Sunday, October 28, 2012

POLISI TABORA  BADO YAENDELEA KUWAPA PRESHA MASHABIKI WA HAPA MKOANI  BAO 1-0 NA POLISI DODOMA

Timu ya maafande wa polisi ya mkoani tabora imeshindwa kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani hiyo jana kwa kukubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa polisi dodoma mchezo uliochezwa jana katika dimba la ALLY HASSAN MWINYI.

Bao la ushindi la polisi dodoma lilifungwa na juma omary mnamo dakika ya 71 ya kimchezo baada ya kutokea prukushani za hapa na pale langoni mwa polisi tabora .

Hadi refa kutoka kagera JENESIA LIKYA anapuliza kipenga cha mwisho timu ya polisi dodoma ilitoka kifua mbele cha bao 1-0 dhidi ya maafande wenzao wa hapa mkoani tabora polisi tabora ambao huu ni mchezo wao wa pili wanafungwa mechi ywa kwanza walifungwa na Rhino rangers timu ya jeshi nayo ya hapa mkoani tabora

Katika michezo mingine rhino rangers imetoka suluhu ya kufungana bao moja kwa  moja 1-1 na timu ya pamaba ya mwanza,kanembwa fc imeifunga moran bao 2-0 mchezo uliochezwa katika dimba la lake tanganyika kigoma,,na mwadui ameonyesha umwamba kwa kumtandika polisi mara bao 3-0 kambarage stadium
Ligi hii itaendelea tena okt.31 mwaka huu kwa timu zote kucheza kundi c hilo .polisi mara vs rhino rangers[karume mara],moran vs polisi tabora[kiteto manyara],polisi dodoma vs pamba [jamhuri dodoma],na kanembwa vs mwadui [lake tanganyika kigoma

MATOKEO YA JUMAPILI FDL
KUNDI C
Polisi tabora vs polisi dodoma 0-1
Mwadui fc vs polisi mara          3-0
Kanembwa vs moran fc             2-0
Pamba vs Rhino rangers              1-1

MSIMAMO KUNDI C
1.JKT Kanembwa  pointi 6 mechi 2
2.Mwadui fc pointi 6 michezo 2
3.Rhino rangers pointi 4 mechi 2
4.Pamba fc pointi 3 mechi 2
5.Polisi dodoma pointi 3 mechi 2
6.Polisi mara pointi 0 mechi 2
7.Polisi tabora pointi 0 mechi 2
8.Moran fc pointi 0 mechi 2

FAHAMU; kuwa kila kundi A,B,C litatoa timu moja ambayo itapanda ligi kuu ya VODACOM PREMIUM LAGER VPL kuungana natimu ambazo zitakuwa zimebaki ligi kuu na pia zitazipisha timu tatu ambazo zitakuwa zinashuka daraja

KIUNGO MPYA MBRAZIL WA COASTAL AAHIDI TAMU TUPU

Deangelis Gabriel Barbosa akiwa na mkewe, Zaira Caroiline na mtoto wao, Lara Barbos.


KIUNGO mshambuliaji mpya wa Coastal Union anayetokea nchini Brazili,Deangelis Gabriel Barbosa mwenye umri wa miaka 27, aliyetua Tanga mwishoni mwa wiki na kuanza mazoezi na timu hiyo ameaahidi kuipa mafanikio ili iweze kushiriki mashindano ya kimataifa barani Afrika.
Barbosa alitua jijini hapa akiwa pamoja na mke wake, Zaira Caroline na mwanae Lara Barbos na ameahidi kuipa mafanikio timu hiyo kwa kushirikiana na wachezaji wengine waliopo kwenye timu hiyo ambayo hivi sasa inafanya vizuri katika mechi zao mbalimbali.
Katika mahojiano na mwandishi wa habari hizi, kiungo huyo amesema anatokea Mtaa wa Bahia katika jiji la Paulo Afonso nchini Brazil na amesema atacheza soka la kisasa kwa ajili ya kuipa heshima timu hiyo ndani na nje ya nchini kwa kuwa anathamini mchezo huo ambao ni kazi yake.
Mchezaji huyo tayari ameanza mazoezi na wenzake na amesafiri na timu hiyo ambayo leo inacheza na JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Azam, Chamanzi, Dar es Salaam ingawa hatacheza kwa sababu viongozi wa Coastal bado wanakamilisha taratibu mbalimbali ikiwemo kibali chake cha kufanya kazi nchini.
Mchezaji huyo siku alipotambulishwa na Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Steven Mgutto, alitaja timu mbalimbali alizochezea kuwa ni pamoja na klabu ya New Road ya Nepal, ambako alipomaliza mkataba wake ndipo amekuja Tanzania.
Mguto alisema wameingia mkataba wa miaka miwili na mchezaji huyo na kueleza endapo kiwango chake kitakuwa kizuri watamuongezea mkataba mwingine.
Barbosa alisema atahakikisha anatoa mchango wake mkubwa kwenye timu hiyo ili aweze kuipa heshima inayostahili ikiwemo kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ili timu hiyo iweze kushiriki mashindano makubwa.
Awali, Katibu wa Coastal Union, Kassim El Siagi aliwataka wanachama pamoja na wapenzi wa timu hiyo, kuendeleza mshikamano uliopo ili kuweza kutimiza malengo yao waliojiwekea ya kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.
Siagi alizitaja klabu ambazo mchezaji huyo aliwahi kuzicheza ni Sports Club ya Paulo Afonso 2004, Maruinense Sporting Club 2006 za Brazil, Churuchill Brothers ya India 2007-2008, Santa Cruz ya PB Brazili, 2009 Flamengo ya Brazili, 2009-2010 Proham  Football Club ya Carribean na 2010 ya New Road Club ya Nepal.

PRISONS WATAKA MECHI YAO NA RUVU PIA IAHIRISHWE

Wachezaji wa Prisons

UONGOZI wa klabu ya Tanzania Prison, umeliomba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuahirisha mechi yao dhidi ya Ruvu Shooting ya Pwani inayotakiwa kufanyika Jumatano ya Oktoba 31, kwenye Uwanja wa Mabatini Mlandizi, Pwani.
Katibu Mkuu wa timu hiyo, Sadiq Jumbe alisema wanaishukuru TFF kwa kuahirisha mchezo wao uliopita dhidi ya Mgambo JKT uliokuwa upigwe kwenye Uwanja wa Mkwakwani jana (Oktoba 27), kufuatia ajali ambayo timu yake ilipata jana.
Alisema sababu kubwa ya kutaka mchezo huo nao uahirishwe ni kutokana na wachezaji wake tegemeo kutokuwa katika hali nzuri, baada ya ajali hiyo.
"Kwa kweli ajali tuliyoipata ni kubwa, kila mtu mawazo yake hayapo, achilia mbali wachezaji walioumia, tunatakiwa tukae muda kutafakari na kuwapa nafasi wachezi walioumia kupumzika na kocha wetu aandae wachezaji watakaochukua namba za waliopata ajali, sasa tunaomba TFF wauahirishe pia mchezo wetu unaofuata dhidi ya Ruvu Shooting," alisema Jumbe.
Wachezaji sita wa Prison waliopata ajali ya basi usiku wa kuamkia Alhamisi iliyopita katika eneo la Hale wilayani Korogwe na kulazwa katika hospitali ya Teule iliyopo wilayani Muheza mkoani Tanga na kisha kuhamishiwa katika hospitali ya mkoa Bombo, wameruhusiwa na hali zao zinaendelea vizuri.
Ajali hiyo ilitokea katika eneo hilo baada ya basi dogo, aina ya Coasta lililowabeba wachezaji na viongozi wa timu hiyo wapatao 21 kuacha njia na kupinduka wakati likiwa njiani kwenda Jijini Tanga.
Hiyo ilifuatia dereva wa gari hilo kushindwa kuumudu usukani, baada ya kumulikwa na mwanga mkali wa taa za lori ambalo lilikuwa mbele yake huku kukiwa na lori lingine pembeni ya barabara limepaki.
Katibu huyo alisema wanamshukuru Mungu kwa kupata nafuuu kwa wachezaji wake na hatimaye kuweza kuruhusiwa kutoka hospitalini ingawa bado wanakabiliwa na majeraha waliyoyapata katika miili yao.
Jumbe ambaye naye aliumia sehemu ya kifuani katika ajali hiyo aliwataja wachezaji walioumia na kukimbizwa hospitalini kabla ya kuruhusiwa ni Issa Mwantika, Lugano  Mwangama, Khalid Fungabreki, Daudi Masungwe ambaye alikuwa amepoteza fahamu na Misango Magai.

 

MAMA CHIKU KUFUNGUA TAIFA CUP KIKAPU TANGA KESHO

Mama Chiku Gallawa

MKUU wa Mkoa wa Tanga, Mama Chiku Gallawa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa michuano ya Kombe la Taifa ya mpira wa Kikapu, Taifa Cup mwaka 2012 yanayotarajiwa kuanza kesho kwenye viwanja vya Mkwakwani na Harbours Club vilivyo jijini Tanga.
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Kikapu Tanga (TRBA), Hamisi Jaffary alisema maandalizi ya mashindano hayo yanaendelea vizuri na waamuzi kumi na mbili ambao watachezesha mashindano hayo tayari wameshawasili jijini hapa tokea mwishoni mwa wiki.
Jaffary alisema mashindano hayo yataanza Octoba 29 na kufikia tamati Novemba 5 mwaka huu na kushirikisha  mikoa mbalimbali hapa nchini ambapo mpaka juzi mikoa kumi na sita ilikwisha kuthibitisha kushiriki mashindano hayo.
Mwenyekiti huyo aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Dar ,Arusha,Moshi,Iringa, Mbeya,Mara, Lindi,Shinyanga,Tabora,Dodoma  na Tanga ambao ndio wenyeji wa mashindano hayo ambapo alisema timu nyengine huenda zitathibitisha katika shirikisho la mipira wa kikapu Taifa ikiwemo Zanzibar ,Unguja na Pemba.
Alisema mkoa  wa Kigoma walijitoa dakika za mwishoni kushiriki mashindano hayo ambayo msimu huu idadi ya washiriki imeongezeka kutokana na kuongezwa kwa idadi ya mikoa.
Mashindano hayo wa mara ya kwanza yalifanyika jijini Tanga 1989 na mara ya mwisho ili kuwa ni 2005 msimu huu shamra shamra zimeonekana kuwa ni muda kubwa kutokana na kuwa maandalizi ya maandalizi yanayofanywa na mikoa shiriki huku viwanja ambazo zitatumika mashindano zimefanyiwa ukarabati wa hali ya juu.
Mkoa wa Tanga unatarajiwa kuwa na wageni watapao 450 ikiwemo wachezaji na viongozi wa timu ambazo zitashiriki michuano hiyo na kutoa wito kwa wakazi wa Tanga kujitokeza kwa wingi kushuhudia michuano hiyo.
Aliongeza kuwa timu  zilianza  kuwasili jijini Tanga tokea Jumamosi na Jumapili ambapo kesho ndio ufunguzi rasmi wa mashindano hayo.

 

AZAM YAZIPANDISHA TENA ULINGONI SIMBA NA YANGA LIGI KUU BARA



YANGA jana imepanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya Azam FC kufungwa na Simba SC mabao 3-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku yenyewe ikishinda 1-0 mjini Arusha dhidi ya wenyeji JKT Oljoro.
Maana yake sasa mwelekeo wa mbio za ubingwa wa ligi hiyo zimegeuka kidogo, Yanga ikiwa inaifukuza Simba sasa kileleni, kwa tofauti ya pointi mbili.
Mwishoni mwa wiki ijayo, Yanga itacheza na Azam FC, mechi ambayo itatengeneza taswira ya namna mzunguko wa kwanza utakavyomalizika.
Azam ikishinda inaweza kurudi nyuma ya Simba SC, lakini tofauti na hapo watu watasubiri kuona kati ya watani hao wa jadi, nani atamaliza mzunguko wa kwanza akiwa kileleni.    
Kabla ya kucheza na Azam, Yanga itacheza Mgambo Shooting Jumatano, wakati Azam itacheza na Coastal Union Chamazi.
Ligi Kuu sasa inazidi kunoga baada ya jana Simba kuzinduka kutoka kwenye wimbi la sare, baada ya kufanikiwa kuichapa Azam FC mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi huo, unaifanya Simba izidi kujitanua kileleni mwa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 22, baada ya kucheza mechi 10, wakati Azam FC inapromoka hadi nafasi ya tatu kwa pointi zake 18, baada ya kucheza mechi tisa, ikiipisha Yanga nafasi ya pili, ambayo imetimiza pointi 20 baada ya kuifunga JKT Oljoro.
Mabao ya Simba jana yalitiwa kimiani na Emanuel Arnold Okwi mawili na Felix Mumba Sunzu Jr. moja, wakati la Azam lilifungwa na John Raphael Bocco ‘Adebayor’.
Hadi mapumziko, tayari Simba walikuwa mbele kwa mabao 2-1, Azam wakitangulia kufunga dakika ya nne, kupitia kwa Adebayor ambaye alimtoka beki Mkenya Paschal Ochieng na kumchambua Juma Kaseja.
Dakika mbili baadaye, Sunzu aliisawazishia Simba, akiunganisha kwa kichwa krosi maridadi ya Mrisho Khalfan Ngassa kutoka wingi ya kulia.
Okwi aliifungia Simba bao la pili dakika ya 40, baada ya kutokea kizaazaa langoni mwa Azam kufuatia mpira uliopigwa langoni mwa timu hiyo na Mwinyi Kazimoto.     
Kipindi cha pili Simba walirudi na moto wao na iliwachukua dakika tano tu kuhitimisha karamu yao ya mabao, baada ya Okwi kuwainua tena vitini mashabiki wa Simba, akifumua shuti la umbali wa mita 19, baada ya kuwatoka mabeki wa Azam.
Mrisho Ngassa ndiye alikuwa nyota wa mchezo wa jana, kutokana na kuisumbua mno Azam, iliyomuuza kwa mkopo Simba miezi miwili iliyopita.
Kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha, Yanga iliibuka na ushindi wa 1-0, bao pekee la beki Mbuyu Twite, hilo likiwa bao lake la tatu tangu ajiunge na timu hiyo kwenye ligi hiyo.
Kwa ushindi huo, Yanga imetimiza pointi 20, baada ya kucheza mechi 10 na kupanda nafasi ya pili.
Mechi nyingine za ligi hiyo jana, African Lyon ilitoka sare ya 1-1 Kagera Sugar Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam na Ruvu Shooting ikaifunga 2-1 Polisi Morogoro Uwanja wa Mabatini, Mlandizi.
Mechi kati ya Mgambo JKT na Prisons iliyokuwa ichezawe jana Uwanja wa Mkwakwani, Tanga imeahirshwa kutokana na wachezaji wa Prisons kupata ajali wakiwa njiani kuelekea Tanga.
Ligi hiyo itaendelea leo kwa michezo miwili kati ya JKT Ruvu na Coastal Union Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam na Toto Africans dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

MBUYU TWITE ADHIHIRISHA THAMANI YAKE YANGA


NI beki, lakini anawazidi washambuliaji kwa kufunga mabao. Huyu ni Mbuyu Twite Banza, beki aliyesajiliwa msimu huu Yanga, kutoka APR ya Rwanda, ambaye jana alifunga bao lake la tatu katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Pamoja na kufanya kazi nzuri ya ulinzi, akicheza beki ya kati kwa pamoja na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ katika kipindi hiki ambacho Kevin Yondan anauguza goti aliloumizwa na Haruna Moshi ‘Boban’, Oktoba 3, mwaka huu, Twite anasaidia sana na mashambulizi pia.
Hupanda kusaidia mashambulizi na kutoa pasi nzuri, lakini pia huyo ndiye tegemeo la Yanga katika mipira ya adhabu hivi sasa.
Ana mashuti makali na ndiyo maana kocha Mholanzi, Ernie Brandts ameamua kumfanya mtaalamu wake wa mipira iliyokufa.
Wakati Yanga wanafurahia matunda ya Twite, wazi wapinzani wao wa jadi, Simba SC watakuwa wanaumia sana kumuona kijana huyo mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) akipiga mzigo wa uhakika Jangwani.
Kwa nini waumie? Simba SC ndio waliokuwa wa kwanza kumsajili Twite baada ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame- wakimtuma Mwenyekiti wao, Alhaj Ismail Aden Rage kwenda kukamilisha usajili wake Kigali, Rwanda.
Rage alikutana na Twite, wakazungumza na kukubaliana, akampa fedha dola za Kimarekani 30,000 na nyingine 1,000 kwa ajili ya tiketi ya kuja Dar es Salaam. Rage alipogeuka tu, Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Abdallah Ahmad Bin Kleb akamfuata Twite.
Bin Kleb akafanikiwa kumbadili mawazo Twite na kuamua kurudisha fedha za Simba, ili aje Yanga, ingawa kidogo umafia ulitumika hapo.
Hadi leo Simba wanadai fedha zao walizompa Twite na tayari TFF imeitaka Yanga irudishe fedha hizo.
Sahau kuhusu yote yaliyopita, kitu ambacho Yanga wanajivunia kwa sasa ni kwamba, Mbuyu Twite ameanza kurudisha gharama zao za usajili.
OKWI AJIBU TUHUMA SIMBA NA KUTENGENEZA UGALI WA MAANA MKATABA MPYA SIMBA


MABAO mawili aliyofunga mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi jana katika mechi dhidi ya Azam FC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana yanamaanisha mambo mawili makubwa kwake.
Kwanza yamemsafisha mbele ya mashabiki wa timu hiyo, kufuatia tuhuma za aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Kassim Mohamed Dewji kwamba haitumikii kwa moyo safi klabu hiyo na pia yamepandisha thamani yake katika kipindi hiki cha mazungumzo ya kusaini mkataba mpya.
Mzambia Felix Sunzu ndiye anayelipwa mshahara mkubwa zaidi Simba SC, Sh. Milioni 5 na Okwi anayelipwa Sh. Milioni 2 anataka alipwe zaidi kwa sababu anaamini ndiye anayeibeba zaidi timu hiyo.
Baada ya mechi ya jana, gumzo kubwa kwa mashabiki wa Simba lilikuwa ni bao la pili alilofunga Okwi- kwamba lilikuwa zuri mno na wanaamini hakubahatisha, kwa sababu amekuwa akifunga mabao kama hayo mara kadhaa.  
Pamoja na hayo, katikati zilibuliwa tuhuma kwamba Okwi ana mapenzi na Yanga na amekuwa akiihujumu timu hiyo- huku habari nyingine zikisema anataka kwenda Azam.
Okwi hakuwahi kuibuka kujibu tuhuma hizo, lakini shughuli yake ya jana ni sawa na majibu, kwani mabao hayo pamoja na kuidhuru Azam, lakini yameifanya Simba ijichimbie kileleni na kuwaacha wapinzani wao, Yanga.
Okwi pia anawapelekea ujumbe viongozi wa Simba kwa mabao yake ya jana, waache kusikiliza maneno ya mitaani na kukumbuka wajibu wao kama viongozi kwa kujitofautisha na mashabiki.


BONIFACE WAMBURA AURA TENA



Boniface Eambura ambaye kwa sasa ndiye Menyekiti wa kamatiu ya Viwango ya Chama cha Ngumi za Kulipwa la Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBA) ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya Viwango ya ECAPBA.
Kwa sasa Boniface Wamnura ni mwenyekiti wa Kamati ya Viwango ya Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC).
Akiwa mtaalam wa uandishi wa habari ambako amefanya kazi kama mwandishi mwandamizi na mhariri kweney vyombo mbalimbali vya habari, Wambura anategemea kuleta ujuzi wake wa mawasiliano kweney shirikisho hili linalokuwa kwa kasi sana katima ukanda huu wa Afrika ya Mashariki na Kati.
Wambura anategemea kuongoza kamati ya watu watano (5) yenye jukumu la kuandaa na kuenndeleza orodha ya viwango vya mabondia toika nchi za Afrika ya Mashariki na Kati.
Baadhi ay wajumbe wanaounda Kamati ya Viwango ya ECAPBA ni pamoja na Simon Mukisa Katogole wa Uganda na Steven Okumu toka Kenya.


MECHI YA MAHASIMU YA LUPOPO NA MAZEMBE YASOGEZWA MBELE KUTOKANA NA VURUGU.

WATU watano wakiwemo polisi wawili wameumia vibaya wakati vurugu zilipozuka kabla ya mchezo wa Jumamosi jijini Lubumbashi ambao unawakutanisha mahasimu wawili timu za Saint-Eloi Lupopo na TP Mazembe mchezo ambao uliahirishwa kutokana na vurugu hizo.  

Taarifa ya polisi imesema kuwa maofisa wawili wa polisi na mashabiki watatu ndio walioumia sana lakini wapo mashabiki wengine wengi ambao walipata majeraha ya kawaida katika kdhia hiyo. 

 Mashuhuda wanasema kuwa vurugu hizo zilizuka wakati mashabiki wa timu zote mbili walipoanza kurushiana mawe kabla ya polisi kuingilia na kuwarushia mabomu ya machozi ili kujaribu kutuliza vurugu hizo.

 Matukio ya vurugu sasa imeonekana kuwa kama tabia za kawaida kwa mashabiki wa soka barani Afrika baada ya kutokea kwa matukio ya aina hiyo mara kwa mara huku mengine yakichukua maisha ya watu.

LIGI ULAYA: AC Milan yajikongoja, Barca yafumua 5-0!


EL_SHAARAWY-AC_MILANKatika Ligi ya Italy, Serie A, AC Milan, jana walijitutumua na kuifunga Genoa Bao 1-0 na huko Spain, kwenye La Liga, vinara Barcelona, wakicheza ugenini Estadio Teresa Rivero, waliitwanga Rayo Vallecano Bao 5-0.
SERIE A
MATOKEO:
Jumamosi Oktoba 27
Siena 0 Palermo 0
AC Milan 1 Genoa 0
++++++++++++++++++++++++++++++
Mchezaji wa AC Milan Stephan El Shaarawy jana alisherehekea Bethdei yake ya kutimiza Miaka 20 kwa kufunga Bao la Kipindi cha Pili ambalo liliipa AC Milan ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Genoa.
Ushindi huo umeifanya AC Milan iwe na Pointi 10 kwa Mechi 9 wakiwa Pointi 12 nyuma ya Mabingwa na vinara Juventus ambao leo wanacheza ugenini na Catania.
RATIBA:
Jumapili Oktoba 28
Catania v Juventus [Stadio Angelo Massimino]
Bologna v Inter Milan [Stadio Renato Della`Ara]
Fiorentina v Lazio [Stadio Artemio Franchi]
Sampdoria v Cagliari [Comunale Luigi Ferraris]
Torino v Parma [Stadio Olimpico Grande Torino]
US Pescara v Atalanta [Adriatico]
AS Roma v Udinese           [Stadio Olimpico]
Napoli v Chievo Verona [Stadio San Paolo]
++++++++++++++++++++++++++++++

LA LIGA:
MATOKEO:
Jumamosi Oktoba 27
Espanyol 0 Málaga 0
Real Betis 1 Valencia 0
Celta Vigo 1 Deportivo La Coruña 1
Rayo Vallecano 0 Barcelona 5
++++++++++++++++++++++++++++++
Wakicheza ugenini, huko Estadio Teresa Rivero, Barcelona, ambao wanaongoza La Liga, waliendelea kujichimbia kileleni baada ya kuishindilia Rayo Vallecano Ba0 5-0.
MAGOLI:
-David Villa, Dakika ya 20
-Lionel Messi, 48
-Xavi, 79
-Fabregas, 80
-Lionel Messi, 89
RATIBA:
Jumapili Oktoba 28
Athletic Bilbao v  Getafe [Estadio San Mamés]
Atlético Madrid v Osasuna [Vicente Calderon]
Levante v Granada [Ciudad de Valencia]
Mallorca v Real Madrid [Estadio Son Moix] [SAA 5 na Nusu Usiku]
Real Zaragoza v Sevilla FC [Estadio La Romareda]
Jumatatu Oktoba 29
Valladolid v Real Sociedad [Estadio Nuevo José Zorrilla]

NI MTANANGE JUMAPILI: Chelsea v Man United!


>>MAN UNITED WAMEIFUNGA Chelsea Mechi 4, SARE 1 katika MECHI 5 za mwisho!
>>CHELSEA hawajafungwa na Man United Stamford Bridge tangu 2002 walipobamizwa 3-0!!
Jumapili Oktoba 28, Uwanja wa Stamford Bridge utashuhudia Mechi kali ya Ligi Kuu England, hakika ni BIGI MECHI, kati ya vinara wa Ligi Chelsea na Manchester United, ambayo bila shaka itatoa mwanga mkubwa kuhusu mbio za Ubingwa Msimu hu.
++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumapili, Oktoba 28, 2012
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Everton v Liverpool
[SAA 12 Jioni]
Newcastle United v West Bromwich Albion
Southampton v Tottenham Hotspur
[SAA 1 Usiku]
Chelsea v Manchester United
++++++++++++++++++++++
Kimsimamo kwenye Ligi, Chelsea wapo Pointi 4 mbele ya Man United ambao wako nafasi ya 3 na nafasi ya pili ipo kwa Man City, waliocheza Mechi moja zaidi, baada ya Jumamosi Oktoba 27, kuifunga Swansea City bao 1-0.
+++++++++++++++++
MSIMAMO Timu za Juu:
1 Chelsea  Mechi 8 Pointi 22
2 Man City  Mechi 9 Pointi 21
3 Man United  Mechi 8 Pointi 18
4 Arsenal  Mechi 9 Pointi 15
5 Everton  Mechi 8 Pointi 15
6 Fulham  Mechi 9 Pointi 14
7 Tottenham  Mechi 8 Pointi 14
8 West Brom  Mechi 8 Pointi 14
9 West Ham  Mechi 9 Pointi 14
10 Swansea  Mechi 9 Pointi 11
+++++++++++++++++
Chelsea wataingia kwenye Mechi hii ya Jumapili bila ya Wakongwe wao, Nahodha John Terry na Frank Lampard, kwa sababu Terry yupo Kifungo cha Mechi 4 na Lampard ameumia mguu na yupo nje kwa Wiki 2.
Man United watamkosa Kiungo Shinji Kagawa amabe ameumia goti.
++++++++++++++++++++++
REKODI-Uso kwa Uso: CHELSEA v MAN UNITED:
-Kwenye Ligi Kuu, Klabu hizi zimekutana mara 40 na Chelsea wameshinda mara 13 na Man United mara 12 na kila Timu imefunga Bao 53. Chelsea ndio Timu pekee ambayo imeifunga Man United mara nyingi katika Ligi Kuu.
-Chelsea hawajafungwa na Man United Uwanjani Stamford Bridge tangu Aprili 2002 walipochapwa 3-0.
-Man United hawajafungwa katika Mechi 5 zilizopita dhidi ya Chelsea wakiwa wameshinda Mechi 4 na Sare 1.
++++++++++++++++++++++
VIKOSI VINATARAJIWA:
SQUADS-CHELSEA_v_MAN_UNITED
WAAMUZI:
Refa: M Clattenburg
Refa Wasaidizi: M McDonough, S Long
Refa wa Akiba: M Jones
FAHAMU:
-Refa Clattenburg Msimu huu amechezesha Mechi 6 za Ligi Kuu England na ametoa KADI NYEKUNDU 2 na KADI za NJANO 24.
-MARA ya MWISHO Clattenburg kuichezesha Man United ilipigwa Bao 6-1 na Man City na alimpa KADI NYEKUNDU Jonny Evans.
 

BPL: Man City yakamata nafasi ya 2!


>>MECHI YAWEKA REKODI KWA MUDA WA NYONGEZA DAKIKA 12!!
BPL_LOGOMabingwa watetezi wa Ligi Kuu England, Manchester City, leo wakiwa kwao Uwanja wa Etihad wamepata ushindi wa bao 1-0 walipoifunga Swansea City katika Mechi ambayo kiwango chao kilikuwa si cha kuridhisha ambacho kiliwafanya baadhi ya Mashabiki wao kuwazomea lakini ushindi huo umewafanya wakamate nafasi ya pili katika Msimamo wa Ligi wakiwa Pointi moja nyuma ya vinara Chelsea ingawa wao wamecheza Mechi moja zaidi.

Bao la ushindi la Man City lilifungwa na Carlos Tevez katika Dakika ya 62 kwa shuti kali.
Mechi hii iliingia dosari kwa kuumia, inadhaniwa vibaya, kwa Kipa wa Swansea Michel Vorm na Beki wa Man City Micah Richards hali ambayo ilifanya Mechi hii ipewe muda wa nyongeza wa Dakika 12 ukiwa ni muda mrefu zaidi kupita Mechi yeyote katika historia ya Ligi Kuu England.
VIKOSI:
Man City: Hart, Richards, Nastasic, Kompany, Clichy, Nasri, Toure, Barry, Kolarov, Tevez, Aguero
Akiba: Pantilimon, Lescott, Toure, Evans, Sinclair, Dzeko, Balotelli.
Swansea: Vorm, Rangel, Chico, Williams, Davies, Ki, Routledge, Britton, de Guzman, Hernandez, Michu
Akiba: Tremmel, Dyer, Graham, Monk, Shechter, Tiendalli, Agustien.
Refa: Martin Atkinson
++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumapili, Oktoba 28, 2012
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Everton v Liverpool
[SAA 12 Jioni]
Newcastle United v West Bromwich Albion
Southampton v Tottenham Hotspur
[SAA 1 Usiku]
Chelsea v Manchester United
++++++++++++++++++++++

DABI ya LIVERPOOL: DAVID MOYES amuonya LUIS SUAREZ


>>MOYES ataka Refa awe makini nae!!!
 
Luis Suarez
>>RODGERS aonya kuhusu KADI NYEKUNDU!!
>>DABI HII INATAWALA KWA NYEKUNDU-20!!
FELLAINIBosi wa Everton, David Moyes, amemuonya Straika wa Liverpool Luis Suarez asilete vitimbwi vyake na kuivuruga Dabi ya Jiji la Liverpool itakayochezwa Jumapili Oktoba 28 Uwanja wa Goodison Park kati ya Mahasimu Everton na Liverpool kwenye Mechi ya Ligi Kuu England, BPL.
Hivi karibuni, Straika huyo wa Liverpool anaetoka Uruguay amekuwa akisakamwa kwa tabia yake ya kuhadaa Marefa kwa kujidondosha makusudi ili kupata Penati na mmoja walioponda tabia ya Suarez ni Meneja wa Stoke City Tony Pulis na hilo limemfanya Moyes amtake Refa wa Dabi hiyo ya Jumapili, Andre Marriner, awe makini.
+++++++++++++++++++++++++++++++++
FAHAMU: Tangu enzi hii ni mojawapo ya Dabi inayoheshimika Duniani yenye ushindani mkali na hii ni Dabi ya 219 ambapo Liverpool wameshinda mara 87, Everton mara 66 na sare 65.
+++++++++++++++++++++++++++++++++
Moyes amesema: “Nina wasiwasi na Suarez kwa sababu ana historia hiyo. Lakini mimi si Refa. Lakini tabia yake inawakera Mashabiki, watasusa Mechi. Ni ngumu kwa Marefa.”
Hata hivyo, Moyes ametaka Wachezaji wanaohadaa Marefa kwa kujiangusha kusudi wafungiwe.
Moyes ametamka: “Sidhani kama wapo Wachezaji wengi wenye tabia hii. Kuwafungia? Ukiwafungia hili tatizo litaondoka”
Nae Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers, pia amemtaka Refa Andre Marriner awe makini hasa kwa vile Dabi ya Liverpool imekuwa ikitawaliwa na Kadi Nyekundu.
Dabi hii ndio inaongoza kwa Kadi Nyekundu nyingi kupita Mechi yeyote ya Ligi Kuu tangu Ligi Kuu England ianzishwe kwa kutolewa Kadi Nyekundu 20 zikiwa 6 zaidi ya Mechi yeyote ile katika historia hiyo.


 

NITAKUWA MVUMULIVU KWA WILSHERE - WENGER.

MENEJA wa Arsenal Arsene Wenger amesema atakuwa mvumilivu juu ya ujio Jack Wilshere baada ya kiungo huyo kucheza mechi yake ya kwanza baada ya miezi 17 wakati timu hiyo ilipopata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Queens Park Rangers jana.

 Wilshere ambaye alikuwa nje ya uwanja kutokana na kusumbuliwa na kifundo cha mguu alicheza kwa dakika 67 katika mchezo huo uliochezwa katika Uwanja wa Emirates baada ya kupangwa katika kikosi cha kwanza pasipo kutegemewa na Wenger.

 Wenger alionyesha kufurahishwa na kiwango alichokionyesha mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza baada ya kuweka wazi kuwa hakumwambia Wilshere kama atacheza mchezo huo mpaka asubuhi.  

Kocha huyo aliendelea kusema kuwa atakuwa akimtumia mchezaji huyo kwa tahadhari wakati akiendelea kurejea katika kiwango chake cha kawaida na amemuondoa katika kikosi chake kitakachocheza mchezo wa Kombe la Ligi dhidi Reading katikati ya wiki hii.

BUNDESLIGA: Mabingwa Dortmund wapata ushindi wa kwanza ugenini!


DORTMUND_BARAFUNIMabingwa watetezi wa Germany, Borussia Dortmund, leo wamepata ushindi wao wa kwanza wa ugenini wa Msimu huu walipoifunga Freiburg kwenye Uwanja uliojaa barafu, ushindi ambao umewaweka nafasi ya 4 wakiwa Pointi 9 nyuma ya vinara Bayern Munich wenye Mechi moja mkononi.
+++++++++++++++++++
MSIMAMO-Timu za Juu:
1 Bayern Munich Mechi 8 Pointi 24
2 Schalke Mechi 9 Pointi 20
3 Eintracht Frankfurt Mechi 8 Pointi 19
4 Borussia Dortmund Mechi 9 Pointi 15
5 Mainz Mechi 9 Pointi 14
+++++++++++++++++++
Bao za ushindi za Dortmund, ambao majuzi waliitwanga Real madrid bao 2-1 katika Mechi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, zilifungwa Kipindi cha Pili na Neven Subotic na Mario Goetze.
Katika Mechi nyingine za Bundesliga, Schalke wamechupa hadi nafasi ya pili baada ya kuifunga 1-0 Nuremberg.
MATOKEO/RATIBA:
Ijumaa Oktoba 26
Augsburg 0 Hamburger 2
Jumamosi Oktoba 27
Schalke 1 Nuremberg 0
Freiburg 0 Borussia Dortmund 2
Mainz 3 Hoffenheim 0
SpVgg Gr, Furth 1 Werder Bremen 1
Fortuna Dusseldorf 1 VfL Wolfsburg 4
Jumapili Oktoba 28
VfB Stuttgart v Eintracht Frankfurt
Bayern Munich v Bayer 04 Leverkusen
Hannover 96 v Borussia Mönchengladbach

 

BPL: Arsenal, Wigan zazinduka!!


BPL_LOGOKatika mfululizo wa Mechi za Ligi Kuu England, BPL, Arsenal leo imefuta machungu ya kufungwa katika Mechi zao mbili zilizopita na kufanikiwa kuichapa QPR bao 1-0 na Timu nyingine pekee iliyoshinda katika Mechi zilizochezwa mapema leo ni Wigan ambayo imeichapa West Ham bao 2-1 huku Mechi nyingine tatu zikimalizika kwa sare.
++++++++++++++++++++++
MATOKEO:
Jumamosi, Oktoba 27, 2012
Aston Villa 1 Norwich City 1
Arsenal 1 Queens Park Rangers 0
Reading 3 Fulham 3
Stoke City 0 Sunderland 0
Wigan Athletic 2 West Ham United 1
++++++++++++++++++++++
Wigan 2 West Ham 1
LEO Wigan wamefanikiwa kupata ushindi wao wa kwanza wa nyumbani kwa Msimu huu walipoifunga West Ham bao 2-1 kwa bao za Ivan Ramis na James McArthur.
Bao pekee la West Ham lilifungwa na James Tomkins katika Dakika ya 90.
VIKOSI:
Wigan: Al Habsi, Ramis, Caldwell, Figueroa, Boyce, McCarthy, McArthur, Beausejour, Kone, Di Santo, Maloney
Akiba: Pollitt, Jones, Watson, Gomez, McManaman, Boselli, Stam.
West Ham: Jaaskelainen, Tomkins, Collins, Reid, McCartney, Jarvis, Noble, Nolan, Diame, Benayoun, Carroll
Akiba: Spiegel, Cole, Maiga, O'Brien, O'Neil, Chambers, Hall.
Refa: Jon Moss
++++++++++++++++++++++
Reading 3 Fulham 3
Goli la Dakika ya mwisho la Hal Robson-Kanu limewanusuru Reading na kuwafanya wapate sare ya bao 3-3 na Fulham.
=================
MAGOLI:
Reading
-Leigertwood  Dakika ya 26′
-McCleary 85′
-Robson-Kanu 90′ .
Fulham
-Ruiz 61′
-Baird 77′
-Berbatov 88′
=================
VIKOSI:
Reading: McCarthy, Cummings, Gorkss, Mariappa, Shorey, Pogrebnyak, Tabb, Leigertwood, Kebe, McAnuff, Roberts
Akiba: Federici, Gunter, Pearce, Le Fondre, Hunt, McCleary, Robson-Kanu.
Fulham: Schwarzer, Riether, Hughes, Hangeland, Riise, Duff, Baird, Diarra, Richardson, Rodallega, Berbatov
Akiba: Stockdale, Senderos, Sidwell, Petric, Ruiz, Karagounis, Dejagah.
Refa: Mike Jones
++++++++++++++++++++++
Stoke City 0 Sunderland 0
Ni Mechi ambayo Stoke City walicheza vyema lakini Sunderland walinyimwa Penati ya wazi baada ya Beki wao Robert Huth kuunawa mpira wa Steven Fletcher na mwishowe matokeo yakabaki 0-0.
VIKOSI:
Stoke: Begovic, Cameron, Shawcross, Huth, Wilson, Kightly, Whitehead, Adam, Nzonzi, Walters, Crouch
Akiba: Sorensen, Jones, Owen, Upson, Etherington, Wilkinson, Palacios.
Sunderland: Mignolet, Gardner, O'Shea, Cuellar, Rose, Larsson, Cattermole, Colback, Johnson, McClean, Fletcher
Akiba: Westwood, Bardsley, Campbell, Kilgallon, Vaughan, Saha, Sessegnon.
Refa: Mark Halsey
++++++++++++++++++++++
Arsenal 1 QPR 0
Bao la Dakika ya 84 la Mikel Arteta limewapa Arsenal ushindi wa bao 1-0 na kuwafanya wachupe hadi nafasi ya 4 katika Msimamo wa Ligi.
Licha ya ushindi, Arsenal pia walipata raha baada ya kumuona Kiungo wao Jack Wilshere akianza Mechi yake ya kwanza baada ya Miezi 17 alipokuwa ni majeruhi.
VIKOSI:
Arsenal: Mannone, Sagna, Mertesacker, Vermaelen, Andre Santos, Arteta, Wilshere, Cazorla, Ramsey, Podolski, Giroud
Akiba: Martinez, Koscielny, Walcott, Coquelin, Arshavin, Jenkinson, Gervinho.
QPR: Julio Cesar, Bosingwa, Mbia, Nelsen, Traore, Wright-Phillips, Diakite, Granero, Hoilett, Taarabt, Zamora
Akiba: Green, Ferdinand, Cisse, Mackie, Onuoha, Ephraim, Faurlin.
Refa: Anthony Taylor
++++++++++++++++++++++
Aston Villa 1 Norwich 1
Katika Mechi iliyoanza mapema huko Villa Park, Aston Villa ilitoka sare ya bao 1-1 na Norwich City.
Aston Villa, ambao wako chini ya Meneja Paul Lambert ambae aliondoka kwa uhasama Norwich City na kuhamia Villa, walitangulia kupata bao alilofunga Christian Benteke katika Kipindi cha Kwanza.
Dakika 7 baada ya Kipindi cha Pili kuanza, Villa walipata pigo alipotolewa kwa Kadi Nyekundu Mchezaji wao Joe Bennett baada kupata Kadi za Njano mbili.
Mwanya huo uliwapa nafasi Norwich kulisakama lango la Villa hadi waliposawazisha katika Dakika ya 79 kwa kichwa cha Michael Turner.
VIKOSI:
Aston Villa: Guzan, Herd, Vlaar, Lowton, Bennett, Albrighton, El Ahmadi, Holman, Delph, Agbonlahor, Benteke
Akiba: Given, Ireland, Bent, Westwood, Bannan, Weimann, Lichaj.
Norwich: Ruddy, Russell Martin, Bassong, Turner, Garrido, Elliott Bennett, Tettey, Johnson, Pilkington, Hoolahan, Holt
Akiba: Rudd, Snodgrass, Howson, Jackson, Morison, Barnett, Ryan Bennett.
Refa: Phil Dowd
++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumamosi, Oktoba 27, 2012
[SAA 12 na Nusu Jioni]
Manchester City v Swansea City
Jumapili, Oktoba 28, 2012
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Everton v Liverpool
[SAA 12 Jioni]
Newcastle United v West Bromwich Albion
Southampton v Tottenham Hotspur
[SAA 1 Usiku]
Chelsea v Manchester United


LORENZO BINGWA MICHUANO YA MOTOGP.

DEREVA nyota wa mashindano ya pikipiki, Jorge Lorenzo amejiweka katika nafasi nzuri ya kunyakuwa taji la pili la dunia la michuano ya MotoGP baada ya kumaliza katika nafasi ya pili ya michuano ya Australian GP. 
 
 Casey Stoner wa Autralia ndio aliyeshinda mbio hizo zilizofanyika katika kisiwa cha Philip kwa mara sita mfululizo lakini dereva mwenzake kutoka timu ya Respol Honda, Dani Pedrosa akipata ajali katikati ya mashindano hayo.  
 
Pedrosa ambaye alikuwa akihitaji kumaliza mbele ya mhispania mwenzake Lorenzo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kunyakuwa taji la dunia katika mashindano hayo ya mwisho kwa maka huu alipata ajali katika mzunguko wa pili. Lorenzo ambaye ni dereva wa Yamaha mara ya kwanza alishinda taji la dunia mwaka 2010.

WILLIAMS, SHARAPOVA KUKWAANA FAINALI WTA.

WANADADA nyota wa mchezo wa tenisi, Serena Williams na Maria Sharapova wanatarajiwa kukutana katika mchezo wa fainali ya michuano ya WTA jijini Istanbul baadae leo. 
 
 Williams kutoka Marekani ambaye anashika namba tatu katika orodha za ubora duniani kwa upande wanawake alifanikiwa kutinga fainali baada ya kumfunga Agnieska Radwanska kwa 6-2 6-1 akitumia muda wa dakika 61. Sharapova ambaye anashika namba mbili alifanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kumfunga mwanadada namba moja katika orodha hizo Victoria Azarenka kwa 6-4 6-2. 
 
 Azarenka ambaye alijihakikishia nafasi ya kumaliza mwaka akiwa katika namba moja baada ya kumfunga Li Na wa China katika mchezo huo alionekana kupata majeraha katika mguu wake kulia hivyo kushindwa kuhimili vishindo vya mpinzani wake.
 
 Sharapova bingwa wa michuano ya wazi ya Ufaransa leo aaingia uwanjani akitafuta taji lake la pili la michuano hiyo ambayo mara ya mwisho alinyakuwa mwaka 2004 lakini atakumbana na wakati mgumu kwa Williams ambaye ameshinda taji hilo mara sita na sasa yuko katika kiwango cha juu kabisa.