Monday, October 15, 2012

Aminia Djz Intercollege Bash yatikisa Tabora

 Majaji waliohusika katika mchakato wa kuwapata washindi kutoka kushoto Ibra Warhymes,Edgar Msongela,Salu Bingo,Veronica Medard na Dulla K
 Huyu ndo mkali wa michano Derick B alieibuka katika nafasi ya kwanza,msanii ambae amepata ofa ya kurekodi ngoma mbili bure
 Lily Ommy kutoka Times Fm aliwakilisha vizuri kama Mc wa tukio zima
 Aminia Djjjjjjjjjzzzzz ebwana daaaaaah!
 Kwenye mashine Dj Kally
 Mshindi wa pili wa kuchana Dyanka G (watatu kutoka kushoto).Jamaa kapata ofa ya kurekodi ngoma moja bure

Mshindi wa kwanza katika ile category ya utangazaji Jackson Joseph (kushoto) jamaa kapata ofa ya kusoma Advanced Certificate in Journalism, Musoma Utalii College na kulia ni mshindi wa Djz jamaa anaitwa Dj K Sam

TENGA KUGOMBEA TENA URAIS TFF, NAFASI YA MAKAMU NI UTITIRI BALAA

Rais wa TFF, Leodegar Chillah Tenga atatetea nafasi yake?
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Chillah Tenga atatetea nafasi yake katika uchaguzi ujao wa shirikisho hilo, Desemba mwaka huu.
Habari ambazo nimezipata kutoka kwa watu walio karibu na Tenga, zinasema kwamba awali beki huyo wa zamani wa kimataifa wa Tanzania aliamua kutogombea, lakini baada ya kushawishiwa na swahiba wake, rais wa Shirikisho la Soka la KImataifa (FIFA), Sepp Blatter sasa atagombea.
“Tenga atagombea tena TFF, unajua Blatter ni rafiki yake na ndiye amemuomba aendelee, na Blatter mwenyewe atakuja hapa kumfanyia kampeni Tenga,”alisema mtu mmoja wa karibu na Tenga.
Taarifa zaidi zinasema tayari Tenga amekwishaanza kuwasiliana na wapiga kura na magwiji wa kampeni kwa ajili ya uchaguzi ujao.
Juhudi za kumpata Tenga mwenyewe kuzungumzia habari hizo hazikufanikiwa, lakini kama atagombea maana yake atachuana na Makamu wake wa sasa, Athumani Nyamlani ambaye kwa muda mrefu inaelezwa amekwishaanza kampeni.
Upinzani zaidi kwa Tenga iwapo kweli atagombea unatarajiwa kutoka kwa Jamal Emil Malinzi, aliyekuwa mpinzani wake katika uchaguzi uliopita Desemba 14, mwaka 2008.
Katika uchaguzi huo, Tenga alitetea nafasi yake kwa kumbwaga Malinzi kwenye ukumbi wa NSSF Waterfront kwa kura 64 dhidi ya kura 39 za Malinzi.
Awali Malinzi alienguliwa kwa kigezo cha uzoefu, lakini akarejeshwa kuwania nafasi hiyo baada ya kushinda rufaa yake.
Katika uchaguzi huo ulioshuhudiwa na Mwakilishi wa FIFA, Ashford Mamelodi, Athumani Nyamlani alishinda nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, baada ya kujikusanyia kura 65 kati ya kura 107 zilizopigwa na kura mbili kuharibika, akimshinda Lawrence Mwalusako aliyepata kura 39 na Ali Mwanakatwe aliyeambulia kura moja.
Nafasi ya Makamu wa Pili wa Rais, ilikwenda kwa Ramadhani Nassib aliyemwangusha mpinzani wake wa karibu, Damas Ndumbaro aliyepata kura 45.
Baadhi ya wagombea wanaotajwa kuwania nafasi ya Makamu wa kwanza wa rais katika uchaguzi ujao ni Frederick Mwakalebela, Wallace Karia, Michael Wambura, Wakili Alex Mgongolwa, Wakili Imani Madega, Wakili Damas Ndumbaro na Lawrcence Mwalusako. 

AZAM TAYARI WAPO MBEYA TANGU JANA

Azam FC

AZAM FC tayari wapo mjini Mbeya tangu jana saa 1:00 usiku, kwa ajili ya yao ya Jumatano, dhidi ya wenyeji Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini humo.
Azam waliondoka Morogoro jana asubuhi baada ya mechi yao ya juzi dhidi ya Polisi kwenye Uwanja wa Jamhuri na watafanya mazoezi kuanzia leo, ili kuzoea hali ya hewa ya mji huo.
Mbeya ni kati ya vituo ambavyo vinawaogopesha vigogo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam, Simba na Yanga kutokana na imani kwamba Prisons haifungiki kwenye Uwanja wake.
Sababu kubwa ni ubovu wa Uwanja wa Sokoine, ambao wenyewe Prisons wameuzoea na wanaujulia, wakati timu nyingine hupata tabu mno.
Kati ya vigogo hao watatu, ambao wanafukuzana kuwania ubingwa wa Ligi Kuu, Azam inakuwa timu ya pili kwenda Mbeya, baada ya Yanga iliyolazimishwa sare ya bila kufungana na Wajelajela hao kwenye mechi yao ya kwanza ya ligi hiyo.
Simba imeanzia Dar es Salaam kucheza na Prisons, Septemba 29, mwaka huu katika mechi ambayo walishinda kwa taabu mabao 2-1 na sasa watarudiana na Wajelajela hao mjini Mbeya katika mzunguko wa pili wa ligi hiyo.   
Mikoa mingine tishio ni Kanda ya Ziwa, ambako Azam tayari imekwishamaliza na kukusanya pointi nne baa ya kuifunga 1-0 Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba kabla ya kulazimishwa sare ya 2-2 na Toto Africans Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Yanga pia imemaliza deni la Kanda ya Ziwa, ikiambulia pointi tatu, baada ya kufungwa 1-0 na Kagera na kushinda 3-1 dhidi ya Toto. 

MILOVAN AMPA 100 OCHIENG

Ochieng katika mechi ya juzi

KOCHA wa Simba SC, Mserbia Profesa Milovan Cirkovick amesema kwamba amevutiwa na uwezo wa beki Mkenya, Paschal Ochieng katika mechi ya juzi dhidi ya Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Akizungumza  baada ya mechi hiyo iliyoisha kwa sare ya bila kufungana, Milovan alisema kwamba amevutiwa mno na uwezo wa Ochieng na kwamba sasa anaweza kuendelea kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza.
Lakini Milovan alisema hakuvutiwa kabisa na uchezaji wa mshambuliaji Daniel Akuffo kutoka Ghana.
“Sikuvutiwa kabisa na Akuffo,”alisema Cirkovick ambaye pia alisikitika kuwakosa wachezaji wake watatu nyota, Mrisho Ngassa, Ramadhan Chombo ‘Redondo’ ambao ni wagonjwa na Okwi, aliyekwenda kuichezea timu ya taifa ya Uganda, dhidi ya Zambia kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani.
Simba iliorejea Dar es Salaam jana na leo inatarajiwa kuendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Kinesi, kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, dhidi ya Kagera Sugar Jumatano Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo, Simba inatarajiwa kuwapokea wachezaji wake watatu iliyowakosa kwenye mechi ya juzi, Okwi, Ngassa na Redondo.
Okwi anatarajiwa kurejea Dar es Salaam leo, wakati Ngassa na Redondo tayari wamepona na leo wanaanza mazoezi na timu hiyo. 
Mechi nyingine za Jumatano zitakuwa kati ya Prisons na Azam FC kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya, Polisi Morogoro na JKT Ruvu Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, Mgambo JKT na Toto Africans Uwanja wa Mkwakwani, Tanga na JKT Oljoro dhidi ya African Lyon Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.
Simba bado ipo kileleni mwa Ligi Kuu kwa pointi zake 17, baada ya kucheza mechi saba, ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 16, ambayo hata hivyo imecheza mechi sita, wakati Yanga inashika nafasi ya tatu kwa pointi zake 11, baada ya kucheza mechi saba pia. 

YANGA WAINGIA KAMBINI CHANGANYIKENI LEO

Said Bahanuzi

KLABU ya Yanga ya Dar es Salaam, inatarajiwa kuingia kambini leo kujiandaa na mchezo wao ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting Jumamosi wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga ambayo katika mechi yake ya mwisho iliifunga Toto Africa mabao 3-1 mjini Mwanza, itaweka kambi kwenye hoteli ya Uplands, Changanyikeni, Dar es Salaam uku ikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa sekondari ya Loyola, Mabibo, Jijini.
Yanga itaendelea kuwakosa mazoezini wachezaji wake wawili majeruhi, beki Kevin Yondan na mshambuliaji Said Bahanuzi. 
Bahanuzi ‘Spider Man’ anatarajiwa kuanza mazoezi mepesi leo kufuatia kuchanika nyama za paja la mguu wa kulia katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba Jumatatu wiki iliyopita.
Bahanuzi aliumia dakika ya 23, baada ya kugongana na beki Benjamin Effe wa Kagera Sugar na kushindwa kuendelea na mchezo, nafasi yake ikichukuliwa na Jerry Tegete katika mechi ambayo Yanga ililala 1-0, beo pekee la Themi Felix.
Daktari wa Yanga, Sufiani Juma alisema mwishoni mwa wiki kwamba, mfungaji huyo bora wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, anaendelea vizuri baada ya kuchanika nyama za paja la mguu wa kulia.
“Lini haswa ataingia kwenye programu kamili ya mazoezi, itategemea na maendeleo yake atakapoanza mazoezi mepesi,”alisema Sufiani.
Kuhusu beki Kevin Yondan aliyeumia kwenye mechi dhidi ya Simba SC, Oktoba 3, mwaka huu baada ya kugongwa na Haruna Moshi ‘Boban’, Sufiani alisema naye anaendelea vizuri na wakati wowote wiki hii ataanza mazoezi mepesi.
Zaidi ya hao, Sufiani alisema Yanga ina majeruhi mwingine mmoja tu, ambaye ni Salum Telela ambaye naye anaendelea vizuri.
Bahanuzi ndiye tegemeo la mabao la Yanga kwa sasa, kwani tangu ajiunge na timu hiyo akitokea Mtibwa Sugar msimu huu, ameifungia mabao 12 katika mechi 13, ikiwemo ile dhidi ya Kagera aliyocheza kwa dakika 23 kabla ya kuumia na kutoka. 
Yanga kwa sasa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa pointi zake 11, baada ya kucheza saba, kushinda tatu, sare mbili na kufungwa mbili.
Simba iliyocheza mechi saba pia, inaongoza ligi hiyo kwa pointi zake 17, ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 16, iliyocheza mechi sita. 

ETO'O ALAUMU MAANDALIZI MABOVU YAMECHANGIA CAMEROON KUTOLEWA AFCON.

MSHAMBULIAJI nyota wa Cameroon, Samuel Eto’o amelaumu maandalizi mabovu ndio yaliyochangia timu yao kushindwa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika itakayofanyika nchini Afrika ya Kusini 2013.

 Pamoja na ushindi waliopata wa mabao 2-1 dhidi ya Cape Verde mchezo ambao uliochezwa jijini Younde kikosi hicho kilishindwa kufuzu baada ya kupoteza kwa mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza wa ugenini dhidi ya timu hiyo iliochezwa jijini Praia.

 Eto’o ambaye ndio amerejea katika kikosi hicho baada ya msuguano na maofisa wa soka nchi hiyo kumalizika alishindwa kukisaidia kikosi chake kufuzu michuano hiyo. 

 Akihojiwa mara baada ya ya mchezo huo Eto’o amesema kuwa kiakili walikuwa na wiki ngumu kabla ya mchezo huo kwakuwa walikuwa wanajua ni lazima wafunge mabao mawili bila kuruhusu nyavu zao kutikiswa ili waweze kwenda kwenye changamoto ya mikwaju ya penati lakini walishindwa na kuruhusu wavu wao kutikiswa. 

 Eto’o aliendelea kusema kuwa sasa inabidi wasahau hayo na kuhamishia nguvu zao kuhakikisha wanafuzu michuano ya Kombe la Dunia ambayo itafanyika nchini Brazil mwaka 2014.

AFCON 2013: Timu 15 za Fainali tayari, Vigogo Cameroun nje!!

  >>TIMU HIZO 15 kujumuika na Wenyeji Afrika Kusini Fainali Januari 2013!!
>>LEO ni DROO kupanga Mechi za Fainali!!!
+++++++++++++++++++++++++++++=
MATOKEO:
Jumapili Oktoba 14
[Kwenye mabano jumla ya Mabao kwa Mechi mbili]
Ethiopia 2 Sudan 0 [5-5]==Ethiopia wamepita kwa Goli za ugenini
Cameroon 2 Cape Verde 1 [2-3]
Algeria 2 Libya 0 [3-0]
Togo 2 Gabon 1 [3-2]
Angola 2 Zimbabwe 0 [3-3] ==Angola wamepita kwa Goli la ugenini
Niger 2 Guinea 0 [2-1]
Burkina Faso 3 Central African Republic 1 [3-2]
E.Guinea 2 Congo 1 DR [2-5]
++++++++++++++++++++++++++++++
AFCON_2013-NORMALBaada ya Wikiendi kuchezwa Mechi za marudiano za Raundi ya Mwisho ya Mchujo ya kuwania kutinga Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2013, Timu 15 zitakazojumuika na Wenyeji Afrika Kusini kwenye Fainali zitakazochezwa kuanzia Januari 19 hadi Feberuari 10 Mwakani zimepatikana.
Miongoni mwa hizo Nchi 15 ni Kisiwa kidogo cha Cape Verde ambacho kinashiriki Fainali kwa mara ya kwanza baada ya kuwatoa Vigogo Cameroun kwa jumla ya Mabao 3-2 kwa kushinda 2-0 kwao katika Mechi ya kwanza na kufungwa 2-1 katika marudiano huku Cameroun wakilazimika kumwomba Straika hatari Samuel Eto’o acheze baada ya kususa lakini hilo halikuwasaidia.
Nao Ethiopia, waliowahi kuwa Mabingwa Mwaka 1962, wanarudi tena kwenye Fainali baada ya Miaka 30 baada ya kugeuza kipigo cha 5-3 ugenini na kushinda nyumbani 2-0 hapo jana na kupita kwa Bao za ugenini baada ya jumla ya Mabao kuwa 5-5.
Droo ya kupanga Mechi za Fainali ya AFCON 2013 itafanyika leo Oktoba 15.
+++++++++++++++++++++++++++++=

TIMU ZILIZOTINGA FAINALI:
-Afrika Kusini [Wenyeji]
-Ghana
-Mali
-Zambia
-Nigeria
-Sierra Leone
-Morocco
-Ethiopia
-Cape Verde
-Angola
-Niger
-Algeria
-Togo
-Congo DR
-Burkina Fasso
-Ivory Coast [Wamepita baada ya kushinda 4-2 Mechi ya kwanza na kuongoza 2-0 ugenini na Mechi kuvunjika Dakika ya 76 kufuatia fujo za Mashabiki wa Senegal].
+++++++++++++++++++++++++++++=

POLAND v ENGLAND: Roy Hodgson kubadili Wachezaji 6!!

>> GERRARD, Johnson, Cole, Lescott, Milner, Defoe kurudi!!
>>LAMPARD, WALCOTT NJE!!
Meneja wa England Roy Hodgson huenda akaibadilisha nusu ya Timu yake ambayo kesho inatarajiwa kucheza ugenini na Poland kwenye Mechi ya Kundi H la Kanda ya Ulaya kusaka nafasi za kucheza Fainali za Kombe la Dunia Mwaka 2014 huko Nchini Brazil.
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO:
KUNDI H
1 England Mechi 3 Pointi 7
2 Montenegro Mechi 2 Pointi 4
3 Poland Mechi 2 Pointi 4
4 Ukraine Mechi 2 Pointi 2
5 Moldova Mechi 3 Pointi 1
6 San Marino Mechi 2 Pointi 0
+++++++++++++++++++++++
LEWANDOSKI_IN_POLANDInategemewa Wachezaji wasiopungua watano watabadilishwa toka kile Kikosi kilichoifunga San Marino 5-0 Ijumaa iliyopita na huenda idadi hiyo ikafika 6 ikiwa ataamua kumbadili Danny Welbeck na kumweka Jermaine Defoe.

Baada ya Wachezaji wa Chelsea, Frank Lampard na Ryan Bertrand, kujitoa baada ya kuumia, Hodgson atawachezesha Ashley Cole, Joleon Lescott na James Milner na pia Glen Johnson na Nahodha Steven Gerrard wako huru kucheza baada ya kumaliza Kifungo cha Mechi moja kufuatia kupewa Kadi.

Hata hivyo, baada ya kufunga Bao mbili kwenye Mechi na San Marino, Danny Welbeck huenda akabakisha namba yake kwenye Timu ingawa Defoe nae ana rekodi nzuri Msimu huu.
Ni wazi James Milner atambadili majeruhi Theo Walcott alieumizwa na Kipa wa San Marino Aldo Simoncini.

Huko Kambi ya Poland, Timu hiyo itamkosa Nahodha wao Jakub Blaszczykowski ambae aliumia akichezea Klabu yake Borussia Dortmund lakini Wachezaji wengine wawili wa Klabu hiyo Bingwa ya Germany, Robert Lewandowski na Lukasz Piszczek, wapo fiti na wanatarajiwa kucheza.

Golini mwa Poland, ambayo sasa ina Kocha mpya Waldemar Fornalik, anategemewa kukaa Kipa wa Manchester United Tomasz Kuszczak ambae sasa yuko kwa mkopo huko Brighton, Timu inayocheza Daraja la Championship huko England badala ya Makipa wa Arsenal, Wojciech Szczesny na Lukasz Fabianski, ambao wamekuwa nje ya Uwanja kwa muda baada ya kuumia.

Hadi sasa kwenye Kundi H, Poland wamecheza Mechi mbili na wana Pointi 4 baada ya kutoka 2-2 na Montenegro na kuifunga Moldova 2-0.

VIKOSI VINATARAIWA:
Poland: Kuszczak; Perquis, Wasilewski, Wojtkowiak, Wawrzyniak; Borysiuk, Mierzejewski, Krychowiak, Wszolek; Lewandowski, Piech
England: Hart; Johnson, Cahill, Jagielka, Cole; Milner, Carrick, Gerrard, Oxlade-Chamberlain; Defoe, Rooney

BRAZIL v JAPAN: Marcelo avunjika!

MARCELO_of_REAL>>MFUPA wa Kidole cha Mguu, kuwa nje hadi Miezi 3!!
Fulbeki wa Brazil na Real Madrid Marcelo amevunjika mfupa wa kidole cha mguu wakati akiwa mazoezini na Timu ya Taifa ya Brazil inayojitayarisha kucheza Mechi ya Kirafiki na Japan huko Wroclaw, Poland Jumanne Oktoba 16 na hili ni pigo kubwa kwa Real Madrid kwani Ijumaa walimpoteza Fulbeki mwingine, Fabio Coentrao, alieumia akiwa na Nchi yake Portugal iliyokuwa ikicheza na Russia.
Wachezaji wote hao wawili watarudi kwenye Klabu yao Real Madrid kwa uchunguzi zaidi.

Baadae Shirikisho la Soka la Brazil lilitoa taarifa kuwa Marcelo anategemewa kuwa nje ya Uwanja kwa kipindi kinachoweza kufikia Miezi mitatu.

Mechi ya Brazil na Japan itakuwa Mechi ya pili ya Kirafiki kwa kila Timu kucheza Barani Ulaya ndani ya Wiki moja kufuatia Brazil kuichapa Iraq 6-0 Alhamisi iliyopita huko Malmo, Sweden na Japan kuitungua France 1-0 huko Paris, France.

Brazil ndio watakuwa Wenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 na Japan wapo kwenye kinyang’anyiro cha kuingia Fainali hizo kutoka Kundi lao la Bara la Asia.

KOMBE la DUNIA: Jumanne Spain v France

>>Iniesta ndani kwa Spain!!
>>FRANCE yapagawishwa kufungwa na Japan!!
ARMADILLO-STANDARDJumanne, Mjini Madrid, Mabingwa wa Dunia na Ulaya, Spain, wanaikaribisha France kwenye Mechi ya Kundi I la Kanda ya Ulaya kusaka nafasi kucheza Kombe la Dunia Mwaka 2014 na kitu pekee kinachomuumiza kichwa Kocha wa Spain, Vicente Del Bosque, ni nani ampange wakati France wao wameweweseka baada ya kuchapwa bao 1-0 na Japan kwenye Mechi ya Kirafiki hivi juzi.

Juzi, wakicheza Stade de France Mjini Paris, France walifungwa bao 1-0 na Japan katika Mechi ya Kirafiki, kwa bao lililofungwa mwishoni na hicho ni kichapo cha kwa kwanza kwa Kocha Didier Deschamps tangu aitwae Timu kutoka kwa Laurent Blanc mara baada ya kutolewa kwenye Robo Fainali ya EURO 2012 walipochapwa na Spain.

France watakwenda huko Madrid bila ya Viungo wa Wakabaji, Abou Diaby na Rio Mavuba, ambao wameumia lakini pia kitu kinachowapa fadhaa ni kuendelea kwa ukame wa magoli kwa Straika wao Karim Benzema ambae amefunga bao 15 tu katika Mechi 53 alizochezea Spain.

Kwa Spain, hali ni murua hasa baada ya kushinda ugenini katika Mechi yao ya pili ya Kundi I walipoitandika Belarus bao 4-0 na kutwaa uongozi wa Kundi hilo kwa tofauti ya magoli mbele ya France.
+++++++++++++++++++++++

MSIMAMO:
KUNDI I
1 Spain Mechi 2 Pointi 6 [Tofauti ya Magoli 5]
2 France Mechi 2 Pointi 6 [Tofauti ya Magoli 5]
3 Georgia Mechi 3 Pointi 4
4 Finland Mechi 2 Pointi 1
Belarus Mechi 3 Pointi 0
+++++++++++++++++++++++
Kocha wa Spain, , Vicente Del Bosque, ambae alimchezesha Kiungo Sergio Busquets kama Sentahafu na kumpa namba Kiungo wa Arsenal, Santi Cazorla, kwenye Mechi na Belarus, anatarajiwa kufanya mabadiliko kwa ajili ya Mechi na France na kumweka Raul Albiol kama Sentahafu na pia kumchezesha Kiungo Andres Iniesta ambae hakucheza na Belarus.

Mechi hii ya Jumanne kati ya Spain na France inazikutanisha Timu zote zenye Pointi 6 kila mmoja na kila Timu inataka ushindi ili kupita moja kwa moja kwenda Fainali za Kombe la Dunia kama Mshindi wa Kundi.

VIKOSI VINATARAJIWA:
Spain: Iker Casillas; Alvaro Arbeloa, Sergio Ramos, Raul Albiol, Jordi Alba; Sergio Busquets, Xabi Alonso, Pedro, Xavi, Andres Iniesta, Cesc Fabregas

France: Hugo Lloris; Mathieu Debuchy, Laurent Koscielny, Mamadou Sakho, Patrice Evra; Moussa Sissoko, Yohan Cabaye, Blaise Matuidi; Franck Ribery, Karim Benzema, Jeremy Menez

RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumanne Oktoba 16
[SAA za BONGO]
Albania v Slovenia
Andorra v Estonia
Belarus v Georgia
Belgium v Scotland
Bosnia-Hercegovina v Lithuania
Czech Republic v Bulgaria
Hungary v Turkey
Iceland v Switzerland
Israel v Luxembourg
Latvia v Liechtenstein
Macedonia v Serbia
Portugal v Northern Ireland
Romania v Netherlands
Russia v Azerbaijan
San Marino v Moldova
Slovakia v Greece
Spain v France
Ukraine v Montenegro
2000 Cyprus v Norway
2100 Faroe Islands v Rep of Ireland
2130 Austria v Kazakhstan
2130 Croatia v Wales
2145 Germany v Sweden
2145 Italy v Denmark
2200 Poland v England

VETTEL KUITOSA RED BULL NA KUHAMIA FERRARI.

BINGWA mara mbili wa dunia wa michuano ya langalanga, Sebastian Vettel anajipanga kujiunga na timu ya Ferrari mwaka 2014 huku Filipe Massa akibakia katika timu hiyo ya Italia kwa mwaka ujao.  
 
Chanzo kutoka ndani ya Ferrari kilihabalisha kuwa Vettel mwenye umri wa miaka 25 tayari amesaini mkataba na timu hiyo kwa ajili ya kijiunga mwaka 2014 lakini itategemea na matokeo ya timu hiyo. Vettel ambaye anatarajiwa kuchukua nafasi ya Fernando Alonso mwenye umri wa miaka 31 ambaye toka ajiunge na timu hiyo baada ya kunyakuwa taji la dunia akiwa na timu ya Renault mwaka 2005 na 2006 ameshindwa kutamba akiwa na Ferrari. 
 
 Vettel ambaye kwasasa yuko timu ya Red Bull ndio anaongoza akiwa na alama sita zaidi ya Alonso katika kinyang’anyiro cha kufukuzia taji la dunia msimu huu.
 
DJOKOVIC ALIPA KISASI KWA MURRAY.

MCHEZA nyota kutoka uingereza Andy Murray ameshindwa kunyakuwa taji la tatu mfululizo la Shanghai Masters baada ya kukubali kipigo kutoka Novak Djokovic wa Serbia. 
 
 Nyota hao ambao wamekutana kwa mara ya kwanza toka Murray anyakue taji la michuano ya wazi ya Marekani, Djokovic alifanikiwa kuibuka mshindi kwa 5-7 7-6 6-3. Katika mchezo huo Murray ambaye anashika namba tatu katika orodha za ubora duniani alionyesha mchezo ambao aliutumia kumuondosha Roger Federer katika hatua ya nusu fainali lakini Djokovic alionyesha kujipanga vyema kulipa kisasi baada ya Murray kumfunga katika michezo miwili iliyopita.
 
 Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Djokovic amesema kuwa mara nyingi anapokutana na Murray huwa anategemea mchezo mgumu na mrefu lakini anashukuru kwamba safari hii yeye ndio aliyeibuka mshindi.
 
by tano juma machibya