Monday, January 14, 2013

YANGA KUONJESHA LADHA ZA UTURUKI JUMAPILI DHIDI YA TIMU LA BONDENI


Kikosi cha Yanga SC
MABINGWA wa soka Afrika Mashariki na Kati, Yanga SC ya Dar es Salaam Jumapili hii watashuka kwenye Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam kumenyana na Black Leopard ya Polokwane, Limpopo nchini Afrika Kusini.
Katibu wa Yanga, Lawrence Mwalusako amesema leo kwamba kikosi cha Yanga kilichokuwa Uturuki baada ya kurejea leo Alfajiri wachezaji watapumzika kwa siku mbili kabla ya Jumatano kuanza mazoezi.
Mwalusako alisema kuhusu lini timu hiyo itawasili, bado hawajajulishwa na Waratibu wa mechi hiyo, kampuni ya Prime Time Promotions.
Yanga ilikuwa Uturuki kwa wiki mbili kwa kambi ya mazoezi na imerejea leo Alfajiri nchini. Katika ziara yake hiyo, ilicheza mechi tatu za kujipima nguvu na kufungwa mbili na kutoka sare moja.
Katika mchezo wake wa kwanza, ilitoka sare ya 1-1 Ariminia Bielefeld ya Daraja la Tatu (sawa na la nne) Ujerumani kabla ya kufungwa 2-1 na Denizlispor FC ya Daraja la Kwanza Uturuki na baadaye 2-0 na Emmen FC ya Ligi Daraja la Kwanza Uholanzi.
Yanga iliweka kambi katika hoteli ya Fame Residence Lara & Spa kilomita chahce kutoka katika Uwanja wa Ndege wa Jiji la Antalya, iliyopo ufukweni mwa bahari ya Mediteranian.
Kikosi cha wachezaji 27 kilikuwa kambini nchini Uturuki, ambacho ni makipa; Ally Mustafa 'Barthez', Said Mohamed na Yussuf Abdul, mabeki Juma Abdul, Shadrack Nsajigwa, Godfrey Taita, Stefano Mwasyika, Oscar Joshua, Mbuyu Twite, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Ladisalus Mbogo na Kelvin Yondani.
Viungo ni Athumani Iddi ‘Chuji’, Frank Domayo, Haruna Niyonzima, Kabange Twite, Nurdin Bakari, Omega Seme, Simon Msuva, Rehani Kibingu, Nizar Khalfani na David Luhende wakati washambuliaji ni Didier Kavumbagu, Said Bahanunzi, Jerry Tegete, George Banda na Hamisi Kiiza na Kocha Mkuu Mholanzi, Ernie Brandts, Kocha Msaidizi, Freddy Felix Minziro na Kocha wa makipa na Razak Ssiwa.
Hiyo inakuwa mara ya tatu kihistoria Yanga kufanya ziara nje ya Afrika baada ya Brazil mwaka 1975 na Romania mwaka 1978. Yanga pia imewahi kuweka kambi Afrika Kusini mwaka 2008.
Leopards ilirejea Ligi Kuu ya Afrika Kusini mwaka juzi tangu ishuke 2008 na msimu uliopita iliponea chupuchupu kushuka tena, baada ya kushika nafasi ya 14 katika Ligi ya timu 16, na kwa msimu huu hadi sasa ipo nafasi ya 12.

MSIMAMO WA LIGI KUU AFRIKA KUSINI:

PosTeamPWDLGFGAGDPts
1Kaizer Chiefs16105131112035
2Orlando Pirates1610422391434
3Platinum Stars1610152618831
4Free State Stars166731413125
5Maritzburg Utd166641814424
6University of Pretoria165831814423
7Bloem Celtic166371618-221
8SuperSport United1631121915420
9Bidvest Wits164751417-319
10Mamelodi Sundowns164661215-318
11Moroka Swallows165292327-417
12Black Leopards163851924-517
13Golden Arrows164481520-516
14Ajax Cape Town164391526-1115
15Chippa United162771320-713
16AmaZulu16268823-1512
Print

No comments:

Post a Comment