Tuesday, January 15, 2013

BPL: MECHI PEKEE LEO, KIPORO CHELSEA v SOUTHAMPTON!

BPL, BARCLAYS PREMIER LEAGUE
Jumatano Januari 16
[SAA 4 DAK 45 Usiku]
Chelsea v Southampton

MABINGWA wa ULAYA, Chelsea, leo Usiku watakuwa kwao Stamford Bridge kucheza Mechi yao ya Kiporo cha BPL, Barclays Premier League, dhidi ya Southampton.
Mechi hii ilikuwa ichezwe Mwezi Desemba lakini iliahirishwa kwa vile Chelsea walisafiri kwenda kwenye Mashindano ya FIFA ya Klabu Bingwa Duniani huko Japan.
Wakiwa nafasi ya 3 kwenye Ligi, Pointi 7 nyuma ya Man City na Pointi 14 nyuma ya Vinara Man United, Chelsea wana umuhimu wa kushinda Mechi dhidi ya Southampton ambao wako nafasi ya 15 na wana Pointi 21, ili wao wapunguze pengo dhidi ya Klabu za Jiji la Manchester.
Katika Mechi 6 zilizopita za Ligi, Chelsea wameshinda Mechi 5.

MSIMAMO-Timu za Juu:
1 Man United Mechi 22 [Tofauti ya Magoli 27] Pointi 55
2 Man City Mechi 22 [Tofauti ya Magoli 24] Pointi  48
3 Chelsea Mechi 21 [Tofauti ya Magoli 24] Pointi 41
4 Tottenham Mechi 22 [Tofauti ya Magoli 22] Pointi 40
5 Everton Mechi 22 [Tofauti ya Magoli 22] Pointi 37
6 Arsenal Mechi 21 [Tofauti ya Magoli 16] Pointi 34
7 West Brom Mechi 22 [Tofauti ya Magoli 1] Pointi 33
8 Liverpool Mechi 22  Tofauti ya Magoli 7] Pointi 31
9 Swansea Mechi 22 [Tofauti ya Magoli 5] Pointi 30
10 Stoke Mechi 22 [Tofauti ya Magoli -3] Pointi 29

Baada ya kuwa na wasiwasi wa kuwakosa Mastraika wao Demba Ba na Fernando Torres ambao walikuwa wakisumbuliwa na maumivu ya paja kwa Ba na ugonjwa kwa Torres, Chelsea wamethibitisha Wachezaji hao wote wako fiti.

MECHI NYINGINE LEO USIKU:
FA CUP-Raundi ya 3=MARUDIANO
Jumatano Januari 16
[SAA 4 Dak 30 Usiku]
Arsenal v Swansea City
[SAA 5 Usiku]
Man Utd v West Ham

DEMBA_BA-ATUA_CHELSEALakini, upo uwezekano wa Chelsea kutomuanzisha Nahodha wao John Terry ambae amepona Goti lakini bado anakosa pumzi kwa Mechi.
Pia Chelsea itawakosa Wachezaji wawili kutoka Nigeria, John Obi Mikel na Victor Moses, ambao wako na Timu ya Taifa kwa ajili ya AFCON 2013 inayoanza Jumamosi hii.
Kwa upande wa Southampton, Wachezaji watakaokosekana ni Chipukizi wa Miaka 17 Luke Shaw, Jose Fonte na Nahodha wao Adam Lallana wote wakiwa na maumivu.
USO kwa USO:
-Chelsea wameshinda Mechi 5 za mwisho walizocheza na Southampton na kufunga Jumla ya Bao 15.
-Mara ya mwisho Southampton kushinda Stamford Bridge ilikuwa Bao 4-2 Mwaka mpya 2002 huku Straika wao hatari wakati huo, James Beattie, akipiga Bao 2.

BPL, BARCLAYS PREMIER LEAGUE
RATIBA:
Jumamosi Januari 19
[SAA 12 Jioni]
Liverpool v Norwich
Man City v Fulham
Newcastle v Reading
Swansea v Stoke
West Ham v QPR
Wigan v Sunderland
[SAA 2 na Nusu Usiku]
West Brom v Aston Villa
Jumapili Januari 20
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Chelsea v Arsenal
[SAA 1 Usiku]
Tottenham v Man United

ALIYEMTOA JASHO TENGA 2008 ACHUKUA FOMU LEO URAIS TFF


JAMAL Emil Malinzi, Mwenyekiti wa Chama cha Soka Kagera (KRFA), anatarajiwa kuchukua fomu ya kugombea Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo mchana, makao makuu ya shirikisho hilo, Ilala mjini Dar es Salaam. 
Habari ambazo  tumezipata kutoka kwa watu wa karibu wa Katibu huyo wa zamani wa klabu ya Yanga, zimesema kwamba Malinzi atachukua fomu mchana wa leo.
Katika uchaguzi uliopita wa TFF uliofanyika Desemba 14, mwaka 2008, Malinzi alikuwa mpinzani mkuu wa rais anayemaliza muda wake, Leodegar Chillah Tenga ambaye amekwishatangaza hagombei tena.
Katika uchaguzi huo, uliofanyika kwenye ukumbi wa NSSF Water Front, Dar es Salaam, Tenga alishinda kwa kura 64 kwa 39.
Awali, Malinzi alienguliwa kwa kigezo cha uzoefu, lakini akarejeshwa kuwania nafasi hiyo baada ya kushinda rufaa yake.
Katika uchaguzi huo ulioshuhudiwa na Mwakilishi wa FIFA, Ashford Mamelodi, Athumani Nyamlani alishinda nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, baada ya kujikusanyia kura 65 kati ya kura 107 zilizopigwa na kura mbili kuharibika, akimshinda Lawrence Mwalusako aliyepata kura 39 na Ali Mwanakatwe aliyeambulia kura moja.
Nafasi ya Makamu wa Pili wa Rais, ambayo kwa sasa imefutwa, ilikwenda kwa Ramadhani Nassib aliyemwangusha mpinzani wake wa karibu, Damas Ndumbaro aliyepata kura 45.
Hadi sasa, mbali na Malinzi mgombea mwingine anayetarajiwa katika nafasi ya Urais ni Athumani Nyamlani, Makamu wa kwanza wa sasa wa Rais wa TFF.
Jumla ya watu 26 hadi jana walikuwa wamekwishachukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali, kuelekea uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Februari 24, mwaka huu.
Hata hivyo, idadi hiyo ni kwa wale wanaochukua fomu hizo katika ofisi za TFF, kwani vilevile zinapatikana kupitia tovuti ya TFF ya www.tff.or.tz ambapo mwisho wa kuchukua na kurejesha ni saa 10 kamili alasiri Januari 18 mwaka huu.
Waliochukua jana ni Michael Wambura anayewania umakamu wa rais wakati kwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji ni Mbasha Matutu, Muhsin Balhabou, Salum Chama, Titus Osoro na Zafarani Damoder.
Idadi kamili ya waliochukua ni Michael Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace Karia (Makamu wa Rais). Kwa upande wa wajumbe na kanda zao kwenye mabano ni Salum Chama (Kagera na Geita), Mugisha Galibona, Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano (Mara na Mwanza).
Epaphra Swai na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo, Elly Mbise na Twahili Njoki (Arusha na Manyara), Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi na Rukwa) na James Mhagama (Njombe na Ruvuma).
Athuman Kambi (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na Singida), Farid Nahdi (Morogoro na Pwani), Khalid Mohamed (Kilimanjaro na Tanga) na Muhsin Balhabou, Shaffih Dauda na Zafarani Damoder (Dar es Salaam).
Naye Said Mohamed amechukua fomu ya kuwania umakamu mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board).

SIMBA SC KUMSAKA TARATIBU MBADALA WA OKWI BAADA YA JANA KUMUUZA KW AKLABU YA ETOILE DU SAHEL YA TUNISIA


Rage kulia akiwa na rais wa Etoile, kushoto na Okwi katikati jana baada ya kumaliza biashara mjini Tunis, Tunisia 


KLABU ya Simba imesema kwamba haitafanya haraka kuziba nafasi ya mshambuliaji wake wa kimataifa wa Uganda, Emannuel Okwi iliyemuuza Etoile du Sahel ya Tunisia jana.
Hans Poppe
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe alisema jana kwamba kwa kuwa wamekwishakamilisha usajili wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika na muda wa kusajili unaisha leo, hawatafanya haraka ya kusajili mchezaji mwingine.
“Daima sisi huwa tunasajili kwa makini na matunda yake ni kuuza wachezaji kwa bei nzuri, mfano Patrick Ochan, Mganda mwingine tuliyemuuza TP Mazembe (ya DRC), hivyo hatutafanya papara tena katika kusajili, ili tupate mkali kama au zaidi ya Okwi,”alisema Poppe.
Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) alisema kwamba watasubiri kuona kama watafuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ndipo wasajili mchezaji mwingine, vinginevyo itakuwa hadi msimu ujao.
Simba jana ilimuuza Okwi klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia kwa dau la dola za Kimarekani 300,000, zaidi ya Sh Milioni 450 za Tanzania.
Okwi, aliyezaliwa Desemba 25, mwaka 1992 aliisajiliwa Simba akitoea SC Villa ya Uganda mwaka 2010 akiwa kinda wa miaka 17, akisajiliwa kwa dau la dola za Kimarekani 40,000.
Baada ya kumaliza mkataba wake wa awali, Desemba mwaka jana aliongeza mkataba wa miaka miwili na Simba SC ambao kabla hajaanza kuutumikia, anahamia Sahel.

BENITEZ NOT THREATENED BY GUARDIOLA BAADA YA KUTANGAZA KUJA ENGLAND


GUARDIOLA AZIWEKA MKAO WA KULA CHELSEA NA MAN CITY, ASEMA ANAPENDA KUFUNDISHA ENGLAND


Pep Guardiola has fuelled the intrigue surrounding his future by stressing his desire to work in England. 
Guardiola sent a message of congratulations to the Football Association as they prepared to launch their 150th anniversary celebrations in London on Wednesday. 
And just like Jose Mourinho, who sent a similar message 24 hours earlier, he outlined his ambitions to coach in England, comments sure to alert the biggest clubs in the country.
Scroll down for video
In demand: A host of Premier League clubs are interested in Guardiola's services
In demand: A host of Premier League clubs are interested in Guardiola's services
'As a player, I couldn't realise my dream to play there,' said Guardiola.
'But I hope in the future I have a challenge to be a coach or a manager there and feel the experience of all the coaches and players that have been there. 
'It is unique, to play in that league. I want to feel the supporters, the environment, the media and the style of the players.
'I am still young, just 41, so I hope in the future I could train there and enjoy that. I have always found English football very fascinating. The support of the home team is amazing. 
Star man: Guardiola built one of the world's best teams while at Barcelona
Star man: Guardiola built one of the world's best teams while at Barcelona
'In Italy, Latin people will support you when you are playing and when you lose, they kill you. In England, I'm always surprised people always support everything and that is nice. That's why I hope to have the challenge to train there.' 
Guardiola has been coveted by the biggest clubs in the world since stepping down as Barcelona coach last year after creating one of the best teams of all time. 
He has spent much of his time in New York, improving his English, and Chelsea, Manchester City, Manchester United and Arsenal have all been linked with a move for his services. 
Anniversary: The Football Association are celebrating 150 years
Anniversary: The Football Association are celebrating 150 years
His plan is to return to work this summer and speculation this week linked him with Bayern Munich, but the Catalan told the FA of his special bond with England and Wembley. 
He added: 'I had the opportunity to play two finals at Wembley and that's why my relationship with England is pretty close.
'I played there twice, once as a player when I was 19 and it was my first Champions League as a player, as Barcelona finally won the Champions League. It was a huge honour to play at the old Wembley. 
'When I was manager of Barcelona, for our second Champions League in three years, it was a real pleasure to play in the new Wembley. 
'Congratulations on this huge anniversary, because 150 years is a lot of years. 'Also because they created the rules of football and have a responsibility for the game. They have been important in the development of our beautiful, beautiful game.'

GORDON STRACHAN MENEJA MPYA SCOTLAND

GORDON_STRACHAN
>>STRACHAN ADAI: 'FALSAFA YANGU NI KUSHINDA KAMA MAN UNITED!'
Chama cha Soka cha Scotland, SFA, kimethibitisha uteuzi wa Gordon Strachan kama Meneja mpya wa Timu ya Taifa ya Scotland.
Strachan, mwenye Miaka 55, amekuwa hana kibarua tangu atoke Klabu ya Middlesbrough Oktoba 2010 lakini sasa amepewa kuiongoza Nchi ya Utaifa wake hadi baada ya EURO 2016.
Akipokea uteuzi huu, Strachan alisema: "Kila Klabu unayokwenda zipo changamoto, na sasa ni mara ya kwanza changamoto zipo mbele ya Taifa. Ukifanikiwa utalifanya Taifa lote liwe na furaha na kujisikia fahari na hicho ni kipaumbele kwangu kuweza kufanya hivyo kwa kusaidiwa na Watu wengine."

Gordon Strachan
-Alianza kucheza Soka Klabu ya Dundee huko Scotland kabla kujiunga Aberdeen Mwaka 1977.
-Alitwaa Ubingwa mara mbili, Scotland Cup mara 3, Kombe la Washindi Ulaya na European Super Cup akiwa na Aberdeen.
-1984 alijiunga na Manchester United na kutwaa FA Cup Mwaka 1985.
-Alidumu Leeds United Miaka 6 na kuiwezesha kupanda Daraja na kutwaa Ubingwa Daraja la juu.
-Ang’atuka Uchezaji akiwa na Coventry na kuingia Umeneja ambako alikaa Miaka mitano.
-Alifika Fainali ya FA CUP akiwa Bosi wa Southampton ambako alikaa Miaka mitatu.
-Mwaka 2005 ajiunga na Celtic kama Meneja na kutwaa Ubingwa mara 3 na kuifikisha Raundi ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI mara mbili.
-Mwaka 2009 awa Meneja wa Middlesbrough na kukaa Mwaka mmoja.

Akizungumzia malengo yake na Scotland, Strachan amesema anataka kuipeleka Nchi hiyo Fainali za Kombe la Dunia na EURO, kibarua ambacho ni kigumu hasa kwa vile mara ya mwisho kwa Scotland kufika Fainali za Mashindano makubwa ilikuwa ni Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 1998 zilizochezwa huko France.

KOMBE LA DUNIA-BRAZIL 2014
[MCHUJO KANDA YA ULAYA]
MSIMAMO
KUNDI A
[Kila Timu imecheza Mechi 4]
1 Belgium Pointi 10
2 Croatia 10
3 Serbia 4
4 Macedonia 4
5 Wales 3
6 Scotland 2

Hadi sasa kwenye Kundi lao la Mechi za Mchujo kuwania kwenda Brazil Mwaka 2014 kwenye Fainali za Kombe la Dunia, Scotland imevuna Pointi 2 tu lakini hilo halikumkatisha tamaa Gordon Strachan ambae ametamka: “Kama tukifanya kazi pamoja kwa umoja najua fika tutafanikiwa. Falsafa yangu ni kushinda Gemu za Soka kama Manchester United!”
Mechi ya kwanza ya Strachan kwenye himaya yake kama Meneja wa Scotland ni ile ya Kirafiki dhidi ya Estonia Mwezi ujao Februari 6.

KADI NYEKUNDU ya KOMPANY YAFUTWA NI JINSI GANI MAREFARII BADO HALI TETE HATA ULAYA!!

>>MAN CITY WASHINDA RUFAA!!
JOEY_BARTON_n_KOMPANYNAHODHA wa Mabingwa wa England Manchester City, Vincent Kompany, leo amepona Kifungo cha Mechi 3 baada ya Kadi Nyekundu aliyopewa na Refa Mike Dean juzi Jumapili, Man City walipoichapa Arsenal 2-0 kufutwa na Tume Huru ya FA, Chama cha Soka England, kufuatia Rufaa iliyowasilishwa na Klabu yake.
Kompany alipewa Kadi Nyekundu katika Kipindi cha Pili, Dakika ya 75, alipokuwa akimkabili Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere.
Mara baada ya Mechi hiyo, Meneja wa Man City Roberto Mancini alidai kutolewa kwa Kompany ni kosa kubwa la Refa Mike Dean.
Endapo kama Kadi hiyo ingebaki kama ilivyo, Kompany angezikosa Mechi 3 dhidi ya Fulham na QPR, kwenye Ligi Kuu England, na Mechi ya Raundi ya 4 ya FA CUP dhidi ya Crystal Palace au Stoke City.
Katika Mechi hiyo hiyo ya Arsenal na Man City, Beki wa Arsenal, Laurent Koscielny, alitolewa nje katika Dakika ya 10 tu kwa kumshika Edin Dzeko, kosa ambalo pia lilizaa Penati iliyopigwa na Edin Dzeko lakini Kipa Szczesny aliokoa baada ya mpira kupiga posti.
Arsenal hawakukata Rufaa kupinga adhabu hiyo

TUJIKUMBUSHE KIDOGO MICHUANO YA MATAIFA KATI YA ZAMBIA VS IVORY COAST AMBAPO JUMAPILI KULE SOUTH KWA MADIBA ITAKUWA KINDUMBWENDUMBWE

LEO ROBO FAINALI-COPA del REY: Real v Valencia, COPPA ITALIA: Inter v Bologna

>>COPA del REY: KESHO ni BARCA v MALAGA!
LEO, Mabingwa wa Spain, Real Madrid, ambao Msimu huu matumaini yao makubwa kutwaa Taji huko Spain yamebaki kwenye COPA del REY, watatinga Uwanjani kwao Santiago Bernabeu kucheza na Valencia katika Mechi ya kwanza ya Robo Fainali ya Kombe hilo na huko Italy, pia kutakuwa na Robo Fainali ya COPPA ITALIA kati ya Inter Milan na Bologna.
Real Madrid, baada ya kucheza bila Supastaa wao Cristiano Ronaldo katika Mechi yao ya mwisho ya La Liga hivi juzi na kutoka 0-0  na Timu goigoi Osasuna kwa vile alikuwa Kifungoni kwa Mechi moja, leo Nyota huyo atatinga dimbani.Cristiano Ronaldo
Huko Italy, washiriki wa Nusu Fainali ya kwanza washajulikana wakati Juventus watakapoivaa Lazio hapo Januari 22.
Mshindi kati ya Inter Milan na Bologna na yule wa Mechi kati ya Fiorentina na AS Roma ndio watacheza kwenye Nusu Fainali ya pili.
Huko Spain, Robo Fainali nyingine za Copa del Rey zitakuwa Jumatano Januari 16, Mechi mbili, na Ijumaa Mechi moja.
Mabingwa watetezi wa COPA del Rey, Barcelona, wao watacheza Jumatano na Malaga Uwanjani Nou Camp.

ROBO FAINALI
Jumanne Januari 15
[SAA 5 Usiku]
Real Madrid CF v Valencia
Jumatano Januari 16
[SAA 3 na Nusu Usiku]
Real Zaragoza v Sevilla FC
[SAA 5 na Nusu Usiku]
Barcelona v Malaga
Ijumaa Januari 18
[SAA 6 Usiku]
Atletico Madrid v Real Betis
Jumatano Januari 23
Marudiano
Sevilla FC v Real Zaragoza
Valencia v Real Madrid CF
Malaga v Barcelona
Real Betis v Atletico Madrid
++++++++++++++++++++++
COPPA ITALIA
ROBO FAINALI
RATIBA:
Jumanne Januari 15
[SAA 5 Usiku]
Inter Milan v Bologna
Jumatano Januari 16
[SAA 5 Usiku]
Fiorentina v AS Roma
NUSU FAINALI:
Jumanne Januari 22
SS Lazio v Juventus
Jumanne Januari 29
Juventus v SS Lazio

BAADA YA OKWI KUWACHANGANYA VIONGOZI WA SIMBA HATIMAYE LEO SIMBA YAMUUZA OKWI DOLA 300,000 ETOILE DU SAHEL


Okwi

MSHAMBULIAJI wa Simba SC, Mganda Emmanuel Okwi ameuzwa klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia kwa dola za Kimarekani 300,000.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema  kwamba, Okwi amekamilisha vipimo na kila kitu na tayari amesaini mkataba.
“Tunasubiri kulipwa fedha zetu tu, viongozi watakwenda Tunisia kuchukua fedha za mauzo ya mchezaji huyo,”alisema Poppe.
Okwi amekuwa akipiga chenga kuripoti kambini Simba SC na alikuwa hata hapokei simu za viongozi wa klabu hiyo kila alipopigiwa.
Kufuatia hatua hiyo, uongozi ulimuengua kwenye programu ya safari ya Oman na sasa inabainika ametua Sahel.
Okwi, aliyezaliwa Desemba 25, mwaka 1992 aliisajiliwa Simba akitoea SC Villa ya Uganda mwaka 2010 akiwa kinda wa miaka 17, akisajiliwa kwa dau la dola za Kimarekani 40,000.
Baada ya kumaliza mkataba wake wa awali, Desemba mwaka jana aliongeza mkataba wa miaka miwili na Simba SC ambao kabla hajaanza kuutumikia, anahamia Sahel.

FA CUP: MARUDIANO MECHI 9 LEO KULE ENGLAND

!


FA_CUP-NEW_LOGO>>KESHO, ARSENAL, MAN UNITED DIMBANI NYUMBANI!!
>>PATA RATIBA KAMILI RAUNDI YA 4 FA CUP

MECHI ZA MARUDIANO- FA CUP-Raundi ya 3
Jumanne Januari 15
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Birmingham v Leeds
Bournemouth v Wigan
Brentfaud v Southend
Leyton Auient v Hull
Wimbledon v Sheffield Wed
Stoke v Crystal Palace
Sunderland v Bolton
[SAA 5 Usiku]
Blackpool v Fulham
West Brom v QPR

LEO Usiku zipo Mechi 9 za Marudiano ya Raundi ya 3 ya FA CUP, kukiwa na Mechi 4 za Klabu za Ligi Kuu England zikwania kutotolewa nishai na Klabu za Madaraja ya chini na ipo Mechi moja, WBA v QPR, ya Klabu za Ligi Kuu England pekee, na moja ya Klabu za Championship pekee, ile kati ya Birmigham na Leeds United.
Hii ni Mechi ya 4 kwa WBA na QPR kukutana Msimu huu ambazo ni mbili katika Ligi Kuu ambazo zote WBA walishinda na sare moja ya kwenye FA CUP.
Kesho Jumatano Usiku, zipo Mechi mbili tu za Marudiano ya Raundi ya 3 FA CUP ambapo Arsenal watacheza na Swansea City Uwanjani Emirates kufuatia sare yao ya 2-2 katika Mechi ya kwanza na huko Old Trafford, Manchester United wataivaa tena West Ham baada ya kutoka 2-2 huko Upton Park.

MECHI ZA MARUDIANO- FA CUP-Raundi ya 3
Jumatano Januari 16
[SAA 4 Dak 30 Usiku]
Arsenal v Swansea City
[SAA 5 Usiku]
Man Utd v West Ham

RAUNDI YA 4
Ijumaa Januari 25
[SAA 4 Dak 30 Usiku]
Millwall v Aston Villa
Jumamosi Januari 26
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Crystal Palace au Stoke City v Manchester City
[SAA 12 Jioni]
Norwich City v Luton Town
Macclesfield Town v Wigan Athletic au Bournemouth
Derby County v Blackburn Rovers
Hull City au Leyton Auient v Barnsley
Middlesbrough v Aldershot Town
Brighton & Hove Albion v Swansea City au Arsenal
Reading v Sheffield United
Huddersfield Town v Leicester
QPR au West Brom v Sheffield Wednesday au MK Dons
Bolton au Sunderland v Everton
[SAA 2 na Nusu Usiku]
West Ham United au Manchester United v Fulham au Blackpool
Jumapili Januari 27
[SAA 9 Mchana]
Southend United au Brentford v Chelsea
[SAA 11 Jioni]
Leeds United au Birmingham City v Tottenham Hotspur
[SAA 1 Usiku]
Oldham Athletic v Liverpool

WAKATI AKINA KITUMBO KINA SHAFFIH WAKIJITOSA KATIKA UJUMBE WAMBURA AJITOSA TFF UMAKAMU WA RAIS, BALHABOU NAYE NDANI


Michael Wambura

IDADI ya wadau waliojitokeza kuchukua fomu za kuwania uongozi katika Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeongezeka ambapo wengine saba wamechukua leo (Januari 15 mwaka huu) na kufanya idadi yao kufikia 26.
Hata hivyo, idadi hiyo ni kwa wale wanaochukua fomu hizo katika ofisi za TFF, kwani vilevile zinapatikana kupitia tovuti ya TFF ya www.tff.or.tz ambapo mwisho wa kuchukua na kurejesha ni saa 10 kamili alasiri Januari 18 mwaka huu.
Waliochukua leo ni Michael Wambura anayewania umakamu wa rais wakati kwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji ni Mbasha Matutu, Muhsin Balhabou, Salum Chama, Titus Osoro na Zafarani Damoder.
Idadi kamili ya waliochukua ni Michael Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace Karia (Makamu wa Rais). Kwa upande wa wajumbe na kanda zao kwenye mabano ni Salum Chama (Kagera na Geita), Mugisha Galibona, Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano (Mara na Mwanza).
Epaphra Swai na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo, Elly Mbise na Twahili Njoki (Arusha na Manyara), Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi na Rukwa) na James Mhagama (Njombe na Ruvuma).
Athuman Kambi (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na Singida), Farid Nahdi (Morogoro na Pwani), Khalid Mohamed (Kilimanjaro na Tanga) na Muhsin Balhabou, Shaffih Dauda na Zafarani Damoder (Dar es Salaam).
Naye Said Mohamed amechukua fomu ya kuwania umakamu mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board).
Wakati huo huo: Uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Makocha wa Soka Tanzania (TAFCA) utafanyika Jumamosi (Januari 19 mwaka huu) kwenye ukumbi wa mikutano wa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa TAFCA, Eugene Mwasamaki, mikoa ambayo tayari imefanya uchaguzi wa viongozi inatakiwa kuwasilisha muhtasari wa mkutano uliowaingiza madarakani. Muhtasari huo uwasilishwe TAFCA kabla ya keshokutwa (Januari 17 mwaka huu).
Mkoa utakaoshindwa kutuma muhtasari ndani ya muda uliotolewa utakosa haki ya kushiriki katika uchaguzi huo uliovutia wagombea watano. Wagombea hao ni Oscar Korosso (Mwenyekiti), Lister Manyara (Makamu Mwenyekiti), Michael Bundala (Katibu Mkuu) na Magoma Rugora na Wilfred Kidao wanaowania ujumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF

WAKATI SIMBA IMEENDA KWA MAFUNGU NCHINI OMAN KESHO INATARAJIA KUCHEZA NA TIMU YA TAIFA YA OMAN >>>JE UMESHAWAHI ONA WAPI KLABU NA TIMU YA TAIFA KUNA SOKA KWELI HUKO???????


Simba SC

MABINGWA wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba Sc, kesho watashuka katika uwanja wa Qaboos Sports Complex nchini Oman kukwaana na timu ya Taifa ya huko iliyoshiriki michuano ya Olimpiki, imefahamika.
 Simba ipo nchini Oman kwa kambi maalum ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu soka Tanzania Bara  na michuano ya kimataifa.
 Katibu Mkuu wa Simba Evodius Mtawala ameiambia Sports Lady leo kwamba mchezo huo utakuwa ni muhimu kwa timu hiyo kwani kocha atautumia katika harakati zake za kukisuka ipasavyo kikosi chake. 
“Kama mnavyojua tangu tumpate kocha mpya (Patrick Liewing) kikosi hajipata kukaa pamoja hivyo huo ndio mwanzo wa kocha kuanza kukiweka sawa kikosi chake,”alisema 
Mtawala aliongeza kuwa, kocha Liewing amefurahishwa na wachezaji wote kuwa pamoja kwa sasa ambapo anaamini kambi hiyo itakuwa na mafanikio zaidi. 
Mbali na mchezo huo, Simba inatarajiwa kucheza mechi nyingine za kirafiki na timu kama Fanja Fc na timu ya jeshi la huko kabla ya kurejea nchini Januari 23.


DIDAS KUNDE AJITAPA KUWAKANDAMIZA RHINO RANGERS HII LEO KATIKA DIMBA LA ALLY HASSAN MWINYI


 
Kocha msaidizi wa timu ya kombaini wilaya ya Tabora mjini bw.Didas Kunde amesema leo piga uwa garagaza muhimu awafunge wapiga kwata wanajeshi wa hapa mkoani tabora na ambao wapo ligi daraja la kwanaza RHINO RANGERS katika mchezo wa kirafiki utakaocheza katika dimba la ALLY HASSAN MWINYI.
M,chezo huo utakuwa wa marudiano kutokana na mchezo wa awali juzi timu ya RHINO RANGERS iliweza kuibuka na ushindi wa bao 2-0 mabao yaliyofungwa na shija sanju na maghembe kipindi cha kwanza kutokana na uzembe wa mabeki wa timu ya kombaini wilaya.

Kwa upande wa timu ya RHINO RANGERS BW.Shija amesema leo wanatarajia kupanga kikosi cha cha kwanza ambacho kitakuw akipimo kizuri kw atimu ya Kagera Sugar ambayo inatarajia kuja kesho au kesho kutwa kuja kucheza na maafande hawa wa tabora kuelekea katika mzunguko wa pili wa ligi daraja la kwanza FDL.

Kikosi cha kombaini wilaya kinaundwa na Mrisho Khalfan,Jackson Sebene,John Zacharia,Josephat  Miggi,Godfrey Magaso,Nassoro Mfoi,Khamis Bingwa,Binamungu Shabaan,Maiko Maningu,Zamoyoni Maiko na Abdalah Juma.

Wengine ni Kilanga Faraji,Mwinyira Stanley,Rashid Kopa,mMsafiri Peter,Herison Moses na Songoro Kasongo wakati makocha ni ANDREW ZOMA Kocha mkuu akisaidiwa na DIDAS KUNDE Kocha msaidizi.
 WAKATI HUO HUO Kuelekea mzunguko wa pili wa ligi daraja la kwanza rhino rangers imeendelea kuimarisha kikosi chake kwa kusajili wachezaji watano ili kuongeza nguvu katika kikosi,wachezaji iliowasajili ni ayoub iddy ,na josephy mapunda nafasi ya beki,doi mobby,mganda mchembe washambuliaji,na emanuely noely nafasi ya kiungo.

wachezaji wa zamani ni abdukarim mtumwa,iddy kihulya,charles mpinuki,james mwambembe,julius masunga,abass mohamedy,stanslaus mwakitosi,steven madhanda,shija sanju,shija mongo,salum mamro,salum majid,usi makame,na frank koe. 

wengine ni josephy salaganda,victor hangaya,bakary mahadhi,said kipanga,issa mohamedy,stanley mlai,samwely mwamasangula,omary magesa,msafiri maiko,ramadhani shabyeji na ally rumba na kuhitimisha idadi ya wachezaji 30 katika klabu hiyo inayonolewa na kocha wa zaman wa mafunzo ya zanzibar akisaidiwa na kocha mongo.

ENGLAND: MECHI ZA KATI YA WIKI, MARUDIANO FA CUP, PIA MECHI YA KIPORO YA CHELSEA SOUTHAMPTON NI KESHO !


BPL_LOGO>>FA CUP: JUMATANO- Man Utd v West Ham, Arsenal v Swansea City
>>BPL: JUMATANO- Chelsea v Southampton
Katikati ya Wiki hii, zipo Mechi za marudiano za Raundi ya 3 ya FA CUP kwa Timu ambazo zilitoka sare Mechi zao za kwanza na pia ipo Mechi moja ya kiporo ya BPL, Barclays Premier League, kati ya Chelsea na Southampton.
ZIFUATAZO NI RATIBA YA MECHI HIZO:
++++++++++++++++++++++
MECHI ZA MARUDIANO- FA CUP-Raundi ya 3
Jumanne Januari 15
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Birmingham v Leeds
Bournemouth v Wigan
Brentfaud v Southend
Leyton Auient v Hull
Wimbledon v Sheffield Wed
Stoke v Crystal Palace
Sunderland v Bolton
[SAA 5 Usiku]
Blackpool v Fulham
West Brom v QPR
Jumatano Januari 16
[SAA 4 Dak 30 Usiku]
Arsenal v Swansea City
[SAA 5 Usiku]
Man Utd v West Ham
**FAHAMU: Mechi za Raundi ya 4 ya FA CUP zitachezwa Wikiendi ya Januari 26.
BPL, BARCLAYS PREMIER LEAGUE
Jumatano Januari 16
[SAA 4 DAK 45 Usiku]
Chelsea v Southampton


FA CUP-RAUNDI YA 4
RATIBA
[KUCHEZWA WIKIENDI YA JANUARI 26]
Nauwich City v Luton Town
Oldham Athletic v Liverpool
Macclesfield Town v Wigan Athletic au Bournemouth
Derby County v Blackburn Rovers
Hull City au Leyton Auient v Barnsley
Middlesbrough v Aldershot Town
Millwall v Aston Villa
Leeds United au Birmingham City v Tottenham Hotspur
Brighton & Hove Albion v Swansea City au Arsenal
Crystal Palace au Stoke City v Manchester City
West Ham United au Manchester United v Fulham au Blackpool
Southend United au Brentfaud v Chelsea
Reading v Sheffield United
Huddersfield Town v Leicester
QPR au West Brom v Sheffield Wednesday au MK Dons
Bolton au Sunderland v Everton

BRANDTS KUMBE ANAIPENDA SIMBA MAFUNZO YA YANGA UTURUKI KUONYESHWA JUMAMOSI TAIFA KWA BLACK LEOPARD YA AFRIKA KUSINI. ERNEST BRANDTS ANASEMA LICHA YA KUTOKUSHINDA UTURUKI LAKINI TIMU IMEKWIVA



Kocha wa Ernest Brandts amesema licha ya kwamba timu yake ilishindwa kupata ushindi katika ziara yake ya mafunzo ya wiki mbili nchini Uturuki lakini ameridhika na namna vijana wake walivyoyapokea mafundisho yake na sasa vijana hao wamekwiva kwa changamoto ya ligi kuu ya soka Tanzania bara duru la lipi.
Brandts ameshukuru uongozi kwa kuweza kuwapa nafasi ya kufanya kambi ya maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya soka Taznania bara kwani uwepo wao Uturuki kwa pamoja wamepata nafasi ya kuiunganisha timu kwa pamoja.
Amesema katika michezo miwili ya mwisho vijana wake walionyesha kuiva vizuri na kwamba amepata muda mzuri wa kukaa na vijana wake na wote wameonyesha kuiva kimazoezi.
Amesema mazingira ya kambi yalikuwa mazuri na huduma nyingine pia zilikuwa nzuri na kwamba malengo yake yametimia.
Amerejea kauli yake aliyotoa kabla ya kuondoka Antalya juu  ya michezo mitatu ya kirafiki aliyopata dhidi ya Armini Bielefeld, Deinizlispor na Emmen FC kwa kusema michezo ilikuwa ni mizuri na wamepata nafasi ya kuona mapungufu machache yaliyojitokeza na anaamini watayafanyia kazi na kuendelea kufanya vizuri.
 Tumecheza michezo mitatu, wa kwanza tulitoka sare na Amrinia Bielefeleld, mchezo ulikua mzuri na timu yangu ilicheza vizuri kwa dakika 90 zote za  mchezo licha ya Arminia kusawazisha bao dakika za lala salama.
 Mchezo wa pili dhidi ya Denizlispor nao pia timu ilicheza vizuri na kuweza kutengeneza nafasi nyingi za kufunga licha ya kwamba walipoteza mchezo huo.
kuhusu mchezo wa mwisho Brandts amesifu zaidi kuwa kikosi kilionyesha kandanda la hali ya juu dhidi ya Emmen FC ulikuwa mzuri pia na kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza kwamba walitawala mchezo na kupata kupata nafasi kadhaa za kufunga mabao lakini kutokua makini kwa washambuliaji wake pia kulichangia kukosa ushindi.
 Mara baada ya kurejea kutoka Antalya Yanga inajipanga kwa mchezo wa kirafiki utakao fanyika jumamosi katika uwanja wa taifa dhidi ya timu ya 
 Black Leopard ya Afrika Kusini ambayo inashiriki ligi kuu ya soka nchini Afrika Kusini.

MPIRA SI UCHAWI NI KUJITUMA BAADA YA KUIWEZESHA TP MAZEMBE NA ZAMBIA SUNZU AENDA KUFANYIWA VIPIMO READING



Football | Barclays Premier League

Sunzu skips training for Reading medical


Zambia centre-back Stopilla Sunzu has taken a temporary break from training for the 2013 Africa Cup of Nations to undergo a pre-transfer medical at English Premier League club Reading.
Sunzu plays for TP Mazembe in the Democratic Republic of Congo and the club said on its website that a three-million-pound (3.6 million euros/$4.8 million) deal had been agreed pending the successful completion of formalities.
Scorer of the winning penalty when Zambia shocked Ivory Coast 8-7 in a shootout to win the 2012 Africa Cup, Sunzu is due in South Africa on January 19, two days before the defending champions face Ethiopia in the opening round.
He was outstanding when the Chipolopolo (Copper Bullets) were held 0-0 at home by Norway last Saturday to complete a winless five-match build-up to the Cup of Nations.

BAADA YA KOMPANY KUTOLEWA KWA KADI NYEKUNDU KWA TACKLING MBAYA KWA WILSHEREMARTIN KEOWN ASEMA TACKLING ZA KOMPANY NI HATARI SANA



I am a huge fan of Vincent Kompany - he is one of the best defenders in the Premier League - but his tackling technique is leaving him wide open to trouble. 
A few times now we have seen the Manchester City captain booked or sent off for launching himself forward with both feet. 
He propels himself at speed and he is a big man so it is quite a force coming at the opposition player, in Sunday's case Arsenal's Jack Wilshere. 
Gutted: Vincent Kompany was dismissed by Mike Dean (right) after a challenge on Arsenal's Jack Wilshere
Gutted: Vincent Kompany was dismissed by Mike Dean (right) after a challenge on Arsenal's Jack Wilshere
Kompany didn't injure Wilshere but there was a degree of luck in that as the England man was running into six studs. When you go in on your backside as Kompany likes to, your feet have to come off the ground. 
Most defenders try to go in with one foot or the other but he goes in with both, giving himself the option of using the left or the right, depending on which way the opponent moves. 
He then tries to retract the foot he is not going to use but it's not always that easy. He doesn't realise how powerful he is - there's such a velocity when he comes in with two feet like that. It is dangerous and Kompany needs to adjust the way he tackles or it will be more red cards.
I sympathise because Kompany is trying to take the ball with the minimum amount of force, but he would be better off waiting a bit longer before making the tackle.
Off you go: Kompany slid in on his backside, a technique which forces him to lift his feet off the ground
Off you go: Kompany slid in on his backside, a technique which forces him to lift his feet off the ground
No way: City manager Roberto Mancini believes Dean got the decision to send his captain off wrong
No way: City manager Roberto Mancini believes Dean got the decision to send his captain off wrong
If he did, then he could see which foot he needed and be able to pinch the ball without risking injuring an opponent. 
Against Arsenal, Wilshere was running into a cul-de-sac, so to lunge in was unnecessary. If he had stayed standing up, Wilshere would have probably run into him. 
I admire that Kompany wants to make tackles and no-one wants to stop him making more, but he just needs to adjust his technique slightly. 
No-one in the Premier League is better at recognising an attacking danger and taking responsibility for his team. Now he just needs to take responsibility for his tackling. 
 
When Vincent goes steaming in...
Vincent Kompany's tackle which earned him a red card on Sunday wasn't the first time the Belgian has thrown himself into a challenge. 
Below, Sportsmail looks back at some other occasions when Manchester City's captain might have seen red.
1. Jack Wilshere (Arsenal), January 2013 - RED CARD
Referee Mike Dean showed Kompany a red card for this challenge on Sunday. Wilshere was bearing down on the Belgian before overrunning the ball and colliding with Kompany.
Ball winner: Kompany (right) won the ball against Wilshere, but was sent off by referee Mike Dean
Ball winner: Kompany (right) won the ball against Wilshere, but was sent off by referee Mike Dean
 
2. Fernando Torres (Chelsea), August 2012 - NO CARD
Kompany escaped punishment for this tackle but was booked for shoulder charging Torres in the Community Shield meet at the beginning of the season. City went on to win the game 3-2.
Crunched: Fernando Torres skips out of the way as Kompany slides in during the Community Shield at Wembley
Crunched: Fernando Torres skips out of the way as Kompany slides in during the Community Shield at Wembley
 
3. Bradley Johnson (Norwich), December 2012 - NO CARD
The Belgian was not penalised for this tackle on Norwich midfielder Johnson. The resultant City breakaway led to an Edin Dzeko goal.
Breakaway: Bradley Johnson was on the receiving end as Kompany won the ball which led to a City goal
Breakaway: Bradley Johnson was on the receiving end as Kompany won the ball which led to a City goal
 
4. Nani (Manchester United), January 2012 - RED CARD
Chris Foy sent Kompany off for this challenge as City lost 3-2 to bitter rivals Manchester United in the FA Cup last season. The 10-man hosts had gone in at half-time 3-0 down.
Dismissed: City fans were up in arms after their captain was red-carded for this tackle
Dismissed: City fans were up in arms after their captain was red-carded for this tackle
 
5. Fernando Forestieri (Watford), January 2013 - NO CARD
City cruised to a 3-0 FA Cup third-round victory after Kompany escaped punishment for this tackle.
Forceful: Kompany might have been cautioned for this lunge during an FA Cup tie
Forceful: Kompany might have been cautioned for this lunge during an FA Cup tie

BAADA YA REFA MIKE DEAN KUMPA KADI NYEKUNDU BEKI WA ARSENAL JUZI YAGUNDULIKA KUWA NI ADUI MKUBWA WA ARSENAL, AKICHEZESHA MECHI ZAO NI MATESO KWAO



Arsenal’s clash with Manchester City at the Emirates Stadium on Sunday may have been as good as over when the hosts, already down to 10 men, went 2-0 behind after 32 minutes.
But the Gunners only needed to check the referee before the game to know luck wasn’t likely to be on their side.
Mike Dean made a controversial, but correct, call to send off Arsenal defender Laurent Koscielny after nine minutes, but the north London side’s record under the match official is be woeful since 2009-10, compared with their rivals.
Marching orders: Mike Dean sends off Arsenal's Laurent Koscielny (left)
Marching orders: Mike Dean sends off Arsenal's Laurent Koscielny (left)
Stats from Opta show that in the 15 Premier League games Arsenal have played when Dean is officiating, they have triumphed just once, making it a winning average of just seven per cent.
It represents a massive contrast with the Premier League’s current top four. Both Manchester clubs, Chelsea and Tottenham have recorded significantly better results under Dean’s watch.
The title winners from the past three years recorded winning averages between 63 and 67 per cent, while even Spurs can claim a 50 per cent success record when the Wirral-born referee has been in charge across a similar amount of games.
Arsenal’s only victory under Dean’s officiating in the last four seasons came earlier last year, a 5-2 win over Tottenham at the Emirates.
But he has been present for some of Arsenal’s most painful recent defeats too including the 2-1 loss at White Hart Lane in the reverse fixture.
Rare result: Arsenal's only victory in a game under Dean's stewardship was the 5-2 win over Spurs
Rare result: Arsenal's only victory in a game under Dean's stewardship was the 5-2 win over Spurs
More recently he oversaw Arsenal’s League Cup exit at Bradford and was also in charge of the competition’s final in 2011 when Birmingham caused an upset to defeat the Gunners at Wembley.
Dean’s decision to send off Koscielny yesterday comes just over a year after a similar incident in a Premier League match between Chelsea and Newcastle.
The December 2011 clash between the two at St James’ Park came to life in the fourth minute when David Luiz denied Demba Ba a clear goal scoring opportunity but was punished with only a yellow card.
Woeful return: The Gunners have struggled for results with Dean in charge
Woeful return: The Gunners have struggled for results with Dean in charge
Chelsea went on to win 3-0 in a result that left Newcastle boss Alan Pardew fuming after the game when he claimed Dean had told him Ba did not have 'control of the ball' so it was not a red-card offence.
Pardew revealed later on Sky Sports' Goals on Sunday that Dean had initially stood by his decision but changed his opinion after reviewing the incident.
‘He said, 'I made a mistake, he should have been sent off',’ said Pardew.
We've been here before: Mike Dean only cautioned David Luiz (blue top nearest penalty area) for denying Demba Ba a goal scoring chance last season
We've been here before: Mike Dean only cautioned David Luiz (blue top nearest penalty area) for denying Demba Ba a goal scoring chance last season

SIMBA SC BALAA OMAN WAPIKA MFUMO HATARI OMAN, MAFTAH AKALIA KUTI KAVU MSIMBAZI




SIMBA sasa wapo kamili. Baada ya kutua kwa nyota wake waliokuwa Taifa Stars na Kombe la Mapinduzi Zanzibar kumekamilisha kikosi chake kilichopiga kambi hapa Muscat, Oman. 
Wachezaji watatu Amir Maftah, Edward Christopher na Mussa Mudde ndio wachezaji ambao hawajajiunga na kambi ya Simba hapa Oman kutokana na sababu mbalimbali. 
Meneja wa timu hiyo, Jamhuri Kihwelo alisema kila mmoja amebaki kutokana na sababu zake. 
"Maftah amebaki kwa tatizo la nidhamu, Mudde amepata matatizo ya kifamilia yuko kwao Uganda." 
Christopher, hata hivyo, amebakizwa baada ya kuumia kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi. 
Maftah alitakiwa kutua jana Jumatatu na wenzake waliokuwa Taifa Stars lakini alizuiwa kuondoka kutokana na utovu wa nidhamu, ambao haukuwekwa wazi na Julio. 
Simba inajifua vilivyo tangu walipofika Januari 9, ingawa walifika kwa mafungu tofauti. 
Walianza wakiwa na wachezaji nane, wakaongezeka kufikia 13 na sasa wametimia 24. 
Nyota walioko Oman ni pamoja na Juma Kaseja, Ramadhani Chombo 'Redondo', Haruna Moshi, Boban', Mzambia Felix Sunzu, Said Nassor 'Cholo', Haruna Shamte, Haruna Chanongo, Kigi Makassy, Abdallah Seseme, Ramadhan Singano, Mrisho Ngassa na Mwinyi Kazimoto. 
Wengine ni Abdallah Juma, Paul Ngalema, Amri Kiemba, Shomari Kapombe, Abel Dhaira na baadhi kutoka timu ya yosso ya Simba. 
Kocha mkuu wa kikosi hicho, Mfaransa Patrick Liewig amesema lengo lake na tabia yake kama dereva ni kuhakikisha Simba inakuwa timu nzuri. 
"Tunatakiwa kufanya kazi ili tufanikiwe ambapo sasa natengeneza timu ya ushindi tu". 

VIWAMJA TOFAUTI
Simba inafanya mazoezi katika viwanja vitatu. Kuna siku inafanya kwenye uwanja wa klabu ya Fanja. 
Mara nyingine wanajifua katika Uwanja wa Klabu ya Michezo inayoitwa Oman. 
Simba pia imefanya mazoezi katika Uwanja wa Michezo wa Sultan Qaboos, ambao unamilikiwa na serikali ya hapa. 

TOTAL FOOTBALL
 

Kocha Liewig amesisitiza kitu anachokifanya sasa ni kutengeneza timu yenye kushirikiana ambayo itashambulia pamoja na kuzuia pamoja lakini pia iwe inafunga mabao. Staili hiyo kwa jina la kimombo huitwa "Total Football", ambayo ilikuwa inachezwa zaidi na timu za Uholanzi kwenye miaka ya 1970. 
Pengine hiyo ni janja ya Liewig kuanza kusuka mbinu za kuidhibiti Yanga, ambayo inanolewa na Mholanzi Ernest Brandt. 
Kumbuka Brandt alikuwemo katika kikosi cha timu ya taifa Uholanzi kilichotikisa na staili hiyo chini ya kocha Rinus Michel. 
"Muhimu ninachokifanya ni kutengeneza kombinesheni ya timu. Nilikuwa Zanzibar na nimeiona timu ikicheza nimegundua upungufu hasa katika ushambuliaji na kujihami".Nataka mambo yafanywe na timu kwa pamoja kwani yatasaidia kuongeza ushirikiano wa wachezaji na timu kuwa ngumu kufungika.

SUNZU,KAZIMOTTO WAUGUA
 

Sunzu alikatiza mazoezi ya jana Ijumaa jioni baada ya kufanya kwa nusu saa. Alikimbizwa hospitali na aligundulika alikuwa na tatizo la kifua. Hata hivyo, kitendo hicho cha kukatiza mazoezi na kulalamika kujisikia vibaya kuliwatia hofu watu pengine tatizo lake la moyo lilikuwa limerudi. 
Sunzu alitaka kukatiza mkataba na Simba kwenye Dirisha Dogo la usajili kwa madai alikuwa ana tatizo la moyo. 
Ingawa baada ya muda alibadili mawazo na kurudi nchini na kujiunga na Simba tena. 
Kipa Dhaira naye alipelekwa hospitali baada ya kufanya mazoezi ya asubuhi. Pia naye alikuwa na tatizo la kifua na alipewa dawa. 
Kazimoto hakufanya kabisa mazoezi na aligundulika alikuwa na malaria. 

SUNZU NA BOBAN
 

Liewig anaeleza kuwa anataka Sunzu na Boban ndio waongoze safu ya ushambuliaji. "Nimeanza na hawa kwa kuwa ndio nilikuwa nao kwa kipindi chote kwa sasa wamekuja hawa wengine mambo yatakuwa mazuri zaidi naweza kuamua namna gani nitakavyowachezesha,"alieleza Liewig. 
Mfaransa huyo anaona nyota hao wawili wanaweza kutengeneza safu kali ya ushambuliaji. 
Kocha huyo amefurahia ujio wa wachezaji wote lakini amesisitiza muda wa siku 10 uliobaki ni mfupi kwa maandalizi yake. 
Simba walikiwa na idadi kubwa ya wachezaji walifanya mazoezi jana Jumatatu katika Uwanja wa Oman na walianza kwa mazoezi ya kukimbia chini ya Julio. 
Katika mazoezi hayo walifanya ya ufundi kwa kucheza pasi ndefu na fupi ambapo kocha amesisitiza lengo ni umakini kwa mchezaji anapokuwa na mpira kwa kutoa pasi na kupokea.