Wednesday, December 19, 2012

AZAM WASAKA NUSU FAINALI NA REAL DE KINSHANSA DRC LEO


Kikosi cha Azam
AZAM FC inashuka dimbani leo kwenye Uwanja wa Martyrs, kumenyana na Real De Kinshasa ya DRC kongo kule, katika mchezo maalum wa kutafuta timu ya kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Hisani mjini hapa, linaloandaliwa na FECOFA, Shirikisho la Soka DRC.
Real imeshika mkia katika Kundi A, wakati Azam pia imeshika mkia katika Kundi B, hivyo zinamenyana leo kuwania tiketi ya Nusu Fainali.  
Azam juzi ilifungwa mabao 2-0 na Shark FC ya hapa, katika mchezo wake wa mwisho wa Kundi B, Kombe la Hisani, kwenye Uwanja wa Martyrs jioni hii.
Mabao ya washindi, timu inayomilikiwa na mdogo wake rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Joseph Kabila yalifungwa na Ndibu Kalala dakika ya 23 na Kalala Kabongo dakika ya 34.
Hata hivyo, kipigo hicho kilichangiwa kwa kiasi kikubwa na uchezeshaji mbovu wa marefa, ambao tangu mwanzo walionekana kuwapendelea wenyeji.
Azam juzi walinyimwa penalti mbili za halali, moja kila kipindi, ya kwanza baada ya shuti la mshambuliaji Gaudence Mwaikimba kuzuiwa kwa mkono na beki wa Shark na ya pili kiungo Humphrey Mieno aliangushwa kwenye eneo la hatari, tena ndani ya sita akiwa amekwishamtoka kipa, lakini zote refa akapeta.
Washika vibendera nao walizima mashambulizi kadhaa ya Azam kwa kudai wachezaji walikuwa wameotea.
Mabao yote Azam walifungwa wakitoka kushambulia na hayakuwa na mushkeli, makosa ambayo walirekebisha na hawakuyarudia kipindi cha pili. Kipindi cha kwanza, timu zilishambuliana kwa zamu, lakini kipindi cha pili Azam walitawala zaidi mchezo na kama si ‘madudu’ ya refa, matokeo yangeweza kubadilika.
Azam ilicheza mechi zote mbili bila makocha wake wote wawili, Waingereza Stewart Hall na Msaidizi wake, Kali Ongala ambao walibaki Nairobi, Kenya pamoja na Daktari Mjerumani Paulo Gomez na wachezaji Kipre Balou na Kipre Tcheche raia wa Ivory Coast, kutokana na kukosa viza za kuingia DRC.
Watano hao, waliwasili mjini DRC jana na leo Azam inatarajiwa kushusha kikosi chake kamili. Beki Joackins Atudo naye anatarajiwa kuungana na timu leo mjini hapa.
Nusu Fainali zitachezwa Desemba 25 wakati Desemba 26 itakuwa Fainali na mechi ya kusaka mshindi wa tatu.  Kundi B, lina timu za DC Motema Pembe, Diables Noirs, FC MK na Real De Kinshasa.  

CHEKA KUZIPIGA ADDIS

Mbabe Cheka
KAMISHENI ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) tayari imemtafutia bondia Francis Cheka mpambano wa marudiano kati yake na bondia Chiotra Chimwemwe wa Malawi katika jiji la Addis Ababa, Ehtiopia.
Mpambano huo utafayika January 26, siku ya ufunguzi wa mkutano wa wakuu wa nchi za Africa (AU Summit) katika jiji hilo la Wafalme la Abesinia!
Cheka na Chimwemwe watakutana jijini Arusha Desemba 26 (Boxing Day) katika mpambano wa kutafuta nani mbabe wa uzito wa Super Middle katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi (IBF AMEPG). Katika mpambano huo mafahali hawa wawili wataumana kiume kwa raundi 12 za dakika tatu kila mmoja!
Mpambano wa Cheka na Chimwemwe jijini Arusha umeandaliwa na kampuni ya Screen Hills (T) Investment ya jijini Dar-Es-Salaam inayomilikiwa na promota maarufu aliyewahi kuwa bingwa wa taifa katika ngumi za ridhaa na kulipwa Andrew George aka Chagga Boy!
Umaarufu wa wawili hawa umewafanya mapromota wanaoandaa tamasha la kuchangisha pesa kwa ajili ya kulisha watu wenye njaa katika bara la Africa kuwaingiza Cheka 26(15)-6(3)-1 na Chiotra 26(15)-4(2)-1 katika mpambano hwa marudiano utakaofanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia tarehe 26 Januaru 2012!
Katika tamasha hilo, pambano kuu litakuwa kati ya bondia Oliver McCall 56(37)-12(1)-0 kutoka Marekani ambaye aliwahi kuwa bingwa wa uzito wa juu duniani akipambana na bondia Sammy Retta - 18(17)-3(2)-0 kutoka Ethiopia kugombea ubingwa wa IBF Africa, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi (IBF AMEPG) katika uzito wa juu (Heavyweight)
Mapambano mengine yatawakutanisha mabondia Daniel Wanyonyi 14(12)-5(2)-2 wa Kenya atakayechuana na bondia Issac Hlatswayo 30(10)-5(3)-1 kutoka Afrika ya Kusini katika kugombea ubingwa wa IBF Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi (IBF AMEPG) katika uzito wa Welterweight
Naye Manzur Ali 7(4)-8(3)-0 bingwa wa uzito wa juu kutoka nchi ya Misri atachuana vikali na bondia Harry Simon 27(20)-0-0 kutoka Namibia ubingwa wa IBF Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi (IBF AMEPG) katika uzito wa Light heavyweight.
Mpambano huu umeidhinishwa na Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) na Cheka kupewa kibali na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC).

UCHAGUZI TWFA LEO MORO

Kila heri mdau Zena Chande 'Zen C'
UCHAGUZI wa viongozi wapya wa Chama cha Soka ya Wanawake Tanzania (TWFA) unafanyika leo kwenye hoteli ya Midlands mjini Morogoro.
Kamati ya Uchaguzi ya TWFA ikiongozwa na Mama Ombeni Zavala ndiyo itakayoendesha uchaguzi huo chini ya usimamizi wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Wagombea katika uchaguzi huo ni Isabela Kapera, Joan Minja na Lina Kessy wanaowania uenyekiti, Rose Kissiwa (mgombea pekee wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti), Amina Karuma na Cecilia Mkafum (wanawania ukatibu mkuu).
Wengine ni Zena Chande (mgombea pekee wa nafasi ya Mjumbe Mkutano Mkuu wa TFF) na Sophia Charles na Triphonia Temba wanaowania ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TWFA.

ROBO FAINALI KOMBE LA UHAI LEO

ROBO Fainali za michuano ya Kombe la Uhai inayoshirikisha timu za vijana wenye umri chini ya miaka 20 za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom zitachezwa leo kwenye viwanja vya Karume na Chamazi jijini Dar es Salaam.
Mtibwa Sugar itaumana na African Lyon kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume katika mechi itakayoanza saa 2 kamili asubuhi. Nazo Azam na JKT Ruvu zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Chamazi kuanzia saa 2 kamili asubuhi.
Mechi nyingine ya robo fainali itakuwa kati ya JKT Oljoro na Simba ambayo itachezwa kuanzia saa 9 kamili alasiri kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume. Coastal Union na Ruvu Shooting zitacheza kwenye Uwanja wa Chamazi kuanzia saa 10 kamili jioni.
Nusu fainali ya michuano hiyo itachezwa Ijumaa ya Desemba 21 mwaka huu Uwanja wa Chamazi, wakati fainali na mechi ya kutafuta mshindi wa tatu zitapigwa Jumapili ya Desemba 23 mwaka huu Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.

MABINGWA WA AFRIKA ZAMBIA WATUA LEO DAR

Kikosi cha Zambia kilichotwaa ubingwa wa Afrika mapema mwaka huu
MABINGWA wa Afrika, Zambia ‘Chipolopolo’ wakiwa na msafara wa watu 32 wanatarajiwa kuwasili nchini leo tayari kwa mchezo wa kujipima nguvu dhidi ya Tanzania, Taifa Stars.
Timu hiyo itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 11 kamili jioni kwa ndege ya PrecisionAir ikitokea Lusaka.
Mbali ya wachezaji 24, msafara wa Zambia ambayo inakuja nchini kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars utakuwa na maofisa wengine wanane wakiwemo wa benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Herve Renard aliyeipa timu hiyo ubingwa wa Afrika mwaka jana nchini Gabon.
Wachezaji kwenye msafara huo ni Chintu Kampamba, Chisamba Lungu, Christopher Katongo, Danny Munyau, Davy Kaumbwa, Derrick Mwansa, Evans Kangwa, Felix Katongo na Francis Kasonde.
Given Singuluma, Hichani Himonde, Isaac Chansa, James Chamanga, Jimmy Chisenga, Jonas Sakuwaha, Joshua Titima, Kalililo Kakonje, Moses Phiri, Mukuka Mulenga, Rainford Kalaba, Rodrick Kabwe, Salulani Phiri, Shadrack Malambo na Stoppila Sunzu.
Mechi dhidi ya Taifa Stars itafanyika Jumamosi (Desemba 22 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni. Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager iko kambini jijini Dar es Salaam tangu Desemba 12 mwaka huu chini ya Kocha Kim Poulsen kujiandaa kwa mechi hiyo.
Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya bluu na kijani, sh. 7,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C, sh. 20,000 kwa VIP B wakati VIP A itakuwa sh. 30,000.
Tiketi zinatarajiwa kuanza kuuzwa siku moja kabla ya mechi katika vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Uwanja wa Uhuru, Mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Ohio na Samora, Sokoni Kariakoo, kituo cha mafuta cha Ubungo OilCom na Dar Live Mbagala.
Pia tiketi zitauzwa Ijumaa (Desemba 21 mwaka huu) kwenye tamasha la Kilimanjaro Premium Lager kuhamasisha washabiki wa Taifa Stars litakalofanyika kwenye viwanja vya Sigara, Chang’ombe.


YANGA ONE YAW BERKO AFUZU FC LUPOPO YA DRC KONGO

Berko afuzu majiribio FC Lupopo
Aliyekuwa kipa namba moja wa timu ya Yanga Yaw Berko amefanikiwa kusajiliwa katika timu ya FC Lupopo ya Jamuhuri ya Demokrasia ya Congo.
Berko ambaye alitaka kuachwa na klabu yake aliondoka nchini hivi karibuni kwenda kwenye majaribio na hatimaye amefanikiwa kujiunga na klabu hiyo ambapo tayari klabu yake iliweka wazi kuwa asipofuzu majaribio hayo angetolewa kwa mkopo ili nafasi yake izibwe na pacha wa Mbuyu, Kabange Twite.

Katibu mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako alisema kuwa kuondoka kwa beko haitaifanya timu hiyo kuyumba  na wala haitafanya vibaya  katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu.
Alisema Yanga ni timu kubwa na ina wachezaji wengi wenye uwezo mkuwa hivyo ni matumaini yake kuwa Ally Mstafa ‘Barthez’ pamoja na Said Mohamed wataziba vilivyo nafasi hiyo ya Berko.

“Ukiangalia hata katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, Berko hakucheza mechi nyingi lakini timu ilifanya vizuri hivyo kuondoka kwake  hakutotufanya tuharibu kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu.
“Tunaimani kubwa na makipa wetu waliyopo hivi sasa  kuwa wana uwezo wa kuiongoza timu yetu kuhakikisha inafanya vizuri mzunguko wa pili kama ilivyo kuwa kwa ule wa kwanza kwa sababu wa uwezo na uzoefu na wamecheza ligi yetu kwa muda mrefu,” alisema Mwalusako.

Berko alijiunga na Yanga SC mwaka 2009, akitokea Liberty Proffessional ya Ghana baada ya uwezo wake wa kulinda lango kumvutia aliyekuwa kocha mkuu wa mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mara 22 Kostadin Papic.
Katika hatua nyingine klabu hiyo leo inatarajia kuweka wazi wachezaji wake iliyowaacha na wale iliyowaongeza kwa kwa ajili ya kuhakikisha inatimza Lengo lake la  kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu  msimu huu ambao kwa sasa unashikiliwa na Simba.

CHIPUKIZI YA ZANZIBAR YAJIPANGA NG'WE IJAYO

Association crest 
WAKATI ligi kuu ya soka Zanzibar ikiwa katika mapumziko hadi baada ya kumalizika sherehe za Mapinduzi mwezi ujao, timu mbalimbali za ligi hiyo zimekuwa katika harakati za kuimarisha vikosi vyao.
Katika mchakato huo, timu ya Chipukizi imeamua kuwatema wachezaji wake wanane na kuwapeleka timu mbalimbali na kusajili wachezaji watatu wapya ili kukiongezea nguvu kichosi hicho kilichopania kutwaa ubingwa wa Zanzibar msimu huu.

Naibu Katibu Mkuu wa timu hiyo Adam Abadía, amesema kuwa wachezaji hao wapya wamesajiliwa kuongeza nguvu katika nafasi ambazo zilikuwa na kasoro wakati wa hatua ya kwanza ya ligi kuu.
Hata hivyo, Katibu huyo hakuwa tayari kuyaweka hadharani majina ya wachezaji hao wapya zaidi ya kusema ni wa nafasi ya kiungo wachezaji wawili na mshambuliaji nafasi moja.
Chipukizi inatarajiwa kuweka kambi Mkoani Tanga hivi karibuni, ili kujiweka sawa kabla kwanza kwa ngwe ya pili ya ligi kuu.
Aliwataja wachezaji wanane waliotemwa na timu yake kuwa ni Vuai Abdalla aliyepelekwa Hard Rock na Ameir Daudi kwenda timu ya Machomanne, wote kwa mkopo.
Katibu Mkuu huyo ametoa wito kwa wachezaji wa timu hiyo kuripoti mapema kujiandaa na kambi inayotarajiwa kuanza Disemba 20, mwaka huu mkoani Tanga.

MAUGO NA MATUMLA KUTETEA TAIFA KRISMAS HII

Bondia Mbwana Matumla kushoto akionesha ufundi wa kutupa masumbwi mbele ya kocha wake Pascal Mhagama kwa ajili ya mpambano wake na David Chalanga wa kenya mpambano utakaochezwa Desemba 25 katika ukumbi wa Dar Live

Kocha wa Mchezo wa Masumbwi Said Chaku kushoto akimwelekeza bondia Mada Maugo jinsi ya kutupa Ngumi wakati wa mazoezi yake ya mwisho kwa ajili ya kumkabili bondia Yiga Juma wa Uganda mpambano utakaofanyika Desemba 25 katika ukumbi wa Dar Live jijini Dar es salaam


ZFA YAILIMA BARUA TFF

Uongozi wa chama cha Zanzibar ZDFA Kupitia Rais wa ZDFA Ibrahim makungu kimeshaliandikia Barua  shirikisho la soka la Tanzania TFF ili  kutekeleza adhabu za wachezaji tisa wa Zanzibar kufungiwa kwa mwaka kutokucheza soka nje na ndani ya Zanzibar na kupinga hoja ya kuwa ZDFA haina ubavu wa kuwafungia wachezaji hao.   kwani ZDFA imesema wao ni wanachama wa CECAFA na inauwezo kuwafungia wachezaji kwani kitendo hicho kimefanyika katika mashindano ya CECAFA na hivyo adhabu hiyo kuanza mara moja wachezaji hao wa Zanzibar Heroes waligawana fedha wakiongozwa na Nadi Haroub  fedha hizo walizipata Mara baada ya kuifunga Tanzania Bara katika mashindano hayo, kama tff itaafiki basi wachezaji hao  watafungiwa mwaka mzima .
ZDFA imesema kuwa kitendo hicho cha wachezaji hao hakivumiliki  na wametoa adhabu hiyo ili  iwe fundisho kwa wachezaji wengine .

 

 

Rainford Kalaba KUIKOSA TANZANIA

Japokuwa anaendelea vizuri na maumivu yake ya nyonga alipokuwa  akichezea klabu yake ya TP Mazembe mwezi  October 10 mwaka  2012 katika michuano ya klabu bingwa afrika katika mechi ya nusu fainali dhidi ya  Esperance ya  Tunisia .

Rain ford Kalaba hatokuwemo katika kikosi cha Zambia dhidi ya Tanzania jumamaosi hii , lakini  
Kocha mkuu wa Timu hiyo  Herve Renard anauhakika kuwa mchezaji huyo atakuwa sawa katika uchaguzi wao mkuu wa mwisho wa kuchagua wachezaji 23 wa kushiriki fainali za matafa ya afrika mwakani nchini afrika kusini  2013.

“Kiukweli hatocheza dhidi ya  Tanzania" kwa sasa ameanza mazoezi hivi karibni na ajafanya mazoezi na timu hivi karibuni  ,” Amesema Renard .

“Anafanya mazoezi mwenyewe hii ina maana ndani ya wiki tano unusu atakuwa sawa kujumuika nasi katika mashindano  AFCON.”

Zambia ipo kundi moja la C la  Nigeria, Ethiopia na  Burkina Faso

 

 

WANALAMBA LAMBA WA AZAM WAFANYA USAJILI BABU KUBWA WASAJILI VIFAA NANE, PIGA MAKOFI TAFADHALI

Katika kukiimarisha kikosi chake kwa ajili ya mzunguko wa pili na mashindano ya Afrika Azam FC imefanya usajili wa wachezaji nane wapya katika kipindi hiki cha dirisha dogo
 
Azam FC ambayo ilikuwa na wachezaji wanne wa kimataifa kufuatia George Odhiambo"blackberry" kuondolewa mapema kutokana na utovu wa nidhamu pia iliwapunguza wachezaji Ibrahim Shikanda na Joseph Owino na hivyo kuwa na nafasi tatu za kimataifa
Hatimaye sasa Azam FC imejaza nafasi hizo kwa kuwasajili Jockins Atudo, beki wa kati wa Harambee Stars na klabu ya Tusker FC, Kiungo mshambuliaji wa Harambee Stars na Sofapaka Humphrey Mieno pamoja na mshambualiaji na mchezaji bora wa mashindano ya CECAFA Challenge Cup Brian Umony.
Pia Azam FC imemsajili kinda anayeshika nafasi ya pili kwa kufunga magoli ligi kuu akiwa na magoli sita nyuma ya Kipre Tchetche na Didier Kavumbangu wenye magoli nane kila mmoja Seif Rashid Abdallah toka Ruvu Shooting Stars
Kama hiyo haitoshi Azam FC ambayo ilikuwa na uwakilishi mkubwa zaidi kwenye mashindano ya CECAFA Challenge Cup mwaka huu kwa kuwa na wachezaji 11, imemewarudisha walinzi Malika Ndeule na Omary Mtaki waliocheza katika vilabu vya African Lyon na Mtibwa Sugar katika mzunguko wa kwanza.
 
Katika kuimarisha safu yake ya ulinzi pia imemsajili mlinzi wa kati wa Tanzania Prisons David Mwantika. Na kumsajili kwa mkopo winga wa Simba Uhuru Selemani.
 
Usajili huu umesimamiwa na mwalimu Stewart Hall mwenyewe ambaye anaamini maboresho haya yatakiongezea nguvu kikosi cha Azam FC katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom inayotarajiwa kuanza januari 20.
Kwa mtanzania wa kweli anayejua na kufuatialia mambo ya soka la ukanda wetu wa Afrika Mashariki na kati na nyumbani kwa umakini, atakuwa amekubaliana waziwazi na Stewart kuwa amefanya usajili makini kwa lengo la kufidia mapungufu ya timu hiyo.
Itakumbukukwa baada ya Azam kuwasimamisha kazi wachezaji wake kadhaa kwa tuhuma za rushwa baada ya mchezo dhidi ya  Simba, swali lilikuwa ni namna gani timu hiyo kwa mara moja itaweza kuziba mapengo hayo yalioachwa na wachezaji muhimuj kabisa kikosini.
Wachezaji waliondolewa walikuwa ni pamoja na nahodha Aggrey Moris, mlinzi tegemezi wa pembeni upande wa kulia Erasto Nyoni, mlinzi mzoefu wa kati Saidi Moradi na mlinda mlango Deo Mushi 'Dida' ambao kwa namna moja ama nyingine walikuwa nguzo ya timu hiyo.
    Binafsi nampongeza kocha wa Kingereza Stewart kwa umakini wake huku akijua wazi kuwa Azam wanadhamana ya watanzania ya kuwawakilisha katika michuano mikubwa barani Afrika ya kombe la shirikisho, hongera Stewart.
Nina amini wengi tumeshuhudia michuano ya chalenji ya Kampala katika Luninga zetu na hakuna wakumdanganya mtu kuwa Umony, Atudo na Hamphrey Mieno kwamba hawakuonyesha soka la kuvutia katika michuano hiyo.
Uhuru Selemani na David Mwantika wadau wa kweli wa soka la Bongo lazima watakuwa wanawajua hakuna haja ya maelezo mengi, lakini pia hata Seif Rashid Abdalah wengi wanamjua hivyo tuseme kuwa Azam inastahili pongezi kwa kutumia vema nafasi ya usajili wa dirisha kuongeza nguvu iliyohitajika ili kufikia lengo. 
Vifaa vipya vya Azam Brian Umony mwenye jezi ya njabo na Jockins Atudo mwenye nyekundu wakati wa michuano ya Chalenji.
 Azam FC ipo jijini Kinshasa DRC ikijiandaa na mzunguko wa pili na mashindani ya kimataifa kwa kusaka uzoefu wa kucheza nje ya nchi na imeshacheza michezo miwili na timu za Dragons and FK Sharks ambapo ilitoka sare 1-1 mchezo wa kwanza na kufungwa mchezo wa pili 0-2.
 
Azam FC inatarajia kurejea nchini December 26 ambapo itaelekea visiwani Zanzibar moja kwa moja kushiriki mashindano ya Mapinduzi Cup ambayo inayashikilia.
Rockersports inawatakia ziara njema huko Congo na mrudi salama Tanzania tayari kwa maandalizi ya ligi ili tuone vifaa hivyo vipya vikicheza katika muondo wa timu mpya kabisa.

 

 

MZEE FERGUSON ANASEMA SAFU YAKE YA USHAMBULIAJI YOTE SASA MOTO. WAARABU WA PSG WAANZA VURUGU MADRID, WATANGAZA KUCHUKUA KUKU NA MAYAI YAKE.


MENEJA wa Manchester United Sir Alex Ferguson amekiri kuwa ujio wa Robin van Persie umeimarisha uwezo wa kikosi chake hususani katika eneo la ushambuliaji.
Akiwa tayari ameshatupia wavuni jumla ya mabao 15 , mshambuliaji huyo raia wa uholanzi hajafanya makosa ya kusubiri kujenga jina Old Trafford, huku meneja wake Ferguron mbali ya kumpongeza yeye, lakini pia amekiri kuwa kwa ujumla kikosi kizima cha United kimebadilika kiuwezo kiasi kupelekea washambuliaji wote kuonyesha makali yao.
 
Amenukuliwa Sir Alex akisema,

Eneo la ushambuliaji kwa hakika limeimarika tangu kujiunga kwa Van Persie na kwakweli ametia nguvu  akifunga magoli 14 kabla ya ushindi wetu wa mabao 3-1 dhidi ya Sunderland mpaka sasa"

"Chicharito sasa ana magoli tisa, Rooney magoli saba, nadhani nafikiri tuna magoli 43 kama timu jambo ambalo ni idadi ya juu katika kipindi hiki cha mwaka"


Sir Alex akazidi kwenda mbele zaidi kwa kutoa maoni yake akilinganisha kipindi hiki cha ujio wa Van Persie na mwaka 1992 wakati wa ujio wa Eric Cantona, akisema kila mchezaji anahitaji mazingira ya aina yake kuzoea mazingira

"Van anafanana kisifa na Eric kwa nyakati za ujio unapo zungumzia umri na ukomavu"

"alikuwa na kipindi kizuri sana wakati wa utumishi wake  Arsenal hivyo hakuna haja ya kurubiri kuzoeamazingira ya Premier League.

"ametokea katika klabu kubwa na amekuja katika klabu kubwa na amejiamarisha kumataifa, mambo yote haya ni muhimu kwetu"





PSG imethibitisha kumtaka Mourinho na Cristiano Ronaldo.
 Sheikh Bin Abdulrahman Al-Thani ameweka wazi kuwa Paris Saint-Germain inawataka Cristiano Ronaldo na kocha wake Jose Mourinho kutoka Real Madrid.
Rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi huko nyuma aliwahi kukaririwa akikanusha taarifa kuwa kigogo hicho cha ligi kuu ya nchini Ufaransa Ligue 1 kuwa kilikuwa na mpango wa kumsainisha kocha wa Madrid na Ronaldo lakini mtu wake wa upande wa pili ameibuka na kusema wazi kuwa ili lengo la kutwaa ligi ya vilabu bingwa Ulaya litimie basi lazima watafute watu muafaka.
Akiongea na Canal Football amesema,
"Cristiano Ronaldo na Jose Mourinho ni miongoni mwa malengo yetu hapa Paris Saint-Germain".
"PSG ni miongoni mwa klabu kubwa duniani. Na hivyo moja ya malengo yetu ni kushinda taji la vilabu Ulaya.
"ni klabu kubwa Ufaransa, hivyo lengo ni kuwa klabu bora Ulaya na duniani kwa ujumla"

 

 

 

Cannavaro NA Gianluca Grava WAFUNGIWA MIEZI SITA ITALIA



Timu ya soka ya Napoli inayoshiriki ligi ya Serie A ya italia itapoteza matuamaini yake ya kutaka kuwania ubingwa wa italia itakatwa Alama mbili huku wachezaji wao  Paolo Cannavaro na  Gianluca Grava wakipigwa miezi sita baada ya kushindwa kutoa taarifa kuhusu upangaji wa matokeo chama cha soka cha italia  (FIGC) Kimethibitisha .

Mlinda mlango wa zamani wa Timu ya taifa ya italia  Azzurri Matteo Gianello  amefungiwa  miezi 39 baada ya kukubali tuhuma  kupanga mipango ya upangaji matokeo dhidi ya  Sampdoria mwaka   2010, huku  Cannavaro na  Grava akiadhibiwa kama mwajiri wa timu hiyo na timu yake ikiwajibika kupata adhabu hiyo 

Kamati ya Nidhamu ya imetangaza kupitia tovuti yake  FIGC ikisomeka : " Tumeikata alama mbili  Napoli na  yuro  Elfu sabini 70,000, (ambazo ni sawa na milioni mia moja sitini na moja za kitanzania)   . Huku mlinda mlango huyo akipata adhabu ya kukaa pembeni kwa miaka mitatu na miezi mitatu wakati  Paolo Cannavaro na  Gianluca Grava."
wakichezea miezi sita kila mmoja .

Japokuwa imeanza vizuri msimu huu,  Napoli ipo nyuma kwa alama nane nyuma viongozi wa ligi hiyo na bingwa mtetezi 
 Juventus, na kukatwa kwa alama mbili kunawafanya  kuwanyuma ya vijana wa Walter Mazzarri's wakisukumwa hadi nafasi ya tano nyuma ya Inter Milan, Lazio na  Fiorentina.

Mwanamashtaka  wa FIGC  Stefano Palazzi alitoa wazo la kufungiwa miezi kumi na sita kwa  Gianello, lakini kamati ya Nidhamu ameigiza kuwa kukatwa alama mbili inatosha kwa ilitakiwa kukatwa alama moja huku wachezaji wake wakipata adhabu kubwa zaidi  .

Lakini Napoli, Cannavaro na  Grava wanaonekana kukata rufani katika chama cha  italia  FIGC kabla ya kwenda katika mahamakama ya   TNAS huko  Rome kwani wanaweza kufanikiwa kufutiwa adhabu hiyo 



CRISTIANO RONALDO ANAISHI KWENYE KIVULI CHA LIONEL 'MABAO' MESSI

Mabao 90 ndani ya mwaka mmoja. Chukua muda kufikiria uzito wa jambo hili. Lionel Messi ameweka kambani mabao hayo ndani ya mwaka 2012; anastahili kutukuzwa na kupewa sifa zote kama mchezaji bora kabisa katika kipindi hiki. Ingawa kama ambavyo Messi anavyostahili sifa kutoka kwa mashabiki, wachambuzi wa soka na wachezaji wenzake, Cristiano Ronaldo nae anafanya kazi kubwa katika kuipa mwanga wa mafanikio klabu kubwa duniani yenye maskani yake pale Santiago Bernabeu.
 
Mchezaji ghali zaidi katika historia ya soka amefunga mabao zaidi ya 169 katika miaka mitatu aliyokaa na Real Madrid; hiyo pekee ni mafanikio tosha. Messi amefunga zaidi ya hayo katika kipindi husika, na katika kipindi hicho amefanikiwa kushinda tuzo ya Ballon d'Or mara tatu huku Ronaldo akiwa ameshinda mara moja tu akiwa na klabu ya Manchester United mwaka 2008. Kuna uwezekano mkubwa Messi atashinda tena tuzo hiyo mwaka huu tena kwa haki, mabao 86 yanayoongea kila kitu. Kwa upande mwingine Ronaldo amefunga mabao machache mwakak - 63, japokuwa kwa namna nyingine mafanikio ya Ronaldo yanavutia zaidi ya Messi.

Pale Barcelona, Messi ndio star, ndio mhimili wa timu. Guardiola aliijenga Barcelona yake kumzunguka kijana huyu mfupi wa kiargentina na Vilanova amefuata mfumo huu (nani anaweza kuwalaumu?). Kila mpira unapokuwepo nje ya nusu ya uwanja wao anaangalia Messi, katika mechi  zote za kutoka kipindi kati ya November 2011 mpaka November 2012, Messi amepokea mipira mingi mara mbili zaidi ya Ronaldo alivyopokea, lakini hii inatokana zaidi na staili ya uchezaji wa Barcelona, Messi ameweza kucheza pasi zaidi ya 700 katika tatu ya mwisho ya uwanja na kujaribu kufanya dribbling zaidi ya mara 130 kuliko Ronaldo.

 Mwaka 2012 pekee, Messi alipata kupiga penati 14, ambazo ni idadi kubwa kuliko idadi kubwa zaidi ya ambazo timu yoyte ya Premier League imefanikiwa kupata katika msimu wa 2011/2012. 

Kila ambapo siku zilivyokuwa zikisogea kwa Messi kuifikia rekodi ya mabao 86, wachezaji wengi wa Barca walizungumzia matamanio yao kuona Messi akiweka rekodi hiyo. Huu ni ushahidi tosha namna magoli ya Messi yalivyoaptikana katika miezi kadhaa iliyopita, wachezaji wenzie waliweka mbele ushindi lakini pia kumpa mwenzao nafasi ya kuweka rekodi. Messi amefunga zaidi ya nusu ya mabao ya Barca katika kipindi cha miezi 12 iliyopita.

Njoo upande ya kesi ya Ronaldo ndani ya Real Madrid, anahangaika kugombea spotlight ndani ya moja ya klabu kubwa kabisa duniani. Galaticos wa Mourinho wanaundwa na watu kama Higuian na Karim Benzema katika safu ya ushambuliaji, washambuliaji wenye uchu barani ulaya. Ronaldo alifunga mabao yasiyopungua 60 katika kipindi cha 2011/2012, hii ni idadi kubwa. Benzema na Higuian wanafuatia wa pili na watatu, walifunga mabao 58. Linganisha hizi takwimu na sapoti ambayo Messi anapokea kutoka kwa wachezaji wenzake wa Barcelona kama , Fabregas na Sanchez ambao wamefunga mabao 30 kwa ujumla. Katika mwaka uliopita, Ronaldo amefunga asilimia 42 ya mabao ya Real Madrid wakati Messi amefunga asilimia 56 ya mabao ya Barcelona. 

Umuhimu na namna mabao ya wachezaji jinsi yalivyofungwa yanavutia kusoma: Messi amefunga 91% ya mabao yake katika mwaka uliopita kwa mguu wake wa dhahabu wa kushoto, wakati Ronaldo amefunga 73% ya mabao yake na mguu wake wenye nguvu zaidi wa kulia. Pia Ronaldo amefunga mabao mengi ya ushindi kuliko Messi. Asilimia 21 kwa Ronaldo dhidi ya asilimia 18 za mabao ya ushindi kwa Messi, kwa maana hiyo mabao mengi ya Muargentina huyu aliyafunga wakati mechi tayari timu yake imeshashinda. 

Ukweli ni kwamba ingekuwa Ronaldo anacheza katika kizazi kingine cha soka, angekuwa akitajwa kuwa mchezaji bora wa dunia kwa kipindi hicho. Imekuwa bahati mbaya kwa upande wa Mreno huyu ambaye amekuwa akipambana kumzidi mchezaji wa soka kwa sasa ambaye anacheza kwenye timu bora kabisa kuwahi kutokea katika ulimwengu wa soka.

Baadhi ya watu wanajaribu kusema kwamba Ronaldo ni Andy Murray wa soka, anastahili sifa zaidi lakini ana bahati mbaya ya kucheza katika kipindi kimoja na Messi na Barcelona hii ya miaka ya hivi karibuni.

Wachezaji hawa wawili siku zote wataendelea kupambanishwa; kila mshabiki wa soka ana maoni yake juu ya wachezaji hawa wawili.

Akizungumzia Messi, Pep Guardiola alisema: "Usijaribu kuandika chochte kumhusu, usijaribu kumuelezea, we mtazame tu."
Wakati Mourinho alipomzungumzia Ronaldo alisema: "Kama Messi ndio mchezaji bora wa dunia basi Ronaldo hastahili kuwepo katika hii dunia kwa ubora wake."  

Mwisho wa siku kuwafananisha wachezaji hawa kunaleta mjadala usioisha. Hivyo ni bora kukaa na kutulia kuangalia wachezaji bora kabisa katika historia ya soka wakishindana kila wiki kucheza kwa ubora mchezo ambao mabilioni ya watu tunaupenda.