Sunday, October 7, 2012

WITO: Suarez AFUNGIWE kwa kujidondosha makusudi!

Jumatatu, 08 Oktoba 2012 05:57
 
>>MENEJA STOKE CITY, Pulis, aitaka FA imuadhibu Suarez!!
>>MENEJA mwingine ataka RVP aadhibiwe!!
EVRA_N_SUAREZBosi wa Stoke City Tony Pulis amekitaka Chama cha Soka England, FA, kimuadhibu Straika wa Liverpool Luis Suarez kwa tabia yake ya kutaka kuwahadaa Marefa kwa kujidondosha makusudi ndani ya boksi ili apate Penati.


Jana, Stoke City ilikuwa Anfield kucheza na Liverpool kwenye Mechi ya Ligi Kuu England ambayo ilimalizika 0-0 na katika Kpindi cha Pili Luis Suarez ‘alijidondosha’ kutaka Penati ambayo Tony Pulis anaamini ulikuwa ni udanganyifu.


Pulis amesema: “Siku nyingi nimepigia kelele hili na Kipindi cha Pili tukio moja lilikuwa aibu kubwa! FA walitazame hili. Wampe Kifungo Mechi 3 na ataacha kujirusha!”
Alipohojiwa, Meneja wa Liverpool, Brendan Rodgers, alijibu: “Sikuona tukio hilo hivyo siwezi kusema chochote lakini chochote anachofanya Luis litakuwa tatizo tu!”


Hata hivyo, kuhusu tukio la Suarez kujidondosha kwa makusudi, FA haiwezi kuchukua hatua yeyote ile kwani Sheria zinawaruhusu kutoa adhabu pale tu matukio yalistahili Kadi Nyekundu na Refa hakuona na si matukio ambayo yangestahili Kadi ya Njano.



Wakati huo huo, Meneja wa Newcastle United  Alan Pardew ameitaka FA imwadhibu Straika wa Manchester United Robin van Persie kwa kile alichodai kumpiga ‘kipepsi’ Kiungo wa Newcastle, Yohan Cabaye, katika Mechi ya jana ya Ligi Kuu England huko Sports Direct Arena ambayo Manchester United iliitandika Newcastle bao 3-0.


Ingawa mwenyewe amekiri hakuliona tukio ambalo lilitokea wakati si Van Persie wala Cabaye kuwa na mpira huku wote wakikimbilia golini, Pardew amedai: “Van Persie alimtazama Cabaye na kumpiga kiwiko, nikiwa mkweli, FA walitazame tukio hilo.”


FA inaweza kulipitia tukio hilo na kutoa adhabu ikiwa tu Refa wa Mechi hiyo, Howard Webb, atakiri hakuliona tukio hilo na kama angeliliona angetoa Kadi Nyekundu.
 

DABI MILANO: Inter Milan YAITUNGUA AC Milan 1-0!

Jumatatu, 08 Oktoba 2012 05:16
 
>>MTU 10 Inter yashinda!!
Kwenye Dabi ya Jiji la Milan huko Italy, kwenye Mechi ya Serie A, kati ya Timu mbili zinazotumia Uwanja mmoja, San Siro, rasmi kama Stadio San Siro Guiseppe Meazza, ‘wenyeji’ wa Mechi hiyo, AC Milan, walipigwa bao 1-0 na Mahasimu wao wakubwa Inter Milan.
++++++++++++++
DABI MILANO=TAKWIMU:
>Mechi: 161
>AC Milan: Ushindi 60
>Inter Milan: Ushindi 52
>Sare: 49
++++++++++++++
AC_MILAN_MONTOLIVOKipigo hichi cha AC Milan, katika Dabi yao ya 161, kimezidisha presha kwa Meneja wao Massimiliano Allegri ambae anasakamwa kwa mwendo mbovu Msimu huu ambao sasa umewaacha wawe nafasi ya 11 kwenye Ligi baada ya kushinda Mechi mbili tu za Ligi kati ya 7.


Bao pekee la Mechi hiyo lilifungwa na Walter Samuel katika Dakika ya 4 baada ya kuunganisha frikiki kwa kichwa.
Katika Dakika ya 48, Inter Milan walijikuta wakibaki Mtu 10 baada ya Yuto Nagamoto kutolewa kwa Kadi Nyekundu kufuatia kulambwa Kadi za Njano mbili.


Hadi Mechi hiyo inamalizika jumla ya Kadi za Njano 9 zilitolewa, 6 kwa AC Milan na 3 kwa kwa Inter Milan.


Baada ya Mechi 7, Inter Milan wapo nafasi ya 5 wakiwa na Pointi 15 na Ligi hiyo inaongozwa na Mabingwa watetezi Juventus wenye Pointi 19 ingawa wamefungana Pointi na Napoli lakini Mabingwa hao wana ubora wa magoli na ndio maana wapo kileleni.


MATOKEO:
Jumamosi Oktoba 6
Chievo Verona 2 Sampdoria 1
Genoa 1 Palermo 1


Jumapili Oktoba 7
AS Roma 2 Atalanta 0
Torino FC 0 Cagliari 1
Siena 1 Juventus 2
Pescara 0 SS Lazio 3
Catania 2 Parma 0
Fiorentina 1 Bologna 0
AC Milan 0 Inter Milan 1
Napoli 2 Udinese 1
 

EL CLASICO: Yabaki vita ya Messi, Ronaldo, wote wafunga 2 katika sare 2-2!!

Jumatatu, 08 Oktoba 2012 04:44
 
>>KWA KLABU: MESSI, RONALDO WAFIKISHA BAO 100 KILA MMOJA 2012!
>>LA LIGA MSIMU HUU: BAO Messi 8, Ronaldo 8!
MESSI_n_RONALDOJana Usiku kwenye Mechi ya La Liga huko Nou Camp, Magwiji wa Soka wa Spain, vinara wa Ligi Barcelona na Mabingwa Real Madrid, walitoka sare ya bao 2-2 na bao zote hizo kufungwa na Maastaa wao wakubwa wenye ushindani mkubwa kati yao, Lionel Messi na Cristiano 


Ronaldo, na kulifanya pambano hilo liwe vita binafsi kati yao.
Kwa bao zao hapo jana, Ronaldo na Messi wamefungana kwa kila mmoja kufunga Bao 8 katika La Liga Msimu huu.
Alikuwa ni Ronaldo aliipeleka mbele Real kwa bao safi katika Dakika ya 23 lakini Dakika 8 baadae Messi akasawazisha kwa frikiki.


Kipindi cha Pili, Messi akapiga bao la pili katika Dakika ya 61 na Dakika 5 baadae Ronaldo akaisawazishia Real.


Sare hiyo imeifanya Real ibaki Pointi 8 nyuma ya Barcelona ambao ndio wanaongoza Ligi na wao kushika nafasi ya 5.


VIKOSI:
Barcelona: Valdes; Dani Alves, Adriano, Mascherano, Jordi Alba; Busquets, Xavi, Iniesta, Pedro, Messi, Fabregas
Akiba: Pinto, Montoya, Bartra, Song, Sergi Roberto, Sanchez, Villa.


Real Madrid: Casillas; Arbeloa, Ramos, Pepe, Marcelo; Alonso, Khedira; Di Maria, Ozil, Ronaldo; Benzema
Akiba: Adán, Coentrão, Kaká, Essien, Albiol, Modric, Higuaín.
Refa: Delgado Ferreiro


MATOKEO:
Ijumaa Oktoba 5
Celta Vigo 2 Sevilla 0


Jumamosi Oktoba 6
Rayo Vallecano 2 Deportivo La Coruna 1
Real Zaragoza 0 Getafe 1
Real Valladolid 1 Espanyol 1
Real Betis 2 Real Sociedad 0


Jumapili Oktoba 7
Levante 1 Valencia 0
Real Mallorca 1 Granada 2
Athletic Bilbao 1 Osasuna 0
FC Barcelona 2 Real Madrid 2
Athletic Madrid 2 Malaga 1
 

BPL: Man United yachupa nafasi ya Pili, Spurs yashinda, Liverpool 0-0!

Jumapili, 07 Oktoba 2012 20:05
 
MAN_UNITED-ANDO_RVP_SHINJI_EVRA>>LIGI KUU kusimama hadi Oktoba 20 kupisha Mechi za Kimataifa!
Katika Mechi za Ligi Kuu England, BPL, zilizochezwa leo, Manchester United, wakicheza huko Sports Direct Arena, waliwatwanga wenyeji wao Newcastle bao 3-0 na kushika nafasi ya pili wakiwa Pointi 4 nyuma ya vinara Chelsea huku huko Anfield Liverpool walitoka 0-0 na Stoke City na ndani ya White Hart Lane, Tottenham wameendeleza wimbi la ushindi kwa kuichapa Aston Villa bao 2-0.
++++++++++++++++++



Matokeo:
Jumapili Oktoba 7
Southampton 2 Fulham 2
Tottenham Hotspur 2 Aston Villa 0
Liverpool 0 Stoke City 0
Newcastle United 0 Manchester United 3
++++++++++++++++++


Southampton 2 Fulham 2
Kona ya Adam Lallana iliunganishwa na Jose Fonte na kuandika Bao la kwanza kwa Southampton katika Dakika ya 4 ambalo lilidumu hadi Dakika ya 70 na Fulham kusawazisha kwa bao la kujifunga mwenyewe Jos Hooiveld baada ya shuti la John Arne Riise lililokuwa likitoka nje kuguswa na Mchezaji huyo wa Southampton na kujifunga.


Fulham walipiga bap la pili kupitia Kieran Richardson katika Dakika ya 90 lakini Southampton walisawazisha katika Dakika ya 90 kwa bao la pili la Jose Fonte.


VIKOSI:
Southampton: Gazzaniga, Richardson, Yoshida, Fonte, Fox, Puncheon, Schneiderlin, Steven Davis, Lallana, Rodriguez, Lambert
Akiba: Kelvin Davis, Hooiveld, Ward-Prowse, Do Prado, Mayuka, Chaplow, Reeves.


Fulham: Schwarzer, Riether, Hughes, Hangeland, Riise, Kacaniklic, Ruiz, Baird, Sidwell, Duff, Rodallega
Akiba: Stockdale, Kelly, Senderos, Kasami, Karagounis, Richardson, Briggs.
Refa: Mark Clattenburg
++++++++++++++++++


Tottenham Hotspur 2 Aston Villa 0
Bao za Kipindi cha Pili za Steven Caulker, Dakika ya 58, na Aaron Lennon, Dakika ya 67, zimewapa ushindi wa bao 2-0 Tottenham walipocheza kwao White Hart Lane na Aston Villa.


VIKOSI:
Tottenham: Lloris, Walker, Gallas, Caulker, Vertonghen, Lennon, Dembele, Sandro, Bale, Defoe, Dempsey
Akiba: Friedel, Huddlestone, Adebayor, Dawson, Sigurdsson, Falque, Townsend.


Aston Villa: Guzan, Bennett, Vlaar, Clark, Lowton, Holman, El Ahmadi, Delph, Albrighton, Benteke, Agbonlahor
Akiba: Given, Bent, N'Zogbia, Westwood, Bannan, Weimann, Lichaj.
Refa: Neil Swarbrick
++++++++++++++++++


Liverpool 0 Stoke City 0
Ule mwendo wa kusuasua wa Liverpool kwenye Ligi Kuu umeendelea tena leo baada ya kushindwa kupata ushindi wakiwa Uwanja wa nyumbani Anfield walipotoka 0-0 na Stoke City iliyosimama imara kabisa.


VIKOSI:
Liverpool: Reina, Wisdom, Skrtel, Agger, Johnson, Gerrard, Allen, Sahin, Fernandez Saez, Suarez, Sterling
Akiba: Jones, Henderson, Cole, Assaidi, Coates, Carragher, Borini.


Stoke: Begovic, Cameron, Huth, Shawcross, Wilson, Walters, Nzonzi, Whelan, Adam, Kightly, Crouch
Akiba: Sorensen, Jones, Edu, Whitehead, Upson, Etherington, Jerome.
Refa: Lee Mason
++++++++++++++++++


Newcastle United 3 Manchester United 0
Bao za Johnny Evans, Dakika ya 8, Patrice Evra, Dakika ya 16 na Tom Cleverly, Dakika ya 71, yamewapa ushindi Manchester United wa bao 3-0 dhidi ya Newcastle.
Bao la Cleverly, bila shaka, litaingia katika ile Listi ya Mabao Bora ya Msimu.


VIKOSI:
Newcastle United: Harper; Santon, Williamson, Perch, Ferguson; Ben Arfa, Tioté, Cabaye, Gutiérrez; Ba, Cissé
Akiba: Alnwick, Simpson, Anita, Bigirimana, Obertan, Sammy Ameobi, Shola Ameobi


Manchester United: De Gea; Rafael, Ferdinand, Evans, Evra; Carrick, Cleverley; Kagawa, Rooney, van Persie, Welbeck
Akiba: Lindegaard, Scholes, Valencia, Anderson, Giggs, Hernandez, Wootton.
Refa: Howard Webb
++++++++++++++++++


RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumamosi Oktoba 20
[Saa 8 Dak 45 Mchana]
Tottenham v Chelsea


[Saa 11 Jioni]
Fulham v Aston Villa
Liverpool v Reading
Man United v Stoke City
Swansea v Wigan
West Brom v Man City
West Ham v Southampton


[Saa 1 na Nusu Usiku]
Norwich v Arsenal
Jumapili Oktoba 21
[Saa 9 na Nusu Mchana]
Sunderland v Newcastle
[Saa 12 Jioni]
QPR v Everton
 

CAF CHAMPIONS LIGI: Nusu Fainali zote Droo!!

Jumapili, 07 Oktoba 2012 19:11
 
Katika Mechi za kwanza za Nusu Fainali za CAF CHAMPIONZ LIGI zilizochezwa jana na leo matokeo ni sare kwa Mechi zote mbili baada ya wenyeji Sunshine Stars kutoka 3-3 na Al Ahly hapo jana na leo huko Lubumbashi TP Mazembe kutoka 0-0 na Mabingwa watetezi Esperance kwenye Mechi iliyotawala kwa Kadi huku Kadi 9 zikitembezwa mojawapo ikiwa Kadi Nyekundu.
Taarifa ya Mechi:


Sunshine Stars 3 Al Ahly 3
MAGOLI:


Sunshine Stars
-Josue Medrano Tamen, Dakika 34
-Dele Olorundare, Penati 73
-Precious Osasco Omoma, 84


Al Ahly
- Mohammed Nagy – Gedo, Dakika ya 18 na 74
-Al Sayed Hamdy, 30


TP Mazembe 0 Espérance Sportive de Tunis 0
Wachezaji wa Mazembe waliopewa Kadi za Njano:
-Kilitcho Kasusula
-Mabi Mputu
-Stopilla Sunzu
-Ngandu Kasongo
-Stopilla Sunzu [Kadi Nyekundu]


Wachezaji wa Esperance waliopewa Kadi za Njano:
-Derbali
-Traoui
-Ragued
-Afful



NUSU FAINALI:
MATOKEO:
Jumamosi Oktoba 6        
Sunshine Stars [Nigeria] 3 Al Ahly [Egypt] 3


Jumapili Oktoba 7         
TP Mazembe [Congo, DR] 0 Espérance Sportive de Tunis [Tunisia] 0
MARUDIANO


Jumamosi Oktoba 20         
22:30 Espérance Sportive de Tunis – Tunisia v TP Mazembe - Congo, The Democratic Republic Of The [Stade El Menzah]


Jumapili Oktoba 21         
20:30 Al Ahly – Egypt v Sunshine Stars – Nigeria [Cairo International Stadium]