Tuesday, January 8, 2013

WAAMUZI WA AFCON WATAJWA.


JUMLA ya waamuzi 18 na washika vibendera 21 wameteuliwa kuchezesha mechi za michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon itakayoanza kutimua vumbi Januari 19 mwaka huu nchini Afrika Kusini. Kuna mabadiliko mawili kwa upande wa waamuzi na nane kwa upande wa washika vibendera kulinganisha na wale ambao walichezesha fainali za michuano hiyo zilizofanyika nchini Equatorial Guinea na Gabon mwaka jana. Katika orodha hiyo inajumuisha waamuzi wawili ambao wamechezesha fainali zilizopita akiwemo Komlan Coulibaly kutoka Mali aliechezesha fainali ya mwaka 2010 nchini Angola na Badar Diatta wa Senegal alichezesha fainali ya mwaka jana kati ya Zambia na Ivory Coast jijini Libreville. Coulibaly mwenye umri wa miaka 42 anatarajia kuweka rekodi ya kuwa mwamuzi alichezesha Afcon mara nyingi zaidi ambapo hii ikiwa ni mara yake ya saba toka alipoteuliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2002. Waamuzi wawili ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza ni pamoja na Sylvester Kirwa kutoka Kenya na Bernard Camille kutoka Seychelles.

No comments:

Post a Comment