiundwa na wachezaji wakongwe nchini, ambayo mwaka 1998 na 1999 ilicheza Kombe la Washindi Afrika.
Uchaguzi wa DRFA utafanyika Desemba 8, mwaka huu na fomu za kugombea nafasi mbalimbali zilianza kutolewa tangu jana, wakati Novemba 4 hadi 8, Kamati ya Uchaguzi, chini ya Mwenyekiti wake, Juma Simba itapitia fomu za walioomba uongozi.
Novemba 9 hadi 13 utakuwa muda wa pingamizi kwa wagombea, ambazo zitajadiliwa Novemba 14 hadi 16, wakati Novemba 17 hadi 19 watatoa fursa ya kukata rufaa, ambazo zitasikilziwa Novemba 20 hadi 24 na baada ya hapo, Novemba 25 yatatangazwa majina ya wagombea waliopitishwa.
Uchaguzi wa DRFA utafanyika siku chache tu kabla ya uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), mwishoni mwa Desemba, mwaka huu.  

 

FA YASUBIRI TAARIFA KUTOKA SERBIA JUU YA KUFUNGIWA WACHEZAJI WAKE KUTOKANA NA VURUGU.

CHAMA cha Soka nchini Uingereza-FA kimethibitisha kuwa hawajapewa taarifa juu ya uamuzi wa maofisa wa polisi nchini Serbia kuwahusisha wachezaji wawili wa timu ya taifa chini ya miaka 21 ya Uingereza kwa vurugu.
 
 Shirikisho la Soka nchini Serbia liliwafungia viungo Nokla Ninkovic na mshambuliaji Ognjen Mundrinski kucheza katika timu za taifa lakini mamlaka ya kisheria ilitangaza kuwashitaki watu 12 katika vurugu hizo yakiwemo majina mawili ya Uingereza.
 
 Katika taarifa ya FA ilithibitisha kuwa hawajapata taarifa rasmi zozote kuhusu kufungiwa kwa wachezaji wake na shirikisho la soka ya Serbia na kwamba wanasubiri maelezo zaidi kuhusiana na sakata hilo. 
 
 Taarifa hiyo ilimalizwa kwa kusema FA itawapa msaada wachezaji pamoja na viongozi waliokumbana na sakata hilo nchini Serbia wiki mbili zilizopita.

DJOKOVIC AJIHAKIKISHIA KUMALIZA NAMBA MOJA.

MCHEZA tenisi nyota kutoka Serbia, Novak Djokovic amejihakikishia nafasi ya kumpita mpinzani wake Roger Federer na kumaliza mwaka 2012 akiwa kinara katika orodha za ubora duniani kwa upande wa wanaume.

 Djokovic alipoteza nafasi yake hiyo kwa Federer mwenye umri wa miaka 31 baada ya kunyakuwa michuano ya Wimbledon lakini Federer ambaye anatoka Switzerland hataweza kutetea taji la Paris Masters.

 Kutokuwepo kwa Federer katika michuano hiyo mikubwa ya dunia ya mwisho kwa mwaka huu ambayo itafanyika Novemba 5 kunampa nafasi Djokovic kurejea katika kiti chake. 

 Djokovic mwenye umri wa miaka 25 anakuwa nyota wa kwanza kumaliza mwaka katika nafasi ya kwanza mfululizo toka Federer alipofanya hivyo kuanzia mwaka 2004 mpaka 2007.

 

CAPITAL ONE CUP: MECHI YA MIGOLI 12, Arsenal yashinda 7-5!!


ARSENE_WENGER-13>>THEO WALCOTT APIGA HETITRIKI!!
Katika Mechi za Raundi ya 4 ya Mtoano ya CAPITAL ONE CUP zilizochezwa Jumanne Usiku, Mechi ya ajabu na vuta nikuvute ni ile iliyochezwa Uwanja wa Madejski ambapo Reading waliongoza 4-0, mapumziko kuwa 4-1 mbele lakini Arsenal wakasawazisha na kuifanya gemu iwe 4-4 hadi Dakika 90 na katika Dakika 30 za nyongeza Arsenal walikwenda mbele 5-4, Reading wakarudisha na kuwa 5-5 na hatimae Arsenal kuibuka Mshindi 7-5 huku Theo Walcott akipiga hetitriki.
+++++++++++++++++++++++++
CAPITAL ONE CUP-MATOKEO:
RATIBA RAUNDI ya 4:
Jumanne Oktoba 30
Sunderland 0 Middlesbrough 1
Swindon 2 Aston Villa 3
Wigan 0 Bradford 0 [Baada Dakika 120, Mshindi Bradford 4-2 kwa Mikwaju ya Penati]
Leeds 3 Southampton 0
Reading 4 Arsenal 4 [Baada Dakika 120, Mshindi Arsenal Bao 7-5]
+++++++++++++++++++++++++
READING 5 ARSENAL 7
MAGOLI:
Reading
-Jason Roberts, 12
-Koscielny, 19
-Leigertwood, 20
-Hunt, 37
-Pogrebnyak, 115
Arsenal
-Walcott, 45, 90 & 120
-Giroud, 64
-Koscielny, 89
-Chamakh, 103 & 120
VIKOSI:
Reading: Federici, Gunter, Gorkss, Morrison, Shorey, Tabb, McCleary, Leigertwood, Robson-Kanu, Roberts, Hunt
Akiba: Stuart Taylor, Pearce, Pogrebnyak, Le Fondre, McAnuff, Church, Harte.
Arsenal: Martinez, Jenkinson, Koscielny, Djourou, Miquel, Arshavin, Frimpong, Coquelin, Walcott, Chamakh, Gnabry
Akiba: Shea, Giroud, Squillaci, Bellerin, Eisfeld, Meade, Yennaris.
Refa: Kevin Friend

WIGAN 0 BRADFORD 0
Bradford washinda kwa Penati 4-2 baada ya sare ya 0-0 katika Dakika 120.
VIKOSI:
Wigan: Al Habsi, Ramis, Watson, Lopez, Stam, Fyvie, Jones, Redmond, Gomez, Boselli, McManaman
Akiba: Pollitt, Kone, Maloney, Beausejour, Golobart, Kiernan, Orsula.
Bradford: Duke, Darby, McHugh, McArdle, Meredith, Hines, Thompson, Doyle, Atkinson, Wells, Hanson
Akiba: McLaughlin, Connell, Gary Jones, Baker, Brown, Bass, Swain.
Refa: Roger East

SUNDERLAND 0 MIDDLESBROUGH 1
MFUNGAJI: McDonald, 39
VIKOSI:
Sunderland: Westwood, Bardsley, O'Shea, Cuellar, Colback, Johnson, Cattermole, Vaughan, Sessegnon, Fletcher, Saha
Akiba: Mignolet, Campbell, Wickham, McFadden, Kilgallon, Meyler, McClean.
Middlesbrough: Steele, Hoyte, Hines, Bikey, Friend, Ledesma, Leadbitter, Bailey, Haroun, Miller, McDonald
Akiba: Leutwiler, Zemmama, Halliday, Parnaby, Park, Reach, Smallwood.
Refa: Phil Dowd

SWINDON 2 ASTON VILLA 3
MAGOLI:
Swindon
-Sorey, 78 & 81
Villa
-Benteke, 30 & 90
-Agbonlahor, 39
VIKOSI:
Swindon: Foderingham, Devera, McCormack, Flint, McEveley, Ritchie, Miller, Ferry, Roberts, Benson, Collins
Akiba: Bedwell, Archibald-Henville, Nathan Thompson, Williams, Louis Thompson, Storey.
Aston Villa: Given, Lowton, Herd, Vlaar, Lichaj, Weimann, Ireland, El Ahmadi, Bannan, Agbonlahor, Benteke
Akiba: Guzan, Bent, Albrighton, Holman, Delph, Stevens.
Refa: Stuart Attwell

LEEDS 3 SOUTHAMPTON 0
MAGOLI:
-Tonge, 35
-El Hadj Diouf, 88
-Becchio, Penati, 90
VIKOSI:
Leeds: Ashdown, Peltier, Lees, Pearce, White, Byram, Austin, Brown, Tonge, Varney, Diouf
Akiba: Kenny, Drury, Green, Becchio, Pugh, Norris, Gray.
Southampton: Kelvin Davis, Butterfield, Hooiveld, Seaborne, Reeves, Mayuka, Chaplow, De Ridder, Ward-Prowse, Lee, Do Prado
Akiba: Gazzaniga, Shaw, Stephens, Chambers, Hoskins, Sinclair, Isgrove.
Refa: Chris Foy
+++++++++++++++++++++++++

CAPITAL ONE CUP
RATIBA RAUNDI ya 4:
Mechi kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku, Bongo Taimu
Jumatano Oktoba 31
Norwich v Tottenham
Liverpool v Swansea [SAA 5 Usiku]
Chelsea v Manchester United