CASILLAS IS A PRIDE OF MADRID - DEL BOSQUE.
KOCHA wa timu ya taifa
ya Hispania, Vicente del Bosque amedai kuwa nahodha wa Real Madrid Iker
Casillas ni mchezaji wa kujivunia wa klabu hiyo. Casillas
ambaye amecheza michezo 143 akiwa na timu ya taifa aliachwa katika
kikosi cha kocha wa Madrid Jose Mourinho katika safari Malaga na badala
yake nafasi ilichukuliwa na golikipa namba mbili Antonio Adan. Real
Madrid ambao ndio mabingwa wa Ligi Kuu nchini Hispania maarufu kama La
Liga walifungwa katika mchezo dhidi ya Malaga mabao 3-2 lakini Del
Bosque ambaye ana umri wa miaka 61 alimtetea Casillas na kudai kuwa bado
ana uwezo. Del
Bosque amedai kuwa Casillas ni mchezaji aliyeanza kucheza klabuni hapo
toka akiwa na umri wa miaka na ameifanyia mengi klabu hiyo hivyo
inatakiwa kujivunia mchezaji wa aina yake.
No comments:
Post a Comment