Saturday, November 17, 2012

 

SERENGETI BOYS KWENYE CHAKULA CHA JIONI HOTEL YA JB BELMONT












Kocha wa serengeti boys na kocha wa Congo brazaville wakiwa kwenye press
Timu ya taifa ya vijana Serengeti Boys jana usiku ilifanyiwa hafla fupi ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na kamati maalumu ya kuhamasisha watanzania kuichangia timu hiyo pamoja kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri katika mchezo wake dhidi ya timu ya vijana kutoka Congo Brazzaville ilifanyika katika hoteli ya JB Belmonte iliyo jijini,  Dar es Salaam.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na wadau mbalimbali kwa lengo la kubadilishana mawazo, pamoja na kutunisha mfuko wa Serengeti ambao inahitaji shilingi milioni 162 ili kufanikisha azma ya kutinga fainali za mataifa ya Afrika, fainali ambazo zitafanyika mwakani nchini Morroco.
Rais wa shirikisho la soka nchini Leodgar Tenga alipata nafasi ya kusema machache ambapo alirejea wito wake wa kuwataka vijana hao kuhakikisha wanafanya vizuri kwa kutekeleza maagizo ya makocha wao Jacob Michelsen na Jamhuri Kihwelu huku wakijua wazi kuwa wamebeba roho za watanzania wengi ambao wanawaunga mkono.
Amewata kuiga mfano wake ambapo mbali ya kuichezea timu ya Taifa katika miaka ya sabini na themanini lakini pia alikuwa nahodha wa timu ya Taifa ambayo ilishiriki kwa mara ya mwisho fainali za mataifa ya Afrika.
Amewataka pia kukumbukuka maneno mazuri aliyozungumza gwiji la zamani la soka barani Afrika Abeid Pele ambaye alikuwepo nchini hivi karibuni ambapo mmoja wa wachezaji wa Serengeti, Hussein Twaha alimnukuu Pele alipozungumza nao uwanja wa Karume pale alipowatembelea maneno ambayo yaliwasisimua wadau waliokuwepo ukumbini hapo.
Alisema , “mpira hauchezwi na watoto wa matajiri bali watoto wa maskini na kipaji pekee hakitoshi kukupeleka kwenye mafanikio bali inahitajika juhudi binafsi” mwisho wa kunukuu.
Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa kamati ya Serengeti Kassim Dewji amewataka vijana hao kusahau maneno ya kuwa Congo imekuja na wachezaji vijeba na badala yake wafanye kazi kuhakikisha wanawadhibiti vilivyo na ushindi upatikane.
Dewji amesema yeye anaamini maandalizi waliyofanya vijana hao ni mazuri na kwamba wahakikishe wanatoka na ushindi wa kishindo katika mchezo wa jumapili ili kuwapa kazi ya ziada katika mchezo wa marudiano utakao fanyika nchini Congo wiki mbili baadaye.
Neno zuri kwa vijana hao kutoka kwa Dewji ni kwamba anaamini watavuka hatua hiyo na wataelekea Morroco Mwakani na kwamba baada ya fainali za Morroco basi Mungu akipenda wachezaji zaidi ya 15 watape timu za kucheza barani Ulaya.
Naye Mwenyekiti wa Azam mzee Said Mohamed alikumbushia namna alivyocheza soka wakati wa ujana wake ambapo alisema alikuwa hodari katika kupenyeza mipira ya krosi ambapo alikuwa na uwezo wa kukimbia na kupiga jambo ambalo lilikuwa likimfurahisha kocha wake na hivyo vijana hao waige mfano wake
Juliana Matagi Yasoda, Kaimu Mkurugenzi ya michezo Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo amesema serikali iko nyuma ya vijana hao na kwamba imemshangaza kuona timu ya taifa ya vijana ikifanyiwa hafla nzuri kama hiyo jambo ambalo hakuwahi kuliona siku za nyuma.
Hata hivyo kilio chake ni kwamba wajitume kwa kadri wawezavyo na kwamba serikali inawasapoti.
Jacob na Kihwelu wamewahamasisha vijana kufanyia kazi yale wanayo wafundisha na kwamba wana imani uwezo mkubwa wa kuwafunga Congo wanao.
Jamhuri Kihwelu amesema   kama wanataka kupata mafanikio na maisha mazuri katika maisha yao, basi muda sasa umefika wa kufanya hivyo ambapo endapo watawafunga CongoBrazaville  basi kila mtu atajitokeza kuwachangia zaidi tofauti na ilivyo sasa.
Timu hiyo ya vijana imehashia kambi yake katika hoteli ya JB Belmonte na itaendelea kuwepo hapo mpaka baada ya mchezo wao dhidi ya Congo Brazzaville mchezo ambao utachezwa jumapili katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

 UCHAGUZI WA TFF SASA KUFANYIKA MWAKANI


Uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) unatarajiwa kufanyika Februari, mwakani.

Akitangaza uchaguzi huo Mwenyekiti wa kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji, Alex Mgongolwa amesema uchaguzi huo umesogozwa mbele ili kupisha marekebisho ya katiba ya TFF kama walivyoagizwa na Shirikisho la Soka barani Afrika. (CAF)

Kipengele kinachotakiwa kuingizwa kinahusu “Club Lincencing” kama ilivyoagizwa na CAF katika waraka wake unaowataka wanachama wote wa CAF kuingiza kwenye katiba zao.
   
Mngongolwa alisema kutokana na ushauri na maagizo ya FIFA, TFF inatakiwa kuunda wa Kamati ya Rufaa ya Uchanguzi (“Elections Appeals Committee”) na kuondokana na utaratibu tulionao hivi sasa ambao Kamati ya Rufaa (“Appeals Committee”) inajigeuza na kuwa Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi wakati wa mchakato wa uchaguzi wa TFF.
  
Pia kuindoa nafasi ya Makamu wa Pili wa TFF pamoja na kutamka kuwa Wawakilishi wa klabu za Ligi Kuu katika Kamati ya Utendaji watachaguliwa moja kwa moja na klabu zenyewe.

Pia azimio la Mkutano Mkuu uliopita la kuruhusu uundwaji wa chombo huru cha kusimamia Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza pamoja na kupitishwa kwa Kanuni zinazokiongoza chombo hicho kama zilivyopendekezwa na klabu za Ligi Kuu na kupitishwa na Kamati ya Utendaji.

Mngongolwa aliendelea kusema kwa vile mapendekezo mawili kati ya matatu ya marekebisho ya Katiba yana uhusiano na Uchaguzi Mkuu wa TFF, kamati yake ikaona ipo haja ya marekebisho kufanyika kabla ya kutangazwa kwa Mkutano Mkuu wa TFF na kuanza kwa mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa TFF.


Aidha, kwa vile TFF haina uwezo wa kuitisha mikutano mikuu miwili – Mkutano Mkuu Maalum kwa ajili ya marekebisho ya Katiba ya TFF; na Mkutano Mkuu wa Uchaguzi – katika kipindi kifupi kijacho, marekebisho ya Katiba yafanywe kwa njia ya Waraka (“Circular Resolution”).

Katika kipindi Novemba 15 mwaka huu  mwenyekiti wa kamati ya sheria na sekretarieti wataandaa waraka ambao utakabidhiwa kwa wajumbe wakamati ya utendaji ya TFF wanaowakilisha kanda na kuhakikisha kila mjumbe anapata fursa ya kutoa ridhaa yake na zoezi hili litadumu kwa siku 21 tu.

Baada ya hapo Kamati ya Utendaji itafanyika Jumamosi Desemba 15, mwaka huu kwa madhumuni ya kupokea taarifa ya zoezi hili na kufanya matayarisho ya Mkutano Mkuu.


Kutokana na Katiba ya TFF kuelekeza kuwa taarifa ya Mkutano Mkuu itolewe kwa wanachama wake angalau siku 60 (“notice period”) kabla ya Mkutano, Kamati ya utendaji inatarajia kuwa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi utafanyika Jumamosi na Jumapili ya tarehe 16 na 17 na Februari 2013.

Kamati ya Utendaji ya TFF inasisitiza kuwa utaratibu huu umeamuliwa kutokana na TFF kutokuwa na uwezo wa kifedha wa kutayarisha mikutano mikuu miwili katika kipindi kifupi kijacho. Kinyume chake ni kuchelewa zaidi kufanyika kwa Mkutano Mkuu, jambo ambalo hatuna budi kuliepuka.

Alimalizia kusema kuwa Kamati ya Utendaji inatarajia kupata ushirikiano wa karibu kutoka kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na wadau wa mpira wa miguu kwa jumla ili kufanikisha zoezi hili na hatimaye kufanikisha Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa TFF.

 

MWANAMBAYA MKURANGA WAANDAA BONANZA


UONGOZI wa Mwanambaya FC ya Mkuranga, Pwani umeandaa bonanza la mchezo wa soka litakaloanza Novemba 20 na kumalizika Novemba 24 mwaka huu.

Bonanza hili litafanyika kwenye uwanja wa Mwanambaya, Mkuranga na timu zilizoalikwa ni Afriroots Soccer Rangers na Salim FC za Dar es Salaam.

Timu ambazo zitafungua dimba siku ya jumanne ni Afriroots Soccer Rangers na Mwanambaya FC, jumatano  zitapambana Afriroots Soccer Rangers na Salim FC.

Novemba 24 uwanja wa Mwanambaya utawaka moto kwa Kombaini ya Mwanambaya kumenyana na Afriroots Soccer Rangers.

Akizungumza jijini Dar es salaam Mlezi wa Afriroots Soccer Academy Mwinyimad Tambaza alisema wamefurahi kualikwa kushiriki bonanza hilo kwani litawafanya kufahamiana na wachezaji wengine nje ya Dar es Salaam.

"Tunafurahi kualikwa kwenye bonanza hili na tutaenda kushiriki ili kuhamasisha michezo na kuongeza marafiki wa timu yetu", alisema Tambaza ambaye pia ni katibu wa chama cha kuendeleza Soka la vijana Dar es Salaam.

STARS WAUNGANA NA DROGBA, ROBBEN WASH UNITED

BIN KLEB AWAFARIJI MPIRA PESA KUFUTIWA UANACHAMA SIMBA, AWANUNULIA TIKETI ZA KUANGALIA MECHI YA SERENGETI BOYS NA KONGO KESHO

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga SC, Abdallah Ahmad Bin Kleb amewafariji wanachama wa Simba wa tawi Mpira Pesa waliofutiwa uanachama kwa kuwanunulia tiketi za kwenda kuangalia mechi ya kesho ya Serengeti Boys na Kongo Brazzaville, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Pichani Bin Kleb akipokea tiketi hizo baada ya kuzilipia.    

WACHEZAJI SERENGETI WASEMA, HATA KAMA WAMEKUJA NA VIBABU, KONGO LAZIMA WAFE KESHO TAIFA

Miraj Adam kulia akizungumza jana na kushoto ni Hussein Twaha


NAHODHA wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys, Miraj Adam amesema kesho watapigana kwa nguvu zao zote, kuhakikisha wanawafunga Kongo Brazzaville ili watimize ndoto zao za kucheza Fainali za Vijana chini ya umri wa miaka 17 nchini Morocco mwakani.
Akizungumza jana kwenye hoteli ya JB Belmonte, Dar es Salaam, Adam alisema kwamba hata kama Kongo Brazzaville wamekuja na wachezaji waliovuka umri kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo, lakini kesho watafungwa tu.
“Kongo watakufa, watake wasitake, nasema Kongo watakufa,”alisema kwa hisia kali Adam anayechezea Simba wakati wa hafla maalum ya chakula cha usiku kuichangia timu hiyo.
Kwa upande wake, Msaidizi wake, Hussein Twaha ‘Messi’ alikumbushia maneno waliyoambiwa na mwanasoka bora wa zamani Afrika, Abedi Ayew Pele katika ziara yake nchini hivi karibuni na kusema yatakuwa kichocheo kwao kufanya vizuri na kukata tiketi ya Morocco.
“Pele alituambia mpira unachezwa na watoto kutoka familia masikini, hata yeye alitoka familia ya kimasikini, akajitahidi akafanikiwa na kufanya watoto wake waingie katika mpira wakitokea familia ya kitajiri, hivyo na sisi tunatumia kauli hii kama kichocheo cha kufanya vizuri ili tufuate nyayo zake,”alisema Twaha, anayechezea Coastal Union.
Kocha Mkuu, Mdenmark Jacob Michelsen alishukuru kwa sapoti ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) katika maandalizi na akasema ana matumaini makubwa ya kuwatoa Kongo, kwani amewaandaa vema vijana wake.
Kocha Msaidizi, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ alisema kwamba wachezaji wanatakiwa kujituma ili kushinda mechi hiyo na kujiwekea mazingira mazuri ya kufuzu.
Rais wa TFF, Leodegar Tenga aliwaambia vijana kwamba amekuwa mchezaji, kocha, kiongozi, Mjumbe wa bodi mbalimbali na Mwenyekiti wa Bodi, lakini katika maisha yake ya soka hakuna kitu anachojivunia kama kuwa Nahodha wa timu ya taifa, hivyo akawataka vijana wakapigane kesho kwenda kuweka historia.
Juzi Michelsen alisema kwamba ana wasiwasi wapinzani wake, Kongo Brazzaville wana wachezaji waliozidi umri, baada ya kuichunguza vizuri Kongo na sasa anaifahahamu vema.
Michelsen alisema kwamba alikwenda kushuhudia mchezo wa kwanza wa raundi iliyopita, baina ya Kongo na Zimbabwe waliotolewa na wapinzani wao hao na kujionea makali ya wapinzani wao.
Pamoja na kukiri kwamba Kongo ni timu bora na ilicheza Fainali zilizopita za Kombe la Dunia nchini Mexico mwaka jana na kutolewa raundi ya pili, Michelsen alisema bado ana wasiwasi timu hiyo ina ‘vijeba’.
“Nilipokwenda kuwaangalia wakicheza na Zimbabwe, nilikuta kikosini mwao kuna wachezaji sita wa kikosi kilichokwenda Mexico kwenye Kombe la Dunia, inanitia shaka kwa sababu hakuna mchezaji anayeweza kucheza michuano mikubwa kama ile akiwa ana umri wa miaka 15.
Mimi ni kocha wa vijana na ninajua, haiwezekani. Ucheze fainali za Kombe la Dunia za U17 una miaka 15, hakuna,”alisema Michelsen, ambaye aliwataja baadhi ya wachezaji anaowatilia shaka wamezidi umri ni Hady Binguila na Charvely Mabiat.
Amesema wamecheza mechi za kujipima nguvu 15 zikiwemo dhidi ya timu za Ligi Kuu na hawajafungwa hata moja, kitu ambacho anaamini ni kipimo cha ubora wa timu yake.
Serengeti jana ilihamia katika hoteli ya JB Belmonte, kutoka hoteli ya Itumbi, ili kuwaweka vizuri kisaikolojia vijana, hizo zikiwa ni jitihada za Kamati maalum iliyoundwa kuisaidia timu hiyo. 
Serengeti imefanikiwa kufuzu hadi Raundi ya Tatu bila jasho, baada ya wapinzani wake wa awali katika Raundi ya Kwanza na ya Pili, Kenya na Misri kujitoa. Iwapo timu hii itafuzu, hii itakuwa mara ya pili kwa Serengeti kukata tiketi ya kucheza fainali hizo, baada ya mwaka 2005.
Hata hivyo, pamoja na kuzitoa Rwanda, Zambia na Zimbabwe, Serengeti haikwenda Gambia mwaka huo kutokana na kuondolewa kwenye michuano hiyo na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), baada ya kubainika walitumia kijana aliyezidi umri, Nurdin Bakari.  

KILIMANJARO MARATHON KUFANYIKA MACHI 3 MWAKANI

Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Kushilla Thomas akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mbio za Kilimanjaro Marathon 2013 katika ukumbi wa Serengeti, ndani ya hoteli ya JB Bellmonte, Dar es Salaam. Kulia kwake ni Katibu wa Riadha Tanzania, Suleiman Nyambui na kushoto Mkurugenzi Msaidizi wa Michezo, Juliana Yassoda na Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe.  
MASHINDANO ya Riadha ya 11 ya Kilimanjaro Marathon yanatarajiwa kufanyika Machi 3, mwakani mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa mashindano hayo usiku huu katika hoteli ya JB Belmonte mjini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bi. Kushilla Thomas alisema bia ya Kilimanjaro Premium Lager inaendelea na udhamini wa mbio hizo zinazoendelea kuwa kubwa na bora kila mwaka huku zikiibua vipaji vipya na kuwapa wanariadha chipukizi fursa ya kukua na kuweza kushindana kimataifa.
“Kilimanjaro Premium Lager inalenga kuendeleza riadha kwa kukuza vipaji, kuwapa wanariadha wetu jukwaa la kushindania na wanariadha kutoka mataifa mbalimbali.” Alisema Kushilla.
Aliongeza kuwa bia ya Kilimanjaro Premium Lager ina lengo la kuhakikisha mashindano hayo yanakuwa na mvuto kwa wanariadha wenye vipaji ili kuongeza ubora wa riadha ya Tanzania ili Watanzania waweze kushiriki kikamilifu kwenye mashindano makubwa duniani.
Kwa upande wake, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema: “Kupata washiriki kutoka nchi mbalimbali inatusaidia kuonyesha dunia kuwa Kilimanjaro Marathon nini lakini kuwaendeleza na kuwapa moyo wanariadha Watanzania ni kipaumbele chetu kikubwa, kwa sababu hiyo tumeanzisha zawadi maalum ya shilingi milioni 3 kwa Watanzania watakaomaliza wakiwa wa kwanza katika mbio za 42km Kilimanjaro Premium Lager Marathon na hii ni mbali na zawadi watayopata kwa nafasi watakazoshinda.”
“Maandalizi ya Kilimanjaro Marathon 2013 yameishaanza ili kuhakikisha mbio hizo zinakuwa bora kama ilivyo utamaduni wetu kuhakikisha tunaboresha kila mwaka ili kuwapa raha ya aina yake washiriki pamoja na watazamaji.”
 “Kwa mara nyingine tena, Kilimanjaro Premium Lager itaendelea kuwathamini wanariadha kwa kuwatunuku zawadi nzuri ya fedha taslimu huku ikiwapa watazamaji burudani ya aina yake.”
Zawadi ya fedha taslimu kwa washindi wa kwanza hadi wa tatu wanaume kwa wanawake kwenye mbio ndefu za km 42.195 zijulikanazo kama Kilimanjaro Premium Lager Marathon itakuwa ni shilingi milioni 3 , washindi wa pili watajipatia shilingi milioni 1.5 kila mmoja huku washindi wa tatu wakijipatia shilingi 850,000 kila mmoja. Zawadi nhii itakuwa ni kivutio kwa wanariadha mashuhuri kushiriki katika mbio hizi zinazoingia mwaka wa 11 tangu kuanzishwa.


Utepe unakatwa

Crew ya wadhamini wa Kili Marathon

Kushilla akizungumza 

Kavishe akizungumza

Kushoto ni Rais wa PARALIMPIKI, Johonson Jasson na kulia na Nyambui

Kavishe akizungumza na John Addison, Mkurugenzi wa Wild Frontiers, waandaaji wa Kili Marathon

Mkurugenzi wa Executive Solutions, Aggrey Marealle akizungumza

Mohamed Omar wa KK Security

Walimbwende wa Executive Solutions

DINNER YA SERENGETI BOYS NDANI YA JB BELMONTE

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga akizungumza katika hafla ya chakula cha usiku kwa ajili ya kuichangia timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys usiku huu kwenye hoteli ya JB Belmonte, Dar es Salaam. Serengeti inatarajiwa kumenyana na Kongo Brazzaville Jumapili, kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika mwakani nchini Morocco.

Katibu wa TFF, Angetile Osiah akizungumza katika hafla ya chakula cha usiku kwa ajili ya kuichangia timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys usiku huu kwenye hoteli ya JB Belmonte, Dar es Salaam.  
Wachezaji na wadau

Kutoka kulia Kocha Mkuu wa Serengeti Jacob Michelsen, Msaidizi wake, Jamhuri Kihwelo na Kamishna Msaidizi wa Polisi, Jamal Rwambow

Nassor bin Slum akizungumza na mchezaji Hussein Twaha

Kutoka kulia Abdallah Bin Kleb, Tenga, Bin Slum na Jaffar Iddi Maganga

Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Serengeti Boys, Kassim Dewji akizungumza kwenye hafla hiyo. Kushoto ni Tenga

Angetile na wachezaji

Wadau

Mwenyekiti wa Kamati ya Vijana, Ahmad 'Msafiri' Mgoyi akiwa na mdau Seyoung Jeong kutoka Korea

Salim Abdallah kulia akiwa na Bin Kleb na Beda Msimbe 

Bin Slum

Kushoto ni Nicky akiwa na Soyoung

Salim akizungumza na CEO wa JB Belmonte, Justus Buguma kushoto
Mwenyekiti wa Azam FC, Said Mohamed akizungumza kuwapa morali vijana 

Mzee Said akisikiliza kwa makini maneno ya vijana

Hussein Twaha akihutubia. hotuba yake ilisisimua sana. Kulia ni Nahodha, Miraj Adam

Mohamed Hussein kushoto akiwa na Farid Mussa

Bin Kleb na Salim

Julio na Michelsen
Hussein Twaha kulia na Peter Manyika 
Julio alitoa hotuba iliyosisimua pia
Evans Aveva kulia na Said Tuliy kushoto

 

BPL: Arsenal yaifumua Spurs Bao 5-2


>>ADEBAYOR afunga Bao, BAADAE ALA KADI NYEKUNDU!!
ADEBAYOR-RED_CARD+++++++++++++++++++++++
RATIBA/MATOKEO:
Jumamosi, Novemba 17, 2012
Arsenal 5 Tottenham Hotspur 2
[SAA 12 Jioni]
Liverpool v Wigan Athletic
Manchester City v Aston Villa
Newcastle United v Swansea City
Queens Park Rangers v Southampton
Reading v Everton
West Bromwich Albion v Chelsea
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Norwich City v Manchester United
+++++++++++++++++++++++
Mchezaji wa zamani wa Arsenal, Emmanuel Adebayor, ambae aliihama Klabu hiyo na kutokomea Manchester City na kisha kuishia Tottenham, leo kwenye Dabi ya London ya Kaskazini, aliiletea Spurs raha pale alipofunga Bao la kwanza katika Dakika ya 10 na Dakika 7 baadae akaishushia Timu yake karaha kubwa alipopewa Kadi Nyekundu kwa rafu mbaya kwa Santi Corzola na kuipa Arsenal mwanya mkubwa kurudisha Bao hilo na kuinyuka Tottenham jumla ya Bao 5-2.
++++++++++++++++++
MAGOLI:
Arsenal 5
Mertesacker 24′ Podolski 42′ Giroud 45′ Cazorla 60′ Walcott 90′
Tottenham 2
Adebayor 10′ Bale 71′
++++++++++++++++++
Ushindi wa leo umeifanya Arsenal ichupe hadi nafasi ya 6 ikiwa na Pointi 19 kwa Mechi 12.
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO Timu za juu:
1 Man United Mechi 11 Pointi 27
2 Man City Mechi 11 Pointi 25
3 Chelsea Mechi 11 Pointi 24
4 Everton Mechi 11 Pointi 20
5 WBA Mechi 11 Pointi 20
6 Arsenal Mechi 12 Pointi 19
7 West Ham Mechi 11 Pointi 18
8 Tottenham Mechi 12 17
+++++++++++++++++++++++
Baada ya Bao la Adebayor na kisha kutolewa kwake, Arsenal ilikuja juu na kufunga Bao 3 kabla Haftaimu kupitia Mertasaker, Podolski na GIrould na Kipindi cha Pili kuongeza nyingine mbili zilizofungwa na Carzola na Walcott.
Bao la pili la Tottenham lilifungwa na Gareth Bale.
VIKOSI:
Arsenal: Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Vermaelen, Wilshere, Arteta, Cazorla, Walcott, Giroud, Podolski
Akiba: Mannone, Andre Santos, Oxlade-Chamberlain, Ramsey, Coquelin, Arshavin, Jenkinson.
Tottenham: Lloris, Walker, Gallas, Vertonghen, Naughton, Lennon, Sandro, Huddlestone, Bale, Adebayor, Defoe
Akiba: Friedel, Dempsey, Dawson, Sigurdsson, Livermore, Townsend, Carroll.
Refa: Howard Webb

LEO NAKULETEA IDADI YA WACHEZAJI 20 WALIOITEKA ULAYA KWA KUZISAIDIA TIMU ZAOUNAFIKIRI NI NANI ZAIDI YA WENZAKE?????????




Kabla ya kuwataja wachezaji bora 20 ambao wameiteka Ulaya, napenda kuthamini mchango wa wachezaji hawa katika timu zao Yaya Toure, Xavi, Mario Gotze, Wayne Rooney, na Hazard. Hawa wamekuwa kwenye viwango bora kabisa msimu huu huku wakiziwezesha timu zao katika kupata matokeo bora.

Frank Ribery (20)

Mfaransa huyu amekuwa akijitolea kila kitu kwa ajili ya klabu yake ya Bayern Munchen. Licha ya matatizo yake ya kugombana na winger mwenzake wa Bayern, Arjen Robben mara kwa mara, Ribbery amekuwa bora mara zote anapoingia ndani ya uwanja. Hivi karibuni Ribbery alikaririwa akisema kwamba anaipenda Bayern kuliko timu ya taifa ya nchi yake, Ufaransa. Ribbery anashika nafasi ya 20 katika viwango hivi.

Edin Dzeko (19)

Amekuwa akitokea pale anapohitajika. Edin Dzeko amekuwa bora zaidi msimu huu hasa pale anapotokea benchi, watu kama Edin huitwa Super Sub. Yeye ndiye mtu ambaye amekuwa akiipa matokeo mazuri Manchester City mara kwa mara pale inapoonekana kushindwa. Huku akiwa na kiatu cha ufungaji bora cha ligi kuu ya Ujerumani pia mchezaji bora wa wachezaji wa ligi kuu ya Ujerumani, Dzeko ameendelea kumuonesha Roberto Mancini yeye ni mchezaji wa aina gani. Dzeko amekuwa wa 19.

Demba Ba (18)

Huu ndio ulikuwa usajili bora wa msimu wa 2011/2012 kulingana na makocha wa timu za ligi kuu ya Uingereza. Baada ya Papiss Cisse kusajiliwa January, 2012, Ba alifunga goli moja tu, tangu msimu huu kuanza imekuwa kinyume chake, Cisse hafungi na Ba amerudi kuwa roho ya timu. Kama akiendelea na kiwango hiki Ba anaweza kuwa mfungaji bora wa ligi kuu ya Uingereza. Ba anashika nafasi ya 18.

Marco Reus (17)

Moja ya vipaji kutoka Ujerumani vinavyokuja kwa kasi ni huyu Marco Reus. Akisajiliwa kutoka Borussia Monchengladbach kuja kuziba pengo la Shinji Kagawa, Marco ameweza kushirikiana vyema na Mjerumani mwenzake, Mario Gotze pia mshambuliaji Lewamdowski katika kuiboresha timu ya Borussia Dortmund. Marco Reus ndiye mchezaji bora wa Ujerumani kwa mwaka huu, 2012. Reus anashika nafasi ya 17.

Thomas Muller (16)

Mchezaji bora kijana wa kombe la dunia, 2010. Baada ya kuwa akitokea benchi msimu uliopita wakati Mario Gomez alipokuwa katika kiwango cha juu. Thomas Muller amekuwa akitengeneza chemistry nzuri na mshambuliaji mwingine wa Bayern Munich, Claudio Pizzaro. Mara nyingi Muller amekuwa hatajwi sana midomoni mwa wapenda kabumbu lakini yeye amaandelea kutunza kiwango chake vyema na sasa yupo kwenye kiwango cha hatari. Amekuwa wa 16.

Klaas-Jan Huntelaar (15)

Wenyewe humwita Hunter, amekuwa akifananishwa na Ruud van Nistelrooy na Marco van Basten kutokana na jinsi anavyouchezea mpira. Kocha wa zamani wa Barcelona Louis van Gaal aliwahi kusema kwamba huyu ndiye mchezaji bora katika dimba la penalti. Tangu ajiunge na Schalke 04 akitokea Milan, Huntelaar amekuwa kwenye kiwango bora na ndiyo mhimili wa Schalke. Hivi sasa ana ushirika mzuri kabisa na Mholanzi mwenzake aitwaye, Ibrahim Affelay. Amekuwa wa 15.

Oscar (14)

Kipaji cha ajabu kutoka Brazil. Uwezo wa kumiliki mpira, nguvu, pasi na jinsi anavyojitoa uwanjani haipingiki kwamba Oscar atakuja kuwa moja ya wachezaji hatari sana katika timu ya taifa ya Brazil. Oscar ndiye mchezaji wa Chelsea anayeng’ara zaidi katika ligi ya mabingwa Ulaya msimu huu kuliko mchezaji yeyote mwingine ndani ya klabu. Goli la pili aliloifunga Juventus katika mechi yake ya kwanza ya ligi ya mabingwa Ulaya halitafutika kirahisi katika vichwa vya wapenzi wengi wa soka. Alipoulizwa atoe maoni yake kuhusiana na goli lile, kipa wa Juventus, Gigi Buffon alisema hivi, “Siwezi kusema ni vizuri kufungwa goli lakini ni vizuri kuwa sehemu ya goli bora kama lile. Hongera kwake”. Oscar ni wa 14.

Maroune Fellaini (13)

Mchezaji ghali zaidi wa klabu ya Everton. Huyu ndiye alikuwa gumzo zaidi wakati ligi ya Uingereza ilipokuwa katika wiki za mwanzo mpaka sasa. Akiwa ni mzaliwa Ubelgiji na asili ya Morocco, Maroune Abdellatif Fellaini amekuwa kiwango bora zaidi msimu huu kuliko msimu mwingine wowote katika maisha yake. Watu wengi wamekuwa wakiifuatilia Everton kwa sababu ya huyu mtu na yeye ndiye ubongo nyuma ya mafanikio ya Everton kwa msimu huu. Anazivutia klabu kubwa nyingi huku Chelsea ikiongoza mbio za kumnyakua, si ajabu kuona akihamia kwenye timu inayoendana na kiwango chake. Amekuwa wa 13.

Gonzalo Higuain (12)

Mtambo wa magoli kutoka mzaliwa wa Ufaransa. Huyu ndiye patna wa Cristiano Ronaldo katika kupasia mipira nyavuni pale Real Madrid kwa sasa. Mafanikio ya Gonzalo msimu huu yamechangiwa zaidi na kuumia na kiwango cha Karim Benzema kushuka. Katika siku za hivi karibuni Higuain amekuwa akishirikiana vyema na Lionel Messi katika kutengeza nafasi za magoli katika timu ya taifa ya Argentina. Amekuwa wa 12.

Luis Suarez (11)

Mchezaji ambaye amekuwa akiandamwa na mikasa ya kutosha tangu adake mpira uliokuwa ukiingia nyavuni katika mechi ya robo fainali ya kombe la Dunia pale Afrika Kusini dhidi ya timu ya Ghana. Pamoja na mikasa mingi kuwa upande wake Luis Suarez hajashuka kiwango na msimu huu tofauti na misimu mingine amekuwa akifunga magoli mengi ingawa timu yake ya Liverpool bado mambo hayajawa mazuri. Ndiye mchezaji anayeng’ara zaidi kwa majogoo wa jiji. Amekuwa wa 11.

Andrea Pirlo (10)

Ule usemi wa ng’ombe hazeeki maini uhalisia wake huonekana hapa. Watumiaji wa mvinyo humfananisha Andrea Pirlo na kinywaji hicho, kadri kinywaji kinavyozidi kukaa ndivyo ubora wake unavyoongezeka. Kadri umri wa Pirlo unavyoongezeka ndivyo kiwango chake kinavyoongezeka. Huyu ndiye chachu hasa ya mafanikio ya Juventus katika kumaliza msimu uliopita bila kufungwa na Italia kufika kwenye fainali ya kombe la Ulaya. Amefunga 10 bora.

Juan Mata (9)

Pamoja na kwamba Didier Drogba ndiye aliyeiwezesha Chelsea kushinda kombe la FA na lile la ligi ya mabingwa Ulaya kwa kiasi kikubwa katika mechi za fainali, Mata ndiye aliyekuwa mchezaji bora wa Chelsea kwa msimu uliopita. Msimu uliopita Mata alikuwa kwenye kiwango bora lakini sasa hivi amekuwa zaidi ya alivyokuwa msimu uliopita. Juan Manuel Mata Garcia anaendelea kuwa mchezaji bora wa Chelsea mpaka sasa. Huyu ndiye mchezaji bora wa ligi ya Uingereza kwa mwezi wa 10, mwaka 2012. Amekuwa wa 9.

Bastian Schweinsteiger (8)


Roho ya timu ya Bayern Munchen, akifunga magoli na kutoa pasi za mwisho za kutosha. Basti kama marafiki zake wanavyomwita ametengeneza chemistry katika timu ya Bayern hasa katika sehemu ya kiungo ya timu. Uwezo mkubwa wa kukota aliokuwa nao, pasi kali ‘zenye macho’ , uwezo mkubwa wa kukaba, uwezo mkubwa wa kumiliki mpira, na mwisho wa yote ni uwezo wake mkubwa wa kupiga mipira iliyokufa unamfanya awe mchezaji wa kipekee. Schweinsteiger ana nafasi kubwa ya kuingia kwenye FIFA FIFPro World XI ya mwaka huu. Amekuwa wa 8.

Andres Iniesta (7)

Mchezaji bora wa Ulaya kwa mwaka 2012, siku zote amekuwa kwenye kiwango bora. Iniesta kwa sasa yupo kwenye kiwango cha juu cha soka katika maisha yake. Yeye ndio mtu anayeng’aa zaidi kwenye timu yenye vipaji lukuki ya Spain. Sababu ya Iniesta kushika namba 7 katika listi hii ni kutokana na makali kupungua kidogo tangu mashindano ya Ulaya kuisha pia ni kutokana na watu waliopo juu yake viwango vyao kuongezeka kwa kiasi kikubwa. Kitu ninachoamini ni kuwa lazima Iniesta atajwe kugombania FIFA Ballon d’Or katika wale watu watatu wa mwisho.

Stephan El Shaarawy (6)

Mashabiki wake humwita ‘The Pharaoh’ kwa sababu amezaliwa na wazazi wenye asili ya Misri pale Savona, Italia. Huyu ndio nguzo ya Milan kwa sasa katika upachikaji mabao baada ya Zlatan Ibrahimovic kuondoka. Akivaa jezi yenye namba ya mwaka aliozaliwa, # 92 (1992), na ikiwa ndio kwanza katimiza miaka 20 juzi tu mwezi October, Firauni huyu amekuwa tishio sana kwa mabeki wa timu pinzani zinazopambana aidha na Italia ama A.C Milan. Nimempa namba 6 kwa sababu anastahili.

Zlatan Ibrahimovic (5)

Mtaalamu huyu mwenye mkanda mweusi wa mchezo wa karate amekuwa mkubwa kuliko ligi ambayo anacheza ndani yake. Tangu kuhama kutoka AC Milan na kutua PSG mambo yamekuwa rahisi sana kwa Ibracadabra. Kutokana na aina yake ya mchezo na kipaji chake watoto wa mjini wanakwambia, Ibra sio wa leo wala kesho wakimaanisha, Zlatan ataendelea kung’aa kwenye medani nzima ya soka kwa kipindi kirefu kidogo mpaka pale atakapoamua kustaafu. Huyu ndiye mfungaji anayeongoza katika ligi kuu ya Ufaransa kwa sasa. Tarehe 14 mwezi huu wa 11, 2012, goli la 4 aliloifunga Uingereza linasemekana kuwa goli la karne. Zlatan Sefik Ibrahimovic ni namba 5.

Radamel Falcao (4)

Ukiwa ni msimu wake wa pili katika ligi kuu ya Spain, Radamel Falcao ameibuka ghafla na kuwa gumzo katika bara lote la Ulaya. Falcao ndio mpinzani mwenye nguvu wa Ronaldo na Messi ambaye alikuwa akinghojewa katika kugombania kiatu cha dhahabu cha ligi kuu ya Spain. Akiwa tayari ameshinda kombe La UEFA akiwa na Porto ya Ureno pamoja Athletico Madrid aliko sasa ambako pia majuzi alishinda UEFA Super Cup pale alipoichabanga Chelsea goli 3 peke yake katika ushindi wa 4-1, Falcao ameendelea kuwa mchezaji wa kutumainiwa katika kila timu anayoitumikia. Falcao anastahili nafasi ya 4.

Robin van Persie (3)

Huyu ndiye mchezaji bora wa ligi kuu ya Uingereza kwa msimu uliopita, 2011/12, huku akiwa hana muda mrefu tangu ajiunge na mashetani wekundu akitokea kwa mahasimu wao wakubwa, Arsenal, RvP amekuwa ndio nguzo katika mashambulizi ya United msimu huu akiwa ameifungia goli 8 tayari na pasi za magoli 3 kwenye ligi kuu, van Persie ameendelea kuwa moja ya nembo za ligi kuu ya Uingereza kwa wakati huu. Hivi karibuni wakati Sir Alex Ferguson alipochaguliwa kuwa kocha bora wa mwezi October alimshukuru Robin kwa kutoa mchango mkubwa sana katika tuzo yake hiyo. Robin van Persie anakuwa wa 3 nyuma ya Ronaldo na Messi.

Cristiano Ronaldo (1)

CR7 kama anavyopenda kujiita. Yeye kaiteka dunia ndani ya uwanja na nje ya uwanja. Cristiano Ronaldo ni moja ya wachezaji adimu sana katika kizazi hiki cha leo. Uwezo wake wa kupasia ‘kamba’ umekua ukiongezeka siku baada ya siku. Ronaldo ndiye mchezaji anayetawala vichwa vya habari vya magazeti kila kukicha pamoja na ‘fundi’ mwingine kutoka Italia aitwaye Super Mario Balotelli. Mtupia mabao huyu ambaye ndio anaongoza magoli katika ligi ya mabingwa Ulaya msimu huu akiwa na goli 5 katika mechi 4 alizocheza amekuwa akisifika kwa bidii yake ya kujituma mazoezini na kwenye mechi. Kutokana na yote haya Cristiano pia anashikilia namba moja pamoja na Leo Messi. Ronaldo ndiye mchezaji bora wa mwaka huu, 2012 wa Goal.com, mtandao wa soka wenye heshima kubwa zaidi.

LIONEL Messi (1)

Ameendeelea kuiteka dunia kutokana na kipaji chake ambacho kinawashangaza wadau wengi wa soka. Huku akishikilia rekodi ya kufunga magoli mengi duniani katika msimu mmoja, magoli 73 katika msimu wa 2011/12 na magoli 76 mpaka sasa kwa mwaka huu akiwa nyuma ya Gerd Muller, urafiki wa Messi na nyavu umezidi kudumishwa siku baada ya siku ikumbukwe kwamba kila goli analofunga Messi kwa hivi sasa ni rekodi katika klabu ya Barcelona kwa sababu yeye ndiye mfungaji bora wa klabu kwa wakati huu. Kwa sasa mchezaji huyu bora wa dunia yuko katika kiwango sawa na mshindani wake wa karibu wa siku zote, Cristiano Ronaldo ndio maana wote wamekuwa vinara kwa kushikilia namba moja.

WENGER: SIJUTII KUMTOSA IBRAHIMOVIC GUNNERS

LONDON, England
'Alikuwa na miaka 16. Nikamuuliza kama yuko tayari kufanya majaribio na kikosi cha wakubwa, akakataa. Je napaswa kujuta katika hilo? Hapana. Kama mtu anakwambia ana ubora unaouhitaji, bila shaka unapaswa kujiridhisha, vinginevyo haiwezekani'
SAA 24 baada ya mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic kufanya kufuru dimbani, Mfaransa anayeinoa Arsenal, Arsene Wenger amesema hajutii kumpoteza mkali huyo wakati alipoenda klabuni Highbury kufanya majaribio akiwa na miaka 16.
Nyota huyo wa klabu ya Paris St German kwa sasa, amepamba vichwa vya habari wiki hii, kutokana na mabao yake yaliyoipa Sweden ushindi wa 4-2 dhidi ya Engalnd, likiwamo moja zuri zaidi kuwahi kufungwa.
Mabao hayo yamefuatiwa na tambo mbalimbalimbali kutoka kwa Ibrahimovic, wengi wakirudi nyuma na kukumbuka kauli yam kali huyo aliyomwambia Wenger wakati alipotua klabuni Highbury mwaka 2000 kuwa 'Yeye sio wa kufanyiwa majaribio.'
Yoso mwingine Cristiano Ronaldo ni kati ya wakali walioonwa na macho ya Wenger, sanjari na mkali wa sasa wa Man City, Yaya Toure aliyekuwa akisakata soka nchini Ubelgiji wakati huo.
Ndipo Ibrahimovic alipojiunga na Ajax, kabla ya kushinda mataji akiwa na AC Milan, Barcelona na Inter, huku akiweka rekodi ya dau la jumla la uhamisho wake kufikia pauni milioni 150. Pia akikumbukwa kwa kuichapa Arsenal mabao matatu na kuing’oa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Na sasa Wenger anafungua kinywa kusema: 'Alikuwa hapa kwa majaribio na kisha amkaenda zake sehemu nyingine. Hilo limetokea kwa wachezaji wengine: Ronaldo, Ibrahimovic. Habari hiyo ni kweli kwamba nilihitaji kumuona, lakini sikuwa namfahamu.
'Alikuwa na umri wa miaka 16. Nikamuuliza kama yuko tayari kufanya majaribio kidogo na kikosi cha wakubwa, akakataa kufanya hivyo.
'Je napaswa kujuta katika hilo? Hapana. Kama mtu anakwambia kuwa yeye ana ubora unaouhitaji, bila shaka unapaswa kujiridhisha binafsi kwa kumuangalia, vinginevyo haiwezekani.'
Nyota ya Ibrahimovic kwa sasa ni angavu mno, kutokana na alichofanya katika ushindi huo wa mechi ya kirafiki, zaidi likiwa ni bao lake la mwisho katika dakika ya 90+1 alilopiga ‘tik-tak’ akiwa umbali wa mita 30 na kufunga.

JEZI YA IBRAHIMOVIC KUMTAJIRISHA DANNY WELBECK


MANCHESTER, England
“Welbeck amekalia bahati ya aina yake. Jezi aliyonayo inaweza kumpatia riba kubwa mno mnadani kwa sababu ya aina ya mabao mazuri, mtu aliyeivaa na kufunga na ukweli kuwa mabao hayo amefunga dhidi ya timu ya taifa ya England – tena katika uwanja mpya kabisa. Kama anaiweka mnadani hivi sasa, anaweza kupata hadi pauni 30,000”
YOSO wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya England, Danny Welbeck, ametakiwa kuiweka sokoni jezi aliyobadilishana na Zlatan Ibrahimovic na inaweza kumpatia hadi kiasi cha pauni 30,000.
Welbeck mmoja wa wakali chipukizi katika klabu yake na timu ya taifa, alibadilishana jezi na Ibrahimovic, baada ya kumalizika kwa pambano la kirafiki baina ya Sweden na England, ambapo Ibra alifunga mabao yote ya Sweden.
Ibra alichagiza mabao yake matatu katika mechi hiyo kwa kufunga la nne mwishoni mwa mchezo, bao lililotajwa kuwa bora zaidi na kwamba jezi aliyofungia bao hilo inaweza kuuzwa na kununuliwa hadi kwa pauni 30,000 kama itawekwa mnadani.....
Tom Rollett wa kampuni ya Exclusive Memorabilia alisema: “Welbeck amekalia bahati ya aina yake.
“Jezi aliyonayo inaweza kumpatia riba kubwa mno mnadani kwa sababu ya aina ya mabao mazuri, mtu aliyeivaa na kufunga na ukweli kuwa mabao hayo amefunga dhidi ya timu ya taifa ya England – tena katikia uwanja mpya kabisa.
“Kama anaiweka mnadani hivi sasa ambapo kila kona gumzo ni Ibrahimovic na mabao yake, dau la juu kabisa linaweza kuwa hadi pauni 30,000.”
Welbeck alijikuta akipata jezi hiyo baada ya wachezaji kama Ryan Shawcross, Joe Hart na Jack Wilshere kupita na kupeana mikono na nyota huyo wa PSG.
Beki wa klabu ya West Brom, raia wa Sweden Jonas Olsson kwa upande wake alipewa viatu vya Ibrahimovic baada ya pambano hilo, na ametangaza kuviweka mnadani ili kukusanya pesa za kutunisha mfuko wa hisani kwa watoto wanaozaliwa mapema ‘njiti.’
Licha ya habari njema hizi kwa Welbeck, imedaiwa kuwa kamwe jezi hiyo ya Ibrahimovic haiwezi kufikia thamani ya ile ya Diego Maradona katika fainali za Kombe la Dunia la mwaka 1986 alipofunga ‘Bao la Mkono wa Mungu’ dhidi ya England.
Jezi ya Maradona kwa sasa iko chini ya umiliki wa nyota wa zamani wa klabu za Spurs na Aston Villa, Steve Hodge, ambapo iko ndani ya Makumbusho ya Taifa ya Soka jijini Manchester. 
Hodge, ambaye alikabidhiwa jezi hiyo na Muargentina huyo mwishoni mwa mchezo alisema: “Sidhani kama jezi ya Ibrahimovic inaweza kuwa na thamani kubwa kuliko ile ninayoimiliki aliyonipa Maradona.”

BPL: NI DABI Emirates, Man United ugenini na Norwich, City nyumbani na Villa!


WENGER_AHIMIZA12Mechi ya kwanza kabisa ya Ligi Kuu England, BPL, Jumamosi ni DABI ya London ya Kaskazini Uwanjani Emirates kati ya Arsenal na Tottenham na baadae vinara Manchester United watashuka Carrow Road kucheza na Norwich City, huko Etihad, Manchester City watacheza na Aston Villa wakati Chelsea wapo ugenini kuivaa West Bromwich Albion katika Mechi inayomkutanisha Meneja aliefukuzwa WBA, Roberto Di Matteo, na aliewahi kuwa Meneja Msaidizi wa Chelsea, Steve Clarke, ambae sasa yupo WBA kama Meneja.
IFUATAYO ni TAHMINI FUPI kwa Mechi hizo:
+++++++++++++++++++++++ 
MSIMAMO Timu za juu: 
1 Man United Mechi 11 Pointi 27
2 Man City Mechi 11 Pointi 25
3 Chelsea Mechi 11 Pointi 24
4 Everton Mechi 11 Pointi 20
5 WBA Mechi 11 Pointi 20
6 West Ham Mechi 11 Pointi 18
7 Tottenham Mechi 11 17
8 Arsenal Mechi 11 Pointi 16
+++++++++++++++++++++++ 
ARSENAL V TOTTENHAM
Arsenal
MENEJA Arsene Wenger: “Katika Dabi za London ya Kaskazini, Siku zote unapata Magoli na Mechi za kusisimua!”
WACHEZAJI: Kuna hatihati kuhusu hali za Olivier Giroud, Theo Walcott, Mikel Arteta na Bacary Sagna kwa kuwa wana maumivu lakini Kipa Wojciech Szczesny huenda akarudi dimbani.
Kiungo Jack Wilshere anarejea tena baada ya kutumikia Kifungo cha Mechi moja kufuatia Kadi Nyekundu aliyopewa kwenye Mechi na Manchester United.
Majeruhi ambao hawatacheza ni Gervinho (enka), Kieran Gibbs (paja), Abou Diaby (paja) na Tomas Rosicky (paja).
KIKOSI KITATOKANA NA: Szczesny, Sagna, Vermaelen, Mertesacker, Santos, Wilshere, Cazorla, Arteta, Coquelin, Podolski, Walcott, Giroud, Mannone, Djourou, Jenkinson, Chamakh, Arshavin, Koscielny, Oxlade-Chamberlain, Ramsey.
TOTTENHAM HOTSPUR
MENEJA Andre Villas-Boas: “Timu zote hazipo zinapotaka kuwepo…lakini wote wameonyesha wanaweza kufanya vizuri zaidi! Ni mapema bado kwenye Ligi!”
WACHEZAJI: Mousa Dembele yupo nje akiuguza musuli za Pajani.
Majeruhi wa muda mrefu ni Scott Parker (Kifundo cha Mguu), Benoit Assou-Ekotto na Younes Kaboul (Wote matatizo ya Goti).
KIKOSI KITATOKANA NA: Friedel, Lloris, Gomes, Cudicini, Walker, Naughton, Gallas, Caulker, Dawson, Vertonghen, Lennon, Sigurdsson, Townsend, Falque, Carroll, Mason, Livermore, Sandro, Huddlestone, Bale, Dempsey, Adebayor, Defoe.
Refa: Howard Webb
MAN CITY V ASTON VILLA
Manchester City
MENEJA Roberto Mancini: "Tuna Timu nzuri na hatuhitaji kununua Mchezaji mwingine Januari"
WACHEZAJI: Kipo Kikosi kamili.
KIKOSI KITATOKANA NA: Hart, Pantilimon, Zabaleta, Maicon, Kompany, Lescott, Nastasic, K Toure, Kolarov, Clichy, Nasri, Milner, Yaya Toure, Barry, Garcia, Silva, Sinclair, Aguero, Tevez, Dzeko, Balotelli, Razak.
Aston Villa
MENEJA Paul Lambert: “Tunajiamini, tutajaribu kushinda!”
WACHEZAJI: Majeruhi ni Darren Bent, Chris Herd, Richard Dunne, Charles N'Zogbia na Joe Bennett..
KIKOSI KITATOKANA NA: Guzan, Given, Lowton, Clark, Vlaar, Lichaj, Baker, Stevens, Herd, Ireland, El Ahmadi, Westwood, Bannan, Delph, Holman, Agbonlahor, Benteke, Bowery, Weimann, Burke, Johnson, Williams.
Ref: J Moss
NORWICH CITY V MAN UNITED
CHICHARITO_SHANGILIANorwich City
MENEJA Chris Hughton: "Lazima tutafute kila uwezekano ili tushinde!"
WACHEZAJI: Beki Russell Martin na Harry Kane ndio majeruhi pekee.
KIKOSI KITATOKANA NA: Ruddy, Whittaker, Turner, Bassong, Garrido, Tettey, Johnson, Hoolahan, Pilkington, Snodgrass, Holt, Bunn, E Bennett, Howson, Jackson, Tierney, R Bennett, Morison.
Manchester United
MENEJA Sir Alex Ferguson: “Hatuwezi kila mara kutegemea tutatoka nyuma Bao 2-0 na kushinda!”
WACHEZAJI: Kuna hatihati kuhusu kuwepo Wachezaji wenye maumivu Wayne Rooney na Jonny Evans.
KIKOSI KITATOKANA NA: De Gea, Lindegaard, Rafael, Ferdinand, Evans, Smalling, Evra, Buttner, Valencia, Carrick, Fletcher, Cleverley, Powell, Scholes, Anderson, Carrick, Giggs, Young, Welbeck, Van Persie, Rooney, Hernandez.
Refa: A Taylor.
WBA V CHELSEA
West Bromwich Albion
MENEJA Steve Clarke: "Mashabiki wanasikia raha kwa vile tunacheza vizuri na kila Wiki tunaonekana wazuri na kuonyesha uwezo wa kushinda!"CHELSEA-MANCINI_n_TORRES
Steve Clarke aliwahi kuwa Meneja Msaidizi Klabuni Chelsea.
WACHEZAJI: Kipa Boaz Myhill atacheza badala ya Nambari Wani Ben Foster ambae ni majeruhi.
Romelu Lukaku haruhusiwi kucheza kwa vile yuko kwa Mkopo WBA kutoka Chelsea.
KIKOSI KITATOKANA NA: Myhill, Daniels, Jones, McAuley, Olsson, Tamas, Dawson, Jara Reyes, Popov, Ridgewell, Mulumbu, Yacob, Brunt Dorrans, Morrison, El Ghanassy, Gera, Fortune, Odemwingie, Long, Rosenberg.
Chelsea
MENEJA Roberto Di Matteo: "Kutimuliwa kama Meneja inamtokea kila Mtu na inakufanya uimarike zaidi na haimaanishi wewe ni Meneja mbovu!"
Di Matteo alikuwa Meneja wa WBA kuanzia Mwaka 2009 na kutimuliwa Mwaka 2011.
WACHEZAJI: Ashley Cole anaweza kurudi baada ya kupona maumivu yake lakini John Terry (goti) na Frank Lampard (Musuli ya mguu) wako nje.
KIKOSI KITATOKANA NA: Cech, Ivanovic, Azpilicueta, Luiz, Cahill, Cole, Bertrand, Mikel, Romeu, Ramires, Mata, Oscar, Hazard, Moses, Marin, Torres, Sturridge, Turnbull.
Refa: M Oliver 
+++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumamosi, Novemba 17, 2012
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Arsenal v Tottenham Hotspur
[SAA 12 Jioni]
Liverpool v Wigan Athletic
Manchester City v Aston Villa
Newcastle United v Swansea City
Queens Park Rangers v Southampton
Reading v Everton
West Bromwich Albion v Chelsea
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Norwich City v Manchester United
Jumapili, Novemba 18, 2012
[SAA 1 Usiku]
Fulham v Sunderland
Jumatatu, Novemba 19, 2012
[SAA 5 Usiku]
WestHam v Stoke City


RONALDO AKIRI KUM-MISS FERGUSON.

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo amekiri kuwa amemkumbuka meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson na kumuelezea kuwa kama baba yake katika soka. Ronaldo mwenye umri wa miaka 27 kwasasa anacheza chini ya Jose Mourinho baada ya uhamisho uliovunja rekodi wakati akiondoka Old Traford ambao ulifikia euro milioni 100. Pamoja na kushinda taji la La Liga msimu uliopita na kufunga mabao 46 katika michezo 38 ya ligi hiyo Ronaldo ambaye ni raia wa Ureno aliweka wazi kuwa bado ni mshabiki mkubwa wa Ferguson pamoja na na kuondoka United miaka mitatu iliyopita. Ronaldo alimsifu kocha huyo kwa kumfundisha mambo mengi na kumfanya kuwa mchezaji bora kama alivyosasa hivyo anamuona kama baba yake katika soka ndio hawezi kuacha kumkumbuka Ferguson. Pamoja na umri wa miaka 71 aliokuwa nao Ferguson lakini Ronaldo anaamini kuwa kocha huyo bado ana vitu vingi vya kuisaidia United ili iweze kupata mafanikio zaidi.

ABO TRIKA KUTUNDIKA DARUGA BAADA YA CHAMPIONS LEAGUE.

KOCHA wa zamani wa timu ya Taifa ya Misri, Hassan Shehata ameweka wazi kuwa nahodha wa timu ya Al Ahly Mohammed Abo Trika atastaafu rasmi kucheza soka baada ya fainali za michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika. Shehata ambaye kwasasa anafundisha katika klabu ya Al Arabi ya Qatar amesema kuwa alizungumza na Trika aliyemuomba ushauri kuhusiana na uamuzi wake wa kustaafu. Kocha huyo ambaye alianza kufanya kazi na Trika wakati alipopewa mikoba ya kuinoa timu ya taifa ya Misri aliendelea kusema kuwa pamoja na kujaribu kumshawishi nyota huyo aachane na maamuzi ya kustaafu ilishindikana. Shehata amesema anaamini mchezaji bado ana uwezo wa kucheza miaka mingine miwili au mitatu kabla ya kustaafu lakini anadhani hilo halitawezekana kutokana na mchezaji huyo kutotaka kubadilisha msimamo wake. Shehata ambaye anajulikana kama Godfather aliomba bodi ya Al Ahly kujaribu kumshawishi nyota huyo mwenye umri wa miaka 34 ili abakie kwa miaka mingine kadhaa katika ulimwengu wa soka.

MADEREVA WA LANGALANGA WASIFU BARABARA ZA AUSTIN, TEXAS.

MADEREVA wa mashindano ya magari yaendayo kasi ya Langalanga wamesifu barabara za Austin, Texas ambako kunafanyika mashindano ya Grand Prix ya Marekani. Dereva wa McLaren ambaye msimu ujao anahamia Marcedes, Lewis Hamilton alisifu barabara hizo ambazo zimejengwa katika siku za karibuni na hayo yakiwa mashindano yake ya kwanza. Madereva wengine waliosifia barabara hizo ni Jenson Button ambaye wanatoka timu moja na Hamilton akidai kuwa unaweza kukimbia kwa kasi na kukata kona ukiwa katika kasi kubwa bila kuteleza kitu ambacho kwenye barabara nyingine huwezi kufanya. Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi leo ambapo Sebastian Vettel wa timu ya Red Bull anatarajiwa kuongoza mbio hizo baada ya kufanikiwa kuendesha kwa kasi zaidi katika mbio za majarabio.

TAARIFA KUTOKA TFF LEO.

Katika kikao chake cha tarehe 3 Novemba 2012, Kamati ya Utendaji ya TFF ilipokea taarifa ya mapendekezo ya marekebisho ya Katiba TFF kama ifuatavyo:
Kuingiza kipengele kinachohusu “Club Lincencing” kama ilivyoagizwa na CAF katika waraka wake unaowataka wanachama wote wa CAF, ikiwemo TFF, kuhakikisha kuwa kipengele hicho kinaingizwa katika katiba zao. Kutokana na ushauri na maagizo ya FIFA, TFF inatakiwa kuunda wa Kamati ya Rufaa ya Uchanguzi (“Elections Appeals Committee”) na kuondokana na utaratibu tulionao hivi sasa ambao Kamati ya Rufaa (“Appeals Committee”) inajigeuza na kuwa Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi wakati wa mchakato wa uchaguzi wa TFF. Kuindoa nafasi ya Makamu wa Pili wa TFF pamoja na kutamka kuwa Wawakilishi wa klabu za Ligi Kuu katika Kamati ya Utendaji watachaguliwa moja kwa moja na klabu zenyewe. Hii inatokana na azimio la Mkutano Mkuu uliopita la kuruhusu uundwaji wa chombo huru cha kusimamia Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza pamoja na kupitishwa kwa Kanuni zinazokiongoza chombo hicho kama zilivyopendekezwa na klabu za Ligi Kuu na kupitishwa na Kamati ya Utendaji.
Baada ya kutafakari mapendekezo hayo, Kamati ya Utendaji ya TFF iliamua kuwa:
Ipo haja ya kuifanyia marekebisho Katiba ya TFF kama iliyopendekezwa. Kwa vile mapendekezo mawili kati ya matatu ya ya marekebisho ya Katiba yana uhusiano na Uchaguzi Mkuu wa TFF, ipo haja ya marekebisho hayo kufanyika kabla ya kutangazwa kwa Mkutano Mkuu wa TFF na kuanza kwa mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa TFF. Aidha, kwa vile TFF haina uwezo wa kuitisha mikutano mikuu miwili – Mkutano Mkuu Maalum kwa ajili ya marekebisho ya Katiba ya TFF; na Mkutano Mkuu wa Uchaguzi – katika kipindi kifupi kijacho, marekebisho ya Katiba yafanywe kwa njia ya Waraka (“Circular Resolution”).
Waraka huo (“Circular Resolution”) uwe umeshatayarishwa na Sekretariati ikishirikiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria ifikapo tarehe 15 Novemba 2012 na ukabidhiwe kwa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji wanaowakilisha Kanda za TFF ambao watahakikisha kuwa kila Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Kanda husika anapata fursa ya kutoa ridhaa yake.
Zoezi la kupata ridhaa ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu liwe limemalizika katika kipindi cha siku 21. Kikao kinachofuata cha Kamati ya Utendaji kitafanyika Jumamosi tarehe 15 Desemba 2012 kwa madhumuni ya kupokea taarifa ya zoezi hili na kufanya matayarisho ya Mkutano Mkuu. Katiba ya TFF inaelekeza kuwa taarifa ya Mkutano Mkuu itolewe kwa wanachama wake angalau siku 60 (“notice period”) kabla ya Mkutano. Hivyo Kamati ya utendaji inatarajia kuwa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi utafanyika Jumamosi na Jumapili ya tarehe 16 na 17 na Februari 2013. Kamati ya Utendaji ya TFF inasisitiza kuwa utaratibu huu umeamuliwa kutokana na TFF kutokuwa na uwezo wa kifedha wa kutayarisha mikutano mikuu miwili katika kipindi kifupi kijacho. Kinyume chake ni kuchelewa zaidi kufanyika kwa Mkutano Mkuu, jambo ambalo hatuna budi kuliepuka. Kamati ya Utendaji ya TFF inatarajia kupata ushirikiano wa karibu kutoka kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na wadau wa mpira wa miguu kwa jumla ili kufanikisha zoezi hili na hatimaye kufanikisha Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa TFF.

BARCELONA KUVAA QATAR AIRWAYS MSIMU UJAO.

KLABU ya Barcelona ya nchini Hispania inatarajia kubadilisha wadhamini wa jezi zao msimu ujao na kuvaa jezi za Qatar Airways kama mdhamini wao rasmi wa jezi zao. Nembo hiyo ya shirika la ndege itachukua nafasi ya Qatar Foundation nembo ambao ndio inayoonekana katika fulana zao msimu huu. 
Mabadiliko hayo ni sehemu ya makubaliano ya udhamini yenye utata ambayo yalisainiwa na Kampuni ya Michezo ya Uwekezaji ya Qatar-QSI mwaka uliopita. Barcelona ilisaini mkataba huo ambao kwa kipindi hicho ndio ulikuwa mkataba wenye faida kubwa katika mchezo wa soka ambao ulikuwa na thamani ya euro milioni 30 kwa mwaka pamoja na kuitangaza nchi hiyo ambayo itakuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2022. Kabla ya kuvaa jezi zenye nembo ya Qatar Foundation Barcelona walikuwa wakivaa nembo ya Shirika la Umoja wa Mataifa linalishughulika na masuala ya watoto-UNICEF ambapo kwasasa nembo hiyo imehamishwa kwa nyuma ya jezi za klabu hiyo. Barcelona walikuwa wakiwalipa UNICEF euro milioni 1.5 kwa mwaka kwa kutumia jina hilo kwenye jezi zao.

PUYOL FITI KUIKABILI ZARAGOZA.

NAHODHA wa klabu ya Barcelona, Carles Puyol anatarajiwa kurejea uwanjani ikiwa ni siku 45 zimepita toka alipoumia kiwiko cha mkono wake wa kulia. Puyol mwenye umri wa miaka 34 anarejea wakati ambapo timu hiyo iitakuwa wageni wa Real Zaragoza katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Hipania maarufu kama La Liga na uwepo unatarajia kuimarisha safu ya ulinzi ambayo imekuwa ikiyumba kwa kuwakosa nyota wake. Beki mwingine nyota wa timu hiyo Gerard Pique naye alirejea uwanjani wiki iliyopita baada ya kuwa nje kwa wiki saba akisumbuliwa na majeraha ya mguu. Msimu uliopita Barcelona iliruhusu nyavu zake kutikiswa mara 29 pekee katika michezo 38 ya La Liga waliyocheza na kumaliza katika nafasi ya pili mbele ya Real Madrid lakini msimu huu tayari wameshakubali kufungwa mabao 14 katika michezo 11 pekee waliyocheza.