Friday, October 26, 2012

SIMBA SC YAMUWEKEA NYOSSO MTEGO WA MWANA UKOME

Juma Nyosso
SIMBA SC inamsubiri kwa hamu beki wake Juma Said Nyosso na pendekezo lake la kuvunja mkataba na klabu hiyo, lakini itamkata maini na jibu moja tu.
Jibu gani hilo? Atatakiwa kuilipa klabu hiyo fedha za kuvunja mkataba.
“Sheria ziko wazi na mkataba wake uko wazi, kabla ya kuusaini aliusoma vizuri, akauelewa akasaini, kwa kuwa yeye ameamua kuvunja mkataba, basi atatakiwa kutulipa fedha za kuvunja mkataba,”alisema kiongozi mmoja wa Simba ambaye hakutaka kutajwa jina gazetini.
Kimsingi Simba imekubali kuvunja mkataba na beki wake huyo iliyedumu naye tangu mwaka 2007, kulingana na maombi yake, na imemtaka afike kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Poppe kujadili suala hilo.
Habari za ndani kutoka Simba SC, zimesema kwamba Nyosso amewasilisha maombi ya kuvunja mkataba na klabu hiyo, baada ya kushushwa kikosi cha pili, akidaiwa kiwango chake kimeshuka hivyo amepewa fursa ya kwenda kukiboresha.
Lakini Nyosso mwenyewe ameona kama hastahili kushushwa timu ya pili na ameomba asitishiwe mkataba wake aondoke, jambo ambalo uongozi wa klabu umelikubali.
Nyosso si kama anatuhumiwa kuhujumu timu, bali anaambiwa uwezo wake umeshuka mno na kwamba amekuwa akiigharimu timu katika siku za karibuni, hivyo amepewa fursa ya kwenda kupandisha kiwango chake.
Adhabu kama hii amewahi kupewa mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina, Carlos Tevez katika klabu ya Manchester City ya England msimu uliopita na aliitumikia vizuri hadi aliporejeshwa tena kikosi cha kwanza, ambako aliisaidia timu kumalizia msimu vizuri kwa kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu.  
Mbali na Nyosso, kiungo Haruna Moshi Shaaban amesimamishwa kwa wiki tatu kwa tuhuma za utovu wa nidhamu na katika kipindi hicho atakuwa akipokea nusu mshahara.
Boban ameamua kurudi nyumbani kwake kupumzika na mkewe hadi adhabu hiyo iishe ajue mustakabali wake, ila amesema anaonewa kwa sababu hakupewa nafasi ya kujibu tuhuma zake kabla ya hatua kuchukuliwa, ingawa amechukulia poa tu.
Wakati huo huo, habari zaidi kutoka ndani ya Simba, zimesema kwamba Mwinyi Kazimoto Mwitula, Ramadhan Suleiman Chombo na Mrisho Khalfan Ngassa nao wanaangaliwa kwa ‘jicho la tatu’ juu ya mwenendo wao kwenye timu hiyo na kwa nyakati tofauti wote wamekwishaitwa kuhojiwa masuala mbalimbali.   

WACHEZAJI WAVIVU YANGA WAWEKEWA MTEGO WA KUTEMWA, TIMU IKO SAWA KWA GWARIDE LA OLJORO KESHO

Brandts akiwaongoza vijana wake mazoezini
UONGOZI wa Yanga umemshauri kocha Ernie Brandts kutumia wachezaji wote badala ya kuwasahau kabisa wengine benchi, ili uweze kubaini wachezaji ambao hawana msaada katika timu na kuweza kuwatema katika dirisha dogo Januari, mwakani.
Katika mechi za karibuni, Yanga ikiwatumia wachezaji tofauti wakiwemo wale ambao wamekuwa benchi kwa muda mrefu kama Nahodha Nsajigwa Shadrack, Nurdin Bakari na Rashid Gumbo.
Yanga imeweka mtego kwa wachezaji ambao wanaridhika kupewa mishahara bure bila kufanya kazi na Januari watatupiwa virago.
Chanzo cha habari kutoka Yanga kimesema kwamba, klabu inataka wachezaji washindani wa namba, ili kuongeza hamasa katika timu, badala ya kuwa na wachezaji wengi wa mazoezi tu.
Yanga wanaonekana kucharuka sasa dhidi ya wachezaji wao kwa ujumla, kuanzia suala la nidhamu na uwajibikaji pia, baada ya kuona wanawekeza fedha nyingi katika usajili, lakini bado timu haichezi soka ya kuvutia, jambo ambalo wanaona linatokana na wahezaji kubweteka.
Juzi Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Abdallah Ahmed Bin Kleb ‘aliwawakia’ wachezaji wa mbele wa timu hiyo kwa uchoyo wa pasi na kukemea tabia inayoonekana kuanza kujitokeza, wachezaji wa timu hiyo kutopendana.
Bin Kleb aliingia ‘kwa hasira’ chumba cha kubadilishia nguo cha Yanga na kuanza kufoka juu ya tabia hiyo, akisema timu inatengeneza nafasi nyingi, lakini kwa uchoyo wa baadhi ya wachezaji kutoa pasi kwa wenzao walio kwenye nafasi nzuri zaidi, inaambulia mabao machache.
Bosi huyo alifanya hivyo baada ya mechi dhidi ya Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ambayo Yanga ilishinda 3-0.
Lakini pia Bin Kleb alimuuliza kocha Mkuu, Mholanzi Ernie Brandts kwa nini timu haichezi vizuri pamoja na kushinda. Brandts alitumia hekima kukwepa kujibu swali mbele ya wachezaji, lakini baadaye alimvuta pembeni Bin Kleb wakazungumza.
Tayari kuna dalili za mgawanyiko ndani ya Yanga baina ya wachezaji na hilo lilijidhihirisha wakati Hamisi Kiiza alipofunga bao lake lililokuwa la tatu katika ushindi wa 3-0, hakwenda kushangilia na wachezaji wenzake, bali alimkimbilia kipa wa akiba, Mghana Yawe Berko kushangilia naye juzi.
Ingawa hajawahi kulalamika, lakini ukiifuatailia Yanga tangu baada ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, Kiiza ndiye ambaye mara nyingi amekuwa hapewi pasi na wenzake anapokuwa kwenye nafasi nzuri, ingawa yeye amekuwa anawapa tu wenzake pasi za mabao.
Pamoja na hayo, hali hiyo inaonekana kidogo kuathiri uchezaji wa Kiiza, anayeonekana kuwa mnyonge na asiye na raha uwanjani na haikushangaza alipotolewa nje kipindi cha kwanza kwenye mechi dhidi ya Simba, Oktoba 3, mwaka huu.
Lakini Kiiza amekuwa akicheza kwa kiwango cha juu mno katika timu yake ya taifa, Uganda, The Cranes pamoja na ‘kusuasua’ Yanga. 
Yanga iko Arusha tangu jana na imefikia katika hoteli ya Joshmal, huku ikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid tayari kwa mechi yao ya Ligi Kuu dhidi ya wenyeji JKT Oljoro kesho kwenye Uwanja huo.
Yanga inashika nafasi ya tatu katika Ligi Kuu, ikiwa na pointi 14, baada ya kucheza mechi tisa, nyuma ya Azam FC yenye pointi 18, baada ya kucheza mechi nane, wakati mabingwa watetezi Simba SC, wapo kileleni kwa pointi zao 19. Simba na Azam zitacheza kesho.  

AZAM FC WAKO KAMILI, WAPANIA KUIPIGA SHOTI SIMBA KESHO

Azam FC
AZAM FC wamepania kuifunga Simba SC kesho katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ili kupanda kileleni mwa ligi hiyo.
Kocha Boris Bunjak kutoka Serbia amekuwa akiwaandaa vizuri vijana wake kwa mazoezi na kisaikolojia pia kuelekea mchezo huo, unaotarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua.
Azam ipo kambini kwake, Chamazi ikijifua vikali na wachezaji wameweka kambi hapo, kwa ajili ya Ligi Kuu.
Kiboko ya nyavu za Simba na Yanga, John Raphael Bocco ‘Adebayor’ yuko fiti kupita maelezo na kiungo bora Afrika Mashariki na Kati kwa sasa, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ aliyekuwa majeruhi mwanzoni mwa msimu sasa amepona kabisa.
Kiungo Abdulhalim Humud aliyekuwa anasumbuliwa na maumivu katika mechi tatu zilizopita kwa sasa yuko fiti kabisa na habari njema zaidi ni kwamba, kiungo mwingine  Mzanzibari Abdi Kassim ‘Babbi’ amerudi kwenye fomu na anafumua mashuti makali na ya mbali ya hatari.
Viungo washambuliaji kutoka Ivory Coast, Kipre Herman Tcheche na Kipre Michael Balou wote wapo fiti sawa na makipa Deo Munishi ‘Dida’, Mwadini Ally, mabeki Ibrahim Shikanda, Erasto Nyoni, Said Mourad na Aggrey Morris.
Kwa ujumla Azam iko tayari kwa mechi hiyo ya kesho ambayo wamepania kushinda ili kulipa kisasi cha kufungwa na Simba katika Kombe la BancABC Sup8R.
Simba yenyewe inaendelea vizuri na kambi yake visiwiani Zanzibar kujiandaa na mchezo huo na inatarajiwa kurejea kesho mchana na moja kwa moja kuelekea uwanjani kukipiga.   

SIMBA TAYARI KULAMBA KONI ZA AZAM KESHO

Kikosi cha Simba

WEKUNDU wa Msimbazi, Simba SC wanatarajiwa kurejea kesho Dar es Salaam wakitokea Zanzibar ambako waliweka kambi ya wiki moja kujiandaa na mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Taifa.
Pamoja na Juma Nyosso na Haruna Moshi kusimamishwa, lakini wachezaji waliobaki wana morali ya hali ya juu na wamepania kushinda mechi ya kwanza kati ya nne, baada ya sare tatu mfululizo.  
Kwa kawaida Simba SC huenda Zanzibar katikati ya Ligi Kuu kuweka kambi linapokaribia pambano dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Yanga SC lakini kwa kitendo cha kwenda kujichimbia huko kwa ajili ya Azam, maana yake wanaipa uzito huo mechi hiyo.
Simba ilienda Zanzibar Jumanne, siku moja baada ya kurejea kutoka Tanga, ambako ililazimishwa sare ya bila kufungana na wenyeji Mgambo JKT Jumapili katika mfululizo wa ligi hiyo.
Matokeo hayo, yaliifanya Simba ifikishe pointi 19, baada ya kucheza mechi tisa na kuendelea kuongoza Ligi Kuu.
Awali ya hapo, Simba ilitoka 2-2 na Kagera Sugar Uwanja wa Taifa na 0-0 na Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani.
Baada ya sare ya Jumapili, Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage amewataka wanachama na wapenzi wa klabu hiyo kuwa watulivu na wasikatishwe na tamaa na sare tatu mfululizo za timu hiyo katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kwani safari bado ni ndefu.
Rage amesema kwamba, hadi sasa timu yao haijafungwa katika Ligi Kuu kuashiria kwamba bado ni timu bora na matokeo ya sare hizo tatu mfululizo pia ni kutokana na uimara wa timu yao.
Rage ameonya wanachama wenye desturi ya kutoa maneno ya uchochezi timu inapoyumba kidogo, waache kufanya hivyo kwa sababu wanaweza kuvuruga amani iliyopo sasa klabuni.
 
 

Wenger ajadili kuporomoka kwa Arsenal


>>ASEMA kufungwa na Schalke ni AJALI tu!!
ARSENE_WENGER-13Kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka Klabuni Arsenal uliofanyika jana mjadala mkali ulizuka baada ya Wadau wa Klabu hiyo kucharuka wakionyesha kukerwa na matokeo mabovu yaliyoiandama hivi karibuni na kusababisha Mwenyekiti Peter Hill-Wood Mtendaji Mkuu Ivan Gazidis na Mwanahisa Mkubwa Stan Kroenke wazomewe wakati wakihutubia hali ambayo ilimfanya Meneja Arsene Wenger asimame na kutoa maelezo yaliyopunguza munkari kwenye Mkutano huo.
Akielezea hali halisi, Wenger alisema fomu ya Timu hivi karibuni imeanguka kidogo lakini ameipa Timu yake changamoto kushinda Mechi ya Jumamosi ya Ligi Kuu England dhidi ya Queens Park Rangers itayochezwa Uwanja wa Emirates.
Arsenal walishika kasi baada ya sare kadhaa Msimu huu ulipoanza lakini katika Mechi zao mbili zilizopita zote wamefungwa wakianza kwa kichapo cha Ligi na Norwich City walipofungwa 1-0 na kuwafanya wawe Pointi 10 nyuma ya vinara Chelsea na kikaja kichapo kutoka kwa Schalke cha bao 2-0 kilichowafanya wapokonywe uongozi wa Kundi lao kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Akiongea kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Arsenal, Wenger alisema anaamini Kikosi chake kitarudia hali yake.
Wenger alisema: “Tulipokuwa West Ham tulicheza vizuri, tulikuwa hatari tukishambulia lakini zikaja hizi Mechi mbili na tumecheza ovyo. Ni ngumu kuelezea. Tumegonga ukuta katika Mechi hizi mbili. Lakini inabidi turudie umakini wetu, tucheze gemu yetu ya kawaida na tusikubali kufungwa kizembe. Tunao Wachezaji wazuri, ushindi utakuja tu!”
Aliongeza: “Kilichotokea Jumatano lazima tukikubali, tunajua hatukucheza vizuri Mechi na Schalke, tumepoteza Mechi moja katika Mechi 43 za Ulaya. Ajali kama hii inaweza kutokea! Kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI bado tupo kwenye nafasi nzuri. Ni muhimu kwenye Ligi tupate matokeo mazuri ili twende juu.”
Akiongelea Kikosi chake, Wenger amesema Wachezaji majeruhi ni Kieran Gibbs (Paja) naTheo Walcott (Kifua) lakini Alex Oxlade-Chamberlain, Jack Wilshere na Bacary Sagna sasa wako fiti na wanaweza kujumuishwa kwenye Kikosi kitakachoivaa QPR.
++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumamosi, Oktoba 27, 2012
[SAA 8 Dak 45 Mchana]
Aston Villa v Norwich City
[SAA 11 Jioni]
Arsenal v Queens Park Rangers
Reading v Fulham
Stoke City v Sunderland
Wigan Athletic v West Ham United
[SAA 12 na Nusu Jioni]
Manchester City v Swansea City
Jumapili, Oktoba 28, 2012
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Everton v Liverpool
[SAA 12 Jioni]
Newcastle United v West Bromwich Albion
Southampton v Tottenham Hotspur
[SAA 1 Usiku]
Chelsea v Manchester United
++++++++++++++++++++++
 

BPL: Wikiendi MOTO, BIGI MECHI-Chelsea v Man United Stamford Bridge!



>>JUMAPILI DABI ya LIVERPOOL ya 219: Everton v Liverpool!
>>KAGAWA nje WIKI 4!!
 
Shinji Kagawa of Manchester United feels the pain of an injury
Shinji Kagawa of Manchester United feels the pain of an injury
>>JUA MAREFA wa KILA MECHI!!
Timu zote 20 za Ligi Kuu England zitashuka dimbani kwa Mechi za Ligi Jumamosi na Jumapili kwa kucheza Mechi 10 lakini kati ya hizo, bila shaka, BIGI MECHI itakuwa ile ya Stamford Bridge ambayo vinara wa Ligi Chelsea wataivaa Manchester United iliyo nafasi ya pili na Mechi ya mvuto ni ile DABI ya Jiji la Liverpool Uwanjani Goodison Park kati ya Everton na Liverpool.
++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumamosi, Oktoba 27, 2012
[SAA 8 Dak 45 Mchana]
Aston Villa v Norwich City
[SAA 11 Jioni]
Arsenal v Queens Park Rangers
Reading v Fulham
Stoke City v Sunderland
Wigan Athletic v West Ham United
[SAA 12 na Nusu Jioni]
Manchester City v Swansea City
Jumapili, Oktoba 28, 2012
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Everton v Liverpool
[SAA 12 Jioni]
Newcastle United v West Bromwich Albion
Southampton v Tottenham Hotspur
[SAA 1 Usiku]
Chelsea v Manchester United
++++++++++++++++++++++
BPL_LOGOLakini, Manchester United watatinga huko Stamford Bridge huku wakiwa na habari mbaya za kumkosa Kiungo wao mahiri kutoka Japan, Shinji Kagawa, ambae atalazimika kuwa nje ya Uwanja kwa Wiki 3 hadi 4 akiuguza goti aliloumia kwenye Mechi na Braga iliyochezwa majuzi Jumanne.
Wakati, Sir Alex Ferguson anathibitisha kukosekana kwa Kagawa pia alithibitisha kurudi tena Uwanjani kwa Chris Smalling ambae alivunjika kidole cha mguu.
Msimu huu, Chelsea wamepoteza Pointi 2 tu kwenye Ligi  na hawajafungwa hata Mechi moja na wako Pointi 4 mbele ya Man United na wakiwa na Wachezaji hatari Eden Hazard, Juan Mata na Oscar wamekuwa tishio katika mashambulizi yao.
Hilo linatambulika kwa Ferguson ambae amesema: “Siku zote ni gemu ngumu kwa Chelsea na Man United. Unazo Timu nzuri. Wote wapo juu baada ya kuanza vyema na Chelsea wanatumia mfumo wa kuvutia na hilo lazima tulikabili. Wamewaleta Oscar na Hazard ni Wachezaji wazuri. Wamemwingiza Mata ambae anafana uchezaji na kina Oscar ambao wanacheza nyuma tu ya Straika wao mmoja. Si mfumo rahisi kuukabili lakini lazima tutafute njia. Kwa sasa hawana Drogba tena na wamebidi wabadilike. Walipokuwa na Drogba walikuwa wanaweza kucheza mipira mirefu au kupitia kati. Sasa hayupo, ni moja kwa moja wanapitisha mipira kupitia kati kwenye Kiungo.”

DABI: Everton v Liverpool
Tangu enzi hii ni mojawapo ya Dabi inayoheshimika Duniani yenye ushindani mkali na hii ni Dabi ya 219 ambapo Liverpool wameshinda mara 87, Everton mara 66 na sare 65.
Katika Mechi 11 za Ligi Kuu ambazo Everton wamekutana na Liverpool wameshinda Mechi 1 tu, sare 3 na kufungwa 7.
Lakini, safari hii, Everton watajiona kama wana nafasi kubwa kuifunga Liverpool hasa kwa vile wao wameanza Msimu vizuri na wapo nafasi ya 4 kwenye Msimamo wa Ligi wakiwa na Pointi 15 huku Liverpool wakiwa nafasi ya 12 na wana Pointi 9 tu.
MAREFA kwa MECHI za WIKIENDI:
Jumamosi Oktoba 27
Aston Villa v Norwich
Refa: P Dowd
Refa Wasaidizi: A Garratt, A Halliday
Refa wa Akiba: M Oliver
Arsenal v Queens Park Rangers
Refa: A Taylor
Refa Wasaidizi: J Collin, J Brooks
Refa wa Akiba: L Mason
Reading v Fulham
Refa: M Jones
Refa Wasaidizi: P Bankes, A Holmes
Refa wa Akiba: L Probert
Stoke City v Sunderland
Refa: M Halsey
Refa Wasaidizi: D Bryan, M Wilkes
Refa wa Akiba: D Drysdale
Wigan Athletic v West Ham United
Refa: J Moss
Refa Wasaidizi: R Ganfield, G Beswick
Refa wa Akiba: G Eltringham
Manchester City v Swansea City
Refa: M Atkinson
Refa Wasaidizi: S Burt, J Flynn
Refa wa Akiba: S Attwell
Jumapili Oktoba 28
Everton v Liverpool
Refa: A Marriner
Refa Wasaidizi: S Ledger, S Bennett
Refa wa Akiba: P Dowd
Newcastle United v West Bromwich Albion
Refa: C Foy
Refa Wasaidizi: H Lennard, R West
Refa wa Akiba: M Halsey
Southampton v Tottenham Hotspur
Refa: L Mason
Refa Wasaidizi: D England, D C Richards
Refa wa Akiba: R East
Chelsea v Manchester United
Refa: M Clattenburg
Refa Wasaidizi: M McDonough, S Long
Refa wa Akiba: M Jones
 

LA LIGA: Mabao zaidi kwa Radamel Falcao??


RADAMEL_FALCAOJumapili kwenye La Liga Atletico Madrid watakuwa wenyeji wa Timu iliyo mkiani Osasuna na Straika wao hatari, Radamel Falcao, ana uhakika wa kufunga mabao baada ya kufunga Bao 16 katika Mechi zake 10 zilizopita alizoichezea Atletico Madrid au Timu yake ya Taifa Colombia.
+++++++++++++++++++++++
WAFUNGAJI BORA LA LIGA:
1 Lionel Messi [Barcelona] Mabao 11
2 Cristiano Ronaldo [Real Madrid] 9
Radamel Falcao [Atlético Madrid] 9
4 Aritz Aduriz          [Athletic Bilbao] 6
Álvaro Negredo [Sevilla FC] 6
Tomer Hemed [Mallorca]  6
+++++++++++++++++++++++
Kwenye La Liga, Mabao ya Falcao yameiinua Atletico Madrid na kuifikisha nafasi ya Pili kwenye Msimamo wa Ligi wakiwa Pointi sawa na vinara Barcelona ambao wamewazidi kwa ubora wa tofauti ya Magoli.
Msimu huu, Atletico Madrid imeshinda Mechi zao zote 11 zilizopita.
Atletico Madrid, ambao mara ya mwisho kutwaa Ubingwa wa Spain ni Msimu wa 1995/6, jana Alhamisi waliichapa Academica de Coimbra ya Portugal bao 2-1 kwenye Mechi ya Kundi la EUROPA LIGI.
RATIBA:
Jumamosi Oktoba 27
Espanyol v Málaga [Cornellà - El Prat]
Real Betis v Valencia [Estadio Manuel Ruiz de Lopera]
Celta Vigo v Deportivo La Coruña [Estadio Balaídos]
Rayo Vallecano v Barcelona [Campo de Fútbol de Vallecas]
Jumapili Oktoba 28
Athletic Bilbao v  Getafe [Estadio San Mamés]
Atlético Madrid v Osasuna [Vicente Calderon]
Levante v Granada [Ciudad de Valencia]
Mallorca v Real Madrid [Estadio Son Moix]
Real Zaragoza v Sevilla FC [Estadio La Romareda]
v Real Sociedad [Estadio Nuevo José Zorrilla]
Jumatatu Oktoba 29
Valladolid v Real Sociedad [Estadio Nuevo José Zorrilla]
 
 

EUROPA LIGI: Liverpool, Newcastle zatungua, Spurs sare!


EUROPA_LIGI_CUPBao la Dakika ya 53 la Steve Downing limewapa Liverpool ushindi wao bao 1-0 walipocheza na Anzhi Makhachkala ya Urusi wakati Newcastle, wakiwa nyumbani St James Park, waliifunga Club Brugge ya Belgium bao 1-0 kwa bao la Gabriel Obertan huku Tottenham, wakicheza ugenini, walitoka 1-1 na  Maribor ya Slovenia.
Nae Rodrigo Palacio alifunga katika Dakikaya 88 na kuipa Inter Milan ushindi dhidi ya Partizan Belgrade, huku wenzao Lazio wakitoka 1-1 na Panathinaikos, Napoli kuchapwa 3-1 na Dnipro Dnipropetrovsk na Udinese wakipigwa 3-1 na Young Boys kwa hetitriki ya Raul Bobadilla.
Mabingwa watetezi Atletico Madrid wamepata ushindi wao wa tatu mfululizo walipoichapa Academica Coimbra bao 2-1 huku Timu nyingine ya Spain, Athletic Bilbao, Washindi wa Pili Msimu uliopita, wakichapwa 2-1 na Olympique Lyon.
MATOKEO-MECHI DEI 3:
Alhamisi, Oktoba 25
Liverpool FC 1 FC Anzhi Makhachkala 0
BSC Young Boys 3 Udinese Calcio 1
Club Atlético de Madrid 2 A. Académica de Coimbra 1
Hapoel TelvAviv FC 1 FC Viktoria Plzen 2
VfL Borussia Mönchengladbach 2 Olympique de Marseille 0
AEL Limassol FC 0 Fenerbahçe SK 1
Newcastle United FC 1 Club Brugge KV 0
CS Marítimo 1 FC Girondins de Bordeaux 1
FC Steaua Bucuresti 2 Molde FK 0
VfB Stuttgart 0 FC København 0
PSV Eindhoven 1 AIK 1
FC Dnipro Dnipropetrovsk 3 SSC Napoli 1
Videoton FC 2 FC Basel 1
KRC Genk 2 Sporting Clube de Portugal 1
FC Rubin Kazan 1 Neftçi PFK 0
FC Internazionale Milano 1 FK Partizan 0
AC Sparta Praha 3 Hapoel Kiryat Shmona FC 1
Olympique Lyonnais 2 Athletic Club 1
Panathinaikos FC 1 S.S. Lazio 1
NK Maribor 1 Tottenham Hotspur 1
Rosenborg BK 1 FC Metalist Kharkiv 2
SK Rapid Wien 0 Bayer 04 Leverkusen 4
Helsingborgs 1 Hannover 2
Levante UD 3 FC Twente 0
BSC Young Boys 3 Udinese 1
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Novemba 8
FC Anzhi Makhachkala v Liverpool FC
Udinese Calcio v BSC Young Boys
A. Académica de Coimbra v Club Atlético de Madrid
FC Viktoria Plzen v Hapoel TelvAviv FC
Olympique de Marseille v VfL Borussia Mönchengladbach
Fenerbahçe SK v AEL Limassol FC
Club Brugge KV v Newcastle United FC
FC Girondins de Bordeaux v CS Marítimo
Molde FK v FC Steaua Bucuresti
FC København v VfB Stuttgart
AIK v PSV Eindhoven
SSC Napoli v FC Dnipro Dnipropetrovsk
FC Basel 1893 v Videoton FC
Sporting Clube de Portugal v KRC Genk
Neftçi PFK v FC Rubin Kazan
FK Partizan v FC Internazionale Milano
Hapoel Kiryat Shmona FC v AC Sparta Praha
Athletic Club v Olympique Lyonnais
S.S. Lazio v Panathinaikos FC
Tottenham Hotspur FC v NK Maribor
FC Metalist Kharkiv v Rosenborg BK
Bayer 04 Leverkusen v SK Rapid Wien
Hannover 96 v Helsingborgs IF
FC Twente v Levante UD
 

 

RATIBA YA NAKUNDI ULAYA YASOGEZWA MBELE.

SHIRIKISHO la Soka barani Ulaya-UEFA limeamua kusogeza mbele upangwaji wa ratiba ya michuano ya Ligi ya Mabingwa na Europa League hatua ya mtoano.
 
 Shughuli hiyo kwa kawaida ilitakiwa kufanyika Desemba 14 mwaka huu lakini wamesogeza mbele kwa siku sita zaidi kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi.  
 
Katika taarifa ya UEFA iliyotumwa katika mtandao imesema kuwa ratiba ya hatua ya mtoano ya michuano hiyo ya Ulaya 2012-2013 ambayo kwa kawaida hufanyika Desemba 14 sasa imesogezwa mbele mpaka Alhamisi Desemba 20 katika makao makuu ya shirikisho hilo jijini Nyon, Switzerland.  
 
Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itafanyika katika Uwanja wa Wembley jijino London Uingereza May 25 mwakani huku fainali ya Europa League yenyewe itafanyika jijini Amsterdam, Uholanzi katika Uwanja wa ArenA 10 siku kumi baadae.

NITASHIKANA MIKONO NA TERRY - ROBERTS.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Reading Jason Roberts amesema kuwa atashikana mikono na John Terry lakini amekataa kuweka wazi kama anafikiri nahodha huyo wa Chelsea ni mbaguzi. 
 
 Terry ambaye ni nahodha wa zamani wa Uingereza amefungiwa mechi nne na kutozwa faini ya paundi 220,000 baada ya kukutwa na hati ya kumfanyia vitendo vya kibaguzi Anton Ferdinand wa Queens Park Rangers mwaka jana.
 
 Akihojiwa kuhusiana na suala hilo Roberts amesema kuwa atashikana mikono na Terry lakini alipoulizwa kama anadhani beki huyo ni mbaguzi alikwepa swali hilo na kurudia sentensi yake ya kwanza.
 
 Ikiwa ni mwaka mmoja umepita toka kutokea kwa tukio hilo la Terry lakini kumekuwa na muendelezo wa matukio ya aina hiyo sehemu tofauti likiwemo tukio la mwezi ambapo beki wa timu ya vijana wa miaka chini ya 21 ya Uingereza Danny Rose alianyiwa vitendo vya kibaguzi wakati wa mechi nchini Serbia. 
 
 Roberts aliungana na wachezaji wengine weusi nchini Uingereza wakiwemo Rio na Anton Ferdinand kutovaa tisheti za kampeni ya kutokomeza ubaguzi michezoni wakidai kusuasua kwa juhudi za kupiga vita suala hilo.

VETTEL AJITENGENEZEA NAFASI NZUR YA KUNYAKUWA TAJI LA INDIAN GRAND PRIX.

DEREVA nyota wa mbio za magari za Langalanga, Sebastian Vettel amefanikiwa kupata nafasi ya kwanza kabla ya kuanza kwa michuano ya Indian Grand Prix nafasi ambayo imemuweka katika nafasi nzuri ya kushinda mashindano hayo kwa mara ya nne mfululizo Jumapili.  
 
Vettel mwenye umri wa miaka 25 raia wa Ujerumani kutoka timu ya Redbull ambaye anaongoza orodha ya madereva bora kwa alama sita zaidi ya Fernando Alonso wa timu ya Ferrari alitumia muda mzuri wa dakika moja na sekunde 27.
 
 Dereva wa timu ya MacLaren Jenson Button alishika nafasi ya pili katika mbio hizo huku Alonso akikamata nafasi ya tatu na nafasi ya nne kwenda kwa Lewis Hamilton wakati tano bora ilifungwa na dereva mwenzake Vettel wa timu ya Redbull Mark Webber.  
 
Mashindano hayo yatafanyika ramsi Jumapili huku Vettel akipambana vilivyo kuhakikisha anashinda na kujiongezea alama ili aweze kuwa bingwa wa dunia mwishoni mwa msimu huu ambao kumebakiwa na mshindano manne pekee.


TANZIA NGUMI.

KOCHA Emanuel Steward ambaye amewafundisha mabondia nguli kama Thomas Hearns, Lennox Lewis na Wladimir Klitschko amefariki dunia akiwa na miaka 68. 
 
 Alianza kujizolea umaarufu wakati alipokuwa akifundisha jijini Detroit ambapo Hearns aliyekuwa mwanafunzi wake alipokuwa bingwa wa dunia mwaka 1980. Steward ambaye ni raia wa Marekani ndio bondia aliyefundisha mabondia wengi zaidi ambao ni mabingwa wa dunia kuliko kocha yoyote wa mchezo huo na alifanya kazi na bingwa wa uzito wa juu Klitschko Julai mwaka huu. 
 
 Klitschko alituma salamu zake za rambirambi kwa Steward akimuelezea kama mwalimu bora wa mchezo huo kupata kutokea na kwamba ulimwengu wa masumbwi umempoteza mtu muhimu. 
 
 Steward ambaye alikuwa akisumbuliwa na kansa ya utumbo pia aliwafundisha mabondia wakubwa kama Wilfred Benitez, Julio Cesar Chavez, Oscar de la Hoya, Evander Holyfield, Mike McCallum na James Toney. 

SEREA AMGARAGAZA TENA AZARENKA.

MCHEZAJI nyota anayeshika namba moja katika orodha za ubora duniani kwa upande wa wanawake mwanadada Victoria Azarenka amebakia katika mashaka kama atamaliza mwaka huu katika nafasi hiyo baada ya kufungwa na Serena Williams kwa mara ya tano katika vipindi tifauti walivyokutana mwaka huu.
 
 Azarenka ambaye anatoka Belarus alikubali kufungwa kwa 6-4 6-4 naWilliams kutoka Marekani katika michuano ya WTA inayofanyika jijini Istabul ambapo sasa itabidi ahakikishe anamfunga Li Na bingwa wa zamani wa michuano ya wazi ya Ufaransa kutoka China ili aweze kujihakikishia nafasi hiyo.  
 
Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Williams amesema kuwa alifanya mazoezi ya nguvu ili aweze kucheza vyema na anatarajia ataendlea kufanya vyema na kama ikishindikana atajaribu kufanya hivyo tena mwakani.
 
 Azarenka ambaye alifungwa na Williams katika michuano ya wazi ya Marekani mwezi uliopita alianza vyema mchezo huo kwa kuongoza katika seti ya kwanza lakini Williams ambaye naye alikuwa akicheza chini ya kiwango alikuja juu na kuhakikisha hapotezi mchezo huo muhimu.