Monday, November 12, 2012


 POLISI MARA YAZINDUKA, RHINO MWENDO MDUNDO, MAJIMAJI YABANWA NYUMBANI
 TIMU ya Polisi Mara jana  ilizinduka usingizi na kuifunga wachovu wa kundi C Morani ya Manyara mabao 3-1 kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Karume, mkoani Mara.


Mabao ya Polisi yalifungwa na Daniel Mayeye dakika ya 13, Yohana Mirobo dakika ya 29 na Hamis Hamza dakika ya 68 na bao la Morani lilifungwa na Amiry  Msuwa dakika ya 76.

Michezo mingine iliyochezwa kwenye kundi C ni kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, ambapo Polisi Tabora walitoka sare ya 0-0 na Mwadui ya Shinyanga

Uwanja wa Lake Tanganika Kigoma Kanembwa ilishindwa kuutumia uwanja wa nyumbani baada ya kutoka sare ya 0-0 na Pamba ya Mwanza.

Kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma, maafande wa Polisi Dodoma walishindwa kuhimili gwaride la maafande wa jeshi la wananchi RHINO RANGERS ya mkoani tabora  kwa kukubali kipigo cha mabao 2-0 mabao yaliyofungwa na Abubakary Omary na jingine lilifungwa na mshambuliaji mwenye nguvu,kasi na mashuti makali Abdalah simba katika dimba la jamhuri dodoma  nyumbani kwa timu ya polisi dodoma.

Kundi A uwanja wa Majimaji mjini Songea, Majimaji na Mlale zote za Ruvuma zilitoka sare ya bao 1-1

Bao la Majimaji lilifungwa na Edward Songo dakika ya 70 kwa kichwa na la Mlale lilifungwa na Chale Haule kwa penalti dakika ya 85.

 
Na ligi hiyo itaendelea tena tarehe 14 kwa michezo minne kati ya    ===kanembwa vs polisi mara
===pamba vs polisi tabora 
===mwadui vs polisi dodoma 
===moran vs rhino rangers
  MSIMAMO KUNDI C
1.RHINO RANGERS MECHI 6 POINTI 14
2.KANEMBWA JKT MECHI6 POINTI 13
3.MWADUI FC MECHI 6 POINTI 10
4.POLISI DODOMA MECHI  POINTI 8
5.PAMBA MECHI 6 POINTI 8
6.POLISI MARA MECHI 6 POINTI 5
7.POLISI TABORA MECHI 6 POINTI 3
8.MORAN FC MECHI 6 POINTI 2

FAHAMU;Kila kundi litatoa timu moja ambayo itapanda ligi kuu ya vodacom tanzania bara VPL msimu ujao na tayari timu ya maafande ya polisi moro imeonyeshwa mlango wa kutokea kwani imemaliza mzunguko wa kwanza wa  VPL ikiwa imecheza mechi 13 na ina pointi 4 inashika mkia.timu zitakazo panda ni kutoka kundi A,B,na C


 MATOKEO TOKA LIGI IANZE oktoba 24
===Kanembwa vspolisi dodoma 3-0
===pamba vs polisi mara 3-2
===rhino rangers vs polisi tabora 2-1
mwadui vs moran 3-0

oktoba 27
====polisi tabora vs polisi dodoma 0-1
====mwadui vs polisi mara 3-0
====kanembwa JKT vs moran 2-0
====pamba vs rhino rangers 1-1

oktoba 31
====polisi mara vs rhino rangers 0-0
====moran vs polisi tabora 1-1
====polisi dodoma vs pamba2-0
====kanembwa vs mwadui 3-2

novemba 4
===polisi mara vs polisi tabora 1-1
===moran vs polisi dodoma1-1
===rhino rangers vs kanembwa JKT 3-1
===mwadui vs pamba...2-0......
 
novemba 7
====polisi tabora vs kanembwa  JKT 1-4
====polisi dodoma vs polisi mara 0-0
====pamba vs moran ya manyara 2-0
 
novemba 8
====rhino rangers vs mwadui FC 2-0
 
novemba 11
====kanembwa vs pamba 0-0
====polisi tabora vs mwadui 0-0
====polisi dodoma vs rhino rangers 0-2
====polisi mara vs moran 3-1
 
na novemba 14
===kanembwa vs polisi mara
===pamba vs polisi tabora 
===mwadui vs polisi dodoma 
===moran vs rhino rangers

SERENGETI BOYS WAIGARAZA FALCON KWENYE MCHEZO WA KIRAFIKI

Beki wa Falcon ya Zanzibar Faki Hamad akiwa amemiliki mpira huku Dickson Ambundo wa Serengeti boys akiangalia jinsi ya kumnyang'anya wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa jana uwanja wa taifa, Serengeti boys ilishinda 2-1.


Mshambuliaji wa Serengeti boys Husein Twaha akipambana na Abassi Juma kwenye mchezo wa kirafiki uliocghezwa uwanja wa taifa jana na Serengeti kushinda bao 2-1.

TIMU ya Taifa ya Vijana waliochini ya miaka 17, "Serengeti boys" jana waliibuka kidedea baada ya kuifunga Falcon ya Zanzibar mabao 2-1 kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo ambao ulikuwa wa kusisimua kutokana na timu zote kutandaza kabumbu safi ulishuhudia timu zote kwenda mapumziko bila kufungana.

Kipindi cha pili kiianza kwa timu zote kufanya mabadiliko lakini Serengeti boys ndio waliweza kunufaika kwani dakika ya 74 walipata bao kupitia kwa Tumaini Baraka.

Baada ya kupata bao hilo Serengeti boys walizidisha mashambulizi na walionyesha wana kiu ya kutafuta mabao zaidi na  dakika ya 82 mshambuliaji Farid Musa alifunga bao kwa shuti la mbali baada ya kumwona golikipa wa Falcon ametoka golini.

Katika kuhakikisha hawatoki uwanjani bila bao wachezaji wa Falcon walifanya shambulizi moja na nahodha wa Serengeti boys Miraji Adam akijifunga wakati akiokoa.

Kocha wa Falcon, Mohamed Mzee alisifu kikosi chake kwa mchezo ila alisema viungo walishindwa kukaa na mpira hali iliyofanya Serengeti boys kutumia nafasi hiyo kuwashambulia.

"Timu imejitahidi kucheza vizuri kwani tumecheza na timu yenye wachezari bora, ila viungo walishindwa kukaa na mpira na kusababisha tushambuliwe", alisema Mzee.

Jakob Michelsen alikipongeza kikosi chake kwa kucheza vizuri kwani wamecheza na timu nzuri

ARUSHA BINGWA SLAM SPRITE

Mabingwa kikapu, timu ya mkoa wa Arusha wakikabidhiwa zawadi ya kombe na Katibu Mkuu wa Shirikisho la mpira wa kikapu (TBF) Michael Maluwe, kwenye uwanja wa ndani wa taifa jana baada ya kuifunga Dodoma vikapu 11 kwa 8.

Mabingwa wa kikapu wa timu ya mkoa wa Dodoma (wachezaji 3+3) wakikabidhiwa zawadi ya ngao na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa kikapu (TBF) Michael Maluwe, kwenye uwanja wa ndani wa taifa janabaada ya kuifunga Arusha vikapu 10 kwa 5



TIMU ya kikapu ya mkoa wa Arusha jana  iliibuka ubingwa wa Slam Sprite baada ya kuifunga Dodoma kwa vikapu 11 kwa 8.

Mashindano hayo ambayo yalianza kuchezwa mikoani yameweza kuibua vipaji vingi ambavyo vitakuwa tunu kwa taifa.


Awali akizungumza, Katibu wa Shirikisho wa Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Michael Maluwe, aliishukuru Kampuni ya Cocala kupitia kinywaji chake cha Sprite kwa kufanikisha mashindano.

Maluwe alisema kupitia kampuni hiyo wameweza kuona nyota ambao watalisaidia taifa kwenye mashindano mbalimbali ndani na nje ya nchi.

"Makampuni mengine yaige mfano kwa Copa Cocala ili kuinua michezo Tanzania", alisema.

Arusha iliibuka bingwa kwenye mchezo wa wachezaji watano na kupewa kombe, fulana na kofia huku Dodoma wao wakiondoka na Ipod kila mchezaji,fulana na kofia.

Kwenye mchezo wa wachezaji watatu kila timu Dodoma iliifunga Arusha vikapu 10 kwa 5 na kufanikiwa kutwaa ngao, fulana na kofia na Arusha kila mchezaji kuondoka na ipod, kofia na fulana.

Kwa upande wa street dancing mkoa wa Kilimanjaron walishinda na kupewa ngao.

Mikoa ambayo ilishiriki katika mashindano hayo ni Arusha, Dodoma, Kilimanjaro, Mwanza, Mbeya pamoja na Dar Es Salaam.

Mkoa wa Dar es salaam hakuweza kufurukuta kwani uliondolewa kwenye makundi kwa kufungwa na Kilimanjaro vikapu 15 kwa 11 na baadae kupotea kabisa baada ya kufungwa na Dodoma vikapu 28 kwa 12.

 

DIDIER KAVUMBANGU MTAMBO MPYA WA MABAO JANGWANI ULIOFUNIKA MASTRAIKA WOTE LIGI KUU MZUNGUKO WA KWANZA



WAKATI mwingine ipo haja ya kukubali ushauri wa kitaalamu, kuwaachia walimu wafanya usajili. Bila shaka katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame Julai mwaka huu Dar es Salaam, Didier Kvumbangu pamoja na kuwafunga Yanga akiwa Atletico ya Burundi jina lake halikuvuma sana kwa sababu hata timu yake haikufanya vizuri sana.  
Kavumbangu aliwafunga Yanga mabao mawili, wakilala 2-0 katika mchezo wa kwanza wa makundi wa Kagame na zaidi ya hapo, Yanga haikufungwa tena hadi inachukua ubingwa.
Lakini mabao ya Didier hayakuchukuliwa kama yalitokana na umahiri wa ufungaji, hapana- bali yalichukuliwa kama ya bahati na pia kuikuta timu hiyo ikiwa haiko sawa kutokana na kuundwa na wachezaji wengi wapya.
Hata hivyo, mwisho wa msimu Yanga ilipoona inahitaji kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji, viongozi waliomba kocha wa timu yao wakati huo, Tom Saintfiet awapendekezee jina la mchezaji kutokana na michuano hiyo ya Kagame.
Mtakatifu Tom aliwashangaza sana viongozi wa Yanga kwa kuwatajia mchezaji aliyewafunga mabao mawili katika mechi ya kwanza, wakati kuna wachezaji wengine wanang’ara kutoka klabu za AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), APR ya Rwanda na nyinginezo.
Uzuri tu viongozi wa Yanga walikubaliana na ombi la kocha huyo Mbelgiji na wakamleta mshambuliaji huyo Dar es Salaam. Awali, kidogo ulitaka kuanza kujitokeza wasiwasi juu ya mchezaji huyo kutokana na kuchelewa kuanza kufunga mabao, hadi minong’ono ikaanza labda jamaa galasa.
Lakini leo unaposoma makala haya, Didier amekwishaifungia Yanga mabao 10 katika mechi 17 alizocheza, zikiwemo za kirafiki tatu za kirafiki.
Amefunga mabao nane kwenye Ligi Kuu, akiwa anamaliza mzunguko wa kwanza huku anaongoza na amemudu kujihakikishia namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha Yanga, mbele ya washambuliaji wengine mahiri kama Said Bahanuzi na Jerry Tegete.
Didier amewafunika washambuliaji wa kigeni wa timu nyingine pia, akiwemo Felix Mumba Sunzu Jr. kutoka Zambia, ambaye kwa sasa ndiye mchezaji ghali zaidi Tanzania akiwa analipwa Sh. Milioni 5 kwa mwezi.
Akiwa katika mwaka wa kwanza wa mkataba wake wa miaka miwili, dhahiri Kavumbangu sasa amewafanya viongozi wa Yanga wamtazame kwa jicho la tatu, kwani hiyo tayari ni lulu kwao. Kuna habari pia, ofa zimeanza kumiminika Jangwani, zikiwemo za klabu za Ulaya kwa ajili ya mchezaji huyo.
Pamoja na hayo, Kavumbangu, mshambuliaji mrefu, mwenye uwezo wa kumiliki mpira, kasi, nguvu, mbinu na maarifa, bado anahitaji muda kidogo japo kumalizia mzunguko wa pili Tanzania, ili kututhibitishia zaidi uwezo wake. Ila kwa sasa hakuna shaka kabisa kusema, amewafunika washambuliaji wote wa kigeni Tanzania akiwemo Sunzu, mchezaji ghali Tanzania.
Add caption



YANGA SC KUTOKA KUZIDIWA POINTI SABA HADI KUONGOZA LIGI KUU KWA POINTI SITA ZAIDI MZUNGUKO WA KWANZA

Yanga wamemaliza kileleni

MZUNGUKO wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, rasmi umemalizika jana ukiacha mechi mbili za viporo za Tanzania Prisons, dhidi ya Mgambo JKT na Ruvu Shooting.
Prisons walipata ajali wakiwa njiani kuelekea Tanga kwa ajili ya mechi yao na Mgambo JKT, hivyo mechi hiyo na ile iliyofuata dhidi ya Ruvu Shooting zikaahirishwa na kupangiwa tarehe nyingine, ili kuwapa wachezaji wake nafasi ya kupona majeruhi.
Mzunguko wa kwanza umemalizika na matokeo yamekuwa tofauti na mwelekeo wa ligi hiyo katika mzunguko huo, hadi katikati yake.
Yanga SC, ambayo haikutarajiwa kushika hata nafasi ya pili, ndiyo imemaliza kileleni kwa pointi zake 29, baada ya mechi hizo 13, ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 24 na Simba SC yenye pointi 23.
Presha ilikuwa upande wa mashabiki wa Yanga ndani ya mechi tano za mzunguko wa kwanza, kutokana na kuanza vibaya, kiasi cha kufikia kumfukuza kocha wake aliyewapa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, Mbelgiji, Tom Saintfiet.
Saintfiet alifukuzwa baada ya mechi mbili za Ligi Kuu, akitoa sare na Prisons mjini Mbeya na kufungwa mabao 3-0 na Mtibwa Sugar mjini Morogoro.
Azam nayo ilianza vema ikiwa nyuma ya Simba SC, lakini ilifukuza kocha wake Mserbia Boris Bunjak baada ya kufungwa mabao 3-1 na Wekundu hao wa Msimbazi.
Naam, Tanzania mechi moja au mbili za kufungwa zinatosha kumfukuzisha kocha na watu sasa wanasubiri hatua itakayochukuliwa na Simba dhidi ya kocha wake, Mserbia pia, Profesa Milovan Cirkovick baada ya klabu hiyo kufungwa mechi mbili mfululizo, 2-0 na Mtibwa Sugar  na 1-0 na Toto.
Tayari kundi la Friends Of Simba ambalo linasaidia sana uendeshwaji wa klabu hiyo limeripotiwa kushinikiza Milovan afukuzwe na Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage amesema Ijumaa wiki hii atachukua maamuzi magumu. Tusubiri.
Lakini tumeshuhudia timu mpya iliyopanda Ligi Kuu msimu huu, ambayo imeleta changamoto mpya, JKT Mgambo pamoja na kuimarika kwa Coastal Union, Kagera Sugar na Mtibwa Sugar, ambazo zinatoa upinzani katika ligi hiyo hata kwa vigogo.
Kwa kiasi kikubwa msimu huu tuna ligi tofauti na ya msimu uliopita na kama timu zitafanya maandalizi mazuri kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili, ni matarajio ya wengi Ligi Kuu itaisha vizuri zaidi.    
  
MSIMAMO WA LIGI KUU TANZANIA
Rnk
TeamMPWDLGFGA+/-Pts
1 Young Africans1392225101529
2 Azam137331711624
3 Simba SC136522011923
4 Mtibwa Sugar136431812622
5 Coastal Union136431614222
6 Kagera Sugar135621510521
7 Ruvu Shooting125251717017
8 JKT Ruvu134361320-715
9 Tanzania Prisons1135389-114
10 JKT Oljoro133551316-314
11 Mgambo JKT12426913-414
12 Toto African132651015-512
13 African Lyon13238920-119
14 Polisi Morogoro13049416-124
Yanga SC 2012
YANGA SC:
Wamemaliza mzunguko wa kwanza wakiwa kileleni mwa Ligi Kuu, wakiwa na pionti zao 26, baada ya kucheza mechi 13, kufungwa mbili dhidi ya Mtibwa Sugar 3-0 na Kagera Sugar 1-0, zote ugenini, kutoa sare mbili 1-1 dhidi ya Simba SC na 0-0 dhidi ya Prisons.
Yanga ambayo msimu uliopita ilishika nafasi ya tatu Ligi Kuu, ilipanda kileleni Novemba 4, baada ya kuifunga Azam FC mabao 2-0 na kuwashusha mabingwa watetezi, walioongoza ligi hiyo tangu mwanzoni.
Katikati ya mzunguko wa kwanza, Yanga ilifikia kuzidiwa pointi saba na Simba lakini Oktoba 31, ikafanikiwa kuwafikia Wekundu hao wa Msimbazi, siku hiyo wao wakiifunga Mgambo JKT 3-0 Dar es Salaam na wapinzani wao wakilazimishwa sare ya bila kufungana na Polisi Morogoro.    
                           P      W    D     L      GF   GA   GD  Pts
1      Yanga SC   13     9      2     2       25   10     15   29
KOCHA; Ernie Brandts (Uholanzi)
Azam FC 2012
AZAM FC:
Imemaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ikiwa katika nafasi ya pili, kwa pointi zake 24, ikiwazidi pointi moja tu mabingwa watetezi, Simba SC. Azam walikuwa na mwelekeo wa kumaliza katika nafasi nzuri zaidi kama si kufungwa mechi mbili mfululizo za mzunguko wa kwanza, dhidi ya Yanga 2-0 na Mgambo JKT 2-1.
Azam ilianza vema tu ligi hiyo, ikiwa nyuma ya Simba tangu mwanzo hadi Oktoba 31, ilipoenguliwa na Yanga katika nafasi ya pili. Ikielekea kwenye mechi yake ya mwisho dhidi ya Mgambo, Azam ilifukuza wachezaji wake wanne, Deo Munishi ‘Dida’, Erasto Nyoni, Said Mourad na Aggrey Morris kwa madai walipokea hongo waifungishe timu hiyo dhidi ya Simba na wanadai wana ushahidi hadi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU). Dhahiri kuondolewa kwa wachezaji hao tegemeo kikosini kulichangia matokeo ya kufungwa na Mgambo katika mechi ya mwisho.                     
                           P      W    D     L      GF   GA   GD  Pts
2      Azam FC     13     7     3      3      17     11    6     24
KOCHA: Stewart Hall (Uingereza)
Simba SC 2012
SIMBA SC:
Mabingwa hao watetezi, waliianza Ligi Kuu vema wakionyesha dalili zote za kutetea ubingwa wao kwa kufanikiwa kuwa kileleni hadi mwishoni mwa mzunguko huo, kabla ya mambo kugeuka ghafla.
Zilianza sare kwanza, 1-1 na Yanga, 0-0 na Coastal Union, 2-2 na Kagera Sugar na baadaye 0-0 na Mgambo, 0-0 na Polisi Morogoro kabla ya kufungwa mechi ya kwanza msimu huu, mbele ya Mtibwa Sugar na kumaliza mzunguko wa kwanza kwa kipigo cha 1-0 kutoka kwa Toto Africans.
Matokeo haya kwa kiasi kikubwa yameivuruga Simba SC na inasemekana Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ anafikiria kujiuzulu na baada ya kufungwa na Mtibwa Sugar, hakujihusisha na chochote juu ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Toto, wakati huo Mwenyekiti wake, Alhaj Ismail Aden Rage yuko bize na shughuli za kisiasa Dodoma. Rage anasema amekwishawajua wanaosababisha matokeo mabaya Simba na Ijumaa atatangaza maamuzi magumu. 
                                P      W    D     L      GF   GA   GD  Pts
3      Simba SC         13     6     5      2      20   11      9     23
KOCHA: Milovan Cirkovick (Serbia)
Mtibwa Sugar 2012
MTIBWA SUGAR:
Ilianza vizuri, katikati ikavurunda na mwishoni mwa mzunguko wa kwanza ikazinduka tena hatimaye imemaliza katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
Inaonekana Mtibwa Sugar inaanza kurejesha makali yake iliyoingia nayo katika soka ya Tanzania miaka ya 1990 hadi wakafanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi hiyo mara mbili mfululizo 1999 na 2000, wakiweka rekodi ya kuwa timu pekee nje ya Simba na Yanga kutetea taji hilo.
Hiyo si kwa sababu tu ipo nyuma ya Yanga, Azam na Simba, bali msimu huu imefanikiwa kuvifunga vigogo vyote vya soka nchini, Simba na Yanga. 
                                P      W    D     L      GF   GA   GD  Pts
4      Mtibwa Sugar   13     6     4      3      18    12     6     22
KOCHA: Mecky Mexime (Mzalendo)
Coastal Union 2012
COASTAL UNION:
Wana Mangushi wamerudi tena kwenye makali yao yaliyowafanya wakawa mabingwa wa ligi hiyo mwaka 1988, kwani hadi sasa wameonyesha upinzani wa kutosha kwenye Ligi Kuu. Wagosi hao wa Kaya wamemaliza katika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa pointi zao 22 sawa na Mtibwa walio nafasi ya nne, lakini wanazidiwa wastani tu wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Hata hivyo, Coastal walianza Ligi Kuu kwa kusuasua kiasi cha kufikia kuwafukuza makocha wake wa awali waliosajili na kuandaa timu kwa ajili ya ligi hiyo, Juma Mgunda na Habib Kondo ambao nafasi zao zilichukuliwa na Hemed Morcco na Ally Kiddy.
                                P      W    D     L      GF   GA   GD  Pts
5      Coastal Union  13     6      4     3       16   14      2     22
KOCHA: Hemed Morocco (Zanzibar)
Kagera Sugar 2012
KAGERA SUGAR:
Kagera Sugar wamemaliza katika nafasi ya sita wakiwa na pointi 21 na wangeweza kumaliza juu ya hapo, kama wangeutumia vizuri mchezo wao wa mwisho kwenye Uwanja wa nyumbani dhidi ya vibonde Polisi Morogoro.
Wakipewa nafasi kubwa ya kushinda, katika mastaajabu ya wengi, Kagera wakalazimishwa sare ya bila kufungana na Maafande hao wa Morogoro kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, hivyo kuwapa nafasi Coastal na Mtibwa kuendelea kuwa juu yao.
Kagera inajivunia kutofungwa na vigogo wa soka nchini, kwani waliifunga Yanga 1-0 na wakatoa sare ya 2-2 na Simba na Dar es Salaam.  
                                 P      W    D     L      GF   GA   GD  Pts
6      Kagera Sugar   13      5     6      2      15   10      5      21
KOCHA: Abdallah Athumani Seif ‘Kibadeni’ (Mzalendo)
Ruvu Shooting 2012
RUVU SHOOTING:
Katika timu zote za majeshi kwenye ligi hiyo, Ruvu Shooting ndio inaonekana kuwa imara zaidi na ndiyo maana ipo katika nafasi nzuri zaidi, ikiwa imebakiza mechi moja ya kiporo dhidi ya Prisons kumaliza mechi zake za mzunguko wa kwanza.
Ruvu ipo katikati ya msimamo wa ligi, nafasi ya saba kwa pointi zake 17 na inaweza kumaliza na pointi 20 iwapo itaifunga Prisons, lakini itaendelea kubaki kwenye nafasi hiyo hiyo, kwani Kagera Sugar waliopo juu ya wana pointi 21.
Timu hii inayotumia Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani ni moja kati ya timu zilizoonyesha kandanda safi ya kuvutia, tena ikiundwa na wachezaji wengi chipukizi, kama Seif Abdallah anayegombea kiatu cha dhahabu.  
                                 P      W    D     L      GF   GA   GD  Pts
7      Ruvu Shooting  12     5      2     5      17     17     0    17
KOCHA: Charles Boniface Mkwasa (Mzalendo)
JKT Ruvu 2012
JKT RUVU:
Imeshuhudiwa katika msimu mwingine, timu hii inazidi kupoteza makali yake, baada ya kumaliza katika nafasi ya nane mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu.
Siyo JKT ile ambayo ilikuwa tishio kwa vigogo, Simba na Yanga bali hii ya sasa ni ‘urojo’ na hali hii inatokea huku ikiwa inaundwa karibu na asilimia kubwa ya wachezaji wake wale wale, walioifanya iwe tishio misimu michache iliyopita, tena wakiwa chini ya kocha yule yule, kiungo wa zamani wa Yanga, Charles Killinda.
                            P      W    D     L      GF   GA   GD  Pts
8      JKT Ruvu     13     4     3      6      13     20    -7    15
KOCHA: Charles Kilinda (Mzalendo)
TZ Prisons 2012
TZ PRISONS:
Imerejea Ligi Kuu msimu huu na hadi sasa unaweza kusema inapambana kuhakikisha inabaki kwenye ligi hiyo msimu ujao. Prisons wana mechi mbili za viporo dhidi ya Mgambo JKT na Ruvu Shooting ambazo zote watacheza ugenini, lakini hadi sasa inashika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa ligi hiyo.
Timu hiyo iliahirishiwa mechi zake  baada ya kupata ajali, ikiwa inaelekea Tanga kumenyana na Mgambo na wachezaji wake sita wakaumia. Inaweza kupanda juu kiidogo iwapo itashinda mechi zake mbili zilizobaki.  
                        P      W    D     L      GF   GA   GD  Pts
9      Prisons     11     3     5      3      8      9      -1    14
KOCHA: Jumanne Charles (Mzalendo)
JKT Oljoro 2012
JKT OLJORO:
Haina makali yake iliyoingia nayo kwenye Ligi Kuu msimu uliopita yaliyowafanya wamalize mzunguko wa kwanza wakiwa kileleni. Msimu huu JKT Oljoro imemaliza katika nafasi ya 10 kwa pointi zake 24 na huwezi kusita kusema ipo kwenye hatari ya kushuka daraja hadi sasa.
Ina pointi 14, sawa na Toto Africans iliyo nafasi ya 11 na inabebwa juu kwa wastani wa bao moja tu katika mabao ya kufunga na kufungwa, huku ikiwa inaizidi kwa pointi mbili tu Africans Lyon iliyo nafasi ya 12- JKT Oljoro hakika imemaliza mzunguko wa kwanza katika eneo baya. 
                           P      W    D     L      GF   GA   GD  Pts
10   JKT Oljoro   13      3     5      5      13    16     -3    14
KOCHA: Mbwana Makatta (Mzalendo)
Mgambo JKT 2012
MGAMBO JKT:
Ligi Kuu ya Bara imepokea timu mpya tushio ambayo imeongeza ladha katika ligi hiyo. Hiyo si nyingine zaidi ya JKT Mgambo ua Handeni, Tanga inayotumia Uwanja wa Mkwakwani, Tanga pamoja na Coastal Union. Ikiwa na mechi moja ya kiporo mkononi dhidi ya Prisons, Mgambo ipo nafasi ya 11 kwa pointi zake 14 na kama ikifanikiwa kushinda mchezo huo, inaweza kupanda hadi nafasi ya saba, itategemea pia na matokeo ya mchezo mwingine wa kiporo kati ya Ruvu Shooting na Prisons. Mgambo walianza kwa kusuasua na watu wakaitabiria itashuka daraja, ila ilipokuja kuzinduka mwishoni mwa msimu, watu wamebadilisha kauli zao. 
                              P      W    D     L      GF   GA   GD  Pts
11   Mgambo JKT   12     4     2      6      9      13     -4    14
KOCHA: Mohamed Kampira (Mzalendo)
Toto Africans 2012
TOTO AFRICANS:
Wana Kishamapanda bado wapo katika wakati mgumu, kwani wamemaliza Ligi Kuu wakiwa katika nafasi ya 12, ambayo ni ndani ya nafasi tatu za kushuka Daraja.
Washukuru sana ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba SC kwenye mchezo wao wa mwisho wa mzunguko wa kwanza, kwani umewainua kidogo, vinginevyo wangemaliza ligi hiyo vibaya zaidi.
Lakini hii ni timu ambayo inacheza kwa ushindani zaidi inapokutana na timu tishio, ila kwa timu ambao zinaonekana si tishio, Toto hufanya vibaya. Bila shaka kuna kudharau mechi, ambako ndiko kunawaponza na kama watabadilika mzunguko wa pili, wanaweza kmufanya vizuri na kubaki Ligi Kuu. 
                                 P      W    D     L      GF   GA   GD  Pts
12   Toto Africans      13     2     6      5      10     15    -5    12
KOCHA: John Tegete (Mzalendo)
African Lyon 2012
AFRICAN LYON:
Hali bado ni tete African Lyon, ikiwa imemaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu katika nafasi ya 13 kwa pointi zalke tisa. Licha ya kunolewa na kocha Muargentina, Pablo Ignacio Velez, lakini Lyon wamekuwa vibonde tu hadi sasa.
Mmiliki wa timu hiyo, Rahim Kangezi ‘Zamunda’ amesema kwamba ametenga dau la dola za Kimarekani 200,000 kwa ajili ya kufanya usajili dirisha dogo ili kuimarisha kikosi na miongoni mwa wachezaji aliowalenga ni Emmanuel Okwi na Mrisho Ngassa wa Simba na Mbuyu Twite wa Yanga. Amesema kwa Twite atatoa dola 100,000, Ngassa dola 40,000 na Okwi dola 60,000. Tusubiri, ila hadi sasa hali tete Lyon.
                             P      W    D     L      GF   GA   GD  Pts
13   African Lyon   13     2     3      8       9      20    -11  9
KOCHA: Pablo Ignacio Velez (Argentina)
Polisi Morogoro 2012
POLISI MOROGORO:
Imerejea Ligi Kuu msimu huu, lakini haitakuwa ajabu mwishoni mwa msimu ikarudi tena kucheza Ligi Daraja la kwanza. Timu ya Morogoro, imemaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, ikiwa inashika mkia. Polisi haijashinda mechi hata moja zaidi ya kutoa sare nne na kufungwa mechi nyingine tisa.
Sijui maajabu gani yatokee, msimu ujao tuendelee kuwa na timu ya Morogoro, kwani kulingana na ushindani wa Ligi Kuu msimu huu, hakuna dalili za Polisi kupona.
                                 P      W    D     L      GF   GA   GD  Pts
14   Polisi Morogoro   13     0     4      9      4      16    -12   4
KOCHA: John Simkoko (Mzalendo)


CHALENJI CUP: Malawi yaibadili Djibouti kama Wageni waalikwa!

Wachezaji wa Taifa Stars walipocheza na Ghana majuzi
>>WENYEJI Uganda wateua Kikosi ndani OKWI & KIIZA!
CECAFA imeamua kuwachukua Malawi, badala ya Cameroun na Zimbabwe, kama Timu ya Wageni waalikwa kuibadili Djibouti katika michuano ya CECAFA Tusker CHALENJI Cup itakayoanza huko Nchini Uganda Novemba 24 na kumalizika Desemba 8.
Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye, amesema wameiteua Malawi kwa sababu katika Mashindano mawili ya CHALENJI CUP yaliyopita Nchi hii imeonyesha Soka safi na nidhamu ya hali ya juu.
Droo ya kupanga Ratiba za Mashindano hayo itafanyika Mjini Kampala, Uganda leo.
Nchi ambazo zitakuwemo kwenye Droo hiyo ni Tanzania, South Sudan, Ethiopia, Rwanda, Sudan, Burundi, Eritrea, Somalia, Zanzibar, Kenya, Malawi na Wenyeji Uganda.
Tayari Timu ya Somalia imeshawasili Nchini Uganda tangu Ijumaa iliyopita.
Wadhamini wa Mashindano haya ni East African Breweries ambao wametoa Dola 450,000 kuendesha michuano hiyo huku Mshindi akipata $30,000, Mshindi wa Pili $20,000 na wa Mshindi wa Tatu ni $10,000.
Uganda yateua Kikosi chake cha CHALENJI CUP
Wakati huo huo, Wenyeji wa CHALENJI CUP, Uganda, wametangaza Kikosi chao kwa ajili ya michuano hiyo na miongoni mwao ni Mastraika hatari wa Ligi Kuu Vodacom, VPL, Emmanuel Okwi wa Simba na Hamisi Kiiza wa Yanga.

KIKOSI KAMILI:

Rugby Cranes Uganda
A.Dhaira, A.Kimera, H.Muwonge, Y. Mugabi, N.Wadada, D.Guma, J.Owino, I.Isinde, E.Ssali, I.Bukenya, G. Walusimbi (captain), S.Namwanja, S.Bengo, M.Mutimba, J.Ochaya, R.Omunuk, S.Matovu, M.Oloya, G.Kizito, M.Kaweesa, J.Sadam, C.Ntambi, A.Feni, A.Gift, B.Umony, H.Kiiza, D.Sserunkukma, R.Ssentogo, J.Mpande, E.Okwi


TERRY AMUWEKA DI MATTEO ROHO JUU.

MENEJA wa klabu ya Chelsea, Roberto Di Matteo ameonyesha kutishwa baada ya beki John Terry kuumia mguu wakati kikosi chake kilipotoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Liverpool katika Uwanja wa Stamford Bridge.  
Terry ndiye aliyefunga bao la kuongoza la Chelsea katika mchezo huo wa jana kabla ya kubebwa katika machela kufuatia kugongana kwa bahati mbaya na Luis Suarez ambaye alifunga bao la kusawazisha katika kipindi cha pili.  
 
Nahodha huyo wa Chelsea ambaye alikuwa anacheza kwa mara ya kwanza akitoka kwenye adhabu ya kufungiwa michezo minne kutokana na kukutwa na hatia ya ubaguzi wa rangi anatarajiwa kufanyiwa vipimo zaidi baadae leo ili kuangalia ukumbwa wa tatizo lake.  
 
Di Matteo amesema kuwa anatarajia kuwa halitakuwa tatizo kubwa kwani bado wanamhitaji na alidhihirisha hilo kwa kiwango cha juu alichokionyesha kwenye mchezo huo kabla ya kutolewa baada ya kuumia.
 
 Kocha huyo pia amesema mshambuliaji nyota wa zamani wa klabu hiyo Didier Drogba ataruhusiwa kufanya mazoezi katika makao makuu yaliyopo Cobham kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Mataifa ya Afrika itakayofanyika Afrika Kusini, Januari mwakani. 

WENGER AMUWINDA DZEKO JANUARI.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amewaweka katika rada zake mshambuliaji wa Manchester City Edin Dzeko baada ya kuruhusiwa kuongeza nguvu katika kikosi chake katika kipindi cha dirisha dogo la usajili Januari mwakani. 

 Viongozi wa klabu hiyo wameamua kumpa fedha Wenger kutokana na klabu hiyo kuonyesha kusuasua kukaa katika nafasi nne za juu za msimamo wa Ligi kuu nchini Uingereza kitu ambacho kinaweza kuwakosesha kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

 Kocha huyo raia wa Ufaransa ametaja nafasi tatu zinazopwaya katika kikosi chake ambazo ni nafasi ya mshambuliaji wa pembeni na kati pamoja na golikipa.

 Mbali na Wenger kumuwinda Dzeko ambaye hana furaha City baada ya kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza lakini pia anawamulika washambuliaji wengine kama Fernando Llorente anayecheza katika klabu ya Athletic Bilbao na Adrian Lopez wa Atletico Madrid.

 Wenger pia ammtengea kitita cha paundi milioni tisa winga wa Crystal Palace Wilfried Zaha mwenye umri wa miaka 20 ingawa mwenyekiti wa klabu hiyo Steve Parish ameshatangaza kiasi cha paundi milioni 15 kwa klabu inayomhitaji mchezaji huyo.

Lionel Messi avunja Rekodi ya Pelé kwa Bao lake la 76 Mwaka huu!! 

>>ANAHITAJI Bao 10 Mwaka 2012 kuivunja Rekodi ya Gerd Muller!!

MESSI-REKODI_MAGOLILionel Messi ameipita Rekodi ya Pele ya kufunga Bbao nyingi katika Mwaka mmoja kwa kufunga Bao lake la 75 na 76 ugenini walipoitwanga Real Mallorca 4-2 hapo jana kwenye La Liga na anahitaji Bao 10 zaidi kuiua Rekodi ya Gerd Muller kwa Bao nyingi ndani ya Mwaka mmoja.
Mwaka 1958, Pele alifunga jumala ya Bao 75 akiichezea Nchi yake Brazil na Klabu yake Santos na Gerd Muller alifunga Bao 85 Mwaka 1972 akiichezea Nchi yake Ujerumani ya Magharibi na Klabu yake Bayern Munich.
Akiongelea rekodi hiyo, Meneja wa Barcelona, Tito Vilanova, alisema: “Rekodi za Leo ni za kustajabisha! Wachezaji wachache wanafikisha idadi hiyo ya Magoli katika Misimu 7 au 8 lakini yeye ni Msimu mmoja tu! Na mengi ya Mabao yake ni Mabao bora!”
LA LIGA:
Msimamo:
[Kila Timu Mechi 11]
1 Barcelona Pointi 31
2 Atletico Madrid 28
3 Real Madrid 23
4 Real Betis 19
5 Malaga 18
6 Levante 17
MATOKEO:
Jumamosi Novemba 10
Rayo Vallecano 3 Celta Vigo 2
Espanyol 0 Osasuna 3
Real Zaragoza 5 Deportivo La Coruna 3
Malaga 1 Real Sociedad 2
Jumapili Novemba 11
Real Valladolid 1 Valencia 1
Athletic Bilbao 2 Swvilla 1
Real Mallorca 2 Barcelona 4
Atletico Madrid 2 Getafa 0
Levante 1 Real Madrid 2
 

LIGI za ULAYA: Vinara Barca, Juve & Bayern ni ushindi tu!!


BARCA_v_REALLigi za Nchi Vigogo wa Ulaya, La Liga huko Spain, Serie A Nchini Italy na Bundesliga ya Ujerumani, ziliendelea Wikiendi na Timu zote zinazoshika hatamu, Barcelona, Juventus na Bayern Munich zimeibuka na ushindi.
Kwenye La Liga, Barcelona iliichapa Real Mallorca 4-2 kwa bao za Xavi, Messi, bao 2, na Tello.
Huko Serie A, Juventus iliifumua Pescara bao 6-1 na kwenye Bundesliga Bayern Munich iliichapa Eintracht Frankfurt 2-0.
LA LIGA:
Msimamo:
[Kila Timu Mechi 11]
1 Barcelona Pointi 31
2 Atletico Madrid 28
3 Real Madrid 23
4 Real Betis 19
5 Malaga 18
6 Levante 17
MATOKEO:
Jumamosi Novemba 10
Rayo Vallecano 3 Celta Vigo 2
Espanyol 0 Osasuna 3
Real Zaragoza 5 Deportivo La Coruna 3
Malaga 1 Real Sociedad 2
Jumapili Novemba 11
Real Valladolid 1 Valencia 1
Athletic Bilbao 2 Swvilla 1
Real Mallorca 2 Barcelona 4
Atletico Madrid 2 Getafa 0
Levante 1 Real Madrid 2
+++++++++++++++++++++++++
SERIE A:
MATOKEO:
Jumamosi Novemba 10
Cagliari o Catania 0
Pescara 1 Juventus 6
Jumapili Novemba 11
Palermo 2 Sampdoria 0
Genoa 2 Napoli 4
Chievo Verona 2 Udinese 2
AC Milan 1 Fiorentina 3
Torino 1 Bologna 0
Parma 0 Siena 0
Lazio 3 AS Roma 2
Atalanta 3 Inter Milan 2
Msimamo--Timu za juu tu:
[Kila Timu Mechi 12]
1 Juventus Pointi 31
2 Inter Milan 27
3 Napoli 26
4 Fiorentina 24
5 Lazio 22
+++++++++++++++++++++++++
BUNDESLIGA:
MATOKEO-Timu za juu tu:
Jumamosi Novemba 10
Freiburg 0 Hamburger 0
Schalke 2 Werder Bremen 1
Bayern Munich 2 Eintracht Frankfurt 0
Augsburg 1 Borussia Dortmund 3
Fortuna Dusseldorf 1 Hoffenheim 1
Jumapili Novemba 11
Wolfsburg 3 Bayer Leverkusen 1
SpVgg Gr. Furth 2 Borussia Monchengladbach 4
Stuttgart 2 Hannover 4
Msimamo-Timu za juu tu:
[Kila Timu Mechi 11]
1 Bayern Munich Pointi 30
2 Schalke 23
3 Eintracht Frankfurt 20
4 Borussia Dortmund 19
5 Bayer Leverkusen 18
6 Hannover 17
 

BPL: City yapanda nafasi ya 2, Chelsea yaporomoka hadi 3!!


BPL_LOGO+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO Timu za juu:
1 Man United Mechi 11 Pointi 27
2 Man City  Mechi 11 Pointi 25
3 Chelsea Mechi 11 Pointi 24
4 Everton Mechi 11 Pointi 20
5 WBA Mechi 11 Pointi 20
6 West Ham Mechi 11 Pointi 18
7 Tottenham Mechi 11 17
8 Arsenal Mechi 11 Pointi 16
+++++++++++++++++++++++
Chelsea 1 Liverpool 1
Nahodha John Terry akiichezea Mechi yake ya kwanza ya Ligi tangu afungiwe Mechi 4 aliifungia Chelsea bao moja lakini Liverpool walizinduka na kusawazisha kupitia Luis Suarez na Mechi kumalizika 1-1 na kuwafanya Chelsea waipishe Man City kwenye nafasi ya pili wakiwa nyuma ya vinara Manchester United.
VIKOSI:
Chelsea: Cech, Azpilicueta, Terry, Ivanovic, Bertrand, Mikel, Ramires, Hazard, Oscar, Mata, Torres
Akiba: Turnbull, Romeu, Moses, Ferreira, Marin, Sturridge, Cahill.
Liverpool: Jones, Wisdom, Carragher, Agger, Johnson, Allen, Gerrard, Sterling, Sahin, Jose Enrique, Suarez
Akiba: Gulacsi, Cole, Assaidi, Henderson, Coates, Downing, Fernandez Saez.
Refa: Howard Webb
Newcastle 0 West Ham 1
Nahodha wa West Ham Kevin Nolan alifunga bao pekee la Mechi hii na kuwapa West Ham ushindi wa bao 1-0 walipocheza na Newcastle.
VIKOSI:
Newcastle: Krul, Simpson, Steven Taylor, Williamson, Santon, Ben Arfa, Cabaye, Gutierrez, Ferguson, Cisse, Ba
Akiba: Elliot, Anita, Amalfitano, Bigirimana, Marveaux, Shola Ameobi, Obertan.
West Ham: Jaaskelainen, O'Brien, Reid, Tomkins, McCartney, Benayoun, Diame, Noble, Jarvis, Nolan, Carroll
Akiba: Spiegel, Cole, Maiga, Collins, Demel, O'Neil, Hall.
Refa: Mike Dean
Man City 2 Spurs 1
Mchezaji alietokea benchi, Eden Dzeko, kwa mara nyingine amewapa ushindi Mabingwa watetezi Manchester City kwa kufunga bao la pili na la ushindi katika Dakika ya 88 walipoifunga Tottenham bao 2-1 baada ya kutanguliwa bao 1.
Bao la Suprs lilifungwa na Caulker na Aguero akaisawazishia City,
VIKOSI:
Manchester City: Hart, Zabaleta, Kompany, Nastasic, Clichy, Toure, Barry, Silva, Tevez, Kolarov, Aguero. 
Akiba: Pantilimon, Maicon, Dzeko, Sinclair, Javi Garcia, Toure, Razak.
Tottenham Hotspur: Friedel, Walker, Gallas, Caulker, Vertonghen, Sandro, Huddlestone, Lennon, Bale, Dempsey, Adebayor. 
Akiba: Lloris, Naughton, Defoe, Dawson, Sigurdsson, Livermore, Carroll.
Refa: Michael Oliver
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumamosi, Novemba 17, 2012
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Arsenal v Tottenham Hotspur
[SAA 12 Jioni]
Liverpool v Wigan Athletic
Manchester City v Aston Villa
Newcastle United v Swansea City
Queens Park Rangers v Southampton
Reading v Everton
West Bromwich Albion v Chelsea
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Norwich City v Manchester United 

 

MAN UNITED: WAFALME KUPINDUA MATOKEO!!


>>MARA 8 Msimu huu wamegeuza KIPIGO kuwa CHEREKO!!
>>FERGIE & CHICHARITO wadai ni HETITRIKI dhidi ya Villa!!
CHICHARITO_SCORES_AGAINST_VILLAJavier Hernandez, maarufu kama Chicharito, amesema uwezo wa Manchester United kuipindua Mechi ambayo wametanguliwa kufungwa na hatimaye wao kuibuka washindi inatokana na Timu kujiamini na kutokata tamaa kitu ambacho wanakipata toka kwa Meneja wao Sir Alex Ferguson ambae anajiamini na Siku zote hakati tamaa.
Msimu huu, ni mara ya 8 kwa Man United kutanguliwa kufungwa lakini mwishoni wao ndio wanaibuka kidedea.
Jumamosi, wakicheza huko Villa Park, Man United walitanguliwa Bao 2-0 na Chicharito, alieingizwa Kipindi cha Pili, aliibuka shujaa kwa kutandika bao zote 3 ingawa bao lake la pili kuna Watu wanaosema ni la kujifunga mwenyewe Beki wa Villa Ron Vlaara kitu ambaco kimepingwa na Chicharito na Sir Alex Ferguson.
+++++++++++++++++++++++++++++
MATOKEO YALIYOPINDULIWA MSIMU HUU:
-Agosti 25: Walitoka 1-0 nyuma na kuifunga Fulham 3-2
-Septemba 2: Walitoka 0-1 na 1-2 nyuma na kuifunga Southampton 3-2
-Septemba 23: Walitoka 1-0 nyuma na kuifunga Liverpool 2-1
-Oktoba 2: Walitoka 1-0 nyuma na kuifunga Cluj 2-1
- Oktoba 20: Walitoka 1-0 nyuma na kuifunga Stoke 4-2
- Oktoba 23: Walitoka 2-0 nyuma na kuifunga Braga 3-2
-Novemba 7: Walitoka 1-0 nyuma na kuifunga Braga 3-1
-Novemba 10: Walitoka 2-0 nyuma na kuifunga Aston Villa 3-2
+++++++++++++++++++++++++++++
Chicharito amesema: “Hatukati tamaa katika historia ya Man United na hili limedhihirishwa mara kadhaa na Bosi [Sir Alex Ferguson] na Manguli wengine wa Klabu hii!”
Chicharito aliongeza: “Lazima nitadai ni Hetitriki kwani nilipiga shuti ambalo lililenga goli na yule Beki akajifunga!”
Sir Alex Ferguson amekubaliana na Chicharito na kusema hiyo ilikuwa ni Hetitriki.
RATIBA MECHI ZIJAZO za Man United:
Novemba
17 Nov  [LIGI KUU ENGLAND]
Norwich City v Man United
20 Nov  [UEFA CHAMPIONZ LIGI]
Galatasaray v Man United
24 Nov  [LIGI KUU ENGLAND]
Man United v Queens Park Rangers
28 Nov  [LIGI KUU ENGLAND]
Man United v West Ham
Desemba
01 Dec  [LIGI KUU ENGLAND]
Reading v Man United
05 Dec  [UEFA CHAMPIONZ LIGI]
Man United v CFR Cluj
09 Dec  [LIGI KUU ENGLAND]
Manchester City v Man United
15 Dec  [LIGI KUU ENGLAND]
Man United v Sunderland
23 Dec  [LIGI KUU ENGLAND]
Swansea City v Man United
26 Dec  [LIGI KUU ENGLAND]
Man United v Newcastle United
29 Dec  [LIGI KUU ENGLAND]
Man United v West Bromwich Albion
Januari 2013
01 Jan  [LIGI KUU ENGLAND]
Wigan Athletic v Man United

ROGER FEDERER AFIKA FAINALI YA ATP WORLD TOUR

Roger Federer fans leave home favourite Andy Murray feeling unloved during ATP World Tour Finals contest
Katika tenisi mchezaji namba mbili kwa ubora wa tenesi duniani ,Roger Federer atacheza fainali ya tenesi ya ATP WORLD TOUR dhidi ya mchezaji namba moja kwa ubora wa tenesi dunia Novak Djokovic.
Federer ametinga hatua ya fainali ya michuano hiyo baada ya kumfunga Andy Murray kwa seti mbili kwa bila kwa ushindi wa 7-6 na 6-2.
 
Naye Novak Djokovic amepigana kutoka nyuma kwa seti moja na kufanikiwa kumchapa Juan Mart -del Potro kwa 4-6 6-3 6-2 na kutinga katika hatua ya fainali.
Fainali ya hiyo ya ATP WORLD TOUR kwa magwiji hao wa mchezo wa tenesi, FEDERER na Djokovic inatazamiwa kupigwa leo.

Roger Federer  Current tournament:Barclays ATP World Tour Finals (Men's Singles)


1
N. Djokovic

Finals
2
R. Federer

Nov 12, 11:00 PM

2
R. Federer
77
6

Semifinals
3
A. Murray
65
2

Nov 11, Completed

2
R. Federer
63
6
3
Round Robin
6
J. del Potro
77
4
6
Nov 10, Completed

2
R. Federer
6
77

Round Robin
4
D. Ferrer
4
65

Nov 8, Completed