Tuesday, January 8, 2013

JERRY SANTO ASEMA BAHATI HAIKUWA YAO COASTAL UNION


Santo katika mechi dhidi ya Azam Kombe la Mapinduzi
NAHODHA wa Coastal Union ya Tanga katika Kombe la Mapinduzi, Mkenya Jerry Santo amesema kwamba kutolewa kwao mapema katika michuano hiyo ya mwaka huu, kumetokana na kukosa bahati, lakini kama soka walicheza.
Akizungumza  jana usiku, Santo aliyewahi kuchezea Simba SC, alisema kwamba Coastal ilicheza soka nzuri na ndiyo maana haikufungwa hata mechi moja, lakini kwa kukosa bahati imetolewa.
“Tulicheza vizuri, mechi zote tulipata nafasi lakini tulitumia moja tu, bahati haikuwa yetu, lakini timu yetu ni nzuri na tunaamini katika Ligi Kuu (ya Bara) tutafanya vizuri,”alisema kiungo huyo wa zamani wa Tusker FC ya Kenya.
Coastal Union ya Tanga ilitolewa katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi, baada ya sare ya bila kufungana na Miembani FC jioni ya jana kwenye Uwanja wa Mao Dze Tung, Zanzibar.

No comments:

Post a Comment