Wednesday, November 28, 2012

Tenga, Wizara wateta kuzuiwa Akaunti ya TFF na TRA!!

>>TRA yataka Akaunti zikatwe Sh. 157,407,968 kama Kodi!
TFF_LOGO12
Wakati TRA imetoa amri ya kufungwa Akaunti ya TFF iliyopo Benki ya NMB na kuiielekeza Benki ya NMB kukata sh. 157,407,968 ikiwa ni malipo ya Kodi ya Mapato ya Mshahara wa Mfanyakazi (P.A.Y.E) ya Makocha Marcio Maximo na Wasaidizi wake, TFF imekimbilia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ili kuumaliza kwa mgogoro huo amao TFF umedai hauhusiki kwa vile Mishahara ya Makocha hao ilikuwa ikilipwa na Serikali.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lina imani kuwa mazungumzo kati yake, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yatamaliza tatizo la kushikiliwa akaunti ya TFF kutokana na malipo ya kodi ya mishahara ya makocha wa kigeni.
Rais wa TFF, Leodegar Tenga alizungumza na waandishi wa habari jana juu ya uamuzi wa TRA kushikilia akaunti ya TFF ikiielekeza Benki ya NMB kukata sh. 157,407,968 ikiwa ni malipo ya Kodi ya Mapato ya Mshahara wa Mfanyakazi (P.A.Y.E) ya makocha Marcio Maximo na wasaidizi wake.
Katika mzozo huo wa muda mrefu, TFF imejitetea kuwa haiwezi kulipa kodi hiyo kwa kuwa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ndiyo mlipaji wa mishahara ya makocha hao, ikiwa ni ahadi ya Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete ya kulipia makocha wa michezo tofauti, ukiwemo mpira wa miguu.
“Hili ni suala nyeti ambalo linahitaji kumalizwa kwa mazungumzo baina ya pande zote. Ninataka kuwahakikishia kuwa suala hili linazungumzwa na tayari nimeshafanya mazungumzo na maofisa wa Wizara na tumekubaliana kukutana na pande zote  wakati wowote; iwe leo jioni au kesho.
“Ni matumaini yangu kuwa suala hili litakwisha na jana nimetoka Kampala (Uganda kwenye Kombe la Chalenji) moja kwa moja na kwenda kuzungumza na viongozi wa Wizara na wamekubali kwamba tuongee pande zote kulimaliza suala hili.
“Nimezungumza na wenzetu wa Serikali kwa sababu najua unyeti wa suala hili. Fedha zilizokamatwa si zetu; ni fedha za klabu na zimetolewa na mdhamini ambaye tumekubaliana namna ya kuzitumia. Fedha hizi hazikutolewa kwa ajili ya kulipia kodi. Lakini TRA wanazishikilia kwa sababu Premier League iko chini ya TFF,” amesema Rais Tenga.
Tenga amesema TRA wanafanya kazi kwa kufuata sheria zao za ukataji kodi na hivyo wana haki ya kufuatilia kwa kuwa kwa mujibu wa sheria, mwajiri ndiye anayetakiwa kukata kodi kutoka kwenye mshahara wa mfanyakazi.
“Hivyo hatuwezi kuilaumu TRA kwa sababu ndivyo sheria inavyosema, lakini pia hatuna uwezo huo wa kulipa fedha hizo kwa sababu, kwanza hatuna na pili sio sisi tunaolipa mishahara ya hawa makocha,” amesisitiza Rais Tenga.
Akizungumzia historia ya suala hilo, Tenga aliishukuru Serikali kwa msaada ambao imekuwa ikiutoa katika mpira na kwamba ahadi ya Rais Kikwete ya kusaidia kulipa makocha wa timu za taifa imeusogeza mpira wa miguu karibu na Serikali na karibu na Rais.
“Rais Kikwete alisema wakati alipoingia madarakani (mwaka 2005) anajua kuwa kuna tatizo kwenye mpira na akatoa ahadi ya kulipa walimu wa mpira. Ahadi hiyo imefanya ukaribu uliopo sasa kati ya mpira na Serikali; kati ya mpira na Rais sasa kuwa mkubwa. Serikali imechangia kwa kiasi kikubwa kwenye mpira, yaani kulipa walimu.
“Sasa sisi ni administrators wa hawa walimu. Tunachofanya ni kuandaa mikataba ambayo ni standard duniani kote kwa mujibu wa taratibu za FIFA (Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu). Kwa kawaida makocha wa kigeni huwa wanatayarishiwa mikataba ambayo ni tax free (isiyo na kodi). Baada ya kuingia nao mikataba, huwa tunaipeleka wizarani ambao ndio wanawalipa makocha moja kwa moja kwenye akaunti zao,” amesema Rais Tenga.
Katika mkutano huo na waandishi, Rais Tenga pia aliipongeza timu ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars kwa kuanza vizuri mashindano ya Kombe la Chalenji, akisema ushindi huo ni ishara nzuri hasa kutokana na ukweli kuwa kikosi hicho kinaundwa na wachezaji wengi chipukizi na akataka Watanzania waendelee kuiunga mkono.
Tenga pia alisema kumekuwepo na malalamiko kuhusu makato ya mechi na kwamba suala hilo ni la muda mrefu na kwamba TFF imepiga hatua kubwa tangu ilipoanza kulishughulikia.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

 

SERENGETI BOYS KUKWEA PIPA LEO ,KUAGWA JIONI HII


Timu  ya soka ya Taifa ya vijana waliochini ya miaka 17 'Serengeti boys' inatarajia kuondoka usiku wa leo kwenda nchini  Congo Braza ville kwa ajili ya mchezo wa marudiano.

 Timu hii inaondoka na msafara wa watu 27 ikiwa ni wachezaji 18 na viongozi tisa huku wakiwa na matumaini makubwa ya kusonga mbele baada ya mchezo wa awali uliochezwa nchini kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

 Serengeti boys ambayo imeundwa na wachezaji chipukizi waliopatikana kutokana na mashindano ya Copa Cocacola inabidi washinde  mchezo huo au sare ya mabao yoyote au isyokuwa na mabao  ili waweze kuandika historia ambayo haijawahi kuandikwa hapa nchini.

 Itakumbukwa kuwa Tanzania iliwahi kufuzu  fainali za mwaka 2005 lakini ikaondolewa na ikafungiwa baada ya kugudulika umri wa mchezaji Nurdin Bakari kuwa haukuwa sahihi  kimashindano .

  Kocha Mkuu wa timu hii Jakob Michelsen amesema timu yake ipo tayari kupambana na Congo Brazaville na anajivunia faida ya bao moja walilolipata nyumbani.

"Wachezaji wapo kamili na wana ari ya kushinda mchezo huo na kwa sababu nyumbani tulishinda tunaamini tutashinda pia", alisema Jacob

 Tunawatakia kila la heri mfanikiwe kufuzu fainali za vijana zinazotarajiwa kuchezwa nchini Morocco, Machi mwakani.

Primetime YAKIRI MAKOSA KULIPA FIDIA !

Kituo cha Runinga cha kulipia cha  Primetime kimeomba radhi  kwa mamia ya wateja ambao walishindwa kutazama pambano la bondia  Ricky Hatton's aliporejea ulingoni mara baada ya kupata matatizo ya kiufundi  .' 

Watu walio jaribu kuweka oda zao katika majira ya saa  moja usiku hadi  saa tatu na dakika hamsini 7.10pm and 9.50pm siku ya jumamosi   hawakuweza kutazama  kutokana matatizo ya kiufundi na kukatika kwa matangazo  .

Wateja wengine walilalamika kuwa walikuwa wakiona mwanga wa bluu na mweusi katika kioo baada ya kulipa pauni  £14.95 sawa na shiligi 35000 elfu za kitanzania na wameimbia bbc radio 4 kuwa  Matangazo yao yalipatwa na matatatizo na wanaweza kuwasiliana na mtu yeyote katika kampuni 

Primetime imesema kuwa itashughurikia kila mteja na italipa wateja wote madai yao hasa wale ambao walishindwa kutazama pambano hilo  

Hiii sio mara kwanza kwa  Primetime Au kituo chochote cha runinga cha kulipia kupata matatizo kama hayo .
Mwaka  2009 kituo hicho kilikumbwa na matatizo makubwa ya kiutangazji  katika pambano la  Carl Froch vs Andre Dirrell.
Sky Box  Frank Warren's Box  walikumbwa na matatizo kama hayo .

Primetime Imesema kuwa matatizo ya kuifundi ina maana  tulishundwa kuendelea kufanya kazi hasa pale simu nyingi zilipo kuwa zikimimi nika tulishindwa kuzimudu na haikuwa na maana kuwa tuliziipuuza .

LUIZ ADRAIANO AFUNGIWA MECHI MOJA KWA KTOONYESHA UUNGWANA KIWANJA

Mshambuliaji wa   Timu ya soka ya  Shakhtar Donetsk  Luiz Adriano amefungiwa mechi moja katika michuano ya ligi ya mabingwa ulaya iliyochezwa jumaane iliyopita mara baada ya kushindwa kuonyesha uanamichezo,  baada ya kufunga goli ambalo halikuwa la kiushindani Dhidi ya  Nordsjaelland.

Kamati ya Nidhamu ya UEFA imemkuta na hatia  MBrazil huyo baada ya kujikuta akizua mijadala na kuvunja taratibu za soka katika mchezo uliochezwa huko  Denmark wiki iliyopita

"Mchezaji huyo wa  Shakhtar amepewa maagizo na 
UEFA  ya kufanya shughuri za kijamiii za mpira wa miguu  .

Luiz Adriano alivunja sheria ya uanamichezo mara baada mpira kusimamishwa kupisha mchezaji wa timu pinzani kupata matibabu  .
Baada ya Mpira kuanzishwa kwa  kundundishwa  Adriano alikimbiza mpira na kumpiga chenga beki  wa Nordsjaelland na baadae kumpiga chenga kipa na kufunga goli ambapo sasa atatumikia adhabu dhidi ya Juventus  December 5, japokuwa mabingwa hao wa  Ukrain wameshafuzu hatua inayofuata baada ya kuifunga  Nordsjaelland 5-2.



UMOJA WA CHAMA CHA WAAMUZI WAKUBALI RADHI YA CHELSEA 



Chama cha Waamuzi uingereza  wameridhia  kauli ya klabu ya chelsea kujutia malalamiko yake ya dhidi ya ubaguzi wa rangi yaliyotolewa dhidi mwamuzi  Mark Clattenburg 'kuwa wamekubali makosa '.

Katika Taarifa ya majumuisho iliyotolewa na Bodi ya waamuzi wanaochezesha michezo ya  kulipwa kisheria   (PGMOL)  ambao huchezesha ligi ya uingereza na  ,Ligi ya mbaingwa ulaya  wamejutia kutokuwa na ushahidi wa kutosha katika malalamiko yao waliyoyatoa  28 October wakimtuhumu mwamuzi kwa ubaguzi wa wa Rangi .

Wiki iliyopita ,Chama cha soka cha uingereza kilitoa taarifa kuwa hakuna kesi ya kujibu Dhidi ya   Clattenburg,

ambaye ana miaka  37, kuwa alimtukana mchezaji wa kimataifa wa nigeria na kiungo wa cheslea  John Obi Mikel ambapo  Chelsea ilifungwa mabao matatu  3-2 dhidi ya Manchester United.

UEFA yatafakari: KUPANUA CHAMPIONZ LIGI iwe na Timu 64, EUROPA LIGI kufutwa!

UEFA_CHAMPIONZ_LIGI_LOGO-BOMBAZUEFA wapo kwenye majadiliano ya kuifutilia mbali EUROPA LIGI ili kuongeza Timu kwenye CHAMPIONZ LIGI zifikie 64 kwenye hatua ya Makundi uamuzi ambao unaweza kuzifanya baadhi ya Nchi, hasa zile zinazotoa Wawakilishi wanne kama vile England, kuwa na Timu 7.
Akiongelea hatua hiyo, Rais wa UEFA, Michel Platini, alisema: “Tunajadili. Tutatoa uamuzi Mwaka 2014. Lakini kwa sasa hamna kilichoamuliwa.”
Mjadala huo ni msimamo wa UEFA wa kutaka kutafuta mfumo mpya wa Mashindano yake Barani Ulaya utakaotumika kati ya Mwaka 2015 na 2018.
Uamuzi huu wa kuifuta EUROPA LIGI hasa unatawaliwa na malamiko ya pande nyingi kuwa tangu michuano hiyo ibadilishwe kutoka UEFA Cup imekosa mvuto na imekuwa ikiishi chini ya kivuli cha CHAMPIONZ LIGI.
Hilo hasa linaonekana kwenye Mapato ya Mashindano hayo ambapo UEFA hupata Pauni Bilioni 1 kutoka CHAMPIONZ LIGI na Pauni Milioni 225 kutoka EUROPA LIGI wakati Mshindi wa CHAMPIONZ LIGI, Chelsea, alivuna Pauni Milioni 49 wakati yule wa EUROPA LIGI, Atletico Madrid, alipata Pauni Milioni 8.5 tu.
Wiki iliyopita, Meneja wa Newcastle, Alan Pardew, alisema EUROPA LIGI ni kero na ngumu kufuzu kwa vile ina Mechi nyingi na hasa Ratiba yake ya kuchezwa Alhamisi Usiku ambapo Timu nyingi hulazimika kuchezesha Vikosi hafifu kwa vile Wikiendi hukabiliwa na Mechi za Ligi Nchini kwao.

 

STARS KAMBINI DAR BAADA YA CHALLENGE

Kim Poulsen akijadiliana jambo na msaidizi wake, Sylvester Marsh 

TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inatarajia kuingia kambini baada ya kumalizika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge inayoendelea Uwanja wa Mandela ulioko Namboole jijini Kampala, Uganda hadi Desemba 8 mwaka huu.
Kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Kim Poulsen, ambaye anakiongoza kikosi cha Bara, Kilimanjaro Stars kwenye mashindano haya, Stars itaingia kambini kujiandaa kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya mabingwa wa Afrika, Zambia, Chipolopolo itakayochezwa Desemba 23, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Baada ya pambano dhidi ya Chipolopolo, wachezaji watapata mapumziko ya wiki mbili kabla ya kuingia tena kambini Januari 6 hadi 20 mwakani kwa ajili ya mechi nyingine za kirafiki ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco.
Kim anatarajia kuongeza kipa mmoja kwenye kikosi chake ili kuwasaidia Nahodha Juma Kaseja na Deogratias Munishi pamoja na chipukizi kadhaa kutoka timu za taifa za vijana za Ngorongoro Heroes na Serengeti Boys.
Vilevile Kim anafuatilia wachezaji wengine kwenye timu ya Zanzibar, Zanzibar Heroes waliopo kwenye Tusker Challenge pia katika kundi C pamoja na timu za Eritrea, Malawi na Rwanda

KOCHA ATAJA SABABU MOJA TU YA KUMTEMA BABBI KIKOSINI ZANZIBAR HEROES

Abdi Kassim 'Babbi'

KOCHA wa timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes, Salum Bausi Nassor amesema kwamba amemtema katika timu hiyo, kiungo mkongwe Abdi Kassim Sadallah ‘Babbi’ kwa sababu ameongezeka uzito na amekuwa mzito sana.
Akizungumza  jana katika Uwanja wa Mandela, Namboole, Bausi alisema kwamba Babbi anatakiwa kupambana na uzito ili arejeshwe Zanzibar Heroes.
“Kama unavyoona, haya mashindano yamekuwa ya kasi sana sasa, na Babbi amekuwa mzito sana na hata huko Azam, anaingizwa dakika 20 za mwisho, lazima uwe na wachezaji wenye kasi, wewe mwenyewe umeona mechi na Eritrea ilivyokuwa ngumu,”alisema.
Awali ya hapo, jana kipa namba moja wa Uganda Abbel Dhaira alisema kwamba anavutiwa sana na uchezaji wa Babbi pamoja na wachezaji wengine, Mrisho Ngassa wa Tanzania Bara na Haruna Niyonzima wa Rwanda.
“Hao ni wachezaji ambao napenda sana kuwatazama, nasikia Babbi hajaja, sijui kwa nini, kocha wao anajua, ila yule mchezaji mzuri sana, anapiga sana mashuti, ana nguvu, ananivutia, namjua vema,”alisema Dhaira.
Zanzibar juzi ilianza kwa sare michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge inayoendelea mjini hapa, baada ya kutoka 0-0 na Eritrea katika mchezo wa Kundi C.
Matokeo hayo yanawaweka katika wakati mgumu kuweza kuendelea na mashindano haya na sasa wanatakiwa kupambana zaidi katika mechi zao mbili zijazo ili washinde na kutinga Robo Fainali.
Nahodha wa Heroes, Nadir Haroub Ally ‘Cannavaro’ pamoja na kuwaomba radhi Wazanzibari kwa sare hiyo, lakini pia ameahidi watajituma na kufanya vizuri katika mechi zijazo.  

KIPA LA MAANA KULIFUNGA KWA MBINDE TAYARI KUTUA SIMBA SC

Abbel Dhaira

KIPA namba moja wa Uganda, Abbel Dhaira anayedakia klabu ya I.B.V FC ya Iceland, amesema kwamba yuko tayari kuhama Ulaya na kuja Tanzania kuchezea klabu ya Simba, iwapo watafika dau lake.
Akizungumza  jana Uwanja wa Mandela, Namboole, Kampala, Dhaira alisema kwamba mwaka jana Simba walimfuata, lakini wakashindwa kumalizana naye na akaendelea kucheza Ulaya.
Hata hivyo, Dhaira ambaye ni miongoni mwa makipa bora katika ukanda huu kwa sasa, alisema anawapa nafasi nyingine Wekundu hao wa Msimbazi.
“Nina siku tatu tu kabla ya kumaliza mkataba wangu na klabu yangu. Kabla ya kuingia nao mkataba mpya, nawapa nafasi nyingine Simba SC,”alisema, Dhaira ambaye aliibukia Express ya hapa mwaka 2006 kabla ya 2008 kuhamia U.R.A. pia ya hapa, ambayo aliichezea hadi 2010 alipohamia Ulaya.
Hata hivyo, Dhaira hataonekana tena kwenye michuano ya mwaka huu ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge baada ya kuumia jicho katika mechi ya kwanza dhidi ya Kenya, Jumamosi.
Akilizungumzia hilo, Dhaira alisema imemsononesha sana kwani alijitoa kwa ajili ya kuja kuisaidia nchi yake kwenye mashindano haya, lakini kwa bahati mbaya ameumia.
“Ni mambo ya kawaida katika mchezo, nashukuru timu yetu ni nzuri na kuna wachezaji wengine wazuri na ndiyo maana imeendelea kufanya vizuri,”alisema.
Simba SC kwa sasa inasaka kipa wa uhakika wa kusaidiana na kipa wake wa kwanza, Juma Kaseja ambaye amekuwa akisotoshwa peke yake bila kupumzika. Na hiyo inafuatia makipa wengine, Wilbert Mweta na Hamadi Waziri kushindwa kuonyesha uwezo wa kumsaidia Kaseja.
Katika mechi za mwishoni za mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Kaseja alionekana kuchoka na kudaka chini ya kiwango chake, jambo ambalo lilisababisha mashabiki wenye ‘akili mbovu’ wamfanyie fujo baada ya kufungwa mabao mawili katika mechi dhidi ya Mtibwa Sugar, Simba ikilala 2-0.
Kwa sababu hiyo, Kaseja alikasirika na kujiengua kwenye kikosi cha timu hiyo akisema hataki tena kuchezea Simba.
Lakini pamoja na matatizo hayo, Kaseja aliitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ambako ameendelea kufanya vizuri na kuonyesha yeye ni Tanzania One wa ukweli.  

MACHO YOTE KWA JOHN BOCCO ADEBAYOR WA CHAMAZI LEO

John Bocco 'Adebayor'

MSHAMBULIAJI tegemeo wa Tanzania, John Bocco ‘Adebayor’ bado anaongoza kwa mabao katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki, CECAFA Tusker Challenge baada ya mechi 14 kuchezwa hadi hadi jana.
Jumla ya mabao 15 hadi sasa yamefungwa katika mechi 14 za makundi yote matatu, zilizopigwa kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole, Kampala.
Bocco anachuana kwa ufungaji na washambuliaji wa Burundi, Chris Nduwarugira na Suleiman Ndikumana, ambao kila mmoja ana mabao mawili pia.
Wengine ambao hadi sasa kila mmoja amefunga bao moja ni Yussuf Ndikumana wa Burundi, Mohamed Jabril wa Somalia kwa penalti, Geoffrey Kizito wa Uganda, Yonatal Kebede Teklemariam, Haruna NiyonzimUganda, David Ochieng, Clifton Miheso na Jean Mugiraneza.
Bocco ana nafasi zaidi ya kuongeza mabao katika mechi za kundi hilo, haswa kwenye mchezo dhidi ya Somalia Desemba 1, kwani hiyo ndio timu dhaifu zaidi kwenye Kundi B.
Lakini Bocco kama atacheza kwa kiwango cha mechi dhidi ya Sudan, anaweza akawa mwiba hata leo mbele ya Burundi.
Kwa sasa Bocco anayechezea Azam FC ya Dar es Salaam, ndiye mshambuliaji pekee kwenye kikosi cha Bara, baada ya washambuliaji wengine, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaochezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemomkrasia ya Kongo (DRC) kuzuiliwa na klabu yao.
WAFUNGAJI CECAFA TUSKER CHALLENGE 2012
John Bocco                   Tanzania  2
Suleiman Ndikumana    Burundi    2
Yussuf Ndikumana        Burundi   1
Mohamed Jabril             Somalia   1(penalti).
Geoffrey Kizito               Uganda   1
Brian Umony                  Uganda   1
Yonatal Teklemariam     Ethiopia   1
Haruna Niyonzima         Rwanda   1
Jean Mugiraneza           Rwanda   1
David Ochieng               Kenya      1
Clifton Miheso                Kenya      1

OKWI ASEMA KOCHA ALIWAAMBIA WASITUMIE NGUVU NYINGI JANA

Okwi

EMMANUEL Okwi, mshambuliaji wa Uganda, The Cranes amesema jana kocha wao Bobby Williamson, raia wa Scotland aliwalekeza kucheza bila kutumia nguvu nyingi, ili kutunza nguvu kwa ajili ya mechi zijazo na ndiyo maana walipata ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Ethiopia katika mchezo wa Kundi A, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker, Challenge.
Akizungumza  baada ya mechi hiyo iliyopigwa Uwanja wa Mandela, Namboole, Okwi anayechezea Simba SC ya Tanzania, alisema kwamba kocha wao alitaka washinde bila kutumia nguvu nyingi, kwa kuwa mashindano bado yapo katika hatua za awali.
“Ni kweli bado mapema sana, mtu ukitumia nguvu nyingi unaweza kuumia na kuiachia timu pengo, sasa kocha amekuwa makini sana na sisi tunafuata maelekezo yake. Na amekuwa mwoga baada ya Abbel Dhaira (kipa) kuumia kwenye mechi na Kenya,”alisema Okwi na kuongeza.
“Na ukiangalia ni kweli, haina maana kuingia Robo Fainali wakati wachezaji wako wengi majeruhi, hautafika mbali, na sisi lengo letu ni kutetea Kombe hapa, tena mashindano yanafanyika nyumbani,”alisema Okwi.
Uganda jana ilishinda 1-0 na sasa inaongoza Kundi hilo kwa pointi zake sita, mabao mawili ya kufunga, haijafungwa bao hata moja, ikifuatiwa na Kenya yenye pointi tatu, mabao mawili ya kufunga na moja la kufungwa, Ethiopia pointi tatu pia bao moja la kufunga na moja la kufungwa na Sudan Kusini ambao hawana pointi wanashika mkia. Matokeo hayo yanamaanisha Uganda tayari imefuzu Robo Fainali, wakati Kenya na Ethiopia japo zina nafasi kubwa, lakini kwa uhakika zaidi ni hadi matokeo ya mechi za mwisho za kundi hilo. 

KILI STARS KUTINGA ROBO FAINALI LEO TUSKER CHALLENGE?

Kim Poulsen kulia akijadiliana jambo na Msaidizi wake, Sylvester

MICHUANO ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge 2012 inatarajiwa kuendelea leo kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole wakati timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars itakapojitupa dimbani kumenyana na Burundi, Int’hamba Murugamba.
Stars, inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, inahitaji ushindi katika mchezo wa leo utakaoanza saa 12:00 jioni, ili kujihakikishia kutinga Robo Fainali, baada ya awali kushinda mabao 2-0 dhidi ya Sudan.
Stars itamenyana na Burundi, ambayo inaongoza Kundi B kwa wastani wa mabao, japokuwa inalingana kwa pointi na Bara. Kabla ya mechi hiyo, Somalia wanaoshika mkia katika kundi hilo, watamenyana na Sudan kuanzia saa 10:00 jioni.
Kocha wa Kilimanjaro Stars, Mdenmark Kim Poulsen amesema kwamba uwezo wa timu yake unazidi kukua siku hadi siku na sasa ana matumaini ya kufanya vizuri zaidi katika michuano hii.
“Tuliwafunga Kenya (mchezo wa kirafiki Mwanza), tumewafunga Sudan, timu zote nzuri, Sudan wapo juu yetu kiuwezo katika viwango vya FIFA. Kwangu siangalii sana viwango vya FIFA, mpira ni pale unapokuwa uwanjani,”alisema Poulsen.
Akilizungumzia kundi lake, B lenye timu za Sudan, Somalia na Burundi, alisema ni gumu na wanatakiwa kupambana ili kufika mbali.
Lakini Poulsen amesema bado anawahitaji mno washambuliaji Mbwana Ally Samatta na Thomas Emanuel Ulimwengu wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) , ambao wamezuiwa na klabu yao.
Kim alisema jitihada za kuwaomba Mazembe wawaruhusu wachezaji hao zinaendelea.
“Sijui itakuwaje wasipokuja, itanibidi tu niwatumie wachezaji hawa hawa waliopo, najua nina mshambuliaji mmoja, lakini nitawatumia hawa hawa waliopo, Simon Msuva anaweza akawa mshambuliaji, nitafanyeje,”.
“Siwezi kuita mchezaji mwingine kutoka nyumbani kwa sasa, kwa sababu mtu lazima umuone uwezo wake, huwezi kumuita tu, kwa hivyo naomba Mungu tu Samatta na Ulimwengu waje,”alisema Kim.
Katika mchezo wa leo, Kim ambaye amekuwa akifuatilia kwa makini mashindano haya ili kujua uwezo wa timu zote, hatarajiwi kuwa na mabadiliko kwenye kikosi chake kutoka kile kilichoifunga Sudan 2-0.
Kama kawaida, Nahodha Juma Kaseja anatarajiwa kuanza, kulia akicheza Erasto Nyoni, kushoto Amir Maftah na mabeki wa kati, Kevin Yondan na Shomary Kapombe. Kiungo mkabaji Frank Domayo, wingi ya kulia Simon Msuva, kushoto Mrisho Ngassa kiungo mchezeshaji Salum Abubakar na Mwinyi Kazimoto atacheza nyuma ya mshambuliaji pekee, John Bocco ‘Adebayor’.
Mfumo wa sasa Kim unaonekana kuwa na tija kwa Stars, kwani analundika viungo wengi, huku akitumia mawinga ambao wanasababisha presha kubwa ya mashambulizi.
Leo kama Bocco atakuwa makini anaweza kufunga zaidi ya mabao mawili aliyofunga kwenye mchezo wa kwanza, kwani kama alivyosema timu inazidi kuimarika siku hadi siku.
MSIMAMO KUNDI A:
                      P   W  D   L    GF GA GD Pts
Uganda          2    2    0    0    2    0    2    6
Kenya            2    1    0    1    2    1    1    3
Ethiopia         2    1    0    1    1    1    0    3
Sudan Kusini 2    0    0    2    0    3    -3   0
MSIMAMO KUNDI B: 
                      P   W  D   L    GF GA GD Pts
Burundi         1    1    0    0    5    1    4    3
Tanzania       1    1    0    0    2    0    2    3
Sudan           1    0    0    1    0    2    -2  0
Somalia         1    0    0    1    1    5    -4  0
MSIMAMO KUNDI C:
                     P   W  D   L    GF GA GD Pts
Rwanda        1    1    0    0    2    0    2    3
Eritrea           1    0    1    0    0    0    0    1
Zanzibar        1    0    1    0    0    0    0    1
Malawi           1    0    0    1    0    2    -2   0
VIWANGO VYA UBORA FIFA
NCHI                 NAFASI
Uganda             86
Malawi              101
Ethiopia            102
Sudan               102
Rwanda             122
Burundi             128
Kenya               130
Tanzania           134
Zanzibar            134
Somalia             193
Eritrea               192
Sudan Kusini     200
(Viwango hivi vimetoka mwezi huu)



ZICO AJIUZULU KUINOA IRAQ.

ALIYEKUWA kocha wa timu ya taifa ya Iraq, Zico ameamua kujiuzulu wadhfa wake huo baada ya kudai kuwa Shirikisho la Soka la nchi hiyo limeshindwa kufikia makubaliano waliyokubaliana katika mkataba wake. Kujiuzulu kwa Zico ambaye ni nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil kumekuja ikiwa bado Iraq inapigania nafasi ya kushiriki michuano ya Kombe la Dunia 2014 itakayofanyika nchini Brazil. Iraq inashika nafasi ya tatu katika kundi B kwa timu za uapnde wa bara la Asia wakiwa na alama 5 katika michezo mitano waliyocheza wakipishana alama moja na Australia ambao wako katika nafasi ya pili huku Japan akiongoza kundi hilo kwa alama 13. Timu mbili ndio zitafuzu moja kwa moja kwenye michuano ya Kombe la Dunia 2014 wakati timu itakayoshika nafasi ya tatu itakwenda katika hatua ya mtoano. 

CAF YATOA ORODHA YA MAKUNDI YALIYOBAKIA KATIKA TUZO ZA MWAKA HUU.

SHIRIKISHO la Soka barani Afrika-CAF limetoa orodha ya makundi yaliyobakia katika tuzo zinazotolewa na shirikisho hilo kwa mwaka huu ambayo ni timu bora ya soka ya wanaume na wanawake pamoja na tuzo ya mchezaji mwenye kipaji zaidi. Mabingwa wa Afrika Zambia, Ivory Coast ambao wanaongoza kwa ubora barani Afrika, Cape Verde ambao wanashiriki kwa mara ya kwanza michuano ya Mataifa ya Afrika 2013 na Jamhuri ya Afrika ya Kati ndio timu zilizoteuliwa kugombea tuzo ya timu bora ya taifa. Mabingwa wapya wa soka wa Afrika kwa upande wa wanawake Equatorial Guinea, timu ya taifa ya wanawake ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Ghana ambao walinyakuwa medali ya fedha katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu, timu ya taifa ya Nigeria maarufu kama Falcon ndio timu zitakazogombea tuzo hizo kwa upande wa wanawake. Katika tuzo ya mchezaji mwenye kipaji zaidi lugha nyingine unaweza kuita Most Promising Talent wachezaji watakaochuana kugombea tuzo hiyo ni pamoja na Mohamed Salah wa Misri, Pape Moussa Konate wa Senegal, na Victor Wanyama wa Kenya. Washindi wa tuzo katika makundi hayo watajulikana Desemba 20 mwaka huu katika sherehe zitakazofanyika jijini Accra, Ghana.

ADRIANO AFUNGIWA MCHEZO MMOJA KWA KUSHINDWA KUCHEZA FAIR PLAY.

SHIRIKISHO la Soka barani Ulaya-UEFA limemfungia mchezo mmoja mshambuliaji wa Shakhtar Donetsk, Luiz Adriano kwa tabia isiyokuwa ya kimichezo wakati wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Nordsjaelland wiki iliyopita. Adriano ambaye ni raia wa Brazil alifunga bao wakati timu yake ikijaribu kurejesha mpira kwa golikipa wa Nordsjaelland kufuatia mchezaji wa timu hiyo kuumia. Katika taarifa ya UEFA iliyotumwa katika wavuti wake imesema kuwa kamati ya nidhamu ya shirikisho hilo imeamua kumfungia mchezaji huyo mechi moja kwa tukio lake hilo. Klabu ya Shakhtar katika taarifa yake imeunga mkono adhabu hiyo iliyotolewa na UEFA na kuonyesha kusikitishwa na tukio hilo lililotokea Novemba 20 mwaka huu. Mara baada ya mchezo kusimama na mchezaji wa Nordsjaelland kupatiwa matibabu mwamuzi aliruhusu mchezo kuendelea ambao beki wa Shakhtar William alipiga mpira kuurejesha kwa wapinzani wao kama Fair Play lakini Adriano aliunasa na kumpiga golikipa chenga na kufunga bao kitendo ambacho kilizua taharuki kwa wachezaji wakilalamikia kitendo cha Adriano.

HIDDINK KUSTAAFU MWISHONI MWA MSIMU.

MENEJA wa klabu ya Anzhi Makhachkala, Guus Hiddink amesema kuwa anatarajia kustaafu kufundisha soka mwishoni mwa msimu huu. Hiddink amewahi kuziongoza timu za taifa za Uholanzi na Korea Kusini katika nusu fainali ya michuano ya Kombe la Dunia na pia kuifikisha Urusi nusu fainali ya michuano ya Kombe la Ulaya pamoja na kushinda Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na klabu ya PSV Eindhoven ya Uholanzi. Kocha huyo ambaye mkataba wake na klabu ya Anzhi unaishia katikati ya mwaka 2013 amesema kuwa bado anajiona ana nguvu za kuendelea kufundisha lakini inabidi awe mwangalifu asifundishe kwa muda mrefu. Hiddink mwenye umri wa miaka 66 ambaye amewahi kuzifundisha pia klabu za Real Madrid na Chelsea amekiri kuwa kama akifanikiwa kuiwezesha Anzhi kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa mwakani anaweza kubakia hapo kwa mwaka mmoja zaidi.

 

UEFA CHAMPIONZ LIGI 2012/13

matches
 
standings
Novemba 20, Tue


Group E
Juventus - Chelsea   3 - 0  
Nordsjælland - Shakhtar Donetsk   2 - 5  
Group F
BATE Borisov - Lille   0 - 2  
Valencia - Bayern   1 - 1  
Group G
Spartak Moscow - Barcelona   0 - 3  
Benfica - Celtic   2 - 1  
Group H
CFR Cluj - Braga   3 - 1  
Galatasaray - Man. United   1 - 0  
Novemba 21, Wed


Group A
Dynamo Kyiv - PSG   0 - 2  
Porto - Dinamo Zagreb   3 - 0  
Group B
Arsenal - Montpellier   2 - 0  
Schalke - Olympiacos   1 - 0  
Group C
Zenit - Malaga   2 - 2  
Anderlecht - AC Milan   1 - 3  
Group D
Ajax - Dortmund   1 - 4  
Man. City - Real Madrid   1 - 1  
<
 
Up
 
Down
 
>
Results powered by xmlscores.com

UEFA EUROPA LIGI 2012/13

matches
 
standings
Novemba 28, Wed


Group I
Hapoel Ironi - Athletic Bilbao    
<
 
Up
 
Down
 
>
Results powered by xmlscores.com
News Items

Real wasonga Copa del Rey, Barca leo!

>>ITALIAN CUP: Dimbani leo!!
COPA_DEL_REYYale Mashindano ya kugombea Kombe la Mfalme, Copa del Rey, jana yaliendelea kwa Mechi za mardiano za Raundi ya Mtoano ya Timu 32 na Real Madrid waliichapa Alcoyano Bao 3-0 na hivyo kuibwaga nje kwa jumla ya Mabao 7-1
Bao za Real zilifungwa na Angel Di Maria na Jose Callejon bao mbili.
Leo, Mechi nyingine za Mashindano hayo zitaendelea na Mabingwa watetezi Barcelona, wanarudiana na Deportivo Alaves, Timu ambayo waliichapa Bao 3-0 katika Mechi ya kwanza.
Huko italy, Hatua ya 4 ya Italian Cup inaendelea leo kwa Mechi kadhaa.
Spain Copa del Rey
Raundi ya Timu 32
Jumanne Novemba 27
[Kwenye mabano jumla ya Mabao kwa Mechi mbili]
Osasuna 2 Sporting Gijon 0 [2-1]
Real Betis 3 Real Valladolid 0 [3-1]
Rayo Vallecano 0 Las Palmas 0 [0-1]
Real Sociedad 2 Cordoba 2 [2-4]
Real Madrid CF 3 Alcoyano 0 [7-1]
Malaga CF 0 Cacereno 1 [4-4, Malaga imefuzu kwa Magoli ya ugenini]
RATIBA:
Jumatano Novemba 28
Copa del Rey
Raundi ya Timu 32
[Kwenye mabano matokeo Mechi ya kwanza]
21:30 Levante v Melilla [0-1]
21:30 Valencia v Llagostera [2-0]
21:30 Getafe CF v Ponferradina [4-0]
21:30 Atletico de Madrid v Jaen [3-0]
23:30 FC Barcelona v Deportivo Alaves [3-0]
23:30 RCD Espanyol v Sevilla FC 1-3]
Italian Cup
Hatua ya 4
17:00 Chievo Verona v Reggina
17:00 Atalanta v AC Cesena
19:00 Bologna v Livorno
21:00 Siena v Torino FC
23:00 Fiorentina v Juve Stabia


BPL: Redknapp, QPR, waanza pamoja kwa sare 0-0 na Sunderland!

>>BENTEKE aipa ushindi Villa!!
HARRY_REDKNAPP12MATOKEO:
Jumanne Novemba 27
Sunderland 0 QPR 0
Aston Villa 1 Reading 0
+++++++++++++++++++++++++++
Ingawa QPR chini ya Meneja mpya  Harry Redknapp hawakuanza kwa ushindi lakini walionyesha Soka la ari kubwa walipotoka 0-0 na Sunderland Uwanjani Stadium of Light kwenye Mechi ya BPL, Barclays Premier League [Ligi Kuu England].
QPR walikosa nafasi kadhaa za kufunga, tatu toka kwa Straika wao Djibril Cisse na nyingine kwa Jamie Mackie na Adel Taarabt ambao mashuti yao yaliokolewa.
Sunderland pia walikosa nafasi moja kupitia Straika wao hatari Steven Fletcher.
Matokeo hayo hayakubadilisha Msimamo wa Timu zote mbili na QPR wameendelea kubaki mkiani wakiwa na Pointi 5 tu kwa Mechi 14 huku Sunderland wakiwa nafasi ya 16 wakiwa na Pointi 13 kwa Mechi 13.
VIKOSI:
Sunderland: Mignolet, Bardsley, Kilgallon, Cuellar, Rose, Larsson, Cattermole, Gardner, Johnson, Sessegnon, Fletcher. 
Akiba: Westwood, Campbell, Colback, Vaughan, Bramble, McClean, 
Saha.
QPR: Julio Cesar, Bosingwa, Hill, Nelsen, Traore, Granero, 
Mbia, Diakite, Taarabt, Mackie, Cisse.
Akiba: Green, Derry, Ferdinand, Park, Wright-Phillips, Da Silva, Hoilett.
Refa: Andre Marriner
+++++++++++++++++++++++++++
MSIMAMO-Timu za mwisho:
14  Newcastle Mechi 13 Pointi 14
15  Wigan Mechi 13 Pointi 14
16  Sunderland Mechi 13 Pointi 13
17  Aston Villa Mechi 14 Pointi 13
18  Southampton Mechi 13 Pointi 11
19  Reading Mechi 13 Pointi 9
20  QPR Mechi 14 Pointi 5
+++++++++++++++++++++++++++
Aston Villa 1 Reading 0
Bao la Dakika ya 80 la Christian Benteke limewapa ushindi Aston Villa wa Bao 1-0 dhidi ya Reading na kuwakwamua kutoka Timu 3 za mkiani na kuwafanya wakamate nafasi ya 17 kwenye Msimamo wa Ligi Kuu England.
VIKOSI:
Aston Villa: Guzan, Lowton, Baker, Clark, Stevens, Holman, Westwood, Bannan, Weimann, Agbonlahor, Benteke
Akiba: Given, Ireland, El Ahmadi, Albrighton, Delph, Bowery, Lichaj.
Reading: Federici, Cummings, Morrison, Mariappa, Shorey, Robson-Kanu, Leigertwood, Tabb, McAnuff, Roberts, Le Fondre
Akiba: Taylor, Pearce, Pogrebnyak, Hunt, McCleary, Harte, Gunnarsson.
Refa: Lee Probert
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumatano Novemba 28
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Chelsea v Fulham
Everton v Arsenal
Southampton v Norwich
Stoke v Newcastle
Swansea v West Brom
Tottenham v Liverpool 
[SAA 5 Usiku]
Wigan v Man City
Man United v West Ham
Jumamosi 1 Desemba 2012
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
West Ham v Chelsea
[SAA 12 Jioni]
Arsenal v Swansea
Fulham v Tottenham
Liverpool v Southampton
Man City v Everton
QPR v Aston Villa
West Brom v Stoke
[SAA 2 Dak 30 Usiku]
Reading v Man United
Jumapili Desemba 2
[SAA 1 Usiku]
Norwich v Sunderland
Jumatatu Desemba 3
[SAA 5 Usiku]
Newcastle v Wigan
 

FIFA yasaini Mkataba Matumizi ya Teknolojia ‘GOLI si GOLI!!’


>>MAJARIBIONI Japan kabla kupasishwa kwa KLABU BINGWA DUNIANI!
>>PIA PATA RATIBA KLABU BINGWA DUNIANI!
GLTYale matumizi ya Teknolojia ya kuwasaidia Marefa kuamua kama Mpira umevuka mstari wa Goli naGOLI_SI_GOLIhivyo ni Goli halali yamepiga hatua mbele baada ya leo FIFA kusaini Mikataba na Kampuni mbili za Waundaji wa Mitambo itakayotumika ya GLT [Goal Line Technology], Kampuni za Hawk-Eye Innovations na Fraunhofer ISS (GoalRef), ili itumike kwenye Mashindano ya FIFA ya kusaka Klabu Bingwa Duniani huko Japan kuanzia Desemba 6 hadi 16.
Michuano hiyo ya Klabu Bingwa Duniani itachezwa kwenye Viwanja viwili, Yokohama, ambako Mfumo wa GoalRef, unaotumia mionzi ya sumaku, utatumika na Uwanja wa Toyota, ambako ule wa Hawk-Eye, unaotumia Kamera, ndio utafungwa.
Mara baada ya kufungwa Mitambo hiyo, Taasisi ya Uswisi, EMPA, Swiss Federal Laboratories for Materials Science and Technology, itayafanya majaribio ya mwisho na yakifanikiwa tu FIFA itaruhusu matumizi yake katika Mechi zote 8 za Klabu Bingwa Duniani.
Lakini pia, kabla kila Mechi, Marefa wana jukumu la kujaribu Mitambo hiyo katika kila Goli Uwanjani na wakiridhika kuwa inafanya kazi vizuri watatoa taarifa kwa Wasimamizi wa Mechi kuwa kwenye Mechi husika wataitumia Mitambo hiyo kuwasaidia katika maamuzi yao.
Hata hivyo, kwa mujibu wa Sheria Namba 5 ya Sheria za Soka, Refa bado anabaki kuwa ndie Mwamuzi wa mwisho kama ni Goli halali au la na Mitambo hiyo inabaki tu kama chombo cha kuwasaidia kufika uamuzi huo na si Mwamuzi wa mwisho.
KLABU BINGWA DUNIANI 2012
TIMU ZITAKAZOSHIRIKI:
Chelsea-BINGWA ULAYA
Corinthians-BINGWA MAREKANI ya KUSINI
Monterrey-BINGWA MAREKANI ya KATI NA KASKAZINI
Auckland City-BINGWA KANDA ya OCEANIA
Usain Hyundai-BINGWA-Barani Asia
Al Ahly-BINGWA-Barani Afrika
Sanfrecce Hiroshima-BINGWA-Japan J-LIGI
RATIBA:
Raundi ya Mchujo - Desemba 6, Yokohama
1 Sanfrecce Hiroshima v Auckland City
ROBO FAINALI - Desembar 9, Toyota
2 Usain Hyundai  v Monterrey
3 MSHINDI Mechi Na 1 v Al Ahly
MSHINDI wa 5- Desemba 12, Toyota
Aliefungwa Robo Fainali 1 v Aliefungwa Robo Fainali 2
NUSU FAINALI
Desemba 12, Toyota
5 Mshindi Mechi Na 3 v Corinthians
Desemba 13, Yokohama
6 Mshindi Mechi Na 2  v Chelsea
MSHINDI wa 3 - Desemba 16, Yokohama
FAINALI - Desemba 16, Yokohama