Thursday, December 6, 2012

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuichezea Simba SC ya Dar es Salaam, baada ya kusaini jana usiku katika hoteli ya Sheraton mjini hapa.
Okwi alisaini mbele ya Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage ambaye ameongozana na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo, Zacharia Hans Poppe.
Baada ya kusaini, Okwi alisema; “Nimefurahi kuongeza mkataba na klabu yangu na ninaahidi kuendelea kuitumikia kwa nguvu zangu zote,”alisema Okwi.
Kwa upande wake, Hans Poppe alisema kwamba anaamini kusaini na Okwi sasa kutawakata vilimilimi wapinzani wao, ambao walikuwa wanamuwania mchezaji huyo.
“Sisi tunajua yote yaliyokuwa yakiendelea kwenye Challenge, tunajua wapinzani wetu walimfuata Okwi huku, lakini huyu mchezaji ana mapenzi yeye mwenyewe na Simba SC,”alisema Hans Poppe.
Okwi aliyezaliwa Desemba 25, mwaka 1992 mjini hapa, alisajiliwa na Simba SC mwaka 2009 akitokea SC Villa      ya hapa, baada ya klabu hiyo kumkosa mshambuliaji mwingine Mganda, Brian Umony aliyewahiwa na SuperSport United ya Afrika Kusini.
Tangu msimu uliopita, Okwi amekuwa akihusishwa na mpango wa kuhamia Yanga au Azam na akiwa kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge iliyoanza Novemba 24 na inafikia tamati kesho, ziliibuka habari za klabu hizo kumfuata kumsainisha mjini hapa.
Okwi jana alifunga bao moja kati ya matatu ya Uganda kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole mjini hapa, yaliyozima ndoto za Tanzania Bara kurejea nyumbani na Kombe la Challenge.
Kwa matokeo hayo, Uganda itamenyana na majirani zao na wapinzani wao wakubwa, Kenya katika fainali Jumamosi, ambao katika mchezo wa kwanza waliitoa kwa mikwaju ya penalti 4-2 Zanzibar, kufuatia sare ya jumla ya 2-2 ndani ya dakika 120.
Zanzibar na Bara zitamenyana katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu siku hiyo hiyo ya Jumamosi kwenye Uwanja wa Namboole.
Hadi mapumziko, Uganda walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililotiwa kimiani na Emmanuel Okwi dakika ya 11, baada ta kuuwahi mpira mrefu uliopigwa na kipa wake, Hamza Muwonge na kufumua shuti kali la umbali wa mita 19, ambalo lilimshinda kipa Juma Kaseja.
Baada ya bao hilo, Okwi aliumia na kutoka nje dakika ya 36 nafasi yake ikichukuliwa na Hamisi Kiiza.
Uganda ndio waliouanza mchezo huo kwa kasi na kulitia misukosuko lango la Stars kwa takriban dakika 10 mfululizo, lakini baada ya hapo timu hizo zikaanza kushambuliana kwa zamu.
Timu zote zilikuwa zikishambulia kutokea pembeni, lakini Uganda ndio walioonekana kuzalisha mashambulizi ya hatari zaidi.
Kipa na Nahodha wa Stars, Juma Kaseja alitoka uwanjani baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza akilaumiana na mabeki wake kwa kufungwa bao la kutanguliwa.
Kipindi cha pili, Waganda walirudi na moto wao tena na kufanikiwa na kupata bao la pili dakika ya 51, safari hii Robert Ssentongo akimtungua Kaseja, baada ya mabeki wa Stars kudhani ameotea.
Pamoja na kufungwa bao la pili, Stars waliendelea kucheza kwa juhudi, ingawa Waganda waliendelea kutawala mchezo.
Mpira uliotemwa na Juma Kaseja kufuatia shuti la Moses Oloya, ulimkuta Ssentongo dakika ya 71 akaukwamisha nyavuni na kuipatia The Cranes bao la tatu. Kutoka hapo, hali ilikuwa mbaya kwa Stars.
Zikiwa zimesalia dakika tano mchezo kumalizika, taa za Uwanja wa Mandela zilizimika, lakini baada ya jitihada za pamoja za FUFA, CECAFA na uongozi wa Uwanja, ziliwaka baada ya dakika saba na mchezo kuendelea hadi filimbi ya mwisho.

 

NASIB NA MIYEYUSHO WATAMBIANA


Kesho ndio siku ambayo mabondia Francis Miyeyusho na Nasib Ramadhan watapima uzito kabla ya kupanda ulingoni desemba 9 mwaka huu kumaliza tambo zao.

Mabondia hao watapima uzito ndani ya red carpet kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam saa tatu asubuhi pia kutakuwepo na burudani mbalimbali.

Watakuwa wanapambana kuwania mkanda wa WBF kama unavyoonekana kwenye picha.


CHINA YATOA VIFAA VYA NGOMA ZA KITAMADUNI KWA TANZANIA.



Balozi wa China nchini Tanzania Lu Youiquing akimwangalia waziri wa habari utamaduni na michezo wa Tanzania Dr Fenella Mukangara jinsi ya avyopiga  gitaa, ambali ni moja ya  vifaa vya ngoma za utamaduni .
 
Balozi wa china nchini Tanzania Lu Youiquing amemkabidhi vifaa mbalimbali vya ngoma, muziki na filamu waziri wa habari, utamaduni na michezo katika Dr Fenella Mukangara kwa lengo la kuimarisha mahusiano katika nyanja za kitamaduni na filamu nchini.

Akiongea wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari Balozi Lu Youiquing amesema vifaa hivyo mbali na kuendeleza sekta nzima ya burudani lakini pia vifaa hivyo vitasaidia kupunguza gharama za utayarishaji wa muziki na uhariri wa picha za filamu kwa wadau wa tasnia hizo.

Kwa upande wake Dr Mukangara amesema wamepokea vifaa vingi ikiwemo ngoma, magitaa na vifaa vingine ambavyo ni adimu nchini ambavyo vitaimarisha ubora wa filamu.

Amesema huo ni muendelezo wa mashirikiano na China katika mipango mbalimbali ya kukuza sekta ya ngoma, muziki na filamu.

Dr Fenera amesema baadhi ya vifaa vitapelekwa chuo cha sanaa na vingine vitapelekwa katika kitengo cha filamu kwa kuwa kuna baadhi ya vifaa ni kwa ajili ya kufanyia editing.

 

MANJI ASOGEZA MBELE MKUTANO WA WANACHAMA WA YANGA SABABU NI MBILI TU

TAARIFA KWA WANAYANGA.
Klabu ya Young Africans ilikuwa ifanye mkutano Wanachama tarehe 08 Disemba 2013, kama ilivyokua imetangazwa na Uongozi hapo awali. Tunapenda kutoa taarifa kuwa tarehe ya mkutano huo sasa imebadilishwa na kusogezwa mbele hadi tarehe 19 Januari 2013 kwa sababu zifuatazo:

1.Kutoa nafasi kwa Wanachama na Wapenzi wa YANGA kushirki kikamilifu maandalizi ya sherehe za Uhuru wa Taifa letu zitakazofanyika tarehe 09, Disemba 2012, na
2.Tuko katika mazungumzo na Kampuni moja maarufu ya kusimamia shughuli za mkutano huo kwa upande wa ufadhili, ili kuweza kutunisha mfuko na Klabu kujiingizia mapato kati ya shilingi za Kitanzania 200,000,000/= (shilingi milioni mia mbili  tu) hadi 350,000,000/= (shilingi milioni mia tatu hamsini tu) na Kampuni husika wameomba kuongezewa muda ili waweze kufanya hiyo kwa ufanisi mkubwa.
Tunapenda kuwashukru Wanachama na Wapenzi wa YANGA kwa mshikamano na umoja uliopo. Tuzidi kuijenga Yanga kwa maendeleo na mafanikio daima.
"YANGA DAIMA MBELE, NYUMA MWIKO"
  YUSUF MEHBUB MANJI
MWENYEKITI
YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB

WAGOMBEA SITA WAPITISHWA KUGOMBEA TAFCA , MWAISABULA NA JULIO NJE

KOZI YA LESENI C KUFANYIKA ARUSHA

SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI TFF LATAKA WACHEZAJI WA CONGO BRAZAVILLE WAPIMWE UPYA

Wachezaji wa U-17 wa Congo Brazaville waliocheza na Serengeti boys
Serengeti boys


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewasilisha barua ya malalamiko yake dhidi ya matumizi ya wachezaji wenye umri mkubwa na unyanyasaji uliofanyuwa kwa maofisa wa timu ya taifa ya vijana walio na umri chini ya miaka 17 wa Serengeti Boys wakati wa mechi ya marudiano ya michuano ya Mataifa ya Afrika kwa Vijana dhidi ya Congo.

Serengteti Boys iliondolewa kwenye mashindano hayo kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mechi ya kwanza iliyofanyika Novemba 18, 2012 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar Es salaam na baadaye kukubali kipigo cha mabao 2-0 kwenye mechi ya marudiano jijini Brazaville Jumapili iliyopita.

Hata hivyo, mechi hizo mbili zilizingirwa na matukio tata, hasa kuhusu umri wa wachezaji wa Congo ambao kimaumbile walionekana kuwa ni umri mkubwa zaidi na kusababisha TFF kuwasiliana na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika (CAF) kuhusu njia zinazowezekana kupata uthibitisho wa umri wa wachezaji hao, lakini ilishindikana na ndipo TFF ilipocheza mechi hiyo ikiwa na imeweka pingamizi.
Katika barua iliyotumwa CAF jana, TFF imerejea barua ya pingamizi aliyokabidhiwa kamisaa wa mechi ya kwanza jijini Dar Es salaam, Bw. Chayu Kabalamula na malalamiko yaliyowasilishwa kwa kamisaa wa mechi ya marudiano kuhusu vurugu walizofanyiwa maofisa wa timu.

Katika barua hiyo, TFF imeomba CAF iagize kuwa wachezaji wote wa Congo waliocheza mechi hizo mbili wapimwe tena kwa kutumia kipimo cha M.R.I na gharama za zoezi hilo zilipiwe na TFF; na pili Shirikisho limeomba kuwa CAF ikubali kuipa Tanzania wiki tatu za kukusanya ushahidi na kuuwasilisha Cairo kwa ajili ya maamuzi.

Kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo, nchi shiriki zinatakiwa kuwapima wachezaji wake kwa kutumia kipimo cha M.R.I ambacho kinaweza kutambua umri wa vijana walio chini ya miaka 17 na kwamba matokeo yake yanatumwa CAF, ambayo itahifadhi matokeo hayo hadi hapo kutakapotokea pingamizi na ndipo itafanyia kazi kwsa kutoa matokeo ya vipimo hivyo.

“Ni matumaini yetu kuwa suala letu litafanyiwa kazi na kutolwewa ufumbuzi ili kulinda soka la vijana barani Afrika dhidi ya vitendo vilivyokomaa vya udanganyifu wa umri,” alisema katibu mkuu wa TFF, Angetile Osiah.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jana, kocha Jacob Michelsen alisema alishangaa kuona wachezaji wenye umri mkubwa zaidi wakichezeshwa kwenye mechi ya marudiano, lakini akaisifu TFF kuwa inafuata njia sahihi ya maendeleo na haina budi kuendelea na programu yake ya soka la vijana.
"Najivunia vijana wangu kwa kuwa walijituma kwa muda wote pamoja na kwamba wenyeji waliongeza wachezaji wenye umri mkubwa zaidi kuliko waliokuja huku," alisema kocha huyo kutoka Denmark.

"Kitu cha msingi ni kufuata njia sahihi ya kuendeleza soka na natumaini TFF iko kwenye njia sahihi na itaendelea na programu yake ya vijana. Hakuna njia ya mkato kama mnataka maendeleo. Ni lazima tufuate njia sahihi na matunda yake tutayaona baadaye.
"Kila mara nasema mambo (ya vijana) huchukua muda mrefu (Things Take Time) na hivyo hatuna budi kuwa wavumilivu.
"Wenzetu walitumia njia za ajabu na hata hiyo penati ya bao la kwanza haikuwa faulo. Ilitokea nje kabisa ya eneo la penati. Refa alimuangalia kibendera akaona ametulia, akamuangalia beki mchezaji akamuona amesimama, mara akaangalia juu na kupuliza filimbi kuonyesha kuwa ni penati."

Naye kocha msaidizi, Jamhuri Kihwelo alishindwa kujizuia na kujikuta akibubujika machozi wakati alipoelezea jinsi alivyoshambuliwa na askari kabla ya mchezo huo.

VODACOM KUFANIKISHA SWAHILI FASHION

KAMPUNI ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, ni miongoni mwa wadhamini watakaorembesha na hatimaye kufanikisha tamasha la tuzo za Swahili Fashion Week 2012 litakalofanyika kuanzia kesho hadi keshokutwa.

Waandaaji wa tuzo hizo kubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati tayari walishatangaza majina ya waliopendekezwa kushiriki katika kuwania tuzo mbalimbali za Swahili Fashion Week 2012 ikiwa pamoja na njia zinazotumika kuwapigia kura washiriki wa tuzo hizo.


Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Udhamini na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa alisema wapenzi wa mitindo nchini wanaweza kununua tiketi za kuingia kwenye tamasha hilo kwa kupitia huduma yao ya M-Pesa.
Alisema tiketi hizo zinauzwa kwa Sh. 20,000 kwa ili mpenzi anaweza kununua kupitia namba +255 767 22 24 41.
 

Tuzo za Swahili Fashion Week 2012 zinazoenda pamoja na sherehe ya miaka mitano tangu kuzaliwa kwa onyesho hili kubwa, mwaka huu zimeongezwa tuzo nyingine tatu kutoka katika tuzo za mwaka jana ili kuweka changamoto kubwa zaidi katika tasnia ya mitindo nchini na ukanda wote wa Afrika Mashariki na Kati.
Jumla ya tuzo 15 zitawaniwa mwaka huu kutoka tuzo 12 za mwaka jana.
 

Tuzo za mwaka huu ni: Best Male Model, Best Female Model, Best East African Model (Mpya), Designer of the Year, East African Designer of the Year, Redd’s Stylish Female Personality, Stylish Male Personality, Innovative Designer, Best Men’s Wear, Fashion TV Program of the Year (Mpya), Vodacom Fashion Blog of the Year, Fashion Photographer of the Year, Fashion Journalist of the Year, Best East African Journalist (Mpya) na Upcoming Designer.
 

Twissa alisema: "Mchakato mzima wa kuchagua mwanamitindo na mbunifu wako bora kwa mwaka huu wa 2012 unasimamiwa na PUSH Mobile ambapo mpiga kura atatakiwa kutuma ujumbe mfupi wa namba ya mshiriki (CODE) unaemkubali na kwenda kwenye namba 15678, huku mchakato mzima wa kuzihakiki kura hizo utafanywa na PKF. Lakini pia kura zinaweza kupigwa kupitia blogu maalum ya kupigia kura ya www.sfw2012awards.blogspot.com."

Washindi wote wa tuzo za Swahili Fashion Week 2012 watatangazwa siku ya ya mwisho ya Maonyesho ya Swahili Fashion Week, Jumamosi ya Desemba 8, 2012 katika hoteli ya Golden Tulip, Dar es Salaam, Tanzania.


Swahili Fashion Week 2012 imedhaminiwa na: Vodacom, EATV, East Africa Radio, USAID Compete, Origin Africa, Golden Tulip Hotel. Amarula, Precision Air, 2M Media, Global Outdoor Ltd, Vayle Springs Ltd, Eventlites, Ultimate Security, BASATA (Baraza La Sanaa Tanzania),  Strut It Afrika, Ndibstyles, PKF Tanzania, DARLING, PUSH Mobile, DarLife, Century Cinemax and 361 Degrees.

AZAM YAMUUZA NGASA

Ngassa akiwa amekaa kwenye 'mchuma' aliopewa na Simba baada ya kujiunga kwa mkopo na klabu hiyo Agosti mwaka huu

AZAM FC imethibitisha kwenye tovuti yake leo kuwa imemuuza mchezaji wake Mrisho Halfan Ngasa kwa klabu ya El Mereikh ya Sudan kwa dola 75,000 (sawa na Sh. milioni 118) katika majadiliano yaliyochukua takriban saa moja kwenye makao makuu ya klabu ya Azam FC na kuhudhuriwa na viongozi wa pande zote mbili.

Kwa mujibu wa Azam FC, El-Mereikh wameshazungumza na mchezaji na kukubaliana maslahi yake binafsi ambapo Mrisho Ngasa atalazimika kusafiri hadi mjini Khartoom, Sudan mara baada ya kuisha kwa mashindano ya CECAFA Challenge Cup ili kuona mazingira ya klabu, kufanya vipimo vya afya na kuangalia makazi yake binafsi.

Kuuzwa kwa Mrisho Ngasa nchini Sudan kunaifanya klabu ya Azam FC kupata kiasi cha zaidi ya Dola 50,000 pesa ambayo Azam FC waliiweka kama kima cha chini cha kumuuza Mrisho Ngasa.

Wakati Azam FC ikimtoa Ngasa iliweka kiasi hicho cha dola 50,000 kwa timu itakayomtaka lakini kutokana na kukosekana na mnunuzi huku Simba ikitoa ofa ya Sh. milioni 25, Azam FC iliamua kumpeleka Ngasa kwa mkopo Msimbazi ili akitokea mteja mwenye kufikia dau hilo waweze kumuuza.

Mengi yalisemwa juu ya biashara ya mkopo kati ya Azam FC na Simba lakini msimamo wa Azam FC uliowekwa kwenye tovuti yao leo umethibitisha baada ya El-Mereikh kufikia dau la kumnunua Mrisho Ngasa.

Mrisho Ngasa, mchezaji mwenye kipaji cha hali ya juu cha kusakata kabumbu anakwenda nchini Sudan kwenye kikosi chenye mafanikio zaidi katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati baada ya TP Mazembe.

Azam FC inamuuza Mrisho Ngasa kwa kuzingatia umuhimu wa maendeleo ya mchezaji mwenyewe kimpira na kwa kipato, pia kwa kuzingatia kwamba Tanzania inahitaji wachezaji wengi wanaocheza nje kwenye vilabu vikubwa ili wanaporudi waweze kuisaidia timu ya Taifa.


Taarifa zinasema Mrisho Ngassa  mwenyewe amepewa dola 50,000 (sawa na Sh. milioni 79) kwa ajili ya kusaini na atalipwa mshahara wa dola 4,000 (sawa na Sh. milioni 6.3) kwa mwezi.

Neema imeendelea kutua kwa Ngassa ambaye wakati alipouzwa na Yanga kwa Sh. milioni 58 kwa Azam FC Mei 2010 aliripotiwa kupewa mkononi Sh. milioni 40 na alipopelekwa kwa mkopo Simba Agosti 2012 alipewa gari aina ya Toyota Verosa pamoja na Sh. milioni 12 na sasa miezi minne tu baadaye ameweka kibindoni milioni 79.

 

Bacary Sagna: Nina furaha kuwepo Arsenal. FA kupigania dimba la Wembley kuandaa fainali Euro 2020, John Terry kukosa fainali ya kombe la dunia la vilabu nchini Japan na Deschamps huenda akasalia katika benchi la ufundi la ufaransa mpaka 2016..


Mlinzi wa Arsenal Bacary Sagna amedai kuwa amekuwa na furaha kuichezea klabu yake hiyo akiondoa uvumi ulionea kuwa ni miongoni mwa wachezaji wenye majina makubwa ambao huenda akaondoka katika klabu hiyo baada ya mazungumzo ya mkataba wake mpya.

Sagna mwenye umri wa miaka 29, alikosekana katika sehemu kubwa ya michezo ya msimu uliopita akisumbuliwa na matatizo ya mguu na sasa akisaka mkataba mpya Emirates wakati huu ambapo mkataba wake wa sasa ukitarajiwa kumalizika mwak 2014.

Mfaransa huyo ambaye anaelekea kujikwaa katika sera ya Arsene Wenger ya kutoa mkataba wa mwaka mmoja mmoja kwa wachezaji wenye umri zaidi ya miaka 30 mwaka ujao, aliripokuwa kuwa hana furaha na mpango uliopendekezwa kwake wa kuongezwa miezi 12 na kuongezewa mshahara wa pauni £60,000 kwa wiki.

Hata hivyo Sagna amekanusha hilo na kusema kuwa yeye ni mwenye furaha ndani ya klabu hiyo.

"Nina furaha. Ninafuraha kurejea uwanjani na kuichezea Arsenal, naangalia mbele kucheza michezo mingi zaidi msimu huu kwa kuwa huko nyuma nilikuwa majeruhi''

FA kupigania dimba la Wembley kuandaa fainali Euro 2020
 Mwenyekiti wa chama cha soka nchini England David Bernstein amesisitiza kuwa dimba la Wembley lazima liwe mwenyeji wa fainali za mataifa ya ulaya mwaka  2020 (euro 2020).

Bernstein amethibitisha kuwa FA itaomba kuwa mwenyeji wa mchezo wa fainali na nusu fainali wakati ambapo Wales na Scotland zimesema kuwa na mpango kama huo wa kuomba uenyeji na wakitaja jiji la Glasgow kuwa mwenyeji wa mchezo wa fainali.

Wembley utakuwa mwenyeji wa fainali ya ligi ya vilabu bingwa ulaya mwaka 2013 na Bernstein anaamini uwanja huo utakuwa muafaka kuandaa fainali hiyo barani Ulaya.

"ni wazi kabisa Wembley ni uwanja wa hadhi ya juu unapaswa kufikiriwa na UEFA na ni jambo ambalo tutalipigia chapuo mapema.

Naye mtendaji mkuu wa Wales Jonathan Ford amethibtisha kupeleka ombi lao UEFA wakitaka michezo hiyo kupelekwa katika dimba la Millennium.

Deschamps huenda akasalia katika benchi la ufundi la ufaransa mpaka 2016.

Didier Deschamps ni kama vile anataka kusalia kuwa kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa mpaka wakati nchi hiyo itakapo kuwa mwenyeji wa fainali za EURO 2016, ikiwa ni baada ya mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa kuambiwa kuwa kimsingi hatafukuzwa kazi hata kama watashindwa kufuzu fainali za kombe la dunia zijazo.

Wakati Ufaransa ikiwa katika kundi moja na mabingwa wa Ulaya na Dunia, Hispania katika michezo ya makundi kuwania kufuzu kombe la dunia, kocha huyo mwenye umri wa miaka 44 bila shaka hafarijiki na kauli hiyo na kwamba anachofanya ni kuhakikisha anaziba mianya midogo midogo inayoweza kumtilia mashaka kibarua chake kwa kuhakikisha anafuzu fainali hizo za mwaka 2014 nchini Brazil.

Alipoajiriwa mwezi July, Deschamps, ambaye alichukua taji la kombe la dunia kama mchezaji akiwa na kikosi cha Ufaransa mwaka 1998, anasema huenda akajiuzulu kama ataishindwa kulipeleka taifa lake katika fainali hizo.


Lakini Rais wa shirikisho la soka la Ufaransa FA (FFF) Noel Le Graet amesema hakuna haja ya kumuweka katika wasiwasi wa lazima afuzu kama tatizo ni hilo.

Amekaririwa Le Graet akisema

"kama tutafuzu kombe la dunia bila shaka Didier ataendelea mpaka 2016,"

"mkataba uko wazi ni kwamba utaongezwa katika mazingira kama hayo".

Le Graet alimsainisha Deschamps mkataba wa miaka miwili.
Amekaririwa akisema,

"hata hivyo hata kama tukishindwa kufuzu jambo ambalo hatulitegemei kuondoka si jambo la lazima. Kutakuwa na mazungumzo".

John Terry kukosa kombe la dunia la vilabu Japan.

Mlinzi wa Chelsea John Terry huenda akawa bado hajaponya majeraha yanayo msibu ya msuli katika kipindi klabu yake itakapokuwa na kibarua cha michuano ya kombe la dunia la vilabu nchini Japan.

Mlinzi huyo tegemeo Terry, ambaye kwasasa ana umri wa miaka 31, alipatwa na maumivu alipogongana na mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez katika mchezo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 mchezo uliopigwa Stamford Bridge mwezi uliopita.

Meneja wa muda wa klabu hiyo Rafa Benitez ameweka wazi hilo kwamba huenda akarejea katika mchezo wa mwisho wa juma hili dhidi ya Sunderland, lakini bado hajarejea sawasawa katika mazoezi na kuna mashaka kuwemo katika safari ya mashariki ya mbali.

Jopo la madaktari limemfanyia uangalizi mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa England hapo jana kuangalia kama kuna uwezekano wa kuwemo safarini baada ya mchezo dhidi ya Sunderland na wamekuwa na majibu ya mashaka.

GOAL LINE TEKNOLOGY YAANZA KUTUMIKA RASMI JAPAN.

TIMU ya Sanfrence Hiroshima ya Japan imeifunga timu ya Auckland City ya New Zealand kwa bao moja kwa bila katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia jana ambao Shrikisho la Soka Dunia-FIFA lilitumia mfumo wa teknologia ya kompyuta katika mstari wa goli kwa mara ya kwanza. Bao Hiroshima lilifungwa dakika ya 66 na Toshihiro Aoyama na kuwapeleka mabingwa hao wa Ligi Kuu nchini Japan maarufu kama J-League katika hatua ya robo fainali ambapo sasa watakwaanza na mabingwa wa soka barani Afrika Al Ahly ya Misri. Hiyo ilikuwa ni mechi ya kwanza kwa FIFA kutumia rasmi mfumo huo ingawa kulikuwa na nafasi finyu za kujaribu ubora wake kutokana na mchezo wenyewe uliokuwa na nafasi chache za kufunga. FIFA inatumia mifumo katika viwanja vilivyopo katika miji ya Yokohama na Toyota ambapo kunafanyika mashindano hayo.

OBI MIKEL AFUNGIWA MECHI TATU.

KIUNGO wa kimataifa wa Nigeria na klabu ya Chelsea, John Obi Mikel amefungiwa mechi tatu na kutozwa faini ya paundi 60,000 baada ya kukwaruzana na mwamuzi aliyechezesha mchezo baina ya timu hiyo Manchester United. Mikel aliripotiwa kuwa alivamia chumba cha waamuzi baada ya mchezo huo uliochezwa katika Uwanja wa Stamford Bridge Octoba mwaka huu kufuatia tuhuma kwamba Mwamuzi Mark Clattenburg alishambulia kiungo huyo kwa maneno ya kibaguzi. Chama cha Soka cha Uingereza-FA kimesema kuwa nyota huyo alikiri kutumia maneno ya kutishia katika chumba cha waamuzi mwishoni mwa mchezo huo uliochezwa Octoba 28 ambapo Chelsea walipoteza kwa kufungwa mabao 3-2. Adhabu hiyo itapelekea nyota huyo kukaa nje uwanja mpaka Desemba 26 mwaka huu kwa ajili ya michezo ya Ligi Kuu ya nchi hiyo pekee lakini atakuwemo katika kikosi kitakachoelekea Japan kwajili ya michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia.

EURO 2020 KUFANYIKA ACROSS EUROPE.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA Gianni Infantino amesema kuwa Kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo imekubali michuano ya Ulaya ya 2020 kuchezwa katika bara zima. Nahodha wa zamani wa Ufaransa, Michel Platini ambaye ni rais wa UEFA ndio aliyetoa wazo la michuano hiyo kuandaliwa na nchi nyingi zaidi mapema mwaka huu ikiwa ni njia ya kupunguza gharama za maandalizi haswa katika kipindi hiki ambacho nchi nyingi zimekuwa zikikumbwa na matatizo ya midororo ya kiuchumi. Infantino amesema michuano ya Euro 2020 itaandaliwa katika miji mbalimbali mikubwa kufuatia uamuzi uliotolewa na kamati hiyo jana. Taarifa za michuano hiyo kuandaliwa katika miji miji mikubwa tofauti haijapokewa vizuri na mashabiki wa soka wakidai gharama za kwenda kutizama timu zao kutoka nchi moja kwenda nyingine zitakuwa kubwa tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo mashabiki husafiri katika nchi moja au mbili ili kushuhudia michuano hiyo. Lakini wakati mashabiki wakilalama gharama za usafiri mashirika ya ndege barani humo yamefurahia habari hiyo kwani ndio utakuwa wakati wa kupata abiria wengi watakaokuwa wakienda katika miji ambayo itakuwa wenyeji wa michuano hiyo.

Ghoulam KUCHEZEAA Algeria NA SIO UFARANSA

Shirikisho la soka linalosimamamia mpira duniani  Fifa limemuidhinisha Mzaliwa wa ufaransa ambaye kwa sasas ni raia wa algeria   Faouzi Ghoulam  kuchezea timu ya taifa ya Algeria  , Shirikisho la soka la  Algerian limetangaza kuwa kijana huyo mwenye miaka 21  ambaye ni mlinzi wa kushoto aliiichezeza ufaransa kwenye timu ya  chini ya miaka 21 lakini leo hii ameamua kuchagua algeria
Nimeamua kuchagua  Algeria kwa sababu ipo moyoni nilivutiwa nayo na ni chaguo sahihi

Huyu ni mchezaji wa pili kufanya hivyo mwaka huu baada ya mchezaji wa Parma naye kufanya hivyo  Ishak Belfodil.

Timu hiyo ipo kundi moja la na  D dhidi  Cote d’Ivoire, Tunisia pamoja na  Togo.

EUROPA LIGI: Liverpool, Spurs zaungana na Newcastle MTOANO!

>>DROO Raundi ya Mtoano ya Timu 32 Desemba 20!
EUROPA_LIGI_CUPKATIKA Mechi za mwisho za Makundi ya EUROPA LIGI, Klabu za England, Liverpool na Tottenham, zilipata ushindi na kujiunga na Newcastle ambao walikuwa tayari wamefuzu kutinga kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ambayo Droo yake itafanyika Desemba 20!
Timu 24 toka EUROPA LIGI zilizofuzu hatua ya Makundi zitaungana na Timu 8 zilizomaliza nafasi za 3 kwenye Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na miongoni mwa hizo ni waliokuwa Mabingwa watetezi wa Ulaya Chelsea ambao Jumatano walitupwa nje ya Mashindano hayo.
+++++++++++++++++++++++++
>>8 TOKA UEFA CHAMPIONZ LIGI kwenda EUROPA LIGI:
[Timu zilizomaliza Nafasi ya 3 kwenye Makundi]
-Dynamo Kiev
-Olympiacos
-Zenit St Petersburg
-Ajax Amsterdam
-Chelsea
-BATE Borisov
-Benfica
-CFR Cluj-Napoca
+++++++++++++++++++++++++++++++++
KLABU 24 ZILIZOFUZU:
Olympique Lyonnais
FC Rubin Kazan
FC Internazionale Milano
Hannover 96
Bayer 04 Leverkusen
FC Metalist Kharkiv
FC Anji Makhachkala
Fenerbahçe SK
VfL Borussia Mönchengladbach
AC Sparta Praha
S.S. Lazio
Club Atlético de Madrid
FC Viktoria Plzeň
Levante UD
KRC Genk
FC Dnipro Dnipropetrovsk
SSC Napoli
Newcastle United FC
FC Girondins de Bordeaux
ZILIZOFUZU ALHAMISI DESEMBA 6:
Steaua Bucharest
Stuttgart
Liverpool
Tottenham
FC Basel au Videoton [KUJULIKANA BAADAE LEO]
+++++++++++++++++++++++++++++++++
Katika Mechi ya Udinese v Liverpool, Bao la ushindi kwa  Liverpool, waliocheza ugenini, lilifungwa na Jordan Henderson katika Dakika ya 23.
Huko White Hart Lane, Bao za Adebayor, Jermaine Defoe na moja la kujifunga wenyewe Panathinaikos baada ya kichwa cha Clint Dempsey kugonga posti na kumgonga mgongoni Karnezis ziliwapa ushindi Tottenham wa Bao 3-1.
Newcastle, ambao walikuwa tayari wamefuzu na waliocheza ugenini, walifungwa Bao 2-0 na Bordeaux.
MATOKEO:
Alhamisi Desemba 6
BSC Young Boys 3 FC Anzhi Makhachkala 1
Udinese Calcio 0 Liverpool 1
Hapoel TelvAviv 2 A. Académica de Coimbra 0
FC Viktoria Plzen 1 Club Atlético de Madrid 0
AEL Limassol 3 Olympique de Marseille 0
Fenerbahçe 0 VfL Borussia Mönchengladbach 3
CS Marítimo 2 Club Brugge 1
FC Girondins de Bordeaux 2 Newcastle United 0
VfB Stuttgart 0 Molde FK 1
FC København 1 FC Steaua Bucuresti 1
FC Dnipro Dnipropetrovsk 4 AIK 0
SSC Napoli 1 PSV Eindhoven 3
KRC Genk 0 FC Basel 0
Sporting Clube de Portugal v Videoton FC [MECHI INACHEZWA BAADAE]
Inter Milan 2 Neftçi PFK 2
FK Partizan 1 FC Rubin Kazan 1
Olympique Lyonnais 2 Hapoel Kiryat Shmona 0
Athletic Club 0 AC Sparta Praha 0
NK Maribor 1 S.S. Lazio 4
Tottenham Hotspur 3 Panathinaikos 1
SK Rapid Wien 1 FC Metalist Kharkiv 0
Bayer 04 Leverkusen 1 Rosenborg 0
Levante 2 Hannover 2
FC Twente 1 Helsingborgs 3
 

CAF: TUZO MCHEZAJI BORA AFRIKA, watatu watajwa!


>>NI YAYA TOURE, ALEX SONG & DIDIER DROGBA!
Shirikisho la Soka Afrika, CAF, limetangaza Majina ya Wanasoka watatu kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika kwa Mwaka 2012 na Mshindi wake atatajwa hapo Desemba 20 huko Accra, Ghana kwenye Hafla Maalum.
Wagombea hao watatu ni Yaya Toure, Mchezaji wa Ivory Coast na Klabu ya Manchester City, ambae ndie alitwaa Tuzo hii Mwaka 2011, Nahodha wa Ivory Coast anaechezea Klabu ya Shanghai Shenhua ya China, Didier Drogba, na Kiungo wa Cameroun na Barcelona, Alexander Song.
WASIFU:
Alexander Song
Alex Song to Barcelona!

Kuzaliwa: 09 Septemba 1987
Klabu: Barcelona (Spain)
Nchi: Cameroon
Ni Mchezaji wa Cameroon ambae Mashabiki wa Arsenal walimteua kuwa ndie Mchezaji wao Bora wa pili kwa Msimu wa 2011/12 na aliihama Klabu hiyo kwenda Barcelona Agosti 2012 baada ya kuichezea Mechi 204 na kufunga Bao 10.
Didier Drogba

Didier Dr...Drogba to...

Kuzaliwa: 11 March 1978
Klabu: Shanghai Shenhua (China)
Nchi: Cote d'Ivoire
Alikuwa na Msimu mzuri wa Mwaka 2011-2012 kwa Klabu na Nchi yake.
Alifunga Bao la kusawazisha na Penati ya ushindi Chelsea ilipoitoa Bayern Munich kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na kutwaa Ubingwa wa Ulaya. Alikosa Penati kwenye Fainali ya AFCON 2012 wakati Ivory Coast ilipotolewa na Zambia waliotwaa Ubingwa lakini ni yeye ndie aliifikisha Nchi yake hapo. Alifunga Bao la ushindi kwenye Fainali ya FA Cup na kuipa Kombe Chelsea. Msimu ulipomalizika alihamia China na kujiunga na Klabu ya Shanghai Shenhua.


Yaya Toure
 Yaya Tour...

Kuzaliwa: 13 May 1983
Klabu: Manchester City (England)
Nchi: Cote d I'voire
Kiungo huyo ndie alikuwa mhimili wa Manchester City kutwaa Ubingwa wa England Msimu wa 2011/12 kwa mara ya kwanza katika Miaka 44 na pia kuifungia Klabu yake Bao 9 katika Mechi 43. Alichaguliwa kuwemo kwenye Kikosi Bora cha PFA cha Ligi Kuu England kwa Msimu wa 2011/12. Pia, alikuwa mmoja wa Wachezaji walioipeleka Ivory Coast Fainali ya AFCON 2012 wakati Ivory Coast ilipotolewa na Zambia.

 

UEFA CHAMPIONZ LIGI: Man United & Arsenal, nani Wapinzani wao MTOANO??

UEFA_CHAMPIONZ_LIGI_LOGO-BOMBAZ>>MAN UNITED kuivaa Celtic, Porto, AC Milan, Real, Valencia au Shakhtar
>>ARSENAL na PSG, Malaga, Barca, Dortmund, Bayern au Juve??
>>DROO RAUNDI ya MTOANO TIMU 16 kupangwa Desemba 20!
>>MECHI KUCHEZWA Februari & Machi 2013!!
Wakati Chelsea wanaweka historia ya kuwa Mabingwa wa kwanza Watetezi kushindwa kufikia hatua ya Mtoano ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na kutupwa kucheza EUROPA LIGI na wenzao Manchester City, Mabingwa wa England, wakiyaaga kabisa Mashindano ya Ulaya Msimu huu, Manchester United na Arsenal ndio pekee toka England zipo Raundi ya Mtoano ya Timu 16.
Timu nyingine toka Visiwa vya Uingereza ambayo ipo Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ni Celtic ya Scotland.

+++++++++++++++++++

TIMU ZILIZOFUZU KUINGIA Raundi ya Mtoano ya Timu 16:
WASHINDI wa MAKUNDI:
Paris St Germain
Schalke 04
Malaga
Borussia Dortmund
Juventus
Bayern Munich
Barcelona
Manchester United
WASHINDI wa PILI wa MAKUNDI:
Porto
Arsenal
AC Milan
Real Madrid
Valencia
Shakhtar Donetsk
Galatasaray
Celtic
+++++++++++++++++++
Kwa mujibu wa Kanuni za UEFA za Droo ya upangaji Ratiba ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16, zile Timu ambazo zimekuwa Washindi wa Makundi watawekwa Kapu Namba 1 na wale waliomaliza Nafasi ya Pili kwenye Makundi wapo Kapu Namba 2.
Droo itafanywa kwa kutoa Jina moja toka Kapu Namba 2 na kufuatia Jina jingine toka Kapu Namba 1 na Timu hizo ndizo zitakazokutana isipokuwa Timu zinazotoka Nchi moja na zile zilizokuwa Kundi moja haziwezi kupambanishwa.
Pia, Mechi za kwanza za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 zitachezwa nyumbani kwa Timu itakayotoka Kapu Namba 2, Timu zilizomaliza Nafasi ya Pili, na marudiano ni nyumbani kwa Washindi wa Makundi.
Kwa mujibu wa Kanuni hizi za UEFA, Wapinzani wa Manchester United na Arsenal wanaweza kuwa kama ifuatavyo:
-MAN UNITED anaweza kucheza na mmoja kati ya Celtic, Porto, AC Milan, Real Madrid, Valencia au Shakhtar Donetsk.
-ARSENAL mpinzani wake ni mmoja kati ya: PSG, Malaga, Barcelona, Borussia Mechi za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 zitachezwa Februari 12 na 20, 2013 na marudiao ni Machi 5 na 13, 2013.
TOKA UEFA CHAMPIONZ LIGI kwenda EUROPA LIGI:
[Timu zilizomaliza Nafasi ya 3 kwenye Makundi]
-KUNDI A: Dynamo Kiev
-KUNDI B: Olympiacos
-KUNDI C: Zenit St Petersburg
-KUNDI D: Ajax Amsterdam
-KUNDI E: Chelsea
-KUNDI F: BATE Borisov
-KUNDI G: Benfica
-KUNDI H: CFR Cluj-Napoca
 

FUPI za LEO: Obi Lupango, Messi anusurika & Fergie atoa Medali kwa Majeshi!!

>>REKODI ya MULLER: Messi hachezi Jumapili, ila zipo Mechi 3 kuvunja REKODI!!
CLATTENBURG_na_CHELSEALEO Mashabiki wa Barcelona wamepata habari njema baada ya kuthibitishwa kuwa Supastaa wao, Lionel Messi, ambae jana alitolewa kwa machela Uwanjani Nou Camp wakati wa Mechi na Benfica, hakuumia sana kama ilivyoogopwa lakini Mashabiki wa Chelsea wamepata pigo baada ya FA kumshushia Kifungo cha Mechi 3 na Faini Pauni 66,000 Kiungo wao John Mikel Obi kwa kosa la kumtishia Refa Mark Clattenburg na huko Jijini Manchester, Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, amepewa heshima kubwa ya kupokea na kutoa Medali kwa Wanajeshi wa Uingereza ambao wamemaliza utumishi wao toka uwanja wa vita wa Afghanistan.


John Mikel Obi
Kiungo wa Chelsea, John Mikel Obi, amefungiwa Mechi 3 na kupigwa Faini Pauni 66,000 kwa kosa la kumtishia Refa Mark Clattenburg ambalo alilikubali na ambalo lilitokea mara baada ya Mechi iliyochezwa Uwanja wa Stamford Bridge hapo Oktoba 28 kati ya Chelsea na Manchester United na Chelsea kunyukwa 3-2.
Ingawa Obi aliomba kusikilizwa binafsi na Jopo la FA lilioendesha Kesi dhidi yake huku akijitetea aliamini kuwa amekashifiwa Kibaguzi, Jopo hilo lilisema anayo hatia lakini halikumpa adhabu kali zaidi kwa vile tu wamekubali utetezi wake kuwa aliamini kabaguliwa.
Awali Chelsea iliwasilisha malalamiko yao kwa FA kwamba Refa Mark Clattenburg alimkashifu Kibaguzi John Mikel Obi wakati wa Mechi hiyo lakini FA ilitupilia mbali malamiko hayo na kumfungulia Kesi Obi kwa kuvamia Chumba cha Marefa mara baada ya Mechi na kumtishia Refa.





Lionel Messi hakuumia sana!MESSI_ASHANGILIA_GOLI
Barcelona imethibitisha kuwa Supastaa wao Lionel Messi amepata mchubuko tu baada ya kutolewa na machela wakati wa Mechi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI waliyotoka sare na Benfica Uwanjani Nou Camp hapo jana.
Messi, alieingizwa Kipindi cha Pili cha Mechi hiyo, alitolewa baada ya Dakika 30 za kuwa Uwanjani alipogongana na Kipa wa Benfica na kuumia goti lake la kushoto na kulikuwa na wasiwasi mkubwa kuwa ameumia sana.
Messi, ambae ameshafunga Mabao 84 kwa Mwaka 2012, anasaka kuivunja rekodi ya Mjerumani Gerd Muller aliyoiweka Mwaka 1972 kwa kufunga Goli 85 akichezea Bayern Munich na West Germany.
Ingawa Messi hatarajiwi kucheza Mechi ya Jumapili ya La Liga ugenini na Real Betis, lakini Barcelona bado wanazo Mechi za La Liga dhidi ya Atletico Madrid na Real Valladolid, na pia ile ya Copa del Rey dhidi ya Cordoba katika Mwezi huu Desemba na hiyo ni fursa kubwa kwake kuvunja rekodi hiyo.
FERGIE_na_MAJESHISir Alex Ferguson
Ferguson leo aliyasahau matayarisho ya Timu yake Manchester United kwa ajili ya Dabi ya Manchester ya Jumapili hii dhidi ya Mahasimu wao Manchester City na kwenda kuwa Mgeni wa Heshima kwa kukabidhi Medali kwa Wanajeshi wa Uingereza ambao wamemaliza utumishi wao toka uwanja wa vita wa Afghanistan.
Wanajeshi hao ambao walizunguka katikati ya Mji kwa Paredi walimalizia kwa ukaguzi uliofanywa na Sir Alex Ferguson na kisha kuwatunukia Medali kila mmoja wao.
+++++++++++++++++++++++++++
LIGI KUU ENGLAND=RATIBA:
Jumamosi 8 Desemba 2012
[SAA 12 Jioni]
Arsenal v West Brom
Aston Villa v Stoke
Southampton v Reading
Sunderland v Chelsea
Swansea v Norwich
Wigan v QPR
Jumapili 9 Desemba 2012
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Man City v Man United
[SAA 12 Jioni]
Everton v Tottenham
[SAA 1 Usiku]
West Ham v Liverpool
Jumatatu 10 Desemba 2012
[SAA 5 Usiku]
Fulham v Newcastle
Jumanne 11 Desemba 2012
[SAA 4 Dak 45 Usiku]

No comments:

Post a Comment