Wednesday, November 14, 2012

KAMATI YA SERENGETI YAKUSANYA MZIGO WA KUTOSHA KUISHINDISHA TIMU

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Saidia Serengeti Boys Ishinde, Kassim Mohamed Dewji akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Serengeti, ndani ya hoteli ya JB Bellmonte, katikati ya Jiji la Dar es Salaam asubuhi ya leo kuhusu maandalizi ya mechi ya Jumapili dhidi ya Kongo Brazzaville, kuwania tiketi ya kucheza Fainali za U-17 Afrika. Dewji amesema Kamati yake imefanikiwa kukusanya Sh. Milioni 35 kati ya Milioni 60 zinazotakiwa kwa maandalizi ya mchezo huo wa kwanza. Wengine kulia ni Henry Tandau, Katibu wa Kamati na kushoto, Angetile Osiah, Mjumbe wa Kamati.  

Mjumbe wa Kamati, Abdallah Ahmad Bin Kleb 

Kutokas kulia Bin Kleb, Tandau, Dewji, Osiah na Mjumbe mwingine wa Kamati, Salim Abdallah

Salim Abdallah kushoto na Osiah kulia

Makamu Mwenyekiti wa Kamati, KD akizungumza kwa simu na Mwenyekiti wake, Ridhiwani Kikwete ambaye hakuhudhuria mkutano kwa sababu yupo msibani kwao Bagamoyo.  

LADY JAYDEE SASA NDANI YA EATV KATIKA DIARY

Mwanamuziki maarufu nchini, Lady Jaydee (kulia), akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Nyumbani Lounge, Oysterbay, Dar es Salaam kuhusu kipindi chake kipya cha Lady Jaydee Diary, kitakachokuwa kikirushwa hewani na kituo cha East African TV, maarufu kama Channel 5 kila Jumapili saa 3:00 usiku. Kushoto ni Mkuu wa vipindi EATV, Lydia Igarabuza.  



MWANAMUZIKI mkongwe nchini, Lady Jadee ameanzisha kipindi cha TV kiitwacho Diary Ya Lady Jaydee, kitakachokuwa kikirushwa hewani na kituo cha East African TV, maarufu kama Channel 5 kila Jumapili saa 3:00 usiku.
Kama msanii, Lady Jaydee amefanikiwa na kutambulika katika kiwanda cha muziki ndani na nje ya nchi, huku akitunukiwa tunzo nyingi zaidi akiwa albamu zake tano. Pamoja na kuwa anaendelea na fani yake ya muziki, Lady Jaydee ameamua kuwafikia na kuwaburudisha wapenzi wa kazi zake kwa njia nyingine.
Lady Jaydee sasa anaanza sura mpya ya burudani kwa kuleta kipindi cha TV kiitwacho DIARY YA LADY JAYDEE, ambacho kutaonekana katika kituo cha TV cha EATV
Diary Ya Lady Jaydee itaonesha maisha na hadithi za kweli za Lady Jaydee kwa lengo la kuburudisha kwa kuonyesha mambo yate mazuri anayopitia au kuyaona Lady Jaydee kuelimisha kwa kushiriki mambo ya kijamii, kutia moyo wengine wafuate ndoto zao kwa uadilifu, kuongeza kipato kama msanii kwa kutangaza biashara mbalimbali na hatimae kudumisha ajira binafsi kwa njia ya sanaa.
Lady Jaydee anatoa shukrani kwa mashabiki kwa kuendelea kumpokea, jambo ambalo linampa nguvu zaidi ya kufanya kaza.
Pia anashukuru sana vyombo vya habari na zaidi anawashukuru EATV na washirika wake kwa kumpa nafasi ya kurusha kipndi chake kipya Diary Ya Lady Jaydee. EATV imekuwa mchango wa aina yake katika kuwakuza wasanii Tanzania.
Lady Jaydee anatoa wito kwa vyombo vya habari kuendelea kushirikiana na naye kwa kila namna, ili kukuza na kuendeleza kipaji chake na sanaa ya muziki wa Tanzania kwa ujumla wake.
Zaidi anatoa wito kwa makampuni kishiriki na kuungana nae ili waweze kumpa nguvu msanii, kutangaza biashara zao na kushawishi ajira katika fani ya muziki.
Na mwisho Lady Jaydee anawaribisha wote kusikiliza CDs zake au kuburidika na kundi lake la Machozi Band au kupata chakula ktk mgahawa wake wa kisasa Nyumbani Lounge au ukiwa umepumzika nyumbani utazame kipindi chake Diary Ya Lady Jaydee ktk EATV.

RHINO RANGERS WAENDELEZA MAUAJI LIGI DARAJA LA KWANZA FDL WAITANDIKA MORAN FC 2-1
 
Timu ya maafande wa jeshi la wananchi  ya mkoani tabora  RHINO RANGERS jana waliendelea  kuwapa raha wakazi wa tabora baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya timu ya moran fc ya kiteto manyara kule.
mabao ya rhino rangers hiyo jana yalifungwa  na SHIJA MONGO na ABDALAH SIMBA mshambuliaji ambaye ananguvu ,kasi,mashuti na mtaalaamu wa kumiliki mpira .
Ligi hiyo inaendelea  tena leo tarehe 15 kwa michezo mitatu katika miji  ya   kigoma,shinyanga namwanza.mechi ambazo zitachezwa hii leo ni kati ya  kanembwa vs polisi mara,,,pamba vs polisi tabora na mchezo wa mwisho utakuwa kati ya mwadui vs polisi dodoma
Mechi hizi zimeahirishwa kutokana na kupisha mchezo uliokuwa katika kalenda ya FIFA kati ya taifa stars timu ya taifa ya Tanzania na timu ya harambee stars timu ya taifa ya Kenya.
  MSIMAMO KUNDI C
1.RHINO RANGERS MECHI 7 POINTI 17
2.KANEMBWA JKT MECHI6 POINTI 13
3.MWADUI FC MECHI 6 POINTI 10
4.POLISI DODOMA MECHI  POINTI 8
5.PAMBA MECHI 6 POINTI 8
6.POLISI MARA MECHI 6 POINTI 5
7.POLISI TABORA MECHI 6 POINTI 3
8.MORAN FC MECHI 6 POINTI 2
FAHAMU;Kila kundi litatoa timu moja ambayo itapanda ligi kuu ya vodacom tanzania bara VPL msimu ujao na tayari timu ya maafande ya polisi moro imeonyeshwa mlango wa kutokea kwani imemaliza mzunguko wa kwanza wa  VPL ikiwa imecheza mechi 13 na ina pointi 4 inashika mkia.timu zitakazo panda ni kutoka kundi A,B,na C
 MATOKEO TOKA LIGI IANZE oktoba 24
===Kanembwa vspolisi dodoma 3-0
===pamba vs polisi mara 3-2
===rhino rangers vs polisi tabora 2-1
===mwadui vs moran 3-0
oktoba 27
====polisi tabora vs polisi dodoma 0-1
====mwadui vs polisi mara 3-0
====kanembwa JKT vs moran 2-0
====pamba vs rhino rangers 1-1
oktoba 31
====polisi mara vs rhino rangers 0-0
====moran vs polisi tabora 1-1
====polisi dodoma vs pamba2-0
====kanembwa vs mwadui 3-2
novemba 4
===polisi mara vs polisi tabora 1-1
===moran vs polisi dodoma1-1
===rhino rangers vs kanembwa JKT 3-1
===mwadui vs pamba...2-0......
novemba 7
====polisi tabora vs kanembwa  JKT 1-4
====polisi dodoma vs polisi mara 0-0
====pamba vs moran ya manyara 2-0
novemba 8
====rhino rangers vs mwadui FC 2-0
novemba 11
====kanembwa vs pamba 0-0
====polisi tabora vs mwadui 0-0
====polisi dodoma vs rhino rangers 0-2
====polisi mara vs moran 3-1

 

YONDAN: HAIKUWA KAZI NYEPESI KUMDHIBITI OLIECH

Kevin Yondan

BEKI wa Yanga, Kevin Yondan amesema kwamba licha ua kuwafunga Kenya, Harambee Stars, lakini wapinzani wao hao ni wazuri na zaidi akamsifia mshambuliaji wa klabu ya Daraja la Pili Ufaransa, AJ Auxerre, Dennies Oliech kwamba ni mtu hatari.
Akizungumza  kwa simu kutoka Mwanza jana, Yondan alisema kwamba walifanya kazi kubwa mno kumdhibiti Oliech, kwani mtu huyo ni hatari.
“Yule jamaa anajua, mimi binafsi ilinibidi nitulize sana akili katika kukabiliana naye, ndiyo maana hakufunga, bila hivyo Yule mtu angefunga,”alisema Yondan.
Hata hivyo, beki huyo wa kati alisema timu yao ilicheza vizuri kwa ujumla jana na anaamini hizi ni dalili nzuri za kuwapa Watanzania.
“Tunamshukuru Mungu kwa ushindi huu, lakini tunaendelea kuomba mashabiki wetu waendelee kutupa sapoti ili tufanye vizuri zaidi,”alisema.
Taifa Stars, jana iliibwaga Kenya, Harambee Stars bao 1-0 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza katika mchezo wa kirafiki ulio katika kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Hadi mapumziko, Stars ilikuwa mbele kwa bao 1-0, lililotiwa kimiani na beki Aggrey Morris katika dakika ya nne, baada ya kupanda kusaidia mashambulizi.
Katika mechi hiyo iliyochezeshwa na refa anayetambuliwa na FIFA, Oden Mbaga, Kenya walitawala dakika 10 za mwanzo, lakini baada ya hapo Stars wakafunguka nao na kuanza kula nao sahani moja na Harambee Stars.
Kipindi cha pili, Kenya walianza na mabadiliko kocha Henri Michel akiwapumzisha James Situma, Jerry Santo na Wesley Kemboi na kuwaingiza Christopher Wekesa, Anthony Akumu na Timbe Ayoub.
Pamoja na mabadiliko hayo, mambo yaliendelea kuwa magumu kwa Harambee Stars, kwani wenyeji waliendelea kucheza kwa makini, wakishambulia na kujilinda zaidi.
Kocha wa Stars naye, Mdemnark, Kim Poulsen aliwatoa Amir Maftah, Salum Abubakar, Mwinyi Kazimoto, Mbwana Samatta, Mrisho Ngassa na Thomas Ulimwengu na kuwaingiza Nassor Masoud ‘Chollo’, Amri Kiemba, Simon Msuva, John Bocco ‘Adebayor’, Shaaban Nditi  na Issa Rashid.  
Baada ya mchezo huo, kocha wa Harambee, Mfaransa Michel alionyesha kukerwa na matokeo hayo na kusema timu yake haikucheza vizuri, wakati Polusen, amefurahia ushindi huo akisema timu yake haijacheza kwa miezi miwili na baada ya siku mbili za mazoezi wameifunga Kenya. 
Taifa Stars; Juma Kaseja, Shomari Kapombe, Amir Maftah/Nassor Masoud ‘Chollo’ dk70, Aggrey Morris, Kevin Yondan, Frank Domayo, Salum Abubakar/Amri Kiemba dk69, Mwinyi Kazimoto/Simon Msuva dk69, Mbwana Samatta/John Bocco dk 84, Mrisho Ngassa/Shaaban Nditi dk72 na Thomas Ulimwengu/Issa Rashid dk 89.  
Harambee Stars; Frederick Onyango, Brian Mandela, Eugene Asike, James Situma/Christopher Wekesa dk 46, Edwin Wafula, Jerry Santo/Anthony Akumu dk 46, Peter Opiyo/Charles Okwemba dk 67, Patrick Obuya, Patrick Osaika/Mulienge Ndeto dk 73, Dennis Oliech na Wesley Kemboi/Timbe Ayoub dk 46.
REKODI YA STARS MWAKA HUU NA RATIBA YA MECHI ZIJAZO:
Februari 23, 2012
Tanzania 0 – 0 DRC (Kirafiki)
Februari 29, 2012
Tanzania 1 – 1 Msumbiji   (Kufuzu Mataifa ya Afrika)
Mei 26, 2012
Tanzania 0 – 0 Malawi
Juni 2, 2012
Ivory Coast 2 – 0 Tanzania (Kufuzu Kombe la Dunia)
Juni 10, 2012
Tanzania 2 – 1 Gambia      (Kufuzu Kombe la Dunia)
Juni 17, 2012
Msumbiji 1 – 1 Tanzania   (Tanzania ilitolewa kwa penalti kufuzu Mataifa ya Afrika)
Agosti 15, 2012
Botswana 3 – 3 Tanzania (Kirafiki)
Novemba 14, 2012
Tanzania 1-0 Kenya (Kirafiki)
Machi 22, 2013
Tanzania Vs Morocco (Kufuzu Kombe la Dunia)
Juni 7, 2013
Morocco Vs Tanzania (Kufuzu Kombe la Dunia)
Juni 14, 2013    
Tanzania Vs Ivory Coast    (Kufuzu Kombe la Dunia)
Septemba 6, 2013
Gambia    Vs Tanzania (Kufuzu Kombe la Dunia)

HATIMA YA MILOVAN SIMBA LEO, KIKAO KIZITO MNO CHAFANYIKA

Kocha wa Simba SC, Milovan Cirkovick kushoto akiwa ameishiwa nguvu baada ya kufungwa na Toto Africans mwishoni mwa wiki katika mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kulia ni wachezaji wake, Shomary Kapombe na Jonas Mkude.

KAMATI ya Utendaji ya klabu ya Simba ya Dar es Salaam inatarajiwa kuwa na kikao kizito leo, kujadili mambo mbalimbali kuhusu mustakabali wa klabu hiyo na mwenendo wa timu yao ya soka kwa ujumla.
Habari kutoka ndani ya Simba, zimesema kwamba kikao hicho kitashirikisha Wajumbe wote wa Kamati hiyo, chini ya Mwenyekiti wake, Alhaj Ismail Aden Rage.
Miongoni mwa ajenda zinazotarajiwa kuwa mjadala nzito ni matokeo ya timu hiyo kushika nafasi ya tatu katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, licha ya kuanza vyema na kufikia kuongoza kwa wastani wa pointi saba zaidi.
Aidha, katika kikao hicho, habari zinasema Makamu Mwenyekiti, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ atawasilisha rasmi barua ya kujiuzulu kwake uongozi, kufuatia kuibuka watu wanaompinga na kushinikiza ajiuzulu.
Lakini pia bado mjadala mpana utakuwa kuhusu mustakabali wa timu kuelekea mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Litajadiliwa suala la kipa Juma Kaseja kuomba kung’atuka baada ya kufanyiwa fujo na mashabiki.
Litajadiliwa suala la kusimamishwa kwa beki Juma Said Nyosso na kiungo Haruna Moshi ‘Boban’. Litajadiliwa suala la kuboreshwa kwa timu kuelekea mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa mwakani.
Lakini pia habari zinasema litajadiliwa pendekezo la kutaka kocha wa timu hiyo, Mserbia Profesa Milovan Cirkovick aondolewe na masuala mengine ya msingi, kama salio la malipo ya kiwanja, ambacho klabu hiyo inataka kujenga uwanja wake wa michezo. 
Kwa ujumla, hamkani si shwari ndani ya Simba hivi sasa, baada ya mabingwa hao wa Ligi Kuu kumaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu wakiwa katika nafasi ya tatu, tena wakizidiwa pointi sita na wapinzani wao wa jadi, Yanga wanaoongoza ligi hiyo.

CHEKA KUPANDA ULINGONI ARUSHA KUMVAA MWAHILA

Bondia maarufu kuliko wote Tanzania Francis Cheka atamvaa Udiadia Mwahia kutoka nchini DRC Kongo kugombea mkanda wa ubingwa wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi.
Mabondia hao watakutana katika mpambano wa kwanza tangu Arusha liwe jiji katika uwanja wa Shekh Amri Abeid tarehe 26 Desemba 2012 siku ya Boxing Day!

Akimtambulisha Francis Cheka kwa waandishi wa habari katika ukumbi wa Maelezo jijini Dar Es Salaam jana , mratibu wa mpambano huo na ambaye alishawahi kuwa bingwa wa Tanzania kwenye ngumi za ridhaa George Andrew alisema kuwa bondia Udiadia Mwahila anakaa Lusaka Zambia ambako ndipo anapofanya shughuli zake za ngumi chini ya promota maarufu Anthony Mwamba!
 Udiadia ana rekodi ya mapambano 12 na ametoka sare pambano moja na hajapoteza hata moja wakati Francis Cheka ana rekodi ya mapambano 33 amepoteza 6 na kutoka sare pambano moja.
George alisema kuwa mpambano huo utatumika kulitangaza jiji la Arusha kama Las Vegas ya ngumi katika bara la Afrika na kulifananisha jiji la Arusha na jiji la Geneva lililoko nchini Switzerland.

Mpambano huo unakuja wakati ambapo mpambano mwingine wa Francis Cheka na bondia kutoka Ujerumani wa kugombea mkanda wa IBF wa mabara ulifutwa baada ya Simon kuumia katika mazoezi.
Naye Rais wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati, Ghuba ya Uarabu na Ghuba ya Uajemi Onesmo Ngowi alisema kuwa wao kama IBF wamesharuhusu maandalizi ya mpambano huo. Rais huyo aliwataka wadhamini pamoja na wananchi wa mkoa wa Arusha na mikoa mingine kujitokeza kwa wingi ili kulifanya pambano hilo kuwa la mafanikio.
 Naye bondia Francis Cheka alisema kuwa amejiandaa kwa kiasi kikubwa na atazidi kufanya mazoezi ili kupata ushindi kwake pamoja na nchi ya Tanzania. Aliendelea kusema kuwa kila Mtanzania anajua uwezo wake kwa hiyo amewataka wote wafike kwa wingi ili kupata uhondo na burudani tosha

 

MWAKALEBELA KUANZA HARAKATI ZA KUMNG'OA BAYI TOC LEO HII

Habari za uhakika kutoka kwa aliyekuwa katibu mkuu wa TFF katika awamu ya kwanza ya uongozi wa Leadgar Tenga, Bwana Frederick Mwakalebela ni kwamba kesho asubuhi ataenda kuchukua fomu za kugombea uongozi wa ukatibu mkuu wa kamati ya Olimpiki Tanzania.

Mwakalebela ambaye ni mmoja ya wadau wenye kuonyesha nia ya dhati katika kukuza michezo kwa kutoa misaada mbalimbali pamoja na kuandaa michuano kama 'Mwakalebela CUP' ambayo imekuwa ikitoa vipaji vingi amesema ameamua kuchukua fomu ya kugombea ukatibu mkuu kwa sababu anaamini ana uwezo na nia ya dhati ya kuongoza kamati hiyo ili kuiwezesha nchi yetu ipige hatua zaidi katika michezo.

Kuchukua fomu kwa Mwakalebela kunamaanisha katibu mkuu huyo wa zamani wa TFF, ameanza mbio za kumng'oa madarakani kidemokrasia Fibert Bayi ambaye amekuwa kiongozi wa kamati hiyo kwa muda mrefu sasa.

Leo ndio siku ya mwisho ya kuchukua fomu.

MATAIFA HURU YA AFRIKA: MAREFA KUFICHWA KUEPUSHA UPANGAJI WA MATOKEO

Marefa  wa fainali zijazo za kombe la mataifa huru ya Afrika watawekwa mbali na watu wengine wakati wa michuano hiyo nchini South Africa ili kuzuia upangaji wa matokeo.

Hali ya ulinzi ilitumika pia katika fainali ya za kombe la dunia mwakak 2010 zilizofanyika nchini SA.

CEO wa kamati ya ndani ya uandaaji Mvuso Mbebe alisema: "Marefa watakuwa mafichoni katika hotel mojawapo ambayo hakuna mtu atakuwa na uwezo wa kuwafikia.

"Hawatokuwa na uwezo wa kuwasiliana na mtu yoyote kutoka nje, kwa sababu hatuwezi kujua nini kinaweza kufanyika katika mawasiliano yao na watu wasioruhusiwa.

Aliongeza: "Watakuwa wanaondoka hotelini, chini ya ulinzi mkali utakaokuwa ukisindikizwa na vikosi maalum vya ulinzi, hali itaendelea mpaka mwisho wa michuano."

Shrikisho la soka la Afrika limepitisha hatua hiyo ya ulinzi wa marefa ambao utaanza kuanzia January 19 mpaka February 10

 

MECHI za KIMATAIFA: Sweden, Ibrahimovitch, waichapa England 4-2! 

>>FRANCE yaifunga ITALY, MESSI ashindwa kutamba JANGWANI, GERMANY, HOLLAND sawa!!

>>BRAZIL 2014: Japan yashinda ugenini, yachungulia safari ya Brazil!!
FIFA_LOGO_BESTWakicheza kwenye Uwanja mpya wa Friends Arena Nchini Sweden, Wenyeji Sweden waliitwanga England Bao 4-2 huku bao zote za Sweden zikifungwa na Straika hatari Zlatan Ibrahimovic.
Bao za England zilifungwa na Danny Welbeck na Caulker.
France, wakicheza ugenini, waliifunga Italy Bao 2-1 kwa bao za Valbuena na Gomis na Bao la Italy kufungwa na Stephan El Shaarawy.
Vigogo Germany na Netherlands walitoka sare ya 0-0.
Huko Jangwani Nchini Saudi Arabia, Nyota Lionel Messi jana alishindwa kuivunja rekodi nyingine ya kuifungia Nchi yake Argentina Bao nyingi ndani ya Mwaka mmoja walipotoka 0-0 na Saudi Arabia.
Nayo Brazil ilitoka 1-1 na Colombia huku Neymar akiifungia Brazil na Cuadrado akiipatia Bao Colombia.
Mabingwa wa Dunia Spain waliicharaza Panama Bao 5-1.
Katika Mechi za Mchujo za kuwania kwenda Brazil 2014 kwenye Fainali za Kombe la Dunia, Japan ilipata ushindi wa ugenini wa Bao 2-1 dhidi ya Oman na matokeo hayo yamewafanya wawe karibu kabisa kufuzu wakiwa na Pointi 13 katika Kundi B huku Timu ya Pili, Australia, ikiwa na Pointi 5 tu.
MECHI ZA KIMATAIFA ZA KIRAFIKI:
MATOKEO:
Jumatano Novemba 14
Kuwait 1 Bahrain 1
Rwanda  2 Namibia 2
Niger  1 Senegal 1
Angola v Congo
Lesotho v Mozambique
Tanzania 1 Kenya 0
Congo, DR 0 Burkina Faso 1
South Korea 1 Australia 2
Cape Verde 0 Ghana 1
China 1 New Zealand 1
Malaysia 1 Hong Kong 1
Georgia  0 Egypt 0
Russia  2 United States 2
United Arab Emirates 2 Estonia 1
Bulgaria 0 Ukraine 1
Czech Republic 3 Slovakia 0
Andorra  0 Iceland 2
Macedonia 3  Slovenia 2
Algeria  0 Bosnia And Herzegovina 1
Cyprus 0 Finland 3
Israel 1 Belarus 2
Armenia 4 Lithuania 2
Saudi Arabia 0 Argentina 0
Tunisia 1 Switzerland 2
South Africa 0 Zambia 1
Liechtenstein 0 Malta 1
Morocco 0 Togo 1
Romania 2 Belgium 1
Chile 1 Serbia 3
Turkey 1 Denmark 1
Luxembourg 1 Scotland 2
Austria 0 Ivory Coast 3
Hungary 0 Norway 2
Gabon 2 Portugal 2
Sweden 4 England 2
Netherlands 0 Germany 0
Poland  1 Uruguay 3
Ireland 0 Greece 1
Albania 0 Cameroon 0
Italy  1 France 2
Alhamisi Novemba 15
Panama 1 Spain 5
Honduras 0 Peru 0
Paraguay 3 Guatemala 1
Brazil 1 Colombia 1
Venezuela 1 Nigeria 3
Bolivia  1 Costa Rica 1
KOMBE LA DUNIA Brazil 2014: Bara la Asia=MCHUJO
Jumatano Novemba 14
Oman 1 Japan 2
Iraq 1 Jordan 0
Qatar 1 Lebanon 0
Iran 0 Uzbekistan 1
Msimamo:
Kundi A:
1 Uzbekistan Mechi 5 Pointi 8
2 South Korea Mechi 4 Pointi 7
3 Iran Mechi 5 Pointi 7
4 Qatar Mechi 5 Pointi 7
5 Lebanon Mechi 5 Pointi 4
Kundi B:
1 Japan Mechi 5 Pointi 13
2 Australia Mechi 4 Pointi 5
5 Iraq Mechi 5 Pointi 5
3 Oman Mechi 5 Pointi 5
4 Jordan Mechi 5 Pointi 4
 

MAN UNITED: Deni lao lapungua!!

Deni ambalo linaikabili Manchester United limeshuka kwa Asilimia 18 baada ya Klabu hiyo kuuza Hisa kwenye Soko la Hisa la New York na kuongeza Mapato kupitia Udhamini mpya na kulifanya Deni hilo liporomoke toka Pauni Milioni 436.9 hapo Juni 30 na kufikia Pauni Milioni 359.7 mnamo Septemba 30.
MAN_UNITED_WALLKwa mujibu wa Takwimu za Mahesabu zilizotolewa leo zinaonyesha Man United ilipata Faida ya Pauni Milioni 20.5 kwa Kipindi cha Miezi mitatu iliyoishia Septemba 30.
Mapato ya Kibiashara kwa Klabu yako kwenye malengo na yanategemewa kufikia si chini ya Pauni Milioni 350 Milioni kwa Mwaka huu wa Fedha baada ya kukua kwa Asilimia 24.
Katika Miezi hiyo mitatu, Wadhamini 10 waliingia Mkataba na Klabu ikiwa ni pamoja na Kampuni kubwa ya Magari huko Marekani General Motors ambayo Nembo ya Gari lake la aina ya Chevrolet itaanza kuoneka kwenye Jezi za Man United kuanzia Msimu wa Mwaka 2014/15.
Licha ya kutotwaa Taji lolote Msimu uliopita, Man United Msimu huu ndio inaongoza Ligi Kuu England na tayari imesonga mbele kwenye Raundi nyingine ya UEFA CHAMPIONZ LIGI huku ikiwa na Mechi mbili mkononi na pengine hii ni kwa sababu ya kuimarisha Kikosi kwa kuwanunua Wachezaji wapya.
Man United imewanunua Shinji Kagawa, Nick Powell na Robin van Persie.
Man United inamilikiwa na Familia ya Kimarekani ya kina Glazer ambao walinunua Mwaka 2005 kwa kutumia Mikopo toka Benki mbalimbali na kuiingiza Klabu hii ambayo ilianzishwa Mwaka 1878 kwenye Deni kubwa ingawa ina Mapato makubwa Kibiashara.
HUKO NYUMA==
TULIANDIKA: Jumanne, 16 Novemba 2010 20:25
Wadau wa Manchester United, hasa Kikundi cha Mashabiki kiitwacho MUST [Manchester United Supporters Turst] kimekuwa kikiwapinga Familia ya Glazer kwa kuitumbukiza Man United kwenye deni na wasiwasi huo ulisababisha kuibuka kwa upinzani uliotaka kuwabwaga Familia hiyo ya Kimarekani na Mashabiki wakivaa Jezi za Kijani na Dhahabu wakati wa mechi za Man United.GREEN_n_GOLD_OF_MAN_UNITED
Rangi za kijani na dhahabu ni rangi za Klabu ya Newton Heath iliyoanzishwa mwaka 1878 na hapo tarehe 26 Aprili 1902 kubadilishwa jina kuitwa Manchester United na rangi kuwa nyekundu, nyeusi na nyeupe zinazotumiwa mapaka sasa.
Newton Heath ilianzishwa na Wafanyakazi wa Depo iliyokuwepo eneo lla Newton Heath la Reli ya Lancashire na Yorkshire..
Mwaka 2005 Familia ya Matajiri kutoka Florida Marekani iitwayo Glazer iliinunua Manchester United na kuiingiza kwenye deni kubwa ambalo, ingawa Menejimenti ya Klabu inadai hilo deni ni kitu cha kawaida na uwezo wa kulilipa upo, Washabiki hawapendeziwi nalo na wameanzisha upinzani mkubwa kwa Familia ya Glazer.
Ndio maana Mashabiki, kwenye mechi za Manchester United, wanavaa skafu, fulana na kofia rangi za kijani na dhahabu ikiwa ni alama ya chimbuko la Manchester United, Klabu ya Newton Heath iliyoanzishwa na Wafanyakazi makabwela wa Depo ya Reli.
Nje ya Uwanja wa Old Trafford fulana za rangi hiyo ya kijani na dhahabu huuzwa huku nyuma zina maandishi [Shairi la Kiingereza] na tafsiri ya haraka ni:
“Roho ya United haiuzwi, Ndio maana kwa fahari tunavaa Kijani na Dhahabu,
Hatutavaa ile Jezi Nyekundu inayosifika, Mpaka Glazer waondoke au wafe,
Hivyo inua viwango vya zamani juu, Kwa Kijani na Dhahabu tutaishi na kufa,
Na hakika siku itafika tena, Tutakapovaa Nyekundu yetu kwa mara nyingine tena!”

GOLI BORA DUNIANI 2012: FIFA yatangaza Wagombea 10!


>>MESSI, NEYMAR wamo, RONALDO hana Bao!!
>>KUPIGIWA KURA, Mshindi kujulikana Januari 7, 2013!!
NEYMAR_v_MESSIZile mbio za kumpata Mshindi wa Tuzo ya FIFA ya PUSKAS kwa ajili ya GOLI BORA la MWAKA zimeanza leo kwa kutangazwa Wagombea 10 na Mabao yao bila ya Jina la Mshindi wake wa kwanza kabisa wa Tuzo hiyo, Cristiano Ronaldo, kuwemo.
Mashabiki Dunia nzima ndio watapiga Kura kuamua lipi Goli Bora kati ya Mabao 10 yaliyoteuliwa na Wataalam wa FIFA.
Mchujo wa kupata Magoli matatu Bora utakamilika hapo Novemba 29 na itaanza Kura nyingine kuchagua Goli Bora kati ya hayo matatu ambapo Mshindi atatangazwa Januari 7, 2013, Siku ambayo pia Dunia itamjua nani atatwaa Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani, FIFA Ballon d’Or.
Tuzo ya FIFA ya PUSKAS kwa ajili ya GOLI BORA la MWAKA ilianzishwa Mwaka 2009 na Mshindi wake wa kwanza ni Cristiano Ronaldo alipofunga Bao katika Mechi ya Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ya Manchester United dhidi ya FC Porto.
+++++++++++++++++++++++++++++
WASHINDI WALIOPITA:
-2011==Neymar: Goli Santos v Flamengo
-2010==Giovanni van Bronckhorst: Goli Netherlands v Uruguay
-2009==Cristiano Ronaldo: Goli Man United v FC Porto
+++++++++++++++++++++++++++++
Tuzo hii ya Puskas ni kwa heshima na kumbukumbu ya Ferenc Puskás, Nahodha na Nyota wa Hungary katika Miaka ya 1950.
WAGOMBEA GOLI BORA:
Agyemang BADU (Ghana - Guinea 1 February 2012)
Hatem BEN ARFA (Newcastle United - Blackburn Rovers 7 January 2012)
Radamel FALCAO (América de Cali - Atletico Madrid 19 May 2012)
Eric HASSLI (Vancouver Whitecaps - Toronto FC 16 May 2012)
Olivia JIMENEZ (Mexico - Switzerland 22 August 12)
Gastón MEALLA (Nacional Potosí - The Strongest 29 January 2012)
Lionel MESSI (Brazil - Argentina 9 June 2012)
NEYMAR (Santos - Internacional 7 March 2012)
Moussa SOW (Fenerbahce - Galatasaray 17 March 2012)
Miroslav STOCH (Fenerbahçe - Gençlerbirliği 3 March 2012

BPL: Kilingeni Jumamosi, kuanza DABI ya London Arsenal v Spurs!!

WALCOTT_WILSHERE_OX
>>DABI hii ni MSHIKEMSHIKE kwa WENGER na VILLAS-BOAS!!!
Baada ya Mechi za Kimataifa za Kirafiki za katikati ya Wiki, Wikiendi hii Ligi Kuu England, BPL, inarudi kwa kishindo na Mechi ya kwanza kabisa Siku ya Jumamosi ni Dabi ya Jiji la London kati ya Arsenal na Tottenham itakayochezwa Uwanja wa Emirates na Mechi ya mwisho Siku hiyo hiyo ni kati ya Norwich City na vinara wa Ligi Manchester United itakayochezwa Uwanja wa Carrow Road.
+++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumamosi, Novemba 17, 2012
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Arsenal v Tottenham Hotspur
[SAA 12 Jioni]
Liverpool v Wigan Athletic
Manchester City v Aston Villa
Newcastle United v Swansea City
Queens Park Rangers v Southampton
Reading v Everton
West Bromwich Albion v Chelsea
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Norwich City v Manchester United
+++++++++++++++++++++++
Arsenal na Tottenham zitaingia kwenye Dabi hiyo huku zikiwa nafasi ya 7 kwa Tottenham na ya 8 kwa Arsenal na kila mmoja atawania ushindi ili kujiiimarisha zaidi hasa baada ya kuwa na mwendo mbovu kwenye Ligi Msimu huu.
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO Timu za juu:
1 Man United Mechi 11 Pointi 27
2 Man City  Mechi 11 Pointi 25
3 Chelsea Mechi 11 Pointi 24
4 Everton Mechi 11 Pointi 20
5 WBA Mechi 11 Pointi 20
6 West Ham Mechi 11 Pointi 18
7 Tottenham Mechi 11 17
8 Arsenal Mechi 11 Pointi 16
+++++++++++++++++++++++
Ikiwa Timu moja itafungwa basi presha kwa Mameneja, Arsene Wenger wa Arsenal na Andre Villas-Boas, itazidi na Wadau wengi watainua Mabango kukandamiza kuwa Klabu ipo mashakani.
Ndio maana Mechi hii ni muhimu mno kwa kila Klabu hasa ukizingatia mwendo wao mbovu wa hivi karibuni ambapo Arsenal wameshinda mara moja tu katika Mechi 8, tena dhidi ya Klabu ya mkian QPR, na wamefungwa jumla ya bao 12 katika Mechi zao 4 zilizopita na wenzao Tottenham wakifungwa katika Mechi 3 kati ya 4 walizocheza mwisho.
+++++++++++++++++++++++
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumapili, Novemba 18, 2012
[SAA 1 Usiku]
Fulham v Sunderland
Jumatatu, Novemba 19, 2012
[SAA 5 Usiku]
WestHam v Stoke City

MAREKEBISHO VIINGILIO SERENGETI BOYS v CONGO

 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefanya mabadiliko kwa kiingilio cha juu cha mechi ya raundi ya mwisho ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 kati ya Tanzania (Serengeti Boys) na Congo Brazzaville itakayochezwa Jumapili (Novemba 18 mwaka huu). Awali kiingilio cha juu katika mechi hiyo itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni kilikuwa sh. 5,000. Lakini kwa lengo la kuwafanya wadau wa kiingilio hicho kuchangia gharama za mechi hiyo sasa kutakuwa na viingilio vitatu tofauti katika viti vya VIP. Kwa VIP A ambayo ina viti 748 kiingilio kitakuwa sh. 10,000, VIP B inayochukua watazamaji 4,160 kiingilio ni sh. 5,000 wakati VIP C yenye viti 4,060 kiingilio ni sh. 2,000. Kwa sehemu nyingine (viti vya rangi ya chungwa, kijani na bluu) ambavyo jumla yake ni 48,590 kiingilio kitabaki kuwa sh. 1,000. Timu ya Congo Brazzaville kwa taarifa tulizopata awali kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu la Congo (FCF) ilikuwa iwasili jana (Novemba 13 mwaka huu) usiku. Lakini timu hiyo haikutokea na sasa tunatarajia itawasili leo (Novemba 14 mwaka huu) saa 8 mchana kwa ndege ya Ethiopian Airlines. Congo itafikia Sapphire Court Hotel. Wakati huo huo, Kamati ya Serengeti Boys itakutana na waandishi wa habari kesho (Novemba 15 mwaka huu). Mkutano huo utafanyika kuanzia saa 5 asubuhi hoteli ya JB Belmont, ukumbi wa Ngorongoro.

KATIKA MAMBO YA KUACHA WACHEZAJI NA KUENDA KATIKA TIMU NYINGINE NA KUNG'ARA NI KUTOKANA NA NINI EBU MCHEKI HUYU NDIYE ATUPELE GREEN, KINDA LILILODUNDWA YANGA LINALOIBEBA COASTAL UNION LIGI KUU


IMEKUWA bahati kwa mshambuliaji chipukizi wa Coastal Union, Atupele Green Jackson ambaye ameibukia Ligi Kuu Bara msimu huu kwa mara ya kwanza na kuwamo kwenye 'First 11' ya kikosi chake.

Atupele alisajiliwa na Coastal akitokea Yanga B na amepata bahati ya kuaminika kikosini na kuwa chaguo la kwanza la kocha Ahmed Morocco.

Nyota huyo mweusi, mrefu na ana umbo kubwa linalomfanya ajiamini na kuwa 'sumu' kwa mabeki wasumbufu.

Wataalamu wa soka nchini wanadai atakapopata uzoefu atakuja kuwa tishio na kulisaidia Taifa la Tanzania.

Kutokana na umbo lake watu humfananisha na Mtanzania, Thomas Ulimwengu anayekipiga Klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri Kidemokrasi ya Congo na wako wote katika timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20, 'Ngorongoro Heroes'.

Ametua Coastal kwa mkataba wa miaka mitatu na kwa kipindi kifupi ameonyesha uwezo wa juu katika mechi alizocheza, lakini amekumbwa na tatizo la ukame wa mabao kwani hadi sasa bado hajaziona nyavu lakini yeye anasema ni hali ya kawaida na anaamini utafika wakati wake atafunga.

Mwanaspoti lilifanya mahojiano naye kwa kirefu na anafafanua kwa undani, siri ya mafanikio, historia na malengo ya maisha yake kwa ujumla.

Sababu ya kuaminiwa
"Nafikiri ni kujituma na ushirikiano wangu mzuri na wachezaji wenzangu lakini pia kufuata maelekezo ya mwalimu," anasema Atupele anayevutiwa na nyota Didier Drogba wa Ivory Coast, Mghana Asamoah Gyan na Mbrazil Ronaldo de Lima wakati Tanzania anamhusudu Haruna Moshi 'Boban'.

Kuhusu kukosa mabao, Atupele anasema: "Sina wasiwasi kwa sababu utafika wakati wangu nami nitafunga.

"Usipofunga unaumia kujiuliza maswali mengo lakini ni hali ya mchezo tu lengo ni kuisaidia timu ifanye vizuri."

Kocha wake, Ahmed Morocco anamzungumzia mchezaji huyo kuwa ni mzuri ndiyo maana anamtumia: "Mchezaji mzuri na muhimu kikosini, kuhusu kufunga tumpe muda."

Nje ya soka
Atupele anasema anapokuwa hana majukumu na soka anapenda kuutumia muda wake mwingi kuendesha gari.
"Napenda sana kuendesha gari na ndiyo furaha yangu ninapokuwa nje ya kazi za mpira," anaeleza.

Pamoja na kupenda kuendesha gari, Atupele anaongeza kuwa bado hajanunua la kwake binafsi na mara nyingi hutumia la rafiki yake, Kiggi Makassy anayekipiga Simba.

Hata hivyo, mpango wake kama mambo yake yataenda vizuri, malengo yake ni kununua gari.

Alifanyiwa usaili na Kondic
Kinda huyo anasema kipaji chake ni cha tangu utotoni na alipata umaarufu akiwa Shule ya Msingi ya Lugalo.
Ni zao la shule ya vipaji ya Global Soccer Academy ambayo ilianzishwa na Wazungu na walikuwa wanadhaminiwa na Kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom.

Alijiunga na kituo hicho akiwa mwanafunzi wa Shule ya Kambangwa kabla ya kutua Yanga.

Alichaguliwa na Yanga baada ya kufanyiwa usaili na kocha wa zamani wa Yanga, Mserbia Dusan Kondic.

"Nilijiunga Yanga baada ya kufanyiwa usaili na kocha Kondic. Tulichukuliwa vijana wote tukaunganishwa na Yanga B tukacheza mechi na timu ya wakubwa nikafanya vizuri na ndipo nikachaguliwa," anaongeza.

Atupele anasema alishawishika kujiunga na Yanga baada ya ushauri kutoka kwa rafiki yake aliyemtaja kwa jina la Hamad Kibopile, ambaye pia alikuwa anaichezea Yanga B.

"Yeye alikuwa anachezea Yanga B na aliponiona Globo akanishawishi nijiunge na Yanga."

Sababu ya kuondoka Yanga
Atupele alihamia Coastal Union baada ya kutofautiana na Yanga kwa masuala ya mkataba.

"Nilihama Yanga baada ya kutofautina kwenye masuala ya mkataba nami ni mchezaji nikaamua kuja kutafuta maisha,"anasema Atupele na kugoma kuongelea kwa undani.

Hata hivyo, licha ya Atupele kutoingia kwa undani kuhusu suala hilo, Mwanaspoti linafahamu kuwa mtafaruku wao ulisababishwa na fedha za usajili kutokwenda sawa na makubaliano waliyopatana.

Atupele aliona pesa hiyo haitoki kama walivyopatana licha ya kuwa tayari alishasaini mkataba kwa ajili ya msimu huu wa 2012-2013 wa Ligi Kuu Bara na alipodai Yanga wakaona isiwe tabu wakamalizana kwa kuuchana.

Atupele ameenda mbali na kusema, endapo Yanga itamhitaji kwa mara nyingine hana tatizo wakikubaliana na uongozi wake kwani anachoangalia ni maslahi.

Anavyoizungumzia Coastal na Taifa Stars
"Coastal ni bora na ina malengo kwenye ligi hii na mambo yakienda sawa tunaamini tutamaliza tukiwa katika nafasi tatu za juu."

Safu ya ushambuliaji ya Coastal ina matatizo baada ya kuwakosa Nsa Job, ambaye ni majeruhi wa mguu pamoja na Pius Kisambale aliyefanyiwa upasuaji.

"Ni pengo kuwakosa wachezaji mliozoeana kucheza kitimu lakini wapo wengine wataziba mapengo."

Historia
Atupele amezaliwa katika familia yenye watoto watano na yeye ni wa nne. Mama yake, Doto Ludete alimzaa yeye pamoja na ndugu zake Kassim, Asha, Abdallah na Tatu.

Atupele amefafanua sababu ya kutofautiana majina na ndugu zake hao kuwa imechangiwa na kuwa na mama na baba tofauti.

Alisoma shule ya Msingi Lugalo na kumalizia Sekondari ya Kambangwa. Hajaoa na hana mtoto.
ATUPELE GREEN JACKSON 
Amezaliwa: Agosti 30,1994
Mahali: Lugalo, Dar es Salaam
Klabu: Yanga 'B' 2009-2012,
Coastal Union 2012-
Taifa: Tanzania

NASSIBU RAMADHANI NA FRANSIC MIYAYUSHO KUGOMBANIA UBINGWA WA WBF DESEMBA 9


Mabondia Nassibu Ramadhani na Fransic Miyayusho wakitunishiana misuri wakati wa kutambulisha mpambano wao wa ubingwa wa WBF utakaofanyika Desemba 9 katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mwandaji wa mpambano wa ubingwa wa WBF Mohamed Bawazir katikati akiwa ameshika mkanda na mabondia Nassibu Ramadhani kushoto na Fransic Miyayusho kulia wengine kulia ni Rais wa PST Emanuel Mlundwa ambao na wasimamizi wa mpambano huo na Kushoto ni Mratibu Paul Kunanga na Kocha wa Nasibu Christopher Mzazi

Mabondia Nassibu Ramadhani na Fransic Miyayusho wakitunishiana misuri wakati wa kutambulisha mpambano wao wa ubingwa wa WBF utakaofanyika Desemba 9 katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mabondia Nassibu Ramadhani na Fransic Miyayusho wakitunishiana misuri wakati wa kutambulisha mpambano wao wa ubingwa wa WBF utakaofanyika Desemba 9 katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


KAMPUNI YA Darworld Links imeandaa mpambano mwingine wa ubingwa wa masumbwi utakaowakutanisha bondia Nassibu Ramadhani na Fransic Miyayusho mpambano utakaofanyika katika Ukumbi wa PTA Sabasaba akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Mohamed Bawazir


Amesema amewakutanisha mabondia hawo kutaka kujua nani zaidi ya mwenzake kwa kuwa viwango vyao vina fanana na vinatambulika kimataifa hivyo amewataka watanzania kujitokeza kuwapa sapoti hususani kudhamini mchezo huo wa masumbwi ata kwa bondia mmoja mmoja kuwagea changamoto mbalimbali mabondia hawa vijana wana uwezo mkubwa wa kutangaza biashara mbalimbali kupitia mchezo wao wa masumbwi kwani makampuni mengi yamekuwa yakiupiga danadana mchezo huu ni mchezo kama michezo mingine nashangaa sana kuona tunakosa


Udhamini tunapoomba sehemu ya makampuni mbalimbali ukienda wanasema hatuhusiki na mchezo huo.

Wengine wanasema kabisa wadhamini wa michezo wakati wanabagua michezo mingine kama ngumi awapewi kipaumbele kabisaa
amewaomba wapenzi na mashabiki kujitokeza siku tarehe 9 Desemba kuja kuangalia ngumi ili zisonge mbele watakaosindikiza mpambano huo wa masumbwi ni 
Fadhili Majia VS Juma Fundi

Moh'd Rashid Matumla VS Doi Miyayusho

Ibrahimu Class 'King Class Mawe' VS Said Mundi wa Tanga

Fred Sayuni VS Deo Samweli

Hassani Kidebe VS Baina Mazola


Mapambano yote ya utangulizi ni mazuri na vijana wanaotakiwa kuendelezwa katika elimu ya masumbwi Duniani ili wawe mabondia wazuri 


Mpambano huo umedhaminiwa na JB BELMONT HOTEL gazeti la Jmbo Leo, Times FM


Na wengine wameobwa kujitokeza katika udhamini huo kwa mawasiliano zaidi 

0716 332933

0784 426542

 

DESEMBA ni HEKAHEKA kwa Chelsea, kusakamwa na Mechi mfululizo!


CLATTENBURG_na_CHELSEA>>Desemba wapo Japan Klabu Bingwa Duniani!!!
>> LAKINI ROBERTO DI MATTEO asifia ukubwa wa Kikosi chake!!
Roberto Di Matteo ana imani na Kikosi chake cha Chelsea kukabili lundo la Mechi, hasa Mwezi Desemba, ambapo watacheza jumla ya Mechi 8 hadi 9, zikiwemo za Mashindano ya FIFA ya Klabu Bingwa Duniani huko Japan.
Pamoja Mashindano hayo ya Japan, wana Mechi za Ligi Kuu England, UEFA CHAMPIONZ LIGI na CAPITAL ONE CUP lakini kati ya hizo ni mbili tu watacheza Stamford Bridge.
Ingawa Di Matteo amekiri kuwa Mechi hizo zitawabana sana lakini amesema: “Zitatubana sana na hizi za Japan ni safari ndefu, upande wa pili wa Dunia na tutabadili majira lakini inabidi kuikabili hali. Tuna Kikosi kikubwa na nadhani tutaidhibiti hali yeyote.”
RATIBA MECHI za CHELSEA:
Novemba 2012
Novemba 17 WBA v Chelsea [BPL]
Novemba 20 Juventus v Chelsea [UEFA CHAMPIONZ LIGI]
Novemba 25 Chelsea v Man City [BPL]
Novemba 28 Chelsea v Fulham
Desemba 2012
Desemba 1 West Ham v Chelsea [BPL]
Desemba 5 Chelsea v Nordsjaelland [UEFA CHAMPIONZ LIGI]
Desemba 8 Sunderland v Chelsea [BPL]
Desemba 13 Bingwa Asia v Chelsea [Japan, FIFA Klabu Bingwa Duniani]
Desemba 16 Mechi Mshindi wa 3 AU FAINALI [Japan, FIFA Klabu Bingwa Duniani]
Desemba 19 Leeds United v Chelsea [CAPITAL ONE CUP]
Desemba 23 Chelsea v Aston Villa [BPL]
Desemba 26 Norwich v Chelsea [BPL]
Desemba 30 Everton v Chelsea [BPL]
Januari 2013
Chelsea v QPR [BPL]

BARUA YA WAZI KUTOKA KWA WADAU WA SOKA KWENDA TENGA KWA UKIUKWAJI WA KATIBA YA TFF

-->
Bwana Leodger Chilla Tenga
Rais wa TFF
Ndugu Tenga,
YAH: UKIUKWAJI WA KATIBA YA TFF
Sisi wadau wa mpira wa miguu Tanzania tunakuandikia barua hii tukiwa na uchungu mkubwa kuhusu mwenendo wa uongozi wako.  Ulipoingia madarakani kwa mara ya kwanza Golden Tulip tarehe 27 Desemba 2004 ulitoa matumaini makubwa kuhusu kuleta mabadiliko makubwa katika uendeshaji wa mpira wetu.  Pamoja na mapungufu mengi yaliyojitokeza ndani ya miaka minane ya uongozi wako haya mawili tutakayoyaeleza hapa chini hayawezi kufumbiwa macho na wanaoutakia mema mpira wa Tanzania.
1.     Kupitisha muda wa uongozi wako bila kibali cha mkutano mkuu.
Mkutano mkuu uliokuingiza madarakani ulifanyika siku ya Jumapili tarehe 14 Desemba 2008.  Kifungu 33(1) cha Katiba ya TFF kinatamka kuwa kipindi cha uongozi ni miaka minne tu.  Hivyo ukomo wa uongozi wako na kamati yako ya utendaji ni saa sita za usiku tarehe 13 Desemba 2012.  Aidha kifungu cha 10(1) cha kanuni za uchaguzi wa TFF kinatamka kuwa tangazo la uchaguzi litatolewa siku 40 kabla ya uchaguzi.  Kwa mantiki hii kamati yako ya uchaguzi ilitakiwa itangaze tarehe ya uchaguzi siku ya Jumatatu tarehe 05 Novemba 2012 au kabla ya hapo.   Leo ni tarehe 13 Novemba 2012 na ofisi yako iko kimya!  Hii haikubaliki, haiwezekani ujiongezee muda wa uongozi bila kibali cha Mkutano Mkuu.  Tutawaomba wajumbe wa Mkutano Mkuu wakuadhibu kwa kosa hili la ukiukwaji wa Katiba.  Pamoja na mapungufu haya ni vyema ukatufahamisha uchaguzi umepanga ufanyike lini au unasubiri wajumbe wa mkutano mkuu wakulazimishe kwa maandishi?
2.     Kufuta nafasi ya Makamu wa Pili wa Rais wa TFF
Yapo maneno yanasemwa eti uongozi wako unataka kufuta nafasi ya pili ya Makamu wa Rais wa TFF kinyemela.  Kama tuhuma hizi ni za kweli tunaoma tukukumbushe yafuatayo:
2.1.1      Nafasi ya makamu wa pili wa Rais wa TFF iko ndani ya Katiba ya TFF kifungu 31(1)
2.1.2      Kifungu cha katiba 30(1) kinatamka wazi kuwa ni mkutano mkuu pekee wenye mamlaka ya kubadili Katiba ya TFF.  Hivyo hakuna njia mbadala ya kubadili Katiba ya TFF.
2.1.3      Kifungu cha Katiba 30(2) kinatamka kuwa tangazo lolote la nia ya kubadili Katiba ya TFF litatolewa siku 45 kabla ya mkutano mkuu.  Uongozi wako utawezaje kutoa tangazo hili ndani ya kipindi cha uongozi wako kilichobakia?
2.1.4      Kifungu cha Katiba 30(6) kinatamka kuwa ombi la kubadili katiba litapigiwa kura NDANI YA MKUTANO MKUU na ili lipite theluthi mbili ya wajumbe sharti iridhie.  Zingatia utashi huu wa Katiba.
Bwana Tenga kama kweli wazo hili lipo basi achana nalo, usijidhalilishe kwa kukiuka Katiba iliyokuweka madarakani.  Nafasi za uongozi katika uchaguzi ujao zitangazwe kwa mujibu wa Katiba iliyokuweka madarakani.  Kama kuna umuhimu wa kubadili Katia hakuna uharaka wowote, subiri awamu ijayo ifanyie kazi wazo hilo, awamu ambayo huenda wewe mwenyewe ukaingoza pia kama ukigombea tena.
Tunasubiri majibu ya hoja zetu za majibu haya tunaomba uwajulishe watanzania wote.
Nakala ya barua hii tunawapelekea wajumbe wote wa Mkutano Mkuu kwa taarifa.
Ni sisi kwa niaba ya wadau wa mpira wa Tanzania.

TAIFA STARS YAIVAA HARAMBEE KIRUMBA KATIKA MZANI WA FIFA LEO

Taifa Stars

TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo inashuka dimbani kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kumenyana na Kenya, Harambee Stars katika mchezo wa kirafiki, ulio kwenye kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Tanzania inakutana na Kenya, zikiwa hazitofautiani sana kwa sasa, japokuwa Harambee inajivunia wachezaji kadhaa wanaocheza soka ya ushindani Ulaya.
Taifa Stars, inayofundishwa na Mdenmark Kim Poulsen, aliyeanza kazi Mei mwaka huu, akirithi mikoba ya Jan Borge Poulsen kutoka Denmark pia, haijashinda mechi yeyote tangu iifunge Gambia 2-1 Juni 10, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 Brazil.
Chini ya Kim, aliyepandishwa kutoka timu za vijana za Tanzania, kazi aliyoanza Aprili mwaka jana, ilitoka sare ya 1-1 Juni 17, ilitolewa na Msumbji kwa mikwaju ya penalti katika mchezo wa kuwania kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani Afrika Kusini, kufuatia sare ya jumla ya 2-2.
Ilijitupa uwanjani mara ya mwisho, katika mchezo wa kirafiki, Agosti 15, mwaka huu mjini Gaborone na kulazimishwa sare ya kufungana mabao 3-3, tena ikitoka nyuma na kusawazisha.
Kenya inayofundishwa na Mfaransa Henri Michel, mara ya mwisho kushinda mechi ilikuwa ni Julai 12, mwaka huu ilipoichapa Botswana nyumbani kwake, Gaborone, mabao 3-1, lakini Harambee Stars katika mechi yao ya mwisho waliyocheza, walifungwa 2-1 nyumbani na Afrika Kusini Oktoba 16, mwaka huu, huo ukiwa mchezo wa kirafiki.
Mchezo huo, unatarajiwa kuinufaisha zaidi timu ya Bara, Kilimanjaro Stars, yenye wachezaji wengi kwenye kikosi hicho, kwani baada ya hapo itaingia kambini kujiandaa na michuano ya Tusker Challenge 2012, itakayofanyika mjini Kampala, Uganda mwishoni mwa mwezi huu. Kenya pia itashiriki michuano hiyo ya Challenge.
Wakati Kenya iliwasili Mwanza jana, Tanzania walianza kujikusanya kambini Jumapili na hadi kufikia juzi kikosi kilikuwa kimekwishakamilika.
Wachezaji walioitwa kwa ajili ya mechi hiyo ni makipa Juma Kaseja (Simba SC) na Deogratius Mushi ‘Dida’ wa Azam FC.
Mabeki; Kevin Yondan (Yanga), Aggrey Morris, Erasto Nyoni (Azam FC), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Nassoro Masoud ‘Cholo’, Shomari Kapombe na Amir Maftah (Simba).
Viungo; Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (Azam FC), Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto, Ramadhan Singano ‘Messi’ na Mrisho Ngassa (Simba), Athuman Iddi ‘Chuji’, Frank Domayo (Yanga) na Shaaban Nditi (Mtibwa Sugar).
Washambuliaji; John Bocco ‘Adebayor’ (Azam FC), Simon Msuva (Yanga), Christopher Edward (Simba), Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wa (TPM, DRC).
REKODI YA STARS MWAKA HUU NA RATIBA YA MECHI ZIJAZO:
Februari 23, 2012
Tanzania 0 – 0 DRC (Kirafiki)
Februari 29, 2012
Tanzania 1 – 1 Msumbiji   (Kufuzu Mataifa ya Afrika)
Mei 26, 2012
Tanzania 0 – 0 Malawi
Juni 2, 2012
Ivory Coast 2 – 0 Tanzania (Kufuzu Kombe la Dunia)
Juni 10, 2012
Tanzania 2 – 1 Gambia      (Kufuzu Kombe la Dunia)
Juni 17, 2012
Msumbiji 1 – 1 Tanzania   (Tanzania ilitolewa kwa penalti kufuzu Mataifa ya Afrika)
Agosti 15, 2012
Botswana 3 – 3 Tanzania (Kirafiki)
Novemba 14, 2012
Tanzania Vs Kenya (Kirafiki)
Machi 22, 2013
Tanzania Vs Morocco (Kufuzu Kombe la Dunia)
Juni 7, 2013
Morocco Vs Tanzania (Kufuzu Kombe la Dunia)
Juni 14, 2013    
Tanzania Vs Ivory Coast    (Kufuzu Kombe la Dunia)
Septemba 6, 2013
Gambia    Vs Tanzania (Kufuzu Kombe la Dunia)

STARS YAHAMASISHWA KUSHINDA LEO DHIDI YA HARAMBEE STARS

Kim Poulsen akiongoza mazoezi ya Stars Uwanja wa Kirumba Mwanza leo 

MDHAMINI wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania,  Taifa Stars, Kilimanjaro Premium Lager amewataka wachezaji wa timu hiyo kuonyesha nidhamu ya hali ya juu wakiwa kambini Mwanza na pia kuhakikisha wanapata ushindi katika mechi zijazo hususani katika mechi ya Jumatano ya kirafiki dhidi ya Harambee Stars.
Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe, amesema wao kama wadhamini wana imani na timu ya taifa na Kocha wake Kim Poulsen.
“Mechi zilizochezwa mpaka sasa hivi tangu tumechukua udhamini zinaridhisha kwa kuwa tumeona kiwango cha timu kikikua siku hadi siku..tuna imani mechi ya Jumatano dhidi ya Harambee Stars tutashinda,” slisema Bwana Kavishe.
Alisema moja ya vitu ambavyo wachezaji wanatakiwa kuzingatia sana ni nidhamu nje na ndani ya uwanja kwani mpira ndio ajira yao kwa hivyo lazima waitetee na kuilinda vizuri.
“Kocha wa sasa hivi anazingatia sana nidhamu na hili lina umuhimu sana katika soka hata uwende wapi duniani..unaweza kuwa mchezaji mzuri sana lakini bila nidhamu kocha anaweza kukuacha katika kikosi chake na kuwachezesha wachezaji wenye nidhamu,” alisema.
Bwana Kavishe aliendelea kusema kuwa wamefurahishwa na kitendo cha TFF kuipeleka timu Mwanza kucheza mechi ya kirafikii dhidi ya Kenya na pia kujiandaa na mashindano ya CECAFA Challenge yanayotarajia kuanza Jijini kampala tarehe 24 mwezi huu.
“Hali ya hewa ya Mwanza na ya Kampala hazipishani sana kwa hivyo tunaamini huu ulikuwa uamuzi sahihi kabisa ili wachezaji wazoee hali ya hewa, alisema.
Stars inashuka dimbani Jumatano saa kumi alasiri dhidi ya Harambee Stars ya Kenya katika Uwanja wa Kirumba. Tangu Stars ipate mdhamini mpya, Kilimanjaro Premium Lager, imeshacheza dhidi ya Ivory Coast, Msumbiji, Botswana na Namibia .
Kilimanjaro Premium Lager imewekeza zaidi ya Shilingi bilioni mbili kuidhamini Taifa Stars kwa miaka mitano ijayo.

HARAMBEE WAWASILI MWANZA, STARS WAFANYA MAZOEZI YA MWISHO KIRUMBA KABLA YA MECHI KESHO

 Baadhi ya wachezaji wa Harambee Stars wakiwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza kwa ajili ya pambano lao la kirafiki dhidi ya Taifa Stars.mchezo utakao chezwa jimatano katia uwanja wa ccm kirumba mwanza

 Baadhi ya wachezaji wa Harambee Stars wakiwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza kwa ajili ya pambano lao la kirafiki dhidi ya Taifa Stars.mchezo utakao chezwa jimatano katia uwanja wa ccm kirumba mwanza

Baadhi ya wachezaji wa Harambee Stars wakiwasili katika hotel ya G&G Jijini Mwanza walikopangiwa ambapo timu hiyo itajipima nguvu na Taifa Stars kwenye uwanja wa CCM Kirumba katika mchezo wa kupimana nguvu .


 Baadhi ya wachezaji wa Harambee Stars wakichangamkia juisi baada ya kuwasili katika hotel ya G&G Jijini Mwanza jana. (Picha zote na George Ramadhan

Golikipa na Nahodha wa Taifa Stars Juma Kaseja akijifua na kipa mwenzake wa Taifa Stars, Deogratius Munisi (Dida) kwenye uwanja wa CCM Kirumba katika matayarisho ya mchezo wao na Harambee  ya kenya
 

Kocha Mkuu wa Taifa Stars Kim Poulsen akimpa maelekezo Mbwana Samatta wakati wa mazoezi ya timu hiyo juzi kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.katika mazoezi

Kocha Mkuu wa Taifa Stars Kim Poulsen akitoa maelekezo kwa wachezaji John Boko (kulia) na Amri Kiemba wakati wa mazoezi ya timu hiyo kwenye uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza

 
 
 Kikosi cha Harambee Stars kikifanyishwa mazoezi na kocha wake Henri Michel
 
Harambee Stars itawatumia Dennis Oliech(nahodha), Ayub Timbe Masika, Brian Mandela Onyango (Santos), Patrick Oboya, Mzee Patrick Ooko Osiako, Jerry Santo, Fredrick Jerim Onyango Oduor, Edwin Simiyu Wafula (AFC Leopards) na Eugene Ambuchi Asike (Sofapaka).

Wengine ni Geofrey Kokoyo Odhiambo, Mulinge Ndeto, Christopher Wekesa Nyangweso, James Wakhungu Situma (Sofapaka), Peter Odhiambo Opiyo, Charles Elphas Okwemba,  Francis Kahata Wambura (Thika United), Andrew Kiriro Tololwa, Osborne Monday (Sofapaka), Wesley Kemboi na Moses Arita.

AFCON 2013: Marefa kupigwa ‘KARANTINI!!’


AFCON_2013-NORMALMarefa watakaochezesha Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2013, huko Afrika Kusini zitakazoanza Januari 19 na kumalizika Februari 10, Mwaka 2013, watatengwa na kadamnasi ili kuepusha upangaji matokeo Mechi.
Kamati Maalum ya Nchi ya Afrika Kusini inayoshughulikia maandalizi ya Fainali hizo, ambayo iko chini ya Bwana Mvuso Mbebe, imesema watatumia taratibu za ulinzi wa aina ile ile uliotumika kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2010 zilizochezwa Nchini Afrika Kusini.
Mvuso Mbebe, akiongea na Kamati ya Bunge la Afrika Kusini, ametamka: “Tutatumia njia ile ile iliyotumika kwenye Fainali za Kombe la Dunia. Marefa watakaa karantini kwenye Hoteli ambayo Watu wengine hawatarhusiwa kuingia. Watasindikizwa na Walinzi kwenda popote na kwenye Mechi.”
Taratibu hizi za kuwapiga ‘Karantini’ Marefa zimeafikiwa na CAF.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
MAKUNDI:
KUNDI A: South Africa, Cape Verde, Morocco, Angola
KUNDI B: Ghana, DR Congo, Niger, Mali
KUNDI C: Zambia, Ethiopia, Nigeria, Burkina Faso
KUNDI D: Ivory Coast, Togo, Tunisia, Algeria
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
VIWANJA:
-Soccer City, Johannesburg [Mashabiki 94,700]
-Moses Mabhida Stadium, Durban [Mashabiki 54,000]
-Nelson Mandela Bay Stadium, Port Elizabeth [Mashabiki 48,000]
-Mbombela Stadium, Nelspruit [Mashabiki 41,000]
-Royal Bafokeng Stadium, Rustenburg [Mashabiki 42,000]
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumamosi Januari 19
South Africa v Cape Verde Islands [Soccer City Saa 1 Usiku]
Angola v Morocco [Soccer City Saa 4 Usiku]
Jumapili Januari 20
Ghana v Congo DR [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 12 Jioni]
Mali v Niger Nelson Mandela Bay Stadium 20:00
Jumatatu Januari 21
Zambia v Ethiopia [Mbombela Stadium Saa 12 Jioni]
Nigeria v Burkina Faso [Mbombela Stadium Saa 3 Usiku]
Jumanne Januari 22
Ivory Coast v Togo [Royal Bafokeng Stadium Saa 12 Jioni]
Tunisia v Algeria [Royal Bafokeng Stadium Saa 3 Usiku]
Jumatano Januari 23
South Africa v Angola [Moses Mabhida Stadium Saa 12 Jioni]
Morocco v Cape Verde Islands [Moses Mabhida Stadium Saa 3 Usiku]
Alhamisi Januari 24
Ghana v Mali [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 12 Jioni]
Niger v Congo DR [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 3 Usiku]
Ijumaa Januari 25
Zambia v Nigeria [Mbombela Stadium Saa 12 Jioni]
Burkina Faso v Ethiopia [Mbombela Stadium Saa 3 Usiku]
Jumamosi Januari 26
Ivory Coast v Tunisia [Royal Bafokeng Stadium Saa 12 Jioni]
Algeria v Togo [Royal Bafokeng Stadium Saa 3 Usiku]
Jumapili Januari 27
Morocco v South Africa [Moses Mabhida Stadium Saa 2 Usiku]
Cape Verde Islands v Angola [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 2 Usiku]
Jumatatu Januari 28
Congo DR v Mali [Moses Mabhida Stadium Saa 2 Usiku]
Niger v Ghana [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 2 Usiku]
Jumanne Januari 29
Ethiopia v Nigeria [Royal Bafokeng Stadium Saa 2 Usiku]
Burkina Faso v Zambia [Mbombela Stadium Saa 2 Usiku]
Jumatano Januari 30
Algeria v Ivory Coast [Royal Bafokeng Stadium Saa 2 Usiku]
Togo v Tunisia [Mbombela Stadium Saa 2 Usiku]
ROBO FAINALI
Jumamosi Februari 2
Mshindi Kundi B v Mshindi wa Pili Kundi A [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 12 Jioni]
Mshindi Kundi A v Mshindi wa Pili Kundi B [Moses Mabhida Stadium Saa 3 na Nusu Usiku]
Jumapili Februari 3
Mshindi Kundi D v Mshindi wa Pili Kundi C [Royal Bafokeng Stadium Saa 12 Jioni]
Mshindi Kundi C v Mshindi wa Pili Kundi D [Mbombela Stadium Saa 3 na Nusu Usiku]
NUSU FAINALI
Jumatano Februari 6
Mshindi RF 3 v Mshindi RF 2 [Mbombela Stadium Saa 12 Jioni]
Mshindi RF 1 v Mshindi RF 4 [Moses Mabhida Stadium Saa 3 na Nusu Usiku]
MSHINDI wa TATU
Jumamosi Februari 9
[Nelson Mandela Bay Stadium Saa 3 Usiku]
FAINALI
Jumapili Februari 10
[Soccer City Saa 3 Usiku]

WAAMUZI KULINDWA ILI WASIPOKEE MLUNGULA AFCON 2013.

Mvuso Mbebe
KAMATI ya maandalizi ya michuano ya Mataifa ya Afrika 2013 inatarajia kuwaweka faragha waamuzi wakati wa michuano hiyo itakayofanyika nchini Afrika Kusini ili kujaribu kuzuia tatizo la upangaji wa matokeo. Ofisa Mkuu wa kamati hiyo Mvuso Mbebe amesema kuwa waamuzi wa michuano hiyo watalindwa kwa kiwango sawa kama ilivyokuwa wakati michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010 ambayo nchi hiyo pia iliandaa. Mbebe amesema watatumia mbinu walizotumia katika michuano ya Kombe la Dunia ambao waliwaweka waamuzi wote katika hoteli ambayo hakuna raia yoyote aliyepata nafasi ya kuwaona na wakiondoka ni kw ajili ya kwenda kuchezesha mechi hivyo ni vigumu kwa watu kukutana nao na kuwarubuni. Watu wa Usalama watakuwa wakiwasindikiza waamuzi hao kutoka hotelini mpaka viwanjani na utaratibu huo utatumika toka mwanzo wa mashindano mpaka mwisho ambapo Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF limeridhia utaratibu huo. Michuano hiyo itaanza kutimua vumbi Januari 19 mpaka Februari 10 2013.

PELE ALAZWA.

Msemaji wa kituo cha afya cha Albert Einstein amesema kuwa mchezaji nguli wa zamani wa soka Edson Arantes do Nascimento maarufu kama Pele amelazwa katika kituo hicho kilichopo jijini Sao Paulo. Msemaji huyo alithibitisha hayo lakini alikataa kuelezea kwa undani zaidi kinachomsumbua nyota huyo mwenye umriwa miaka 72 ikiwa ni shinikizo kutoka kwa familia yake ambao hawakutana ugonjwa unaomsumbua nyota huo kuwekwa wazi. Kwa mujibu wa gazeti moja la michezo la Folha de Sao Paulo nyota huyo ambaye pia anajulikana kwa jina la utani la The King au Mfalme aliripotiwa kufanyiwa upasuaji wa nyonga. Pele anahesabiwa kama mmoja wapo ya wachezaji bora kabisa kuwahi kutokea katika mchezo wa soka akiwa ameshinda Kombe la Dunia katika vipindi vitatu tofauti mwaka 1958, 1962 na 1970 huku akiwa amefunga mabao 1,281 katika kipindi chote alichosakata kabumbu.

MTAZAME CRISTIANO RONALDO ANAVYOONEKANA BAADA YA KUPASULIWA JUU YA JICHO...MWENYEWE AONDOA HOFU MASHABIKI WAKE NA KUSEMA ATARUDI UWANJANI HARAKA HUKU AKIWA 'FITI' 100%...!

Sasa niko poa...! Ronaldo anavyoonekana katika picha yake aliyoiweka katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa facebook.
STRAIKA wa kimataifa wa Ureno na klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo amewashukuru mashabiki kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook na kuwaambia kuwa wasiwe na wasiwasi kuhusiana na jeraha alilopata Jumapili la juu ya jicho kwani sasa yuko 'fiti' na atakuwa tayari kuichezea klabu yake mwishoni mwa wiki. 

Cristiano ameandika: "Najihisi vizuri na natumai kuwa nitarejea uwanjani haraka."

Nyota huyo Mreno ameweka pia picha yake kwenye ukurasa wake wa Facebook, akimbatanisha na maelezo ya picha ambayo yanawashukuru mashabiki kwa kumuunga mkono wakati wote: "Ahsante kwa salamu za kunitakia kheri mlizonitumia tangu siku nilipoumia. Najihisi vizuri na, natumai kurudi uwanjani mara moja nikiwa fiti kwa 100%".

CHELSEA na Tuhuma za Ubaguzi kwa Refa Clattenburg: Wadai wako sahihi!! 

>>REFA CLATTENBURG AANZA MAZOEZI!!

CLATTENBURG1KLABU ya Chelsea imedai wao si ‘wanafiki’ kufuatia kumtuhumu Refa Mark Clattenburg ni ‘Mabaguzi’ wakati wao walimtetea na kumuunga mkono Nahodha wao, John Terry, wakati akishitakiwa kwa tuhuma za Ubaguzi na hatimae kupatikana na hatia na FA, Chama cha Soka England, na kufungiwa Mechi 4 na kutwangwa Faini ya Pauni Laki 220,000.
Mwenyekiti wa Chelsea, Bruce Buck, amesema sakata hizo mbili za Ubaguzi zisiunganishwe kwa vile Klabu yao ilikuwa haina namna nyingine bali kumshitaki Refa Mark Clattenburg kwa kutamka neno la Kibaguzi dhidi ya Mchezaji wao John Mikel Obi wakati wa Mechi ya Ligi Kuu England kati ya Chelsea na Manchester United iliyochezwa Stamford Bridge Wiki mbili zilizopita.
Mwenyekiti huyo amewatuhumu Wanahabari kwa kuziunganisha Kesi za Terry na Clattenburg na kudai wao imebidi wazitenganishe ili waonekana wakweli.
Alidai: “Ni jukumu letu kuliacha suala la Terry na kuripoti makosa ya Refa. Tumefanya hivyo kwa nia njema tu!”
Madai ya Chelsea kuhusu Refa Clattenburg yamezishangaza Klabu za England na hata Mameneja wa Man United, Sir Alex Ferguson, na Arsenal, Arsene Wenger, wamezungumza kutoamini kwao tuhuma hizo na kutaka suala hilo kushughulikiwa vinginevyo.
Lakini Mwenyekiti Bruce Buck ameonyesha kukerwa na msimamo wa Klabu nyingine na kudai haikuwa haki wao kulaumiwa.
WAKATI HUO HUO, huku kukiwa na minong’ono hatima ya Refa Mark Clattenburg itajulikana Wiki hii, Refa huyu, ambae alisimama kufanya mazoezi na wenzake tangu atuhumiwe kwenye Mechi hiyo Chelsea na Man United iliyochezwa Oktoba 28, ameanza tena mazoezi ingawa Wiki hii pia hakupangiwa Mechi kama ilivyofanyika kwa Wiki mbili sasa tangu atuhumiwe.

Messi ni MCHEZAJI BORA La Liga Msimu wa 2011/12!!

>>KWA WIKI hii: MESSI ndie Bora, Bayern Klabu Bora kufuatana na AP!!
>>CHICHARITO amfuatia Messi kwa Ubora wa Wiki!!
MESSI_ASHANGILIA_GOLIFowadi wa Barcelona Lionel Messi amechaguliwa kuwa ndie Mchezaji Bora wa LFP, Liga de Fútbol Profesional, maarufu kama La Liga au Primera Division, huko Spain na vile vile kujikita kileleni mwa Listi ya Ubora ya kila Wiki Duniani inayotolewa na AP, Associated Press, ambalo ni Shirika la Habari maarufu Duniani, ambalo pia limeichagua Bayern Munich kuwa Klabu Bora ya Wiki Duniani huku Javier Hernandez ‘Chicharito’ akikamata nafasi ya Pili.
Tuzo hiyo ya Messi toka kwa LFP imetokana na kura za Wachezaji wenzake pamoja na Makocha wa Timu za Madaraja mawili ya juu ya huko Spain.
+++++++++++++++++++++++++++
LISTI KAMILI ya TUZO za LFP:
-MCHEZAJI BORA: Lionel Messi [Barcelona]
-KIPA BORA: Iker Casillas [real Madrid]
-BEKI BORA: Sergio Ramos [Real Madrid]
-KIUNGO MKABAJI BORA: Xabi Alonso [Real Madrid]
-KIUNGO MSHAMBULIAJI BORA: Iniesta [Barcelona]
-KOCHA BORA: Pep Guardiola [Barcelona]
-KIPAJI cha MWAKA: Isco [Malaga]
-MCHEZAJI KIHAKI [Fair Play]: CARLES PUYOL [Barcelona]
+++++++++++++++++++++++++++
UTEUZI wa AP [Associated Press]
Associated Press, ambalo ni Shirika la Habari maarufu Duniani, limetangaza uteuzi wa Wiki wa Mchezaji Bora Duniani na Klabu Bora Duniani ambao wamepata Kura toka kwa Jopo la Wanahabari Magwiji Duniani na kwa Mchezaji Bora Lionel Messi ndie alietwaa na kwa Klabu ni Bayern Munich.
Messi amezoa Tuzo hii ya AP baada ya juzi kuivunja Rekodi ya Pele ya kufunga Mabao 75 katika Mwaka mmoja yeye alipopachika Bao 2 walipoifunga Real Mallorca Bao 4-2 kwenye La Liga.
Kwenye Kura hizo, nyuma ya Messi alikuwa ni Javier Hernandez, ‘Chicharito’ wa Manchester United ambae ametambuliwa kwa kuifungia Man United mabao muhimu Wiki iliyopita dhidi ya Braga na Aston Villa.
Mchezaji alieshika nafasi ya 3 ni yule wa Juventus Fabio Quagliarella.
Katika upigaji Kura huo wa Jopo la Wanahabari, Messi alipata Pointi 139, Hernandez 98 na Quagliarella 67.
Nafasi ya 4 imeshikwa na Kipa wa Celtic, Fraser Forster, baada ya kuonyesha Ushujaa mkubwa walipoifunga Barcelona kwenye Mechi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Nafasi ya 5 ni Edinson Cavani (5th), Franck Ribery, wa 6, Cristiano Ronaldo, nafasi ya 7 na Marouanne Fellaini amepewa nafasi ya 8.
Kwa upande wa Klabu, Bayern Munich ndio imeshinda uteuzi wa Klabu Bora ya Wiki kufuatia kuitwanga Lille 6-1 kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI na kuifunga Eintracht Frankfurt 2-0 kwenye Bundesliga.
Juventus, ambao walichapwa 3-1 na Inter Milan, waliibuka na kuwasha Bao 10 katika Mechi mbili kwa kuzifunga Kllabu ya Denmark, Nordsjaelland, 4-0 kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI na kuitwanga Pescara Bao 6 kwenye Serie A.
Manchester United wao wametwaa nafasi ya 3 na Celtic' nafasi ya 4.

UNITED NAYO YAINGIA KATIKA MBIO ZA KUMUWANIA ZAHA.

KLABU ya Manchester United inajiandaa ktika mbio mbio za kumnasa kinda wa klabu ya Crystal Palace, Wilfried Zaha. Meneja wa United Sir Alex Ferguson amekuwa akifuatilia maendeleo ya kinda huo kwa miezi kadhaa na sasa ameamua rasmi kusajili katika kipindi cha dirisha dogo la usajili Januari mwaka huu. Mbali na United pia klabu za Arsenal, Liverpool, Manchester City na Tottenham Hotspurs nazo zimekuwa zikimfuatilia winga huyo na wako tayari kuanza mbio za kumsajili katika kipindi cha dirisha dogo la usajili. Mkataba wa Zaha katika klabu hiyo ya ligi daraja la kwanza unaishia 2017 na Mwenyekiti wa klabu hiyo amedai kuwa klabu itakayomhitaji nyota huyo itabidi itoe paundi milioni 20 ingawa dau hilo linaonekana kubwa sana hivyo linaweza kushuka mpaka paundi milioni 10.