Friday, December 28, 2012

MEIRELES APUNGUZIWA ADHABU YA KUFUNGIWA MECHI 11 MPAKA MECHI 4 - YATHIBITIKA HAKUMTEMEA MATE MWAMUZI

Mchezaji wa zamani wa Liverpool na Chelsea kiungo Raul Meireles amepata nafuu ya kupunguziwa adhabu ya kutocheza mechi 11 mpaka kufikia mechi 4.
Mchezaji huyo wa Fenerbahce, 29, alikata rufaa baada ya kuhukumiwa kwa kosa la kumtemea mate mwamuzi kufuatiwa kupewa kadi nyekundu katika mechi ya iliyowakutanaisha mahasimu wao ligi ya Uturuki klabu ya Galatasary.

Shirikisho la soka la Uturuki limesema ilikuwa ni vigumu kwa mchezaji kutema mate kwa kuwa alikuwa anaongea wakati wote wa tukio hilo, hata hivyo bado atakabiliwa na adhabu ya kukosa mechi nne kwa kumtukana mwamuzi.

VIDEO YA AMBWENE YESSAYA--------MONEY

BAADA YA KUPANDIKIZIWA INNI JINGINE ABIDAL ASEMA YUPO FITI


BEKI wa Barcelona Eric Abidal amesema anajisikia vyema na yuko tayari kurejea tena uwanjani ikiwa ni miezi nane imepita toka afanyiwe upasuaji wa kupandikizwa ini jingine. Akihojiwa Abidal mwenye umri wa miaka amesema ni muda mwingi umepita toka afanyiwe upasuaji na amekuwa akipambana ili aweze kurejea katika hali yake kawaida. Abidal alifanyiwa upasuaji wa kupandikiza ini jingine April 10 ikiwa ni mwaka mmoja toka alipoondolewa uvimbe wa kansa katika ini lake Machi 2011. Beki huyo alianza kufanya mazoezi na wachezaji wenzake Desemba 19 siku ambayo ndiyo taarifa za kocha wa klabu Tito Vilanova kurudiwa na tatizo la kansa ya koo zilipotangazwa. Vilanova naye alifanyiwa upasuaji mwingine wa kuondoa uvimbe huo wa kansa na baadae kuruhusiwa kutoka hospitali ambapo kwasasa anaendelea na matibabu ya mionzi kwa kipindi cha wiki sita.

ARSENAL YAMTENGEA VILLA PAUNDI MILIONI 16.


KLABU ya Arsenal imetangaza dau la paundi milioni 16 kwa ajili ya kumnasa mshambuliaji wa Barcelona, David Villa. Meneja wa klabu hiyo Arsene Wenger ameonyesha nia ya kumtaka mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31 lakini maofisa wa Arsenal wameambiwa kuwa watahitajika kulipa kiasi cha paundi milioni 20 kama watahitaji kumng’oa mshambuliaji hyo wa kimataifa wa Hispania. Hatahivyo kiasi hicho cha fedha kilichotajwa na Barcelona kinaweza kuwa kikubwa kwa Arsenal kwasababu ya umri wa Villa. Mbali na Arsenal Chelsea nao wameonesha nia ya kutaka kumsajili nyota huyo ambaye ni mfungaji wa kihistoria nchini Hispania ili aweze kusaidiana na Eden Hazard na Fernando Torres katika safu ya ushambuliaji wa klabu hiyo.

NYOTA W AURUGUAY NA KLABU YA NAPOLI ASEMA HAKUNA KILICHOBADILIKA - CAVANI.


MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Uruguay na klabu ya Napoli ya nchini Italia, Edinson Cavani amesisitiza kuwa hakuna chochote kilichobadilika baada ya kugundua kuwa klabu yake hiyo ilikataa ofa ya euro milioni 55 ili wamuuze. Cavani ndiye mshambuliaji ghali zaidi katika Ligi Kuu nchini Italia maarufu kama Serie A akiwa amefunga mabao 13 katika ligi bao moja nyumba Stephan El Shaarawy ambaye anaongoza kwa ufungaji kwasasa. Dau hilo kubwa ambalo lilitolewa na klabu ambayo haijajulikana halijamuathiri nyota huyo ambaye amsisitiza bidii zake katika mazoezi ndizo zilizomfanya kufikia thamani hiyo. Cavani amesema taarifa za Napoli kukataa dau hilo haziwezi kumwathiri kwani amepanga kuendelea kuisaidia klabu hiyo katika mwaka 2013 kwa bidii zote ili waweze kupata mafanikio katika kila mashindano. Napoli inashika nafasi ya sita ikiwa nyuma ya klabu za Juventus, Fiorentina, Lazio na Inter Milan katika msimamo wa Serie A.

BPL: NI MOTO KUAGA 2012 WIKIENDI!!

BPL_LOGOKLABU ZOTE 20 zitaingia dimbani Jumamosi na Jumapili kucheza Mechi zao za mwisho za Mwaka 2012 kwenye BPL, Barclays Premier League, kwa akina sie tunaiita Ligi Kuu England, na zipo Mechi kadhaa ambazo, bila shaka, zitakuwa tamu na mvuto, na baadhi ya hizo ni zile za Arsenal v Newcastle, Everton v Chelsea.
Zifuatazo ni Dondoo muhimu kuhusu mitanange hiyo ikiwa pamoja na Hali za Wachezaji wa kila Timu na Marefa:
+++++++++++++++++++++++
RATIBA:  
Jumamosi 29 Desemba 2012
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Sunderland v Tottenham
[SAA 12 Jioni]
Aston Villa v Wigan
Fulham v Swansea
Man United v West Brom
Norwich v Man City
Reading v West Ham
Stoke v Southampton
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Arsenal v Newcastle
+++++++++++++++++++++++
SUNDERLAND V TOTTENHAM HOTSPUR 
Sunderland wataivaa Spurs bila Beki wa kushoto Danny Rose ambae haruhusiwi kucheza dhidi ya Klabu yake Tottenham kwa vile yupo hapo Sunderland kwa Mkopo.
Badala ya Danny Rose, huenda Sunderland wakamchezesha Phil Bardsley kwenye nafasi hiyo.
Tottenham wanaweza kuwa nao tena majeruhi wao waliopona Clint Dempsey na Tom Huddlestone na pia upo uwezekano wa Wachezaji wao walioumia kwa muda mrefu na sasa kuwa fiti kuanza Mechi yao ya kwanza na hao ni Benoit Assou-Ekotto na Scott Parker.
MATOKEO MECHI WALIZOCHEZA MWISHONI:
Sunderland 1 Man City 0
Aston Villa 0 Tottenham 4
Refa: Martin Atkinson
[Gemu; 15 Kadi za Njano 59 Kadi Nyekundu: 0]
Wasaidizi: P Kirkup & S Burt
Refa wa Akiba: Mike Dean
ARSENAL V NEWCASTLE UNITED 
Wachezaji wawili wa Arsenal, Olivier Giroud na Tomas Rosicky, wameshapona na wanaweza kucheza kwenye Mechi kama watapangwa lakini Andre Santos na Abou Diaby bado ni majeruhi na wanatarajiwa kurudi Wiki ijayo.
Newcastle wana majeruhi kwa Wachezaji wao wanane na hivi karibuni Listi hiyo imeongezeka na Vurnon Anita (enka) na Jonas Gutierrez (goti).
Kiungo wa Newcastle Cheick Tiote amemaliza Kifungo chake cha Mechi moja lakini Mike Williamson atatumikia Kifungo cha Mechi moja baada ya kufikisha Kadi za Njano 5.
MATOKEO MECHI WALIZOCHEZA MWISHONI:
Man United 4 Newcastle 3
Wigan 0 Arsenal 1
Refa: Chris Foy
[Gemu: 13 Kadi za Njano: 21 Kadi Nyekundu: 0]
Wasaidizi: S Child & H Lennard Refa wa Akiba: Anthony Taylor
NORWICH CITY V MANCHESTER CITY 
Norwich watacheza bila ya Beki wao Steven Whittaker ambae ni majeruhi na nafasi yake itachukuliwa na Russell Martin.
Manchester City wanaweza kuwa nao tena Samir Nasri na Gael Clichy ambao wamepona maumivu yao lakini watamkosa Mchezaji wao machachari Mario Balotelli ambae ni mgonjwa.
MATOKEO MECHI WALIZOCHEZA MWISHONI:
Norwich 0 Chelsea 1
Sunderland 1 Man City 0
Refa: Mike Jones
[Gemu: 12 Kadi za Njano: 44 Kadi Nyekundu: 1]
Wasaidizi: S Ledger & M McDonough
Refa wa Akiba: Craig Pawson
MANCHESTER UNITED V WEST BROMWICH ALBION
Manchester United watakuwa nao tena Danny Welbeck, ambae amepona ugonjwa, na majeruhi Ashley Young na Phil Jones waliopona maumivu.
Nae Shinji Kagawa ameshapona Goti lake na anatarajiwa kuanzia Benchi kwa mujibu wa Meneja wao Sir Alex Ferguson.
Majeruhi wa West Brom ni Beki Jonas Olsson, Goran Popov na Kiungo Youssouf Mulumbu.
MATOKEO MECHI WALIZOCHEZA MWISHONI:
Man United 4 Newcastle 3
QPR 1 West Brom 2
Refa: Jon Moss
[Gemu: 10 Kadi za Njano: 27 Kadi Nyekundu: 1]
Wasaidizi: A Garratt & C Breakspear
Refa wa Akiba: Phil Dowd  
READING V WEST HAM UNITED
Meneja wa Reading Brian McDermott amethibitisha hawana majeruhi na pia upo uwezekano wa Straika wao Jason Roberts kucheza baada ya kupona maumivu.
Straika wa West Ham Carlton Cole anaweza kucheza baada ya FA kuifuta Kadi Nyekundu aliyopewa Wiki iliyopita walipocheza na Everton.
MATOKEO MECHI WALIZOCHEZA MWISHONI:
Reading 0 Swansea 0
West Ham 1 Everton 2
Refa: Michael Oliver
[Gemu:: 11 Kadi za Njano: 26 Kadi Nyekundu: 1]
Wasaidizi: S Bennett & M Scholes
Refa wa Akiba: Paul Tierney
ASTON VILLA V WIGAN ATHLETIC 
Timu hizi zote hazina Listi za majeruhi lakini zinatoka kwenye vipigo vizito mfululizo.
MATOKEO MECHI WALIZOCHEZA MWISHONI:
Aston Villa 0 Tottenham 4
Everton 2 Wigan 1
Refa: Kevin Friend
[Gemu: 11 Kadi za Njano: 42 Kadi Nyekundu: 2]
Wasaidizi: J Flynn & D England
Refa wa Akiba: Howard Webb
FULHAM V SWANSEA CITY  
Fulham hawana majeruhi lakini Swansea kuna hatihati kuhusu Wachezaji wao Mahamadou Diarra, Mladen Petric na Straika wao hatari Muchu ambao wana maumivu.
MATOKEO MECHI WALIZOCHEZA MWISHONI:
Fulham 1 Southampton 1
Reading 0 Swansea 0
Refa: Andre Marriner
[Gemu: 10 Kadi za Njano: 38 Kadi Nyekundu: 0]
Wasaidizi: R West & S Massey
Refa wa Akiba: Neil Swarbrick
STOKE CITY V SOUTHAMPTON 
Bosi wa Stoke City Tony Pulis atalazimika kutafuta Mabeki wengine kwa vile Nahodha wao Ryan Shawcross na Geoff Cameron wote wapo kwenye Kifungo cha Mechi moja baada kulimbikiza Kadi za Njano 5 kila mmoja.
Southampton watamkosa Nahodha Adam Lallana ambae ameumia goti.
MATOKEO MECHI WALIZOCHEZA MWISHONI:
Stoke 3 Liverpool 1 
Fulham 1 Southampton 1
Refa: Mark Clattenburg
[Gemu: 10 Kadi za Njano: 35 Kadi Nyekundu: 4]
Wasaidizi: S Beck & S Long
Refa wa Akiba: Lee Mason
+++++++++++++++++++++++
MECHI ZIJAZO:  
Jumapili 30 Desemba 2012
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Everton v Chelsea
[SAA 1 Usiku]
QPR v Liverpool
Jumanne 1 Januari 2013
SAA 9 Dak 45 Mchana]
West Brom v Fulham
[SAA 12 Jioni]
Man City v Stoke
Swansea v Aston Villa
Tottenham v Reading
West Ham v Norwich
Wigan v Man United
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Southampton v Arsenal
Jumatano 2 Januari 2013
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Chelsea v QPR
Liverpool v Sunderland
[SAA 5 Usiku]
Newcastle v Everton

KLABU ZOTE KUGOMEA LIGI KUU VODACOM??

TFF_LOGO12
KLABU ZASUBIRI FEDHA ZAO TRA ZICHEZE LIGI KUU
Klabu 14 ambazo timu zao zinashiriki Ligi Kuu ya Vodacom zimesema hazitacheza hatua ya pili ya Ligi hiyo inayotarajiwa kuanza Januari 26 mwakani hadi zitakaporejeshewa fedha zao zilizochukuliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutoka kwenye moja ya akaunti za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Novemba 23 mwaka huu, TRA kwa uwezo ilionao kisheria iliielekeza benki ya NMB kuilipa fedha hizo (sh. 157,407,968) kutoka kwenye moja ya akaunti za TFF ikiwa ni Kodi ya Lipa Kama Unavyopata (PAYE) kutoka kwenye mishahara ya waliokuwa makocha wa timu za Taifa.
Serikali ndiyo inayolipa mishahara ya makocha hao moja kwa moja kwenye akaunti zao, lakini ilikuwa haikati PAYE kutoka kwenye mishahara hiyo, hivyo malimbikizo kufikia sh. 157,407,968.
TFF bado inaendelea na mazungumzo na pande husika (Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa upande mmoja na TRA kwa upande mwingine) ili fedha hizo zirejeshwe kwani zilitolewa na mdhamini wa Ligi Kuu (kampuni ya Vodacom) kwa ajili ya maandalizi ya timu hizo tayari kwa mzunguko wa pili wa Ligi hiyo.


OFISA WA CAF KUTUA MWAKANI KUKAGUA VIWANJA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) litamtuma nchini ofisa wake Abbas Sendyowa kukagua viwanja na hoteli ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa utaratibu wa klabu kupata leseni zitakazoziwezesha kushiriki michuano inayoandaliwa na Shirikisho hilo.
Ofisa huyo kutoka Uganda atawasili nchini Januari 7 mwakani ambapo anatarajiwa kukamilisha kazi hiyo Januari 14 mwakani na baadaye kupeleka ripoti yake CAF.
Utekelezaji wa kazi yake nchini utahusisha mwakilishi kutoka TFF, mwakilishi kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, mameneja wa viwanja husika na Ofisa Usalama wa TFF.

NAZARIUS KILUNGEJA AONDOLEWA UCHAGUZI RUREFA
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekubaliana na uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Rukwa (RUREFA) kumuondoa Nazarius Kilungeja kugombea uenyekiti katika uchaguzi wa chama hicho.
Kutokana na uamuzi huo, Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeiagiza Kamati ya Uchaguzi ya RUREFA kuendelea na mchakato wa uchaguzi huo kama ilivyopangwa awali.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

IBF YAMPONGEZA CHEKA KWA KUTWAA UBINGWA



Shirilisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) limepongeza bingwa mpya wa uzito wa Super Middle katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki yaa Kati, Mtanzania Francis Cheka.
Katika barua yake aliyomtumia Francis Cheka ya tarehe 28/12/2012 Mwenyekiti wa kamati ya Ubingwa wa IBF/USBA Lindsey Tucker alisema "Tunachukua fursa hii kukutakia maisha na mafanikio mazuri kama bingwa wa IBF na kumhimiza kuishi kama bingwa". Cheka atatakiwa kutetea taji lake katika kipindi cha miezi sita kufikia mwezi wa 6 mwakani dhidi ya mpinzani ambaye ana rekodi ya mapambano yasiyopungua 15 na mengi awe ameyashinda hususan mapambano mawili ya mwisho.
Aidha IBF inampongeza bondia Chiotcha Chimwemwe kutoka Malawi kwa ushupavu wake na ushindani mzuri katika pambano hilo lililofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid katika jiji la Arusha tarehe 26 Desemba, 2012.
Imetolewa na:
Onesmo A.M. Ngowi
Rais
IBF/USBA Afrka, Ghuba ya Uajemi an Mashariki ya Kati

SIMBA SC YAWAACHIA MAKINDA WAKE MANOTI YOTE YA UHAI CUP



KUFUATIA kupewa zawadi ya mshindi wa tatu katika mashindano ya Kombe la Uhai yaliyomalizika hivi karibuni, uongozi wa Simba umeamua kuwapa wachezaji wake fedha zote (Sh laki tano) za zawadi kwa mshindi wa nafasi hiyo wagawane. 
Hatua hii ya uongozi ina lengo la kuwafanya wachezaji walioshiriki mashindano hayo wajitume zaidi katika mashindano mengine ambayo watahitajika kuitumikia klabu ya Simba.

FAINALI UNIQUE MODEL 2012 LEO@NEW MAISHA CLUB


FAINALI za shindano la kumsaka mwanamitindo mwenye sifa za kipekee ‘Unique Model’ kwa mwaka 2012 zinatarajiwa kufanyika leo kwenye ukumbi wa New Maisha Club uliopo Oyesterbay jijini Dar es Salaam  ambapo warembo 12 watachuana kuwania taji hilo. 
Mkurugenzi wa Unique Entertainment inayoandaa shindano hilo, Methuselah Magese alisema kwamba maandalizi ya shindano hilo yamekamilika, hivyo amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kushuhudia fainali hizo. 
Alisema  shindano hili linatarajiwa kuwa na ushi ndani mkubwa kutokana na washiriki wake kuwa na viwango vya hali ya juu hali itakayowapa mtihani mkubwa majaji katika maamuzi yao. 
Magese aliwataja washiriki hao ni Janecy Maluli,Judith Sangu,Vestina Charles,Catherine Masumbigana,Darling Godfrey,Amina Ayoub,Elizabeth Pertty,Lulu Mramba ,Sadory Kendra,Elizabeth Borniface na Zeenarth Habib ambao walikuwa kambini kwenye hoteli ya Lamada kwa wiki mbili chini ukufunzi wa Wancy Nells kwa upande wa miondoko na Denis Lucas kwa upande wa shoo. 
Aidha, Magesa alisema tayari Baraza la sanaa la Taifa (BASATA) limeteuwa majina matatu ya majaji  watakaoshiriki katika kumchagua mshindi wa taji hilo linoloshikiliwa na Asia Dachi kuwa ni wabunifu  Asia  Idarous Khamsini,Gymkhana Hilall  ‘paka wear’ na Martin Kadinda ‘Singo Button’. 
Shindano hilo limedhaminiwa na Giraffe Ocean view Totel,Kitwe General Traders,Sophanaa Investment ltd,Dtv,88.4 clouds fm,Magazeti ya  Tanzania Daima na Kiu,Mashujaa Investment Ltd,Blogu za Michuzi,jiachie,Mtaa kwa Mtaa, Unique Entertainment,, Lamada Apartments & Hotel, Fabak fashions,Genessis Health Center na Yung don Records,Paka Wear na Mtoko Design litapambwa na burudani toka bendi ya mashujaa ikiongozwa na rapa maarufu Chalz Baba, msanii wa ngoma za asili toka kwa Costa Siboka na msanii wa bongo flava B-shop.

FAINALI KAWAMBWA CUP KUPIGWA KESHO VIWANJA VYA MWANAKELENGE



FAINALI za mashindano ya kombe la mbunge wa Bagamoyo, Dk Shukuru Kawambwa ambaye pia ni Waziri  wa Elimu na Mafunzo ‘Kawambwa Cup’ zinatarajiwa kupigwa lkesho kwenye uwanja wa Mwanakelenge kwa kuzikutanisha timu za Mataya Fc na Beach Boys Fc, ambapo mshindi ataondoka na kombe pamoja na kitita cha sh.400,000. 
Timu hizo zilitinga faianli hiyo hiyo baada ya Mataya kuichapa Chaulu Fc mabao 3-1, huku Beach Boys iliwafunga Matimbwa Fc mabao 2-0 katika mechi za nusu fainali zilizopigwa juzi. 
Mratibu wa mashindano hayo, Masau Bwire alisema jana kwamba maandalizi ya fanali hizo yamekamilika ambapo pamoja na zawadi hizo, bingwa huyo pia atazawadiwa seti mbili za jezi, mipira miwili na seti moja ya vizuia ugoko. 
Alisema, mshindi wa pili atazawadiwa seti mbili za jezi, mipira miwili, seti moja ya vizuia ugoko, na fedha taslimu sh 200,000, huku mshindi wa tatu atapata jezi seti moja, mpira mmoja, seti moja ya vizuia ugoko na fedha taslimu sh 100,000, huku mwamuzi bora, kipa bora na  mfungaji bora kila mmoja atazawadiwa sh 50,000. 
Bwire aliongeza kuwa mgeni rasmi katika fainali hizo anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na MIchezo Dk Fenella Mukangara, huku pia Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodger Tenga atahudhuria fainali hizo na uongozi wa Chama cha soka mkoani Pwani (COREFA), pia utahudhuria.

WAKALI HAWA YANGA SC NDIO WATAKAOKWENDA UTURUKI


 
Mabingwa mara mbili mfululizo wa Kombe la Vilabu Bingwa Afrika Mashariki al maarufu(Kagame Cup )timu ya Young Africans inatarajia kuondoka alfajiri ya jumapili kuelekea nchini Uturuki ambako itaweka kambi ya mazoezi kwa muda wa wiki mbili       Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga mitaa ya Twiga/Jangwani, Afisa Habari wa klabu ya Yanga Baraka Kizuguto amesema timu itaondoka alfajiri ya jumapili kwa shirika la ndege la Turkish Airline, ambapo itakua na msafara wa watu 34, wachezaji 27 na viongozi 7.
Timu itaondoka majira ya saa 10:30 alfajiri na itafika katika mji wa Instabul majira ya saa  5 kasoro dakika 10, kisha baadae majira ya saa 9 alasiri itaondoka kwenda katika mji wa Antalya uliopo kusini mwa nchi ya Uturuki ambapo itafika saa 10 ndio haswa itakapokuwa kambi ya timu alisema 'Kizuguto'
Kizuguto amesema timu itafikia katika hotel ya Sueno Beach iliyopo pembezoni mwa bahari ya Meditreanian, na itakua ikifanya mazoezi katika viwanja vikubwa viwili vilivyopo katika hotel hiyo na kiwanja kidogo cha nyasi bandia.
Majina ya watakosafiri keshokutwa alfajri ni:
Walinda Mlango: Ally Mustafa 'Barthez', Said Mohamed na Yusuph Abdul
Walinzi wa Pemebeni: Juma Abdul, Shadrack Nsajigwa, Godfrey Taita, Stephano Mwasika na Oscar Joshua
Walinzi wa kati: Mbuyu Twite, Nadir Haroub, Ladisalus Mbogo na Kelvin Yondani
Viungo: Athumani Idd, Frank Domayo, Haruna Niyonzima, Kabange Twite, Nurdin Bakari na Omega Seme
Viungo wa Pembeni: Saimon Msuva, Rehani Kibingu, Nizar Khalfani na David Luhende
Washambuliaji: Didier Kavumbagu, Said Bahanunzi, Jerson Tegete, George Banda na Hamis Kiiza 
Viongozi watakaoambatana na timu hiyo ni
Kocha Mkuu: Ernest Brandts,
Kocha msaidizi: Fred Felix Minziro,
Kocha wa makipa: Razaki Siwa,
Daktari wa timu: Dr.Suphian Juma,
Meneja wa timu:  Hafidh Saleh,
Afisa wa Habari : Baraka Kizuguto
na kiongozi mkuu wa msafara: Mohamed Nyenge ambae ni mjumbe wa kamati ya utendaji wa klabu ya Yanga

MFARANSA WA SIMBA SC ATAKUWAPO MECHI NA TUSKER JUMAMOSI TAIFA


Liewig
KOCHA mpya wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba SC, Mfaransa Patrick Liewig atakuwapo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Jumamosi siku timu hiyo ikimenyana na mabingwa wa Kenya, Tusker FC.
Ofisa Habari wa Simba SC, Ezekiel Kamwaga amesema kwamba, awali kocha huyo alitarajiwa kuawasili nchini jana, lakini imeshindikana baada ya kukosa nafasi kwenye ndege.
Alisema kocha huyo ambaye anakuja kurithi mikoba ya Mserbia Profesa Milovan Cirkovick, atakishuhudia kikosi cha Simba kikicheza mechi hiyo kabla ya kuendelea na taratibu nyingine ikiwemo kusaini mkataba wa kazi na baadaye kuanza kutumikia kibarua chake kipya.
Tusker FC ilianza vema ziara yake nchini, baada ya kuichapa Yanga 1-0 katika mchezo ulipigwa kwenye Uwanja wa Taifa juzi.
Simba SC wamepangwa kundi moja, A na Tusker FC ya Kenya, Bandari ya Unguja na Jamhuri ya Pemba katika michuano ya Kombe la Mapinduzi, inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi hivi karibuni visiwani Zanzibar.
Aidha, katika Kundi B, washindi wa pili wa Ligi Kuu ya Bara, Azam FC ya Dar e Salaam pia, imepangwa na Mtibwa Sugar ya Morogoro, Coastal Union  ya Tanga na Miembeni ya Unguja.
Michuano ya Kombe la Mapinduzi, ambayo ni maalum kwa ajili ya kuherehekea Mapinduzi matukufu ya Zanzaibar, inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 2, hadi kilele cha miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Januari 12, mwakani, huku ikishirikisha timu kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Kwa mujibu wa ratiba ya michuano hiyo iliyotolewa na Kamati Maalum ya Kusimamaia michuano hiyo, inaonesha kuwa katika mchezo wa kwanza utakaochezwa siku ya ufunguzi itakuwa ni kati ya Bandari kutoka Unguja ambayo itacheza na Jamhuri kutoka kisiwani Pemba ambao ni wawakilishi wa Zanzibar katika Kombe la Shirikisho Barani Afrika, pamabanolitakalochezwa katika uwanja wa Mao Tse Tung mjini Unguja, huku usiku wa siku hiyo hiyo katika Uwanja wa Amaan kisiwani Unguja pambano la ufunguzi rasmi katika mashindano hayo likiwakutanisha mabingwa wa soka nchini Tanzania, Simba SC ambao watapambana na mabingwa wa soka nchini Kenya, Tusker.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo jumla ya timu nane zitashiriki katika mashindano hayo ambayo yamejipatia umaarufu mkubwa visiwani hapa, timu hizo zimegawanya katika makundi mawili ambayo ni kama ifuatavyo:
Awali michuano hiyo ilitarajiwa kuanza kisiwani Pemba tarehe 1 Januari, lakini kutokana na kujitoa katika mashindano kwa klabu ya Al-Ahly ya Misri kutokana na klie kilichoelezwa sababu za kiusalama, mechi zote sasa zitachezwa kisiwani Unguja na ufunguzi ukipangwa kuanza tarehe 2 badala ya tarehe 1 januari.
Bingwa wa michuano hiyo ataondoka na zawadi ya kombe na fedha taslim Tsh.Milioni kumi (10,000,000), mshindi wa pili Milioni tano (5,000,000), pamoja na zawadi nyengine ambazo zimegawanywa katika makundi tofauti ikiwemo zawadi ya mfungaji bora, mchezaji bora, mwamuzi bora, kipa bora, mwandishi wa habari bora, timu bora na zawadi nyeanginezo.

MABINGWA WA KOMBE LA HISANI AZAM FC KAMBINI LEO


Azam FC
MABINGWA wa Kombe la Hisani la DRC, Azam FC wanatarajiwa kuanza mazoezi leo kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, baada ya mapumziko mafupi ya sikukuu ya Krisimasi.
Katika maozezi hayo, wachezaji watatu wa kigeni, beki Joackins Atudo, kiungo Humphrey Mieno wote wa Wakenya na mshambuliaji Brian Umony wa Uganda hawatakuwapo, kwa sababu bado wana udhuru hadi baada ya sikukuu ya Krisimasi.
Azam ilitua Dar es Salaam Jumatatu usiku, ikitokea Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ilikotwaa Kombe la Hisani, linaloandaliwa na FECOFA, Shirikisho la Soka la DRC.
Azam walitwaa taji hilo Jumamosi iliyopita, baada ya kuwachapa wenyeji, Dragons FC kwa penalti 4-2 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90.
Azam iliingia fainali, baada ya kufanikiwa kuitoa kwa mikwaju ya penalti 5-4 Shark FC ya DRC Ijumaa, kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90 kwenye Uwanja wa Martyrs.
Kikosi cha Azam kilichoshiriki mashindano hayo ni Kipre Tchetche, Seif Abdallah, Kipre Balou, Zahor Pazi, Jackson Wandwi, Malika Ndeule, Uhuru Suleiman, Omar Mtaki, Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo, Gaudence Mwaikimba, Abdi Kassim, Luckson Kakolaki, Samih Hajji Nuhu, Mwadini Ally, Himid Mao, David Mwantika, Waziri Salum, Humphrey Mieno na Joackins Atudo.
Katika mashindano hayo, Gaudence Mwaikimba aliibuka mfungaji bora kwa mabao yake matatu, ukiachilia mbali mawili ya penalti. Mchezaji mwingine wa kigeni wa Azam, Brian Umony wa Uganda, atajiunga na timu hiyo baada ya sikukuu pia.
Azam wamepangwa Kundi B, katika Kombe la Mapinduzi pamoja na Mtibwa Sugar ya Morogoro, Coastal Union  ya Tanga na Miembeni ya Unguja.
Kundi A lina timu za Simba SC, Tusker FC ya Kenya, Bandari ya Unguja na Jamhuri ya Pemba.
Michuano ya Kombe la Mapinduzi, ambayo ni maalum kwa ajili ya kuherehekea Mapinduzi matukufu ya Zanzaibar, inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 2, hadi kilele cha miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Januari 12, mwakani, huku ikishirikisha timu kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Kwa mujibu wa ratiba ya michuano hiyo iliyotolewa na Kamati Maalum ya Kusimamaia michuano hiyo, inaonesha kuwa katika mchezo wa kwanza utakaochezwa siku ya ufunguzi itakuwa ni kati ya Bandari kutoka Unguja ambayo itacheza na Jamhuri kutoka kisiwani Pemba ambao ni wawakilishi wa Zanzibar katika Kombe la Shirikisho Barani Afrika, pamabanolitakalochezwa katika uwanja wa Mao Tse Tung mjini Unguja, huku usiku wa siku hiyo hiyo katika Uwanja wa Amaan kisiwani Unguja pambano la ufunguzi rasmi katika mashindano hayo likiwakutanisha mabingwa wa soka nchini Tanzania, Simba SC ambao watapambana na mabingwa wa soka nchini Kenya, Tusker.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo jumla ya timu nane zitashiriki katika mashindano hayo ambayo yamejipatia umaarufu mkubwa visiwani hapa, timu hizo zimegawanya katika makundi mawili ambayo ni kama ifuatavyo:
Awali michuano hiyo ilitarajiwa kuanza kisiwani Pemba tarehe 1 Januari, lakini kutokana na kujitoa katika mashindano kwa klabu ya Al-Ahly ya Misri kutokana na klie kilichoelezwa sababu za kiusalama, mechi zote sasa zitachezwa kisiwani Unguja na ufunguzi ukipangwa kuanza tarehe 2 badala ya tarehe 1 januari.
Bingwa wa michuano hiyo ataondoka na zawadi ya kombe na fedha taslim Tsh.Milioni kumi (10,000,000), mshindi wa pili Milioni tano (5,000,000), pamoja na zawadi nyengine ambazo zimegawanywa katika makundi tofauti ikiwemo zawadi ya mfungaji bora, mchezaji bora, mwamuzi bora, kipa bora, mwandishi wa habari bora, timu bora na zawadi nyinginezo.

BAFANA YATAJA KIKOSI CHA AFCON, MC CARTHY NA MULOMOWANDAU NJE



Football | Bafana Bafana

Mulomowandau Mathoho (L) with Benni McCarthy © Gallo Images

McCarthy, Mathoho out of Bafana


Bafana Bafana have started their training camp at Orlando Stadium in Soweto which runs from Thursday until Saturday.
The squad consists of 31 players – the 24 that was selected for the international friendly match against Malawi last weekend in Durban and an additional seven more.
Coach Gordon Igesund will announce the final 23-man squad on Sunday.
Almost all players reported for national duty with the exception of striker Benni McCarthy and defender Eric Mathoho who have been withdrawn from the camp due to injuries. McCarthy is suffering from a troublesome hamstring while Mathoho has a knee injury.
“It is a blow when any player called up for the national team pulls out due to injury. It would have been a great situation to have both of them here,” said Igesund.
Ayanda Patosi and Andile Jali were given a break as a precautionary measure. Both have niggling ankle injuries but are expected to join their compatriots at training on Friday.
Due to club commitments, England-based Kagisho Dikgacoi and Dean Furman, as well as Darren Keet who plays in Belgium will not be part of the training camp.
“I already have 19 players in my mind but I still have some decisions to make for the rest, so there are still some places up for grabs.
“These are exciting but also testing times for me and the players because at the end of the day only 23 players can make the squad. We saw in the match against Malawi that all players want to be part of this fiesta. But it does not mean if players are excluded from the Afcon squad it is the end of the road, we still have plenty of tournaments to come,” added Igesund.
“What I am happy about is the great vibe in the squad and you can see all the players are eager to do their best which makes life harder for me and my technical team.”
 
 
 
Players in camp:
Goalkeepers: Itumeleng Khune, Wayne Sandilands, Senzo Meyiwa
Defenders:Bevan Fransman, Thabo Nthete, Siyabonga Sangweni, Siyanda Xulu, Siboniso Gaxa, Tshepo Masilela, Thabo Matlaba
 
Midfielders: Oupa Manyisa, Reneilwe Letsholonyane, Siphiwe Tshabalala, Sifiso Myeni, Thanduyise Khuboni, May Mahlangu, Delron Buckley, Lerato Chabangu, Thuso Phala, Ayanda Patosi, Daine Klate
Strikers: Bernard Parker, Lehlohonolo Majoro, Tokelo Rantie
 
Additional players:
Anele Ngcongca, Andile Jali, Teko Modise, Bongani Khumalo, Ricardo Nunes, Thulani Serero, Katlego Mphela

MAMENEJA VITANI! Wenger, Pardew wataka adhabu kwa Fergie!!

>>FA YAWAANDIKIA BARUA REDKNAPP & MANCINI KUJIELEZA!!
>>FERGIE AMPANDISHIA PARDEW!!
WENGER_AHIMIZA12WAKATI FA, Chama cha Soka England, kimethibitisha kuwaandikia Barua za kuwataka kujieleza, Mameneja wa Man City na QPR, Roberto Mancini na Harry Redknapp, kufuatia kauli zao baada ya Mechi zao za kulalamika kuhusu Marefa na kudokeza uchezeshaji usio wa haki, Mameneja wa Arsenal, Arsene Wenger, na wa Newcastle, Alan Pardew, wamesema Sir Alex Ferguson alistahili Kadi Nyekundu kwa kubishana na Marefa kwenye Mechi kati ya Manchester United na Newcastle iliyochezwa Boxing Dei.
Akijiingiza kwenye mzozo huo, Arsene Wenger amesema Sir Alex Ferguson alipaswa kuadhibiwa na Refa Mike Dean kwa kitendo chake cha kabla Kipindi cha Pili kuanza kwenye Mechi kati ya Manchester United na Newcastle cha kumvaa Refa Mike Dean na kumlalamikia kisha kumkabili Refa wa Akiba Neil Swarbrick na pia Refa Msaidizi Jake Collin.
Katika Mechi hiyo ambayo Man United walishinda Bao 4-3, Ferguson alikuwa amekasirishwa na Refa Mike Dean kufuta Ofsaidi iliyotolewa ishara na Msaidizi wake Jake Collin na kuamua ni Bao kwa vile Jonny Evans alijifunga mwenyewe.
Wakati Kipindi cha Pili kinataka kuanza, Ferguson alimvaa Refa Mike Dean na kumlalamikia kisha akamvaa Refa wa Akiba Neil Swarbrick na pia Refa Msaidizi Jake Collin.
Lakini FA ilithibitisha jana kuwa Sir Alex Ferguson hatachukuliwa hatua yeyote kwa vile Refa Mike Dean hakutaja lolote kwenye Ripoti yake ya Mechi.
Wenger amesema Sheria ni msumeno na Refa Mike Dean alipaswa kumwadhibu Ferguson.
Arsene Wenger ashawahi kukumbana na Kadi Nyekundu toka kwa Refa Mike Dean Agosti 2009 alipotolewa Uwanjani kwa kuipiga teke chupa ya maji wakati Arsenal inachapwa 2-1 na Man United Uwanjani Old Trafford.


WAKATI HUO HUO, Sir Alex Ferguson amemshambulia Meneja wa Newcastle, Alan Pardew kwa kutamka kuwa alipaswa kupewa Kadi Nyekundu kwa kubishana na Refa Mike Dean na Wasaidizi wake wakati Newcastle ilipochapwa 4-3 na Man United Uwanjani Old Trafford.
Ferguson amejibu mapigo kwa kusema: “Alan Pardew amejitokeza na kuniponda mimi. Yeye ndio mbaya zaidi kwa kuvamia Marefa, anadiriki hata kuwasukuma na kisha analeta mzaha kuhusu hilo! Ameshasahau msaada niliompa!”
Ferguson ameongeza: “Sikufanya kosa! Sikutoa kashfa yeyote! Nlikuwa nikiongea na Refa tu! Tatizo ni kuwa tupo Klabu kubwa na mimi ni Meneja wa Klabu kubwa Duniani hivyo kila kitu kinakuzwa! Sio Newcastle Klabu ndogo iliyo huko Kaskazini Mashariki!”
Pardew aliwahi kufungiwa Mechi mbili na kudundwa Faini ya £20,000 kwa kumsukuma Refa Msaidizi wakati Newcastle inaifunga 2-1 Tottenham Hotspur hapo Tarehe 18 Agosti.


HIVI PUNDE TU, FA, Chama cha Soka England, kimethibitisha kuwaandikia Barua za kuwataka kujieleza, Mameneja wa Man City na QPR, Roberto Mancini na Harry Redknapp, kufuatia kauli zao baada ya Mechi zao za kulalamika kuhusu Marefa na kudokeza uchezeshaji usio wa haki, kitendo ambacho ni kinyume cha Kanuni za FA.
Mancini, Meneja wa Man City, alilalamika kuhusu Refa Kevin Friend baada kufungwa 1-0 na Sunderland kwenye Mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa Desemba 26 kwa Refa huyo kutopiga Filimbi ya Faulo aliyochezewa Mchezaj wake Pablo Zabaleta na badala yake kuachia mpira uchezwe na kuzaa Goli la Adam Johnson, Winga wa zamani wa Man City, lililowaua City 1-0.
Mancini alidai: “Pengine Refa alivimbiwa na Mlo wa Krismasi! Haiwezekani Waamuzi wawili wasione tukio hilo! [Akimaanisha Refa Na Msaidizi wake]”
Nae Harry Redknapp, Bosi wa QPR, yuko matatani baada ya kuhamaki na maamuzi ya Refa Chris Foy ambayo alidai ni ‘Skandali!’ wakati walipofungwa 2-1 na West Brom na kutupwa mkiani mwa Ligi Kuu England Siku ya Boxing Dei.
Refa Chris Foy alilikubali Goli la kujifunga mwenyewe Kipa Robert Green ambae alionekana akibanwa waziwazi na Mchezaji wa WBA, Marc-Antoine Fortune, na pia aliwayima Penati ya wazi mwishoni baada ya Beki Liam Ridgewell kuunawa mpira.
Redknapp amewaka: "Ile ni Faulo ya wazi kwa Kipa wetu na ile ni Penati ya wazi! Hii ni kashfa!”
Msimamo wa FA kwa Mameneja ni kwamba hawatakiwi kuwalaumu Marefa kuhusu maamuzi yao na wakifanya hivyo wanaandikiwa Barua kutaka maelezo yao na kama hayaridhishi hufunguliwa Mashitaka.