Sunday, January 20, 2013

TIMU YA MAAFANDE WA POLISI TABORA YAWAPIGISHA KWATA KOMBAIN YA WILAYA 2-1 ALLY HASSAN MWINYI JANA>>>>>WAKATI HUO HUO TIMU YA KAGERA SUGAR INATARAJIA KUWASILI MKOANI TABORA TAYARI KWA MCHEZO W AKESHO DHIDI YA RHINO&NA JUMANNE DHIDI YA POLISI TABORA


 

 Timu ya maafande wa mkoani tabora polisi tabora jana ilitoka nyuma ya bao 1-0 na kuibuka na ushindi w amabao 2-1 katika mchezo w akirafiki uluochezwa katika dimba la ALLY HASSAN MWINYI  kuanzia majira ya saa 4;30 za jioni.

Bao la kuongoza kwa timu ya kombaini wilaya lilifungw ana nahodha wa timu hiyo GOFREY MAGASO akiunganisha krosi ya kona iliyochongwa toka upande wa mashariki na winga ABDALAHA JUMA.

Hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza timu ya kombaini wilaya ilienda kifua mbele kwa bao 1-0 lililofungwa mnamo dakika ya 33.
Kipindi cha pili kocha wa polisi tabora ambaye amesainishwa mkata akitokea dar es salaam alifanya mabadiliko katika timu yake ndipo alipopata mafanikipo mnamo dakika ya 67 ya kipindi cha pili baaada ya mshambuliaji wake IDDY KIBWANA kuachia shuti kali lililoenda moja klwa moja wavuni.

Naye IBRAHIM MUSSA liunganisha krosi nzuri iliyochongwa na iddy kibwana na kuiandikia polisi bao la 2 na la ushindi kwao.hadi dakika 90 za mchezo polisi tabora walitoka kifua mbele kwa goli 2-1 na kuonesha matumaini kwa mashabiki w amkoani tabora.

Na kuelekea katika duru la pili la michuano ya ligi daraja la kwanza timu ya polisi tabora imesajili wachezaji watano kutoka timu mbali mbali hapa tanzania wachezaji hao ni DANIEL KINDU na JEREMIA wote kutoka timu ya Samaria,JAPHARI kutoka katika timu ya A.F.C Arusha ,AMOS AMBAN kutoka timu ya polisi dodoma na RAYGAN MBUTA kutoka timu ya polisi dodoma naye kw amkopo.
Wachezaji wa zamani watimu hiyo ni JOHN MTULI,JAMAI JUMANNE,JOSEPHY KILINDI,ERNEST NKANDI,HUSSEIN ABDALAH,RAMADHAN SEMWA,IDDY KIBWANA,ATHUMAIN MPONDELA,HUSSEIN ABDALAH,MUSSA BOAZ,DAVID JOSEPHY,KAIZAR KILOWOKO,ABDUL  AZIZ,IBRAHIM MUSSA,SAMUEL KILINDI na RAMADHAN FIRSTEEN

WAKATI HUO HUO timu ya Kagera sugar ya manungu turiani BUKOBA inatarajia kuwasili leo kuanzia majira ya saa mbili kamili za uskiku ikitoka Bukoba tayari kwa michezo yake ya kirafiki siku ya jumatatu kesho na jumanne.

Kesho jumatatu inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya jeshi la wananchi tanzania RHINO RANGERS mchezo w akirafiki utakaofanyika katika dimba la ALLY HASSAN MWINYI kuanzia majira ya saa kumi na nusu za jioni na kesho kutwa jumanne itacheza na wapiga kwata wa hapa mkoani tabora POLISI TABORA katika dimba hilo hilo la ALLY HASSAN MWINYI.

Pia siku hiyo ya jumanne nayo timu ya wnaakisha mapanda ya mwanza TOTO AFRICAN inatarajia kushuka dimbani hapa mkoani tabora na timu ya RHINO RANGERS mchezo wa kujipima nguvu kuelekea katika duru la pili la vodacom bara na ligi daraja la kwanza FDL ambayo inatarajia kutimua vumbi siku ya jumamosi ya Januari 26 kati  VPL ni kati ya African Lyon v Simba [National Stadium, Dar es Salaam]Mtibwa Sugar v Polisi Morogoro [Manungu, Morogoro] Coastal Union v Mgambo JKT [Mkwakwani, Tanga] Ruvu Shootings v JKT Ruvu [Mabatini, Pwani]  Azam v Kagera Sugar [Azam Complex, Dar es Salaam]  JKT Oljoro v Toto Africans [Sheikh Amri Abeid, Arusha]
Na  Januari 27Yanga v Tanzania Prisons [National Stadium, Dar es Salaam]

No comments:

Post a Comment