Tuesday, October 30, 2012

SIMBA WAWAFUATA KIBABE MAAFANDE WANYONGE MOROGORO

Wachezaji wa Simba SC

SIMBA SC tangu inaondoka leo Dar es Salaam kwenda Morogoro tayari kwa mchezo wao dhidi ya Polisi mjini Morogoro katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kesho, wakitoka kushinda mabao 3-1 dhidi ya Azam FC Jumamosi na kujiimarisha kileleni.
Mabingwa hao watetezi juzi na jana walifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Kinesi, Urafiki, Manzese, Dar es Salaam na kwa ujumla timu vizuri kuelekea mchezo huo wa tatu kucheza nje ya Uwanja wa Taifa, msimu huu baada ya awali kucheza mechi mbili Tanga dhidi ya Coastal Union na Mgambo JKT ambazo zote walilazimishwa sare ya bila kufungana.
Simba imeshinda mechi zake zote Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kutoa sare mbili tu, dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Yanga 1-1 na 2-2 dhidi ya Kagera Sugar ya Bukoba.
Wekundu hao wa Msimbazi, wapo kileleni mwa Ligi Kuu kwa pointi zao 22 baada ya kucheza mechi 10, wakifuatiwa na wapinzani wao wa tangu enzi za bibi na babu, Yanga SC wenye pointi 20 katika nafasi ya pili.
Beki Juma Said Nyosso na kiungo Haruna Moshi Shaaban ‘Boban’ wanaendelea kutumikia adhabu zao za kusimamishwa, lakini wachezaji wote wengine wapo fiti kabisa, ukiondoa Obadia Mungusa aliyefukuzwa mapema tu kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu.
Simba itamenyana na Polisi iliyorejea Ligi Kuu msimu huu, ambayo inashika mkia katika ligi hiyo, ikiwa haijashinda hata mechi moja tangu kuanza kwa ligi hiyo zaidi ya kutoa sare mbili.
Lakini hiyo haiifanyia Simba idharau mechi hiyo na kocha Mserbia, Milovan Cirkovick ameanza maandalizi ya mapema kwa ajili ya mechi hiyo.
Hofu kubwa kwa Simba ni hali ya Uwanja wa Jamhuri, Morogoro- ni mbaya na kulingana na uzoefu walioupata wa kucheza kwenye Uwanja mwingine mbovu wa Mkwakwani, Tanga wanajua watakuwa na shughuli pevu keshokutwa.
Hadi sasa Simba ndio timu pekee katika Ligi Kuu, ambayo haijapoteza mechi, ikiwa imeshinda mechi sita na kutoa sare nne, wakati Yanga imefungwa mechi mbili na Azam FC na Coastal Union zinazoifukuzia timu hiyo, zimefungwa mechi moja moja.  

MIGAMBO WAIFUATA YANGA NA VIRUNGU VILIVYOITULIZA SIMBA MKWAKWANI

Kikosi cha Mgambo JKT
TIMU ya soka ya Mgambo JKT ya mjini Handeni mkoani Tanga, imeondoka leo mjini Tanga, ilikokuwa imeweka kambi kwenda Dar es salaam ambako kesho itashuka dimbani kwenye Uwanja wa Taifa kucheza na wenyeji Yanga katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Mgambo inayoshika nafasi ya 10 kwenye msimamo wa Ligi Kuu hadi sasa kwa kuwa na pointi 10 ikiwa imecheza michezo tisa, imeondoka na wachezaji wake 22 na viongozi watatu kwa ajili ya pambano hilo ambalo timu hiyo ilisema kuwa inalichukulia kwa umakini mkubwa ili waweze kuibuka na ushindi kutokana na kujiandaa vilivyo.
Kocha Mkuu wa timu hiyo Mohamed Kampira, alisema jana mjini hapa kwamba, Yanga waailichukulie kuwa watawafunga kirahisi katika mchezo huo badala yake wategemee kupata upinzani hasa kutokana na kwamba timu hiyo ya Mgambo imejiandaa kuibuka na ushindi ili waweze kukaa katika nafasi nzuri katika mzunguko huu wa kwanza.
"Tunaondoka kesho asubuhi (leo) kwenda Dar es salaam, kama timu tumejiandaa vizuri na tunatarajia kuwapa wakati mgumu Yanga na kuishinda, wasitarajie mteremko, sisi ni timu na tunaamini kwamba tutaibuka na pointi zote tatu," alisema kwa kujiamini Kampira aliyevaa viatu vya aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Stephen Matata aliyetimuliwa baada ya timu hiyo kuanza vibaya kwa kufungwa michezo mitano mfululizo tangu kuanza kwa ligi hiyo.
Kampira alisema hadi sasa wachezaji wake wamekuwa na ari kubwa ya kuibuka na ushindi na hakuna majeruhi wote wapo katika hali nzuri ya kupambana na timu hiyo inayousaka ubingwa mwaka huu kwa udi na uvumba na kwamba amewata mashabiki wa timu hiyo kuiamini kwa wachezaji watafanya kazi iliyokusudiwa.
Mgambo JKT ambayo baada ya kumtimua kocha ilikuwa imeshikwa na kocha msaidizi Josepj Lazaro ambaye aliipa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Morogoro, akaifunga Mtibwa Sugar bao 2-1 kwenye uwanja wa Manungu, ikaifunga Toto African bao 2-0 na ikatoka sare ya 0-0 na Simba mchezo ambao Kampira ilikuwa ni mchezo wake wa kwanza kukaa kwenye benchi la timu hiyo.
Wakati huo huo, mashabiki wa klabu ya Coastal Union ya Jijini hapa, wameipongeza timu yao kwa ushindi walioupata juzi walipoifunga JKT Ruvu bao 3-0 katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es salaam hatau ambayo walisema inatia faraja na wamewataka wacheji wazidi kuongeza bidii ili lengo la kumaliza ikiwa nafasi za juu litimie.
Mmoja wa mashabiki hao Fred Tayasar alisema wamejisikia furaha ushindi huo lakini pia umewapa majonzi makubwa kwa mchezaji wao Nsa Job kuvunjika mguu katika pambano hilo hatua ambayo alisema wapenzi wa timu hiyo wanaangalia uwezekano wa kumchangia fedha kwa ajili ya kumpa ili aweze kujikimu katika kipindi atakachokuwa nje ya uwanja.


BUNJAK ATUPIWA VIRAGO AZAM, KOCHA USHINDI AREJESHWA KAZINI


bunjak akiwa na kalimangonga ongala mechi ya simba
KOCHA Mserbia wa Azam FC, Boris Bunjak amefukuzwa rasmi leo na sasa aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Muingereza Stewart Hall anarudishwa kazini.
Habari kutoka ndani ya Azam FC zimesema kwamba, sababu za kufukuzwa kwa Mserbia huyo ni kushuka kwa kiwango cha timu, hali iliyosababisha sasa ianguke hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
Tayari Bunjak amekwishapewa haki zake zote na ataondoka Alhamisi, siku ambayo Stewart atawasili kuanza tena kazi Azam FC.
Bunjak anaondoka Azam baada ya kuiongoza timu katika mechi 16, akifungwa nne tu, zote dhidi ya Simba ikiwemo ya juzi ya Ligi Kuu, waliyofungwa 3-1 na kutoa sare tatu.
Bunjak mwenye leseni ya Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA), alitua Azam, Agosti 7, mwaka huu akitokea FC Damac ya Saudia Arabia aliyoanza kuifundisha mwaka jana na kabla ya hapo alifundisha klabu kibao za kwao, zikiwemo FK Sloga Kraljevo, FK Javor Ivanjica, Crvena Zvezda Gnjilane, FK Radnicki Nis, FC Uralan Elista, FK Mladi Radnik, FK Crvena Zvezda Beograd, Al-Shaab, FK Hajduk Kula na Al-Nasr.
Awali, Bunjak aliyezaliwa Novemba 17, mwaka 1954 ( miaka 57), alicheza soka katika klabu za FK Sloga (Kraljevo), FK Vozdovac (Beograd), FK Radnicki (Kragujevac), FK Olimpia (Ljubljana), FK Sumadija (Arandjelovac), FK Sloga (Kraljevo), FK Borac (Cacak) na FK Sloga (Kraljevo).
Stewart alifukuzwa kwa kosa la kukaidi maagizo ya Bodi ya Ukurugenzi ya klabu hiyo, kumpanga Mrisho Khalfan Ngassa katika mechi ya fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame dhidi ya Yanga.
Mserbia huyo anakuwa kocha wa tano kufukuzwa Azam, ndani ya miaka minne tangu ianze kucheza Ligi Kuu, 2008 baada ya Stewart, Mbrazil Neider dos Santos, Sylvester Marsh na Itamar Amorin, Mbrazil mwingine.
Lakini Stewart angalau aliacha kumbukumbu ya taji na Medali Azam, baada ya kuiwezesha kutwaa Kombe la Mapinduzi Januari, kushika nafasi ya pili katika Ligi Kuu Aprili, kabla ya kushika nafasi ya pili Kombe la Urafiki na Kagame miezi miwili iliyopita, mambo ambayo bila shaka yamemfanya afikiriwe tena.
Stewart ana sifa ya kutokuwa mbinafsi na mwenye kuwaamini watu wa chini yake, kwa mfano namna ambavyo alikuwa akimpromoti Kali Ongala. Alimkuta Kali kama mchezaji, lakini kwa sababu ya umri kumtupa mkono, akashauriana naye awe Kocha Msaidizi na mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga, akakubali.
Chini ya Stewart, Kali alikuwa akiachiwa timu aiongoze ili kumjengea kujiamini zaidi na mwezi uliopita aliachiwa timu kwenye Kombe la Urafiki, akaifikisha fainali, ambako ilifungwa na Simba kwa penalti kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90.  
WASIFU WA BORIS BUNJAK:
JINA KAMILI: Boris Bunjak
KUZALIWA: Novemba 17, 1954 (Miaka 57)
KLABU ALIZOCHEZEA:
1967- 1975: FK Sloga (Kraljevo)
1975- 1978  FK Vozdovac (Beograd)
1978- 1979  FK  Radnicki (Kragujevac)
1979- 1980  FK Olimpia (Ljubljana)
1980- 1981  FK  Sumadija (Arandjelovac)
1981- 1985  FK  Sloga (Kraljevo)
1985- 1986  FK  Borac (Cacak)
1986- 1990  FK  Sloga (Kraljevo)
KLABU ALIZOFUNDISHA:
1990-1993:   FK Sloga (Kraljevo)
1995-1996:   FK Javor (Ivanjica)
1996-1997:   Crvena Zvezda (Gnjilane)
1999:                      FK Radnicki (Nis)
2000:                      FC Uralan Elista (Urusi)
2000-2002:   FK Mladi (Radnik)
2002-2004:   FK Crvena Zvezda (Beograd)
2004:                      Al-Shaab (UAE)
2005:                      FK Hajduk (Kula)
2006-2007:   Al-Nasr (Oman)
2009:                      Al Oruba Sur (Oman)
2011:                      FC Damac (Saudi Arabia)
2011:                      AL NASER (Oman)
  
REKODI YA BORIS BUNJAK AZAM
Azam 2-1 Polisi                   (BancABC)
Azam 1-2 Simba B              (BancABC)
Azam 8-0 Trans Camp        (Kirafiki)
Azam 1-0 Prisons               (Kirafiki)
Azam 2-0 Coastal Union     (Kirafiki)
Azam 2-3 Simba SC           (Ngao ya Jamii)
Azam 1-0 Kagera Sugar     (Ligi Kuu)
Azam 2-2 Toto African        (Ligi Kuu)
Azam 3-0 JKT Ruvu           (Ligi Kuu)
Azam 1-0 Mtibwa Sugar     (Ligi Kuu)
Azam 1-0 African Lyon       (Ligi Kuu)
Azam 2-3 Simba SC           (Kirafiki)
Azam 1-0 Polisi                  (Ligi Kuu)
Azam 0-0       Prisons         (Ligi Kuu)                                      
Azam 1-1 Ruvu Shooting    (Ligi Kuu)
Azam 1-3 Simba                 (Ligi Kuu)

TFF YASAKA MILIONI 225 ZA KUIPELEKA MOROCCO SERENGETI BOYS

Rais wa TFF, Tenga akizungumza na Waandishi wa Habari leo, Kulia ni Sunday Kayuni, Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF na kushoto, Katibu, Angetile Osiah 


RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Chillah Tenga amesema kwamba timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys inahitaji zaidi ya Sh Milioni 225 kwa ajili ya kampeni yake iliyobakia ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika mwakani nchini Morocco.
Akizungumza na Waandishi wa Habari makao makuu ya TFF, Ilala, Dar es Salaam, Tenga alisema kwamba shirikisho lake kwa sasa halina fedha hizo, kwa sababu hiyo haina mdhamini, zaidi ya kutegemea misaada ya wadau.
Tenga alisema tayari Kamati ya Vijana ya TFF imekwishakutana kuweka mikakati ya kuiwezesha Serengti kushiriki vema kampeni hizo, ikiwemo kuunda Kamati ya kuisaidia timu hiyo.
Hata hivyo, Tenga hakuitaja Kamati iliyoundwa kwa sababu bado hawajazungumza na Wajumbe walioteuliwa.
Alisema kocha wa timu hiyo, Mdenmark Jacob Michelsen ameomba mechi za kujipima nguvu kabla ya kucheza na Kongo Brazaville kuwania tiketi ya Morocco na Kamati ya Vijana inahangaikia suala hilo kwa sasa.
Alisema tayari kuna mwaliko kutoka Botswana wa Serengeti kwenda kucheza, lakini kutokana na ukosefu wa fedha wanashindwa hadi sasa kutoa jibu.
Kikosi cha wachezaji 25 cha Serengeti Boys kipo kambini mjini Dar es Salaam tangu Oktoba 21, mwaka huu kujiandaa na mechi hiyo, ya kwanza ikichezwa nyumbani Novemba 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, wakati mechi ya marudiano itachezwa wiki mbili baadaye.
Tanzania imefuzu bila jasho hadi kufika hatua hiyo, baada ya wapinzani wake wa awali, Kenya na Misri kujitoa katika Raundi ya Kwanza na ya Pili.
Kama Tanzania itafuzu kushiriki Fainali hizo za mwakani, itapoza machungu ya mwaka 2005 walipofuzu kucheza Fainali za Vijana wa umri huo kwa kuzitoa Rwanda, Zambia na Zimbabwe, lakini baadaye kwa sababu ya ‘kufoji’ umri wa Nurdin Bakari, ikaondolewa mashindanoni.
Zaidi ya Fainali za Mataifa ya Afrika 1980 na CHAN 2009, katika soka ya wanaume, Tanzania haijashiriki fainali nyingine zozote za Afrika tangu iingie kwenye soka ya kimataifa.

UCHAGUZI DRFA JIRANI KABISA NA UCHAGUZI WA TFF

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA), Juma Simba ‘Gadaffi’ (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari leo, kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) juu ya uchaguzi wa chama hicho. Simba amesema uchaguzi wa DRFA utafanyika Desemba 8, mwaka huu na fomu za kugombea nafasi mbalimbali zitaanza kutolewa kesho. Novemba 4 hadi 8, Kamati yake itapitia fomu za walioomba uongozi, Novemba 9 hadi 13 utakuwa muda wa pingamizi kwa wagombea, ambazo zitajadiliwa Novemba 14 hadi 16, wakati Novemba 17 hadi 19 watatoa fursa ya kukata rufaa, ambazo zitasikilziwa Novemba 20 hadi 24 na baada ya hapo, Novemba 25 yatatangazwa majina ya wagombea waliopitishwa. Tarehe hii mpya ya uchaguzi wa DRFA inaufanya usogeleane na uchaguzi wa TFF, ambao utafanyika pia Desemba.   

TENGA ACHEMSHA VITA YA RUSHWA TFF

Rais wa TFF, Leodegar Tenga (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari leo, makao makuu ya shirikisho hilo, Ilala, Dar es Salaam. Kulia ni Sunday Kayuni, Mkurugenzi wa Ufundi na kushoto ni Angetile Osiah, Katibu Mkuu


RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Chillah Tenga amesema kwamba vita dhidi ya rushwa katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ni ngumu na inahitaji sapoti kubwa ya wadau na wapenzi wa mchezo wenyewe ili kuifanikisha.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, makao makuu ya TFF, Ilala mjini Dar es Salaam, Tenga alisema kwamba pamoja awali kuwepo kwa mazingira ya ushahidi wa rushwa, lakini wanashindwa kwa sababu wao wana mipaka yao.
“Hili la rushwa kwa kweli ni gumu, ni gumu kwa sababu sisi tuna mipaka yetu, lazima tupate ushirikiano na vyombo husika. Lazima tupate ushirikiano wa wapenzi wenyewe wa mpira,”alisema Tenga.
Beki huyo wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, alisema wakati mwingine inakuwa vita hiyo inakuwa ngumu zaidi anaposikia hata Waandishi wa Habari wanahusika.
“Mimi sijathibitisha, lakini watu wananiambia viongozi wenyewe wanashiriki mchezo huu. Tena nasikia hadi nyinyi Waandishi wa Habari wakati mwingine mnatumiwa kupenyeza rushwa, kwa kweli inasikitisha,”alisema Tenga.
Kuhusu vipimo vya dawa za kulevya katika Ligi Kuu, Tenga alisema kwamba mchakato wa zoezi hilo unaendelea na walichokifanya kwa sasa ni kuwataaribu na kuwapa muda wahusika waache taratibu.
Alisema wamewapa nusu msimu watumiaji wa mihadarati katika soka ya Tanzania kujiondoa taratibu na tayari wamekwishawaambia hadi  viongozi wa klabu zote, ili zoezi hilo likianza liende vizuri.
“Hatutaki kuwaadhiri vijana wetu, ndiyo maana tumewaambia mapema, ili wale ambao wanavuta bangi kwa mfano, waanze taratibu kula chwingamu waache bangi, ili wakati utakapofika, hakutokuwa na mzaha,”alisema Tenga.

SIMBA SC HAKUNA KULALA, INAUA MMOJA INAWINDA MWINGINE

Wachezaji wa Simba SC

SIMBA SC tangu jana wameendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo wao ujao dhidi ya Polisi mjini Morogoro katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, wakitoka kushinda mabao 3-1 dhidi ya Azam FC Jumamosi na kujiimarisha kileleni.
Mabingwa hao watetezi jana walifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Kinesi, Urafiki, Manzese, Dar es Salaam na kwa ujumla timu vizuri kuelekea mchezo huo wa tatu kucheza nje ya Uwanja wa Taifa, msimu huu baada ya awali kucheza mechi mbili Tanga dhidi ya Coastal Union na Mgambo JKT ambazo zote walilazimishwa sare ya bila kufungana.
Simba imeshinda mechi zake zote Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kutoa sare mbili tu, dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Yanga 1-1 na 2-2 dhidi ya Kagera Sugar ya Bukoba.
Wekundu hao wa Msimbazi, wapo kileleni mwa Ligi Kuu kwa pointi zao 22 baada ya kucheza mechi 10, wakifuatiwa na wapinzani wao wa tangu enzi za bibi na babu, Yanga SC wenye pointi 20 katika nafasi ya pili.
Beki Juma Said Nyosso na kiungo Haruna Moshi Shaaban ‘Boban’ wanaendelea kutumikia adhabu zao za kusimamishwa, lakini wachezaji wote wengine wapo fiti kabisa, ukiondoa Obadia Mungusa aliyefukuzwa mapema tu kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu.
Simba inatarajiwa kuondoka kesho Dar es Salaam kwenda Morogoro kwa ajili ya mchezo dhidi ya Polisi ambayo inashika mkia katika ligi hiyo, ikiwa haijashinda hata mechi moja tangu kuanza kwa ligi hiyo zaidi ya kutoa sare mbili.
Lakini hiyo haiifanyia Simba idharau mechi hiyo na kocha Mserbia, Milovan Cirkovick ameanza maandalizi ya mapema kwa ajili ya mechi hiyo.
Hofu kubwa kwa Simba ni hali ya Uwanja wa Jamhuri, Morogoro- ni mbaya na kulingana na uzoefu walioupata wa kucheza kwenye Uwanja mwingine mbovu wa Mkwakwani, Tanga wanajua watakuwa na shughuli pevu keshokutwa.
Hadi sasa Simba ndio timu pekee katika Ligi Kuu, ambayo haijapoteza mechi, ikiwa imeshinda mechi sita na kutoa sare nne.

YONDAN, BAHANUZI WARUDI RASMI KAZINI YANGA

Bahanuzi


BEKI Kevin Yondan na mshambuliaji Said Bahanuzi waliokuwa nje ya Uwanja kwa zaidi ya wiki mbili kutokana na kusumbuliwa na majeruhi, leo wanatarajiwa kuanza programu rasmi ya mazoezi na wenzao baada ya kupata ahueni ya kutosha.
Wachezaji hao wamekuwa wakifanya mazoezi mepesi kwa zaidi ya wiki moja baada ya kupata ahueni kidogo na sasa wamepona kabisa na leo kocha Mholanzi, Ernie Brandts anatarajiwa kuwajumuisha kwenye programu yake kamili, Uwanja wa sekondari ya Loyola, Mabibo, Dar es Salaam.
Yanga imerejea kutoka Arusha, ambako Jumamosi ilivuna pointi tatu kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji JKT Oljoro, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid na kupanda nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, wakitimiza pointi 20 baada ya kucheza mechi 10.
Yanga sasa iko nyuma kabisa ya wapinzani wao wa jadi, Simba SC wanaoongoza Ligi Kuu kwa pointi zao 22, baada ya kucheza mechi 10 pia.
Mabingwa hao wa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame sasa wanajiandaa na mchezo wao ujao wa ligi hiyo, dhidi ya Mgambo JKT Jumatano Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mgambo JKT pamoja na kwamba imepanda Ligi Kuu msimu huu, lakini imeonyesha ni timu ya ushindani baada ya kutoa sare ya bila kufungana na Simba SC, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Kwa sababu hiyo, Yanga wamechukua tahadhari ya kutosha kuelekea mchezo huo na tangu jana Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Abdallah Ahmad Bin Kleb amekuwa ‘akienda mbio’ kuhakikisha timu inashinda keshokutwa.   
Kurejea kwa Yondan na Bahanuzi kunaongeza matumaini ya ushindi kwa Yanga katika mchezo huo, ingawa upande mwingine ni mtihani kwa Brandts, kwani katika kipindi ambacho wachezaji hao wako ‘wadini’, walioshika nafasi zao wamekuwa wakifanya vizuri.     
Mbuyu Twitwe aliyehamishwa kutoka beki ya kulia hadi beki ya kati tangu Yondan aumie Oktoba 3, amekuwa akifanya vizuri sawa na Jerry Tegete aliyempokea Bahanuzi Oktoba 8, alipoumia naye amekuwa akifanya vizuri pia.
Kwa kuzingatia Twite alikuwa ‘uchochoro’ alipokuwa akicheza pembeni, watu wanasubiri kuona kama Brandts atamrudisha huko huko baada ya Yondan kurejea, au ataamua mmoja kati yao na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ataanzia benchi.
Upande wa Tegete na Bahanuzi, kuna uwezekano mmoja wao atakuwa anaanzia benchi kwa sasa na mwingine kumpokea mwenzake baadaye. 

COASTAL WAISHUSHA TENA AZAM FC MBIO ZA UBINGWA LIGI KUU

Azam FC

USHINDI wa mabao 3-0 wa Coastal Union dhidi ya JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana, umebadilisha kabisa taswira ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya Wagosi hao wa Kaya kupanda hadi nafasi ya tatu wakiiengua Azam.
Mapinduzi katika Ligi Kuu yalianza Jumamosi, baada ya Yanga kupanda hadi nafasi ya pili kutokana na ushindi wao wa bao 1-0 dhidi ya JKT Oljoro, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha huku Azam FC ikifungwa na Simba SC mabao 3-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kushuka nafasi ya tatu.
Lakini Coastal jana imeishusha Azam kwa nafasi moja zaidi, na sasa mbio za ubingwa wa Ligi Kuu zinaonekana kuwa za farasi watatu, lakini Azam si miongoni mwao, bali Simba, Yanga na Coastal.
Mwishoni mwa wiki ijayo, Yanga itacheza na Azam FC, mechi ambayo itatengeneza taswira ya namna mzunguko wa kwanza utakavyomalizika.
Azam ikishinda inaweza kurudi nyuma ya Simba SC, lakini tofauti na hapo watu watasubiri kuona kati ya watani hao wa jadi, nani atamaliza mzunguko wa kwanza akiwa kileleni.    
Kabla ya kucheza na Azam, Yanga itacheza Mgambo Shooting Jumatano, wakati Azam itacheza na Coastal Union Chamazi.
Ligi Kuu sasa inazidi kunoga baada ya juzi Simba kuzinduka kutoka kwenye wimbi la sare, baada ya kufanikiwa kuichapa Azam FC mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi huo, unaifanya Simba izidi kujitanua kileleni mwa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 22, baada ya kucheza mechi 10, wakati Azam FC inapromoka hadi nafasi ya nne kwa pointi zake 18, baada ya kucheza mechi tisa, ikiipisha Coastal yenye pointi 19 katika nafasi ya tatu na Yanga sasa ni ya pili kwa pointi zake 20.
Mechi nyingine za ligi hiyo juzi, African Lyon ilitoka sare ya 1-1 Kagera Sugar Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam na Ruvu Shooting ikaifunga 2-1 Polisi Morogoro Uwanja wa Mabatini, Mlandizi.
Mechi kati ya Mgambo JKT na Prisons iliyokuwa ichezawe juzi Uwanja wa Mkwakwani, Tanga imeahirshwa kutokana na wachezaji wa Prisons kupata ajali wakiwa njiani kuelekea Tanga.
JKT Ruvu jana ilifungwa 3-0 na Coastal Union Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam na Toto Africans ilitoka sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.


Wenger alitolea mimacho CAPITAL ONE CUP!


ARSENE_WENGER-13Wakiwa bado wanasaka Kombe lao la kwanza tangu Mwaka 2005 na leo wako ugenini kucheza Raundi ya 4 ya Mtoano ya CAPITAL ONE CUP, zamani CARLING CUP, dhidi ya Reading, Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema wao watapigania kila Kombe ambalo wanashiriki Msimu huu.
+++++++++++++++++++++++++
CAPITAL ONE CUP
RATIBA RAUNDI ya 4:
Mechi kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku, Bongo Taimu
Jumanne Oktoba 30
Sunderland v Middlesbrough
Swindon v Aston Villa
Wigan v Bradford
Leeds v Southampton
Reading v Arsenal
Jumatano Oktoba 31
Norwich v Tottenham
Liverpool v Swansea [SAA 5 Usiku]
Chelsea v Manchester United
+++++++++++++++++++++++++
Leo Usiku, Arsenal wanawania kutinga Robo Fainali ya 10 mfululizo kwenye Kombe la Ligi ambalo sasa linaitwa CAPITAL ONE CUP watakaposafiri kwenda Madejski Stadium kucheza na Reading.
Wenger amekiri kuwa vipo Vikombe wanavyoviwekea umuhimu mkubwa lakini hawadharau Mashindano yeyote na amesema: “Tutapigana katika kila Kikombe ingawa huwa unapanga namna ya kucheza kwa sababu tupo pia kwenye Mashindano muhimu kama Ligi, UEFA.”
Kwenye Kombe kama hili CAPITAL ONE CUP mara nyingi Timu kubwa huchezesha Wachezaji wao wasiocheza mara kwa mara Kikosi cha Kwanza na wale Chipukizi toka Kikosi cha Akiba.
Wakati huo huo, Wenger amemsifia Andrey Arshavin kwa mchango wake hasa alipoingizwa wakati walipoifunga QPR bao 1-0 Jumamosi iliyopita na ameahidi kumchezesha Mechi ya leo.
Msimu uliopita Arshavin alipondwa sana kwa uchezaji wake lakini Wenger amesema: “Ni Mchezaji mzuri! Atacheza Mechi na Reading. Kila Siku anakuja mazoezini na ana mkazo! Utaona Jumamosi alipocheza alicheza vizuri lakini Watu wanamponda na hilo halikubaliki.”
 

Messi atunzwa BUTI ya DHAHABU Ulaya!


LIONEL_MESSIStaa wa Barcelona na Argentina, Lionel Messi, ametunzwa Kiatu cha Dhahabu, hii ikiwa ni mara yake ya pili, kwa kufunga Bao nyingi katika Ligi Msimu uliopita.
Messi, Miaka 25, aliweka rekodi huko Spain kwa kuifungia Bao 50 Barcelona na kumpiku Staa wa Real Madrid Cristiano Ronaldo kwa Bao 4.
Akipokea Tuzo hiyo, Messi alisema: “Hii ni zawadi kwa kufunga Mabao lakini bila Wachezaji wenzangu nisingefunga. Kwa hiyo hii ni zawadi yetu wote!”
Messi alitwaa Buti ya Dhahabu kwa mara ya kwanza Mwaka 2010 kwa kufunga Bao 34 na kuisaidia Barcelona kutwaa Ubingwa.
Messi, ambae ndie Mchezaji Bora Duniani, pia yumo kwenye Listi ya Wagombea Tuzo ya FIFA ya 2012 ya Ballon d'Or ambayo hutunukiwa Mchezaji Bora na yeye ni miongoni mwa Wachezaji 23 watakaoiwania.
Kocha wa Barcelona, Tito Vilanova alisema: “Hatutaona Mchezaji mwingine kama yeye! Si kwa magoli anayofunga bali kwa jinsi anavyouelewa mchezo ndilo linamfanya awe bora! Jumamosi, alikimbia Mita 50 kurudi nyuma kusaidia ulinzi wakati wa kona wakati tunaongoza bao 5-0! Si Wachezaji wengi wangefanya hivyo!”
Messi alikabidhiwa Tuzo hiyo ya Buti ya Dhahabu na Luis Suarez Miramontes ambae ni Mchezaji wa zamani wa Kimataifa wa Spain alieshinda Ballon d'Or Mwaka 1960.


Mario Balotelli of Manchester City, who has been nominated for the Ballon D'Or
Mtukutu Balotelli naye yumo
Golden Boy: Lionel Messi has been shortlisted for the Ballon D'Or but he's already won the Golden Boot for being Europe's top goalscorer last season
Lionel Messi amerodheshwa kwenye wachezaji wanaowania Ballon D'Or, wakati tayari amekwishashinda tuzo Kiatu cha Dhahabu kwa kuwa mfungaji bora Ulaya msimu uliopita
Impressive feat: Messi scored 50 league goals for Barcelona last season, the highest haul in Europe
Messi alifunga mabao 50 katika ligi akiwa na Barcelona msimu uliopita ambayo ni rekodi Ulaya
On the list: Wayne Rooney of Manchester United is the only Englishman to have made the Ballon D'Or shortlist
Wayne Rooney wa Manchester United ni Muingereza pekee katika orodha ya wanaowania Ballon D'Or shortlist
Cristiano Ronaldo of Real Madrid, who has been nominated for the Ballon D'Or
Ronaldo naye yumo

BORA kwa DUNIA: Rooney ni Mchezaji pekee England 2012 Ballon d'Or


>>KOCHA BORA: FERGIE, MANCINI & MATTEO wamo!!
>>WENGER HAYUMO!!
>>NDANI: Messi, Ronaldo, Xavi, Iniesta, Drogba, Balotelli!!
FERGIE_n_MOURINHOWayne Rooney ndie Mchezaji pekee mwenye asili ya Uingereza ambae yumo kwenye Listi ya Wachezaji 23 ambao wamo kwenye kinyang’anyiro cha kuwania Mchezaji Bora Duniani, FIFA BALLON D'OR, na kwenye Listi ya kuwania MENEJA BORA wamo Mameneja watatu toka LIGI KUU ENGLAND ambao ni Roberto Mancini, Sir Alex Ferguson na Roberto Di Matteo.
Pamoja na Rooney, Wachezaji wengine wanaochezea LIGI KUU ENGLAND ambao wamo kwenye Listi ni mwenzake wa Manchester United, Robin van Persie, na Wachezaji watatu wa Manchester City Sergio Aguero, Yaya Toure na Mario Balotelli.
++++++++++++++++++++++++++
WASHINDI waliopita wa Kiingereza wa BALLON D'OR:
=1956: Stanley Matthews
=1964: Denis Law
=1966: Bobby Charlton
=1968: George Best
=1978/79: Kevin Keegan
=2001: Michael Owen
++++++++++++++++++++++++++
Lakini, hapo Novemba 29, Listi hizo za Wachezaji na Mameneja zitapunguzwa na kubakishwa Wagombea watatu tu ambapo Mshindi atapatikana huko Zurich, Uswisi hapo Januari 7 Mwaka 2013.
Uteuzi huo utafanywa na Makepteni na Makocha Wakuu pamoja na Wawakilishi wa Wanahabari wa Kimataifa watakaoteuliwa na Gazeti la France Football ambalo ndio Washirika wa FIFA kwenye Tuzo hii.
LISTI ya WACHEZAJI BORA:
-Sergio Aguero (Manchester City/Argentina),
-Xabi Alonso (Real Madrid/Spain),
-Mario Balotelli (Manchester City/Italy),
-Karim Benzema (Real Madrid/France),
-Gianluigi Buffon (Juventus/Italy),
-Sergio Busquets (Barcelona/Spain),
-Iker Casillas (Real Madrid/Spain),
-Cristiano Ronaldo (Real Madrid/Portugal),
-Didier Drogba (Shanghai Shenhua/Ivory Coast),
-Radamel Falcao (Atletico Madrid/Colombia),
-Zlatan Ibrahimovic (Paris St Germain/Sweden),
-Andres Iniesta (Barcelona/Spain),
-Lionel Messi (Barcelona/Argentina),
-Manuel Neuer (Bayern Munich/Germany),
-Neymar (Santos/Brazil),
-Mesut Ozil (Real Madrid/Germany),
-Gerard Pique (Barcelona/Spain),
-Andrea Pirlo (Juventus/Italy),
-Sergio Ramos (Real Madrid/Spain),
-Wayne Rooney (Manchester United/England),
-Yaya Toure (Manchester City/Ivory Coast),
-Robin van Persie (Manchester United/Netherlands),
-Xavi (Barcelona/Spain)
LISTI ya MAKOCHA BORA:
-Vicente del Bosque (Spain/Spain Timu ya Taifa),
-Roberto Di Matteo (Italy/Chelsea),
-Alex Ferguson (Scotland/Manchester United),
-Pep Guardiola (Spain/Barcelona),
-Jupp Heynckes (Germany/Bayern Munich),
-Juergen Klopp (Germany/Borussia Dortmund),
-Joachim Loew (Germany/Germany Timu ya Taifa),
-Roberto Mancini (Italy/Manchester City),
-Jose Mourinho (Portugal/Real Madrid),
-Cesare Prandelli (Italy/Italy Timu ya Taifa)
 

CAPITAL ONE CUP: Jumatano ni Chelsea v Man United!


CAPITAL_ONE_CUP-BEST+++++++++++++++++++++++++
Mechi za Raundi ya 4 ya Mtoano ya CAPITAL ONE CUP ambalo zamani lilikuwa likiitwa Carling Cup au Kombe la Ligi zitachezwa Jumanne na Jumatano Usiku huku Mechi ya mvuto ni ile Jumatano huko Stamford Bridge kati ya Chelsea na Manchester United ingawa mara nyingi kwenye Kikombe hiki Timu nyingi huchezesha Wachezaji wasiokuwa na namba za kudumu kwenye Vikosi vya Kwanza na wale Chipukizi toka Timu zao za Akiba.
Na hii itakuwa ni mara ya pili ndani ya Siku 3 kwa Chelsea na Man United kukutana Uwanjani Stamford Bridge ambapo Jumapili Man United waliitwanga Chelsea Bao 3-2 katika Mechi ya Ligi Kuu England iliyoshuhudia Wachezaji wawili wa Chelsea, Ivanovic na Torres, kutolewa kwa Kadi Nyekundu.
Mabingwa watetezi, Liverpool, wao watakuwa nyumbani kucheza na Swansea City Siku ya Jumatano.
+++++++++++++++++++++++++
CAPITAL ONE CUP
RATIBA RAUNDI ya 4:
Mechi kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku, Bongo Taimu
Jumanne Oktoba 30
Sunderland v Middlesbrough
Swindon v Aston Villa
Wigan v Bradford
Leeds v Southampton
Reading v Arsenal
Jumatano Oktoba 31
Norwich v Tottenham
Liverpool v Swansea [SAA 5 Usiku]
Chelsea v Manchester United
+++++++++++++++++++++++++
DONDOO MUHIMU za CAPITAL ONE CUP:
-KABLA LILIKUWA ni Carling Cup na Bingwa Mtetezi ni Liverpool.
-Linaitwa CAPITAL ONE CUP kwa sababu Mdhamini wake ni Kampuni ya masuala ya Fedha, Capital One.
-Linashirikisha Timu za Ligi za juu England 92 kwa mtindo wa Mtoano [Timu 20 toka Ligi Kuu na 24 kila moja kutoka Madaraja ya Npower, Ligi 1 na 2.
-Bingwa wa michuano hii hucheza EUROPA LIGI Msimu unaofuata kuanzia Raundi ya Tatu ya Mtoano.

NINA NDOTO ZA KUSTAAFU SOKA NIKIWA BARCELONA - MESSI.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi amesema kuwa ana ndoto za kustaafu kucheza soka akiwa katika klabu hiyo ambayo imemfundisha toka mdogo na kuanza rasmi kucheza soka la kulipwa 2004. 
 
 Kauli ya nyota huyo imekuja wakati akipokea tuzo ya kiatu cha dhahabu aliyopewa kufuatia kuongeza orodha ya wafungaji barani Ulaya msimu uliopita akiwa na mabao 50. 
 
 Messi aliishukuru Barcelona kwa kumoa nafasi ya kutambua kipaji chake wakati walipomchukua katika shule yao ya michezo akiwa na umri wa miaka 13 mwaka 2000.
 
 Messi mwenye umri wa miaka 25 sasa ana mkataba wa miaka minne ambao una thamani ya paundi milioni 250 na maofisa wa klabu hiyo wamesema kuwa wako tayari kuuboresha zaidi mkataba huo.  
 
 
Mpaka sasa nyota huyo ameshafunga mabao 270 kwa klabu yake hiyo na 31 kwa timu ya taifa ya Argentina. 

WAZIRI MKUU SENEGAL AMTAKA RAIS WA FSF KUJIUZULU.

WAZIRI Mkuu wa Senegal, Abdoul Mbaye amemtaka rais wa Shirikisho la Soka la Senegal-FSF Augustin Senghor kujiuzulu wadhfa wake huo kutokana na vurugu zilizotokea wakati wa mchezo wa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika kati ya nchi hiyo na Ivory Coast.

 Maofisa watatu wa juu wa shirikisho hilo walijiuzulu Jumatatu ikiwa ni wiki moja toka makamu wa rais Lamotte Louis kujitoa katika kamati ya utendaji baada ya kukubali kuwajibika kwa vurugu zilizotokea uwanjani.

 Hatahivyo, Senghor alikataa kujiuzulu baada ya kujitetea kuwa serikali ilikuwa ikiingilia mambo yao ya michezo. Akihojiwa Senghor amesema kuwa haoni haja ya kujiuzulu kwani hakuna mtu yoyote mwenye haki ya kuwalazimisha kujiuzulu kwasababu walichaguliwa kihalali na muda wao wa kukaa madarakani bado haujakwisha.

 Senghor aliendelea kusema kuwa ataitisha mkutano wa dharura kesho kwa wajumbe 23 wa kamati ya utendaji waliobakia ili kuziba pengo la wajumbe wanne waliojiuzulu.

No comments:

Post a Comment