Tuesday, January 8, 2013

ADEBAYOR AKUBALI KUREJEA TOGO.


MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Togo, Emmanuel Adebayor hatimaye amekubali kujiunga na kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo kwa ajili ya michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon baada ya kusitisha mgomo wake. Adebayor aligoma kuichezea nchi yake akishinikiza Shirikisho la Soka la Togo-TFF kuwalipa wachezaji malimbikizo ya posho zao. Rais wa shirikisho hilo Gabriel Ameyi alitangaza jana kuwa kikosi cha nchi hiyo kitasafiri kuelekea Afrika Kusini pamoja na nahodha wake Adebayor ambaye alifanya mazungumzo na rais wan chi hiyo Faure Gnassingbe kuhusiana na tatizo hilo. Ameyi amesema watakuwa pamoja na nahodha huyo nchini Afrika Kusini baada ya mazungumzo na rais Gnassingbe kwenda sawa ingawa mshambuliaji huyo anayecheza katika klabu ya Tottenham Hotspurs hakuzungumza chochote wakati anaondoka Ikulu. Togo inakabiliwa na mchezo wa ufunguzi dhid ya Ivory Coast Januari 22 jijini Rustenburg, ukiwa ni mchezo wa kundi D ambalo pia linajumuisha timu za Algeria na Tunisia.

No comments:

Post a Comment