Tuesday, January 8, 2013

CAPITAL ONE CUP: LEO NUSU FAINALI BRADFORD v VILLA

CAPITAL_ONE_CUP-BEST>>KESHO CHELSEA v SWANSEA!!
NUSU FAINALI za CAPITAL ONE CUP, zamani likiitwa Carling Cup au Kombe la Ligi, zitaanzwa kuchezwa leo kwa Mechi kati ya Bradford City na Aston Villa na kesho ni Chelsea v Swansea City.
Nusu Fainali za Mashindano haya huchezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.

DONDOO za LIGI CUP:
-Aston Villa wameshinda Kombe hili mara 5 mara ya mwisho ni 1996
-Chelsea wameshinda mara 5 ikiwa ni pamoja na 2005 na 2007
-Bradford na Swansea hawajawahi kutwaa Kombe hili.

DONDOO za MECHI BRADFORD v VILLA
Uwanja: Coral Windows Stadium
Hali za Wachezaji
Kuna hatihati kuhusu kucheza kwa Wachezaji wa Bradford Fowadi James Hanson na Beki James Meredith ambao wana maumivu.
Straika wa Aston Villa Darren Bent huenda akabaki na namba baada ya juzi kufunga Bao dhidi ya Ipswich kwenye FA Cup lakini Christian Benteke, ambae hakucheza na Ipswich, anategemewa sana kuchezeshwa badala ya Bent.
Wakati Winga hatari wa Villa, Gabby Agbonlahor, amepona, Marc Albrighton ana hatihati kucheza kwa vile ana maumivu ya mguu.
Uso kwa Uso
-Timu hizi zinakutana kwa mara ya 39 lakini ni mara ya kwanza tangu Februari 2001 ambapo Villa ilishinda Bao 3-0.
-Aston Villa wameifunga Bradford mara mbili kwenye Kombe la Ligi, Bao 4-3 Mwaka 1961 walipocheza ugenini na 7-1 Mwaka 1964 walipocheza nyumbani.
RATIBA-NUSU FAINALI
[Mechi zote kuanza SAA 4 DAK 45 Usiku]
Jumanne Januari 8
Bradford v Aston Villa
Jumatano Januari 9
Chelsea v Swansea City
MARUDIANO
Jumanne Januari 22
Aston Villa v Bradford
Jumatano Januari 23
Swansea City v Chelsea
FAINALI
Jumapili Februari 24
Uwanja wa Wembley, London

No comments:

Post a Comment