Tuesday, January 8, 2013

CAPITAL ONE CUP: TIMU YA DARAJA LA CHINI BRADFORD 3 VILLA 1

>>WABABE WA ARSENAL WACHUNGULIA FAINALI WEMBLEY!
>>LEO NUSU FAINALI: CHELSEA v SWANSEA!!
CAPITAL_ONE_CUP-BESTBradford City jana imejiwekea daraja zuri la kutinga Fainali ya CAPITAL ONE CUP baada ya kuichapa Aston Villa Mabao 3-1 Uwanjani Valley Parade katika Mechi ya kwanza ya Nusu Fainali na Timu hizi zitarudiana huko Villa Park hapo Januari 22.
Bradford, ambao wapo Ligi 2 wakiwa nafasi 60 chini ya Aston Villa walio Ligi Kuu England, kwenye Robo Fainali waliibwaga nje Arsenal kwa Penati 3-2 baada kutoka sare 1-1.

MAGOLI:
Bradford 3
-Wells Dakika ya 19
-McArdle 77
-McHugh 88
Aston Villa 1
-Weimann 82

Hadi mapumziko, Bradford walikuwa mbele kwa Bao 1-0 kwa Bao la Nahki Wells huku Kipa wao, Matt Duke, akiokoa michomo baada ya michomo kutoka kwa Aston Villa na hasa Christian Benteke.

DONDOO za LIGI CUP:
-Aston Villa wameshinda Kombe hili mara 5 mara ya mwisho ni 1996
-Chelsea wameshinda mara 5 ikiwa ni pamoja na 2005 na 2007
-Bradford na Swansea hawajawahi kutwaa Kombe hili.

Ikiwa Bradford watatinga Fainali, watakuwa Klabu ya kwanza kutoka Madaraja ya chini kuingia Fainali tangu Rochdale ilivyofanya hivyo Mwaka 1962.
Leo huko Stamford Bridge, Chelsea wataikaribisha Swansea City katika Mechi ya kwanza ya Nusu Fainali nyingine.
VIKOSI:
Bradford City: Duke, Darby, McHugh, McArdle, Good, Atkinson, Jones, Doyle, Hanson, Hines (Turgott - 65' ), Wells
Akiba: McLaughlin, Ravenhill, Reid, Jones, Turgott, Hannah, Connell
Aston Villa: Given, Clark, Bennett, Baker, Lowton, N'Zogbia, Delph, Bannan, Agbonlahor (Bent - 57' ), Benteke, Weimann
Akiba: Guzan, Stevens, Lichaj, Ireland, Carruthers, Bent (Burke - 85' ), Burke
Refa: Howard Webb
RATIBA/MATOKEO:
NUSU FAINALI
[Mechi zote kuanza SAA 4 DAK 45 Usiku]
Jumanne Januari 8
Bradford 3 Aston Villa 1
Jumatano Januari 9
Chelsea v Swansea City
MARUDIANO
Jumanne Januari 22
Aston Villa v Bradford
Jumatano Januari 23
Swansea City v Chelsea
FAINALI
Jumapili Februari 24
Uwanja wa Wembley, London

COPA DEL REY: MALAGA, VALENCIA ROBO FAINALI! COPPA ITALIA: LAZIO IPO NUSU FAINALI!LLEO NI BALAAA TUPU MCHEZAJI BORA DUNIA UWANJAN NA PIA MCHEZAJI MWENYE MAWAZO MENGI KWA SASA CR NAYE ATAKUWA DIMBANI

BARCA_v_REAL>>LEO VIGOGO BARCA DIMBANI, REAL KUMEKUCHA, JUVE KUIVAA AC MILAN!!
HUKO Spain na Italy jana zilichezwa Mechi za Makombe makubwa katika Nchi hizo, Copa del Rey kwa Spain na COPPA ITALIA kwa Italy, lakini leo zile Timu Vigogo ndio zitakuwa Uwanjani kucheza Mechi zao na huko Spain macho yapo kwa Real Madrid kama wataweza kupindua kipigo cha 2-1 walichopewa katika Mechi ya kwanza na Celta Vigo ili wasonge mbele lakini huko Italy macho yapo kwenye Mechi kati ya Juventus na AC Milan.
COPA del REY

COPA del REY
RAUNDI ya 4
MATOKEO:
Jumanne Januari 8
[Jumla ya Magoli kwa Mechi 2 katika Mabano]
Valencia 2 Osasuna 1 [4-1]
Malaga 4 Eibar 1 [5-2]

Malaga walibomoa Eibar Bao 4-1 na kuingia Robo Fainali ya Copa del Rey kwa jumla ya Mabao 5-2.
Valencia nao wametinga Robo Fainali baada ya kuifunga Osasuna Bao 2-1 na kusonga kwa jumla ya Mabao 4-1.
MECHI za MARUDIANO
[Matokeo Mechi ya kwanza katika Mabano]
Jumatano Januari 9
Sevilla v Real Mallorca [5-0]
Real Madrid v Celta Vigo [1-2]
Real Zaragoza v Levante [1-0]
Alhamisi Januari 10
Getafe v Atletico Madrid [0-3]
Barcelona v Cordoba [2-0]
Real Betis v Las Palmas [1-1]
COPPA ITALIA

ITALIAN CUP
ROBO FAINALI
MATOKEO:
Jumanne Januari 8
SS Lazio 3 Catania 0

Lazio wamefuzu kuingia Nusu Fainali ya Coppa Italia baada ya kuichapa Catania Bao 3-0.
Lazio, ambao walifunga Bao zao kupitia Stefan Radu na Bao mbili za Hernanes, kwenye Nusu Fainali watacheza na Mshindi kati ya Juventus au AC Milan ambao wanacheza leo.
ITALIAN CUP
ROBO FAINALI
RATIBA:
Jumatano Januari 9
Juventus v AC Milan
Jumanne Januari 15
Inter Milan v Bologna
Jumatano Januari 16
Fiorentina v AS Roma

SIMBA SC WAPAA OMAN LEO, WAACHA KIKOSI TISHIO MAPINDUZI


Simba SC
MABINGWA wa Bara, Simba SC wanatarajiwa kuondoka leo Dar es Salaam kwenda Oman kuweka kambi ya wiki mbili kujiandaa na Ligi Kuu pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika. 
Kuhusu Kombe la Mapinduzi, Simba imegawa vikosi viwili na kile ambacho kilichukua Kombe la Sup8R Banc ABC kwa kuzifunga Azam FC na Mtibwa Sugar ndicho kitabaki kwenye Kombe la Mapinduzi chini ya kocha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ na Mganda Richard Hamatre.
Kikosi hicho cha Mapinduzi kina wakali kama Ramadhan Singano ‘Messi’, Edward Christopher, Abdallah Seseme, Haruna Chanongo, Hassan Isihaka, Hassan Hatibu, Miraj Adam na wengine ambao wote wanachezea Simba A.
Wachezaji wanaobaki kwenye Kombe la Mapinduzi, watakwenda Oman baada ya mashindano hayo pamoja na kocha Julio.
Simba SC kesho inatarajiwa kumenyana na Azam FC katika Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Mchezo huo utakuwa ni marudio ya Nusu Fainali ya mwaka jana, ambayo Azam FC waliitoa Simba SC kwa kuichapa mabao 2-1.
Kocha Msaidizi wa Azam FC, Muingereza Kalimangonga Sam Daniel Ongala, maarufu kama Kali, amesema kwamba wamefurahia kukutana na Simba SC katika Nusu Fainali kuliko Tusker ya Kenya, kwa sababu hiyo itakuwa njia ya mkato kwao kuingia Fainali.
Ikiwa Oman, Simba itakaa kwa wiki mbili na itacheza mechi tatu za kujipima nguvu dhidi ya timu ambazo wameandaliwa na wenyeji wao Fanja FC. Aidha, wameandaliwa makocha watatu huko, wakiongozwa na beki wa zamani wa Simba SC, Talib Hilal kuungana na makocha wa Simba kuinoa klabu hiyo ikiwa nchini humo.
Hiyo ni ziara ya mafunzo, ambayo lengo lake ni kuiweka sawa Simba SC kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.

CHUJI ASEMA DENIZLISPOR LILIKUWA BONGE LA KIPIMO YANGA JANA


Chuji ndani ya Uturuki
KIUNGO wa Yanga, Athumani Iddi ‘Chuji’ amesema kwamba Denizlispor FC waliyocheza nayo jana mchezo wa kirafiki kilikuwa kipimo kizuri kwao, kwani timu hiyo ni nzuri zaidi ya ile waliyocheza nayo awali, DSC Arminia Bielefeld ya Ujerumani.
Akizungumza  kutoka Uturuki jana, Chuji alisema kwamba mechi ya jana imewasaidia sana kujua mapungufu na ubora wao kwa kuwa walicheza na timu nzuri iliyowazidi uwezo.
“Hii timu ni nzuri sana, kwa kweli imetupa changamoto nzuri na sisi wenyewe kama wachezaji tumeona hicho kitu,”alisema Chuji.
Yanga SC jana ilifungwa mabao 2-1 na Denizlispor FC ya Denizli, nchini Uturuki katika mchezo wake wa pili wa kujipima nguvu katika ziara yake ya Uturuki, bao la kufutia machozi likifungwa na Jerry Tegete.
Pamoja na kufungwa na timu hiyo inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, iitwayo Bank Asya 1. Lig, ambayo msimu uliopita ilimaliza katika nafasi ya 10, imeelezwa Yanga ilicheza soka ya kuvutia.
Denizlispor Football iliyoanzishwa mwaka 1966, inatumia Uwanja wenye kuingiza mashabiki 19,500 wa Denzili Ataturk na mafanikio yake makubwa hivi karibuni ilikuwa mwaka 2002 waliposhika nafasi ya tano katika Ligi Kuu ya nchini humo na kufuzu kwenye mchujo wa Kombe la UEFA.
Mwaka huo, ilifanya maajabu kwa kuzifunga timu zenye majina Ulaya kama FC Lorient, Sparta Prague na Olympique Lyonnais, kabla ya kufungwa katika Raundi ya Nne na FC Porto ya Ureno, ambao walitwaa ubingwa wa michuano hiyo mwishowe.
Katika mchezo wake wa kwanza wa kujipima nguvu, Yanga ilitoka 1-1 na DSC Arminia Bielefeld ya Ujerumani, bao la timu hiyo ya Jangwani likifungwa na Tegete.
Kikosi cha Yanga jana kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdu, Kabange Twite, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Athumani Iddi ‘Chuji’, Haruna Niyonzima, Nurdin Bakari, Jerry Tegete/Didier Kavumbangu, Said Bahanuzi/Hamisi Kiiza na Simon Msuva.

WACHEZAJI 11 WANAOUNDA KIKOSI CHA WACHEZAJI BORA WA DUNIA NI HWA HAPA

CAPITAL ONE CUP: LEO NUSU FAINALI BRADFORD v VILLA

CAPITAL_ONE_CUP-BEST>>KESHO CHELSEA v SWANSEA!!
NUSU FAINALI za CAPITAL ONE CUP, zamani likiitwa Carling Cup au Kombe la Ligi, zitaanzwa kuchezwa leo kwa Mechi kati ya Bradford City na Aston Villa na kesho ni Chelsea v Swansea City.
Nusu Fainali za Mashindano haya huchezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.

DONDOO za LIGI CUP:
-Aston Villa wameshinda Kombe hili mara 5 mara ya mwisho ni 1996
-Chelsea wameshinda mara 5 ikiwa ni pamoja na 2005 na 2007
-Bradford na Swansea hawajawahi kutwaa Kombe hili.

DONDOO za MECHI BRADFORD v VILLA
Uwanja: Coral Windows Stadium
Hali za Wachezaji
Kuna hatihati kuhusu kucheza kwa Wachezaji wa Bradford Fowadi James Hanson na Beki James Meredith ambao wana maumivu.
Straika wa Aston Villa Darren Bent huenda akabaki na namba baada ya juzi kufunga Bao dhidi ya Ipswich kwenye FA Cup lakini Christian Benteke, ambae hakucheza na Ipswich, anategemewa sana kuchezeshwa badala ya Bent.
Wakati Winga hatari wa Villa, Gabby Agbonlahor, amepona, Marc Albrighton ana hatihati kucheza kwa vile ana maumivu ya mguu.
Uso kwa Uso
-Timu hizi zinakutana kwa mara ya 39 lakini ni mara ya kwanza tangu Februari 2001 ambapo Villa ilishinda Bao 3-0.
-Aston Villa wameifunga Bradford mara mbili kwenye Kombe la Ligi, Bao 4-3 Mwaka 1961 walipocheza ugenini na 7-1 Mwaka 1964 walipocheza nyumbani.
RATIBA-NUSU FAINALI
[Mechi zote kuanza SAA 4 DAK 45 Usiku]
Jumanne Januari 8
Bradford v Aston Villa
Jumatano Januari 9
Chelsea v Swansea City
MARUDIANO
Jumanne Januari 22
Aston Villa v Bradford
Jumatano Januari 23
Swansea City v Chelsea
FAINALI
Jumapili Februari 24
Uwanja wa Wembley, London

FA CUP: EVERTON YANYUKA 5-1, IPO RAUNDI YA 4!

FA_CUP-NEW_LOGO>>ARSENAL v SWANSEA KURUDIWA JANUARI 16!!
JANA Usiku, Everton, wakiwa ugenini, wameinyuka Cheltenham Mabao 5-1 na kuingia Raundi ya 4 ya FA CUP ambayo watacheza tena ugenini na Mshindi kati ya Bolton au Sunderland na ile Mechi ya marudiano kati ya Arsenal na Swansea City itachezwa Januari 16 Uwanjani Emirates.

MAGOLI:
Cheltenham 1
Penn Dakika ya 51.
Everton 5
Jelavic Dakika ya 12
Baines 21 (Penati)
Osman 49
Coleman 58
Fellaini 89

Swansea City na Arsenal zilitoka sare ya Bao 2-2 katika Mechi ya Raundi ya 3 ya FA CUP iliyochezwa Uwanja wa Liberty majuzi Jumapili.
Mshindi wa Mechi hiyo atacheza Raundi ya 4 ugenini na Brighton & Hove Albion, Timu ya Daraja la chini iliyoshangaza kwa kuibwaga nje Newcastle katika Raundi ya 3.

MECHI ZA MARUDIANO- FA CUP-Raundi ya 3
**FAHAMU: Kwa Timu zilizoenda sare kwenye Raundi ya 3 Mechi zake zitachezwa Januari 15 na 16.
Jumanne Januari 15
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Birmingham v Leeds
Bournemouth v Wigan
Brentfaud v Southend
Leyton Auient v Hull
Wimbledon v Sheffield Wed
Stoke v Crystal Palace
Sunderland v Bolton
[SAA 5 Usiku]
Blackpool v Fulham
Jumatano Januari 16
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Arsenal v Swansea City
[SAA 5 Usiku]
Man Utd v West Ham
West Brom v QPR
RAUNDI YA 4
[KUCHEZWA WIKIENDI YA JANUARI 26]
Norwich City v Luton Town
Oldham Athletic v Liverpool
Macclesfield Town v Wigan Athletic au Bournemouth
Derby County v Blackburn Rovers
Hull City au Leyton Auient v Barnsley
Middlesbrough v Aldershot Town
Millwall v Aston Villa
Leeds United au Birmingham City v Tottenham Hotspur
Brighton & Hove Albion v Swansea City au Arsenal
Crystal Palace au Stoke City v Manchester City
West Ham United au Manchester United v Fulham au Blackpool
Southend United au Brentfaud v Chelsea
Reading v Sheffield United
Huddersfield Town v Leicester
QPR au West Brom v Sheffield Wednesday au MK Dons
Bolton au Sunderland v Everton

MAKOMBE ULAYA: LEO COPA del REY & ITALIAN CUP!

>>NI KIMBEMBE KWA REAL MADRID KWENYE COPA del REY!!
>>ITALIAN CUP: NI JUVE v AC MILAN!!
BARCA_v_REALVIGOGO, Real Madrid, wakiwa wamepoteza matumaini ya kutetea Ubingwa wao wa La Liga wakiwa Pointi 16 nyuma ya vinara FC Barcelona, Jumatano watacheza Mechi ya marudiano ya COPA del REY na Celta Vigo Uwanjani Santiago Bernabeu huku wakitakiwa kupindua kipigo cha 2-1 walichokipata katika Mechi ya kwanza la sivyo Msimu wao wote utabaki kuomba waifunge Manchester United kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ili wawe na matumaini ya kuambua Taji.
Barcelona, ambao ndio Mabingwa watetezi, wana kazi nyepesi kidogo kwani wapo nyumbani Nou Camp kucheza na Cordoba Timu ambayo waliichapa 2-0 katika Mechi ya kwanza.
Huko Italy, Italian Cup inaingia hatua ya Robo Fainali na Mechi ya mvuto kabisa ni ile ya Juventus v AC Milan.
COPA del REY
RAUNDI ya 4
MECHI za MARUDIANO
Jumanne Januari 8
[Matokeo Mechi ya kwanza katika Mabano]
Valencia v Osasuna [2-0]
Jumatano Januari 9
Sevilla v Real Mallorca [5-0]
Real Madrid v Celta Vigo [1-2]
Real Zaragoza v Levante [1-0]
Alhamisi Januari 10
Getafe v Atletico Madrid [0-3]
Barcelona v Cordoba [2-0]
Real Betis v Las Palmas [1-1]
ITALIAN CUP
ROBO FAINALI
Jumanne Januari 8
SS Lazio v Catania
Jumatano Januari 9
Juventus v AC Milan
Jumanne Januari 15
Inter Milan v Bologna
Jumatano Januari 16
Fiorentina v AS Roma

NFF YAMPUUZIA KUHUSIANA NA SUALA L MSHAMBULIAJI WA NEWCASTLE UNITED AMEOBI.


SHIRIKISHO la Soka la Nigeria, NFF limesema kuwa halitamchukulia hatua yoyote dhidi ya Shola Ameobi kufuatia kushindwa kukubali mwaliko wa kuiwakilisha timu ya taifa ya nchi hiyo maarufu kama Super Eagles katika michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon itakayofanyika Afrika Kusini. Mshambuliaji huyo aliitwa na kocha wa nchi hiyo Stephen Keshi pamoja na wachezaji wengine 31 lakini hakuonekana na wala hakutoa sababu zozote. Ameobi mwenye umri wa miaka 31 aliitwa kuichezea Super Eagles katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki miezi miwili iliyopita na ilikuwa ajumuishwe katika kikosi cha wachezaji 23 kitachoshiriki michuano ya Afcon inayoanza kutimua vumbi Januari 19 na kumalizika Februari 10 mwaka huu. Ingawa mkataba wa mchezaji huyo unaitaka klabu yake ya Newcastle United ambayo inashiriki Ligi Kuu nchini Uingereza kumuachia wakati wa mashindano kocha wa Super Eagle Keshi hakutaka kumuondoa kwenye kikosi chake mpaka wiki iliyopita. Katibu Mkuu wa NFF Musa Ahmadu amesema hawatakata rufani katika Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kumzuia Ameobi kutoichezea Newcastle wakati wa mashindano hayo na kudai wana mambo mengi muhimu ya kufanya katika kuandaa kuliko hilo suala la mchezaji huyo. Ahmadu alidai kuwa wapo wachezaji wengi wazuri ambao wanaweza kuisaidia nchi hiyo kufanya vyema kwenye michuano hiyo hivyo kutokuwepo kwa mchezaji huyo hadhani kama kutawaathiri sana.

KIUNGO BORA WA AFRIKA NA MCHEZAJI BORA WA AFRIKA YAYA TOURE AREJEA NA HALI YAKE YA KAWAIDA


KIUNGO nyota wa kimataifa wa Ivory Coast, Yaya Toure amerejea katika hali yake ya kawaida baada ya kukosa Siku mbili za mazoezi katika kambi ya timu ya taifa ya nchi hiyo iliyopo jijini Abu Dhabi baada ya kupata homa kali. Kaka yake mkubwa Kolo ambaye wanacheza wote katika klabu ya Manchester City ameeleza kuwa mdogo wake Yaya alipewa muda wa kupumzika kwa ajili ya matibabu ya homa na kifua lakini hivi sasa amepona. Ivory Coast ambao wanapewa nafasi kubwa ya kunyakuwa taji la michuano ya Mataifa Afrika inayotarajiwa kutimua vumbi Januari 19 imepangwa katika kundi D pamoja na timu za Togo, Algeria na Tunisia. Kikosi hicho kinatarajia kucheza mchezo wa kirafiki na Misri Januari 14 kabla ya kuelekea Afrika Kusini ambapo wataanza kampeni zao kwa kupambana na Togo Januari 22.

MESSI JANA ALINYAKUWA BALLON D'OR KWA MARA YA NNE MFULULIZO NA KICHEKI KIKOSI BORA CHA DUNIA.


MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi ameweka rekodi kwa kunyakuwa tuzo ya mchezaji bora wa dunia maarufu kama FIFA Ballon d’Or katika sherehe zilizofanyika jijini Zurich, Switzerland. Messi mwenye umri wa miaka 25 alinyakuwa tuzo hiyo mbele ya Andres Iniesta ambaye wanacheza wote Barcelon na mshambuliaji nyoa wa Real Madrid Cristiano Ronaldo. 
Mwaka 2012 ulikuwa na mafanikio makubwa kwa Messi baada ya kufunga mabao mengi na kuipita rekodi iliyowekwa miaka 40 iliyopita na Gerd Muller ambaye alifunga mabao 85 huku yeye akimaliza mwaka jana akiwa amefunga mabao 91. Akishukuru mara baada ya kupokea tuzo hiyo Messi aliwashukuru waandaji na wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine katika kupiga kura ya kumchagua kubeba tuzo hiyo kwa mara ya nne. 
Nyota huyo pia aliwashukuru wachezaji wenzake wa Barcelona akiwemo Iniesta ambaye walikuwa wakigombea wote tuzo makocha na viongozi bila kusahau wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya Argentina na mashabiki wake wote wa ujumla.
  
KIKOSI bora cha mwaka 2012 maarufu kama FIFPro waliosimama mbele kulia na timu zao katika mabano Xabi Alonso (Real Madrid, Hispania), Xavi Hernandez (Barcelona, Hispania), Andres Iniesta (Barcelona, Hispania), Lionel Messi (Barcelona, Argentina), Radamel Falcao (Atletico Madrid, Colombia), Cristiano Ronaldo (Real Madrid, Ureno), Marcelo (Real Madrid, Brazil), Sergio Ramos (Real Madrid, Hispania), Gerard Pique (Barcelona, Hispania), Dani Alves (Barcelona, Brazil) na Iker Casillas (Real Madrid, Hispania).
 

WAAMUZI WA AFCON WATAJWA.


JUMLA ya waamuzi 18 na washika vibendera 21 wameteuliwa kuchezesha mechi za michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon itakayoanza kutimua vumbi Januari 19 mwaka huu nchini Afrika Kusini. Kuna mabadiliko mawili kwa upande wa waamuzi na nane kwa upande wa washika vibendera kulinganisha na wale ambao walichezesha fainali za michuano hiyo zilizofanyika nchini Equatorial Guinea na Gabon mwaka jana. Katika orodha hiyo inajumuisha waamuzi wawili ambao wamechezesha fainali zilizopita akiwemo Komlan Coulibaly kutoka Mali aliechezesha fainali ya mwaka 2010 nchini Angola na Badar Diatta wa Senegal alichezesha fainali ya mwaka jana kati ya Zambia na Ivory Coast jijini Libreville. Coulibaly mwenye umri wa miaka 42 anatarajia kuweka rekodi ya kuwa mwamuzi alichezesha Afcon mara nyingi zaidi ambapo hii ikiwa ni mara yake ya saba toka alipoteuliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2002. Waamuzi wawili ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza ni pamoja na Sylvester Kirwa kutoka Kenya na Bernard Camille kutoka Seychelles.

ADEBAYOR AKUBALI KUREJEA TOGO.


MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Togo, Emmanuel Adebayor hatimaye amekubali kujiunga na kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo kwa ajili ya michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon baada ya kusitisha mgomo wake. Adebayor aligoma kuichezea nchi yake akishinikiza Shirikisho la Soka la Togo-TFF kuwalipa wachezaji malimbikizo ya posho zao. Rais wa shirikisho hilo Gabriel Ameyi alitangaza jana kuwa kikosi cha nchi hiyo kitasafiri kuelekea Afrika Kusini pamoja na nahodha wake Adebayor ambaye alifanya mazungumzo na rais wan chi hiyo Faure Gnassingbe kuhusiana na tatizo hilo. Ameyi amesema watakuwa pamoja na nahodha huyo nchini Afrika Kusini baada ya mazungumzo na rais Gnassingbe kwenda sawa ingawa mshambuliaji huyo anayecheza katika klabu ya Tottenham Hotspurs hakuzungumza chochote wakati anaondoka Ikulu. Togo inakabiliwa na mchezo wa ufunguzi dhid ya Ivory Coast Januari 22 jijini Rustenburg, ukiwa ni mchezo wa kundi D ambalo pia linajumuisha timu za Algeria na Tunisia.

JERRY SANTO ASEMA BAHATI HAIKUWA YAO COASTAL UNION


Santo katika mechi dhidi ya Azam Kombe la Mapinduzi
NAHODHA wa Coastal Union ya Tanga katika Kombe la Mapinduzi, Mkenya Jerry Santo amesema kwamba kutolewa kwao mapema katika michuano hiyo ya mwaka huu, kumetokana na kukosa bahati, lakini kama soka walicheza.
Akizungumza  jana usiku, Santo aliyewahi kuchezea Simba SC, alisema kwamba Coastal ilicheza soka nzuri na ndiyo maana haikufungwa hata mechi moja, lakini kwa kukosa bahati imetolewa.
“Tulicheza vizuri, mechi zote tulipata nafasi lakini tulitumia moja tu, bahati haikuwa yetu, lakini timu yetu ni nzuri na tunaamini katika Ligi Kuu (ya Bara) tutafanya vizuri,”alisema kiungo huyo wa zamani wa Tusker FC ya Kenya.
Coastal Union ya Tanga ilitolewa katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi, baada ya sare ya bila kufungana na Miembani FC jioni ya jana kwenye Uwanja wa Mao Dze Tung, Zanzibar.

STARS INAONDOKA KESHO BILA MASTAA WA YANGA


Kim Poulsen, kocha Stars
TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars itakayocheza mechi ya kujipima nguvu na Ethiopia Januari 11, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Addis Ababa, Ethiopia inatarajiwa kuondoka kesho mchana mjini Dar es Salaam kwenda kucheza mechi hiyo.
Stars chini ya Kocha Mkuu Mdenmark, Kim Poulsen, itakuwa na timu ya mwisho kucheza na Ethiopia kabla ya Wahabeshi hao kwenda Afrika Kusini kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazoanza Januari 19 mwaka huu.
Ethiopia iko kundi C pamoja na mabingwa watetezi Zambia, Nigeria na Burkina Faso. Ethiopia itacheza mechi yake ya kwanza Januari 21 mwaka huu dhidi ya Zambia.
Katika mechi yake ya mwisho, Taifa Stars iliifunga Zambia bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Desemba 22 mwaka jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi hiyo ya kirafiki dhidi ya Ethiopia ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya mchujo dhidi ya Morocco kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia 2014. Mechi hiyo itachezwa Machi mwaka huu.
Wachezaji wanaliotwa kwa ajili ya mechi hiyo ni Juma Kaseja kutoka Simba ambaye pia ndiye nahodha wa Stars, Aishi Manula na Mwadini Ally wote kutoka Azam. Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Amir Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga) na Shomari Kapombe (Simba).
Viungo ni Salum Abubakar (Azam), Athuman Idd (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Khamis Mcha (Azam), Frank Domayo (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).
Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Simba), Simon Msuva (Yanga), na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Wakati benchi la Ufundi lina Kim, Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Tasso (Meneja), Dk. Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa timu), Frank Mhonda (Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).
Hata hivyo, kocha Poulsen yuko hatarini kuwakosa wachezaji wa Yanga, Kevin Yondani, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Athuman Idd ‘Chuji’, Frank Domayo na Simon Msuva ambao wapo na timu yao Uturuki.

TEGETE AIFUNGIA YANGA LA KUFUTIA MACHOZI IKILALA 2-1 UTURUKI


Tegete kushoto akiwa na Kiiza

YANGA SC imefungwa mabao 2-1 jioni hii na Denizlispor FC ya Denizli, nchini Uturuki katika mchezo wake wa pili wa kujipima nguvu katika ziara yake ya Uturuki, bao la kufutia machozi likifungwa na Jerry Tegete.
Pamoja na kufungwa na timu hiyo inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, iitwayo Bank Asya 1. Lig, ambayo msimu uliopita ilimaliza katika nafasi ya 10, Yanga ilicheza soka ya kuvutia.
Denizlispor Football iliyoanzishwa mwaka 1966, inatumia Uwanja wenye kuingiza mashabiki 19,500 wa Denzili Ataturk na mafanikio yake makubwa hivi karibuni ilikuwa mwaka 2002 waliposhika nafasi ya tano katika Ligi Kuu ya nchini humo na kufuzu kwenye mchujo wa Kombe la UEFA.
Mwaka huo, ilifanya maajabu kwa kuzifunga timu zenye majina Ulaya kama FC Lorient, Sparta Prague na Olympique Lyonnais, kabla ya kufungwa katika Raundi ya Nne na FC Porto ya Ureno, ambao walitwaa ubingwa wa michuano hiyo mwishowe.
Katika mchezo wake wa kwanza wa kujipima nguvu, Yanga ilitoka 1-1 na DSC Arminia Bielefeld ya Ujerumani, bao la timu hiyo ya Jangwani likifungwa na Tegete.
Kikosi cha Yanga leo kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdu, Kabange Twite, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Athumani Iddi ‘Chuji’, Haruna Niyonzima, Nurdin Bakari, Jerry Tegete/Didier Kavumbangu, Said Bahanuzi/Hamisi Kiiza na Simon Msuva.

KOCHA AZAM ASEMA HERI SIMBA KULIKO TUSKER NI KIFO


Kali Ongala

KOCHA Msaidizi wa Azam FC, Muingereza Kalimangonga Sam Daniel Ongala, maarufu kama Kali, amesema kwamba wamefurahia kukutana na Simba SC katika Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi kuliko Tusker ya Kenya, kwa sababu hiyo itakuwa njia ya mkato kwao kuingia Fainali.
Akizungumza  jana usiku baada ya mechi dhidi ya Mtibwa Sugar, mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga, alisema kwamba Tusker ni timu ambayo imeonyesha kiwango kikubwa mno cha soka katika mashindano hayo hadi sasa, hivyo wangekutana nayo mapema ingekuwa mtihani mgumu.
“Hatuihofii timu yoyote, lakini kukutana na Simba SC badala ya Tusker katika Nusu Fainali ni afadhali kwetu, kwa sababu Tusker ni timu ngumu, ambayo imeonyesha kiwango kikubwa mno cha soka hadi sasa,”alisema Kali.
Kali amesema nia na dhamira ya Azam FC ni kutetea Kombe la hilo la Mapinduzi na hawaihofii timu yoyote watakatokutana nayo.
Azam FC itamenyana na Simba SC katika Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi Januari 10, mwaka huu kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Hiyo inafuatia Azam kutoka sare ya bila kufungana na Mtibwa Sugar usiku wa jana kwenye Uwanja wa Amaan visiwani hapa, katika mchezo wa mwisho wa Kundi B la michuano hiyo. 
Azam imemaliza na pointi tano na kuongoza Kundi B, ikifuatiwa na Miembeni iliyomaliza na pointi nne.
Miembeni itamenyana na kinara wa Kundi A, Tusker ya Kenya keshokutwa katika Nusu Fainali ya kwanza.
Katika mchezo wa jana, Azam ikiongozwa na washambuliaji wawili, Gaudence Mwaikimba aliyekuwa katikati na Brian Umony aliyekuwa akishambulia kutokea pembeni ililitia misukoko miwili mitatu lango la Mtibwa, lakini leo kipa Hussein Sharrif ‘Casillas’ alisimama imara kwa dakika zote 90 na kuokoa hatari zote.
Mtibwa iliyocheza na washambuliaji wawili pia, Hussein Javu na Juma Zuilio ililitia misukosuko pia lango la Azam, lakini Mwadini Ally kipa wa Azam alikuwa makini kuokoa hatari zote.
MSIMAMO WA KUNDI A:
                        
                      P    W  D   L    GF GA GDPts
Tusker FC      3    2    1    0    7    2    5    7
Simba SC       3    1    2    0    6    4    2    5
Jamhuri FC     3    1    0    2    4    6    -2  3
Bandari FC     3    0    1    2    3    8    -5  1
MSIMAMO WA KUNDI B:
                              
                         P    W  D   L    GF GA GDPts
Azam FC           3    1    2    0    3    1    2    5
Miembeni           3    1    1    1    5    4    1    4
Coastal Union    3    0    3    0    1    1    0    3   
Mtibwa Sugar    3    0    2    1    2    5    -3  2   
WAFUNGAJI WA MABAO:
Adeyum Saleh              Miembeni       3
Jesse Were                  Tusker FC       3
Haruna Chanongo        Simba SC       2
Mfanyeje Mussa           Jamhuri          2
Ismail Dunga                Tusker FC      1
Michael Olunga            Tusker FC      1
Andrew Tolowa             Tusker FC      1
Joackins Atudo             Azam FC        1
Gaudence Mwaikimba  Azam FC        1
Amour Janja                 Bandari          1
Mohamed Hamdani      Miembeni       1
Rashid Roshwa            Miembeni       1
Juma Mpakala              Mtibwa           1
Ally Mohamed              Mtibwa           1
Felix Sunzu                 Simba SC       1
Kiggi Makassy             Simba SC       1
Shomary Kapombe      Simba SC       1
Fahad Abdallah           Jamhuri          1
Ally Bilal                      Jamhuri          1
Faudhi Ally                  Bandari           1
Haitham Juma             Bandari           1
Jerry Santo                  Coastal U       1
RATIBA KOMBE LA MAPINDUZI:
Janauri 2, 2013
Tusker 5-1 Bandari
Simba SC 2-2 Jamhuri
Januari 3, 2013
Mtibwa Sugar 1-4 Miembeni
Azam FC 0-0 Coastal Union  
Januari 4, 2013
Jamhuri 2-1 Bandari
Simba SC 1-1 Tusker FC
Januari 5, 2013
Mtibwa Sugar 1-1 Coastal Union
Miembeni 1-2 Azam
Januari 6, 2013
Tusker 1-0 Jamhuri
Simba SC 1-1 Bandari
Januari 7, 2013
Miembeni 0-0 Coastal Union
Azam FC 0-0 Mtibwa Sugar
Januari 9, 2013
Tusker  FC Vs Miembeni FC
Januari 10, 2013
Azam FC Vs Simba SC
Januari 12, 2013
FAINALI
ORODHA YA MABINGWA KOMBE LA MAPINDUZI
2003   Mtibwa Sugar
2004   Yanga SC
2005   Yanga SC
2006   Simba SC
2007   Yanga SC
2008   Simba SC
2009   Miembeni FC
2010   Simba FC
2011   Azam FC
2013   ????????

MFARANSA SIMBA ATAKA DVD ZA LIBOLO NA TIMU YAKE DHIDI YA TIMU KALI MECHI KAMA MBILI AU ZAIDI

MFARANSA SIMBA ATAKA DVD ZA LIBOLO NA TIMU YAKE DHIDI YA TIMU KALI MECHI KAMA MBILI AU ZAIDI

Liewig
KOCHA Mfaransa wa Simba SC, Patrick Liewig amesema kwamba anataka DVD za mechi ngumu za timu hiyo pamoja na DVD za mechi za karibuni za wapinzani wao wa kwanza katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Recreativo de Libolo ya Angolal.
Simba SC itaanza na Recreativo de Libolo ya Angola, katika Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Februari 17 hadi 19 na kurudiana nayo kati ya Machi 2 na 4, mwakani.
Akizungumza  jana, Mfaransa huyo alisema kwamba anahitaji DVD hizo ili kuijua vema Simba ilikuwa inachezaji na ina wachezaji wa aina gani.
Aidha, kuhusu DVD za Recreativo de Libolo, Liewig alisema ni vema akizipata ili awajue wapinzani wake, lakini kwake muhimu zaidi ni DVD za Simba.
Akizungumzia suala hilo, Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ alisema kwamba DVD za mechi za Simba tayari zipo na watampatia kocha huyo, wakati DVD za Recreativo de Libolo bado wanazitafuta.
Simba SC inatarajiwa kuondoka kesho Dar es Salaam kwenda Oman kuweka kambi ya wiki mbili kujiandaa na Ligi Kuu pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika. 
Liewig aliyesaini mkataba wa miezi 18 wiki iliyopita kuifundisha Simba, akimpokea Mserbia Milovan Cirkovick aliyetupiwa virago baada ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Bara ni kocha wa zamani wa Akademi ya Paris Saint Germain (PSG) ya Ufaransa, ASEC Mimosas ya Ivory Coast na Club Africain ya Tunisia.
Babu huyo ana Stashahada ya Juu ya ukocha na Shahada ya tatu ya ualimu wa soka ya vijana aliyotunukiwa na Mkurugenzi wa Ufundi wa Ufaransa, Gerard Houiller.
Liewig pia amehudhuria kozi za ufundishaji mazoezi ya viungo Juni mwaka 1999 katika Chuo Kikuu cha Dijon.
Kwa upande wa uzoefu, Liewig alifanya kazi PSG kuanzia mwaka 1989 hadi 1999 kama Kocha Mkuu wa akademi na kuna wakati alikuwa akishirikishwa pia katika programu za timu A, ingawa majukumu yake zaidi yalikuwa ni kwa Under 20, Under 18 aliowawezesha kutwaa Kombe la French Junior Gambardella na Under 16.
Kuanzia mwaka 1989 hadi 1990:  alikuwa Meneja Mkuu wa Tomislav IVIC, 1990 hadi 1991 alikuwa Msaidizi wa Henri Michel, 1991 hadi 1994 alikuwa Msaidizi wa Artur Jorge, 1994 hadi 1996 alikuwa Msaidizi wa Luis Fernandez, 1996 hadi 1998: alikuwa Msaidizi wa Ricardo Gomez, 1998 hadi 1999 alikuwa Msaidizi wa Alain Giresse.
Liewig pia alifundisha Al Wahda FC ya Abu Dhabi kuanzia 1999 hadi 2001, ambayo aliipa ubingwa wa Ligi Kuu ya nchi hiyo na Kombe la Ligi.
Januari mwaka 2003 alikuwa Msimamizi wa Chama cha Soka UAE katika fainali za Afrika za U20 nchini Burkina Faso.
Kuanzia mwaka 2004 hadi 2009 alikuwa Kocha wa ASEC Mimosas ya Ivory Coast aliyoipa mataji matatu ya Ligi Kuu ya nchini humo mfululizo, 2004, 2005 na 2006, Super Cup ya nchini humo 2005, 2007, 2008 na 2009 na akaiwezesha kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa mara tatu, mara moja akiifikisha Nusu Fainali.
Amekuwa Kocha bora wa Ivory Coast miaka mitatu mfululizo, 2004, 2005 na 2006 na tangu Septemba mwaka jana hadi Juni mwaka huu, alikuwa kocha wa Club Africain ya Tunisia

OMAR OMAR MFALME WA MNANDA BONGO KUZIKWA KESHO MIKOROSHINI


Omar Omar

MSANII nyota wa miondoko ya Mchiriku, Omari Omari, aliyefariki leo afajiri atazikwa kesho saa 7 mchana.
Kwa mujibu wa King Sapeto, rafiki wa karibu wa marehemu, mazishi yatafanyika Temeke Mikoroshini jijini Dar es Salaam na kuanzia leo ndugu na jamaa wa marehemu wanategemea ujumbe mzito kutoka kwa viongozi wa Serikali watakaopishana kwenda kutoa mkono wa faraja kwenye nyumba ya msiba.
Kwa siku za hivi karibuni viongozi wa serikali na vyama mbali mbali vya siasa wamekuwa mstari wa mbele kwa kushiriki bega kwa bega kwenye misiba ya wasanii, hivyo watu wa karibu na Omari Omari wanategemea hali hiyo pia itatokea kwa ndugu yao kipenzi. "Hatutegemi ubaguzi wa misiba" anaeleza mmoja wa ndugu wa marehemu.
Omari Omari aliyetamba na wimbo “Kupata Majaaliwa” ndani yake kukiwa na mstari mkali unaosema ndefu amekosa ng’ombe lakini mbuzi kapewa, alifariki katika hospitali kuu ya Temeke baada ya kuugua ugonjwa wa kifua kikuu. Msiba uko Temeke Mikoroshini nyumbani kwa baba yake.

WAWILI TU YANGA KUJIUNGA NA STARS ITAKAYOMENYANA NA ETHIOPIA


Domayo
WACHEZAJI wawili tu wa Yanga, beki Kevin Yondan na kiungo Frank Domayo ndio watajiunga na kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kinachotarajiwa kuondoka kesho mchana kwenda Ethiopia, imeelezwa.
Yanga ambayo imepiga kambi ya maandalizi nchini Uturuki ilizuia nyota wake kujiunga na kambi ya Stars iliyoanza jumapili iliyopita jijini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo huo utakaopigwa keshokutwa katika uwanja wa Taifa wa Addis Ababa.
Akizungumza leo mjini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema kwamba Kocha Mkuu wa Stars, Mdenmark Kim Poulsen na Mholanzi Ernie Brandts wa Yanga, wamekubaliana Yondan na Domayo pekee, kati ya wachezaji watano Yanga waliotwa Stars ndio wajiunge na timu hiyo.
Amesema wachezaji hao wanatarajiwa kuwasili nchini usiku wa leo tayari kwa safari kesho na endapo watachelewa watakwenda Ethiopia peke yao, huku wachezaji wengine wa Yanga walioitwa Stars ambao wataendelea kubaki nchini Uturuki ni pamoja na Athuman Iddy ‘Chuji’, Simon Msuva na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ watakaojiunga na Stars watakaporejea nchini Januari 13.
Wambura aliongeza kuwa wachezaji 16 wa Stars wataondoka kesho saa 9:00 Alasiri tayari kwa mchezo huo maalum kwa kuipa maandalizi ya mwisho Ethiopia kabla ya kwenda Afrika Kusini kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazoanza Januari 19 mwaka huu.
Aidha, Wambura aliongeza kuwa, tayari wachezaji wa Simba, Azam FC na Mtibwa Sugar waliokuwa Zanzibar na timu zao zinazoshiriki michuano ya kombe la Mapinduzi inayoendelea Visiwani Zanzibar wamewasili leo kuungana na wenzao.
“Hata hivyo Azam  Fc imeruhusu kipa mmoja tu Aishi Manula huku Mwadini Ally ambaye pia aliitwa Stars ataendelea kubaki na timu kwenye kombe la Mapinduzi,”alisema Wambura
Wambura aliongeza kuwa kikosi cha Stars kilichoanza rasmi mazoezi jana, leo asubuhi kilifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Karume na jioni kinatarajiwa kujinoa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Aliwataja wengine wachezaji waliopo ni pamoja na Juma Kaseja kutoka Simba ambaye pia ndiye nahodha wa Stars na  Manula ( Azam FC), huku kwa upande wa Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Amir Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), na Shomari Kapombe (Simba).
Viungo ni Salum Abubakar (Azam), Amri Kiemba (Simba), Khamis Mcha (Azam), Mwinyi Kazimoto (Simba) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), wakati washambuliaji ni Mbwana Samata, Thomas Ulimwengu  (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC) na  Mrisho Ngasa (Simba).
Stars ambayo pia itautumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi ya mechi ya mchujo dhidi ya Morocco kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia 2014, mchezo utakaochezwa Machi mwaka huu.
Katika maandalizi yake hayo, mara ya mwisho  Stars ilikwaana na Zambia Desembza 22 mwaka jana kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na  kuibanjua bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki

ARMINIA ILIYOTOKA 1-1 NA YANGA NI YA DARAJA LA NNE UJERUMANI, WAPINZANI WA LEO KWELI DARAJA LA KWANZA


Yanga SC

YANGA SC ipo Uturuki kwa ziara ya wiki mbili na Jumamosi iliyopita ilicheza mechi ya kwanza ya kujipima nguvu na klabu ya DSC Arminia Bielefeld, au Deutscher Sportclub Arminia Bielefeld kwa jina kamili inayojulikana pia kama Die Arminen au Die Blauen.
Hii ni klabu ya soka kutoka mji wa Bielefeld, North Rhine-Westphalia, yenye wanachama  8,738 inayotumia jezi za rangi nyeusi, nyeupe na bluu na inacheza Ligi Daraja la Nne Ujerumani, inayoitwa 3. Liga, na msimu uliopita ilishika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa Ligi inayoshirikisha timu 18.
Imewahi kupanda na kushuka Ligi Kuu ya Ujerumani, maarufu kama Bundesliga, mara saba, ambayo kwa Ujerumani ni rekodi. Mwaka 1971 ilikumbwa na kashfa ya kuwahonga wapinzani wao katika Bundesliga.
Arminia imekuwa ikicheza mechi zake za nyumbani katika Uwanja wa Bielefelder Alm tangu mwaka 1926 na kuanzia mwaka 2004, Uwanja huo umekuwa ukiitwa SchucoArena, kutokana na dili la udhamini walilopata.
KUHUSU LIGI WANAYOCHEZA;
3. Fußball-Liga ni Ligi Daraja la Nne Ujerumani, ambayo ilianza kuchezwa msimu wa 2008–2009, ikichukua nafasi ya Regionalliga kama ligi ya nne kwa ukubwa Ujerumani.
Katika mfumo wa ligi za soka Ujerumani, inatenganishwa na 2. Bundesliga na Semi-Professional Regionalliga, hivyo inakuwa kama Daraja la Nne na huchezwa katika makundi matatu, yenye jumla ya klabu 18 zilizogawanywa katika makundi hayo.
Kwa mujibu wa tovuti ya Yanga, timu hizo zilitoka sare ya 1-1 Jumamosi.
WAPINZANI WA LEO KWELI DARAJA LA KWANZA;
Leo Yanga inacheza mechi ya pili ya kujipima nguvu dhidi ya timu ya Denizlispor FC yenye maskani yake Denizli, nchini Uturuki, ambayo kweli inashiriki Ligi Daraja la Kwanza, iitwayo Bank Asya 1. Lig na msimu uliopita ilimaliza katika nafasi ya 10.
Denizlispor Football iliyoanzishwa mwaka 1966, inatumia Uwanja wenye kuingiza mashabiki 19,500 wa Denzili Ataturk na mafanikio yake makubwa hivi karibuni ilikuwa mwaka 2002 waliposhika nafasi ya tano katika Ligi Kuu ya nchini humo na kufuzu kwenye mchujo wa Kombe la UEFA.
Mwaka huo, ilifanya maajabu kwa kuzifunga timu zenye majina Ulaya kama FC Lorient, Sparta Prague na Olympique Lyonnais, kabla ya kufungwa katika Raundi ya Nne na FC Porto ya Ureno, ambao walitwaa ubingwa wa michuano hiyo mwishowe.  Je, matokeo yatakuwaje kwenye mechi hiyo leo?