Tuesday, January 8, 2013

KOCHA AZAM ASEMA HERI SIMBA KULIKO TUSKER NI KIFO


Kali Ongala

KOCHA Msaidizi wa Azam FC, Muingereza Kalimangonga Sam Daniel Ongala, maarufu kama Kali, amesema kwamba wamefurahia kukutana na Simba SC katika Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi kuliko Tusker ya Kenya, kwa sababu hiyo itakuwa njia ya mkato kwao kuingia Fainali.
Akizungumza  jana usiku baada ya mechi dhidi ya Mtibwa Sugar, mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga, alisema kwamba Tusker ni timu ambayo imeonyesha kiwango kikubwa mno cha soka katika mashindano hayo hadi sasa, hivyo wangekutana nayo mapema ingekuwa mtihani mgumu.
“Hatuihofii timu yoyote, lakini kukutana na Simba SC badala ya Tusker katika Nusu Fainali ni afadhali kwetu, kwa sababu Tusker ni timu ngumu, ambayo imeonyesha kiwango kikubwa mno cha soka hadi sasa,”alisema Kali.
Kali amesema nia na dhamira ya Azam FC ni kutetea Kombe la hilo la Mapinduzi na hawaihofii timu yoyote watakatokutana nayo.
Azam FC itamenyana na Simba SC katika Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi Januari 10, mwaka huu kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Hiyo inafuatia Azam kutoka sare ya bila kufungana na Mtibwa Sugar usiku wa jana kwenye Uwanja wa Amaan visiwani hapa, katika mchezo wa mwisho wa Kundi B la michuano hiyo. 
Azam imemaliza na pointi tano na kuongoza Kundi B, ikifuatiwa na Miembeni iliyomaliza na pointi nne.
Miembeni itamenyana na kinara wa Kundi A, Tusker ya Kenya keshokutwa katika Nusu Fainali ya kwanza.
Katika mchezo wa jana, Azam ikiongozwa na washambuliaji wawili, Gaudence Mwaikimba aliyekuwa katikati na Brian Umony aliyekuwa akishambulia kutokea pembeni ililitia misukoko miwili mitatu lango la Mtibwa, lakini leo kipa Hussein Sharrif ‘Casillas’ alisimama imara kwa dakika zote 90 na kuokoa hatari zote.
Mtibwa iliyocheza na washambuliaji wawili pia, Hussein Javu na Juma Zuilio ililitia misukosuko pia lango la Azam, lakini Mwadini Ally kipa wa Azam alikuwa makini kuokoa hatari zote.
MSIMAMO WA KUNDI A:
                        
                      P    W  D   L    GF GA GDPts
Tusker FC      3    2    1    0    7    2    5    7
Simba SC       3    1    2    0    6    4    2    5
Jamhuri FC     3    1    0    2    4    6    -2  3
Bandari FC     3    0    1    2    3    8    -5  1
MSIMAMO WA KUNDI B:
                              
                         P    W  D   L    GF GA GDPts
Azam FC           3    1    2    0    3    1    2    5
Miembeni           3    1    1    1    5    4    1    4
Coastal Union    3    0    3    0    1    1    0    3   
Mtibwa Sugar    3    0    2    1    2    5    -3  2   
WAFUNGAJI WA MABAO:
Adeyum Saleh              Miembeni       3
Jesse Were                  Tusker FC       3
Haruna Chanongo        Simba SC       2
Mfanyeje Mussa           Jamhuri          2
Ismail Dunga                Tusker FC      1
Michael Olunga            Tusker FC      1
Andrew Tolowa             Tusker FC      1
Joackins Atudo             Azam FC        1
Gaudence Mwaikimba  Azam FC        1
Amour Janja                 Bandari          1
Mohamed Hamdani      Miembeni       1
Rashid Roshwa            Miembeni       1
Juma Mpakala              Mtibwa           1
Ally Mohamed              Mtibwa           1
Felix Sunzu                 Simba SC       1
Kiggi Makassy             Simba SC       1
Shomary Kapombe      Simba SC       1
Fahad Abdallah           Jamhuri          1
Ally Bilal                      Jamhuri          1
Faudhi Ally                  Bandari           1
Haitham Juma             Bandari           1
Jerry Santo                  Coastal U       1
RATIBA KOMBE LA MAPINDUZI:
Janauri 2, 2013
Tusker 5-1 Bandari
Simba SC 2-2 Jamhuri
Januari 3, 2013
Mtibwa Sugar 1-4 Miembeni
Azam FC 0-0 Coastal Union  
Januari 4, 2013
Jamhuri 2-1 Bandari
Simba SC 1-1 Tusker FC
Januari 5, 2013
Mtibwa Sugar 1-1 Coastal Union
Miembeni 1-2 Azam
Januari 6, 2013
Tusker 1-0 Jamhuri
Simba SC 1-1 Bandari
Januari 7, 2013
Miembeni 0-0 Coastal Union
Azam FC 0-0 Mtibwa Sugar
Januari 9, 2013
Tusker  FC Vs Miembeni FC
Januari 10, 2013
Azam FC Vs Simba SC
Januari 12, 2013
FAINALI
ORODHA YA MABINGWA KOMBE LA MAPINDUZI
2003   Mtibwa Sugar
2004   Yanga SC
2005   Yanga SC
2006   Simba SC
2007   Yanga SC
2008   Simba SC
2009   Miembeni FC
2010   Simba FC
2011   Azam FC
2013   ????????

No comments:

Post a Comment