Sunday, January 20, 2013

BPL: WEST BROM 2 ASTON VILLA 2


 
BPL_LOGOPeter Odemwingie, Mchezaji ambae alitemwa na Nigeria kuwemo kwenye Kikosi cha Nchi hiyo kwenye AFCON 2013, leo ameiokoa Klabu yake West Bromwich Albion baada ya kufunga Bao la kusawazisha katika Dakika ya 83 walipotoka nyuma kwa Bao 2-0 na kutoka sare 2-2 na Aston Villa katika Mechi ya BPL, Barclays Premier League.

MAGOLI:
West Brom 2
-Brunt Dakika ya 49
-Odemwingie 83
Aston Villa 2
-Benteke Dakika ya 12
-Agbonlahor 31

Aston Villa, wakicheza ugenini katika Dabi ya Miji ya Kati ya England, walitangulia 2-0 kwa Bao za Christian Benteke na Gabriel Agbonlahor.
Lakini Kipindi cha Pili Chris Brunt alifunga Bao la Kwanza na Odemwingie kusawazisha.
VIKOSI:
West Brom: Foster, Jones, McAuley, Olsson, Ridgewell, Morrison, Dorrans, Yacob, Brunt, Lukaku, Odemwingie
Akiba: Myhill, Popov, Rosenberg, Thomas, Thorne, Dawson, Tamas.
Aston Villa: Guzan, Vlaar, Clark, Baker, Lowton, Westwood, Delph, N'Zogbia, Bennett, Agbonlahor, Benteke
Akiba: Marshall, Ireland, Bent, Holman, Bowery, Bannan, Lichaj.
Refa: Lee Probert

BPL, BARCLAYS PREMIER LEAGUE
RATIBA:
Jumapili Januari 20
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Chelsea v Arsenal
[SAA 1 Usiku]
Tottenham v Man United
Jumatatu Januari 21
[SAA 5 Usiku]
Southampton v Everton

No comments:

Post a Comment