Sunday, November 25, 2012

NAHODHA SUDAN ATAKA JEZI YA YANGA HATA KESHO

Hamisi Leon, Nahodha wa Sudan Kusini

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Sudan ya Kusini, Hamisi Leon amewataka viongozi wa Yanga waje Uganda katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge kushuhudia uwezo wake kwa mara nyingine.
Mshambuliaji huyo wa Waw Salam ya Sudan Kusini, alikaribia kusajiliwa na Yanga Julai mwaka huu wakati wa michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, lakini akazidiwa kete na Didier Kavumbangu aliyekuwa anachezea Atletico ya Burundi.
Hata hivyo, wakati huu ambao Kavumbangu yuko mbioni kuhamia Qatar anakotakiwa kwa dau zuri, Yanga ina nafasi ya kumsajili Leon.
Akizungumza na waandishi wa habari  katika mahojiano maalum hiyo  jana, Leon ambaye ni Nahodha wa Sudan Kusini alisema kwamba alifanya mazungumzo na Yanga alipokuwa Dar es Salaam na amekuwa na mawasiliano nao hata akiwa Sudan.
Leon alisema kwamba anaipenda Yanga na atafurahi siku moja akijiunga nayo, kwani anaamini atacheza vizuri na kupata mafanikio makubwa.
“Mimi ninajiamini nina uwezo na sibahatishi, nawaambia viongozi wa Yanga waje kuniona tena hapa Uganda, sijui kama watavutiwa na mshambuliaji mwingine zaidi yangu,”alisema Leon.
Leon pamoja na kung’ara katika mchezo wa jana wa Kundi A, dhidi ya Ethiopia, lakini alishindwa kuiepusha timu yake na kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa wawakilishi hao wa CECAFA kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani Afrika Kusini.    

KIFAA KIPYA AZAM CHATISHA KAMPALA, NI MKENYA MIENO MREFU BALAA

Humphrey Mieno
MCHEZAJI mpya wa Azam, Humphrey Mieno jana alionyesha uwezo mkubwa katika mechi ya Kundi A, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge dhidi ya Uganda kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole, mjini hapa.
Akicheza kama kiungo mshambuliaji, Mieno alionyesha uwezo mkubwa wa kumiliki mpira kutulia nao, kutoa pasi na kuwazidi nguvu wachezaji wa timu pinzani katika kugombea mipira, haswa ya juu.
Mieno ambaye ni mrefu, alikuwa akiipa wakati mgumu safu ya ulinzi ya Uganda ambayo ililazimika kumchunga mno.
Ana akili sana ya mchezo- na wakati wote yupo mchezoni na jana mara mbili alikaribia kufunga kama si jitihada za kipa Abel Dhaira, ambaye baadaye alitoka kufuatia kuumia.
Mieno anayechezea Sofapaka ya Kenya, ni kati ya wachezaji watatu walio mbioni kusajiliwa na Azam kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho la soka Afrika (CAF).
Wengine ni Eugene Asike kutoka Sofapaka pia na Serge Wawa Paschal raia wa Ivory Coast anayechezea El Merreikh ya Sudan. Azam FC imepania kuboresha kikosi chake katika dirisha dogo, baada ya kufukuza wachezaji wanne mwishoni mwa mzuynguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa tuhuma za kuhujumu timu hiyo.
Wachezaji hao ni kipa Deo Munishi ‘Dida’ na mabeki Erasto Nyoni, Aggrey Morris na Said Mourad, wanaodaiwa kufanya hujuma katika mechi dhidi ya Simba, Oktoba 27, mwaka huu.
Azam imekwishasema imelifikisha suala hilo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa ajili ya hatua zaidi ili kukomesha desturi hiyo.
Wakati Azam ikiwa katika mpango wa kusajili wachezaji watatu wapya wa kigeni, tayari kikosini ina wachezaji wanne wa kigeni, ambao ni mabeki Mkenya Ibrahim Shikanda, Mganda Joseph Owino na viungo washambuliaji Kipre Michael Balou na Kipre Herman Tcheche kutoka Ivory Coast.
Kwa sababu hiyo, Azam itatakiwa kupunguza wachezaji wawili katika wageni wake wa sasa ili ibaki na wageni watano kulingana na kanuni za Ligi Kuu. Tayari Azam wako katika mpango wa kumuhamishia Simba SC, Owino.
Azam pia mbali na wachezaji wa kigeni, imejipanga kusajili wachezaji wakali wa nyumbani, waliong’ara katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, ili kuimarisha zaidi kikosi chake.      

KOCHA KENYA ALILIA KITASA CHA AZAM


Shikanda
KOCHA wa muda wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, James Nandwa amesikitika kumkosa beki wa Azam FC ya Tanzania, Ibrahim Shikanda katika Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, Tusker Challenge zinazoendelea mjini hapa.
Akizungumza  katika mahojiano maalum mjini namboole uganda jana Nandwa anayemshikia timu hiyo kwa muda Mfaransa Henri Michel, alisema kwamba alimuita Shikanda katika kikosi chake cha Tusker Challenge, lakini akashindwa kuja kwa sababu ni majeruhi.
“Nilimuita Shikanda, lakini akasema yeye ni mgonjwa hawezi kuja, kwa kweli kwangu na kwa benchi zima la ufundi tumesikitika kumkosa beki mzuri kama Yule, ambaye anafanya vizuri hadi katika klabu yake,”alisema Nandwa.
Hata hivyo, kocha huyo alisema kwamba anakubaliana na matokeo na ataendelea na wachezaji alionao kuhakikisha kwamba anarejea na Kombe Kenya.
“Michuano ni migumu, hasa kundi letu, kama unavyoona tumefungwa na Uganda, lakini bahati haikuwa yetu. Tulitengeneza nafasi nyingi tukashindwa kuzitumia, wenzetu wametumia nafasi waliyopata.
Na ugumu zaidi upo kwenye kundi. Hakuna timu dhaifu. Kuna Ethiopia ambao wamefuzu kucheza Fainali za AFCON (Mataifa ya Afrika). Sudan Kusini umewaona wameisumbua Ethiopia, hili ni kundi gumu sana,”alisema Nandwa.
Hata hivyo, amesema watapambana kushinda mechi zao zote zilizosalia ili watinge Robo Fainali.    
Kenya jana wameanza vibaya CECAFA Tusker Challenge baada ya kuchapwa na Uganda bao 1-0 kwenye Uwanja wa Mandela, uliopo Namboole, Kampala, Uganda.
Mbaya wao jana alikuwa ni mshambuliaji wa Saigon Xuan Thanh ya Vietnam, Geoffrey Kizito aliyefunga bao hilo pekee la ushindi dakika ya 74, akiunganisha krosi ya Iguma Dennis.
Kwa ushindi huo, Korongo wa Kampala anafungana na Ethiopia kuongoza Kundi A, kwa pointi zake tatu kila timu. 
Hadi mapumziko hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango la mwenzake na timu zote zilishambuliana kwa zamu.
Kenya walianza kwa kasi kwa dakika tano wakicheza soka iliyowasisimua mashabiki wake wachache waliokuwapo uwanjani, lakini Uganda wakazinduka nao na kuanza kuwapa raha mashabiki wao kwa soka safi.
Mchezo uliendelea kuwa hivyo kwa timu hizo kushambuliana kwa zamu, kila upande wakicheza kwa kujiamini.
Lakini sifa ziende kwa safu zote mbili za ulinzi kutokana na kucheza kwa umakini wa hali ya juu.
Kipindi cha pili timu hizo ziliporejea uwanjani, zililazimika kusimama kwa takriban dakika saba baada ya taa za uwanjani kuzimika na baada ya mafundi kutatua tatizo hilo, ndipo kabumbu likaanza tena.  
Michuno hiyo itaendelea kesho kwa mechi mbili, Burundi na Somalia saa 10:00 jioni na baadaye Tanzania Bara na Sudan saa 12:00 jioni.
Uganda; Abel Dhaira/Hamza Muwonge, Iguma Dennis, Godfrey Walusimbi,Henry kalungi, Isaac isinde, Hassan Wasswa, Geoffrey Kizito, Moses Oloya, Emmanuel Okwi, Hamisi Kiiza na Brian Umony.
Kenya; Duncan Ochieng, Anthony Kimani, Abdallah Juma, Jockins Atudo, David Owino, David Ochieng, Lama Salim Mohamed, Bernard Wanyama, Humphrey Mieno, Anthony ‘Muki’ Kimani/Enock Obiero na Clifton Miheso/Paul Were.

MZUNGU WA CRANES ASEMA KIIZA NA OKWI NDIO KILA KITU KAMPENI ZA UBINGWA TUSKER CHALLENGE

Okwi wa kwanza kulia waliosimama na Kiiza mbele yake

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Uganda, The Cranes, Bobby Williamson raia wa Scotland, amesema kwamba wachezaji Hamisi Friday Kiiza na Emmanuel Arnold Okwi ni tegemeo lake katika kampeni za kutwaa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge mwaka huu mjini hapa.
Akizungumza katika mahojiano maalum mjini kampala, kocha huyo kipenzi cha Waganda alisema anawategemea sana Okwi na Kiiza kutwaa taji la pili mfululizo la Tusker Challenge katika fainali za nyumbani.
Alisema wachezaji hao wamekuwa wakiimarika siku hadi siku na ndiyo maana ameendelea kuwa nao katika kikosi cha The Cranes tangu ameana nao miaka mitatu iliyopita.
“Kila siku uwezo wao unazidi kupanda na nadhani wakati au bahati yao ya kucheza Ulaya haijafika tu, wote ni viwango vya kucheza Ulaya au nchi nyingine kubwa kuliko kwetu Afrika Mashariki,”alisema.
Aliwasifu wana nidhamu na ni wazalendo- wana mapenzi na timu yao ya taifa. “Wanajituma sana nikiwa nao, wana nidhamu na wanapenda nchi yao, nawapenda sana, wananifurahisha,”alisema.
Bobby alizipongeza pia klabu zao, Simba (Okwi) na Yanga (Kiiza) zote za Tanzania kwa kuwatunza na kuwalea vizuri wachezaji hao, ndiyo maana uwezo wao umekuwa ukipanda siku hadi siku.
“Unajua mchezaji anatunzwa na klabu, kama klabu haikai vizuri na mchezaji hawezi kuwa katika kiwango kizuri, na kama hana kiwango kizuri siwezi kumchukua timu ya taifa. Kwa hivyo hata klabu zao nazishukuru kwa kunilelea vizuri hawa vijana,”alisema.
Okwi na Kiiza jana waliiongoza Cranes kuilaza 1-0 Kenya katika mchezo wa ufunguzi wa Tusker Challenge uliopigwa kwenye Uwanja wa Mandela, uliopo Namboole, Kampala, Uganda.
Shukrani kwake, mshambuliaji wa Saigon Xuan Thanh ya Vietnam, Geoffrey Kizito aliyefunga bao hilo pekee la ushindi dakika ya 74, akiunganisha krosi ya Iguma Dennis.
Kwa ushindi huo, Korongo wa Kampala anafungana na Ethiopia kuongoza Kundi A, kwa pointi zake tatu kila timu. 
Hadi mapumziko hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango la mwenzake na timu zote zilishambuliana kwa zamu.
Kenya walianza kwa kasi kwa dakika tano wakicheza soka iliyowasisimua mashabiki wake wachache waliokuwapo uwanjani, lakini Uganda wakazinduka nao na kuanza kuwapa raha mashabiki wao kwa soka safi.
Mchezo uliendelea kuwa hivyo kwa timu hizo kushambuliana kwa zamu, kila upande wakicheza kwa kujiamini.
Lakini sifa ziende kwa safu zote mbili za ulinzi kutokana na kucheza kwa umakini wa hali ya juu.
Kipindi cha pili timu hizo ziliporejea uwanjani, zililazimika kusimama kwa takriban dakika saba baada ya taa za uwanjani kuzimika na baada ya mafundi kutatua tatizo hilo, ndipo kabumbu likaanza tena.  
Michuno hiyo itaendelea kesho kwa mechi mbili, Burundi na Somalia saa 10:00 jioni na baadaye Tanzania Bara na Sudan saa 12:00 jioni.
Katika mchezo huo, kikosi cha Uganda kilikuwa; Abel Dhaira/Hamza Muwonge, Iguma Dennis, Godfrey Walusimbi,Henry kalungi, Isaac isinde, Hassan Wasswa, Geoffrey Kizito, Moses Oloya, Emmanuel Okwi, Hamisi Kiiza na Brian Umony.
Kenya; Duncan Ochieng, Anthony Kimani, Abdallah Juma, Jockins Atudo, David Owino, David Ochieng, Lama Salim Mohamed, Bernard Wanyama, Humphrey Mieno, Anthony ‘Muki’ Kimani/Enock Obiero na Clifton Miheso/Paul Were.

STARS YAANZA KAZI KAMPALA LEO USIKU

John Bocco 'Adebayor' ataongoza safu ya ushambuliaji Stars leo?

TIMU ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars leo inatarajiwa kuanza kampeni zake za kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge leo itakapomenyana na Sudan kuanzia saa 12:00 jioni Uwanja wa Mandela, Namboole mjini hapa.
Mchezo huo, utatanguliwa na mchezo mwingine wa Kundi B kati ya Somalia na Burundi, kuanzia saa 10:00 jioni kwenye Uwanja huo huo.
Kocha wa Kilimanjaro Stars, Mdenmark Kim Poulsen amesikitishwa na kutowasili kwa washambuliaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
“Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaweza wasicheze katika mechi ya kwanza kwa sababu hawajafika, lakini mimi nikiwa kocha nimejiandaa vizuri na nina imani na wachezaji waliopo,” alisema.
“Nina imani TFF wanafuatilia suala hili na wachezaji hawa watajiunga na wenzao hivi karibuni lakini hii haituzuii kufanya vizuri kwani tumejiandaa vizuri,” alisema.
Alisema wachezaji wote wana hali nzuri na wana ari ya kushinda mechi yao ya kwanza dhidi ya Sudan ambazi zimo katika Kundi B pamoja na Burundi na Somalia ambazo zitacheza leo pia.
Hata hivyo, jana Kili Stars walilalamikia Uwanja mbovu wa Chuo Kikuu cha Kampala Kampasi ya Biashara, waliopelekwa kufanya mazoezi kujiandaa na mechi ya leo.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura aliwasilisha malalamiko hayo kwa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Uganda (FUFA), Rodgers Mulindwa ambaye ameahidi kuyafanyia kazi.
“Tutalifanyia kazi suala hilo, tutakuwa na kikao kesho (leo) litawasilishwa na litapatiwa usumbufu, mwanzo huwa na matatizo, lakini mambo yatakuwa mazuri,”alisema Mulindwa.
Hata hivyo, inashangaza Stars kupelekwa katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Kampala Kampasi ya Biashara, wakati kwenye mpango wa awali kabisa wa FUFA ilitakiwa kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Nakawa.    

UGANDA NA KENYA KATIKA PICHA LEO NAMBOOLE

Wachezaji wa Uganda, The Cranes wakimpongeza Geoffrey Kizito wa mbele kulia, baada ya kuwafungia bao pekee la ushindi dhidi ya Kenya, Harambee Stars katika mchezo wa Kundi A, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge Uwanja wa Mandela, Namboole usiku wa leo. 

Kizito akikimbia kushangilia

Kizito akishangilia na Brian Umony nyuma yake aliyempanda mgongoni

Humphrey Miano wa Kenya kushoto akigombea mpira na Kizito. Kulia ni David Ochieng wa Kenya pia

David Owino wa Kenya akimdhibiti Hamisi Kiiza wa Uganda mbele yake

Owino na Kiiza
Owino na Kiiza

Gwaride la sherehe za ufunguzi wa mashindano

UGANDA YAICHAPA KENYA 1-0 TUSKER CHALLENGE

Kizito akishangilia baada ya kufunga usiku huu Uwanja wa Mandela. Kushoto ni Hamisi Kiiza akimkimbilia kumpongeza

WENYEJI Uganda, The Cranes wameanza vema michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge baada ya kuilaza Kenya, Harambee Stars bao 1-0 kwenye Uwanja wa Mandela, uliopo Namboole, Kampala, Uganda.
Shukrani kwake, mshambuliaji wa Saigon Xuan Thanh ya Vietnam, Geoffrey Kizito aliyefunga bao hilo pekee la ushindi dakika ya 74, akiunganisha krosi ya Iguma Dennis.
Kwa ushindi huo, Korongo wa Kampala anafungana na Ethiopia kuongoza Kundi A, kwa pointi zake tatu kila timu.  
Hadi mapumziko hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango la mwenzake na timu zote zilishambuliana kwa zamu.
Kenya walianza kwa kasi kwa dakika tano wakicheza soka iliyowasisimua mashabiki wake wachache waliokuwapo uwanjani, lakini Uganda wakazinduka nao na kuanza kuwapa raha mashabiki wao kwa soka safi.
Mchezo uliendelea kuwa hivyo kwa timu hizo kushambuliana kwa zamu, kila upande wakicheza kwa kujiamini.
Lakini sifa ziende kwa safu zote mbili za ulinzi kutokana na kucheza kwa umakini wa hali ya juu.
Kipindi cha pili timu hizo ziliporejea uwanjani, zililazimika kusimama kwa takriban dakika saba baada ya taa za uwanjani kuzimika na baada ya mafundi kutatua tatizo hilo, ndipo kabumbu likaanza tena.   
Michuno hiyo itaendelea kesho kwa mechi mbili, Burundi na Somalia saa 10:00 jioni na baadaye Tanzania Bara na Sudan saa 12:00 jioni.
Uganda; Abel Dhaira/Hamza Muwonge, Iguma Dennis, Godfrey Walusimbi,Henry kalungi, Isaac isinde, Hassan Wasswa, Geoffrey Kizito, Moses Oloya, Emmanuel Okwi, Hamisi Kiiza na Brian Umony.
Kenya; Duncan Ochieng, Anthony Kimani, Abdallah Juma, Jockins Atudo, David Owino, David Ochieng, Lama Salim Mohamed, Bernard Wanyama, Humphrey Mieno, Anthony ‘Muki’ Kimani/Enock Obiero na Clifton Miheso/Paul Were.


HATTON ASTAAFU NGUMI KWA MARA YA PILI BAADA YA KIPIGO.

BONDIA Ricky Hatton kutoka Uingereza mbaye amewahi kuwa bingwa wa dunia wa uzito wa Light Weight ametangaza kustaafu tena mchezo huo baada ya kupewa kipigo na Vyacheslay Senchenko katika pambano lililofanyika jijini Manchester. Hatton mwenye umri wa miaka 34 hajapigana toka mwaka 2009 lakini kurejea kwake ulingoni baada ya muda huyo kuliishia katika raundi ya tisa katika pambano hilo lililofanyika Jumamosi. Bondia anadai kuwa alikuwa akihitaji pambano moja ili kuona kama anaweza kurejesha makali yake kama zamani lakini hilo limeshindikana hivyo hana budi kuachana na mchezo huo ili kufanya mambo mengine. Hatton alitangza kurejea ulingoni Septemba mwaka huu ikiwa ni miezi 14 toka alipotangaza kustaafu mchezo huo kwa mara kwanza. Pambano la mwisho kucheza kabla ya kuamua kuachana na mchezo huo lilikuwa dhidi ya Manny Pacquiao lililofanyika jijini Las Vegas, Marekani mwaka 2009 ambalo alipoteza. 

SNEIJDER HATIHATI INTER.

MENEJA wa michezo wa klabu ya Inter Milan, Marco Branca amependekeza kuwa kiungo Wesley Sneijder hatachezeshwa mpaka atakapokubali kuongeza mkataba wake. Kiungo huyo wa kimataifa kutoka Uholanzi mwenye umri wa miaka 28 amekuwa nje ya uwanja toka Septemba mwaka huu baada ya kuumia amekuwa akihusishwa na taarifa za kuondoka katika klabu hiyo katika kipindi cha dirisha dogo la usajili Januari mwaka huu. Sneijder alihusishwa na taarifa za kuhamia Uingereza katika klabu ya Manchester United mwaka 2011 lakini alikanusha tetesi hizo na kudai hajafanya mazungumzo rasmi juu ya kuhamia huko. Branca amesema kuwa kwasasa watakuwa wavumilivu wakati wakiangalia uwezekano wa kumshawishi nyota huyo ili aongeze mkataba utakaomuwezesha kubakia klabuni hapa kwa muda zaidi. Sneijder alijiunga na Inter Milan mwaka 2009 akiwa amecheza katika vilabu vya Ajax Amsterdam ya Uholanzi na Real Madrid ya Hispania.

GUARDIOLA AIMEZEA MATE BRAZIL.

MENEJA wa zamani wa klabu ya Barcelona, Pep Guardiola atafurahi kama akipewa kibarua cha kuinoa Brazil ambayo wiki iliyopita ilimtimua kocha wake Mano Menezes. Tetesi hizo Guardiola kutaka kuinoa Brazil ziliandikwa na gazeti la michezo la Lance ambalo lilidai kutoa taarifa hizo kwa mtu wa karibu wa kocha huyo. Guardiola ambaye aliifundisha Barcelona kwa mafanikio baada ya kuchukua mikoba ya kuinoa kutoka kwa Frank Rijkaard mwaka 2008, aliamua kuacha kuifundisha timu hiyo katika kipindi cha majira ya kiangazi na kuamua kupumzika. Katika kipindi cha miaka minne ambayo amekuwa akiinoa Barcelona, Guardiola amefanikiwa kunyakuwa mataji 14 yakiwemo mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

BOLT, FELIX WANYAKUWA TUZO YA WANARIADHA BORA WA MWAKA.

WANARIADHA nyota wanaoshikilia medali za dhahabu katika michuano ya Olimpiki, Usain Bolt na Allyson Felix wamenyakuwa tuzo ya wanariadha bora wa mwaka kwa wanaume na wanawake. Wanaridha hao walitunukiwa tuzo hizo na Shirikisho la Riadha la Kimataifa-IAAF katika sherehe zilizofanyika jijini Barcelna, Hispania jana. Bolt ambaye ni raia wa Jamaica alifanikiwa kutetea medali zake katika mbio za mita 100 na 200 jijini London anakuwa mwanaridha wa kwanza kushinda tuzo hiyo mara nne mfululizo. Katika michuano ya olimpiki Felix alinyakuwa medali tatu za dhahabu na kufanikiwa kunyakuwa tuzo hiyo mbele ya Jessica Ennis wa Uingereza ambaye naye alikuwepo katika orodha ya mwisho ya wawanariadha wanaogomea tuzo hiyo. 
Felix ambaye anatoka Marekani alifanikiwa kunyakuwa medali za dhahabu katika mbio za mita 200 na pia alikuwa sehemu ya wanariadha walioshinda mbio za kupokezana vijiti za mita 100 na 400 hivyo kuwa mwanamke wa kwanza kushinda medali tatu za dhahabu katika michuano hiyo toka mwaka 1988.

MOURINHO ALIA NA MWAMUZI.

BAO lililofugwa na Benat Etxebarria jana usiku liliipa ushindi wa kushangaza wa bao 1-0 dhidi ya Real Madrid katika mchezo uliochezwa jijini Seville na kuwaacha mabingwa hao watetezi nyuma kwa alama nane kwa Barcelona ambao wanaongoza La Liga huku wakiwa bado na mchezo mmoja mkononi. Matokeo hayo yanaifanya Madrid kubakia katika nafasi ya tatu wakiwa wamejikusanyia alama 26, huku wakiwa wamepitwa alama tano na Atletico Madrid ambao wanashika nafasi ya pili. Mahasimu wa Madrid, Barcelona wanaweza kuongeza pengo na kufikisha alama 11 kama wakiwafanikiwa kushinda mchezo wao wa baadae leo dhidi ya Levante ambao wanashika nafasi ya sita. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo meneja wa Madrid Jose Mourinho amelaumu waamuzi kwa kushindwa kumudu mchezo huo na kuonyesha upendeleo kwa wapinzani wao kitu ambacho kilichangia kwa kiasi wao kupoteza mchezo huo muhimu.

RONALDO DE LIMA: PEP GUARDIOLA ANA VIGEZO VYOTE VYA KUINGOZA BRAZIL . CARLO ANCELOTTI BADO ANAMTAMANI ALEXANDRE PATO. BRANDAN ROGERS ANASEMA LIVERPOOL MATAJI BADO KIDOGO NA BAADA YA KUSHINDWA KUWAFUNGA ASTON VILL WENGER ANASEMA WALICHOSHWA NA MONTPELLIER.


 Ronaldo De Lima ambaye kwasasa ana heshima kubwa nchini kwake Brazil amesema kocha wa zamani wa  Barcelona Pep Guardiola ndiye chaguo lake la kwanza kurithi nafasi ya Mano Menezes aliyetimuliwa kazi hivi karibuni.
Kocha Menezes alitimuliwa kazi ijumaa baada ya kile kilichoelezwa kuwa hakuwa na matokeo mazuri katika michezo mbalimbali ya timu ya taifa hilo wakati huu ambapo Brazil ambayo inaandaa michuano ya kombe la dunia 2016.
Japo kwamba Ronaldo hakubaliani na maamuzi ya kufukuzwa kazi Menezes, amesema itakuwa ni vema kumsaka kocha ambaye ana vigezo sahihi ambayo ni kama alivyo navyo kocha wa zamani wa Barcelona Pep Guardiola.
Akiongea na Globo, amesema.
"kila mtu anapapara, lakini kila siku unatakiwa kuangalia kwa picha kubwa. Siwezi kufanya maamuzi hayo, lakini  Brazil inahitaji kurejea tulikokuwa tena,"
"tuna makocha wakubwa Brazil, na tunahitaji mtu ambaye anaonyesha utulivu ndani ya timu,
"Guardiola ni kocha bora duniani kwasasa. Alifanya kazi nzuri Barcelona na anaweza kuwa chaguo bora kwa Brazil. Hebu tuone kama mashabiki watampenda ama laa"

Rodgers: Liverpool itatwaa mataji muda si mrefu.
Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers amesema miaka michache ijayo klabu yake italeta changamoto mpya ya kutwaa mataji ya ligi ya England.
Kwasasa Liverpool iko katika 12 katika msimamo wa ligi kuu ambapo kuelekea kweny mchezo dhidi ya Swansea City kocha huyo anayetokea Ireland ya kaskazini anasena anamatumaini kuwa mazuri.
Liverpool haiajawahi kumaliza ligi kuu ya England ikiwa katika nafasi ya kucheza michuano ya klabu bingwa Ulaya tangu Rafa Benitez alipokuwa akiiongoza na kwasasa iko nyuma ya kikosi cha kocha wao huyo wa zamani kwa alama tisa ambapo Chelsea iko katika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi ya England.
Rodgers anasisitiza kuwa pamoaj na kwamba kujenga kikosi ni muhimu lakini pia ina weza ikato changamoto muda mfupi ujao na kuwapa raha mashabiki wake.
"sioni sababu ya kwanini tusitoe changamoto katika kipindi cha miaka michache ijayo. Wakati mwingine unaweza kudondoka kwa hatua chache kabla ujaanza kujijenga upya"
Kwasasa Luis Suarez wa Liverpool anaongoza orodha ya wafungaji wa Premier League akiwa tayari amefunga jumla ya mabao 10 baada ya michezo 12 ya msimu huu ambapo Rodgers amesema ataendelea kumtumia mruguayi ambaye yuko kwenye fomu.
Ancelotti: Pato anastahili kuchezea Paris Saint-Germain.
 Carlo Ancelotti amezidi kutia utambi tetesi za Paris Saint-Germain kuwa huenda waanzisha tena mpango wao wa kumtaka mshambuliaji wa AC Milan Alexandre Pato akidai kuwa mshambuliaji huyo ana vigezo vyote vinavyotakiwa.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa iliaminika kuwa alikiwa karibu kukamilisha uhamisho wake wa euro milioni 35 kuelekea Parc des Princes mwezi Januari lakini baadaye mpango huo ukaonekana kwenda kombo.
Hata hivyo kuna taarifa kuwa pande mbili hizo zinaelekea kukubaliana kutokana na kile kinachoelezwa kuwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 hana raha na maisha ya soka ndani ya klabu ya AC Milan.
Wakati hayo yakiwa hivyo, Ancelotti ambaye alimfundisha mshambuliaji huyo kule Rossoneri kati hya miaka ya 2007 na 2009 ameeleza kuwa nyota huyo kutoka Marekani ya Kusini anafanana na hadhi ya PSG na shaka yoyote uwezo wake.
"hajawahi kunipigia simu. Mimi si rafiki yake alikuwa mchezaji wangu nilipokuwa Milan, lakini kiukweli ana vigezo vya kuichezea PSG"
"ni mfungaji mzuri lakini hatuwesi kusaini wafungaji wote wazuri duniani. Tuna wachezaji katika nafasi hiyo kama vile Jeremy Menez, Ezequiel Lavezzi na Zlatan Ibrahimovic."
Wenger ajitetea baada yua kushindwa kuwafunga Aston Villa.
 Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa kilicho wafanya washindwe kuifunga Aston Villa na kwenda sare ya bila mabao ni mchoko.
Washika mtutu walishinda kutengeneza nafasi dhidi ya Villa na kulazimika kugawana alama moja kila upande matokeo ambayo yamewaweka mbele kwa tofauti ya alama moja dhidi ya Chelsea katika msimamo wa ligi.
Mchezo wa katikati ya wiki dhidi ya Montpellier ilipelekea meneja huyo kuwapumzisha vijana wake kutoka katika jiji la London Jack Wilshere, Bacary Sagna na Thomas Vermaelen katika mchezo huo.
Wenger anaamini mchezo wa katikati ya wiki ulikuwa ni sehemu ya sababu za vijana wake kucheza chini ya kiwango jambo ambalo hakulipinga kuwa walikuwa chini ya kiwango.
Arsenal imefunga goli moja tu katika michezo mitatu iliyocheza ugenini.
Matokeo hayo yanamfanya wenger kusema
"ni kweli. Ila sijui sababu ni nini. Tuna timu nzuri ya ulinzi na tuna wachezaji wazuri wazuiaji sehemu ya kiungo na tuna washambuliaji watatu, lakini hii inaweza kutokea iliwakutokea huko nyuma ni tofauti unapocheza nyumbani na ugenini."

 

 

BPL: Arsenal yanasa Villa Park, yatoka 0-0 na Villa!

 >>YABAKI nafasi ya 6, kuenguliwa na West Ham Jumapili??
+++++++++++++++++++++++
MATOKEO:
Jumamosi Novemba 24
Sunderland 2 West Brom 4
Everton 1 Norwich 1
Man United 3 QPR 1
Stoke 1 Fulham 0
Wigan 3 Reading 2
Aston Villa 0 Arsenal 0
+++++++++++++++++++++++
WENGER_AHIMIZA12Arsenal leo imeshindwa kujitutumua na kujisogeza mbele kwenye Msimamo wa Ligi Kuu England walipotoka sare ya 0-0 na Aston Villa Uwanjani Villa Park na kubaki nafasi yao ile ile ya 6 lakini wapo hatarini kupokonywa endapo Jumapili, West Ham wataifunga Tottenham katika Mechi itakayochezwa Uwanjani White Hart Lane.
Mechi hii, iliyochezwa kwenye Mvua kubwa, ilikuwa na kosa kosa za kila upande na Villa pia kunyimwa Bao baada ya Andreas Weimann kufunga lakini uamuzi ukawa ni Ofsaidi.
Mwishoni, Arsenal walikuja juu lakini wakakosa Bao kadhaa hasa Aaron Ramsey aliekosa nafasi mbili za wazi.
Mechi ifuatayo kwa Arsenal ni hapo Jumatano Usiku watakapokuwa Uwanjani Goodison Park wakiwa wageni wa Everton.
VIKOSI:
Aston Villa: Guzan, Lowton, Vlaar, Clark, Stevens, El Ahmadi, Westwood, Weimann, Bannan, Agbonlahor, Benteke
Akiba: Given, Ireland, Albrighton, Holman, Delph, Bowery, Lichaj.
Arsenal: Szczesny, Jenkinson, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Arteta, Ramsey, Oxlade-Chamberlain, Cazorla, Podolski, Giroud
Akiba: Mannone, Sagna, Vermaelen, Wilshere, Coquelin, Arshavin, Gervinho.
Refa: Lee Mason .
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO:
1 Man United Mechi 13 Pointi 30
2 Man City Mechi 12 Pointi 28
3 WBA Mechi 13 Pointi 26
4 Chelsea Mechi 12 Pointi 24
5 Everton Mechi 13 Pointi 21
6 Arsenal Mechi 13 Pointi 20
7 West Ham Mechi 12 Pointi 19
8 Tottenham Mechi 12 Pointi 17
9 Fulham Mechi 13 Pointi 16
10 Swansea Mechi 12 Pointi 16
11 Stoke City Mechi 13 Pointi 16
12 Liverpool Mechi 12 Pointi 15
13 Norwich Mechi 13 Pointi 15
14 Newcastle Mechi 12 Pointi 14
15 Wigan Mechi 13 Pointi 14
16 Sunderland Mechi 12 Pointi 12
17 Aston Villa Mechi 13 Pointi 10
18 Reading Mechi 12 Pointi 9
19 Southampton Mechi 12 Pointi 8
20 QPR Mechi 13 Pointi 4
+++++++++++++++++++++++
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumapili Novemba 25
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Swansea v Liverpool
[SAA 12 Jioni]
Southampton v Newcastle
[SAA 1 Usiku]
Chelsea v Man City
Tottenham v West Ham
Jumanne Novemba 27
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Sunderland v QPR
[SAA 5 Usiku]
Aston Villa v Reading
Jumatano Novemba 28
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Chelsea v Fulham
Everton v Arsenal
Southampton v Norwich
Stoke v Newcastle
Swansea v West Brom
Tottenham v Liverpool
Man United v West Ham
[SAA 5 Usiku]
Wigan v Man City


BPL: Man United waipiku City wapo kileleni, WBA yaipiku Chelsea iko 3!!

Katika Mechi za BPL, Barclays Premier League, Ligi Kuu England, zilizochezwa leo, Manchester United walitoka nyuma kwa Bao 1-0 na kupiga Bao 3 ndani ya Dakika 8 na kutwaa uongozi wakiwa Pointi mbili mbele ya Mabingwa Watetezi Man City ambao kesho wapo Stamford Bridge kucheza na Chelsea ambao leo wameipoteza nafasi yao ya 3 iliyochukuliwa na West Bromwich Albion walioshinda ugenini dhidi ya Sunderland.
+++++++++++++++++++++++
RATIBA/MATOKEO:
Jumamosi Novemba 24
Sunderland 2 West Brom 4
Everton 1 Norwich 1
Man United 3 QPR 1
Stoke 1 Fulham 0
Wigan 3 Reading 2
[SAA 2 Dak 30 Usiku]
Aston Villa V Arsenal
MAN UNITED 3 QPR 1
BPL_LOGOMeneja mpya wa QPR Harry Redknapp alikuwepo kwenye Jukwaa la Watazamaji akishuhudia Timu yake ikifunga Bao la kuongoza kupitia Jamie Macjie katika Dakika ya 64 lakini Bao 3 ndani ya Dakika 8 ziliwapa ushindi Manchester United wa Bao 3-1  wakiwa nyumbani kwao Old Trafford.
Bao za Man United zilifungwa na Jonny Evans, Dakika ya 64, Darren Fletcher Dakika ya 68 na Javier Hernandez Dakika ya 72.
Ushindi huo, ambao umefanya Man United wakae tena kileleni mwa Ligi wakiwa Pointi 2 mbele ya Man City, ulikuja baada ya Meneja Sir Alex Ferguson kuwatoa Paul Scholes na Ashley Young na kuwaingiza Anderson na Chicharito ambao walileta uhai kwenye Timu.
QPR wanaendelea kubaki mkiani.
VIKOSI:
Man United: Lindegaard, Da Silva, Evans, Ferdinand, Evra, Young, Fletcher, Scholes, Rooney, Welbeck, van Persie
Akiba: De Gea, Jones, Anderson, Smalling, Hernandez, Cleverley, Powell.
QPR: Julio Cesar, Hill, Nelsen, Mbia, Traore, Derry, Faurlin, Mackie, Taarabt, Dyer, Cisse
Akiba: Green, Diakite, Ferdinand, Wright-Phillips, Granero, Ephraim, Hoilett.
Refa: Lee Probert
WIGAN 3 READING 2
Hetitriki ya Jordi Gomez imewapa Wigan ushindi wa Bao 3-2 ndani ya Uwanja wao DW Stadium dhidi ya Reading ambao walifunga Bao zao kupitia Morrison na la pili baada ya Kipa wa Wigan Al Habsi kujifunga mwenyewe.
VIKOSI:
Wigan: Al Habsi, Boyce, Ramis, Figueroa, Stam, McCarthy, Jones, Beausejour, Gomez, Kone, Maloney
Akiba: Pollitt, Di Santo, McManaman, McArthur, Boselli, Fyvie, Lopez.
Reading: Federici, Gunter, Morrison, Gorkss, Shorey, Robson-Kanu, Leigertwood, Tabb, McAnuff, Le Fondre, Roberts
Akiba: Taylor, Mariappa, Pogrebnyak, Hunt, McCleary, Harte, Cummings.
Referee: Howard Webb
EVERTON 1 NORWICH 1
Bao la kusawazisha la Dakika ya 90 la Sebastian Bassong limewapa sare ya 1-1 Norwich ambao walikuwa ugenini Uwanja wa Goodison Park ambapo Everton walitangulia kufunga katika Dakika ya 12 kwa Bao la Steven Naismith.
Hii ni Mechi ya 6 mfululizo kwenye Ligi kwa Norwich kutopoteza Mechi.
VIKOSI:
Everton: Howard, Jagielka, Heitinga, Distin, Baines, Pienaar, Naismith, Hitzlsperger, Oviedo, Osman, Jelavic
Akiba: Mucha, Hibbert, Gueye, Barkley, Vellios, Kennedy, Duffy.
Norwich: Ruddy, Whittaker, Bassong, Ryan Bennett, Garrido, Johnson, Tettey, Snodgrass, Hoolahan, Pilkington, Holt
Akiba: Bunn, Howson, Jackson, Morison, Elliott Bennett, Barnett, Tierney.
Refa: Mike Jones
STOKE 1 FULHAM 0
Bao la Dakika ya 26 la Kiungo Charlie Adam baada ya kushushiwa na Peter Crouch limewapa Stoke City ushindi wa Bao 1-0 dhidi ya Fulham.
VIKOSI:
Stoke: Begovic, Cameron, Shawcross, Huth, Shotton, Walters, Nzonzi, Whelan, Etherington, Adam, Crouch
Akiba: Sorensen, Palacios, Jones, Whitehead, Upson, Kightly, Jerome.
Fulham: Schwarzer, Riether, Hughes, Senderos, Riise, Baird, Sidwell, Karagounis, Dejagah, Berbatov, Petric
Akiba: Etheridge, Kelly, Kasami, Duff, Diarra, Rodallega, Banya.
Refa: Michael Oliver
SUNDERLAND 2 WEST BROM 4
West Bromwich Albion leo wameinyuka Sunderland Bao 4-2 na kutwaa nafasi ya 3 kwenye Msimamo wa Ligi na huu ni ushindi wao wa 4 mfululizo ikiwa ni mara ya kwanza kufanya hivi tangu Mwaka 1980.
Bao za WBA zilifungwa na Zoltan Gera, Shane Long, Romelu Lukaku na Mark-Antoine Fortune.
Bao mbili za Sunderland zilifungwa na Craig Gardner na Sessegnon.
VIKOSI:
Sunderland: Mignolet, Bardsley, O'Shea, Cuellar, Rose, Larsson, Cattermole, Colback, Johnson, Sessegnon, Fletcher
Akiba: Westwood, Gardner, Campbell, Kilgallon, Vaughan, McClean, Saha.
West Brom: Myhill, Jones, Olsson, McAuley, Ridgewell, Odemwingie, Yacob, Morrison, Brunt, Gera, Long
Akiba: Luke Daniels, Popov, Rosenberg, Dorrans, Lukaku, Tamas, Fortune.
Refa: Mike Dean
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO:
1 Man United Mechi 13 Pointi 30
2 Man City Mechi 12 Pointi 28
3 WBA Mechi 13 Pointi 26
4 Chelsea Mechi 12 Pointi 24
5 Everton Mechi 13 Pointi 21
6 Arsenal Mechi 12 Pointi 19
7 West Ham Mechi 12 Pointi 19
8 Tottenham Mechi 12 Pointi 17
9 Fulham Mechi 13 Pointi 16
10 Swansea Mechi 12 Pointi 16
11 Stoke City Mechi 13 Pointi 16
12 Liverpool Mechi 12 Pointi 15
13 Norwich Mechi 13 Pointi 15
14 Newcastle Mechi 12 Pointi 14
15 Wigan Mechi 13 Pointi 14
16 Sunderland Mechi 12 Pointi 12
17 Reading Mechi 12 Pointi 9
18 Aston Villa Mechi 12 Pointi 9
19 Southampton Mechi 12 Pointi 8
20 QPR Mechi 13 Pointi 4
+++++++++++++++++++++++
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumapili Novemba 25
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Swansea v Liverpool
[SAA 12 Jioni]
Southampton v Newcastle
[SAA 1 Usiku]
Chelsea v Man City
Tottenham v West Ham
Jumanne Novemba 27
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Sunderland v QPR
[SAA 5 Usiku]
Aston Villa v Reading
Jumatano Novemba 28
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Chelsea v Fulham
Everton v Arsenal
Southampton v Norwich
Stoke v Newcastle
Swansea v West Brom
Tottenham v Liverpool
Man United v West Ham
[SAA 5 Usiku]
Wigan v Man City