Tuesday, January 8, 2013

CAPITAL ONE CUP: TIMU YA DARAJA LA CHINI BRADFORD 3 VILLA 1

>>WABABE WA ARSENAL WACHUNGULIA FAINALI WEMBLEY!
>>LEO NUSU FAINALI: CHELSEA v SWANSEA!!
CAPITAL_ONE_CUP-BESTBradford City jana imejiwekea daraja zuri la kutinga Fainali ya CAPITAL ONE CUP baada ya kuichapa Aston Villa Mabao 3-1 Uwanjani Valley Parade katika Mechi ya kwanza ya Nusu Fainali na Timu hizi zitarudiana huko Villa Park hapo Januari 22.
Bradford, ambao wapo Ligi 2 wakiwa nafasi 60 chini ya Aston Villa walio Ligi Kuu England, kwenye Robo Fainali waliibwaga nje Arsenal kwa Penati 3-2 baada kutoka sare 1-1.

MAGOLI:
Bradford 3
-Wells Dakika ya 19
-McArdle 77
-McHugh 88
Aston Villa 1
-Weimann 82

Hadi mapumziko, Bradford walikuwa mbele kwa Bao 1-0 kwa Bao la Nahki Wells huku Kipa wao, Matt Duke, akiokoa michomo baada ya michomo kutoka kwa Aston Villa na hasa Christian Benteke.

DONDOO za LIGI CUP:
-Aston Villa wameshinda Kombe hili mara 5 mara ya mwisho ni 1996
-Chelsea wameshinda mara 5 ikiwa ni pamoja na 2005 na 2007
-Bradford na Swansea hawajawahi kutwaa Kombe hili.

Ikiwa Bradford watatinga Fainali, watakuwa Klabu ya kwanza kutoka Madaraja ya chini kuingia Fainali tangu Rochdale ilivyofanya hivyo Mwaka 1962.
Leo huko Stamford Bridge, Chelsea wataikaribisha Swansea City katika Mechi ya kwanza ya Nusu Fainali nyingine.
VIKOSI:
Bradford City: Duke, Darby, McHugh, McArdle, Good, Atkinson, Jones, Doyle, Hanson, Hines (Turgott - 65' ), Wells
Akiba: McLaughlin, Ravenhill, Reid, Jones, Turgott, Hannah, Connell
Aston Villa: Given, Clark, Bennett, Baker, Lowton, N'Zogbia, Delph, Bannan, Agbonlahor (Bent - 57' ), Benteke, Weimann
Akiba: Guzan, Stevens, Lichaj, Ireland, Carruthers, Bent (Burke - 85' ), Burke
Refa: Howard Webb
RATIBA/MATOKEO:
NUSU FAINALI
[Mechi zote kuanza SAA 4 DAK 45 Usiku]
Jumanne Januari 8
Bradford 3 Aston Villa 1
Jumatano Januari 9
Chelsea v Swansea City
MARUDIANO
Jumanne Januari 22
Aston Villa v Bradford
Jumatano Januari 23
Swansea City v Chelsea
FAINALI
Jumapili Februari 24
Uwanja wa Wembley, London

No comments:

Post a Comment