Tuesday, December 11, 2012

.CANNAVARO, CHOLLO, SELEMBE, AGGREY MORRIS NA MCHA VIALLI WAFUNGIWA KUCHEZA POPOTE DUNIANI


Kikosi cha Zanzibar kilichocheza Challenge Uganda
NAHODHA wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’  ni miongoni mwa wachezaji 16, waliofungiwa kwa muda usiojulikana kucheza soka popote duniani na Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), ambacho pia kimeivunja rasmi timu ya taifa, Zanzibar Heroes kwa tuhuma ya utovu wa nidhamu.
Akitangaza maamuzi ya kikao cha Kamati Utendaji ya ZFA kilichofanyika leo mchana ofisi za chama hicho zilizopo Kiembe Samaki, nje kidogo ya mji wa Zanzibar, Makamu wa Rais wa ZFA Unguja, Alhaj Haji Ameir, alisema Wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji waliohudhuria kikao wameunga mkono hatua hiyo, ili iwe fundisho kwa wachezaji wengine.
Kikao hicho cha dharura kimekuja kufuatia sakata la wachezaji wa Zanzibar Heroes kuamua kugawana kiasi cha dola za Kimarekani 10,000 walizopata baada ya kushika nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge iliyomalizika wiki iliyopita mjini Kampala, Uganda, kufuatia kuifunga Bara, Kilimanjaro Stars kwa penalti 6-5, baada ya sare ya 1-1.
Inadaiwa kuwa wachezaji hao waliamua kugawana fedha hizo kwa madai kuwa wamekuwa wakidhulumiwa fedha zao na ZFA.
Hata hivyo katika ufafanuzi uliotolewa leo na Katibu Mkuu wa ZFA Taifa, Kassim Haji Salum, amesema haijawahi kutokea wachezaji wa timu hiyo kudhulumiwa haki yao akikumbushia fedha za zawadi walizopata mwaka 1995 katika mashindano kama haya yaliyofanyika nchini Uganda na Zanzibar ikafanikiwa kutwaa ubingwa na mwaka 2009 waliposhika nafasi ya tatu na mara zote walipewa stahili zao.
Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa Zanzibar, Salum Bausi ambaye jana alitangaza rasmi kujiuzulu kuifundisha timu hiyo, amesema hatua hiyu ni sahihi kabisa kwa sababu kitendo hicho kimewafedhehesha wadau wa soka na Wazanzibari kwa ujumla.
Tayari ZFA Taifa walikwishatuma barua rasmi kwa TFF juu ya hatua hiyo huku nakala ya barua hizo zikitarajiwa kusambazwa kwa vilabu wanavyochezea wachezaji hao.
Wachezaji wanne walionusurika na adhabu hiyo ni wale walioamua kuzirejesha fedha hizo ambao majina yao hayakutatwa kwa sababu maalum, hata hivyo taarifa zilizopo ni kuwa wachezaji hao wanatoka katika klabu ya Kipanga timu inayomilikiwa na JWTZ, Jamhuri, Zimamoto na KMKM.
Kikosi cha Zanzibar kilichokwenda Challenge ni makipa; Mwadini Ali (Azam), Suleiman Hamad (Black Sella), Abdalla Juma (Kipanga), mabeki; Nassor Masoud 'Chollo' (Simba), Samir Haji Nuhu (Azam), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub Ali 'Canavaro' (Yanga), Aziz Said Ali (Kmkm), Mohammed Juma Azan (JKU) na Ali Mohammed Seif (Mtende Rangers).
Viungo ni; Hamad Mshamata (Chuoni), Ali Bakar (Mtende Rangers), Is-haka Mohammed (JKU), Twaha Mohammed(Mtibwa Sugar), Suleiman Kassim 'Selembe' (Coastal Union), Saad Ali Makame (Zanzibar All Stars), Makame Gozi (Zimamoto), Issa Othman Ali (Miembeni), Aleyuu Saleh (Black Sella), Khamis Mcha Khamis 'Viali' (Azam) na washambuliaji; Amir Hamad (JKT Oljoro), Jaku Juma Jaku (Mafunzo), Abdallah Othman (Jamhuri), Nassor Juma (JKU) na Faki Mwalim (Chipukizi).

 

 

KLABU BINGWA DUNIANI: NUSU FAINALI Jumatano & Alhamisi!

>>NGULI ABOUTRIKA kuiongoza Al Ahly dhidi ya Wabrazil Corinthians!!
>>ALHAMISI: Chelsea v Monterrey!!
FIFA_CLUB_WORLD_CUPMOHAMED ABOUTRIKA, wenyewe huko Misri, Siku zote humuita kwa upendo mkubwa, ‘Malaika’, ‘Nguli’ au ‘Mtu wa Amani’, baada ya kuifungia Al Ahly Bao la pili na la ushindi walipoichapa Sanfrecce Hiroshima ya Japan Bao 2-1 Jumapili, Siku ya Jumatano atawaongoza Mabingwa hao wa Afrika kucheza na Mabingwa wa Marekani ya Kusini, Corinthians ya Brazil, kwenye Nusu Fainali ya Mashindano ya FIFA kusaka Klabu Bingwa Duniani Uwanja wa Toyota, Japan.
+++++++++++++++++++++
RATIBA:
[SAA za BONGO]
Jumatano Desemba 12
MSHINDI wa 5:
[Saa 4 na Nusu Asubuhi]
Usain Hyundai v Sanfrecce Hiroshima
NUSU FAINALI
[Saa 7 na Nusu Mchana]
Al Ahly v Corinthians
Alhamisi, Desemba 13
[Saa 7 na Nusu Mchana]
Monterrey v Chelsea
+++++++++++++++++++++
Kabla ya Mechi hiyo ya Nusu Fainali hapo Jumatano, kutakuwepo Mechi ya kusaka Mshindi wa Tano kati ya Usain Hyundai ya Korea Kusini na Sanfrecce Hiroshima ya Japan.
Nusu Fainali nyingine itachezwa Alhamisi kati ya Chelsea, Mabingwa wa Ulaya, na Monterrey ya Mexici, ambao ni Mabingwa wa Marekani ya Kati na Kaskazini.
VIKOSI:
CORINTHIANS:
MAKIPA: JULIO CESAR, CASSIO, DANILO FERNANDES
MABEKI: ALESSANDRO, CHICAO, WALLACE, FABIO SANTOS, PAULO ANDRE, ANDERSON POLGA, GUILHERME ANDRADE, FELIPE
VIUNGO: RALF, PAULINHO, DOUGLAS, WILLIAN ARAO, DANILO, EDENILSON
MAFOWADI: Juan MARTINEZ, Paolo GUERRERO, EMERSON, JORGE HENRIQUE, GIOVANNI, ROMARINHO
KOCHA: TITE
AL AHLY:
MAKIPA: Sherif EKRAMY, Ahmed ADEL, Mahmoud ABOU ELSEOUD
MABEKI: Saadeldin SAAD, Ramy RABIA, Sherif ABDELFADEEL, Wael GOMAA, Mohamed NAGUIB
VIUNGO: Shehab AHMED, Mohamed BARAKAT, Ahmed KENAWI, Hossam GHALY, Sayed MOAWAD, AHMED FATHI, Hossam ASHOUR, TREZEGUET
MAFOWADI: EMAD METEAB, Walid SOLIMAN, GEDO, ELSAYED HAMDI, Abdalla SAID, Mohamed ABOUTRIKA, Dominique DA SYLVA
KOCHA: EL BADRY Hossam
++++++++++++++++++
MABINGWA WALIOPITA:
-2000 - Corinthians
-2005 - Sao Paulo
-2006 - Internacional
-2007 - AC Milan
-2008 - Manchester United
-2009 - Barcelona
-2010 - Inter Milan
-2011 – Barcelona
++++++++++++++++++
KLABU BINGWA DUNIANI 2012
TIMU ZITAKAZOSHIRIKI:
Chelsea-BINGWA ULAYA
Corinthians-BINGWA MAREKANI ya KUSINI
Monterrey-BINGWA MAREKANI ya KATI NA KASKAZINI
Auckland City-BINGWA KANDA ya OCEANIA
Usain Hyundai-BINGWA-Barani Asia
Al Ahly-BINGWA-Barani Afrika
Sanfrecce Hiroshima-BINGWA-Japan J-LIGI
RATIBA/MATOKEO:
Raundi ya Mchujo - Desemba 6, Yokohama
Sanfrecce Hiroshima 1 Auckland City 0
ROBO FAINALI - Desembar 9, Toyota
Usain Hyundai 1 Monterrey 3
Sanfrecce Hiroshima 1 Al Ahly 2
MSHINDI wa 5- Desemba 12, Toyota
[Saa 4 na Nusu Asubuhi]
Usain Hyundai v Sanfrecce Hiroshima
NUSU FAINALI
Desemba 12, Toyota
[Saa 7 na Nusu Mchana]
Al Ahly v Corinthians
Desemba 13, Yokohama
[Saa 7 na Nusu Mchana]
Monterrey v Chelsea
MSHINDI wa 3 - Desemba 16, Yokohama
[Saa 4 na Nusu Asubuhi]
FAINALI - Desemba 16, Yokohama
[Saa 7 na Nusu Mchana]

 

 

 WAGOMBEA WA MPIRA WA MIGUU  MKOA W ATABORA TAREFA WAENDELEA NA KAMPENI

 Wagombea uongozi wa mpira wa miguu mkoa wa tabora bado wameendelea na kampeni za kuomba kura kwa wapenzi na wadau wa mpira wa miguu mkoa wa tabora TAREFA kwa kipindi cha miaka minne ijayo.

Leo hii mgombea wa uongozi ngazi ya ukatibu bw.FATTY DEWJ REMTULA amenadi sera zake kwa wapenzi na wadau wa mpira wa miguu mkoa wa tabora TAREFA.FATTY REMTULA anachuana na mgombea anayetetea nafasi yake katika ukatibu mzee ALBERT SITTA

Wagombea wengine katika uchaguzi huo wa  TAREFA  nao wameendelea kutoa sera zao kwa wananchi ili waweze kuinua kiwango cha mpira wa mkoa w atabora nao ni mussa ntimizi,yusuph kitumbo,Laurent paul katika nafasi ya uenyekiti wa TAREFA.

Wengine ni Alaija mwiga mgombea pekee katika nafasi ya makamu mwenyekiti na mussa msananga naye ni mgombea pekee katika nafasi ya mweka hazina na nafasi ya mweka hazina msaidizi ipo wazi.

Katika nafasi ya mjumbe wa mkutano mkuu TFF ina wagombea wanne nao ni dick mlimuka,milambo kamili,ramadhani maghembe,na charles mwakambaya,na katika nafasi ya mwakilishi wa vilabu TFF ina wagombea watatu nao ni achery manjori,razack j. kumba,na lwamba yussa nao kila mmoja anatoa sera zake ili aje kubadili taswira ya mpira w amiguu mkoa w atabora.

Na katika nafasi ya ujumbe wa utendaji TFF inawagombea watatu nao ni stanslaus sizya,abdul moham,edy amani na james erick kapepele wote kila mmoja wanatoa sera zao kw awadau.

JANETH MICHAEL ni mgombea pekee katika nafasi ya mwakilishi w ampira wa miguu kw aupande wa wanawake naye ananadi sera zake kwa wadau mpaka tarehe 21-12-2012,na tarehe 22-12-2012 ndiyo siku ya kupata viongozi watakaochaguliwa katika uchaguzi utakaofanyika kwenye ukumbi wa idara ya maji mkoa wa tabota TUWASSA.

 

 

 

COASTAL YAANZA NA MOTO WAKE KOMBE LA UHAI


TIMU ya Coastal Union ya Tanga imeanza vizuri michuano ya kuwania Kombe la Uhai inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom baada ya kuifunga Tanzania Prisons mabao 2-1.
Mechi hiyo ya kundi A imechezwa leo asubuhi (Desemba 11 mwaka huu) Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam. Coastal Union ilimaliza kipindi cha kwanza ikiwa tayari imepachika mabao hayo yaliyofungwa dakika ya 24 na 33 kupitia kwa Ramadhan Same na Yusuf Chuma.
Tanzania Prisons ambayo itacheza mechi yake pili kesho jioni (Desemba 12 mwaka huu) Uwanja wa Azam ulioko Chamazi dhidi ya JKT Ruvu ilipata bao lake dakika moja kabla ya filimbi ya mwisho.
Mechi nyingine za kesho ni Toto Africans dhidi ya Coastal Union itakayochezwa saa 2 asubuhi Uwanja wa Azam. Katika kundi B, Simba na African Lyon zitaoneshana kazi asubuhi Uwanja wa Karume wakati Azam na Polisi Morogoro zitacheza saa 10 jioni kwenye uwanja huo huo.
Kundi C kesho ni Kagera Sugar vs Oljoro JKT saa 2 asubuhi Uwanja wa Karume, na Yanga na Ruvu Shooting zitaumana saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Azam.

 

 

UCHAGUZI TWFA KUFANYIKA MOROGORO DESEMBA 19


UCHAGUZI wa viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu kwa Wanawake Tanzania (TWFA) unatarajia kufanyika Desemba 19 mwaka huu mjini Morogoro.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TWFA, Ombeni Zavala, uchaguzi huo utatanguliwa na Mkutano Mkuu wa TWFA. Wajumbe wapiga kura wote wa mikoa iliyofanya uchaguzi wake na kutoa taarifa za uchaguzi wao ofisi za TWFA wanatakiwa kufika Morogoro siku moja kabla (Desemba 18 mwaka huu).
Wagombea waliopitishwa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ni kama ifuatavyo; wanaowania uenyekiti ni Isabela Kapera, Joan Minja na Lina Kessy. Rose Kissiwa ni mgombea pekee wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti.
Wanaowania ukatibu mkuu ni Amina Karuma na Cecilia Mkafu. Nafasi ya mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inagombewa na Zena Chande pekee baada ya Furaha Francis kujitoa kutokana na sababu za kifamilia.
Sophia Charles na Triphonia Temba wanawania nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya chama hicho.
Wagombea Rahim Maguza, Macky Mhango na Rose Msamila wameondolewa kwa kushindwa kikidhi matakwa ya Katiba ya TWFA Ibara ya 28(2)

 

 

DHAIRA YUPO KWENYE NDEGE ANAKUJA DAR KUMWAGA WINO SIMBA SC

Dhaira

MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba, kipa namba moja wa Uganda, Abbel Dhaira anatua leo saa 11:00 Dar es Salaam akitokea Uganda, kwa ajili ya kusaini mkataba wa kuanza kuitumikia klabu hiyo.
Akizungumza  leo, Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) aliyepigana vita dhidi ya Uganda, amesema kwamba ki;a kitu safi na Dhaira anakuja kumalizana na Simba.
Dhaira amekwishasema atafurahi kujiunga na Simba kwa kuwa ni klabu kubwa Afrika na inacheza Ligi ya Mabingwa Afrika na angependa kuungana na Mganda mwenzake, Emmanuel Okwi huko.
Tayari Simba SC imefikia makubaliano na kipa huyo namba moja wa Uganda, aliyemaliza mkataba wake na klabu ya I.B.V FC ya Iceland na amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili kwa dau ambalo halijafahamika.
Dhaira alisema kwamba amefikia makubaliano na Simba kusaini mkataba wa miaka miwili kuja kuanza maisha mapya Dear es Salaam.
Dhaira ambaye aliibukia Express ya hapa mwaka 2006 kabla ya 2008 kuhamia U.R.A. pia ya hapa, ambayo aliichezea hadi 2010 alipohamia Ulaya atatua Dar es Salaam Jumatatu kumaliza kila kitu Simba.
Ikimpata Dhaira, Simba SC itakuwa imepata kipa wa uhakika wa kusaidiana na kipa wake wa kwanza, Juma Kaseja ambaye amekuwa akisotoshwa peke yake bila kupumzika. Na hiyo inafuatia makipa wengine, Wilbert Mweta na Hamadi Waziri kushindwa kuonyesha uwezo wa kumsaidia Kaseja.
Katika mechi za mwishoni za mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Kaseja alionekana kuchoka na kudaka chini ya kiwango chake, jambo ambalo lilisababisha mashabiki wenye ‘akili mbovu’ wamfanyie fujo baada ya kufungwa mabao mawili katika mechi dhidi ya Mtibwa Sugar, Simba ikilala 2-0.
Kwa sababu hiyo, Kaseja alikasirika na kujiengua kwenye kikosi cha timu hiyo akisema hataki tena kuchezea Simba.
Lakini pamoja na matatizo hayo, Kaseja aliitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ambako ameendelea kufanya vizuri na kuonyesha yeye ni Tanzania One wa ukweli.  

 

 

KAMATI YA MGONGOLWA YAKETI KESHO KUMJADILI NGASSA

Wakili Mgongolwa

KAMATI ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), chini ya Mwenyekiti wake, Wakili Alex Mgongolwa, inatarajiwa kukutana kesho mjini Dar es Salaam kujadili uhalali wa kuuzwa kwa mchezaji Mrisho Ngassa.
Ofisa Habari wa TFF, Boniphace Wambura Mgoyo amesema mchana wa leo katika Mkutano na Waandishi wa Habari kwamba, Kamati hiyo inakutana kufuatia malalamiko yaliyowasilishwa na klabu ya Simba iliyokuwa inamtumia mchezaji huyo kwa mkopo kutoka Azam FC.
Hata hivyo, Kamati hiyo itakutana huku kukiwa kuna taarifa kwamba, Simba SC na Azam FC zimefikia makubaliano ya kumuuza kwa pamoja mshambuliaji huyo kwenda El Merreikh ya Sudan.
Habari za ndaniambazo nimezipata  kutoka kwenye kikao cha pamoja kati ya Simba na Azam jana, zimesema kwamba Merreikh imeongeza dau la kumnunua Ngassa kutoka dola za Kimarekani 70,000 hadi 100,000, zaidi ya Sh. Milioni 150 za Tanzania.
Baada ya kuongeza dau hilo, Azam ilikutana na Simba kujadili pamoja ofa hiyo mpya na kukubaliana kumuuza na kugawana nusu kwa nusu.
Upande wa Azam uliwakilishwa na mmoja wa Wakurugenzi wa bodi ya klabu hiyo, wakati kwa Simba waliwakilishwa na Makamu wao Mwenyekiti, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’.
Upande wa maslahi ya mchezaji umeboreshwa pia, Ngassa sasa atapewa dola za Kimarekani 75,000 zaidi ya Sh. Milioni 120,000 kwa kusaini mkataba wa miaka miwili na mshahara utabaki kuwa dola 4,000 (Sh. Milioni 6).
Habari zinasema kwamba, baada ya makubaliano hayo, leo Simba na Azam watasaini mkataba na Azam na kumuuza rasmi mchezaji huyo.
Hata hivyo, tangu wakati kikao hicho kinaendelea jioni ya jana, Ngassa alikuwa akitafutwa ili kuhusishwa, lakini hakupatikana kwenye simu.
Wasiwasi umeibuka kwamba huenda Ngassa anaweza akawa ameghairi mpango wa kwenda Merreikh kutokana na ushauri mbaya wa watu wake wa karibu. Mchezaji mmoja wa timu ya taifa, alisema jana kwamba Ngassa anafikiria kuachana na mpango wa kucheza Sudan, kwa sababu anasikia ni nchi ya Kiislamu na haina starehe.
Wapembuzi wa mambo wanasema kwamba, ilipofikia Ngassa anahitaji ushauri nasaha, kwani nafasi aliyopata ni adimu na ni muhimu kwa taifa na hata kwa maslahi yake binafsi.
Achilia mbali maslahi mazuri, lakini anakwenda kucheza timu ya ushindani ambayo itakuza kiwango chake aweze kuisaidia timu ya taifa pia. Merreikh ni timu ambayo karibu kila mwaka inashiriki Ligi ya Mabingwa.
Dili la Ngassa kwenda Merreikh awali liliingia katika mgogoro, baada ya Azam kumuuza bila kuishirikisha Simba.
Ikumbukwe, Azam walimtoa kwa mkopo Ngassa mwanzoni mwa Agosti, mwaka huu baada ya kukerwa na kitendo cha mchezaji huyo kubusu jezi ya timu yake ya zamani, Yanga, katika Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Alifanya hivyo, baada ya kufunga bao la ushindi akitokea benchi na kuiwezesha Azam kutinga fainali ya michuano hiyo, ambako walifungwa na Yanga 2-0, naye kwa mara nyingine akitokea benchi na kushindwa kufunga, hivyo kutuhumiwa kucheza kinazi.
Ilielezwa kwamba Simba walitoa Sh. Milioni 25 kumnunua kwa mkopo mchezaji huyo, ingawa baadaye Simba wakasema waliununua mkataba wa mwaka mmoja aliobakiza mchezaji huyo Azam FC, nao wakamuongezea wa mwaka mmoja kwa kumsainisha kwa Sh. Milioni 30, kati ya hizo Milioni 12 akipewa taslimu na 18 akipewa gari.

 

 

SIMBA KUANZA LIBOLO, AZAM NA AL NASIR AFRIKA

Kikosi cha Simba kitakachoivaa klabu ya Recreativo Libolo ya nchini Angola
CAIRO, MISRI
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa ratiba ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho. 
Simba ya Tanzania, ambayo ni klabu inayoaminika zaidi Afrika Mashariki kwa kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa inaanza Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kucheza na Recreativo do Libolo ya Angola. 
Azam FC, ambayo itacheza Kombe la Shirikisho kwa mara ya kwanza mwakani imepangwa na vibonde Al Nasir Juba ya Sudan Kusini. 
Simba itaanza nyumbani jijini Dar es Salaam Februari 17 na itarudiana na mabingwa hao wa Angola wiki mbili baadaye jijini Luanda, Angola. 
Simba ikivuka kigingi hicho cha mabingwa wa Angola, itakumbana ana kwa ana na El Merreikh ya Sudan ambayo inataka kumnunua Mrisho Ngassa wa Azam aliyekuwa akicheza Simba kwa mkopo. 
Kwa upande wa Azam ambayo nayo itaanzia nyumbani Dar es Salaam ikicheza siku moja kabla ya Simba yenyewe ikivuka hatua hiyo ya kwanza itacheza na mshindi kati ya Johansens ya Sierra Leone dhidi ya Barrack Y. C. II ya Liberia. 
Kwa upande wa Zanzibar, Jamhuri itacheza na St. Georges ya Ethiopia kwenye Ligi ya Mabingwa na ikivuka itakwaana na Djoliba ya Mali. 
Hata hivyo kwa upande wa Simba watakuwa wakikutana na timu ambayo ilianzishwa mwaka 1942 na inayotumia Uwanja wa Manispaa unaoitwa Calulo wenye uwezo wa kubeba mashabiki 10,000. 
Mabingwa hao wa Angalo ambao katika historia wametwaa ubingwa mara mbili tu mwaka 2011 na 2012 makao makuu yao yapo Libolo katika Jimbo la Cuanza Sul. 
Baadhi ya wachezaji wa timu hiyo inayofundishwa na Kocha Zeca Amaral ni Mendes, Ze Kalanga, Yuri, Nuno Silva na Andres Madrid. 
Kocha wa timu ya taifa ya Rwanda, Sredejovic Milutin 'Micho' alisema jana Jumatatu kuwa Simba imepangiwa timu ngumu. 
"Ni ratiba ngumu sana kwa Simba, wana nafasi ndogo ya kusonga mbele. Hii timu ndio mabingwa wa Angola, ni wazuri sana," alisema Micho. 
Simba ambayo makamu wake mwenyekiti Geofrey Nyange 'Kaburu' amesisitiza kwamba kesho Jumatano watamtangaza Kocha Mkuu, bado haijakamilisha usajili wake mdogo. 
Simba na Azam ndizo zinazoiwakilisha Tanzania Bara mwakani huku Yanga ikiwa haina nafasi yoyote ya kushiriki michuano mikubwa zaidi ya Kombe la Kagame Julai nchini Sudan.

UMONY AANGUKA AZAM, SIMBA WAISHIA KUNAWA

Brian Umony, kifaa kipya Azam 
MSHAMBULIAJI wa Uganda, Brian Umony ametua Azam FC ya Dar es Salaam kwa mkataba wa miaka miwili, akitokea KCC ya kwao, Uganda.
Awali, Umony alifanya mazungumzo na Simba SC ya Dar es Salaam pia na kufikia nao makubaliano, lakini Wekundu hao wa Msimbazi kwa kitendo cha kuchelewa kumalizamna naye, sasa ‘wanaishia kunawa’.
Umony alikuwa pia akiwaniwa na El Merreikh ya Sudan, ambayo nayo ilituma mwakilishi wake kwenda kuzungumze naye Uganda wiki iliyopita.
Brian amerejea nyumbani Uganda na kujiunga na KCC baada ya kumaliza mkataba wake, Becamex Binh Duong F.C. ya Vietnam.
Mwaka 2009, baada ya Simba kuzidiwa kete na SuperSport United ya Afrika Kusini, ikamsajili Emmanuel Okwi aliyekuwa SC Villa wakati huo.
Umony aliichezea Supersport United hadi 2010 alipohamia University of Pretoria ya Afrika Kusini pia hadi mwaka 2011 alipohamia Portland Timbers ya Marekani kwa mkopo na mwaka huu akatua Becamex Binh Duong F.C. Brian anang’ara katika Kombe la Challenge, hadi sasa ana mabao matatu.

SIMBA SC WAENDA UARABUNI KUSAKA MAKALI

Kikosi cha Simba kilichocheza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara
MABINGWA wa Tanzania Bara, Simba SC wanatarajiwa kwenda Oman kuweka kambi ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika.
Habariza ndani kutoka Simba,  , zinasema kwamba Simba itakwenda nchini humo kwa mwaliko wa klabu kongwe ya huko, Fanja FC.
Ikiwa huko, Simba itacheza pia mechi za kujipima nguvu dhidi ya timu tishio katika Ligi Kuu ya Oman, wakiwemo wenyeji wao hao, Fanja FC.
Simba inakuwa timu ya tatu ya Ligi Kuu kuwa katika mpango wa ziara ya nje ya nchi, baada ya wapinzani wao katika mbio za ubingwa msimu huu, Yanga na Azam nao kutangaza ziara zao.
Wakati Azam watakwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ndani ya siku mbili hizi, Yanga watakwenda Uturuki mwishoni mwa mwezi huu.
Mbali na Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa, mapema Januari Simba na Yanga zitacheza pia Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, michuano ambayo itafanyika mjini Kigali, Rwanda.
Yanga watakwenda kama mabingwa watetezi, baada ya kutwaa Kombe hilo Julai mwaka huu mjini Dar es Salaam, wakati Simba watakwenda kwa tiketi ya kuiwakilisha nchi kwenye michuano hiyo, wakiwa mabingwa wa Bara.
Kwa miaka miwili mfululizo, timu za Bara zinaonekana kurejesha utawala wake kwenye michuano hiyo, kutokana na fainali mbili mfululizo zilizopita kuzikutanisha timu za Tanzania tupu.
Mwaka 2011, Yanga iliifunga Simba SC 1-0, bao pekee la Mghana Kenneth Asamoah na kutwaa taji la nne, wakati mwaka huu Watoto hao wa Jangwani, walikutana na Azam FC katika mchezo wa Kombe uwanjani na kushinda 2-0, mabao ya Hamisi Kiiza na Said Bahanuzi.
Azam, Simba na Yanga kwa sasa ndio washindani wa taji la Ligi Kuu nchini, ambao wanaonekana kutaka kujiimarisha vizuri kabla ya kuanza kwa hatua ya lala salama ya ligi hiyo.

BPL: Fulham 2 Newcastle 1

>>LEO KIPORO: Sunderland v Reading
BPL_LOGOJANA Usiku, wakiwa kwao Craven Cottage, Fulham walimaliza ukame wao wa kutoshinda katika Mechi 7 kwa kuifunga Newcastle Bao 2-1 matokeo ambayo yamewafanya Newcastle waendelee Msimu huu wa Ligi bila ushindi hata mmoja wa ugenini.
++++++++++++++++
MAGOLI:
Fulham 2
Sidwell 19′ Rodallega 63′
Newcastle 1
Ben Arfa 54′
++++++++++++++++
Steve Sidwell aliwafungia Bao Fulham, likiwa Bao lao la kwanza kwa Fulham katika Masaa matano ya Soka, baada ya shuti lake kumbabatiza Beki na kutinga.
Newcastle walisawazisha kwa Bao la Hatem Ben Arfa, ambae hiyo ilikuwa Mechi yake ya kwanza baada ya kukosa Mechi 4 kwa kuwa na maumivu.
Hata hivyo, kichwa cha Hugo Rodallega kilichotinga kimiani kilifawanya Wenyeji Fulham watoke na ushindi wa Bao 2-1.
Leo Usiku kutakuwa na Mechi ya kiporo kati ya Sunderland na Reading, Mechi ambayo ilikuwa ichezwe Agosti 25 lakini ikaahirishwa baada ya Stadium of Light kufurika maji kufuatia mvua kubwa, na ikichezwa leo itazifanya Timu zote za Ligi Kuu England ziwe zimecheza Mechi 6 kila mmoja.
VIKOSI:
Fulham: Schwarzer, Riise, Hangeland, Baird, Hughes, Riether, Sidwell, Duff, Kacaniklic (Dejagah - 62' ), Berbatov, Rodallega (Petric - 86' )
Akiba: Etheridge, Senderos, Richardson, Karagounis, Diarra, Petric, Dejagah
Newcastle United: Krul, Coloccini, Santon, Simpson, Williamson, Anita (Marveaux - 86' ), Ben Arfa (Sh Ameobi - 70' ), Gutierrez, Tiote (Bigirimana - 86' ), Cisse, Ba
Akiba: Harper, Perch, Ferguson, Tavernier, Bigirimana, Marveaux, Sh Ameobi
Refa: Mason
Watazamaji Uwanjani: 25,270
+++++++++++++++++++++++++++++++++
MSIMAMO:
[Kila Timu Mechi 16 isipokuwa inapotajwa]
1 Man United Pointi 39
2 Man City 33
3 Chelsea 29
4 Everton 26
===============
5 Tottenham 26
6 WBA 26
7 Arsenal 24
8 Swansea 23
9 Stoke 23
10 Liverpool 22
11 West Ham 22
12 Norwich 22
13 Fulham 20
14 Newcastle 17
15 Southampton 15
16 Aston Villa 15
===============
17 Wigan 15
18 Sunderland Mechi 15 Pointi 13
19 Readind Mechi 15 Pointi 9
20 QPR 7
+++++++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumanne 11 Desemba 2012
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Sunderland v Reading
Jumamosi 15 Desemba 2012
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Newcastle v Man City
[SAA 12 Jioni]
Liverpool V Aston Villa
Man United V Sunderland
Norwich v Wigan
QPR v Fulham
Stoke v Everton
Jumapili 16 Desemba 2012
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Tottenham v  Swansea
[SAA 1 Usiku]
West Brom v West Ham
Jumatatu 17 Desemba 2012
[SAA 5 Usiku]
Reading v Arsenal

Clarke, Fellaini ni Bora Novemba, Barry wa Man City ashitakiwa na FA!!

FELLAINIBosi wa WBA, Steve Clarke, na Staa wa Everton, Marouane Fellaini, wamezikwaa Tuzo za Ubora kwa Mwezi Novemba kwenye Ligi Kuu England huku Kiungo wa Manchester City Gareth Barry akishitakiwa kwa utovu wa nidhamu kufuatia tukio baada ya Dabi ya Manchester Jumapili ambapo Klabu yake ilibamizwa 3-2 na Manchester United Uwanjani Etihad.
Meneja wa West Bromwich Albion, Steve Clarke, ametajwa kuwa ndie Meneja Bora wa Ligi Kuu England kwa Mwezi Novemba kwa kushinda Mechi 4 na kufungwa moja ingawa sasa wapo kwenye wimbi la kufungwa Mechi 4 mfululizo.
Nae, Fellaini, Mchezaji wa Kimataifa wa Belgium, amezawadiwa Tuzo ya Mchezaji Bora baada ya kufunga Bao 4 kwenye Mwezi ambao Everton wamefungwa Mechi moja tu.
Hadi sasa Fellaini ameshafunga Bao 8 kwa Msimu huu.
Wakati huo huo, Chama cha Soka England, FA, kimetangaza kuwa kimemfungulia Mashitaka Kiungo wa Manchester City Gareth Barry kwa utovu wa nidhamu baada ya kuripotiwa kutumia maneno ya matusi dhidi ya Marefa wa Mechi kati ya Manchester City na Manchester United iliyochezwa Uwanja wa Etihad Jumapili iliyopita.
Barry amepewa hadi Saa 1 Usiku Siku ya Alhamisi awe amejibu Mashitaka yake.
Kwenye Dabi hiyo ya Manchester, frikiki ya Dakika za Majeruhi ya Robin van Persie iliwapa Bao la ushindi Manchester United wa Bao 3-2 na kuzua tafrani toka kwa Mashabiki wa Man City ambapo mmoja wao alirusha Sarafu iliyompasua Beki wa Man United, Rio Ferdinand, juu ya jicho wakati akishangilia Bao la ushindi huku mwingine wakati huo huo akivamia Uwanja kutaka kumvaa Ferdinand wakati akiuugulia kuumizwa lakini Kipa wa Man City Joe Hart akamdhibiti.
Hadi sasa Polisi wanamsaka yule alierusha Sarafu lakini yule alievamia Uwanja pamoja na wengine wanane walikamatwa na Polisi na kufunguliwa Mashitaka ambayo watasomewa Mahakamani mwanzoni mwa Januari.

BREAKING NEWS: HATIMAYE SIMBA NA AZAM WAFIKIA MAKUBALIANO YA KUGAWANA FEDHA ZA USAJILI ZA NGASSA

Baada msuguano wa takribani wiki mbili kuhusu nani hasa anastahili hasa kuchukua fedha za usajili wa mchezaji Mrisho Ngassa kati ya vilabu vya Simba na Azam, hatimaye leo hii umepatikana muafaka.

Viongozi wa pande mbili za vilabu hivyo wamekutana na kukubaliana kwamba watamuuza mchezaji Mrisho Ngassa kwenda klabu ya El Merreikh kwa ada ya usajili ya $100,000 na fedha hizo zitagawanywa kwa Simba na Azam FC.

Kwa upande wa mchezaji mwenye Mrisho Ngassa atapokea kiasi cha $75,000 kama gharama ya usajili kwa mkataba wa miaka miwili, na pia atalipwa kiasi cha $4000 kama mshahara kwa kila mwezi.

Simba na Azam zilikuwa zikigombana kuhusu nani hasa alikuwa mmiliki halali wa mchezaji huyu.

ARSENAL YAMMENDEA NANI KATIKA DIRISHA DOGO.

KLABU ya Arsenal inaangalia uwezekano wa kumnyakuwa winga wa kimataifa wa Ureno na klabu ya Manchester United, Nani katika kipindi cha usajili wa dirisha januari mwakani. Nani mwenye umri wa miaka 26 yupo mguu nje mguu ndani Old Traford baada ya meneja wa United kushindwa kumuongeza mkataba na Wenger anataka kutumia nafasi hiyo ili kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya kuwania taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya pamoja na Ligi Kuu nchini Uingereza. Winga huyo ambaye alikosa mchezo wa Jumapili dhidi ya mahasimu wao Manchester City amekuwa akigombea namba na kiungo wa united anayechipukia Davide Petrucci mapema msimu huu. Wenger pia anapanga kumsajili kiungo wa kimataifa wa Senegal na klabu ya West ham United Mohamed Diame ambaye mkataba wake unatarajiwa kugharimu kiasi cha paundi milioni 3.5.

FEDERER AKUTANA NA PELE.

MCHEZAJI tenisi nyota duniani Roger Federer amekutana na nguli wa soka wa zamani duniani Pele nchini Brazil mwishoni mwa wiki. Federer alikwenda kumtembelea Pele nyumbani kwake nchini humo na kwenda kubadilishana zawadi na mmoja wa wachezaji bora kabisa kuwahi kutokea katika historia ya mchezo wa soka. Pele alipewa fulana ya tenisi yenye ujumbe maalumu kutoka kwa Federer wakati naye alimpa nyota huyo wa tenisi fulana yake aliyokuwa akiitumia miaka 1960 ambayo imesainiwa nay eye mwenyewe. Federer alikuwa nchini Brazil kwa ajili ya michuano ya maonyesho ambayo imeandaliwa na kampuni ya Gillette akiwa pamoja na nyota wengine kama Maria Sharapova, Caroline Wozniacki, Serena Williams na Jo-Wilfried Tsonga.

PACQUIAO APUUZA USHAURI WA KUACHANA NA NGUMI ALIOPEWA NA MKEWE PAMOJA NA MAMA MZAZI.

BINGWA wa zamani wa ngumi duniani Manny Pacquiao amepuuza ushauri wa mama pamoja na mke wake wa kuachana na ngumi kufuatia kipigo alichopata kutoka kwa mpinzani wake Juan Manuel Marquez wa Mexico. Pacquiao raia wa Philipines alipigwa kwa knock out katika raundi ya sita na Marquez katika pambano lisilokuwa la ubingwa lililofanyika Las Vegas, Marekani Jumamosi iliyopita. Bondia huyo mwenye umri wa miaka 33 aliwasikiliza mke wake Jinkee na mama Dionisia wakilia kwa uchungu kutaka aachane na mchezo wa ngumi lakini Pacquiao amesema kuwa kwasasa atapumzika na baadae atarejea tena ulingoni. Akihojiwa na luninga moja nchini kwao Jinkee amesema huwa anapata wakati mgumu wakati anapomuona mumewe anapokea kipigo kama cha Jumamosi na siku zote amekuwa akimsisitiza kuachana na mchezo huo ili aweze kufanya mambo mengine ambayo anapenda. Lakini Pacquiao ambaye ameanza kucheza ngumi akiwa na umri wa miaka 16 amesisitiza kuwa kipigo hicho hakimaanishi kuwa uwezo wake wa kupigana umekwisha.

SIJAWAHI KUKUTANA NA MTU KAMA MOURINHO - ETO'O.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Cameroon, Samuel Eto’o amesema kuwa hajawahi kukutana na mtu wa aina ya Jose Mourinho katika maisha yake. Wawili hao walifanya kazi pamoja wakati mourinho akiinoa Inter Milan na Eto’o kuweka wazi kuwa walipata wakati mgumu wakati kocha huyo alipoondoka katika klabu hiyo na kwenda kuinoa Real Madrid mwaka 2010. Eto’o anemuelezea Mourinho kama mtu muungwana na kocha mzuri na kuwa mmoja wa watu wachache wa aina yake ambao amewahi kukutana nao ambapo katika mwaka huo walishinda mataji matatu makubwa muhimu. Nyota huyo pia alizungumzia muda aliokuwa chini ya kocha wa zamani wa Barcelona Pep Guardiola na kukiri kuwa alipata wakati mgumu wakati akiondoka katika klabu hiyo lakini alidai kuwa mpaka sasa wana mahusiano mazuri na kocha huyo.