Thursday, November 29, 2012

ZANZIBAR YAIKALISHA RWANDA NAMBOOLE

Khamis Mcha ‘Vialli’ akiruka kushangilia baada ya kufunga bao la kwanza. Kushoto ni Jaku Juma.


MABAO mawili ya kiungo wa Azam FC, Khamis Mcha ‘Vialli’ usiku huu yameipa Zanzibar ushindi wa 2-1 dhidi ya Rwanda, katika mchezo wa Kundi C, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge uliofanyika kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole, Kampala.
Kwa ushindi huo, Zanzibar Heroes imefufua matumaini ya kwenda Robo Fainali ya michuano hii, ikipanda kileleni mwa Kundi hilo, kwa pointi zake nne, Rwanda ikishuka nafasi ya pili kwa pointi zake tatu, sawa na Malawi, wakati Eritrea inashika mkia kwa pointi yake moja.
Vialli alifunga mabao yake moja kila kipindi, la kwanza dakika ya sita na la pili dakika ya 61, yote akionyesha yeye ni fundi na mwenye akili na maarifa ya soka kutokana na kutulia na kumtungua kipa hodari kabisa katika ukanda huu, Jean Claude Ndoli.
Rwanda ilipata bao lake kupitia kwa Dadi Birori dakika ya 79, ambaye aliingia uwanjani dakika ya 66 kuchukua nafasi ya Tumaine Ntamuhanga.
Mchezo wa leo kama ulivyokuwa mchezo wa kwanza kati ya Malawi na Eritrea ulitibuliwa na mvua iliyoharibu mandhari ya Uwanja wa Mandela, hivyo haikuwa wa ufundi zaidi ya ‘butua butua’.
Nahodha wa Zanzibar, Nadir Heroub ‘Cannavaro’ alisema baada ya mechi hiyo kwamba wamefuta makosa yao ya mchezo wa kwanza na sasa Wazanzibari wasubiri Kombe, wakati Haruna Niyonzima wa Rwanda, alilalamikia Uwanja mbovu leo kuwasababisha kucheza ovyo.  
Katika mchezo wa leo, kikosi cha Zanzibar kilikuwa; Mwadini Ally, Nassor Masoud ‘Cholo’, Samir Hajji Nuhu, Aggrey Morris, Nadir Haroub Ali 'Canavaro, Sabri Ali, Khamis Mcha 'Vialli', Abdulaghan Gulam, Jaku Juma, Seif Abdallah/Adeyom Saleh Ahmed dk88 na Suleiman Kassim ‘Selembe’.
Rwanda; Jean Claude Ndoli, Emery Bayisenge, Hamdani Bariyanga, Ismail Nshutiyamagara, Mwemere Ngirishuti/Jean Claude Iranzi dk46, Jean Baptiste Mugiraneza, Haruna Niyonzima, Jimmy Mbagara, Jerome Sina, Jean D’Amour Uwimana/Fabrice Twagizimana dk24 na Tumaine Ntamuhanga/Dadi Birori dk66.


MSIMAMO KUNDI C:
                     P   W  D   L    GF GA GD Pts
Zanzibar        2    1    1    0    2    1    1    4
Rwanda         2    1    0    1    3    2    1    3
Malawi           2    1    0    1    3    4    -1  3
Eritrea           2    0    1    1    2    3    -1  1

Beki wa Zanzibar, Nassor Masoud 'Chollo' akiondoka na mpira mbele ya kiungo wa Rwanda, Haruna Niyonzima

Kikosi cha Rwanda leo

Kikosi cha Uganda leo

Vialli kushoto akishangilia bao lake la pili, kulia ni Suleiman Kassim 'Selembe' 

Wachezaji wa Zanzibar wakishangilia bao la pili kwa staili ya kupiga kasia

 

BUNDESLIGA: TAJI la Dortmund hatihati!!

>>MTANANGE Jumamosi ALLIANZ ARENA: Bayern v Dortmund!!
BORUSSIA_DORTMUND_JUKWAAMabingwa watetezi Borussia Dortmund wanasafiri kwenda Munich Wikiendi hii kuwavaa vinara wa Bundesliga Bayern Munich wakiwa Pointi 11 nyuma yao na wanajua wazi matokeo mengine yeyote bila ya ushindi ni kuwa Taji lao ‘kwishnei!’
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO-Timu za Juu:
[Kila Timu imecheza Mechi 14]
1 Bayern Munich Pointi 37
2 Bayer Leverkusen 27
3 Borussia Dortmund 26
4 Schalke 24
5 Eintracht Frankfurt 24
6 Hannover 20
7 Mainz 20
+++++++++++++++++++++++
Ingawa kuna Mechi nyingi tu zimebaki na wao wakiwa nafasi ya 3, Kocha wa Mabingwa Borussia Dortmund, Juergen Klopp, anafahamu fika Jumamosi wanahitaji ushindi kwa kila hali.
Kitu cha kutia moyo kwa Borussia Dortmund ni kuwa wameifunga Bayern Munich katika Mechi 4 kati ya 5 walizocheza nao mwisho na Mechi waliyopteza ni ile waliyocheza mwishoni ambayo Bayern walitwaa German Super Cup mwanzoni mwa Msimu huu.
Lakini Bayern ya Msimu huu ni kali na wamefungwa Bao 5 tu Msimu huu kwenye Bundesliga.
RATIBA:
Ijumaa Novemba 30
Fortuna Dusseldorf v Eintracht Frankfurt
Jumamosi Desemba 1
Bayern Munich v Borussia Dortmund
Schalke v Borussia Monchengladbach
Mainz v Hannover
SpVgg Gr. Furth v Stuttgart
Augsburg v Freiburg
Bayer Leverkusen v Nuremberg
Jumapili Desemba 2
Hoffenheim v Werder Bremen
Wolfsburg v Hamburger
+++++++++++++++++++++++
 

CECAFA CHALLENGE CUP 2012: Zenji yashinda, yashika hatamu Kundi C!!

>>IJUMAA: Lala salama Kundi A!
CECAFA_TUSKER_CUP_2012Kwenye michuano ya kusaka Nchi Bingwa ya Afrika Mashariki na ya Kati, CECAFA TUSKER CHALENJI CUP 2012 inayoendelea huko nchini Uganda, Zanzibar Heroes leo wamejiweka nafasi nzuri kutinga Robo Fainali kutoka Kundi C baada ya kuichapa Malawi Mabao 2-1 na kutwaa uongozi wa Kundi hilo.
MABAO mawili ya Zanzibar yalifungwa na Kiungo wa Azam FC, Khamis Mcha ‘Vialli’ dakika ya 6 na 61, na la Rwanda limefungwa na Dadi Birori dakika ya 79.
+++++++++++++++++++++++++++++++++
MAKUNDI:
KUNDI A: Uganda, Ethiopia, Kenya, South Sudan
KUNDI B: Sudan, Tanzania, Burundi, Somalia
KUNDI C: Rwanda, Malawi, Zanzibar, Eritrea
+++++++++++++++++++++++++++++++++
Katika Mechi nyingine ya Kundi C, Malawi iliifunga Eritrea Bao 3-2 kwa Bao za Chiukepo Msowoya, Miciam Mhone na Patrick Masanjala na yale ya Eritrea kufungwa na Amir Hamad Omary na Yosief Ghide kwa penalti.
Michuano hii itaendelea Ijumaa Novemba 30 kwa Mechi za mwisho za Kundi A kwa Mechi za Kenya v Ethiopia na Uganda v South Sudan.
RATIBA/MATOKEO:
KUNDI A:
Novemba 24:  Ethiopia 1 South Sudan 0, Uganda 1 Kenya 0
Novemba 27: South Sudan 0 Kenya 2, Uganda 1 Ethiopia 0
Novemba 30: Kenya v Ethiopia,  South Sudan v Uganda
MSIMAMO:
[Kila Timu Mechi 2]
1 Uganda Pointi 6
2 Kenya 3 [Tofauti ya Magoli: 1]
3 Ethiopia 3 [Tofauti ya Magoli: 0]
4 South Sudan 0
KUNDI B:
Novemba 25: Burundi 5 Somalia 1, Tanzania 2 Sudan 0
Novemba 28: Somalia 0 Sudan 1, Tanzania 0 Burundi 1
Desemba 1: Sudan v Burundi, Somalia v Tanzania
MSIMAMO:
[Kila Timu Mechi 2]
1 Burundi Pointi 6
2 Kili Stars 3 [Tofauti ya Magoli: 1]
3 Sudan 3 [Tofauti ya Magoli: -1]
4 Somalia 0
KUNDI C:
Novemba 26: Zanzibar 0 Eritrea 0, Rwanda 2 Malawi 0
Novemba 29: Malawi 3 Eritrea 2, Rwanda 1 Zanzibar 2
Desemba 1: Malawi v Zanzibar, Eritrea v Rwanda
MSIMAMO:
[Kila Timu Mechi 2]
1 Zanzibar Pointi 4
2 Rwanda 3 [Tofauti ya Magoli: 1]
3 Malawi 3 [Tofauti ya Magoli: -1]
3 Eritrea 1
FAHAMU: Washindi wawili wa juu wa kila Kundi pamoja na Timu mbili zitakazoshika nafasi za 3 Bora zitaingia Robo Fainali.
ROBO FAINALI: Desemba 3 & 4
NUSU FAINALI: Desemba 6
FAINALI: Desemba 8
 

FIFA KLABU BINGWA DUNIANI: Chelsea yatangaza Kikosi kwenda Japan!!

>>CHELSEA kucheza Desemba 13 na Mshindi Usain Hyundai v Monterrey!!
>>BARANI ASIA: MCHEZAJI BORA 2012==SHINJI KAGAWA!
CHELSEA_ULAYA_2012AWakati Chelsea inatangaza Kikosi chake cha kwenda Japan kuwania kuwa Klabu ya pili toka England, baada ya Manchester United, kutwaa Kombe la Dunia kwa Klabu, Nchi hiyo Japan na Klabu ya Manchester United imetoa Mchezaji Bora Barani Asia kwa Wachezaji wa Kimataifa, Tuzo ambayo ni mara ya kwanza kutolewa, na Mshindi huyo ni Shinji Kagawa.
CHELSEA
Kocha wa muda wa Chelsea, Rafael Benitez, ametangaza Kikosi kikali kwa ajili ya Michuano ya kuwania Taji la FIFA la Klabu Bingwa Duniani ambayo wao wataanza kucheza hatua ya Nusu Fainali dhidi ya Mshindi kati ya Bingwa wa Barani Asia, Usain Hyundai kutoka Korea na Monterrey, ambao ni Mabingwa wa Marekani ya Kati na Kaskazini.
Kikosi cha Chelsea kina Majina yote makubwa wakiwemo Nahodha wao John Terry na Frank Lampard ambao wote bado wamo kwenye Listi yao ya sasa ya Majeruhi wao.
Meneja Rafael Benitez ana uzoefu mkubwa kwenye Mashindano ya Klabu Bingwa Duniani kwani hii itakuwa mara yake ya 3 kushiriki ambapo aliipeleka Liverpool Mwaka 2005 na kutolewa Fainali na 2010, aliiongoza Inter Milan, iliyofikishwa huko na Jose Mourinho, kutwaa Ubingwa wa Dunia.
KIKOSI KAMILI:
Makipa: Petr Cech, Ross Turnbull, Hilario
Mabeki: Branislav Ivanovic, Ashley Cole, David Luiz, Paulo Ferreira, Gary Cahill, John Terry, Cesar Azpilicueta, Ryan Bertrand
Viungo: Oriol Romeu, Ramires, Frank Lampard, Oscar, John Obi Mikel, Eden Hazard, Marko Marin, Lucas Piazon
Mafowadi: Fernando Torres, Juan Mata, Victor Moses, Daniel Sturridge
BARANI ASIA: MCHEZAJI BORA 2012==SHINJI KAGAWA!
KAGAWA_N_GIL
Kiungo wa Japan na Manchester United Shinji Kagawa ametwaa Tuzo ya kwanza kabisa kutolewa na Shirikisho la Soka Barani Asia, AFC, ya Mchezaji Bora wa Mwaka 2012 kwa Wachezaji wa Kimataifa, wale wanaocheza nje ya Asia.
Katika kutwaa Tuzo hiyo Shinji Kagawa aliwashinda Yuto Nagatomo wa Japan anaecheza Klabu ya Inter Milan na Kipa Veterani wa Australia anaechezea Fulham, Mark Schwarzer.
Washindi hao walitajwa huko Kuala Lumpur, Malaysia hii leo.
Mchezaji wa Korea ya Kusini, anaechezea Klabu Bingwa ya Asia, Lee Keun-ho, ndie Mchezaji Bora kwa Wachezaji wanaocheza ndani ya Asia.
Lee aliwashinda Kiungo wa Iran Ali Karimi na Beki wa China Zheng Zhi.
Katika Tuzo nyingine mpya anayozawadiwa Mchezaji wa kutoka nje ya Asia anaecheza Asia Mshindi ni Mbrazil Rogerio De Assis Silva Coutinho wa Klabu ya United Arab Emirates Al Jazira.
KLABU BINGWA DUNIANI 2012
TIMU ZITAKAZOSHIRIKI:
Chelsea-BINGWA ULAYA
Corinthians-BINGWA MAREKANI ya KUSINI
Monterrey-BINGWA MAREKANI ya KATI NA KASKAZINI
Auckland City-BINGWA KANDA ya OCEANIA
Usain Hyundai-BINGWA-Barani Asia
Al Ahly-BINGWA-Barani Afrika
Sanfrecce Hiroshima-BINGWA-Japan J-LIGI
RATIBA:
Raundi ya Mchujo - Desemba 6, Yokohama
1 Sanfrecce Hiroshima v Auckland City
ROBO FAINALI - Desembar 9, Toyota
2 Usain Hyundai  v Monterrey
3 MSHINDI Mechi Na 1 v Al Ahly
MSHINDI wa 5- Desemba 12, Toyota
Aliefungwa Robo Fainali 1 v Aliefungwa Robo Fainali 2
NUSU FAINALI
Desemba 12, Toyota
5 Mshindi Mechi Na 3 v Corinthians
Desemba 13, Yokohama
6 Mshindi Mechi Na 2  v Chelsea
MSHINDI wa 3 - Desemba 16, Yokohama
FAINALI - Desemba 16, Yokohama

 

ARUDI KOCHA BRAZIL: BIG PHIL kwa ajili ya 2014 World Cup!!

>> CARLOS ALBERTO PARREIRA Mkurugenzi Ufundi!!
>>MECHI ya KWANZA kuivaa England Februari 2013!!
Luiz_Felipe_ScolariLuiz Felipe Scolari ameteuliwa kuwa Kocha wa Brazil ikiwa ni mara yake ya pili baada ya Kocha huyo, aliewahi kuzifundisha Chelsea na Portugal, kuiongoza Brazil Mwaka 2002 kutwaa Kombe la Dunia lililochezwa huko Nchini Japan na Korea ya Kusini.
Scolari, Miaka 64, amembadili Mano Mezes alietimuliwa Wiki iliyopita na sasa ataiongoza Nchi yake kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 zitazochezwa Nchini Brazil.
+++++++++++++++++++++++++++
MAFANIKIO ya SCOLARI KIMATAIFA:
-2002: ATWAA Kombe la Dunia na Brazil walipoifunga Germany 2-0 Fainali.
-2004: AFIKA Fainali Euro 2004 akiwa na Portugal, wafungwa 1-0 na Greece
-2006: AIONGOZA Portugal kushika Nafasi ya 4 Kombe la Dunia
+++++++++++++++++++++++++++
Mkongwe Carlos Alberto Parreira, aliewahi kuwa Kocha wa Brazil, ameteuliwa kumsaidia Scolari na amepewa wadhifa wa Mkurugenzi wa Ufundi.
Scolari, akipokea uteuzi huo, alisema: “Sina presha, nina furaha! Nimemshukuru Rais wa FA mara 1000 kwa kuniteua!”
Mwaka 2001, Scolari aliinusuru Brazil katika janga la kutofuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka wakati walipokuwa wakifanya vibaya kwenye Mechi za Mchujo na hatimae kuifikisha Fainali alipopewa Timu na pia kutwaa Ubingwa wa Dunia.
 

FIFA Ballon d’Or 2012: NI RONALDO, INIESTA & MESSI!

>>KOCHA BORA: DEL BOSQUE, GUARDIOLA & MOURINHO!
>>MAFOWADI 15 FIFA/FIFPro World XI 2012 wamo ROONEY, RVP, SUAREZ, AGUERO, BALOTELLI, DROGBA, ETO’O!!
>>GOLI BORA: NEYMAR, FALCAO & STOCH!!
MESSI_n_RONALDOWagombea wa Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani kwa Mwaka 2012, FIFA Ballon d’Or, wametangazwa leo na FIFA huko Anhembi Convention Center Mjini Sao Paulo, Brazil katika Mkutano uliohudhuriwa na Viongozi wa FIFA, akiwemo Rais wao, Sepp Blatter na Katibu Mkuu Jerome Valcke na pia Mchezaji Nguli wa Brazil, Ronaldo, na Wachezaji watatu waliotajwa kugombea Tuzo hiyo ni Cristiano RONALDO, Portugal, Andres INIESTA, Spain na Lionel MESSI, Argentina.
Kwa upande wa Kinamama, Wagombea ni MARTA, Brazil, Alex MORGAN, USA na Abby WAMBACH, USA.
Sambamba na hao, pia zilitajwa Listi za Wagombea Tuzo nyingine ambao ni:
KOCHA BORA kwa Wanaume:
-Vicente DEL BOSQUE, Spain (Spain)
-Pep GUARDIOLA, Spain (FC Barcelona)
-Jose MOURINHO, Portugal (Real Madrid)
KOCHA Bora kwa Wanawake:
-Bruno BINI, France (France)
-Norio SASAKI, Japan (Japan)
-Pia SUNDHAGE, Sweden (USA)
Wagombea hao wa Tuzo hizo walipatikana kwa Kura za Manahodha na Makocha wa Timu za Taifa za Wanaume na Wanawake pamoja na Wawakilishi wa Wanahabari walioteuliwa na Gazeti la France Football ambao ni Washirika wa FIFA katika Tuzo hizi.
Pamoja na hao pia yalitangazwa Majina ya Wagombea wa Goli Bora, wanaowania Tuzo ya FIFA Puskás ambao ni:
- FALCAO (América de Cali-Atletico Madrid, 19 May 2012)
-NEYMAR (Santos-Internacional, 7 March 2012) –
-Miroslav STOCH (Fenerbahçe-Gençlerbirliği, 3 March 2012).
Pia, yalitangazwa Majina ya Fowadi 15 ambao wanaungana na Makipa watano, Mabeki 20, na Viungo 15, waliotangazwa kabla, kufanya jumla ya Wachezaji 55 watakaowania nafasi 11 za kuwemo kwenye Listi ya Wachezaji 11 watakauonda Timu Bora Duniani, FIFA/FIFPro World XI 2012, yenye Kipa mmoja, Mabeki wanne, Viungo watatu na Mafowadi watatu.
LISTI HIYO ya Wachezaji 55:
WALIOTEULIWA HADI SASA:
MAKIPA 5 WALIOTEULIWA:
-Gianluigi Buffon (Italy, Juventus)
-Iker Casillas (Spain, Real Madrid)
-Petr Cech (Czech Republic, Chelsea)
-Joe Hart (England, Manchester City)
-Manuel Neuer (Germany, Bayern Munich).
MABEKI 20:
-Jordi Alba (Spain, Barcelona)
-Gareth Bale (Wales, Tottenham Hotspur)
-Giorgio Chiellini (Italy, Juventus)
-Ashley Cole (England, Chelsea)-
-Dani Alves (Brazil, Barcelona)
-David Luiz (Brazil, Chelsea)
-Patrice Evra (France, Manchester United)
-Rio Ferdinand (England, Manchester United)
-Mats Hummels (Germany, Borussia Dortmund)
-Branislav Ivanovic (Serbia, Chelsea)
-Vincent Kompany (Belgium, Manchester City)
-Philipp Lahm (Germany, Bayern Munich)
-Marcelo (Brazil, Real Madrid)
-Javier Mascherano (Argentina, Barcelona)
-Pepe (Portugal, Real Madrid)
-Gerard Piqué (Spain, Barcelona)-
-Carles Puyol (Spain, Barcelona)
-Sergio Ramos (Spain, Real Madrid)
-John Terry (England, Chelsea)
-Thiago Silva (Brazil, Paris St-Germain).
VIUNGO 15:
-Xabi Alonso (Spain / Real Madrid),
-Sergio Busquets (Spain / FC Barcelona),
-Cesc Fabregas (Spain / FC Barcelona),-
-Steven Gerrard (England / Liverpool)
-Eden Hazard (Belgium / Chelsea)
-Andres Iniesta (Spain / FC Barcelona)
-Frank Lampard (England / Chelsea)
-Luka Modric (Croatia / Real Madrid)
-Mesut Özil (Germany / Real Madrid)
-Andrea Pirlo (Italy / Juventus)
-Franck Ribery (France / Bayern Munich)
-David Silva (Spain / Manchester City)
-Bastian Schweinsteiger (Germany / Bayern Munich)
-Yaya Touré (Ivory Coast / Manchester City)
-Xavi Hernandez (Spain / FC Barcelona)
MAFOWADI 15:
-Sergio Agüero (Argentina, Manchester City)
-Mario Balotelli (Italy, Manchester City)
-Karim Benzema (France, Real Madrid)
-Edinson Cavani (Uruguay, AS Napoli)
-Didier Drogba (Ivory Coast, Shanghai Shenhua)
-Samuel Eto’o (Cameroon, Anzhi Makhachkala)
-Radamel Falcao (Colombia, Atletico Madrid)
-Mario Gomez (Germany, Bayern Munich)
-Zlatan Ibrahimovic (Sweden, Paris Saint-Germain)
-Lionel Messi (Argentina, Barcelona)
-Neymar (Brazil, Santos)
-Robin van Persie (The Netherlands, Manchester United)
-Cristiano Ronaldo (Portugal, Real Madrid)
-Wayne Rooney (England, Manchester United)
-Luis Suarez (Uruguay, Liverpool)
Washindi wote wa Tuzo hizi watatangazwa huko Kongresshaus Mjini Zurich, Uswsisi hapo 7 January 2013.

TAIFA QUEENS YAPAA LEO KWENDA SINGAPORE KUSHIRIKI MASHINDANO YA KIMATAIFA YA MABARA

Naibu Mkurugenzi wa maendeleo ya Michezo, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juliana Yasoda akimkabidhi bendera ya Taifa nahodha wa timu ya taifa ya netiboli inayokwenda nchini Singapore kushiriki mashindano ya kimataifa. Katikati ni Mwenyekiti wa Chaneta, Anna Bayi.

TIMU ya Taifa ya Netiboli ‘Taifa Queens’ imeondoka nchini leo saa tisa kuelekea nchini Singapore kwenye michezo ya kimataifa inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho kutwa na kumalizika Disemba 8 mwaka huu nchini humo.

Kikosi cha timu hiyo chenye wachezaji 12 pamoja na viongozi wawili kimeagwa leo na kukabidhiwa bendera na Naibu Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo Juliana Yasoda.

Akizungumza na jijini mara baada ya kuagwa, Katibu Mkuu wa Chama Cha Netiboli Tanzania (CHANETA), Rose Mkisi alisema kuwa timu hiyo imeongozana na Mwenyekiti wa CHANETA na Daktari katika safari hiyo.

Mkisi alisema timu ikitua itaendelea na mazoezi baada ya mapumziko ya siku moja.

Kikosi hicho kinachoundwa na wachezaji kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kilipata maandalizi ya kutosha baada ya kukaa kambini mjini Morogoro kujiandaa na michuano hiyo.

Mkisi aliongeza kuwa kikosi hicho kinatarajiwa kufanya vizuri katika michuano zinazoshiriki timu kutoka kwenye shirikisho la Kimataifa la Netiboli (IFNA) kwa nchi itakayofanya vizuri ambapo Tanzania ipo nafasi ya tatu kwa Kanda ya Afrika.

PETER TINO "THE STRIKER" AKABIDHI SERENGETI BOYS BENDERA NA UJUMBE MZITO WA KWENDA KUIVAA CONGO BRAZAVILLE










Mshambuliaji wa zamani wa timu ya Taifa Taifa Stars Peter Tino jana usiku aliwakabidhi timu ya Taifa ya vijana waliochini ya miaka 17 "Serengeti boys" bendera na ujumbe mzito.

Tino ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye halfa hiyo aliwaasa wachezaji kucheza kwa kujituma wakijua kuwa nyuma yao kuna watanzania wanawafatilia na ndio maana wamepewa bendera ya taifa kwa sababu wanaiwakilisha nchi.

"Nyie ni jeshi la Tanzania mnakwenda kupigana mkiwa tayari mmeshashinda nyumbani hivyo vyovyote mnatakavyofanyiwa nyie fikirie mchezo tu", alisema Tino.

Pia aliwaambia kwenye mchezo kuna mbinu chafu ambazo zinaweza kutumika ili kuwadhoofisha kisaikolojia ila wasilitilie maanani bali wafikirie mchezo.

"Mchezo wenu ni sawa na mchezo wetu tuliocheza 1980 dhidi ya Zambia na dakika ya 89 mimi niliwanyamazisha Wazambia mbele ya Rais Mugabe baada ya kufunga bao na kufanikiwa kufuzu mataifa ya Afrika, alisema Tino.

Akizungumza na wachezaji Rais wa Shirikisho la Soka nchini Leodgar Chilla Tenga aliwaasa wachezaji wakazingatie kile tu walichofundishwa na kocha kwani anajua mchezo huu utakuwa mgumu

Timu iliondoka na ndege ya shirika la ndege la Kenya na msafara wa watu 27, wachezaji 18 na viongozi tisa huku wakiwa na matumaini makubwa ya kusonga mbele baada ya mchezo wa awali uliochezwa nchini kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Kocha wa timu hiyo, Jacob Michelsen alisema kuwa anajua nakwenda kucheza natimu bora ila wao ni bora pia kwani wana faida ya bao la nyumbani.

"Wachezaji wapo kamili na wana ari ya kushinda mchezo huo na kwa sababu nyumbani tulishinda tunaamini tutashinda pia", alisema Jacob

Serengeti boys ambayo imeundwa na wachezaji chipukizi waliopatokana kutokana na mashindano ya Copa Cocacola wanatamani kushinda mchezo ili waweze kuandika historia ambayo haijawahi kuandikwa hapa nchini.

Serengeti boys wamefika hatua hii baada ya kufuzu hatua ya kwanza baada ya Kenya kujiondoa na hatua pili Misri kujitoa pia

LENZI YA MICHEZO tunawatakia kila la heri mfanikiwe kufuzu fainali za vijana zinazotarajiwa kuchezwa nchini Morocco, Machi mwakani

 

Ronaldo, Iniesta na Messi WAMETANGAZWA KUWANIA TUZO YA FIFA Ballon d’Or 2012


Watakao wania tuzo ya mwanasoka Bora wa Dunia ya  FIFA Ballon d’Or  kwa mwaka  2012 na kwa wanawake wametangazwa leo hii huko   Anhembi  Sao Paulo.
Ambapo Rais wa FIFA  Joseph S. Blatter, Katibu mkuu wa fifa   Jérôme Valcke, Mkuu wa jarida la L’Equipe na mkuu wa soka la ufaransa  François Morinière, na mchezaji mahiri raia wa Brazil  Ronaldo Luiz Antonio Nazalia De Lima  na Marta, ambaye aliwahi kushinda tuzo hiyo walihudhuria .

Wakiwatajwa kiherufi na kimpangillio  watakao wania tuzo hiyo ya FIFA Ballon d’Or  Ni Cristiano RONALDO, Ureno (Real Madrid )  , Andres INIESTA, Uispania  na  Lionel MESSI, Argentina, wakati  MARTA, Kutoka Brazil, Alex MORGAN, Kutoka USA na  Abby WAMBACH, kutoka  USA wao watashindania kwa upande wa wanawake .

kwa upande wa Makocha  wanaume  ni : Vicente DEL BOSQUE, Uispania, Pep GUARDIOLA, Uispania (FC Barcelona) na  Jose MOURINHO, Kutoka Ureno  (Real Madrid)  kwa upande wa  wanawake  Bruno BINI, Ufaransa , Norio SASAKI, Japan (Japan) na , Pia SUNDHAGE, raia wa  Sweden  akifundisha (USA) .

Wachezaji wengine watatu wanaowania goli zuri zaidi kwa maana ya tuzo ya   FIFA Puskás : FALCAO alifunga goli katika mechi kati ya  (América de Cali-Atletico Madrid, 19 May 2012), NEYMAR  kati ya (Santos dhidi -Internacional, 7 March 2012) na  Miroslav STOCH kati ya  (Fenerbahçe dhidi -Gençlerbirliği, 3 March 2012).

Washindi watapewa zawadi zao katika makao makuu ya  FIFA Ballon d’Or Gala huko  Kongresshaus  Zurich Tarehe 7 January 2013 zawadi nyingine ni Uuungwana Michezoni FAIR PLAY na Tuzo ya Heshima rais wa fifa 

LIGI YA PREMIER YA UINGEREZA JANA USIKU



Man Utd. 1 vs 0 West Ham
November 28, 2012 8:00 PM UTC
Old Trafford — Manchester
Referee:‬ M. Jones‎
Attendance:‬ 75572‎
Tottenham 2 vs 1 Liverpool
November 28, 2012 7:45 PM UTC
White Hart Lane — London
Referee:‬ P. Dowd‎
Attendance:‬ 36162‎
Everton 1Arsenal 1
Chelsea 0Fulham 0
Wigan Athletic 0Manchester City 2
Man Utd 1West Ham United 0

 

KASHFA YA MACHANGUDOA KATIKA KAMBI YA HARAMBEE STARS, YAWAREJESHA NAIROBI WACHEZAJI NYOTA PAUL WERE NA KELVIN OMONDI.


Paul Were na Kevin Omondi.
Kocha James Nandwi.

KOCHA wa timu ya Taifa ya Kenya Harambee Stars James Nandwa amewatimua wachezaji wake wawili tegemeo katika kikosi chake kufuatia kutoroka kambi ya timu yao hapo jana usiku.
Wachezaji hao ni winga Paul Were na kiungo Kevin Omondi ambapo wachezaji hao waliondoka na kuelekea kwenye starehe baada ya kupewa pesa zao za posho au Bonas ya mchezo wao dhidi ya Sudani Kusini ambao walichomoza na ushindi wa mabao 2-0.
Taarifa zinasema wachezaji hao walitoweka katika kambi yao iliyoko katika hoteli ya Sky Sports iliyoko Kireka na kwenda kustarehe usiku mzima wakichanganywa na posho walizopewa kufuatia ushindi.
Mbaya zaidi wachezaji hao walirejea hotelini na machangudoa jambo ambalo kocha James Nandwa amekielezea kitendo hicho kuwa ni cha aibu na kisichokubalika.
Kevin Omondi alikuwa katika kiwango kizuri katika mchezo wao dhidi ya Sudani Kusini hapo jana ambapo alitoa pasi za mwisho zilizo zaa magoli yote mawili ya Harambe ukiwa ni ushindi wa kwanza kwa Harambee Stars.
Wachezaji hao wanatarajiwa kurejea Nairobi huku adhabu zaidi zikiwasubiri kutoka shirikisho la soka la Kenya (FKF) alivyo nukuliwa Francis Nyamweya.

WESLEY SNEIJDER AIFUNGULIA MILANGO MANCHESTER CITY


MILAN, Italia
Nyota huyo wa kimataifa wa Uholanzi, kwa sasa amezuiwa kujumuika na kikosi cha kwanza cha Inter, hadi atakapokubali kusaini mkataba mpya wa kuichezea klabu hiyo, utakaoambatana na punguzo la mshahara wake
KIUNGO Wesley Sneijder amefungua milango ya kuhamia klabu ya Manchester City kwa kutoa kauli kuwa hana uhakika kama anataka kuendelea kubaki San Siro yaliko makazi ya Inter Milan, zaidi ya kipindi cha usajili wa majira ya baridi.
Nyota huyo wa kimataifa wa Uholanzi, kwa sasa amezuiwa kujumuika na kikosi cha kwanza cha Inter, hadi atakapokubali kusaini mkataba mpya wa kuichezea klabu hiyo, utakaoambatana na punguzo la mshahara wake.
Kwa hasira Sneijder akakataa katakata kukubali masharti hayo ya Inter na kuamua kuchagua kuihama klabu hiyo pindi dirisha la usajili wa majira ya baridi litakapofunguliwa Januari mwakani.
Klabu za Manchester United, Schalke 04 na Anzhi Makhachkala, ni miongoni mwa zinazomuwinda mkali huyo mwenye miaka 28, hali inayozalisha vita kali ya kufuatilia kujua hatima yake.
‘Nina furaha kuwa hapa, lakini sijui nini kitatokea baadaye,’ alijibu Mholanzi huyo alipoilzwa na mashabiki kuhusu uwezekano wa kutimka klabuni hapo Januari mwakani.
Maelezo hayo ya Sneijder bila shaka yanafungua milango kwa klabu zinazosaka saini yakena bosi wa Manchester City, Mtaliano Roberto Mancini ni mmoja wa mashabiki wakubwa wa kiungo huyo mahiri.
Inafahamika namna Mancini alivyojaribu mara mbili bila mafanikio kusaka saini ya Sneijder kutua Man City, na taarifa kutoka hapa zinapasha kuwa nyota huyo anaweza kupatikana kwa dau  pauni milioni 15.

VILLAS-BOAS AMKATIA TAMAA GARETH BALE

Gareth Bale (mwenye mpira) wa Tottenham Hotspur akimtoka beki wa Southampton wakati wa mechi kati ya timu hizo
LONDON, England
'Ni wazi kwamba Tottenham kama klabu ya soka ingependa kumbakisha yeye hapa kwa muda mrefu kadri iwezekanavyo, lakini tunatambua kwamba wachezaji bora na wazuri kama hawa wanakuwa na thamani kubwa sokoni, ambalo ndio asili ya mchezo'

ANDRE Villas-Boas amekiri kuwa, Tottenham ina kibarua kigumu cha kuhakikisha inaendelea kumbakisha Gareth Bale, baada ya kumshuhudia akifanya vitu adimu kuhitimisha mechi nane bila kichapo Liverpool na kuichapa mabao 2-1 jana usiku.
Bale alikimbia na mpira kwa mita 50 huku akichambua mabeki wanne wa Liverpool, kabla ya kumtengea Aaron Lennon kuipa Spurs bao la kwanza na kisha kumtungua mlinda mlango Pepe Reina kwa bao la umbali wa mita 30.
Bale alisaini mkataba wa kubaki Spurs kiangazi kilichopita, lakini hiyo haijazuia harakati za Barcelona na Real Madrid kusaka saini ya mkali huyo mwenye miaka 23, na Villas-Boas amekiri kuwa yeye kama kocha hana nguvu ya kumzuia winga huyo kuondoka.
'Kwa sasa yeye yuko katika kiwango cha juu, akifanya mambo makubwa kwa Spurs na kimsingi sisi kama timu tunavutiwa mno na afanyacho kwa ajili yetu. Yuko katika levo ya juu kulinganisha na wakati wowote,' Villas-Boas alisema.
'Ni wazi kwamba Tottenham kama klabu ya soka ingependa kumbakisha yeye hapa kwa muda mrefu kadri iwezekanavyo, lakini tunatambua kwamba wachezaji bora na wazuri kama hawa wanakuwa na thamani kubwa sokoni, ambalo ndio asili ya mchezo.'

FERGUSON AITOA CHELSEA MBIO ZA UBINGWA WA ENGLAND


MANCHESTER, England
KOCHA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, amekenulia meno mwanzo mbaya wa kocha wa Chelsea, Rafa Benitez klabuni Stamford Bridge, na kutabiri ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu ni kinyang’anyiro cha timu za jiji la Manchester.
Chelsea inayoshikilia ubingwa wa soka barani Ulaya, iko nyuma kwa pointi saba nyuma ya vinara Man United na sita, nyuma ya mabingwa watetezi Man City.
Fergie bosi wa Man United, alisema: “Matokeo ya leo usiku yanatuweka sisi mbali kidogo na Chelsea katika mbio za ubingwa wa ligi.
“Sisi bado tuko mbele tukiongoza msimamo wa ligi, lakini Man City wako karibu yetu na msimu bado ni mrefu.
“Umuhimu wa kushinda bao 1-0 katika baadhi ya mechi, unawaonesha wapinzani wako kiasi cha ujasiri mlichonacho.
“Kama utaangalia baadhi ya mechi muhimu za matokeo ya bao 1-0 tuliowahi kupata... rejea nyuma kabisa tulipoicaha Newcastle wakati wakiwa pointi tisa juu yetu mwaka 1996 – ushindi wetu wa 1-0 usiku huo, ukatuwezesha kutupa ubingwa.
“Kulikuwa na umuhimu wa ushindi wa 1-0. tulifanya hivyo kwa wengi wao.”

MALAWI YAWAFUNGA KWA MBINDE ERITREA

Mshambuliaji wa Malawi, Rodrick Gonani akimtoka beki wa Eritrea, Yohannes Nega katika mchezo wa Kundi C, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole, Kampala, Uganda jioni hii. Malawi ilishinda 3-2, mabao ya Chiukepo Msowoya dakika ya nne, Miciam Mhone dakika ya 10 na Patrick Masanjala dakika ya 66, wakati ya Eritrea yalifungwa na Amir Hamad Omary dakika ya 72 na Yosief Ghide kwa penalti dakika ya 89. 

Kocha wa Rwanda, Milutin Sredojevic ‘Micho’ akiwa na wasaidizi wake, Mugisha Ibrahim ambaye ni kocha wa makipa na Eric Nshimiyimana, ambaye ni Kocha Msaidizi, wakifuatilia mchezo wa Kundi C kati ya Malawi na Eritrea Uwanja wa Mandela, Namboole, Kampala, Uganda.

Kocha wa Tanzania, Kim Poulsen akiwa na Msaidizi wake, Sylvester Marsh wakifuatilia mchezo kati ya Rwanda na Malawi. Chini ni Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

WAZEE WA KUZAMIA NCHI ZA WATU WAKIPIGA MICHAKATO...

Wachezaji wa timu ya taifa ya Eritrea, wakiwa Uwanja wa Mandela, Namboole, mjini Kampala, wakifuatilia mchezo kati ya Tanzania na Burundi jana. Wachezaji wa Eritrea wana sifa kubwa ya kutorokea nchi za watu wakienda kwenye mashindano, kiasi cha serikali ya nchi yao kuwawekea sheria nguvu ya kuweka fedha za kwao 100,000 kama bondi kabla ya kusafiri.

NDIKUMANA AWATEGA SIMBA SC

Ndikumana
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba SC, Suleiman Yamin Ndikumana kwa sasa ndiye anaongoza kwa kufunga mabao katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge inayoendelea mjini hapa.
Ndikumana aliyewahi pia kucheza Norway na Uturuki, jana alifunga bao la tatu katika mashindano haya, akiichezea Burundi dhidi ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars. 
Sasa anamzidi kwa bao moja, John Bocco ‘Adebayor’ wa Kilimanjafo Stars.
Jumla ya mabao 17 hadi sasa yamefungwa katika mechi 16 za makundi yote matatu, zilizopigwa kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole, Kampala.
Bocco anafungana na mshambuliaji mwingine wa Burundi, Christopher Nduwarugira, wakati wachezaji wengine ambao hadi sasa kila mmoja amefunga bao moja ni Farid Mohamed, Yussuf Ndikumana wa Burundi, Mohamed Jabril wa Somalia kwa penalti, Geoffrey Kizito wa Uganda, Yonatal Kebede Teklemariam, Haruna NiyonzimUganda, David Ochieng, Clifton Miheso na Jean Mugiraneza.
Kwa sasa Bocco anayechezea Azam FC ya Dar es Salaam, ndiye mshambuliaji pekee kwenye kikosi cha Bara, baada ya washambuliaji wengine, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaochezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemomkrasia ya Kongo (DRC) kuzuiliwa na klabu yao.
WAFUNGAJI CECAFA TUSKER CHALLENGE 2012
Suleiman Ndikumana   Burundi    3 (1 penalti)
John Bocco                  Tanzania  2
Chris Nduwarugira        Burundi   2
Yussuf Ndikumana       Burundi   1
Mohamed Jabril            Somalia   1(penalti).
Geoffrey Kizito              Uganda   1
Brian Umony                 Uganda   1
Yonatal Teklemariam     Ethiopia  1
Haruna Niyonzima         Rwanda  1
Jean Mugiraneza           Rwanda  1
David Ochieng               Kenya     1
Clifton Miheso                Kenya     1
Farid Mohamed              Sudan     1 

KAZIMOTO, KAPOMBE HATARINI KUWAKOSA WASOMALI JUMAMOSI


Kazimoto
WACHEZAJI wawili wa Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, beki Shomary Kapombe na kiungo Mwinyi Kazimoto, walishindwa kumaliza mechi za jana, baada ya kuumia na sasa wako hatarini kuikosa mechi ya mwisho ya Kundi B, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge dhidi ya Somalia, Desemba 1.
Wachezaji hao wa klabu ya Simba, wote waliumia kipindi cha pili na kutolewa, nafasi ya Kapombe ikichukuliwa na Issa Rashid wa Mtibwa Sugar nay a Mwinyi ikichukuliwa na Shaaban Nditi wa Mtibwa pia.
Wote walitoka wakichechemea, kuashiria wamepata maumivu makali kidogo na Kocha Mkuu wa Stars, Mdenmark, Kim Poulsen alisema ataangalia hali zao leo na kesho.
Kim pia alisema kwamba sasa imetosha kuzungumzia suala la washambuliaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kama watajiunga na timu hiyo au la.
“Kwangu sasa lazima ifikie wakati iwe inatosha, sitaki kuwazungumzia tena wachezaji hao, waulizeni TFF,”alisema Poulsen baada ya kuulizwa kama mawasiliano na klabu yao kama yanaendelea juu ya kuombea ruhusa.
Mazembe imekataa kuwaruhusu wachezaji hao kwa sababu michuano ya Challenge haimo kwenye kalenda ya FIFA.
Kutokana na kukosekana kwa washambuliaji hao, Stars sasa inabaki na mshambuliaji mmoja tu kikosini, John Bocco ‘Adebayor’ wa Azam FC, ambaye Watanzania wanatakiwa kumuombea dua asiumie ili aendelee kuibeba timu yao ya taifa.

POULSEN HAJAKATA TAMAA, ALIA NA BAHATI JANA

Kim Poulsen jana

KOCHA Mkuu wa timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Kim Poulsen, raia wa Denmark, amesema kwamba bado ana matumaini ya kutinga Robo Fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge licha ya jana kuchapwa 1-0 na Burundi.
Mbaya wa Kim na Stars jana, alikuwa mshambuliaji wa zamani wa Simba SC ya Dar es Salaam, Suleiman Ndikumana aliyefunga bao hilo dakika ya 52, katika mchezo huo wa Kundi B, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole.
Akizungumza mara baada ya mechi ya jana, Poulsen alisema kwamba anaamini wakishinda mechi ya mwisho dhidi ya Somalia, watasonga mbele.
Hata hivyo, Kim alisema haidharau Somalia kwani imeonyesha mchezo mzuri katika mechi zake zote mbili pamoja na kufungwa.
“Nina muda mzuri kidogo wa kujiandaa na mchezo huo hadi Jumamosi, tutajiandaa vizuri na nina matumaini ya kushinda,”alisema.
Akizungumzia mchezo wa jana, Kim alisema walitengeneza nafasi nyingi nzuri, lakini wakashindwa kuzitumia, mipira ikigonga mwamba na mingine ikiokolewa ikiwa inaelekea nyavuni, hivyo hana wa kumlaumu kwa matokeo hayo, bali habati haikuwa yao jana.
Burundi walipata bao lao kwa penalti jana Nahodha huyo wa Burundi, anayechezea Inter Stars ya nyumbani kwao kwa sasa, akifunga baada ya yeye mwenyewe kuangushwa kwenye eneo la hatari na Shomary Kapombe.
Hadi mapumziko hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango la mwenzake na Burundi walifanya mashambulizi mawili ya hatari zaidi, lakini sifa zimuendee ‘TZ One’, Juma Kaseja aliyeokoa hatari hizo.
Stars hawakucheza soka yao ya chini kutokana na hali mbaya ya Uwanja, kujaa matope, kuwa wenye kuteleza kutokana na mvua kubwa iliyonyesha kutwa nzima ya leo.
Kipindi cha pili Stars walijitahidi kutaka kusawazisha mabao hilo, lakini bahati haikuwa yao na zaidi waliishia kukosa mabao mawili ya wazi.
Kwa matokeo hayo, Burundi imeendelea kuongoza Kundi A, kwa pointi zao sita, mabao sita ya kufunga na moja la kufungwa, wakati Bara inabaki nafasi ya pili kwa pointi zake tatu, Sudan ya tatu ikiwa na pointi moja sawa na Somalia.
Kikosi cha Stars jana kilikuwa; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Amir Maftah, Shomary Kapombe/Issa Rashid, Kevin Yondan, Frank Domayo, Mrisho Ngassa, Salum Abubakar, John Bocco, Mwinyi Kazimoto/Shaaban Nditi na Simon Msuva/Amri Kiemba.

STARS WAOMBEWA VIAU VYA KUCHEZEA KWENYE MVUA KAMPALA

Mashabiki wanaoiunga mkono Stars mjini hapa

MASHABIKI wa Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars waliopo hapa, wameliomba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwatumia wachezaji wa timu hiyo viatu vya kuchezea kwenye mvua, kabla ya mechi ya mwisho ya Kundi B, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge Jumamosi.
Wakizungumza baada ya mechi ya jana dhidi ya Burundi, ambayo Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, walichapwa 1-0 kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole mjini mashabiki hao walisema hali ya hewa ya mji huu kwa sasa itaendelea kuwa ya mvua na TFF inapaswa kuchukua tahadhari baada ya matokeo ya jana.
“Leo tumefungwa kwa sababu Uwanja ulikuwa unateleza kutokana na mvua na wenzetu Burundi walikuwa wana viatu vya mvua, kwa hivyo Uwanja haukuwasumbua, sasa na sisi lazima wachezaji wetu wapatiwe viatu hivyo,”alisema  Ally Abubakar aliyetoka River Side, Ubungo, Dar es Salaam kuja kuishangilia timu ya taifa.  
Mbaya wa Stars jana, alikuwa mshambuliaji wa zamani wa Simba SC ya Dar es Salaam, Suleiman Ndikumana aliyefunga bao hilo dakika ya 52, katika mchezo huo wa Kundi B, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole.
Burundi walipata bao lao kwa penalti jana Nahodha huyo wa Burundi, anayechezea Inter Stars ya nyumbani kwao kwa sasa, akifunga baada ya yeye mwenyewe kuangushwa kwenye eneo la hatari na Shomary Kapombe.
Hadi mapumziko hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango la mwenzake na Burundi walifanya mashambulizi mawili ya hatari zaidi, lakini sifa zimuendee ‘TZ One’, Juma Kaseja aliyeokoa hatari hizo.
Stars hawakucheza soka yao ya chini kutokana na hali mbaya ya Uwanja, kujaa matope, kuwa wenye kuteleza kutokana na mvua kubwa iliyonyesha kutwa nzima ya leo.
Kipindi cha pili Stars walijitahidi kutaka kusawazisha mabao hilo, lakini bahati haikuwa yao na zaidi waliishia kukosa mabao mawili ya wazi.
Kwa matokeo hayo, Burundi imeendelea kuongoza Kundi A, kwa pointi zao sita, mabao sita ya kufunga na moja la kufungwa, wakati Bara inabaki nafasi ya pili kwa pointi zake tatu, Sudan ya tatu ikiwa na pointi moja sawa na Somalia.

ZANZIBAR KUJARIBU BAHATI TENA LEO TUSKER CHALLENGE, KUKIPIGA NA RWANDA NI VITA YA NIYONZIMA NA CANNAVARO

Zanzibar Heroes
MASHUJAA wa visiwani, Zanzibar Heroes leo wanatupa kete yao ya pili katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge kwa kumenyana na Rwanda katika mchezo wa Kundi C, utakaoanza saa 12:00 jioni Uwanja wa Mandela, Namboole, mjini hapa.
Mchezo huo utatanguliwa na mchezo mwingine, kati ya Malawi na Eritrea ambao utaanza saa 10:00 jioni kwenye Uwanja huo.
Zanzibar walilazimishwa sare ya bila kufungana na Eritrea katika mchezo wa kwanza, wakati Malawi ilifungwa mabao 2-0 na Rwanda.
Zanzibar wanahitaji kushinda mechi ya leo, ili kuweka hai matumaini ya kuingia Robo Fainali ya michuano hii, ingawa mbele ya Rwanda huo utakuwa mtihani mgumu kwao.
Moja kati ya burudani zinazotarajiwa kwenye mechi hiyo ni kushuhudia wachezaji wawili wa klabu moja, Yanga SC ya Dar es Salaam, beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wa Zanzibar na kiungo Haruna Niyonzima wa Rwanda, wakichuana leo, tena wote wakiwa manahodha wa timu zao za taifa.
Baada ya sare katika mechi ya kwanza, Cannavaro pamoja na kuwaomba radhi Wazanzibari kwa sare hiyo, lakini pia ameahidi watajituma na kufanya vizuri katika mechi zijazo. 
MECHI ZILIZOSALIA:
RATIB KUNDI A:
Novemba 30, 2012:
Kenya v Ethiopia                  (Saa 9:00 Alasiri)
Sudan Kusini v Uganda       (Saa 12:00 jioni)
RATIBA KUNDI B:
Desemba 1, 2012:
Sudan v Burundi                 (Saa 9:00 Alasiri)
Somalia v Tanzania             (Saa 12:00 jioni)
RATIBA KUNDI C:
Novemba 29, 2012:
Malawi v Eritrea                   (Saa 9:00 Alasiri)
Rwanda v Zanzibar             (Saa 12:00 jioni)
Desemba 2, 2012:
Malawi v Zanzibar               (Saa 9:00 Alasiri)
Eritrea v Rwanda                (Saa 12:00 jioni)
MSIMAMO KUNDI A:
                      P   W  D   L    GF GA GD Pts
Uganda          2    2    0    0    2    0    2    6
Kenya             2    1    0    1    2    1    1    3
Ethiopia          2    1    0    1    1    1    0    3
Sudan Kusini  2    0    0    2    0    3    -3  0
MSIMAMO KUNDI B:
                     P   W  D   L    GF GA GD Pts
Burundi         2    2    0    0    6    1    5    6
Tanzania       2    1    0    1    2    1    1    3
Sudan           2    1    0    1    1    2    -1  3
Somalia         2    0    0    2    1    6    -5  0
MSIMAMO KUNDI C:
                      P   W  D   L    GF GA GD Pts
Rwanda         1    1    0    0    2    0    2    3
Eritrea            1    0    1    0    0    0    0    1
Zanzibar         1    0    1    0    0    0    0    1
Malawi            1    0    0    1    0    2    -2  0
VIWANGO VYA UBORA FIFA
NCHI                 NAFASI
Uganda             86
Malawi              101
Ethiopia            102
Sudan               102
Rwanda             122
Burundi             128
Kenya                130
Tanzania           134
Zanzibar            134
Somalia             193
Eritrea               192
Sudan Kusini     200
(Viwango hivi vimetoka mwezi huu)


BPL: Man United BADO JUU, City wapo, Chelsea yanasa tena!

>>LIVERPOOL yachapwa na Spurs, Everton na Arsenal drooo!!
BPL_LOGOMechi 8 za Ligi Kuu England, BPL [Barclays Premier League], zilichezwa Jumatano  Usiku na Bao la Sekunde ya 31 la Robin van Persie limeendelea kuwaweka Manchester United kileleni mwa Ligi wakiwa Pointi 1 mbele ya Man City walioichapa Wigan 2-0 lakini sare ya Chelsea na Fulham imewabakisha Chelsea nafasi ya 3 na kuwafanya wawe Pointi 7 nyuma ya vinara Man United.
+++++++++++++++++++++++++++
MATOKEO:
Jumatano Novemba 28
Chelsea 0 Fulham 0
Everton 1 Arsenal 1
Southampton 1 Norwich 1
Stoke 2 Newcastle 1
Swansea 3 West Brom 1
Tottenham 2 Liverpool 1
Wigan 0 Man City 2
Man United 1 West Ham 0
+++++++++++++++++++++++++++
WIGAN 0 MAN CITY 2
Hadi Haftaimu Bao zilikuwa 0-0 lakini Bao mbili zilizofungwa na Mario Balotelli na James Milner katika Dakika za 69 na 72 ziliwapa ushindi Man City na kuwabakiza nafasi ya pili Pointi 1 nyuma ya Man United.
VIKOSI:
Wigan: Al Habsi, Stam, Boyce, Lopez, Figueroa, McCarthy, Jones, Gomez, Kone, Beausejour, Di Santo. Subs: Pollitt, McManaman, McArthur, Boselli, Fyvie, Golobart, Redmond.
Man City: Hart, Maicon, Kompany, Nastasic, Zabaleta, Javi Garcia, Toure, Silva, Barry, Aguero, Balotelli. Subs: Pantilimon, Toure, Kolarov, Milner, Sinclair, Tevez, Dzeko.
Refa: Mark Halsey
MAN UNITED 1 WEST HAM 0
Bao la Sekunde ya 31 tangu mpira uanze la Robin van Persie baada ya pande la Michael Carrick limewapa Man United ushindi wa Bao 1-0 na kuwabakisha kileleni mwa Ligi.
VIKOSI:
Man United: Lindegaard, Da Silva, Smalling, Evans, Evra, Carrick, Anderson, Cleverley, Rooney, van Persie, Hernandez
Akiba: De Gea, Jones, Ferdinand, Young, Welbeck, Fletcher, Buttner.
West Ham: Jaaskelainen, Demel, Reid, Collins, O'Brien, Taylor, Diame, Tomkins, Jarvis, Nolan, Carroll
Akiba: Spiegel, Cole, Maiga, Spence, O'Neil, Moncur, Lletget.
Refa: Mike Jones
TOTTENHAM 2 LIVERPOOL 1
Uwanjani White Hart Lane, Aaron Lennon na Gareth Bale walipachika Bao kwa Tottenham lakini pia Bale alijifunga mwenyewe na Mechi kwisha 2-1 kwa ushindi kwa Tottenham.
VIKOSI:
Tottenham: Lloris, Walker, Gallas, Dawson, Vertonghen, Lennon, Sandro, Dembele, Bale, Dempsey, Defoe
Akiba: Friedel, Huddlestone, Naughton, Sigurdsson, Livermore, Townsend, Carroll.
Liverpool: Reina, Johnson, Agger, Skrtel, Downing, Allen, Henderson, Gerrard, Jose Enrique, Sterling, Suarez
Akiba: Jones, Sahin, Assaidi, Carragher, Fernandez Saez, Shelvey, Wisdom.
Refa: Phil Dowd
STOKE 2 NEWCASTLE 1
Newcastle walitangulia kufunga kwa Bao la Papiss Cisse katika Dakika ya 47 lakini Bao za Walters na Jerome za Dakika ya 81 na 85 ziliwainua kidedea Stoke City kwa Bao 2-1.
VIKOSI:
Stoke: Begovic, Shotton, Huth, Shawcross, Cameron, Walters, Nzonzi, Whelan, Etherington, Adam, Crouch
Akiba: Sorensen, Palacios, Jones, Whitehead, Upson, Kightly, Jerome.
Newcastle: Krul, Simpson, Coloccini, Williamson, Santon, Anita, Perch, Tiote, Gutierrez, Ba, Cisse
Akiba: Elliot, Bigirimana, Marveaux, Sammy Ameobi, Ranger, Ferguson, Tavernier.
Refa: Howard Webb
SWANSEA 3 WEST BROM 1
Swansea wameifunga WBA Bao 3-1 kwa Bao za Michu na mbili za  Routledge huku bao la WBA likifungwa na Romelu Lukaku.
VIKOSI:
Swansea: Tremmel, Rangel, Williams, Chico, Davies, Britton, Hernandez, Ki, Dyer, Routledge, Michu
Akiba: Cornell, Monk, Shechter, Moore, de Guzman, Tiendalli, Agustien.
West Brom: Myhill, McAuley, Olsson, Ridgewell, Jones, Yacob, Morrison, Mulumbu, Brunt, Odemwingie, Lukaku
Akiba: Daniels, Popov, Rosenberg, Long, Dorrans, Tamas, Fortune.
Refa: Lee Mason
CHELSEA 0 FULHAM 0
Hii ni Mechi ya pili mfululizo kwa Meneja mpya wa Chelsea Rafael Benitez kutoka 0-0.
VIKOSI:
Chelsea: Cech, Azpilicueta, Ivanovic, Luiz, Cole, Romeu, Ramires, Hazard, Oscar, Bertrand, Torres
Akiba: Turnbull, Mata, Mikel, Moses, Ferreira, Marin, Cahill.
Fulham: Schwarzer, Riether, Senderos, Hughes, Riise, Duff, Diarra, Sidwell, Karagounis, Rodallega, Berbatov
Akiba: Etheridge, Kelly, Baird, Kasami, Petric, Frei, Dejagah.
Refa: Anthony Taylor
EVERTON 1 ARSENAL 1
Uwanjani Goodison Park, Arsenal walitangulia kwa bao la mapema la Theo Walcott aliefunga katika Sekunde ya 50 tu tangu Mechi ianze lakini Marouane Fellaini akaisawazishia Everton.
VIKOSI:
Everton: Howard, Hibbert, Jagielka, Distin, Baines, Naismith, Gibson, Osman, Pienaar, Fellaini, Jelavic
Akiba: Mucha, Heitinga, Oviedo, Hitzlsperger, Gueye, Barkley, Vellios.
Arsenal: Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Vermaelen, Walcott, Ramsey, Arteta, Wilshere, Cazorla, Girou
Akiba: Mannone, Rosicky, Oxlade-Chamberlain, Coquelin, Jenkinson, Gervinho, Gibbs.
Refa: Michael Oliver
SOUTHAMPTON V NORWICH
VIKOSI:
Southampton: Gazzaniga, Clyne, Yoshida, Fonte, Shaw, Puncheon, Schneiderlin, Cork, Lallana, Lambert, Ramirez
Akiba: Kelvin Davis, Hooiveld, Steven Davis, Rodriguez, Do Prado, Mayuka, Reeves.
Norwich: Bunn, Whittaker, Ryan Bennett, Bassong, Garrido, Snodgrass, Johnson, Tettey, Pilkington, Hoolahan, Holt
Akiba: Rudd, Martin, Howson, Jackson, Morison, Elliott Bennett, Barnett.
Refa: Mark Clattenburg
+++++++++++++++++++++++++++
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumamosi 1 Desemba 2012
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
West Ham v Chelsea
[SAA 12 Jioni]
Arsenal v Swansea
Fulham v Tottenham
Liverpool v Southampton
Man City v Everton
QPR v Aston Villa
West Brom v Stoke
[SAA 2 Dak 30 Usiku]
Reading v Man United
Jumapili Desemba 2
[SAA 1 Usiku]
Norwich v Sunderland
Jumatatu Desemba 3
[SAA 5 Usiku]
Newcastle v Wigan
 

UFUKWENI COPACABANA: Hodgson ashuhudia umahiri wa Brazil!!

>>ASHUHUDIA, Bibi na Bwana wakipiga DANADANA!!!
ROY_HODGSON-ENGLAND_MENEJAAkiwa ziarani, Rio de Janeiro, akitembea kwenye Ufukwe wa Copacabana, Roy Hodgson, Meneja wa England, alishuhudia kitu kilichomfungua macho na kubaini kuwa Wabrazil ni wakali kujenga vipaji vyao na kukubali kuwa wakati umefika kwa England kuchukua hatua za makusudi ili waweze kufanya vyema zaidi katika Ulimwengu wa Soka.BRAZIL_SAMBA
Hodgson ameeleza: “Niliwaona Watu wawili, Mwanamke na Mwanaume, wakiwa wamesimama Mita 25 toka kila mmoja na yule Mwanaume alikuwa akiupiga mpira kichwani kwa Mwanamke na yule Mama anarudisha kwa Kichwa miguuni kwa yule jamaa! Nilisimama kutazama danadana ile itachukua muda gani…iliendelea kwa Dakika 12 bila kusimama wala mpira kudondoka chini! Nikakata tamaa nikaondoka, niliporudi tena pale niliwakuta bado wapo, danadana inaendelea na mpira uko juu tu haugusi chini!”
Aliongeza: “Hapa England, tunafanya mazoezi ya kujenga ufundi wa kumiliki mpira kwa Dakika 5 au 10 tu, kisha tunataka kucheza Gemu!”
Hodgson amesema hiyo inaonyesha tofauti kati ya Brazil, ambao wametwaa Kombe la Dunia mara 5, na England iliyotwaa mara moja tu na tangu Mwaka 1996, walipofika Robo Fainali ya EURO 1996, hawajaweza kuvuka Robo Fainali yeyote ya Mashindano makubwa.
Ingawa amekiri kuwa hali ya hewa ya Brazil, ambako ni joto, ukilinganisha na England kwenye baridi na mvua kunawafanya wapata urahisi wa kucheza Soka mfululizo, lakini pia amelaumu miundo mbinu ukilinganisha na Nchi nyingine za Ulaya ambazo zina Viwanja vingi vya ndani ambavyo huweza kutumika wakati wowote wa Mwaka hata wakati wa Winta kali ambapo Nchi hufunikwa barafu.