Thursday, January 10, 2013

BAADA YA KUIKWEPA KWEPA TUSKER SASA AZAM ANAKIBARUA KIGUMU KUTOKA KWA MABINGWA HAWA WA KENYA


Kikosi cha Tusker leo

TUSKER FC imefanikiwa kuingia fainali ya Kombe la Mapinduzi usiku huu baada ya kuifunga Miembeni FC ya hapa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Kwa ushindi huo, Tusker itamenyana na Azam katika fainali ya michuano hiyo keshokutwa kwenye Uwanja wa huu huu wa Amaan.
Hadi mapumziko hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango la mwenzake na zote zilishambuliana kwa zamu na kila timu ilipoteza nafasi mbili za wazi za kufunga mabao.
Lakini kipindi cha pili Tusker walirekebisha makosa yao na kufanikiwa kupata mabao yaliyowavusha Fainali ya michuano hii.
Bao la kwanza alifunga Luke Ochieng dakika ya 52 kabla ya Jesse Were kufunga la pili dakika ya 72, ambalo linakuwa bao lake la nne katika mashindano haya.
Katika mchezo huo, kikosi cha Miembeni FC kilikuwa; Abdulsamad Sele, Kassim Hamad, Adeyum Saleh, Salum Hajji, Ibrahim Abbas, Sabri Ally, Suleiman Ali/Omar Tamim dk 83, Laurent Mugia/Salim Seif ‘Bakayoko’ dk83, Monja Liseki ‘Anelka’/Peter Ilunda dk 10, Rashid Roshwa/Mohamed Salum dk58 na Issa Othman ‘Amasha’.
Tusker FC; Samuel Odhiambo, Luke Ochieng, Bright Jeremiah, Mark Odhiambo, Martin Kizza/Humphrey Okoth dk89, Frederick Onyango, Justine Monga/Andrew Tololwa dk54, Khalid Aucho, Jesse Were/Andrew Sekayambya dk73, Ismail Dunga na Robert Omonok.

BPL WIKIENDI: BIGI MECHI MAN UNITED v LIVERPOOL, ARSENAL v MAN CITY!


BARCLAYS PREMIER LEAGUE, BPL, inarejea kilingeni Wikiendi hii baada ya kuzipisha Mechi za Raundi ya 3 ya FA CUP Wikiendi iliyopita na Mechi zenye mvuto ni zile BIGI MECHI mbili zitakazochezwa Jumapili, Man United v Liverpool, na Arsenal v Man City.

RATIBA:
Jumamosi 12 Januari 2013
[SAA 12 Jioni]
Aston Villa v Southampton
Everton v Swansea
Fulham v Wigan
Norwich v Newcastle
Reading v West Brom
Stoke v Chelsea
Sunderland v West Ham
Jumapili 13 Januari 2013
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Man United v Liverpool
[SAA 1 Usiku]
Arsenal v Man City
Jumatatu 14 Januari 2013
[SAA 5 Usiku]
QPR v Tottenham

EVRA_N_SUAREZAkiongelea Mechi yao na Liverpool, Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, amesema maombi yake kuhusu Mechi hiyo ni kuwa iweke Vichwa vya Habari kwenye Vyombo vya Habari vinavyohusu mpira tu.
Mara ya mwisho kwa Man United kukutana na Liverpool Uwanjani Old Trafford, Gemu hiyo iligubikwa na kituko cha Straika wa Liverpool, Luis Suarez, kukataa kumpa mkono Patrice Evra lakini katika Mechi yao ya mwisho iliyochezwa huko Anfield Mwezi Septemba, Wachezaji hao walipeana mikono.
Suarez aligoma kumpa mkono Evra baada ya kuadhibiwa kwa kumkashifu Kibaguzi Evra kwenye Mechi ya nyuma Liverpool walipokutana na Man United.

MSIMAMO:
1 Man Utd Mechi 21 [Tofauti ya Magoli 26] Pointi 52
2 Man City Mechi 21 [Tofauti ya Magoli 22] Pointi 45
3 Tottenham Mechi 21 [Tofauti ya Magoli 12] Pointi 39
4 Chelsea Mechi 19 [Tofauti ya Magoli 21] Pointi 38
5 Arsenal Mechi 20 [Tofauti ya Magoli 18] Pointi 34
6 Everton Mechi 20 [Tofauti ya Magoli 8] Pointi 33
7 West Brom Mechi 21 [Tofauti ya Magoli 2] Pointi 33
8 Swansea Mechi 21 [Tofauti ya Magoli 5] Pointi 29
9 Stoke Mechi 21 [Tofauti ya Magoli 1] Pointi 29
10 Liverpool Mechi 20 [Tofauti ya Magoli 5] Pointi 28
11 West Ham Mechi 20 [Tofauti ya Magoli 0] Pointi 26
12 Norwich Mechi 21 [Tofauti ya Magoli -10] Pointi 25
13 Fulham Mechi 21 [Tofauti ya Magoli -5] Pointi 24
14 Sunderland Mechi 20 [Tofauti ya Magoli -5] Pointi 22
15 Newcastle Mechi 20 [Tofauti ya Magoli -11] Pointi 20
16 Aston Villa Mechi 21 [Tofauti ya Magoli -24] Pointi 19
17 Southampton Mechi 20 [Tofauti ya Magoli -11]  Pointi 18
18 Wigan Mechi 21 [Tofauti ya Magoli -17] Pointi 18
19 Reading Mechi 20 [Tofauti ya Magoli -17] Pointi 13
20 QPR Mechi 20 [Tofauti ya Magoli -20] Pointi 10

Ferguson ametamka: “Siku zote kutakuwa na kukuzwa kwa Mechi kati ya Manchester United na Liverpool kwa sababu tu ya Historia ya Timu hizi, ambazo ndizo zenye mafanikio makubwa kupita zozote nyingine Nchini humu!”
Ferguson ameongeza kuwa Watu wengi huleta Ajenda zao kuhusu Mechi hii na kuzikuza kupita kiasi na akatamka: “Bahati mbaya Mwaka jana kulikuwa na matukio ya Suarez. Natumai sasa hilo limepitwa na kila Klabu itilie mkazo Gemu tu!”

MUACHENI MOURINHO AFANYE KAZI YAKE - RONALDO.


MSHAMBULIAJI nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amewataka mashabiki wa klabu hiyo kuacha kumshambulia Jose Mourinho na badala waelekeze nguvu zao katika kuiwaunga mkono. Kauli hiyo ya Ronaldo imekuja kufuatia mashabiki wa klabu hiyo kumzomea Mourinho kabla ya kuanza kwa mchezo Kombe la Mfalme dhidi ya Celta Vigo ambao ulichezwa katika Uwanja wa Santiago Bernabeu huku Madrid walishinda mchezo huo kwa mabao 4-0. Katika mchezo huo Ronaldo ambaye ndiye mfungaji anayeongoza katika klabu hiyo akiwa amepachika mabao 174 katika michezo 172 aliyocheza toka ahamie kutoka Manchester United alifunga mabao matatu na na kuibuka nyota wa mchezo huo. Ronaldo amesema mashabiki hao inabidi waache tabia hiyo kwani bado kuna mataji mengi ambayo wanaweza kushinda mwaka huu na akiwa kama kocha lazima awe na uamuzi wa mwisho hivyo mashabiki na wachezaji wanapaswa kuheshimu na kumuunga mkono.
No comments:

LICHA YA JANA KUSHINDA BAO 4-0 HALI YA HEWA REAL NI MBAYAMASHABIKI WADAI MOURINHO AMEVURUGA MVUTO WA REAL

>>KUMBWAGA CASILLAS KWAMLETEA CHUKI!!
>>KLABUNI HALI SI SHWARI!!
>>MPASUKO WA WACHEZAJI, WA SPAIN NA URENO!!
IKER_CASILLASKUFUATIA Kura ya Maoni huko Madrid na kuchapishwa na Gazeti maarufu, Marca, Mashabiki Asilimia 62 wa Real Madrid wametoa msimamo wao kuwa Kocha wa Klabu hiyo, Jose Mourinho, ameuharibu mvuto wa Klabu hiyo maarufu.
Kura hiyo ya Maoni iliyohusisha Wanachama 704 na Asilimia 54.4 wametaka aendelee kubaki lakini Asilimia 41.8 wametaka aondoke huku mafanikio yake kiutendaji yakishuka kutoka 8.82 kati ya 10 aliyopata Machi 2011 hadi 6.68 kati ya 10.JOSE_MOURINHO-poa
Kura hiyo ya Maoni iliendeshwa na Sigma Dos na ni ushahidi tosha hali si shwari ndani ya Real Madrid ambao ndio Mabingwa watetezi wa La Liga lakini hadi sasa wako Pointi 16 nyuma ya Vinara Barcelona na pia wapo hatarini kutupwa nje ya Copa del Rey ambako walifungwa 2-1 na Celta Vigo katika Mechi ya kwanza na leo ni marudio yake Uwanjani Santiago Bernabeu.
Hali hii ya sasa ndani ya Real Madrid pia itamletea matatizo makubwa Rais wao Florentino Perez ambae Mwaka huu anakabiliwa na Uchaguzi katika nafasi yake.
Mashabiki wengi wa Real wanachukizwa na tabia ya Jose Mourinho ya ‘kiugomvi ugomvi’ na Siku zote kudai Timu yake inaonewa wakati Mashabiki hao wana msimamo kuwa Klabu yao ni ya Kiungwana ambayo Siku zote inakubali kushinda na kushindwa kiungwana.
Hivi karibuni, Mourinho alishutumiwa sana kwa kumpiga Benchi Kipa na Nahodha wao Iker Casillas huku kukiwa na tuhuma kuwa hali si njema miongoni mwa Wachezaji ikidaiwa kuna mgawanyiko upande mmoja ukiwa wa Wachezaji wa Spain na mwingine Wachezaji kutoka Ureno.

CAPITAL ONE CUP: CHELSEA YAPIGWA STAMFORD BRIDGE,MICHU STAY ON FIRE AWATUMIA SALAMU WANAOMTAKA KATIKA DIRISHA HILI LA USAJILI!

CAPITAL_ONE_CUP-BESTSwansea imeshinda nyumbani kwa Chelsea kwa mara ya kwanza katika Miaka 87 baada ya jana kushinda 2-0 katika Mechi ya kwanza ya Nusu Fainali ya CAPITAL ONE CUP.
Ingawa Chelsea walitawala Mechi, hasa Kipindi cha Kwanza, lakini makosa ya Beki wao Branislav Ivanovic yalimruhusu Michu kufunga Bao la kwanza.

MAGOLI:
Chelsea 0
Swansea 2
-Michu Dakika ya 39
-Graham 90
+++++++++++++++++++
Branislav Ivanovic alirudia makosa na pasi yake ya nyuma kunaswa na Graham katika Dakika za mwishoni na kupachika Bao la pili.
Timu hizi zitarudiana tena Liberty Stadium hapo Januari 23.
Juzi, kwenye Mechi nyingine ya Nusu Fainali ya Kwanza, Bradford City iliichapa Aston Villa Bao 3-1.
VIKOSI:
Chelsea: Turnbull, Ivanovic, Cole, David Luiz, Cahill, Azpilicueta, Ramires (Lampard - 71' ), Mata, Oscar (Marin - 83' ), Hazard, Torres (Ba - 81' )
Akiba: Hilario, Ferreira, Bertrand, Lampard, Marin, Ake, Ba
Swansea City: Tremmel, Chico, Williams, Rangel, Davies, Britton, Michu (Graham - 83' ), Pablo, Routledge (Tiendalli - 62' ), De Guzman, Ki Sung-Yeung
Akiba: Vorm, Monk, Tiendalli, Dyer, Agustien, Graham, Shechter
Refa: Taylor
RATIBA/MATOKEO:
NUSU FAINALI
[Mechi zote kuanza SAA 4 DAK 45 Usiku]
Jumanne Januari 8
Bradford 3 Aston Villa 1
Jumatano Januari 9
Chelsea 0 Swansea City 2
MARUDIANO
Jumanne Januari 22
Aston Villa v Bradford
Jumatano Januari 23
Swansea City v Chelsea
FAINALI
Jumapili Februari 24
Uwanja wa Wembley, London

RONALDO APIGA HAT-TRICK AKIISAIDIA REAL MADRID KUTINGA ROBO FAINALI YA KING'S CUP AU COPA DEL REY NA HUKO ITALY KIBIBI CHAONYESHA UMWAMBA KWA AC MILAN .


MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Ureno na klau ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo jana amekuwa nyota ya mchezo baada ya kufanikiwa kuifungia klabu yake mabao matatu katika ushindi wa mabao 4-0 waliopata dhidi ya Celta Vigo ambao umewapeleka katika hatua ya robo fainali ya Kombe la Mfalme. Ronaldo ambaye alishika nafasi ya pili katika tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa dunia, alifunga mabao mawili ndani ya dakika 25 za kipindi cha kwanza na kumalizia lingine moja katika dakika za lala salama na kuihakikishia timu yake ushindi. Madrid imefanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kuifunga Celta Vigo kwa jumla ya mabao 5-2 kwenye michezo miwili waliyokutana na sasa wanatarajia kukutana na Valencia wiki ijayo. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Mkurugenzi wa Michezo wa klabu hiyo alisifu uwezo wa nyota huyo ambao umekuwa ukiisaidia klabu hiyo kupata matokeo mazuri.

COPA del REY
MATOKEO/RATIBA-MECHI za MARUDIANO
[Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili katika Mabano]
Jumatano Januari 9
Sevilla 1 Real Mallorca 2 [6-2]
Real Madrid 4 Celta Vigo 0 [5-2]
Real Zaragoza 2 Levante 0 [3-0]
Alhamisi Januari 10
Getafe v Atletico Madrid [0-3]
Barcelona v Cordoba [2-0]
Real Betis v Las Palmas [1-1]

COPPA ITALIA

ROBO FAINALI
RATIBA/MATOKEO:
Jumatano Januari 9
Juventus 2 AC Milan 1
Jumanne Januari 15
Inter Milan v Bologna
Jumatano Januari 16
Fiorentina v AS Roma

Vucinic aifikisha Juve Nusu Fainali
Bao la Dakika za nyongeza la Mirko Vucinic limewafikisha Mabingwa Italy, Juventus, Nusu Fainali ya COPPA ITALIA walipotoka nyuma kwa Bao moja na kuifunga AC Milan Bao 2-1.
AC Milan, ambao pia Msimu uliopita walitupwa nje na Juve katika hatua kama hii, waliongoza kwa Bao la Dakika ya 6 la Stephan El Shaarawy lakini Juventus walisawazisha kwa frikiki ya Sebastian Giovinco.
Hadi Dakika 90 zinakwisha Bao zilikuwa 1-1 na ndipo Dakika 30 za Nyongeza zikachezwa na katika Dakika ya 6 tu ya muda huo, Mirko Vucinic akafunga Bao la ushindi kwa Juventus ambao sasa watacheza na Lazio kwenye Nusu Fainali.

SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA LATOA TAHADHARI KWA WALE WALIOANZA KAMPENI LASEMA MARUFUKU KUFANYA KAMPENI !!!


Shirikisho la soka nchini (TFF) limewaonya watu walioanza kampeni za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo kabla tarehe haijatangazwa.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, baadhi ya watu wenye nia ya kugombea tayari wameanza kampeni kwa ajili ya uchaguzi huo wakati bado kamati inayosimamia uchaguzi haijatoa ruhusa.

Uchaguzi huo ambao rais wa shirikisho hilo, Leodegar Tenga, hawezi kugombea tena kwa mujibu wa katiba, umepangwa kufanyika mwezi ujao katika sehemu ambayo itatangazwa.

 Katibu wa TFF, Angetile Osiah, amesema ruhusa ya kuanza kwa kampeni za uchaguzi huo bado haijatolewa na kamati inayosimamia uchaguzi.

Alisema watu wenye nia ya kugombea walioanza kampeni hizo wanakwenda kinyume na taratibu za uchaguzi mkuu.
 Osiah amesema hakuna ruhusa kwa mtu yeyote kuanza kampeni kabla ya tarehe ya uchaguzi kutangazwa na kwamba anayefanya hivyo anakiuka sheria za uchaguzi.

 Amesema kampeni ni hatua za mwisho za uchaguzi na zinaruhusiwa kufanyika baada ya kutangazwa na kuongeza huwezi kuanza kampeni wakati tarehe za uchaguzi na utoaji fomu bado hazijajulikana.

 Amesema kuwa  TFF itawachukulia hatua kali watakaobainika kuanza kampeni hizo huku akisisitiza wasubiri muda sahihi ufike ndiyo waanzae kampeni zao.

 TFF itatoa  taarifa kamili kuhusiana na uchaguzi huo zitajulikana kesho baada ya kamati ya utendaji kumaliza kikao chake na kutoa tamko rasmi la lini na wapi uchaguzi mkuu utafanyika.

Viongozi wa kuchaguliwa wa TFF waliopo madarakani tayari wamemaliza muda wao, huku rais Tenga hatagombea tena mwaka huu, kwa mujibu kamati ya uchaguzi mkuu.

YONDAN, DOMAYO WAOTA MBAWA STARS, WABAKI ULAYA


Yondan
WACHEZAJI Frank Domayo na Kelvin Yondani waliokuwa wameondoka jana jioni kuelekea nchini Ethiopia wameshindwa kuungana na wachezaji wenzao wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars baada ya jana jioni kufika Istambul  kukuta tiketi zao za kwenda Addis Ababa ni za tarehe 09 Februari 2013  hali iliyopelekea kukwama Istambul na kuamua kurejea mjini Antalya kuungana na wachezaji wenzao waliopo kambi.
Kikosi cha wachezaji 27 waliopo kambi mjini Antalya kimeendelea na mazoezi ya asubuhi kujiandaa na mchezo huo wa kesho amabao utakua ni mchezo wa mwisho kabla ya timu ya Young Africans kuanza safari ya kurejea nchini Tanzania siku ya jumapili.

CHAMA CHA NGUMI ZA KULIPWA AFRIKA MASHARIKI NA KATI ECAPBA YATEUA WAAMUZI


Chama Cha Ngumi za Kulipwa Cha Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBA) kinachoratibu ubingwa wa ECAPBF kimewateua waamuzi wa mpambano kati ya Mtanzania Thomas Mashali na bondia Bernard Mackoliech kutoka nchini Kenya.

Mpambano huo ni wa kutetea ubingwa wa ECAPBF uzito wa Middle ambao Thomas Mashali aliupata baada ya kumsambaratisha bondia Med Sebyala kutoa nchini Uganda mwaka jana.

Akitangaza waamuzi hao, Rais wa ECAPBA Onesmo Ngowi alisema kuwa Mark Hatia atakuwa msimamizi mkuu wa pambano hilo. Nemes Kavishe ambaye ndiye Mweka Hazina wa ECAPBA atakuwa ndiye refarii wa mpambano huo. Majaji watatu watakuwa ni Fidel Haynes, Said Chaku na Sakwe Mtulya.

Mpambano huo utafanyikia wakati wa sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar katika ukumbi wa Friends Corner, wilaya ya Kinondoni, jijini Dar-Es-Salaam.

Katika hatua nyingine, ECAPBA inajiandaa kuhamia katika jiji la Arusha baada ya kuombwa na uongozi wa jiji hilo kuhamishia makao yake makuu ili kuwa karibu na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC).

Juhudi za ECAPBA kuhamia Arusha zinafanywa na Meya wa jiji hilo, Mstahiki Gaudence Lyimo ambaye ni mpenzi wa michezo na maendeleo ya vijana.

STARS WAFIKA SALAMA ADDIS, WAANZA KUJIFUA LEO JIONI



KIKOSI cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kimefika salama hapa Addis Ababa tayari kwa mechi ya kirafiki dhidi ya wenyeji Ethiopia kesho kwenye Uwanja wa Taifa wa Addis Ababa kuanzia saa 11.30 jioni za Tanzania na Ethiopia.
Stars imefikia katika hoteli ya Hilton na leo itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Addis Ababa kwa saa moja kuanzia saa 11.30 jioni.
Stars imewasili hapa na wachezaji 16 tayari kwa mchezo huo maalum kwa kuipa maandalizi ya mwisho Ethiopia kabla ya kwenda Afrika Kusini kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazoanza Januari 19 mwaka huu.
Wachezaji wawili wa Yanga, beki Kevin Yondan na kiungo Frank Domayo watajiunga na kikosi cha timu mjini hapa wakitokea Antalya, Uturuki.
Kocha Mkuu wa Stars, Mdenmark Kim Poulsen na Mholanzi Ernie Brandts wa Yanga, wamekubaliana Yondan na Domayo pekee, kati ya wachezaji watano Yanga waliotwa Stars ndio wajiunge na timu hiyo.
Wachezaji wengine wa Yanga walioitwa Stars ambao wataendelea kubaki nchini Uturuki ni pamoja na Athuman Iddy ‘Chuji’, Simon Msuva na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ watakaojiunga na Stars watakaporejea nchini Januari 13.
Wachezaji waliopo hapa ni pamoja na Juma Kaseja kutoka Simba ambaye pia ndiye nahodha wa Stars na Aishi Manula ( Azam FC), huku kwa upande wa Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Amir Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), na Shomari Kapombe (Simba).
Viungo ni Salum Abubakar (Azam), Amri Kiemba (Simba), Khamis Mcha (Azam), Mwinyi Kazimoto (Simba) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), wakati washambuliaji ni Mbwana Samata, Thomas Ulimwengu  (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC) na  Mrisho Ngasa (Simba).
Stars ambayo pia itautumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi ya mechi ya mchujo dhidi ya Morocco kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia 2014, mchezo utakaochezwa Machi mwaka huu.
Katika maandalizi yake hayo, mara ya mwisho  Stars ilikwaana na Zambia Desembza 22 mwaka jana kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na  kuibanjua bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki

GAPCO WADHAMINI TENA KILI MARATHON




KWA mara nyingine tena kampuni ya mafuta ya GAPCO Tanzania imetambua umuhimu wa wanariadha wenye ulemavu kwa kuwapa fursa ya kushiriki kwenye mbio za Kilimanjaro Marathon 2013 kwa kudhamini mbio ya nusu marathon kwa ajili ya walemavu itakayojulikana kama GAPCO GAPCO 21km Disabled Half Marathon.
Mkuu wa Mauzo na Maskoko wa GAPCO, Ben Temu amesema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kuwa “Ushiriki wa wanariadha wenye ulemavu unaleta msisimko mpya kwenye Kilimanjaro Marathon kwa mara nyingine tena. Kukimbia marathon kunaendana na mambo ambayo GAPCO inayaamini katika shughuli zake za kila siku – mtazamo chanya, kipaumbele katika kujiamini na azma ya kusonga mbele”.
 “Ushiriki wa walemavu ni ushaidi kwamba watu wenye ulemavu sio tu kwamba wanaweza kufanya mambo makubwa bali pia inadhiirisha kuwa wana uwezo wa kutimiza jukumu lolote kwa ufanisi wa hali ya juu. Kama wadhamini tunahimiza jamii nzima pamoja na makampuni mengine yajitolee kudhamini walemavu waweze kushiriki Kilimanjaro Marathon katika siku zijazo,” alisema.
Mbio za hizo zitakuwa na sehemu tatu ambazo ni kiti cha magurumu (wheelchair), baiskeli ya miguu mitatu, na walemavu wanaokimbia. Washindi watajipatia zawadi nono ambazo jumla yake ni zaidi ya shilingi milioni 3.
GAPCO ina nia thabiti ya kuwasaidia wanariadha walemavu ili waweze kutimiza ndoto zao na kuthibitisha kwamba wanaweza.
Kwa mujibu wa John Addison, Mkurugenzi Mkuu wa Wild Frontiers, waadaaji wa mbio hizo, Kilimanjaro Marathon ni kati yam bio zenye mvuto zaidi duniani kutokana na kwamba zinafanyika chini ya Mlima Kilimanjaro na ndio maana huvutia washiriki kutoka nchi zaidi ya 40 kila mwaka. Mbio hazivutii wanariadha peke yao bali pia watalii ambao huchangia pato la taifa”, alisema.

KIUNGO MTALAAMU WA AZAM AMBAYE ALIWAHENYESHA AKINA DROGBA KATIKA DIMBA LA TAIFA KWA MARA YA KWANZA ABDUHALIM HUMUD GAUCHO AONGEZA NGUVU AZAM VISIWAN ZANZIBAR,NA PAZI ATOLEWA KWA MKOPO JESHINI


KIUNGO mshambuliaji wa mabingwa wa Kombe la Mapinduzi, Azam FC, Zahor Iddi Pazi ametolewa kwa mkopo katika klabu ya JKT Ruvu Pwani.
Kutolewa kwa mkopo kwa Zahor, mtoto wa kipa wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Iddi Pazi ‘Father’ kunafuatia kusajiliwa kwa wachezaji kadhaa wapya Azam katika dirisha dogo.
Miongoni mwa waliosajiliwa ni Humphrey Mieno, Joackins Atudo kutoka Kenya, Brian Umony kutoka Uganda na David Mwantika kutoka Prisons ya Mbeya.
Zahor licha ya kuwa mchezaji mzuri amekuwa hana bahati ndani ya kikosi chs Azam tangu asajiliwe msimu uliopita.
Mwanzoni mwa msimu, Zahor aliomba kwenda kucheza kwa mkopo Coastal Union ya Tanga, lakini uongozi wa klabu hiyo ukamkatalia.
Katika hatua nyingine, kiungo Abdulhalim Humud aliyekuwa majeruhi tangu Novemba mwaka jana, amejiunga na kikosi cha timu hiyo kilichopo Zanzibar kwenye Kombe la Mapinduzi.
Humud ambaye mashabiki wake humuita Gaucho, wakimfananisha na Mwanasoka Bora wa Zamani wa Dunia, Mbrazil Ronaldinho Gaucho aliwasili Zanzibar jana, ingawa haijulikani kama atashiriki hatua iliyobaki ya Kombe la Mapinduzu au la.
Azam jana iliingia Fainali ya Kombe la Mapinduzi, baada ya kuifunga Simba SC kwa penalti 5-4, kufuatia sare ya kufungana mabao 2-2 ndani ya dakika 120 usiku huu kwenye Uwanja wa Amaan, visiwani hapa.
Hadi mapumziko, Azam FC walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililotiwa kimiani na kiungo Mkenya, Humphrey Mieno dakika ya 10, akiunganisha kwa kichwa kona maridadi iliyochongwa na kiungo mzalendo, Ibrahim Mwaipopo.
Azam ilishambulia zaidi baada ya bao hilo, kabla ya Simba kuzinduka dakika tatu baadaye na kuanza kushambulia pia.
Mchezo huo ulisimama kwa dakika tano kuanzia ya 14 hadi 19 kutokana na umeme kukatika uwanjani hapo, hali iliyolazimisha kuwashwa kwa Jenereta.
Kipindi cha pili Simba walibadilika mno kiuchezaji na kuanza kutawala mchezo jambo ambalo liliwasaidia kupata bao la kusawazisha dakika ya 78, ambalo lilifungwa na Rashid Ismail.
Simba ilipoteza nafasi mbili za wazi za kufunga mabao ndani ya dakika 45 za kipindi cha pili na mchezo ukamalizika timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1.
Katika dakika 30 za nyongeza, Simba walifanikiwa kupata bao lililoelekea kuwa la ushindi dakika ya 110, mfungaji Miraj Madenge.
Azam walionekana kupagawa baada ya kupigwa bao la pili na kuanza kucheza rafu za ovyo na kutoa maneno machafu kwa refa, jambo ambalo liliwaponza kupoteza wachezaji wawili ndani ya dakika mbili.
Refa Waziri Shekha alianza kumtoa nje kwa kadi nyekundu kiungo Mwaipopo dakika ya 114 na baadaye Jabir Aziz dakika ya 116. 
Wakati refa huyo akijiandaa kupuliza kipyenga cha kuhitimisha mchezo na mashabiki wa Simba wakiwa wameuteka Uwanja wa Amaan kwa shangwe zao, beki Emily Mgeta alimuangusha kwenye eneo la hatari beki Malika Ndeule na hivyo kuwa adhabu ya penalti.
Beki Mkenya, Joackins Atudo ambaye amekuwa akipewa dhamana ya kupiga penalti kwa sasa Azam FC, alikwenda kupiga mkwaju huo na kuukwamisha nyavuni kuwapatia Watoto wa Bakhresa bao la kusawazisha.
Kutoka hapo, mchezo ulihamia kwenye mikwaju ya penalti na usiku huo bahati haikuwa yake kiungo matata chipukizi wa Simba, Haroun Athumani Chanongo, kwani pamoja na kupiga penalti nzuri iliyokuwa ya pili kwa timu yake, iligonga mwamba wa juu katikati na kudunda chini kisha kurejea uwanjani.
Wachezaji wa Simba waliofunga penalti zao jana ni Komabil Keita ya kwanza, Jonas Mkude ya tatu, Miraj Adam ya nne na Ramadhani Mkiparamoto ya tano, wakati wa Azam waliofunga ni Gaudence Mwaikimba ya kwanza, Himid Mao ya pili, Atudo ya tatu, Samir Hajji Nuhu ya nne na Malika Ndeule ya tano.
Kwa matokeo hayo sasa, Azam itamenyana na mshindi wa mechi ya leo kati ya Tusker na Miembeni katika fainali Jumamosi.

BAADA YA JANA MNYAMA KUSHINDWA KUUNGURUMA VISIWANI LEO NI TUSKER NA MIEMBENI KATIKA UWANJA WA AMAAN NUSU FAINALI YA PILI


Monja Liseki wa Miembeni
TUSKER FC inashuka dimbani leo usiku kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar kumenyana na Miembeni katika Nusu Fainali ya pili ya Kombe la Mapinduzi.
Mchezo huo, unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua, kwani kwa sasa Miembeni ndiyo timu inayoiwakilisha vema Zanzibar katika mashindano haya na inaungwa mkono na Wazanzibari wengi.
Kocha wa Miembeni Salum Bausi amesema hawahofii Tusker na leo atawaonyesha kwamba mpira ni zaidi yua nguvu 
Nahodha wa Tusker, Joseph Shikokoti amesema kwamba haoni timu ya kuwazuia kutwaa Kombe la Mapinduzi.
Shikokoti aliyewahi kuchezea Yanga alisema kwamba anafahamu Azam ni wazuri na  watakutana nayo fainali, lakini hawawezi kuwazuia wasitwae Kombe.
“Hili Kombe letu, tumeona uwezo wa Azam ni wazuri, lakini tutawafunga tukikutana nao, hawana uwezo wa kutuzuia,”alisema Shikokoti.
Katika Nusu Fainali ya kwanza jana,Azam iliitoa Simba SC kwa penalti 5-4 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 120

BAADA YA KUFUNGWA NA DENIZLISPOR FC YANGA WAENDELEA KUJIFUA ULAYA


Tmu ya  Young Africans leo asubuhi imeendelea na mazoezi katika viwanja vya Fame Residence baada ya jana kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Denizlispor FC ya ligi daraja la kwanza Uturuki, mchezo ambao ulishia kwa Denizlispor FC kushinda kwa mabao 2-1, mechi liofanyika katika uwanja wa Selen football - Kamelya Complex Antalya.

Kocha Brandts ameendelea kukinoa kikosi chake na kufanyia marekebisho ya baadhi ya makosa yaliyojitokeza katika mchezo wa jana ambao hata hivyo Yanga iliutawala kwa kipindi chote cha mchezo lakini maamuzi ya mwamuzi kipindi cha pili yaliinyima Young Africans ushindi.
Denizlispor FC timu ambayo imeshuka kutoka ligi kuu ya uturki mwaka juzi, inapigania kurudi tena katika Ligi kuuya Uturuki, jana ilishindwa kutamba kabisa mebele ya Young Africans ambayo iliweza kucheza soka safi na la kuvutia mda wote wa mchezo.
Brandts amemtupia lawama mwamuzi wa mchezo jana, kwamba maamuzi yake ndio yalipelekea timu yake kupoteza mchezo huo, kwani vijana wake waliweza kucheza vizuri kuanzia nafasi ya ulinzi mpaka ushambuliaji hali iliyowashangaza waturuki hao.
Tazama goli la kwanza mshambuliaji wao aliunawa mpira kabla ya kufunga na bado mwamuzi akalikubali bao alilofunga, bao la pili Nadri Cannavaro alichezwa mazdhambi mshika kibendera akanyanyua kuwa ni faulo lakini cha ajabu mwamuzi aliamuru ipigwe penati, kiukweli mwamuzi alichangia kutufanya tupoteze mchezo huo alisema 'Brandts'
Wachezaji wanaendelea na mazoezi mpaka siku ya jumamosi ambayo itakua ni siku ya mwisho kabla ya siku ya jumapili kuanza safari ya kurudi nchini Tanzania tayari kabisa kwa mbio za kuuchukua Uibingwa wa Ligi ya Kuu ya Vodacom 2013. 

Wachezaji wa Young Africans wakiwa mazoezin leo asubuhi katika viwanja vya Fame Residence football

Young Africans imeendelea na mazoezi yake leo asubuhi katika viwanja vya Fame Residence Football ambapo imekuwa ikifanya mazoezi tangu kuwasili katika mjii wa Antalya.

MNYAMA AENDA OMAN AKIKUMBUKIA ICECREAM ZA AZAM KULAMBISHWA JANA NA AZAM NA KUTINGA FAINALI MAPINDUZI


Wachezaji wa Azam wakiwa wamembeba shujaa wao wa leo Malika Ndeule
AZAM FC imeingia Fainali ya Kombe la Mapinduzi usiku huu, baada ya kuifunga Simba SC kwa penalti 5-4, kufuatia sare ya kufungana mabao 2-2 ndani ya dakika 120 usiku huu kwenye Uwanja wa Amaan, visiwani hapa.
Hadi mapumziko, Azam FC walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililotiwa kimiani na kiungo Mkenya, Humphrey Mieno dakika ya 10, akiunganisha kwa kichwa kona maridadi iliyochongwa na kiungo mzalendo, Ibrahim Mwaipopo.
Azam ilishambulia zaidi baada ya bao hilo, kabla ya Simba kuzinduka dakika tatu baadaye na kuanza kushambulia pia.
Mchezo huo ulisimama kwa dakika tano kuanzia ya 14 hadi 19 kutokana na umeme kukatika uwanjani hapo, hali iliyolazimisha kuwashwa kwa Jenereta.
Kipindi cha pili Simba walibadilika mno kiuchezaji na kuanza kutawala mchezo jambo ambalo liliwasaidia kupata bao la kusawazisha dakika ya 78, ambalo lilifungwa na Rashid Ismail.
Simba ilipoteza nafasi mbili za wazi za kufunga mabao ndani ya dakika 45 za kipindi cha pili na mchezo ukamalizika timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1.
Katika dakika 30 za nyongeza, Simba walifanikiwa kupata bao lililoelekea kuwa la ushindi dakika ya 110, mfungaji Miraj Madenge.
Azam walionekana kupagawa baada ya kupigwa bao la pili na kuanza kucheza rafu za ovyo na kutoa maneno machafu kwa refa, jambo ambalo liliwaponza kupoteza wachezaji wawili ndani ya dakika mbili.
Refa Waziri Shekha alianza kumtoa nje kwa kadi nyekundu kiungo Mwaipopo dakika ya 114 na baadaye Jabir Aziz dakika ya 116.  
Wakati refa huyo akijiandaa kupuliza kipyenga cha kuhitimisha mchezo na mashabiki wa Simba wakiwa wameuteka Uwanja wa Amaan kwa shangwe zao, beki Emily Mgeta alimuangusha kwenye eneo la hatari beki Malika Ndeule na hivyo kuwa adhabu ya penalti.
Malika amebebwa juu juu
Beki Mkenya, Joackins Atudo ambaye amekuwa akipewa dhamana ya kupiga penalti kwa sasa Azam FC, alikwenda kupiga mkwaju huo na kuukwamisha nyavuni kuwapatia Watoto wa Bakhresa bao la kusawazisha.
Kutoka hapo, mchezo ulihamia kwenye mikwaju ya penalti na usiku huu bahati haikuwa yake kiungo matata chipukizi wa Simba, Haroun Athumani Chanongo, kwani pamoja na kupiga penalti nzuri iliyokuwa ya pili kwa timu yake, iligonga mwamba wa juu katikati na kudunda chini kisha kurejea uwanjani.
Wachezaji wa Simba waliofunga penalti zao leo ni Komabil Keita ya kwanza, Jonas Mkude ya tatu, Miraj Adam ya nne na Ramadhani Mkiparamoto ya tano, wakati wa Azam waliofunga ni Gaudence Mwaikimba ya kwanza, Himid Mao ya pili, Atudo ya tatu, Samir Hajji Nuhu ya nne na Malika Ndeule ya tano.
Kwa matokeo hayo sasa, Azam itamenyana na mshindi wa kesho kati ya Tusker na Miembeni katika fainali Jumamosi.
Katika mchezo huo, kikosi cha Simba SC kilikuwa; William Mweta, Miraj Adam, Paul Ngalema, Hassan Khatibu/Hassan Isihaka dk89, Komabil Keita, Jonas Mkude, Ramadhani Singano/Miraj Madenge dk71, Abdallah Seseme/Said Demla dk 61, Rashid Ismail, Marcel Kaheza/Ramadhan Mkipalamoto dk72 na Haroun Chanongo.
Azam FC; Mwadini Ally, Himid Mao, Samir Hajji Nuhu, David Mwantika, Joackins Atudo, Kipre Balou, Seif Abdallah/Gaudence Mwaikimba dk69, Ibrahim Mwaipopo, Brian Umony/Malika Ndeule dk104, Humphrey Mieno/Jabir Aziz dk79 na Uhuru Suleiman.