Tuesday, January 8, 2013

NFF YAMPUUZIA KUHUSIANA NA SUALA L MSHAMBULIAJI WA NEWCASTLE UNITED AMEOBI.


SHIRIKISHO la Soka la Nigeria, NFF limesema kuwa halitamchukulia hatua yoyote dhidi ya Shola Ameobi kufuatia kushindwa kukubali mwaliko wa kuiwakilisha timu ya taifa ya nchi hiyo maarufu kama Super Eagles katika michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon itakayofanyika Afrika Kusini. Mshambuliaji huyo aliitwa na kocha wa nchi hiyo Stephen Keshi pamoja na wachezaji wengine 31 lakini hakuonekana na wala hakutoa sababu zozote. Ameobi mwenye umri wa miaka 31 aliitwa kuichezea Super Eagles katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki miezi miwili iliyopita na ilikuwa ajumuishwe katika kikosi cha wachezaji 23 kitachoshiriki michuano ya Afcon inayoanza kutimua vumbi Januari 19 na kumalizika Februari 10 mwaka huu. Ingawa mkataba wa mchezaji huyo unaitaka klabu yake ya Newcastle United ambayo inashiriki Ligi Kuu nchini Uingereza kumuachia wakati wa mashindano kocha wa Super Eagle Keshi hakutaka kumuondoa kwenye kikosi chake mpaka wiki iliyopita. Katibu Mkuu wa NFF Musa Ahmadu amesema hawatakata rufani katika Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kumzuia Ameobi kutoichezea Newcastle wakati wa mashindano hayo na kudai wana mambo mengi muhimu ya kufanya katika kuandaa kuliko hilo suala la mchezaji huyo. Ahmadu alidai kuwa wapo wachezaji wengi wazuri ambao wanaweza kuisaidia nchi hiyo kufanya vyema kwenye michuano hiyo hivyo kutokuwepo kwa mchezaji huyo hadhani kama kutawaathiri sana.

No comments:

Post a Comment