Sunday, October 21, 2012

 

  KAMATI YA UCHAGUZI MKOA WA TABORA YACHAGUA VIONGOZI WATAKAOONGOZA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU WILAYA YA TABORA MJINI KWA MIAKA MINNE IJAYO

 

NA TANO JUMA

Uchaguzi wa viongozi ngazi ya wailaya leo umefanyika katika shule ya msingi Gongoni mkoani tabora kuchagua viongozi watakaowakilisha ngazi ya TFF wilaya TUFA kwa kipindi cha miaka minne ijayo.

 

 

Katika uchaguzi huo uliosimamiwa na mwenyekiti mwanadada Maimuna Abbas kiloga,,katibu Osward Moris na Adamu Fundikira na mjumbe Dioniz john .na ngazi zilizokuwa zinagombewa ni Mwenyekiti,,katibumkuu,katibu msaidizi,Mweka hazina ,mweka hazina msaidizi,Mwakilishi wa vilabu ,Nafasi ya wajumbe wa mkutano mkuu,,pamoja na kamati tendaji ya wilaya.

 

 Kwa upande wa mwenyekiti iliwakilishwa na mgombea mmoja naye ni ABDUL MOHAMED AMAN ambaye alichaguliwa kwa kura 32 za ndiyo na za hapana ni 33 kwa hiyo nafasi ipo wazi kutokana na kura kutokidhi kiwango na kamati imeridhia itakaa na kujadili nafasi hiyo itagombewa upya.

 

 Katika nafasi ya katibu mkuu iligombewa na mtu mmoja naye ni JUMA H. MAPUNDA ambaye alipatiwa kura 46 na kutetea nafasi yake kwa mara ya pili na nafasi ya katibu msaidizi iligombewa pia na mtu mmoja naye ni YASSIN KAYUGO ambaye alipita kwa kura za ndiyo 46 na za hapana 17.

 

 

Nafasi ya mweka hazina ilikuwa na mgombea mmoja ambaye ni MAURID AMIRI SANSA ambaye alipigiwa kura za ndiyo 27 na za hapana 35 kwa hiyo nafasi imeachwa wazi itagombewa upya kutokana na mgombea kutofikisha idadi ya kura zilizokuwa zimepangwa,,na nafasi ya MWEKA HAZINA MSAIDIZI iligombewa na ALLY MAULID KABAKA ambaye alishinda kwa kura 44 alizopigiwa.

 

Na katika nafasi ya wawakilishi wa vilabu iligombewa na watu wawili ambao ni ERASTO D MAPUNDA,NA MILAMBO KAMILI YUSUF na milambo kamili aliibuka na ushindi wa kura 39 na mpinzani wake alipata kura 23.

 

Na nafasi ya wajumbe wa mkutano mkuu  ilikuwa na wagombea wawili ambao ni JUMA SABURI na ANDREW ZOMA  na wajumbe waliokuwa wanapiga kura walimchagua andrew zoma kuwa mshindi kwa kumpigia kura 46 zilizosababisha kushinda na mpinzani wake alipigiwa kura 14 tu.

 

Na nafasi ya  kamati ya utendaji ngazi ya wilaya walichaguliwa BARAKA HAMISI SIMBA,JOACKIM ERENEST HELA HELA,na HASSAN S HASSAN ambao walipigiwa kura za ndiyo wote kwani wagombea waliokuwa wanahitajika katika nafasi hiyo ilikuwa inahitaji wagombea watatu na waliogombea walikuwa watatu hivyo wajumbe wakaamua kupiga kura za ndiyo kwa wote.

 

Wajumbe waliojitokeza wameonesha ni jinsi gani walivyo na imani kubwa kwa viongozi waliowachagua lakini wanachangamoto kubwa kutokana na chama kuwa na ukata wa fedha ambao umesomwa kuwa na jumla ya akaunti ya fedha shilingi elfu 84,700 tu.

 

 

SIMBA WAJENGA MAZOEA NA DROO, WATOKA 0-0 NA MGAMBO MKWAKWANI

Simba SC

SIMBA SC imelazimishwa sare ya tatu mfululizo jioni hii kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, baada ya kutoka 0-0 na wenyeji Mgambo Shooting katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Matokeo hayo, yanaifanya Simba ifikishe pointi 19, baada ya kucheza mechi tisa na kuendelea kuongoza Ligi Kuu, ingawa wameuweka rehani usukani wa ligi hiyo kwa Azam ambayo Jumatano inacheza na Ruvu Shooting Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.
Azam yenye pointi 17, ikishinda itafikisha pointi 20 na kupanda kileleni, tena ikiwa nyuma kwa mchezo mmoja, kwani hadi sasa imecheza mechi saba. Yanga iliyocheza mechi nane, ina pointi 14 katika nafasi ya tatu.
Katika mechi hiyo iliyochezeshwa na refa Athumani Lazi wa Morogoro, dakika 45 za kwanza, timu zote zilishambuliana kwa zamu na zilionyesha kiwango kizuri, ushindani mkubwa- kwa ujumla ilikuwa burudani.
Kipindi cha pili kadhalika pamoja na kocha Mserbia, Profesa Milovan Cirkovick kufanya mabadiliko akiwatoa Mrisho Ngassa na Amri Kiemba na kuwaingiza Edward Christopher na Salim Kinje, bado walishindwa kuifunga Mgambo iliyopanda Ligi Kuu msimu.
Katika dakika 10 za mwisho, ilishuhudiwa Mgambo wakicheza kwa kujihami zaidi kutokana na presha kali ya mashambulizi ya Simba SC.
Katika mechi hiyo, kikosi cha Mgambo kilikuwa; Godson Mmasa, Yassin Awadh, Salum Mlima, Bakari Mtama, Salum Kipanga, Ramadhani Malima, Chande Magoja/Nassor Gumbo dk85, Mussa Ngunda, Issa Kandulu, Fully Mganga na Juma Mwinyimvua.
Simba SC;Juma Kaseja, Nassor Masoud ‘Chollo’, Amir Maftah, Hassan Hatibu, Paschal Ochieng, Jonas Mkude, Amri Kiemba/Salim Kinje dk88, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Emmanuel Okwi na Mrisho Ngassa/Edward Christopher dk 79.
Katika mechi nyingine leo, JKT Ruvu imetoka sare ya 1-1 na JKT Oljoro Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam na Prisons imeifunga Toto Africans 1-0 kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

 

 

TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF LEO.


KAMATI YA LIGI YAIONYA AFRICAN LYON
 

Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeipa onyo kali timu ya African Lyon kutokana na washabiki wake kuweka bango lililoandikwa ‘We believe in 0777’ kwenye mechi yake dhidi ya Azam iliyochezwa Oktoba 6 mwaka huu Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.
 Bango hilo ambalo si la mdhamini wa Ligi Kuu ya Vodacom halitakiwi kuonekana tena kwenye mechi ambazo African Lyon inacheza vinginevyo Kamati ya Ligi itachukua hatua kali dhidi ya timu hiyo.
 Kamati ya Ligi imezikumbusha timu zote zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom kuzingatia kanuni zinazotawala ligi hiyo ili iweze kuendeshwa kwa ufanisi.

 



PAMBANO LA YANGA, RUVU SHOOTING LAINGIZA MIL 47/-
 
 

Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Ruvu Shooting lililochezwa jana (Oktoba 20 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa wenyeji Yanga kushinda mabao 3-2 limeingiza sh. 47,615,000. 


Watazamaji 8,233 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000, na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 8,420,578.47 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 7,263,305.08. 



Mgawo mwingine wa mapato hayo ni posho ya msimamizi wa kituo sh. 120,000, kamishna wa mechi sh. 203,000, waamuzi sh. 381,000, mwamuzi wa akiba sh. 70,000, usafi na ulinzi wa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (stadium technical support) sh. 2,000,000. 


Umeme sh. 300,000, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000, ulinzi wa mechi sh. 3,500,000 wakati tiketi ni sh. 2,959,100. Gharama za mchezo sh. 2,806,859.49, uwanja sh. 2,806,859.49, Kamati ya Ligi sh. 2,806,859.49, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,684,115.69 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,122,743.80.

Tegete na Baraka Jaffari

Tegete akimpiga tobo beki wa Ruvu, Ibrahim Shaaban, kulia ni George Assey

Haruna Niyinzima akiteseka katikati ya viungo wa Ruvu

David Luhende akipambana na wachezaji wa Ruvu

Bao...Seif Abdallah akiinuka kushangilia, huku Yaw Berko akigalagala...hili lilikuwa bao la kwanza 

Juma Abdul aliyeruka juu kupiga mpira kichwa mbele ya mshambuliaji wa Ruvu, Abrahaman Mussa

Tegete na Baraka jaffari

Tegete na Baraka jaffari

Ruvu wakishangilia bao la pili

Niyonzima akimgeuza mchezaji wa Ruvu

Bao...Ruvu wamefunga

Ruvu baada ya kufunga  bao la pili

Yaw Berko akiruka bila mafanikio, mpira unatinga nyavuni 

Nurdin Bakari akikosa bao la wazi

Makocha wa Yanga, Brandts na Msaidizi wake, Minziro

Shamte Ally na Nizar Khalfan benchi

Athumani Iddi 'Chuji' na Hamisi Kiiza benchi 

Ruvu wakiomba dua kabla ya mechi

11 wa Yanga walioanza

11 wa Ruvu walioanza 

Kipa wa Ruvu Benjamin Haule akipangua shuti la mpira wa adhabu la Mbuyu Twite

Hamisi Kiiza akimghasi kipa Benjamin Haule

Kiiza akishughulika

Benjamin Haule akitibiwa na daktari wa Ruvu, Simon Sugule baada ya kuumia

David Luhende akidhibitiwa na beki wa Ruvu

Kavumbangtu chini ya ulinzi

Bao la mpira wa adhabu la Twite

Tegete akiondoka  na mpira baada ya Twite kufunga

Rashid Gumbo akienda chini baada ya kukwatuliwa na Ernest wa Ruvu

 

 

YANGA YAKABIDHIWA NEMBO WALIZOCHAGUA NA KAMPUNI YA SIMU ZA MKONO VODACOM

 Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Laurence Mwalusako (kati) akipokea jezi walizokabidhiwa na Vodacom zikiwa na doa jeusi kutoka kwa Meneja Mahusiano ya Nje wa kampuni ya Sima za mkononi VODACOM, Salum Mwalimu (kushoto). Kulia ni Ofisa Udhamini wa kampuni hiyo, Ibrahim Kaude


Meneja Mahusiano ya Nje wa kampuni ya Sima za mkononi VODACOM, Salum Mwalimu akionesha jezi walizokabidhi kwa klabu ya Yanga zikiwa na doa jeusi.

 

 

 

HATIMAYE SERENGETI YAINGIA KAMBINI, TFF YAIWEKEA MIKAKATI MIZITO IFUZU AFRIKA


KIKOSI cha wachezaji 25 wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys kimeingia kambini leo mjini Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi ya raundi ya mwisho ya michuano ya Afrika kwa vijana.


Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura amezungumza  leo kwamba, Serengeti Boys ambayo iko chini ya Kocha Mdenmark, Jakob Michelsen itacheza mechi hiyo ya raundi ya tatu na mshindi kati ya Congo Brazzaville na Zimbabwe ambapo tayari Congo Brazzaville imefanikiwa kupata ushindi wa ugenini wa mabao 2-1. 


Mechi ya marudiano itachezwa jijini Brazzaville kati ya Oktoba 26-28 mwaka huu.
Katika mechi hiyo ya raundi ya tatu, Serengeti Boys itaanzia nyumbani katika mchezo utakaofanyika Novemba 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, wakati mechi ya marudiano itachezwa wiki mbili baadaye.


Wambura amesema TFF ipo katika mikakati ya kuhakikisha Serengeti Boys inapata mechi mbili za kirafiki za kimataifa kabla ya kumvaa mshindi kati ya Congo Brazzaville na Zimbabwe. Fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 zitafanyika Machi mwakani nchini Morocco.


Tanzania imefuzu bila jasho hadi kufika hatua hiyo, baada ya wapinzani wake wa awali, Kenya na Misri kujitoa katika Raundi ya Kwanza na ya Pili.


Kama Tanzania itafuzu kushiriki Fainali hizo za mwakani, itapoza machungu ya mwaka 2005 walipofuzu kucheza Fainali za Vijana wa umri huo kwa kuzitoa Rwanda, Zambia na Zimbabwe, lakini baadaye kwa sababu ya ‘kufoji’ umri wa Nurdin Bakari, ikaondolewa mashindanoni.


Zaidi ya Fainali za Mataifa ya Afrika 1980 na CHAN 2009, katika soka ya wanaume, Tanzania haijashiriki fainali nyingine zozote za Afrika tangu iingie kwenye soka ya kimataifa.

 

 

Francis Cheka KUKUNG'UTANA MDEUTSCHELAND



Mpambano unaosubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wa ngumi nchini Tanzania na Ujerumani kati ya Francis Cheka na Benjamin Simon wa Ujerumani sasa utafanyika tarehe 18 November katika ukumbi wa Universal jijini Berlin nchini Ujerumani. 
 
Awali mpambano huo ulikuwa ufanyike tarehe 17 November jijini Berlin, Ujerumani na tayari bondia Francis Cheka ameshasaini mkataba wa kukutana na mbabe huyo wa Ujerumani anayejulikana kwa jina la “Iron Ben” kwa ajili ya ukali wa makonde yanayowasulubu wapinzania wake.


Bondia Benjamin Simon ana rekodi ya mapambano 24 ambapo amepoteza pambano moja wakati bondia Francis Cheka ana rekodi ya mapambano 33 amepoteza mapambano 6.


Akimwandikia “Eva Rolle” wa kampuni ya “Primetime Event Management” ya Ujerumani ambaye ndiye promoter wa mpambano huo, mwenyekiti wa ubingwa wa IBF/USBA Lindsey Tucker alimfahamisha kuwa Rais wa IBF/USBA Daryl Peoples au yeye mwenyewe Lindsey Tucker watawasiliana na mama huyo kuhusu maofisa watakaosimamia mpambano huo.
 
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa wababe hao kukutana kugombea mkanda wa IBF wa mabara (IBF I/C) na mpambano wao unategemnea kutoa ushindani mkubwa. 
 

Mshindi katika mpambano huo ataingia moja kwa moja katika orodha ya mabondia 15 bora kwenye uzito wa Super Middle duniani.

 

 

TANZANIA YAPATA MWAKILISHI MISS EAST AFRICA 2012


Mrembo atakaewakilisha Tanzania katika mashindano ya mwaka huu ya Miss East Africa ni Jocelyne Diana Maro (22)

Mrembo huyo alipatikana kufuatia mchakato ulioendeshwa na kamati maalum ya kuratibu zoezi hilo kwa zaidi ya miezi mitatu iliyopita na kuwashinda warembo wengine 148 waliojitokeza kutaka kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss East Africa 2012
Jocelyne amehitimu shahada ya Business Economics mwezi wa saba mwaka huu katika chuo kikuu cha Keele University, Nchini Uingereza
Maandalizi ya mashindano hayo yanaendelea vizuri na yapo kwenye hatua za mwisho ikiwa ni pamoja na kukamilisha taratibu zote za BASATA ili kufanikisha mashindano hayo yatakayofanyika tarehe 07 December, 2012 katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam
Mashindano ya Miss East Africa mwaka huu tayari yameanza kuvuta hisia za watu wengi barani Africa kufuatia kiwango cha juu cha warembo wanaowania taji hilo.

Nchi zilizothibitisha kushiriki mashindano hayo ni wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Nchi zingin000e zilizoalikwa kushiriki ni pamoja na Ethiopia, Eritrea, Somalia, Djibouti, Southern Sudan, Malawi, pamoja na visiwa vya Seychelles, Madagascar, Reunion, Comoros, na Mauritius.


Mashindano ya Miss East Africa yanalenga kukuza ushirikiano na kutangaza utamaduni wa Afrika Mashariki, pamoja na kutangaza utalii wa Tanzania kama Nchi wenyeji wa mashindano hayo makubwa katika ukanda huu wa Afrika

Mashindano ya Miss East Africa yanamilikiwa na kuandaliwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam,.

 

 

Wanyama ALA NYAMA USKOCHI

Victor Wanyama 

Mkenya, Victor Wanyama amefunga mabao mawili kwa kuisadia klabu yake ya Celtic kuinyeshea klabu ya St. Mirren kwa mabao 5-0, na kuendeleza uongozi wao katika ligi kuu ya premier nchini Scotland.

Ushindi huo umeipa Celtic matumaini makubwa huku ikijiandaa kwa michuano ya kuwania kombe la klabu bingwa barani ulaya dhidi ya Barcelona.

Hata hivyo, St Mirren ilipoteza nafasi nyingi za kufunga wakati wa mechi hiyo. Garry Hooper aliifungia celtic bao lake la kwanza kunako dakika ya kumi na tano kabla ya Efe Ambrose kufungwa bao la pili.

Wanyama naye akafunga bao la tatu kunako dakika ya 32 na dakika chache baadaye Wanyama aklafunga bao la pili.

Kocha wa St Mirren Danny Lennon amesema amehuzunishwa sana na matokeo ya mechi hiyo, kwani wachezaji wake hawakucheza kama kawaida yao.

Lakini kocha wa Celtic, Neil Lennon amesema mechi hiyo imekuwa fursa nzuri kwa wachezaji wake kujiandaa kwa mechi yao ya wiki ijayo dhidi ya Barcelona

 

 

 (FKF) limethibitisha kuwa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars itashiriki katika michuano ya kuwania kombe la mataifa bingwa kanda ya Afrika Mashariki na Kati-


Shirikisho la mchezo wa soka nchini Kenya, Football Kenya Federation (FKF) limethibitisha kuwa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars itashiriki katika michuano ya kuwania kombe la mataifa bingwa kanda ya Afrika Mashariki na Kati-CECAFA ambayo imepangiwa kuanza tarehe ishirini na nne mwezi ujao hadi Desemba tarehe nane.

Mwenyekiti wa FKF, Sam Nyamweya ameyasema hayo Jumamosi baada ya kukamilisha mazungumzo na mwenyekiti wa CECAFA, ambaye pia ni rais wa shirikisho la mchezo wa soka nchini Tanzania, Leodgar Tenga.
 
Awali FKF, ilikuwa imetangaza kuwa Harambee Stars haitashiriki katika mashindano hayo na badala yake itaaangazia michuano ya kufuzu kwa fainali za wachezaji wanaoshiriki katika ligi za nyumbani barani Afrika CHAN.
 
Harambee Stars inajiandaa kuchuana na Burundi baadaye mwaka huu.
Wakati huo huo Nyamweya amesema hawataomba mechi hizo za CHAN kuahirishwa na kwamba Harambee Stars itashiriki kikamilifu.
 
Harambee Stars imepangiwa kucheza mechi yake ya kwanza tarehe Mosi Desemba siku sita tu baada ya kuanza kwa michuano ya CECAFA mjini Kampala na kocha wa Harambee Stars, atalazimika kuwa na vikosi viwili ili kushiriki katika mechi zote.
 
Malumbano makali yalikuwa yameibuka kati ya viongozi wa soka nchini Kenya na katibu mkuu wa CECAFA, Wycliffe Musonye, baada ya Kenya kutangaza kuwa haitashiriki katika fainali hizo kulalamikia uamuzi wa viongozi wa CECAFA wa kuhamisha mashindano hayo kutoka Nairobi hadi Kampala.

 

ROONEY atimiza Goli 200 kwa Klabu, RIO amkera FERGIE!


FERGIE_na_SIMUJANA OLD TRAFFORD, ambako Manchester United waliitwanga Stoke City Mabao 4-2 katika Mechi ya Ligi Kuu England, Wayne Rooney alifikisha Mabao 200 kwa kufungia Klabu, Man United na Everton, lakini pia uamuzi wa


Beki Rio Ferdinand kutovaa Fulana ya Kampeni za Ubaguzi, ‘KICK IT OUT’, wakati wa kupasha moto kabla ya Mechi hiyo umemtibua Meneja wake Sir Alex Ferguson.

Katika Mechi hiyo ya jana, Rooney alifunga Bao 3, moja akijifunga mwenyewe na kuipa Stoke City uongozi wa bao 1-0, lakini alijirekebisha na kusawazisha na kisha, baadae, kuipigia Man United bao jingine ambalo liliipa Man United ushindi wa bao 4-2 huku bao nyingine mbili zikifungwa na Robin van Persie na Danny Welbeck.


Kwa kujifunga mwenyewe na kisha kuifungia Man United mabao katika Mechi moja, Wayne Rooney amekuwa Mchezaji wa kwanza wa Man United kufanya hivyo tangu David Beckham alipokumbwa na mkasa kama huo Mwaka 2001.


Wakati Rooney akifanya miujiza yake, Man United imekumbwa na mvutano kati ya Meneja wao Sir Alex Ferguson na Mchezaji wake Rio Ferdinand kuhusu kuisapoti Kampeni ya kupinga Ubaguzi wakati ambao Wiki hii Kampeni ya ‘KICK IT OUT’ ndio imeshamiri na Wachezaji kuombwa kuvaa Tisheti zenye maandishi hayo ili kupinga Ubaguzi.


Majuzi Ijumaa, Ferguson alitamka kuwa Mchezaji wa Reading Jason Roberts amepotoka baada ya kutamka waziwazi hatavaa Tisheti hizo ikiwa ni kuonyesha kukerwa kwake na usimamizi duni wa kupinga ubaguzi na hasa kumuona John Terry, ambae alipatikana na hatia ya kumkashifu Kibaguzi Mdogo wake Rio Ferdinand, Anton Ferdinand, kupewa adhabu hafifu ya kufungiwa Mechi 4 na Faini ya Pauni 220,00 wakati Straika wa Liverpool Luis Suarez alifungiwa Mechi 8.


Sir Alex Ferguson amesema watalishughulikia suala la Rio Ferdinand kugoma kuvaa Tisheti hizo ndani ya Klabu.


Akiongea mara baada kuifunga Stoke City bao 4-2, Ferguson alisema: “Nimehuzunishwa. Nilisema jana Wachezaji wavae Fulana hizo ili kuiunga PFA [Professional Footballers' Association] na kila Mchezaji afuate. Sasa yeye katuangusha. Tutalishughulikia suala hili, usiwe na wasiwasi!”


Baadae Ferguson akaongeza: “Niliongea na Wanahabari kuhusu hili. Imenifedhehesha.”
Hata hivyo, baadhi ya Wadau wameibuka kuunga mkono uamuzi wa Rio Ferdinand wakidai uamuzi huo ni wa Mtu binafsi katika kitu anachokiamini.


Akiongea na RADIO 5, Mchezaji wa zamani wa Wales aliewahi kuichezea Man United, Robbie Savage, amesema: “Ninaheshimu misimamo ya Jason Roberts na Rio Ferdinand. Ukifikiria zaidi utashangazwa na alichokisema Ferguson. Anasema amefedheheshwa. Hili si suala lake. Fergie ni Meneja Bora kupita wote katika historia lakini ni uamuzi binafsi wa Rio kuvaa au kutovaa Tisheti ile!”

 

ULAYA: Barca, Juve zachanja mbuga kileleni! Real yajikongoja!!


>> SERIE A: Juve wajikita kileleni, Pogba aifungia bao!!
LIONEL_MESSI================================
LA LIGA
Jumamosi Oktoba 20
Málaga 2 Valladolid 1
Real Madrid 2 Celta Vigo 0
Valencia 3 Athletic Bilbao 2
Deportivo La Coruña 4 Barcelona 5
================================
Huko Spain, kwenye La Liga, Supastaa Lionel Messi, aliipigia Barcelona hetitriki wakati Timu yake ilipoishinda ugenini Deportivo la Coruna bao 5-4 na Mahasimu wao, Real Madrid, wakiwa nyumbani Santiago Bernabeu, waliifunga Celta Vigo bao 2-0 huku Cristiano Ronaldo akifunga bao moja kwa Penati.
Katika Mechi ya Deportivo la Coruna na Barcelona, Wafungaji walikuwa:
Deportivo:
-Pizzi, Dakika ya 26, Penati
-Alex Bergantinos, 37 na 47
-Jordi Alba, 79 [Kajifunga mwenyewe]
Barcelona:
-Jordi Alba, Dakika ya 3
-Cristiano Tello, 8
-Messi, 18, 43 na 77
Kwenye Dakika ya 49, Mchezaji wa Barcelona Javier Mascherano alitolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Ndani ya Santiago Bernabeu, Real waliifunga Celta Vigo bao 2-0 kwa bao za Gonzalo Higuain katika Dakika ya 11 na Ronaldo kwa Penati ya Dakika ya 67.


RATIBA:
Jumapili Oktoba 21
[Kwenye Mabano Jina la Uwanja]
Getafe v Levante [Coliseum Alfonso Perez]
Espanyol v Rayo Vallecano [Cornellà - El Prat]
Granada v Real Zaragoza [Estadio Los Cármenes]
Osasuna v Real Betis [Estadio El Sadar]
Real Sociedad v Atlético Madrid [Estadio Anoeta]


Jumatatu Oktoba 22
Sevilla FC v Mallorca [Estadio Ramon Sanchez Pizjuan]
================================



SERIE A: Juve wajikita kileleni, Pogba aifungia bao!!
MATOKEO:
Jumamosi Oktoba 20
Juventus 2 Napoli 0
Lazio 3 AC Milan 2
================================

Huko Italy, kwenye Serie A, Mabngwa Juventus wameendelea kujikita kileleni baada ya kuichapa Napoli bao 2-0 kwa bao za Jose Martin Caceres, katika Dakika ya 80 na Paul Pogba, Dakika ya 82, hilo likiwa bao lake la kwanza kwa Juve tangu ahamie akitokea Manchester United.
Kwenye Mechi nyingine iliyochezwa jana, Lazio iliwapiga AC Milan bao 3-2 na bao za Lazio zilifungwa na Hermanes, Dakika ya 25, Candreva, 41, Miroslav Klose, 49.
Bao za AC Milan zilifungwa na  Nigel de Jong, Dakika ya 61 na Stephan El Shaarawy, 79.


RATIBA:
Jumapili Oktoba 21
[Kwenye Mabano Jina la Uwanja]
Cagliari v Bologna [Sant'Elia]
Atalanta v Siena [Atleti Azzurri d'Italia]
Chievo Verona v Fiorentina [Bentegodi]
Inter Milan v Catania [Stadio Giuseppe Meazza]
Palermo v Torino [Renzo Barbera]
Parma v Sampdoria [Ennio Tardini]
Udinese v US Pescara [Stadio Friuli]
Genoa v AS Roma [Luigi Ferraris]

 

BPL: Arsenal walala hoiii!!


>>WENGER alia na ‘Pira Bovu’ la Arsenal!!!
ARSENE_WENGER-13Katika Mechi ya mwisho jana ya Ligi Kuu England, BPL, Arsenal walijikuta wako Pointi 10 nyuma ya vinara Chelsea baada ya kuchapwa bao 1-0 huko Uwanjani Carrow Road na Norwich City ambayo jana ndio ilipata ushindi wake wa kwanza wa Ligi kwa Msimu huu.

Bao lililowaua Arsenal lilifungwa katika Dakika ya 19 na Grant Holt baada ya mkwaju wa Alexander Tettey kutemwa na Kipa Vito Mannone na Holt kukwamisha mpira wavuni.

Huku wakipata habari njema baada ya Kiungo wao mahiri Jack Wilshere kuwepo benchi kwa mara kwanza baada ya kuwa majeruhi kwa Miezi 14, Arsenal walishindwa kupunguza pengo na wapinzani wao wakubwa Chelsea, Manchester City na Manchester United, ambao wote walishinda Mechi zao za jana zilizochezwa mapema.

Kipigo hicho kimewaacha Arsenal wakiwa nafasi ya 9 na wana Pointi 12.
Mara baada ya Mechi Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, alikiri Timu yake haikuwa na umakini wa kawaida lakini alikataa kumlaumu Mchezaji yeyote.

VIKOSI:
Norwich: Ruddy, Russell Martin, Turner, Bassong, Garrido, Elliott Bennett, Johnson, Hoolahan, Tettey, Pilkington, Holt
Akiba: Rudd, Snodgrass, Howson, Jackson, Surman, Morison, Ryan Bennett.
Arsenal: Mannone, Jenkinson, Mertesacker, Vermaelen, Andre Santos, Ramsey, Arteta, Cazorla, Gervinho, Giroud, Podolski
Akiba: Martinez, Wilshere, Oxlade-Chamberlain, Djourou, Coquelin, Arshavin, Gnabry.
Referee: Lee Probert
+++++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA
Jumapili Oktoba 21
[SAA 9 na Nusu Mchana]
Sunderland v Newcastle
[SAA 12 Jioni]
QPR v Everton

CAF CHAMPIONZ LIGI: Esperance FAINALI, Mazembe NJE!

>>FAINALI kuivaa Al Ahly au Sunshine Stars!!
NUSU FAINALI:
[MARUDIANO]
[SAA za BONGO]
Jumamosi Oktoba 20         
Espérance Sportive de Tunis 1 TP Mazembe 0 [Jumla Mabao Mechi mbili 1-0]
Jumapili Oktoba 21         
20:30 Al Ahly v Sunshine Stars [Cairo International Stadium]
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Jana huko Stade El Menzah, Tunis, Tunisia, Mabingwa watetezi wa Afrika, Espérance Sportive de Tunis, walifanikiwa kuifunga TP Mazembe ya Congo DR bao 1-0 katika Mechi ya marudiano ya Nusu Fainali ya CAF CHAMPIONZ LIGI na kutinga Fainali ya Mashindano hayo ya kutafuta Klabu Bingwa Afrika.
Katika Mechi ya kwanza iliyochezwa huko Lubumbashi Wiki mbili zilizopita, Mazembe na Esperance zilitoka 0-0.

Bao la ushindi la Esperance katika Mechi ya jana lilifungwa na Mohamed Ben Mansour katika Dakika ya 70.

Kwenye Fainali Esperance inangoja Mshindi wa marudiano ya Nusu Fainali nyingine itakayochezwa leo huko Cairo, Misri kati ya wenyeji Al Ahly na Sunshine Stars ya Nigeria, Timu ambazo zilitoka sare bao 3-3 katika Mechi ya kwanza.

Fainali itachezwa Mwezi ujao Novemba na Mshindi atapata kitita cha Dola Milioni 1 na Nusu na ataiwakilisha Afrika katika Mashindano ya FIFA ya kusaka Klabu Bingwa Duniani yatakayochezwa huko Japan Mwezi Novemba.

BUNDESLIGA: Bayern wapiga 5-0, Dortmund wafa!


BORUSSIA_DORTMUND_JUKWAABayern Munich, wakicheza ugenini, leo wameitandika Fortuna Dusseldorf bao 5-0 na kuweka rekodi mpya kwenye Bundesliga kwa kushinda Mechi 8 mfululizo lakini Mabingwa watetezi Borussia Dortmund wamechapwa bao 2-1 na Schalke hii ikiwa ni Dabi ya 141 ya Ruhr iliyochezwa nyumbani kwa Dortmund Uwanja wa Signal Iduna Park mbele ya Mashabiki. 80,645.
Ushindi wa Bayern Munich umewafanya wazidi kuongoza Ligi wakiwa na Pointi 24 zikiwa ni Pointi 5 mbele ya Timu ya pili Eintracht Frankfurt huku Dortmund wakiwa nafasi ya 4 wakiwa na Pointi 12.
Bao za Bayern zilifungwa na Mario Mandzukic, Luiz Gustavo, Rafina, na bao mbili za Thomas Muller.
Kwenye Mechi ya Borussia Dortmund na Schalke, Schalke walipata bao la kwanza katika Dakika ya 14 kupitia Fowadi wa Holland Ibrahim Affelay na kuongeza bao la pili katika Dakika ya 47 mfungaji akiwa Marco Hoger.
Bao la Dortmund lilifungwa na Robert Lewandowski katika Dakika ya 55.
================================
MATOKEO/RATIBA:
[Kwenye Mabano Jina la Uwanja]
Ijumaa Oktoba 19
TSG Hoffenheim 3 SpVgg Greuther Fürth 3


Jumapili Oktoba 20
Bayer Leverkusen 2 Mainz 2
Borussia Dortmund 1 Schalke 2
Eintracht Frankfurt 3 Hannover 1
Fortuna Düsseldorf 0 Bayern Munich 5
VfL Wolfsburg 0 SC Freiburg 2
Werder Bremen v Borussia Monchengladbach [Weserstadion]

Jumapili Oktoba 21
Nurnberg v FC Augsburg [EasyCredit-Stadion]
Hamburg SV v VfB Stuttgart [HSH Nordbank Arena]
=================================

UAMUZI WA MURRAY KUMCHUKUA ROBSON BADALA YANGU ULINIONGEZEA CHANGAMOTO YA KUFANYA VIZURI ZAIDI - WATSON.

MWANADADA nyota katika mchezo wa tenisi, Heather Watson ameweka bayana kuwa hakufurahishwa na uamuzi wa Andy Murray kumchukua Laura Robson katika michuano ya tenisi ya olimpiki ya wawili wawili iliyofanyika London mwaka huu.

 Katika michuano hiyo Murray na Robson waliambulia medali ya fedha lakini Watson mwenye umri wa miaka 20 amesema kuachwa huko ndiko kulikomfanya ajifue zaidi na kunyakuwa taji lake la kwanza la Grand Slam la michuano ya wazi ya Japan iliyofanyika jijini Osaka. 

Watson amesema kuwa michuano ya olimpiki ni ya kipekee na kila mtu angependa kucheza lakini ulikuwa ni uamuzi wa Murray kumchagua Robson kama mchezaji mwenza na kumaliza michuano hiyo na medali ya fedha kitu ambacho ni kizuri kwasababu wamewakilisha vyema waingereza.

 Ushindi wa Watson wa michuano hiyo ya Japan umemuingiza katika orodha za wachezaji 50 bora wa mchezo huo kwa upande wa wanawake nafasi mbili nyuma ya Robson lakini mwanadada huyo bado anaonyesha kiu ya kupata mafanikio zaidi huko mbele.