Saturday, February 2, 2013

AFCON 2013: GHANA YATINGA NUSU FAINALI!


>>NUSU FAINALI KUCHEZA NA MSHINDI KATI YA BUKINA FASO v TOGO!
AFCON_2013-NA_KABUMBU_LIANZEGHANA leo wametinga Nusu Fainali ya Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2013, kwa kuipiga Cape Verde Bao 2-0 na Bao zote kufungwa na Mubarak Wakaso.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++
ROBO FAINALI
Jumamosi Februari 2
Ghana 2 Cape Verde 0
[SAA 3.30 Moses Mabhida Stadium, Durban]
Afrika Kusini v Mali
Jumapili Februari 3
[SAA 12 Jioni Royal Bafokeng Stadium, Rustenburg]
Ivory Coast v Nigeria
[SAA 3.30 Mbombela Stadium, Nelspruit]
Burkina Faso v Togo
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Kwenye Nusu Fainali Ghana watacheza na Mshindi kati ya Burkina Faso na Togo.
Bao la kwanza la Ghana lilifungwa kwa Penati ya Dakika 54 baada ya Asamoah Gyan kuchezewa Rafu na Carlitos na la pili kupigwa Dakika ya 90 kwa Ghana kupiga kaunta ataki huku Kipa wa Cape Verde Vozinha akiwa Golini kwa Ghana akitaka kuicheza Kona iliyookolewa na Ghana.
Baadae leo, Robo Fainali ya pili itachezwa kati ya Wenyeji Afrika Kusini na Mali.
VIKOSI:
GHANA: F Dauda, J Pantsil, J Boye, I Vorsah, H Afful, M Rabiu (M), E Agyemang-Badu, A Adomah, K Asamoah, C Atsu, A Gyan
Akiba: D Agyei, R Boateng, M Awal, A Annan, D Boateng, J Akaminko, S Asante, E Clottey, R Boaky, J Mensah
CAPE VERDE: J Vozinha, S Nivaldo, F Varela 6 N Nando, T Carlitos, P Marco Soares, V Tony, E Babanco, R Nhuck, J Tavares, D Ryan Mendes
Akiba:T Fredson, N Stenio, O Guy Ramos, L Platini, R Ze Luis, L Josimar, A Gege, A Rony, P Pecks, J Djaniny
RATIBA:
NUSU FAINALI
Jumatano Februari 6
Ghana v Burkina Faso/Togo [Mbombela Stadium Saa 12 Jioni]
Afrika Kusini/Mali v Ivory Coast/Nigeria [Moses Mabhida Stadium Saa 3 na Nusu Usiku]
MSHINDI wa TATU
Jumamosi Februari 9
[Nelson Mandela Bay Stadium Saa 3 Usiku]
FAINALI
Jumapili Februari 10
[Soccer City, Johannesburg Saa 3 Usiku] 
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
AFCON 2013==AFRIKA KUSINI
VIWANJA:
-Soccer City, Johannesburg [Mashabiki 94,700]
-Moses Mabhida Stadium, Durban [Mashabiki 54,000]
-Nelson Mandela Bay Stadium, Port Elizabeth [Mashabiki 48,000]
-Mbombela Stadium, Nelspruit [Mashabiki 41,000]
-Royal Bafokeng Stadium, Rustenburg [Mashabiki 42,000]

BPL: Chelsea hoi Newcastle, Ba ahofiwa kuvunjwa Pua!!


BPL_LOGO>>PODOLSKI AIPA USHINDI ARSENAL!!
Arsenal, wakicheza kwao Emirates, waliibuka Washindi lakini Chelsea waliocheza St James Park wakiwa na Straika wa zamani wa Newcastle, Demba Ba, akirudi hapo kwa mara ya kwanza tangu ahame hivi majuzi na kulazimika kutolewa baada ya kula Buti ya puani na Beki Fabricio Coloccini, walichapwa Bao 3-2 na Newcastle ambayo Mchezaji wao mpya Moussa Sissoko alipiga Bao 2, moja likiwa la ushindi katika Dakika ya 90.
++++++++++++++++++++++
RATIBA/MATOKEO:
Jumamosi Februari 2
QPR 0 Norwich 0
Arsenal 1 Stoke 0
Everton 3 Aston Villa 3
Newcastle 3 Chelsea 2
Reading 2 Sunderland 1
West Ham 1 Swansea 0
Wigan 2 Southampton 2
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Fulham v Man United
++++++++++++++++++++++
WIGAN 2 SOUTHAMPTON 2
Bao la Dakika ya 90 la Maloney limewapa sare ya Bao 2-2 Wigan walipoivaa Southampton.
+++++++++++++++++++
MAGOLI:
Wigan 2
-Caldwelli Dakika ya 25
-Maloney 90
Southampton 2
-Lambert Dakika ya 64
-Schneiderlin 85
+++++++++++++++++++
VIKOSI:
Wigan: Al Habsi, Scharner, Caldwell, Figueroa, Stam, McCarthy, McArthur, Beausejour, Espinoza, Di Santo, Maloney
Akiba: Robles, Jones, Henriquez, Gomez, McManaman, Golobart, Campabadal.
Southampton: Boruc, Clyne, Yoshida, Hooiveld, Shaw, Schneiderlin, Cork, Puncheon, Ramirez, Rodriguez, Lambert
Akiba: Kelvin Davis, Steven Davis, Fox, Ward-Prowse, Lee, Lallana, Richardson.
Refa: Andre Marriner
WEST HAM 1 SWANSEA 0
Bao la Dakika ya 77 la Straika Andy Carrol, ambae amekuwa majeruhi kwa kipindi sasa na akicheza Mechi yake ya kwanza tangu Novemba, limewapa ushindi wa Bao 1-0 West Ham walipokuwa kwao kucheza na Swansea City.
VIKOSI:
West Ham: Jaaskelainen, O'Brien, Tomkins, Reid, Taylor, Noble, Diame, Vaz Te, Nolan, Jarvis, Carroll
Akiba: Spiegel, Carlton Cole, Collison, Pogatetz, Joe Cole, Chamakh, O'Neil.
Swansea: Tremmel, Rangel, Chico, Williams, Davies, de Guzman, Britton, Ki, Hernandez, Michu, Routledge
Akiba: Cornell, Dyer, Lamah, Monk, Shechter, Moore, Tiendalli.
Refa: Lee Probert
READING 2 SUNDERLAND 1
Jimmy Kebe leo alipiga Bao 2 na kuipa Reading ushindi wa Bao 2-1 dhidi ya Sunderland.
+++++++++++++++++++
MAGOLI:
Reading 2
-Kebe Dakika ya 7 & 85
Sunderland 1
-Gardner Dakika ya 29 [Penati]
+++++++++++++++++++
VIKOSI:
Reading: Federici, Kelly, Pearce, Mariappa, Harte, Kebe, Leigertwood, McAnuff, McCleary, Pogrebnyak, Akpan
Akiba: Stuart Taylor, Shorey, Karacan, Le Fondre, Morrison, Guthrie, Blackman.
Sunderland: Mignolet, N'Diaye, Bramble, O'Shea, Colback, Larsson, Gardner, Vaughan, Johnson, Fletcher, Sessegnon
Akiba: Westwood, Bardsley, Rose, Graham, Wickham, Mangane, McClean.
Refa: Lee Mason
NEWCASTLE 3 CHELSEA 2
Mchezaji mpya wa Newcastle, Moussa Sissoko, aliekuwa akicheza Mechi yake ya kwanza Uwanja wa Nyumbani St James Park, alifunga Bao mbili moja likiwa ndilo la ushindi katika Dakika ya 90 walipoichapa Chelsea Bao 3-2.
+++++++++++++++++++
MAGOLI:
Newcastle 3
-Guiterrez Dakika ya 41
-Sissoko 68 & 90
Chelsea 2
-Lampard Dakika ya 55
-Mata 61
+++++++++++++++++++
Mchezaji wa zamani wa Newcastle, Demba Ba headed, alirudi Uwanjani St James Park kwa mara ya kwanza lakini ilibidi atolewe baada ya kupigwa Buti ya uso na Beki wa Newcastle Fabricio Coloccini katika harakati za kuokoa.
VIKOSI:
Newcastle: Krul, Debuchy, Steven Taylor, Coloccini, Santon, Perch, Cabaye, Gouffran, Sissoko, Gutierrez, Cisse
Akiba: Elliot, Anita, Yanga-Mbiwa, Bigirimana, Marveaux, Obertan, Shola Ameobi.
Chelsea: Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Cole, Ramires, Lampard, Oscar, Mata, Bertrand, Ba
Akiba: Turnbull, Torres, Ferreira, Marin, Azpilicueta, Benayoun, Ake.
Refa: Howard Webb
EVERTON 3 ASTON VILLA 3
Marouane Fellaini aliiokoa Everton Uwanjani kwao Goodison Park aliposawazisha Bao katika Dakika ya 90.
+++++++++++++++++++
MAGOLI:
Everton 2
-Anichebe Dakika ya 21
-Fellaini 69 & 90
Aston Villa 3
-Benteke Dakika ya 2 & 61
-Agbonlahor 24
+++++++++++++++++++
VIKOSI:
Everton: Howard, Jagielka, Heitinga, Distin, Baines, Mirallas, Gibson, Osman, Pienaar, Fellaini, Anichebe
Akiba: Mucha, Jelavic, Oviedo, Naismith, Hitzlsperger, Neville, Duffy.
Aston Villa: Guzan, Lowton, Vlaar, Clark, Bennett, Westwood, El Ahmadi, Agbonlahor, N'Zogbia, Weimann, Benteke
Akiba: Given, Bent, Holman, Sylla, Bowery, Dawkins, Baker.
Refa: Mike Jones
ARSENAL 1 STOKE CITY 0
Lukas Podolski ameibuka Shujaa wa Emirates kwa kuifungia Arsenal Bao moja na la ushindi walipoitungua Stoke City Bao 1-0.
+++++++++++++++++++
MAGOLI:
Arsenal 1
-Podolski Dakika ya 78
Stoke City 0
+++++++++++++++++++
VIKOSI:
Arsenal: Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Diaby, Arteta, Wilshere, Oxlade-Chamberlain, Walcott, Giroud
Akiba: Mannone, Rosicky, Podolski, Andre Santos, Ramsey, Cazorla, Jenkinson.
Stoke: Begovic, Shotton, Shawcross, Huth, Wilkinson, Walters, Cameron, Nzonzi, Whelan, Etherington, Crouch
Akiba: Sorensen, Jones, Owen, Adam, Whitehead, Kightly, Jerome.
Refa: Chris Foy
QPR 0 NORWICH 0
Kipa wa Norwich City Mark Bunn aliokoa Penati ya Kipindi cha Pili iliyopigwa na Adel Taarabt na kuipa Timu yake Pointi 1 walipocheza ugenini na Timu ya mkiani QPR.
Pia Kipa wa QPR Julio Cesar aliokoa michomo kadhaa na kuifanya Timu yake iambue Pointi 1 tu licha ya kuitawala Mechi.
VIKOSI:
QPR: Julio Cesar, Da Silva, Samba, Hill, Traore, Wright-Phillips, Mbia, Derry, Townsend, Taarabt, Mackie
Akiba: Green, Park, Granero, Jenas, Ben Haim, Zamora, Bothroyd.
Norwich: Bunn, Martin, Bassong, Turner, Garrido, Snodgrass, Tettey, Johnson, Pilkington, Hoolahan, Holt
Akiba: Camp, Whittaker, Howson, Jackson, Elliott Bennett, Becchio, Barnett.
Refa: Jon Moss

KIIZA AINUSURU YANGA KUZAMA KWA MTIBWA


Kiiza akitoka eneo la lango la Mtibwa baada ya kufunga bao la kusawazisha, kulia Tegete akimpongeza


YANGA SC leo imepunguzwa kasi, baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Mtibwa Sugar ya Morogoro katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni hii.
Hadi mapumziko, Mtibwa walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililowekwa kimiani na kiungo wa zamani wa Simba SC, Shaaban Kisiga ‘Malone’ dakika ya 44.
Kisiga aliyewika pia SC Villa ya Uganda na Azam FC ya Dar es Salaam alifunga bao hilo akiunganisha kwa kichwa kona maridadi ya beki Issa Rashid ‘Baba Ubaya’.
Pamoja na kufungwa, Yanga ndio waliotawala zaidi kipindi cha kwanza na walikosa mabao matatu ya wazi, mawili kupitia kwa Didier Kavumbangu na moja Jerry Tegete.
Kwa ujumla umaliziaji mbovu ndio uliowagharimu Yanga kutoka uwanjani baada ya dakika 45 za kwanza wakiwa hawajapata bao.
Kipindi cha pili, Yanga walipigana haswa kusaka mabao, lakini Mtibwa walikuwa imara hiio leo.
Kipa Hussein Sharrif ‘Cassillas’ alizuia michomo mingi ya washambuliaji wa Yanga ambao hakika siku ya leo bahati haikuwa yao.
Alikuwa ni mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Hamisi Kiiza ‘Diego’ aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Didier Kabumbangu aliyeinusuru Yanga kuzama katika mchezo wa leo baada ya kufunga bao la kusawazisha dakika ya 86, akiunganisha pasi nzuri ya Said Bahanuzi aliyetokea benchi pia kuchukua nafasi ya Frank Domayo.
Baada ya bao hilo, Yanga waliongeza kasi kusaka bao la ushindi, hata hivyo Jerry Tegete alipoteza nafasi nzuri ya mwisho baada ya kupewa pasi nzuri na Simon Msuva, lakini akashindwa kuumiliki vyema mpira.
Matokeo hayo yanaifanya Yanga itimize pointi 33 baada ya kucheza mechi 14 na inaendelea kuongoza Ligi Kuu, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 32, zote zimecheza mechi 14.      
Katika mchezo wa leo, kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’/Nurdin Bakari, Simon Msuva, Frank Domayo/Said Bahanuzi, Didier Kavumbangu/Hamisi Kiiza, Jerry Tegete na Haruna Niyonzima.
Mtibwa Sugar; Hussein Sharrif ‘Casillas’, Said Mkopi, Issa Rashid, Rajab Mohamed, Salum Swedi, Shaaban Nditi, Vincent Barnabas, Rashid Gumbo, Hussein Javu, Shaaban Kisiga ‘Malone’ na Ally Mohamed ‘Gaucho’.

TENGA ATEUA WAWILI WAPYA TFF


Tenga

RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga ameteua wajumbe wawili kuingia kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF baada ya nafasi mbili kuwa wazi kutokana na mmoja kuteuliwa kuongoza kamati nyingine ya TFF na mwingine kufariki dunia.
Iddi Mtiginjolla ambaye alikuwa mjumbe wa Kamati ya Nidhamu hivi karibuni aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF baada ya Shirikisho kufanya mabadiliko ya katiba yaliyotokana na maagizo ya Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Mpira wa Miguu (FIFA), wakati mjumbe mwingine wa Kamati ya Nidhamu, Shaaban Semlangwa alifariki dunia katikati ya mwaka uliopita.
Wajumbe wapya walioteuliwa ni Jesse Mguto- alikuwa Hakimu Mkazi na kwa sasa ni mwanasheria na Wakili wa Mahakama Kuu. Ana Digrii ya Sheria. Mwingine ni Yohane Masala ambaye kwa sasa ni Mwanasheria Mwandamizi wa Serikali (Principal State Attorney). Ana Digrii ya Kwanza na ya Pili ya Sheria na Digrii ya Pili katika masuala ya Amani na Haki (MA in Peace and Justice).
Rais Tenga amesema ana imani na uwezo wa watu hao na kwamba watafanya kazi yao kwa uadilifu ili Shirikisho liendelee kuboresha utawala bora.

SAMATTA NA ULI WAJA KESHO KUIKABILI CAMEROON JUMATANO TAIFA


Samatta na Ulimwengu kulia

WASHAMBULIAJI wa Taifa Stars, Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanatarajia kutua nchini kesho (Februari 3 mwaka huu) tayari kwa mechi ya Cameroon itakayochezwa Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Samata na Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) watawasili saa 11.10 jioni kwa ndege ya PrecisionAir na kwenda moja kwa moja kambi hoteli ya Tansoma.
Wachezaji wa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager wanaanza kuripoti kambini leo jioni (Februari 2 mwaka huu) mara baada ya mechi kati ya Yanga na Mtibwa Sugar.
Mechi hiyo iliyo katika Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) pia itatumika kwa ajili ya kutoa ujumbe wa vita dhidi ya Malaria viwanjani, ugonjwa unaoongoza barani Afrika kwa kusababisha vifo vya watoto na wajawazito.
TFF kama ilivyo Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na FIFA imekuwa msitari wa mbele katika kueneza kampeni ya vita dhidi ya Malaria inayoongozwa United Against Malaria (UAM). Rais wa TFF, Leodegar Tenga na nahodha wa Cameroon, Samuel Eto’o ni miongoni mwa mabalozi wa vita dhidi ya Malaria barani Afrika.
Wakati huo huo: Kundi la kwanza la Cameroon likiongozwa na kiungo wa zamani wa Toulouse ya Ufaransa ambaye sasa yuko Al Ahli ya Falme za Kiarabu (UAE), Achille Emana na Meneja wa timu hiyo Rigobert Song litatua nchini kesho (Februari 3 mwaka huu) saa 4.40 usiku kwa ndege ya KLM.
Wachezaji wengine katika kundi hilo ni Vincent Aboubakary anayechezea timu ya Valenciennes iliyoko Ligi Kuu ya Ufaransa, kipa Charles Itandje anayedakia timu ya POAK FC ya Ugiriki, Kocha wa viungo Sylvain Monkam.
Mshambuliaji wa Anzhi Makhachkala ya Urusi ambaye ndiye nahodha wa Cameroon, Samuel Eto’o ataongoza kundi la pili litakalowasili nchini Februari 4 mwaka huu (saa 3.45 asubuhi) kwa ndege ya Kenya Airways kupitia Nairobi, Kenya.
Wengine katika ndege hiyo Herve Tchami wa Budapest Honved ya Hungary, beki Nicolas Nkoulou wa Marseille ya Ufaransa, mshambualiji Jean Paul Yontcha wa SC Olhanense ya Ureno na daktari wa timu Dk. Boubakary Sidik wakati Kocha wa timu hiyo Jean Paul Akono na msaidizi wake Martin Ndtoungou watawasili saa 4.40 asubuhi kwa ndege ya Kenya Airways akitokea Afrika Kusini.
Februari 4 mwaka huu kuna kundi lingine litakaloingia saa 4.40 usiku kwa ndege ya KLM ambalo lina beki Jean Kana Biyick wa Rennes ya Ufaransa, mshambuliaji Fabrice Olinga wa Malaga FC ya Hispania, beki Allan Nyom wa Udinese ya Italia ambaye yuko kwa mkopo Granada ya Hispania na beki wa kushoto Henri Bedimo wa Montpellier ya Ufaransa.
Wachezaji waliobaki wakiongozwa na kiungo wa Barcelona, Alexandre Song watawasili Februari 5 mwaka huu kwa muda tofauti kwa ndege za KLM na Kenya Airways.

RHINO RANGERS WAANZA VYEMA DURU LA PILI LIGI DARAJA LA KWANZA FDL KWA KUWABAMIZA POLISI TABORA BAO 1-0 LA ABDALAH SIMBA




Timu ya wanajeshi ya mkoani tabora RHINO RANGERS imeanza vyema duru la pili la ligi daraja la kwnaza baada ya kuwafunga mahasimu wao wakubwa wa enzi za bibi na babu POLISI TABORA pia wa nkoani tabora bao 1-0 bao lililofungwa na mshambuliaji wao hatari ABDALAH SIMBA dakika ya 15 ya kipindi cha kwanza aliyeunganisha krosi maridadi kutoka kwa kiunga machachari salum majdi alimaarufu CHUJI.

Hadi dakika 90 za mchezo refarii Mbaraka Almasi kutoka mwanza timu ya rhino rangers bao 1-0 na polisi hawana kitu na kuendelea kujikita kileleni mwa ligi daraja la kwanza FDL kwa kufikisha pointi 20 mara baada ya kucheza michezo 8 ,wakifuatiwa na JKT Kanembwa ambao kesho watacheza na polisi dodoma kw apointi zao 16.
MATOKEO MENGINE KATIKA KUNDI C polisi mara vs pamba 2-1Mengine nitawatumia nikipata matokeo


TIMU YA JESHI YA MKOANI TABORA RHINO RANGERS IMEANZA VYEMA DURU LA PILI LA LIGI DARAJA LA KWANZA KWA KUIFUNGA POLISI BAO 1-0 HII LEO


picha za leo katika uwanja wa ally hasaan mwinyi  balaaaaaa kw apikipikiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

timu ya wanajeshi ya mkoani tabora iliyoanza leo katika picha ya pamoja

mgeni rasmi kutoka dodoma akisalimiana na marefarii wa leo


nahodha w atimu mwakitosi akimtambulisha mgeni rasm kwa wachezaji wa rhino hii leo-------

<<<<<<<<<<>>>>>>>>>PICHA ZINGINE BADAE NITAKULETEA NA MATOKEO MENGINE

MZUNGUKO WA PILI WA LIGI DARAJA LA KWANZA KUANZA LEO.


Mzunguko wa pili wa pili daraja la kwanza(FDL) unaanza leo ambapo Villa Squad na Moro United zitakuwa zikiumanau katika uwanja wa Karume, Dar es Salaam katika moja ya mechi za kundi B za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inayoanza mzunguko wa lala salama.
Kundi A litakuwa na mechi kati ya Mbeya City na Burkina Faso itakayochezwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Majimaji na Kurugenzi katika Uwanja wa Majimaji mjini Songea, na Polisi Iringa dhidi ya Mkamba Rangers kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora mjini Iringa.
Mechi nyingine ya Kundi B itakuwa Transit Camp na Ndanda itakayochezwa Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani. Kundi C ni Polisi Dodoma na Kanembwa JKT (Uwanja wa Jamhuri, Dodoma), Morani dhidi ya Mwadui (Uwanja wa Kiteto, Manyara), Polisi Mara na Pamba (Uwanja wa Karume, Musoma), Polisi Tabora na Rhino Rangers (Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora).
Ligi hiyo inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa Machi mwaka huu ambapo mshindi wa kila kundi atapanda daraja kucheza Ligi Kuu msimu ujao.

FERGIE AKANA SHITAKA LA FA!!


>>AOMBA AWASILISHE UTETEZI KIMAANDISHI, FA KUAMU NINI KINAFUATA!!
FERGIE_KAZINISIR ALEX FERGUSON mekana Shitaka alilofunguliwa na FA, Chama cha Soka England, kufuatia kauli yake kuhusu Refa Msaidizi baada ya Timu yake Manchester United kutoka sare 1-1 na Tottenham kwenye Mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa Januari 20 Uwanjani White Hart Lane.
Ferguson alimyooshea kidole Refa Msaidizi Simon Beck kwa kushindwa kuashiria Penati baada ya Straika wake Wayne Rooney kuangushwa ndani ya Boksi.
Mara baada ya kauli ya Ferguson, FA ilimtaka Meneja huyo kujieleza na ikaamua kufungua Mashitaka rasmi na alipewa hadi Ijumaa Saa 1 Usiku, Bongo Taimu, kuyajibu.
Kauli ambazo zimemtia matatani Ferguson ni pale alipotamka: “Kulikuwa hamna njia Mshika Kibendera angeweza kutoa ile [Penati!]-aliwapa kila kitu! Kilikuwa kitu cha wazi na alikuwa Yadi 10 au 12 na hakutoa! Wao walipewa kila kitu!”
Pia alikumbushia tukio ambalo Refa Msaidizi Simon Beck alipowakatili Man United Aprili 2010 walipofungwa 2-1 na Chelsea kwa Mshika Kibendera huyo kutokutoa Ofsaidi ya wazi dhidi ya Didier Drogba aliefunga Bao la ushindi.
Akikana Mashitaka hayo, Ferguson aliomba awasilishe Ushahidi wake Kimaandishi na sasa FA itatathmini majibu yake na kuamua kama impe Adhabu ya Kufungiwa Mechi na Faini au mojawapo.
Kihistoria, Ferguson na FA wana misuguano ya muda mrefu na Machi 2011 alifungiwa Mechi 5 na kupigwa Faini Pauni 30,000 kwa kumtuhumu Refa Martin Atkinson kwa kuipendelea Chelsea.

JULIO ASEMA YANGA NA AZAM WANA POINTI ZA SIMBA, PIGA UA KOMBE LINABAKI MSIMBAZI


Kocha wa Simba, Jamhuri Kihwelo akizungumza na Waandishi wa Habari mchana huu Msimbazi. Kulia ni Ofisa Habari wa klabu hiyo, Ezekiel Kamwaga.


KOCHA Msaidizi wa mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba SC, Jamhuri Mussa Kihwelo amesema kwamba Yanga wana pointi zao tatu sawa na Azam, hivyo hawana shaka ya kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mwishoni mwa msimu.  
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa mikutano wa klabu ya Simba SC, Mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam mchana wa leo, Jamhuri maarufu kama Julio alisema kwamba kwa sasa wanazidiwa pointi sita na Yanga, lakini anaamini mwisho wa msimu watatetea ubingwa wao tu.
“Tutawafunga Yanga na kuchukua pointi tatu, tutawafunga Azam FC na kuchukua pointi tatu na sisi tunajua Yanga na Azam watafungwa pia mechi nyingine na sisi tutashinda zote na kupanda kileleni,”alisema Julio.
Kwa sasa katika msimamo wa Ligi Kuu, Yanga wapo kileleni kwa pointi zao 32, wakifuatiwa na Azam yenye pointi 30, wakati Simba SC ina pointi 26.
Jamhuri alisema kwamba Simba inaendelea vizuri na maandalizi yake ya mchezo wa keshokutwa dhidi ya JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na wana matumaini makubwa ya kushinda.
Beki huyo wa zamani wa Simba SC, alisema anafahamu JKT Ruvu ni timu nzuri na ngumu, lakini hawataweza kuizuia timu yao kubeba pointi tatu hiyo kesho

TUZO ZA WANAMICHEZO BORA TZ APRILI 27


Kapombe

TUZO za Wanamichezo Bora wa Tanzania wa mwaka 2012 zinazoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) zitafanyika Aprili 27 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Kamati inayoratibu tuzo hiyo ilifanya kikao chake cha kwanza Jumanne wiki hii, ambapo wajumbe wa kamati hiyo walikubaliana mambo mbalimbali ya kimsingi kuhakikisha tuzo zinakuwa na mvuto kama ilivyokuwa miaka iliyopita na pengine ziwe bora zaidi.
Kutokana na hali hiyo vyama vyote vya michezo vilivyosajiliwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT), ambavyo vipo hai na vinaendesha mashindano vitaandikiwa barua kwa ajili ya kutoa mependekezo yao ya wanamichezo waliofanya vizuri kwa mwaka jana upande wa michezo yao na yawasilishwe kabla ya Februari 28, mwaka huu.
Tunaomba ieleweke kuwa vyama vitatoa mapendekezo na hivi sasa Kamati ya Tuzo inafanya mazungumzo na kampuni mbalimbali zinazohusika na mambo ya mawasiliano ili kuona namna zitakavyoshirikiana na wadau katika kuchambua majina hayo, ambapo kila chama kimetakiwa kiwasilishe majina matano ya wanamichezo wao kwa kila jinsia kama ni mchezo unaochezwa na jinsia mbili, lakini kama ni mchezo wa jinsia moja watatakiwa kuwasilisha majina matano ya jinsia husika tu.
Yapo marekebisho kadhaa yamefanyika ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya tuzo kutoka 36 za mwaka jana hadi kufikia 42 mwaka huu na idadi inaweza kuongezeka ama kupungua kulingana na sifa za wanamichezo ambazo vyama vitaleta.
Tunaomba wadau watupe ushirikiano wa kutosha katika jambo hili ili kuzifanya tuzo ziwe bora na kuhakikisha kila anayestahili kupata tuzo anazawadiwa kwa kuthamini kile alichokifanya, ambapo ukumbi utakapofanyika tuzo hizo utatangazwa hivi karibuni baada ya kukamilisha baadhi ya mambo.
Idadi ya michezo itakayopewa tuzo pamoja na aina nyingine ya tuzo zitakazotolewa ikiwemo Tuzo ya Heshima tutaendelea kujulishana kadri siku zitakavyokuwa zinasonga mbele. Washindi wa kila tuzo ndiyo mmojawapo ataibuka kuwa Mwanamichezo Bora wa Tanzania Mwaka 2012.
Dhamira ya kamati yangu ni kutaka kuhakikisha kuwa TASWA haikukosea kututeua na tutaleta wanammichezo sahihi na hatimaye kumpata yule bora ambaye ataungana na wengine waliopata kutwaa tuzo hiyo miaka ya nyuma.
Wanamichezo ambao wamepata kutwaa Tuzo ya Mwanamichezo Bora Mwaka wa Tanzania ni Samson Ramadhan (2006),  Martin Sulle (2007) na Mary Naali (2008) wote wakiwa wanariadha, wakati mwaka 2009 alikuwa Mwanaidi Hassan na mwaka 2010 alikuwa pia Mwanaidi Hassan ambaye ni mcheza netiboli na mwaka 2011 alikuwa mwanasoka Shomari Kapombe

CAMEROON YALETA FULL MZIKI KUIVAA STARS JUMATANO


Nahodha wa Cameroon, Eto'o

SHIRIKISHO la Soka Cameroon (FECAFOOT) limetaja msafara wake wa watu 36 wakiwemo wachezaji 21 wa timu yao ya Taifa Indomitable Lions) wakiongozwa na Nahodha Samuel Eto’o Fils kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumatano.
Kiongozi wa msafara wa timu hiyo itakayoanza kuingia nchini keshokutwa (Februari 3 mwaka huu) ni Mwakilishi wa Serikali ya Cameroon, Dieudone Wassi. Naibu kiongozi wa msafara wa Cameroon itakayofikia hoteli ya New Africa ni Makamu wa Rais wa FECAFOOT, John Ndeh.
Mbali ya Et’oo, wachezaji wengine waliomo kwenye msafara huo ni Charles Itandje, Benoit Assou Ekoto, Jehu Rustand Youthe (Union Douala), Fabrice Olinga Essono, Allam Nyam, Bouba Aminou, Benoit Angwa, Herve Tchami, Henri Bedimo, Nicolas Nkoulou, Jean Makoun, Jean Kana Biyick, Joel Matip, Vincent Aboubakar, Alexandre Song, landre Nguemo, Pierre Wome, Jean Nyontcha, Achille Emana na Charles Eloundou.
Wengine ni Andre Nguidljol Nlend (Mkurugenzi wa Utawala FECAFOOT), Jean Paul Akono (Kocha Mkuu), Martin Ndtouungou Mpile (Kocha Msaidizi), Jacque Songo’O (Kocha wa makipa), Dk. Baoubakary Sidiki (Daktari wa Timu) na Emmanuel Francis Ambane (Psychologist).
Pia wapo Tchonkontey Monkam (Fitness Trainer), Rigobert Song (Meneja wa Timu), Aoudou Mvotoung (Team Security), Fouda pascal Linus (Ofisa Habari FECAFOOT), Boubakar Ndou (Meneja Vifaa), Daniel Tcheuffa Tecky (Physiotherapist), Elias Kalaguem (Physiotherapist) na Justin Addo (Wakala wa Mechi).
Wakati huo huo, kikosi cha Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kitaingia kambini kesho jioni (Februari 2 mwaka huu) kwenye hoteli ya Tansoma.
Aidha, kiingilio cha chini kwenye mechi ya FIFA Date kati ya Taifa Stars na Cameroon itakayochezwa Jumatano (Februari 6 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kitakuwa ni sh. 5,000 kwa viti vya kijani.
Viti vya bluu ni sh. 7,000 wakati viti vya rangi ya chungwa itakuwa sh. 10,000. Kwa viti vya VIP viingilio ni kama ifuatavyo; VIP C sh. 15,000, VIP B sh. 20,000 na VIP A sh. 30,000.
Tiketi zitaanza kuuzwa siku moja kabla ya mchezo katika vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Ohia/Samora, kituo cha mafuta OilCom Ubungo, Dar Live Mbagala na kituo cha mafuta Buguruni.

REFA SWAI KUCHEZESHA YANGA NA MTIBWA KESHO



KLABU za Yanga na Mtibwa Sugar zinapambana kesho (Februari 2 mwaka huu) katika moja ya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom. Mchezo huo utafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mwamuzi Ronald Swai kutoka Arusha ndiye atakayechezesha mechi hiyo inayotarajiwa kuwa na upinzani mkali, kwani wakati Yanga ikiongoza ligi hiyo, wapinzani wao Mtibwa Sugar katika mechi iliyopita walilala mbele ya Polisi Morogoro ambayo ni ya mwisho katika msimamo wa ligi kwa sasa.
Polisi Morogoro itakuwa mwenyeji wa African Lyon kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro wakati Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Mgambo Shooting na Ruvu Shooting inayofundishwa na Charles Boniface Mkwasa.
Keshokutwa (Jumapili) kutakuwa na mechi mbili. Simba itaumana na JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku Tanzania Prisons ikiikabili Coastal Union katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Wakati huo huo; Villa Squad na Moro United zinaumana kesho (Februari 2 mwaka huu) Uwanja wa Karume, Dar es Salaam katika moja ya mechi za kundi B za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inayoanza mzunguko wa lala salama.
Kundi A litakuwa na mechi kati ya Mbeya City na Burkina Faso itakayochezwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Majimaji na Kurugenzi katika Uwanja wa Majimaji mjini Songea, na Polisi Iringa dhidi ya Mkamba Rangers kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora mjini Iringa.
Mechi nyingine ya Kundi B itakuwa Transit Camp na Ndanda itakayochezwa Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani. Kundi C ni Polisi Dodoma na Kanembwa JKT (Uwanja wa Jamhuri, Dodoma), Morani dhidi ya Mwadui (Uwanja wa Kiteto, Manyara), Polisi Mara na Pamba (Uwanja wa Karume, Musoma), Polisi Tabora na Rhino Rangers (Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora).
Ligi hiyo inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa Machi mwaka huu ambapo mshindi wa kila kundi atapanda daraja kucheza Ligi Kuu msimu ujao.

SIMBA YAMUANDALIA MAPOKEZI MAZITO MALKIA WA NYUKI


Rahma Al Kharoos
KLABU ya Simba SC imemuandalia mapokezi ‘baab kubwa’ mfadhili wao wa ziara ya Oman, Mama Rahma Al Kharoos, Malkia wa Nyuki, anayetarajiwa kutua nchini Jumanne.
Ofisa Habari wa Simba SC, Ezekiel Kamwaga alisema  jana  mchana kwamba, wanachama na wapenzi wa klabu hiyo wanatakiwa kufika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam siku hiyo kumpokea mfadhili huyo.
“Mama huyu ametusaidia sana kwa kweli, katika kambi yetu ya Oman alitumia zaidi ya Sh. Milioni 80 ambazo ziliisaidia sana timu kwa maandalizi, kwa hiyo tunaomba twende tukampokee siku hiyo, ili kulipa fadhila kwake,”alisema Kamwaga.
Kamwaga alisema kwamba Mama Rahma atakuwa Mkuu wa Msafara wa Simba itakapokwenda nchini Angola kucheza na Libolo ya huko katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu wiki iliyopita, Simba iliweka kambi ya wiki mbili kujiandaa na hatua hiyo kwa ufadhili kamili wa Malkia wa Nyuki. Hayo yalikuwa majibu kwa wapinzani wao wa jadi, Yanga SC walioweka kambi ya wiki mbili pia nchini Uturuki.
Matunda ya ziara ya Oman ni Simba kuanza Ligi Kuu ya kishindo ikiitandika 3-1 African Lyon na keshokutwa itaingia kwenye mchezo wa pili kusaka pointi dhidi ya JKT Ruvu ya Pwani.

ARSENAL YATAMBULISHA KIFAA KIPYA



Arsenal unveiled new signing Nacho Monreal on the same day that manager Arsene Wenger revealed fellow left back Kieran Gibbs will be out for up to eight weeks.
The Frenchman is likely to field the error-prone Andre Santos when German giants Bayern Munich visit for their Champions League clash on February 19.
The Arsenal boss said Gibbs' latest injury setback forced the club's £8.5million purchase of Monreal from Malaga on transfer deadline day, with under-fire Santos currently the only fit Arsenal left back.
Scroll down for video
In the mix: Nacho Monreal joins Andrey Arsahvin in training this afternoon after his unveiling
In the mix: Nacho Monreal joins Andrey Arsahvin in training this afternoon after his unveiling
Spanish connection: Monreal (right) walks out to training with Mikel Arteta (centre) and Frenchman Abou Diaby (left)
Spanish connection: Monreal (right) walks out to training with Mikel Arteta (centre) and Frenchman Abou Diaby (left)
Settling in: Monreal appeared to enjoy his first session with Arsenal
Settling in: Monreal appeared to enjoy his first session with Arsenal
Wenger said: 'We had a blow with the Gibbs injury, which is a bit longer than expected. We expected (it to be) two to three weeks (but) it will be four to six, so we were in a position where we had to make a quick decision. That explains our buy.
'We bought Monreal as well because we believe he can integrate our style of play and adapt very quickly to that. He has the characteristics to play our game because he is very mobile, he has a good left foot and is very good in combination play. It is of course vital in our style of play.
'I believe we need two left backs. You cannot play every single game with the same player. We had two before, we have two again now. 
Ineligible: Nacho Monreal is unable to play in the Champions League clash with Bayern
Ineligible: Nacho Monreal is unable to play in the Champions League clash with Bayern
Looking up: Wenger drafted in Monreal from Malaga on deadline day
Looking up: Wenger drafted in Monreal from Malaga on deadline day
Looking up: Wenger drafted in Monreal from Malaga on deadline day
'If Gibbs is out for four to six weeks, from six it can easily go to eight (before he is competitive again) and that means two months in a very decisive period. It’s vital to have another left back.'
Gibbs will almost certainly miss Arsenal's Champions League home tie against Bayern and will struggle to regain fitness in time for the return leg in Germany on March 13.
Loss: Kieran Gibbs limped off the pitch against Liverpool
Loss: Kieran Gibbs limped off the pitch against Liverpool
Stand-in: Andre Santos is likely to deputise in Gibbs' place against Bayern Munich
Stand-in: Andre Santos is likely to deputise in Gibbs' place against Bayern Munich
Monreal is cup-tied for Arsenal's European games after playing for Malaga earlier in the competition, so Wenger will be forced to field Santos or, more likely, move captain Thomas Vermaelen to left back.
The Arsenal boss insisted Monreal's move to the Emirates did not mean the end of Santos' career at the club and argued widespread criticism of the player was unfair.
Wenger said: 'Honestly, I believe that Kieran Gibbs will be out for the Champions League because we are only three weeks away from Bayern now. I don’t think he will be available. But Vermaelen can play there. Santos could have a key role as well, yes.
'Does Santos have a future at this club? Yes, why not? Maybe people speak that he had a difficult game but he lacks competition. 
Tormentors? Arjen Robben
Tormentors? Franck Ribery
Tormentors? Arjen Robben and Franck Ribery (right) will be hoping to run riot against Santos
Pulling the strings: Toni Kroos
Pulling the strings: Bastian Schweinsteiger
Pulling the strings: Toni Kroos and Bastian Schweinsteiger (right) will hope to dictate the tempo against Arsenal
'He is a style of player who need competition because he is not a nervous type of player, he is a stamina type of player and get sharper through competition.
'If you analyse his performance, you will be less critical. The first critics after the game are always a bit emotional because you have one or two big mistakes in your mind and we are all the same on that front. But when you watch the games again, you will see that he has done some good things.'
Wenger will make a decision today on whether Monreal, 26, will feature on Saturday against Stoke City, but said Mikel Arteta could return after missing nearly a month of action with a calf strain. 
Vermaelen, however, is a slight doubt after picking up an ankle injury.

 VIDEO  Arsene Wenger talks about his last minute buy 

 

 

MTOTO WA ZIDANE, ENZO AMTANDIKA MWENZAKE TEKE LA HATARI NA KULIMWA NYEKUNDU



It's a case of 'like father, like son' for this talented young player. 
Zinedine Zidane's son Enzo showed he really is following in his father's footsteps this week when he was sent off for Real Madrid in an Under 18s game for this studs-up challenge.
Skilful midfielder Enzo saw red when his team took on Aspire International in the Al Kass International Cup in Doha, Qatar.
Scroll down for video..
Vicious: Enzo Zidane (right) was red-carded for this horror tackle in an Under 18s match for Real Madrid
Vicious: Enzo Zidane (right) was red-carded for this horror tackle in an Under 18s match for Real Madrid
Like father like son: Enzo's father Zinedine (right) was sent off in the 2006 World Cup final for this headbutt on Italy's Marco Materazzi
Like father like son: Enzo's father Zinedine (right) was sent off in the 2006 World Cup final for this headbutt on Italy's Marco Materazzi
No choice: Argentinean referee Horacio Elizondo sent Zidane to the stands
No choice: Argentinean referee Horacio Elizondo sent Zidane to the stands
But the young player's blushes were spared when his team-mates rallied back from two goals down to win the game 3-2 with a late winner.
Today the Spanish club - managed by Fernando Morientes - take on Brazilian side Fluminense in their quarter-final clash which Enzo will miss through suspension.
Meanwhile, Liverpool's young team will face Italian giants Inter Milan for a place in the semi-finals.
The tournament - at the exclusive Aspire Academy in the city where Manchester United last week trained - is one of the premier youth tournaments in the world.
Temper: Zidane was also red-carded while at Juventus for butting a Hamburg player during a Champions League clash in 2000
Temper: Zidane was also red-carded while at Juventus for butting a Hamburg player during a Champions League clash in 2000
Unparalleled: Zidane (left) was one of the best players of recent times
Unparalleled: Zidane (left) was one of the best players of recent times
VIDEO: Watch Enzo's tackle

KMKM YAANZA VEMA LIGI KUU ZBAR



KMKM imeanza vyema mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Zanzibar, maarufu kama Zanzibar Grand Malt Premier League, baada ya kuichapa Mafunzo mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Mao Tse Tung, Kisiwani Unguja jana.
KMKM ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wao tegemeo Maulid Ibrahim katika dakika ya 35 ya kipindi cha kwanza, mpaka mapumziko matokeo yalikuwa yanasomeka 1-0.
Kipindi cha pili katika mchezo huo kiliingia dosari baada ya mchezaji wa KMKM Faki Mwalim kutolewa nje kwa kadi nyekundu kufuatia mchezo mbaya.
Mafunzo walifanikiwa kusawazisha katika dakika ya 79 kupitia kwa Ame Khamis, hata hivyo bao hilo halikudumu kwani licha ya KMKM kucheza pungufu mchezaji mmoja walifanikiwa kupata bao la ushindi katika dakika ya 82 kupitia kwa Jaku Joma.
Kwa matokeo hayo KMKM wanaendelea kuongoza msimamo wa ligi hiyo baada ya kufikisha pointi 26 wakifuatiwa na Mafunzo yenye pointi 22.
Katika mchezo mwingine, uliofanyika kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba, mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Super Falcon wamefanikiwa kuanza vyema mzunguko wa pili baada ya leo kuchomoza na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Chipukizi ya Chake Chake.
Bao pekee la ushindi kwa Super Falcon lilifungwa katika dakika na Omar Mohammed katika dakika ya 69.
Ligi hiyo inatarajia kuendelea tena kesho katika viwanja viwili tofauti katika visiwa vya Unguja na Pemba. Kisiwani Pemba katika Uwanja wa Gombani kutakuwa na pambano kati ya Duma timu inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Uchumi Kisiwani Pemba, ikionyeshana kazi na Jamhuri ambao tarehe 16 ya mwezi huu watakuwa na mechi ya Kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika watakapoikaribisha St. George kutoka Ethiopia kabla ya kurejeana wiki mbili baadae, itakumbukwa kuwa Jamhuri ambao ni washindi wa pili wa ligi iliyopita walitakiwa kuiwakilisha Zanzibar katika kombe la Shirikisho lakini kutokana na Mabingwa wa Soka Zanzibar kuamua kujitoa katika michuanop hiyo kutokana na ukata Jamhuri wamechukua nafasi hiyo huku Zanzibar ambao ni mwanachama mshiriki wa CAF wakiwa hawana uwakilishi katika michuano ya kombe la Shirikisho inayoandaliwa na CAF.
Kwa upande wa Kisiwa cha Unguja hapo kesho kutakuwa na mchezo mmoja katika Uwanja wa Amaan, ukiwakutanisha Bandari na Malindi.

BIN KLEB AZUNGUMZIA TUHUMA ZA WACHEZAJI YANGA KULOGANA


Bin Kleb kulia akizungumza na Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro'

MWENYEKITI wa Kamati ya Mashindano ya klabu ya Yanga SC, Abdallah Ahmad Bin Kleb amesema kwamba hakuna suala la ushirikina ndani ya klabu yao, bali kuna watu ambao ni wapinzani wao wanapandikiza chuki kwa wachezaji wao, ili kuvuruga umoja na amani iliyopo ndani ya kikosi chao kwa sasa.
Akizungumza n jana, Bin Kleb alisema kwamba amesikia wapo wachezaji walitaka kushikana mashati mazoezini wakituhumiana kulogana, lakini baada ya uongozi kulifanyia kazi suala hilo, umegundua kuna watu wanapandikiza chuki baina ya wachezaji wao hao.
Mshambuliaji Mrundi, Didier Kavumbangu anadaiwa kumvaa Jerry Tegete na kumtuhumu kwamba anamloga kumpunguza kasi uwanjani, ili ang’are yeye.
“Hakuna kitu kama hicho, kuna watu wanawachonganisha hawa wachezaji, wewe fikiria sasa wao ndio wanacheza kama washambuliaji pacha na wanaelewana sana, hakuna anayekaa benchi kati yao, sasa hilo suala la kulogana linatoka wapi?”alihoji Bin Kleb.
Kiongozi huyo alisema jambo ambalo anaweza kukiri ndani ya Yanga hivi sasa ni  ushindani mkubwa wa namba ndani ya kikosi kizima na ili mchezaji apate nafasi kwenye kikosi cha kwanza, lazima afanye kazi haswa.
“Tumezungumza nao wachezaji na tutaendelea kuzungumza nao, wanapaswa kuwa makini, mtu kama hafanyi vizuri atafute sababu za msingi za kitaalamu na si kutuletea mambo ya Kiswahili kwenye timu.
Leo ukipandikiza chuki eti Tegete anamloga Kavumbangu, kwa sababu Tegete anafunga na Kavumbangu hafungi, je wakati wa mzunguko wa kwanza Kavumbangu alipokuwa anafunga Tegete hafungi, nani alikuwa anamloga mwenzake?”alihoji Bin Kleb.
Kiongozi huyo amesema kwamba wanapocheza washambuliaji wawili kama pacha lazima mmoja ndiye awe anafunga sana na wengine watafunga zikitokea nafasi. “Angalia hata Manchester United, Wayne Rooney ndiye alikuwa mfungaji wa timu, lakini kasajiliwa Van Persie mambo yamebadilika. Van Persie ndiye anafunga sana sasa hivi, ikitokea Rooney akapata nafasi naye anafunga. Huwezi kusikia mtu Analia kalogwa,”alisema Bin Kleb.
Kleb amewaasa wachezaji wa Yanga kuwa makini na watu wenye lengo la kuwachonganisha kuvuruga amani iliyopo ndani ya kikosi chao kwa sasa ambayo ndiyo siri ya mafanikio yao, ikiwemo kutwaa Kombe la Kagame, kuongoza Ligi na kwa ujumla kufanya vizuri.
“Tunaelekea kuzuri, sasa vema wachezaji wetu wakatuliza sana akili zao na kuwa makini na adui zetu, wanaotaka kuwavuruga ili timu ishuke kiwango,”alisema.
Yanga inatarajiwa kushuka dimbani tena leo kucheza mechi ya pili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro, mchezo ambao utafanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika mchezo wake wa kwanza, Yanga ilishinda 3-1 dhidi ya Prisons ya Mbeya na kuzidi kujichimbia kileleni mwa ligi hiyo, baada ya kufikisha pointi 32, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 30 na Simba pointi 26. Ikumbukwe, katika mechi yha mzunguko wa kwanza, Yanga ilifungwa 3-0 na Mtibwa mjini Morogoro.