Tuesday, January 8, 2013

MESSI JANA ALINYAKUWA BALLON D'OR KWA MARA YA NNE MFULULIZO NA KICHEKI KIKOSI BORA CHA DUNIA.


MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi ameweka rekodi kwa kunyakuwa tuzo ya mchezaji bora wa dunia maarufu kama FIFA Ballon d’Or katika sherehe zilizofanyika jijini Zurich, Switzerland. Messi mwenye umri wa miaka 25 alinyakuwa tuzo hiyo mbele ya Andres Iniesta ambaye wanacheza wote Barcelon na mshambuliaji nyoa wa Real Madrid Cristiano Ronaldo. 
Mwaka 2012 ulikuwa na mafanikio makubwa kwa Messi baada ya kufunga mabao mengi na kuipita rekodi iliyowekwa miaka 40 iliyopita na Gerd Muller ambaye alifunga mabao 85 huku yeye akimaliza mwaka jana akiwa amefunga mabao 91. Akishukuru mara baada ya kupokea tuzo hiyo Messi aliwashukuru waandaji na wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine katika kupiga kura ya kumchagua kubeba tuzo hiyo kwa mara ya nne. 
Nyota huyo pia aliwashukuru wachezaji wenzake wa Barcelona akiwemo Iniesta ambaye walikuwa wakigombea wote tuzo makocha na viongozi bila kusahau wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya Argentina na mashabiki wake wote wa ujumla.
  
KIKOSI bora cha mwaka 2012 maarufu kama FIFPro waliosimama mbele kulia na timu zao katika mabano Xabi Alonso (Real Madrid, Hispania), Xavi Hernandez (Barcelona, Hispania), Andres Iniesta (Barcelona, Hispania), Lionel Messi (Barcelona, Argentina), Radamel Falcao (Atletico Madrid, Colombia), Cristiano Ronaldo (Real Madrid, Ureno), Marcelo (Real Madrid, Brazil), Sergio Ramos (Real Madrid, Hispania), Gerard Pique (Barcelona, Hispania), Dani Alves (Barcelona, Brazil) na Iker Casillas (Real Madrid, Hispania).
 

No comments:

Post a Comment