Tuesday, January 8, 2013

KIUNGO BORA WA AFRIKA NA MCHEZAJI BORA WA AFRIKA YAYA TOURE AREJEA NA HALI YAKE YA KAWAIDA


KIUNGO nyota wa kimataifa wa Ivory Coast, Yaya Toure amerejea katika hali yake ya kawaida baada ya kukosa Siku mbili za mazoezi katika kambi ya timu ya taifa ya nchi hiyo iliyopo jijini Abu Dhabi baada ya kupata homa kali. Kaka yake mkubwa Kolo ambaye wanacheza wote katika klabu ya Manchester City ameeleza kuwa mdogo wake Yaya alipewa muda wa kupumzika kwa ajili ya matibabu ya homa na kifua lakini hivi sasa amepona. Ivory Coast ambao wanapewa nafasi kubwa ya kunyakuwa taji la michuano ya Mataifa Afrika inayotarajiwa kutimua vumbi Januari 19 imepangwa katika kundi D pamoja na timu za Togo, Algeria na Tunisia. Kikosi hicho kinatarajia kucheza mchezo wa kirafiki na Misri Januari 14 kabla ya kuelekea Afrika Kusini ambapo wataanza kampeni zao kwa kupambana na Togo Januari 22.

No comments:

Post a Comment